You are on page 1of 4

Airtel yamkabithi

Mwansasu gari Lake

Mkazi

wa

Kyela,

Edom

Na Father Kidevu Blog


Mkazi wa kyela mkoani Mbeya Bwana Edom Dickson
Mwansasu amekabithiwa gari aina ya Toyota IST na
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mara baada
ya kuibuka mshindi kupitia droo ya wiki ya pili ya
promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi iliyofanyika siku
ya ijumaa iliyopita
Bwana Edom Mwansasu mwenye umri wa miaka 40
anajishughulisha na shughuli za kilimo huko
Ngonga Kyela Mkoani Mbeya ameibuka mshindi
baada ya kununua na kujiunga na vifurushi vya
siku vya huduma ya Airtel yatosha kila siku.
Akiongea baada ya kukabithiwa gari bwana Edom
Mwansasu alisema ninafuraha sana kuwa mshindi
na kutumiza ndoto yangu ya kumiliki gari.
Nilipopigiwa simu sikuamini kuwa nimeshinda gari ,
nilifurahi sana nakupasha habari kwa familia
yangu. Sijawahi kumiliki gari hivyo najisikia furaha
sana Airtel kunizawadia mimi hii gari kupitia hii
promosheni ya Airtel yatosha.
Kwa kupitia gari hili sasa na uhakika wa usafiri
mimi pamoja na familia yangu lakini pia litanisaidia

katika kazi yangu ya kilimo na kuniwezesha


kusafirisha mazao yangu kirahisi ukilinganisha na
awali nilikuwa natumia baskeli au kukodi gari.
Nawapongeza sana Airtel na nawashauri watanzania
kuendelea kutumia huduma ya Airtel yatosha na
kuamini kuwa nao wanaweza kubahatika na
kushinda kama mimi aliongeza Mwansasu
Kwa upande wake Kamanda mkuu wa polisi wa
Mkoa wa Mbeya Bwana Hemed Msangi alisema
kwanza kabisa napenda kuwapongeza Airtel kwa
kuanzisha promosheni hii kabambe inayowawezesha
watanzania kutoka sehemu mbalimbali kujishindia
magari.
Naamini kwa kupitia promosheni hii mtawawezesha
watanzania wengi kujikwamua kiuchumi na
kuwawezesha kufanya shughuli zao za kijamii na
kiuchumi kirahisi na kwa ufanisi zaidi.
Nawapongeza washindi wote waliopatikana mpaka
sasa. Lakini natumia fulsa hii kuwaomba wananchi
wadumishe amani maana kama sio amani tulionayo
basi promosheni kama hizi zisingeweza kufanyika
Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja biashara wa
Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushi
Alisema promosheni hii ya Airtel yatosha zaidi ni

mahususi kwa wateja wetu Tanzania nzima


wanaotumia huduma hii ya Airtel Yatosha kuweza
kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku .
Kujiunga na vifurushi vya Airtel yatosha mteja
anatakiwa kupiga *149*99# au kwa kununua vocha
vya Airtel yatosha au kununua kupitia huduma ya
Airtel Money na kuunganishwa moja kwa moja
kwenye droo itakayomwezesha kushinda.
Mpaka sasa washindi 10 wamepatika ambapo kati
yao wawili wanatoka kanda ya nyanda za juu kusini
na leo tunamkabithi mshindi wetu wa Mbeya Bwana
Edom Mwansansu gari lake na kisha tutamkabithi
mshindi wa mkoa wa sumbawanga bwana Saidi
Mashiko ambaye ni mganga wa tiba za jadi na mkazi
wa Katavi hivi karibuni
Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu
kujiunga na vifurushi hivi vya Airtel yatosha na
kupata nafasi ya kujishindia gari aina ya Toyota IST
kila siku. Aliongeza Mushi
Washinde wengine waliojishindia Toyota IST toka
promosheni hii ianze ni pamoja na Ramadhani
Dilunga mkazi wa Pwani, Namtapika Kilumba Mkazi
wa Mtwara, said Mashiko mkazi wa katavi, Hamim
Yoyo mkazi wa Korogwe Tanga, Esther Mashauri
Mkazi wa Mwanza, Ibrahim Kimondo mkazi wa

Kondoa pamoja na Mwajabu Churian, Sakina


Libwana na Justin Wilium wote wakazi wa Dar ES
Salaam.

You might also like