You are on page 1of 52

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI NDUGU KABWE ZUBERI ZITTO (MB), WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI, KUHUSU

MAPENDEKEZO YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014 (Inatolewa chini ya Kanuni ya 105(8) ya kanuni za Bunge Toleo la mwaka 2013) _________________________________ 1. UTANGULIZI Mheshimiwa Spika, Bajeti ya serikali kimsingi ni policy instrument inayotolewa kama mpango wa hati ya mapato na matumizi. Aidha hati hujumuisha makadirio ya makusanyo na matumizi ambayo Serikali imetayarisha na fedha iliyotumia au ambayo itatumika kwa mwaka ujao. Bajeti ya Serikali huoanisha makadirio ya fedha yanayohitajiwa na Wizara zote, idara zinazojitegemea, Wakala na Serikali za Mitaa kwa mwaka husika wa fedha. Bajeti ya Serikali ina sehemu tatu, yaani; makadirio ya mapato, matumizi ya kawaida ya kila siku na matumizi ya maendeleo. Matumizi ya kawaida na ya maendeleo ndiyo hufanya jumla ya fedha yote inayotumiwa na Serikali kwa mwaka wa fedha unaohusika. Bajeti ya Serikali pia inajulikana kama Taarifa ya Mwaka wa Fedha ya nchi.

Page 1 of 52

Mheshimiwa Spika, katika Bajeti Mbadala za mwaka 2011/12 na 2012/13 Kambi Rasmi ya Upinzani ilipendekeza masuala kadhaa ili kusaidia kuongeza mapato ya Serikali kwa upande mmoja na kwa upande wa pili kusaidia kupunguza umasikini wa kipato kwa wananchi wa kawaida na hivyo kuboresha maisha yao. Masuala tuliyoyapendekeza ni pamoja na: 1. Kupunguza misamaha ya kodi hadi kufikia asilimia moja ya pato la Taifa kama wenzetu wa Uganda na Kenya. Serikali ilikubaliana na pendekezo hili kwa maneno lakini imeshindwa kulitekeleza licha ya kutoa ahadi za kufanya hivyo kila mwaka. Hivi sasa misamaha ya kodi imefikia asilimia 4.3 ya Pato la Taifa. 2. Kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani hadi kufikia asilimia 20 ya Pato la Taifa. Katika Bajeti ya Mwaka huu Serikali inatarajia kufikia lengo hili ambalo lilitolewa na Kambi ya Upinzani Bungeni katiika bajeti zilizopita licha ya miaka yote kubezwa kwamba haiwezekani. Iwapo Misamaha ya kodi ikipunguzwa, utoroshaji fedha nje ukadhibitiwa na ukwepaji kodi katika idara ya forodha ukapunguzwa, Tanzania inaweza kukusanya asilimia 25 ya Pato la Taifa kama mapato ya ndani. Bajeti mbadala ya upinzani inaelekea huko. 3. Kuongeza Kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa umma hadi Tsh 315,000 kwa Mwezi. Inashangaza kuwa katika mwaka wa fedha 2013/14 Serikali imeshindwa hata kutangaza
Page 2 of 52

kima cha chini licha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kueleza katika hotuba yake katika sherehe za Mei Mosi huko Mbeya na Waziri wa Utumishi kuahidi kuwa kima cha chini kitatangazwana Waziri wa Fedha. 4. Kuweka kiwango cha chini cha kodi ya Mapato kwa mwananchi (PAYE) kuwa asilimia tisa (9) na kitozwe kwa mapato yanayozidi Tshs 150,000. Kwa mwaka wa pili mfululizo Serikali imeendelea kuwahadaa wafanyakazi nchini kwa kushusha kiwango hicho kwa asilimia moja tu. 5. Kuifanyia marekebisho sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004 kwa kufuta sehemu ya Kodi ya Mapato inayotoa fursa kwa kampuni za madini kutumia sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 1973 iliyofutwa (grandfathering). Pendekezo letu lilikuwa na lengo la kutaka kuweka mfumo wa straightline method of depreciation ya asilimia 20 badala ya sasa ambapo Kampuni za Madini ufanya 100 percent depreciation kwenye mitambo yao mwaka wa kwanza na hivyo kuchelewesha kulipa Corporate Tax. Pendekezo hili ambalo lingeipatia Serikali mapato mengi na kwa sasa bado halijatekelezwa kwa Kampuni za madini zenye mikataba. 6. Kuanzishwa kwa Real Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita na kwamba kila mwenye nyumba ya kupangisha lazima atambuliwe na kulipa kodi inavyostahili kutokana na
Page 3 of 52

