You are on page 1of 2

LUFUFU: NINAKIRI KUTAFSIRI FILAMU BILA IDHINI YA

WAMILIKI
Na Frank Shija-MAELEZO
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mukandala Lufufu inayojishughulisha na kazi
ya kutafsiri Filamu kwa Lugha ya Kishwahili Bw. Derick Mukandala
maarufu kwa jina la Mzee Lufufu amekiri kuwa kazi yake anaifanya kienyeji
ili hali akifahamu ni makosa.
Kauli hiyo ameitoa jana katika kikao baina yake na Bodi ya Filamu ambapo
alieleza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo kwa muda mrefu bila kuzingatia
utaratibu huku akijua kuwa ni makosa kwa mtu kutumia kazi ya msanii
mwingine bili idhini yake.
Nikiri tu kwamba nimekuwa nikifanya makosa kwa kutafsiri Filamu bila
kuwa na idhini ya wahusika wa filamu hizo Alisema Lufufu.
Mzee Lufufu aliongeza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo ya kutafsiri
Filamu bila vibali akiamini kuwa hakuna ubatili wowote.
Aidha Mzee Lufufu pamoja na kujua ni makosa kutafsiri Filamu bila idhini
alikuwa anatarajia kufanya kazi na Kampuni moja ya kutoka nchini Norway
ambapo kama amngefanikiwa kufanya Documentary ambayo ingejulikana
kwa jina la The Film Dubber from Dar es Salaam Mzee Lufufu hiyo
ingeaminisha ulimwengu kuwa Tanzania inaruhusu uharamia wa kazi za
wasanii kitu ambacho siyo sahihi.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
amesema kuwa siyo dhambi kutafsiri Filamu, ila ni lazima anayetaka
kufanya kazi hiyo azingatie dheria za nchi na taratibu zinaotakiwa
kuzingatiwa.
Fissoo amesema kuwa sheria ya Filamu nchini kifungu namba 17
kinamtaka anayetaka kufanya kazi ya kutafsiri awasilishe muswada wake
katika ofisi za Bodi ya Filamu ili uhakikiwa na wataalamu kabla ya kupewa
idhini ya kuendelea na kazi hiyo.
Aliongeza kuwa ili kazi ya kutafsiri Filamu ni sharti mhusika kupata idhini
ya mwenye Haki Miliki ya filamu husika hivyo ni vyema kuwasiliana na
COSOTA ili kufanya utaratibu wa kupata uhalali akitolea mfano wa Filamu

ya Nelia iliyotengenezwa nchini Zimbabwe na baadaye ilifanyiwa tafsiri


katika lugha ya Kiswahili hapa jijini Dar es Salaam baada ya kufuata
taratibu zote.

You might also like