You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TANGAZO
MIGODI YA DHAHABU YA GEITA, BULYANHULU, BUZWAGI NA
NORTH MARA KUANZA KULIPA USHURU WA HUDUMA KWA
KIWANGO CHA 0.3% YA MAPATO GHAFI KWA
HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI
Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutangazia umma kuwa
mgodi wa dhahabu wa Geita unaomilikiwa na kampuni ya
AngloGold Ashanti; na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North
Mara inayomilikiwa na kampuni ya Acacia Mining, imeanza kulipa
ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato
ghafi kwa Halmashauri husika. Halmashauri zitakazonufaika na
malipo hayo ni: Mji wa Geita; Wilaya ya Geita; Mji wa Kahama;
Wilaya ya Msalala; na Wilaya ya Tarime. Malipo hayo yanaanza
tarehe 1 Julai, 2014. Malipo hayo yanafuatia makubaliano kati ya
Serikali na Kampuni zinazomiliki migodi husika kufanya
marekebisho kwenye Mikataba ya Maendeleo ya Uchimbaji Madini
(Mining Development Agreement - MDA) baina ya Serikali na Migodi
ya Geita, Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara kuhusu ulipaji wa
ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya Local
Government Finance Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala
ya Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa
awali.

Mha. Ngosi C.X. Mwihava


KAIMU KATIBU MKUU
25 Februari, 2015

You might also like