You are on page 1of 4

WAMILIKI WA VIWANDA WATAKIWA KUTOA

USHIRIKIANO KWA WADADISI WA SENSA YA


VIWANDA.
Na. Aron Msigwa MAELEZO.
SERIKALI imewataka wamiliki wa viwanda kuwapa
ushirikiano wadadisi wa Sensa ya Viwanda
watakaopita katika maeneo yao kwa lengo la
kukusanya takwimu sahihi za viwanda vilivyopo
nchini na mchango vinaotoa katika maendeleo ya
taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na
Biashara Maria Bilia wakati wa ufunguzi wa
mafunzo ya siku 14 ya wadadisi wa Sensa ya
Viwanda yanayoendelea katika chuo cha Takwimu
cha Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la
Changanyikeni jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa mafanikio ya Sensa hiyo yatatokana
na wamiliki wa viwanda kuthamini na kutambua
umuhimu za Sensa hiyo kwa kutoa ushirikiano kwa
wadadisi watakaopita katika maeneo yao kupata
taarifa zinazohusu masuala mbalimbali ikiwemo
uzalishaji wa bidhaa na masuala ya ajira;
Amesema upatikanaji wa takwimu sahihi kuhusu
Sekta ya Viwanda nchini Tanzania utaiwezesha
Serikali kuweka Sera na mipango endelevu ya

maendeleo itakayoisaidia sekta hiyo kupiga hatua


kimaendeleo.
Sensa hii ya viwanda ni muhimu kwa maendeleo ya
nchi yetu, na mafanikio yake yatatokana na wenye
viwanda kutupa ushirikiano maana bila wao kutoa
takwimu sahihi mipango ya maendeleo kuhusu
viwanda haitatekelezeka kwa sababu ya kukosa
takwimu sahihi Amesema Bilia.
Kuhusu sampuli ya viwanda vitakayoguswa na
Sensa hiyo amesema ni pamoja na maeneo ya
viwanda yaliyoajiri watu wengi na yanayohusisha
uzalishaji mkubwa wa bidhaa za viwandani ,maeneo
ya uzalishaji wa bidhaa za kokoto, bidhaa za vyakula
na maeneo yaliyoajiri mtu zaidi ya mmoja.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo amesema
kuwa Sensa hiyo ya viwanda itakayohusisha
viwanda vyote nchini inafanywa kwa ushirikiano wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Wizara ya Viwanda na
Biashara.
Amesema kukamilika kwa Sensa hiyo kutaliwezesha
taifa kuwa na takwimu sahihi za viwanda na
kutambua mchango wa Sekta ya viwanda katika
uchumi wa taifa na mchango wa ajira kwa
wananchi.

Kuhusu mafunzo hayo ya siku 14 kwa wadadisi 200


watakaoendesha zoezi hilo amesema Ofisi ya Taifa ya
Takwimu kupitia Chuo cha Takwimu cha Mashariki
mwa Afrika inaendesha mafunzo hayo kwa vitendo
na nadharia ili kuwawezesha na kuwajengea uwezo
wadadisi hao kukusanya takwimu bora.
Lengo la kuendesha Sensa hii ni kuhakikisha
kuwa nchi yetu inapiga hatua na kuwa nchi yenye
maendeleo ya kati kwa kuwa na matumizi sahihi ya
takwimu ztu
Kaimu Mkurugenzi wa Shirikisho la wenye Viwanda
nchini Bw.Hussein Kamote akizungumza wakati wa
ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya wamiliki
wa Viwanda nchini amesema kuwa Sensa ya
viwanda
itakayofanyika
nchini
mwezi
huu
italiwezesha taifa
kuwa na takwimu sahihi
zinazohusu sekta ya viwanda.
Sensa hii ya viwanda ni muhimu sana kwa
maendeleo ya taifa nawaomba wenye viwanda watoe
ushirikiano wa kutosha maana bila wao zoezi hili
litakuwa gumu
Ameongeza kuwa Sensa ya viwanda ni muhimu
kutokana na mchango wake katika nchi nyingi za
Asia ambazo zimefanikiwa na kupiga hatua
kimaendeleo kwa sababu ya kuwa Sensa endelevu

na takwimu sahihi za sekta ya viwanda na mchango


wake katika pato la taifa.

You might also like