biashara

ya

kupangisha

nyumba/vyumba. Serikalibado haijatekeleza pendekezo hili, hakuna sera ya nyumba na hivyo Serikali kupoteza mapato mengi sana kwenye sekta ya nyumba, kodi za nyumba kuwa juu sana na kuumiza vijana wanaoanza maisha na kutozwa kwa mwaka mzima. 7. Kushushwa kwa tozo ya kuendeleza stadi (skills development levy SDL) kutoka asilimia sita (6) ya sasa mpaka asilimia nne (4). Katika pendekezo hilo tulishauri kuwa waajiri wote walipe kodi hii ikiwemo Serikali na Mashirika ya Umma. Serikali imechukua pendekezo hili kwenye mapendekezo ya Bajeti ya mwaka 2013/14 lakini bila kuhusisha mwajiri Mkuu, Serikali. Ni vema kodi hii ilipwe na waajiri wote nchini na ishuke kuwa asilimia 4. 8. Kuwepo na utaratibu wa kuweka stiker maalumu kwa kazi za sanaa zinazotolewa na mamlaka za serikali kuonyesha uhalali wa muuzaji wa kazi hizo ili wasanii wanaozitengeneza wanufaike na kazi zao. Pendekezo hili lilikubaliwa na Serikali na hivi sasa TRA na COSOTA wameanza kufanya kazi hii ili kuhakikisha wasanii wetu wanafaidi jasho lao. 9. Kuzuia kabisa kusafirisha ngozi ghafi kwenda nje ya nchi na badala yake kuwe na mpango wa kuziongezea thamani na kuzitumia ngozi ghafi hapa nchini ili kuleta tija katika uchumi wa taifa kwa kutengeneza ajira na kuongeza thamani ya mauzo nje. Serikali iliamua kupandisha ushuru. Kambi ya
Page 4 of 52

Upinzani Bungeni inaamini kuwa kuna haja kubwa ya kuzuia kuuza mazao ghafi nje ili kukuza ajira za ndani na kuongeza thamani ya mauzo yetu nje. 10. Kujenga Mazingira ya ukuaji wa uchumi vijijini (rural

growth) kwa kuboresha miundombinu ya umeme, barabara, maji na Umwagiliaji. Tulipendekeza kutumia shilingi bilioni 450 kila mwaka kwa ajili ya kutekeleza azma hii. Fedha hizi zitasimamiwa na Mamlaka ya Maendeleo Vijijini (Rural Development Authority) ambayo nayo tulipendekeza iundwe chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Pendekezo hili Serikali imelidharau na madhara yake ni kuwa maendeleo ya vijijini hayana uratibu mzuri na hivyo kusahaulika kabisa. 11. Kukarabati Reli ya Kati na matawi yake ya Tanga - Arusha na Mpanda. Tuliitaka serikali kutenga Tsh 443 bilioni kwa RAHCO kwa ajili ya maendeleo ya reli nchini. Serikali imetenga fedha kidogo sana kwenye miundombinu ya Reli. Mwaka huu tunapendekeza kodi maalumu ya kuendeleza Reli. 12. Kujenga uwezo wa viwanda vya ndani ili kuviwezesha na kuuza nje bidhaa za kilimo na mifugo kuzalisha

zilizoongezewa thamani. Tuliitaka serikali kupiga marufuku uuzaji nje wa korosho ghafi kama ilivyovyo kwa ngozi ghafi kwa kuanzia. Serikali haijaweka mkakati wowote wa kuhakikisha korosho yote nchini inabanguliwa kabla ya kuuzwa nje.

Page 5 of 52

13.

