You are on page 1of 3

DKT.

MAGUFULI: WANANCHI WA MWANGA-KIKWENILOMWE KUTOBOMOLEWA NYUMBA ZAO


Mwandishi Wetu
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ametangaza
kutobomoa nyumba zilizopo kando kando ya
barabara
ya
Mwanga-Kikweni/Vuchama-hadi
Lomwe km 40.6 na kusema kuwa barabara hiyo
itajengwa kwa kiwango cha lami kwa kutumia
upana wake uliopo sasa hivi.
Dkt. Magufuli alitoa kauli hiyo ya faraja kwa wakazi
wa Kikweni Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro
kabla ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya
Mwanga-Kikweni/Vuchama-Usangi hadi Lomwe(km
40) itakayojengwa kwa kiwango cha lami hivi
karibuni.
Waziri wa Ujenzi amechukua uamuzi huo kutokana
na maeneo mengi ya milimani ambapo barabara
hiyo inapita kuwa na mashamba ya watu tofauti na
sehemu nyingine.
Nikiwa kama Waziri wa ujenzi katika maeneo haya
ya milima sitatumia sheria ya mita 30 kila upande
katika ujenzi wa barabara hii ili nyumba na
mashamba ya wakazi wa huku yasiathirike

Dkt. Magufuli aliongeza kuwa ujenzi wa Barabara


una sheria zake ndio maana ameamua kutumia
sheria ya barabara namba 13 ya mwaka 2007
kifungu cha 13 na 20 kinachompa mamlaka
kupunguza upana wa barabara
Aidha, Waziri Magufuli aliwatoa hofu wakazi wote
waliowekewa alama ya X katika nyumba zao na
kuwataka kuendelea na shughuli zao kama
kawaida kwasababu nyumba hizo hazitabomolewa.
Katika hatua nyingine Dkt. Magufuli aliwataka watu
wote waliojenga vibanda karibu na barabara ya
zamani waanze kuondoka mapema kabla ya ujenzi
wa barabara hiyo kuanza hivi karibuni.
Nawaomba wote mlioweka vibanda karibu na
barabara mtoe kwa hiari yenu ili tutengeneze
barabara hii bila vikwazo na kwa haraka tofauti na
awali ambapo tulikuwa tunatangaza zabuni kwa
kilomita chache alisisitiza Waziri Magufuli
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
Leonidas Gama amemshukuru Waziri Magufuli kwa
hatua yake hiyo na kusema kuwa kufunguka kwa
barabara hiyo ni mkombozi mkubwa kwa wilaya ya
Mwanga na Mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.

Wilaya yetu hii inapakana na nchi jirani hivyo hata


kiusalama ni vizuri barabara hii ikajengwa kwa lami
ili irahisishe mawasiliano kwa haraka zaidi katika
Wilaya yetu hii alisema Mkuu wa Mkoa
Naye Mbunge wa Mwanga ambaye pia ni Waziri wa
Maji Profesa Jumanne Maghembe ameishukuru
Serikali na kusema kuwa kukamilika kwa barabara
hiyo kutawaondolea kero kubwa ya usafiri
wananchi wa Usangi na mwanga na kuwasaidia
kufanya biashara kwa urahisi zaidi tofauti na awali.
Kukamilika kwa barabara hii kutasaidia kuinua
uchumi mkubwa uliopo huku Usangi tofauti na hali
iliyopo sasa Alisema Profesa Maghembe.

You might also like