You are on page 1of 5

Na Anna Nkinda Maelezo, Lindi

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama


Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama
Salma Kikwete ameitaka jamii kutumia sauti zao
kuwasemea watoto wenye mahitaji maalum kwani watoto
hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali na hawana
mtu wa kumwambia matatizo yao.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete alitoa rai hiyo jana alipotembelea kitengo cha
wanafunzi wenye mahitaji maalum kilichopo shule ya
Msingi Mpilipili wilaya ya Lindi mjini.
Alisema watoto wenye mahitaji maalum wanakabiliwa na
changamoto nyingi ukilinganisha na watoto wengine pia
matatizo yao hayafanani hivyo basi ni jukumu la kila mtu
katika jamii kuwasaidia watoto hao ili waweze kuishi kama
watoto wengine.
Katika kitengo hiki kuna watoto wenye tatizo la usonji
(Autism) na wasiosikia (viziwi), kila mtoto anahitaji lake na
pale anapokabiliwa na tatizo anatakiwa kusaidiwa kwa
haraka ili asijisikie kunyanyapaliwa. Nawapongeza walimu
mnaowafundisha watoto hawa kwani kazi hii ni ngumu na
inahitaji moyo wa ziada, alisema Mama Kikwete.
Akisoma taarifa ya kitengo cha wanafunzi wenye mahitaji
maalum mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mpilipili
Fadhili Mtitima alisema kitengo hicho kilianzishwa mwaka
1993 kikiwa na wanafunzi watano na hivi sasa kuna
wanafunzi 20 wenye tatizo la usonji 16 kati yao wavulana
ni 16 na wasichana wawili na wasiosikia (viziwi) wawili
msichana mmoja na mvulana mmoja.

Mwalimu Mtitima alisema njia zinazotumika kuwapata


wanafunzi hao ni wanafunzi wa kawaida kutoa taarifa ya
uwepo wa watoto wenye mahitaji maalum katika mitaa yao
kwa walimu, wazazi ambao wamehamasika huwaleta
watoto kujiunga na shule, kutoa hamasa na matangazo
kwa jamii katika maadhimisho ya wiki ya elimu kwa wote
na kupitia sensa ya watoto inayofanyika kila mwaka.
Changamoto zinazotukabili ni watoto wengi wanaoishi
mbali na kitengo wanakosa fursa ya kupata elimu
kutokana na umbali uliopo, baadhi ya wazazi wa watoto
wenye ulemavu hawawaandikishi watoto wao wakiwa na
imani kuwa watoto hawa hawafundishiki, idadi ya walimu
haitoshelezi kwani kuna walimu wawili kati ya wanne
wanaohitajika kufundisha watoto wenye tatizo la usonji.
Kitengo hakina mwalimu mtaalamu wa elimu ya
walemavu wasiosikia na walimu kutojitokeza kujiendeleza
katika mafunzo ya kufundisha wanafunzi wenye mahitaji
maalum, alisema Mwalimu Mtitima.
Akiwa shuleni hapo Mama Kikwete aliwaita na
kuwasalimia wanafunzi wa kawaida na kuwahimiza
kusoma kwa bidii, kufuata sheria za shule na kuwatii
walimu wao kwa kufanya hivyo watafanya vizuri katika
masomo yao na kufika hadi elimu ya Chuo kikuu.
Licha ya kusoma kwa bidii na kuhudhuria darasani
mwanafunzi bora anatakiwa kuwahi shuleni na kufanya
kazi za shule ikiwa ni pamoja na kusafisha eneo lake,
alisisitiza.
Kwa upande wa mimba za utotoni aliwasihi
vishawishi na mazingira yatakayowapelekea

kuepuka
kupata

ujauzito kwani mimba zitawazuia kuendelea na masomo na


hivyo kukatisha ndoto za maisha yao.
Wakati huo huo Mama Kikwete alifanya vikao na viongozi
wa Halmashauri kuu ya tawi ya Chama Chama Cha
Mapinduzi
katika matawi ya Mtuleni B na Mpilipili
Kaskazini na kuwataka wazazi kuwakanya watoto wao
pale wanapoona njia wanayoenda siyo sahihi.
Mama Kikwete alisisitiza, Hivi sasa vijana wengi
tuliowazaa sisi wenyewe wanatumika kufanya vurugu
zinazotishia
amani ya nchi lakini tukumbuke vita
inapotokea waathirika wakubwa ni wanawake, watoto,
walemavu na wazee hivyo basi tukae chini na kuzungumza
na watoto wetu ili wasikubali kufanya mambo haya.
Katika Tawi la Mtuleni B Mama Sharifa Mkufu ambaye ni
balozi wa nyumba kumi katika mtaa wa Ripsi alimshukuru
Mama Kikwete kwa semina ya mabalozi aliyoiandaa
iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana ambayo
imemsaidia katika utendaji wake wa kazi.
Nilisoma katiba ya Chama na kuitisha kikao cha mwezi na
kuwafundisha wengine yale niliyojifunza, watu waliuliza
maswali mbalimbali yahusuyo chama chetu na kutoa
maoni yao baada ya hapo utendaji wangu umebadilika
naweza kufanya kazi zangu vizuri tofauti na mwanzo,
Mama Mkufu alisema.
Aidha MNEC huyo aliongea na wananchi waliohudhuria
mkutano wa hadhara uliofanyika katika tawi la Mpilipili
Kaskazini
na
kuwasisitiza
kujitokeza
kwa
wingi
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura,
kuipigia kura ya ndiyo katiba inayopendekezwa na

kuchagua kiongozi mwenye sifa katika uchaguzi mkuu


ujao.
Mama Kikwete alisema, Nawapongeza wananchi wa Kata
hii katika uchaguzi uliopita wa Serikali ya mitaa
mmewachagua wanawake wengi kuwa viongozi wenu hili
ni jambo jema, pia nawapongeza wanawake waliojitokeza
kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Ninawaomba
wanawake wenzangu katika uchaguzi mkuu ujao msiogope
jitokezeni kwa wingi kugombea nafasi za uongozi.
Akiwasalimi wananchi waliohudhuria mkutano huo Mkuu
wa wilaya ya Lindi Dkt. Nassoro Hamidi aliwaomba viongozi
wa dini kuwahimiza waumini wao kukubali matokeo ya
uchaguzi kwani katika Ulimwengu wa kawaida kama watu
hawatakubali matokeo ya uchaguzi matokeo yake huwa ni
vurugu zinazohatarisha amani.
Dkt. Hamidi alisisitiza, Pigeni vita ukabila na udini ugomvi
wa hivi vitu unaweza kusababisha vita katika jamii ili
amani iliyopo iendelee kudumu na tuweze kuitumia gesi
inayopatikana katika mkoa wetu ambayo itatuletea
maendeleo ni lazima tuishi kwa upendo, umoja na
mshikamano.
Naye Omary Chatanda ambaye alikuwa Mwenyekiti wa
mkoa wa Lindi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) na kuhamia CCM aliwasihi vijana wenzake
kutokubali
kutumika
katika
vurugu
zinazoharibu
maendeleo yao kwani chama chochote cha siasa lengo lake
kuu ni kushika dola.
Mama Kikwete yupo wilayani humo kwa ajili ya kuimarisha
kazi za chama hicho ikiwa ni pamoja na kufanya vikao na

viongozi na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya


mwaka 2010 .

You might also like