Kuboresha

elimu

na

afya

hasa

kwa

shule

na

zahanati/Vituo vya Afya vilivyo katika maeneo ya vijijini kwa kutoa motisha kwa wafanyakazi wa sekta hizi walio kwenye Halmashauri za Wilaya. Tulipendekeza pia kuanzishwa kwa posho za mazingira magumu ya vijiji sawa kwa kiwango cha mara moja na nusu ya mishahara yao. Serikali haijatekeleza pendekezo hili. 14. Kuanzisha pensheni ya uzeeni kwa wazee wote nchini wenye umri wa zaidi ya miaka 60. Serikali ipo kimya kuhusu suala hili muhimu sana kwa wazee nchini. 15. Kuanzisha Chuo Kikuu cha Mtwara (Mtwara University for Petroleum Studies) ili kufundisha wataalamu wa kutosha wa sekta ya Mafuta na Gesi na kuliandaa Taifa kuwa na wasomi mahiri wa maeneo hayo na hivyo kufaidika na utajiri wa Mafuta na Gesi uliopo nchini kwetu. Serikali ipo kuhusu pendekezo hili ambalo lingeweza hata kupunguza matatizo haya yanayoendelea mkoani Mtwara. 16. Kupunguza mzigo wa matumizi ya magari ya Serikali kwa kupiga mnada baadhi ya mashangingi na kuweka mfumo wa kukopesha magari kwa watumishi wote wa umma wanaostahili magari kama alivyofanya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania. Katika Bajeti ya serikali ya mwaka ujao wa fedha imeahidi kuwakopesha watumishi wake magari lakini hakuna uhakika iwapo hilo liotafanyika.
Page 6 of 52

17.

Aidha tulipendekeza hatua ili kuweza kukabiliana na (Multinational Corporations) na hatimaye

ukwepaji wa kodi unaofanywa na makampuni makubwa ya kimataifa kuliongezea taifa mapato. Hatua hizo ni pamoja na: (i) Kutunga sheria kwa kuimarisha zaidi sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004 kwamba, mikopo ya makampuni kwenye uwekezaji, kwa sababu za kikodi, isizidi asilimia 70 ya mtaji wote uliowekezwa na hii ianze mara moja bila kujali mikataba iliyopo. Pendekezo hili limetekelezwa kikamilifu. (ii) Kutunga sheria kuhakikisha kwamba riba kwenye mikopo kutoka Makampuni yanayohusiana (sister companies) haitaondolewa kwenye kutoza kodi (not tax deductible). Pendekezo hili limetekelezwa kikamilifu. (iii) Kuhakikisha kwamba serikali inakusanya kodi kwa kiwango cha asilimia 30 kama ongezeko la mtaji (capital gains) kutokana na mauziano ya Kampuni yoyote ambayo mali zake zipo Tanzania. Pendekezo hili limetekelezwa kikamilifu. Hata hivyo Wizara ya Nishati na Madini imeshindwa kushirikiana na TRA kupata kodi ya tshs 329 bilioni kutoka kampuni ya Mantra Resources baada ya kuuza mradi wa Mkuju Uranium.

Page 7 of 52

Mheshimiwa Spika, baadhi ya mapendekezo yetu yalichukuliwa na Serikali ya CCM na kuyafanyia kazi kama nilivyoonyesha hapo juu. Kwa yale ambayo yalitekelezwa vizuri yameleta matokeo mazuri. Lakini kuna mapendekezo mengine serikali imeyachukua lakini imeshindwa kuyatekeleza kama ambavyo tulishauri. Licha ya mapendekezo yaliyotekelezwa vizuri kuleta sifa kwa serikali, Kambi Rasmi ya Upinzani itaendelea kuwaonyesha njia serikali na CCM ya namna bora na rahisi ya kuiondoa nchi katika giza hili la uchumi na lindi la umasikini lililotengenezwa na Serikali hii ya CCM kwa makusudi lakini sasa inashindwa kuwa na mkakati makini wa kuweza kutoka.

2. DENI LA TAIFA (FUNGU 22) Mheshimiwa Spika, Deni la Taifa limeendela kuwa changamoto kubwa Kwa uchumi wetu. Kukua Kwa Deni la Taifa kusababisha bajeti ya Serikali kuendelea kuwa tegemezi na hivyo kushindwa kutatua kero za kiuchumi za wananchi. Kwa bahati mbaya wananchi wengi hawaelewi undani wa deni la taifa na athari zake katika maisha yao ya kawaida. Jambo la kusikitisha ni kwamba Serikali imekuwa ikitumia mwanya wa wananchi kutokufahamu kwa undani athari za deni la taifa kuendelea kukopa mikopo mikubwa yenye masharti ya kibiashara (kwa maana ya riba kubwa). Kuendelea kukopa Kwa namna hiyo kunaendelea kuwabebesha walipa kodi wa Tanzania mzigo mkubwa wa madeni ambayo
Page 8 of 52

