You are on page 1of 4

Msipo tutetea Bungeni nasi hatuta watetea kwenye kura

Na Mroki Mroki
LEO Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litaanza vikao
vyake katika Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge hilo mjini
Dodoma.
Wabunge kutoka majimbo na vyama mbalimbali vya siasa
watakutana na kujadili masuala mbalimbali ya kitaifa na
kimataifa kuhusiana na maendeleo ya nchi na utekele\zaji wa
miradi yake mbalimbali yote ikiwa ni kuwaletea maendeleo
wananchi.
Pamoja na mambo mengine hii leo wananchi kupitia luninga zetu
kwa wale watakao pata wasaa wa kutazama watashuhudia kiapo
cha utii kwa Mbunge ambapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ndugu yangu, George Mcheche Masaju, ataapishwa baada ya
kuteuliwa na
Rais kufuatia kujiuzuru kwa aliyekuwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Mwita Werema.
Hili linafanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 24 ya Bunge.
Niimani yamngu kubwa kuwa wabunge wote bila kujali itikadi
zao za kiasiasa watampa ushirikiano mkubwa Masaju katika
utekelezaji wa majukumu yake mapya Bungeni humo na nje ya
Bunge.
Aidha, kwa Mujibu wa Kanuni ya 86 (1) ya Kanuni za Kudumu za
Bunge, jumla ya Miswada Mitatu (3) itasomwa na kupitishwa na
Bunge. Miswada hiyo ni ile ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa

Mwaka 2014 (The Tax Administration Bill, 2014) ambao


utapigiwa kura tu.
Pia kutakuwa na mswada wa Sheria ya Takwimu wa mwaka 2013
(The Statistic Bill, 2013) huu bunge litakaa kama kamati na
kusomwa kwa mara ya tatu, na mswada mwingine ni ule wa
Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2) wa Mwaka 2014.
(The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 2) Bill,
2014).
Pamoja na Miswada hiyo, Bunge pia litajadili Taarifa za
Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali zilizowasilishwa
katika Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge kuhusu Hesabu
zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika
ya Umma kwa mwaka 2012/2013, ambapo pia Serikali itatolea
majibu baadhi ya Hoja.
Kwa kuzingatia Kanuni ya 117 (15) katika Mkutano wa 18 wa
Bunge, Kamati za Bunge zitapewa nafasi ya kuwasilisha Taarifa
za Mwaka za Shughulii za Kamati na zitapangiwa muda wa
kujadiliwa kwa kadri Spika atakavyoelekeza.
Aidha, Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza na
kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Ardhi,
Kilimo, Mifugo Maji na Uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo
katika matumizi ya Ardhi itapewa nafasi ya kuwasilisha Taarifa
yake, ambapo taarifa hiyo itajadiliwa Bungeni.

Wananchi pia tutapata fursa ya kuwasikia wabunge wetu ambao


tumewapa nafasi ya kutuwakilisha Bungeni humo wakiuliza
maswali mbalimbali kuhusiana na kero zinazotukabili katika
maeneo yetu na serikali kuyatolea majibu kupitia Mawaziri wa
Wizara husika ambapo maswali ya kawaida takribani 125 ya
msingi yanaweza ulizwa na wabunge.
Nimeainisha tu baadhi ya vitu muhimu ambavyo vitajadiliwa
bungeni humo katika mkutano huu, na huenda yakaibuka
mengine lakini yawe ya msingi na tija kwa taifa letu.
Binafsi natarajia wabunge watatumia vyema nafasi zao na
kujadili hoja kwa kutoa hoja na si kulumbana na baadae
kupelekea mifarakano na lugha za zihaka kama walivyokuwa
wakifanya vikao vingine.
Wabunge mkawatetee wananchi kwa hoja zilizo na mashiko na
kamwe msitetee masalahi yenu ndani ya bunge bali wale walio
wapigia kura huku mkiwa tayari mmenza kusikia kengele
masikiponi mwenu ikilia kuashiria muda wenu kumalizika hivyo
mnatakiwa kurudi kwao kuomba ridhaa tena.
Lile la kufika Bungeni na kusaini mahudhurio na kisha kupotea
mtaani nalo silitaraji katika kikao hiki na niimani yangu kuwa
mtahudhuria Bunge kikamilifu na si kukaa kimya bali kuchangia
mijadala yote.
Ninawaombea hekima na busara tu kutoka kwa Mungu katika
mkutano huo na mkafanye kazi yenu kikamilifu lakini

mkikumbuka kuwa sasa tunawasikiliza na kuwatazama maana


hizi ndio dakika za lala salama katika wadhifa mlio nao na sisi
ndio waamuzi wa hatma yenu majimboni.
Kama mwananchi na mpiga kura, nasema usipo tutetea nasi
hatuta kutetea katika kura utakayo kuja kuiomba hapo baadae,
hivyo Mbunge timiza wajibu wako wa kutusemea kero zetu na
kuleta ufumbuzi wa matatizo hayo.

You might also like