yanazidi kufanya hali ya maisha kwa wananchi iendelee kuwa ngumu kwa kuwa Serikali inatumia fedha nyingi kulipa madeni badala ya kuzitumia fedha hizo kugharamia miradi ya maendeleo. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, deni la taifa liliongezeka kwa asilimia 38 kutoka Shilingi trilioni 7.6 mwaka 2008 mpaka Shilingi trilioni 10.5 mwaka 2009/2010. Mwaka 2010/2011 deni hilo liliendelea kuongezeka kutoka shilingi trilioni 10.5 na kufikia kiasi cha shilingi trilioni 14.441 Aidha, katika mwaka wa fedha 2011/2012 deni hilo liliendelea kuongezeka zaidi kutoka shilingi trilioni 14.441 na kufikia kiasi cha shilingi trilioni 16.975. Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa mwaka 2012, deni la taifa liliongezeka kwa kasi ya ajabu kutoka shilingi trilioni 18.8 (Desemba 2011) hadi kufikia shilingi trilioni 22.7 (Desemba, 2012). Mheshimiwa Spika, hata hivyo kwa mujibu wa hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Fedha aliyoisoma Juni 13, 2013 akiwasilisha bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2013/2014, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi machi 2013, deni la Taifa lilikuwa limeongezeka tena na kufikia shilingi trilioni 23.7. Kati ya hizo shilingi trilioni 18.3 zinawakilisha deni la nje, ikiwa ni sawa na asilimia 77 ya deni lote la Taifa. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inatumia fursa hii kuwajulisha wananchi wote wa
Page 9 of 52

Tanzania kwamba hali duni ya maisha waliyo nayo na umasikini mkubwa walio nao unasababishwa kwa kiasi kikubwa na Serikali kukopa mno nje jambo ambalo linaongeza ugumu wa maisha. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapenda pia kuwajulisha wananchi kwamba jukumu la kulipa deni la taifa kimsingi ni la wananchi na wanalilipa kwa njia mbali mbali zikiwemo kodi mbalimbali jambo ambalo linafanya maisha yao yaendelee kuwa magumu. Kwa mfano ukichukuwa jumla ya deni la taifa, ukaligawanya kwa idadi ya wananchi wote wa Tanzania, utakuta kwamba kila mtu (bila kujali mtoto mchanga, mzee, mlemavu, mwanafunzi, asiye na ajira nk) anadaiwa kiasi cha shilingi 526,977 kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali Na 1 hapa chini;

Jedwali Na. 1 Mgawanyo wa Deni la Taifa kwa Kila Mtanzania DENI LA TAIFA1 Shilingi 23,673,530,000,000 IDADI YA WATU TANZANIA2 44,928,923

Deni la taifa Idadi ya Watu = Deni la Taifa kwa kila mtu Hivyo; Sh. 23,673,530,000,000 44,928,923 =

Sh. 526,977

1 2

Deni la Taifa kwa Mujibu wa Hotuba ya Waziri wa Fedha ya tarehe 13 Juni, 2013 ni Shilingi Trilioni 23.7 Kwa Mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2012, Idadi ya Watu Tanzania ilikuwa ni 44,928,923

Page 10 of 52

Mheshimiwa Spika, ikiwa mtanzania masikini anayeishi chini ya dola moja au shilingi 1,500 kwa siku angeamua kulipa deni hili kwa shilingi 500 kwa siku ili abaki na shilingi 1,000 za kutumia kwa siku hiyo, itamlazimu kulipa shilingi 15,000 kwa mwezi kama malipo ya deni la taifa. Hii ina maana kwamba kwa mwaka mmoja atalazimika kulipa 180,000. Kwa maana hiyo, iwapo kila mtu angechukua jukumu la kulipa deni hili la taifa kwa kiwango hicho, ingechukua miaka mingi kumaliza kulilipa deni hilo. Mheshimiwa Spika, kiasi hiki cha fedha cha shilingi 15,000 ambacho kila mtanzania atatakiwa alipe kila mwezi kwa ajili ya deni la Taifa kingekuwa kinabaki kwa mwananchi na akakifanyia ujasiriamali angeweza kuondokana kabisa na umasikini. Hii ni kwa sababu kiwango hicho hakina riba na atakuwa anakipata kwa miaka mitatu mfululizo. Lakini kwa sababu Serikali imeamua kuwafukarisha wananchi wake kwa kukopa kupita kiasi, sasa mwananchi analazimika kurudi nyuma kimaendeleo kwa kutoa shilingi 15,000 kila mwezi kwa miaka mitatu mfululizo kulipa deni la taifa. Fedha hizo hazimjengi mwananchi kiuchumi bali zinambomoa kwa kuwa zinatoka bila faida yoyote kwake.
Page 11 of 52

Mheshimiwa Spika, serikali imekuwa ikijinasibu kuwa inakopa fedha hizi kwa ajili ya mitradi ya maendeleo. Lakini inashangaza kuwa fedha hizo zilizokopwa zimetumika lakini miradi hiyo ambayo imetumia fedha hizi haijaleta hayo maendeleo ambayo serikali imekuwa ikiyasema na kumwondolea mwananchi wa kawaida umasikini. Fedha hizo zimeendelea kutumika zikimwongezea mwananchi deni na umasikini. Hii inathibitishwa na uhalisia kwamba licha uchumi kukua kwa kasi ya asilimia saba kwa mwaka kwa miaka kumi mfululizo, umasikini umepungua kwa asilimia mbili tu na idadi ya watu masikini wa kutupwa imeongezeka kwa kiwango cha watu milioni mbili na nusu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Mheshimiwa Spika, hali ya hatari zaidi ni kwamba kuna madeni mengine ambayo hayajajumuishwa kwenye Deni la Taifa na hivyo kulifanya Deni halisi la Taifa kuwa kubwa kuliko linaloonyeshwa kwenye taarifa mbalimbali za Serikali na ile ya CAG. Kwa mfano, kuna madai ya PSPF ya shilingi bilioni 716.6 kati ya madai ya shilingi trilioni 6.5 ambayo Serikali imekubali kuyalipa. Mheshimiwa Spika, katika taarifa hiyo ya CAG ya mwaka 2012, kuna jumla ya shilingi bilioni 619 ambazo zipo kwenye Deni la Taifa lakini hazina vithibitisho. Katika ripoti yake Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameandika: Uhakiki wa mchanganuo wa madeni ya Taifa kama ulivyokuwa tarehe 30 Juni 2012 ulibaini kuwepo kwa marekebisho ya Deni ya shilingi 619.8 bilioni ambao uongozi haukuweza kutoa maelezo ya kuridhisha.
Page 12 of 52

Udhaifu kama huu unazua hisia kwamba kitengo cha Deni la Taifa kinatumika kuiba fedha za umma kwa kisingizio kwamba ni malipo ya Deni la Taifa. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inaitaka Serikali kutoa maelezo yaliyonyooka mbele ya Bunge hili kuelezea ni kwanini shilingi bilioni 619.8 zimeongezwa kwenye deni la taifa bila maelezo wala vielelezo vyovyote? Uhimilivu wa Deni la Taifa Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa muda mrefu imekuwa ikiitaka Serikali ipunguze au iachane kabisa na mikopo yenye masharti ya kibiashara ambayo inazidi kuliongeza Deni la Taifa. Kinyume na nia hii njema ya Kambi ya Upinzani ya kujitegemea kibajeti, Serikali hii ya CCM imeendelea kupuuza mawazo haya mazuri kwa kisingizio kwamba Deni la Taifa ni himilivu na kwamba nchi yetu inakidhi vigezo vya kimataifa vya kukopesheka. Mheshimiwa Spika, kwa taarifa ni kwamba baadhi ya vigezo vya kimataifa ambavyo Serikali inasema Tanzania imekidhi na hivyo inaweza kukopesheka vimeshapitiliza ukomo wake na kwa maana hiyo deni la taifa sio himilivu tena (Tazama Jedwali Na. 3). Jedwali Na. 3 Matokeo ya Upimaji wa Uhimilivu wa Deni la Taifa
Kiashiria la Taifa Page 13 of 52 Matokeo (Asilimia) Ukomo 50

Deni la Taifa kwa sasa/Pato 18.9

Chanzo: Kitabu cha Hali ya Uchumi 2012 uk. 77

Mheshimiwa Spika, matokeo ya upimaji wa uhimilivu wa deni la taifa uliofanywa na Serikali kwa kutumia kigezo cha asilimia ya uwiano wa Deni la Taifa na Pato la Taifa si ya kweli kwani kwa kutumia hesabu rahisi tu za kugawanya na kutafuta asilimia ambazo mwanafunzi wa darasa la pili anaweza kufanya ni kwamba tayari tumeshavuka ukomo wa kukopesheka. Hii ni kwa sababu uwiano wa deni la taifa na pato la taifa kwa sasa ni asilimia 53 wakati ukomo wa kukopesheka ni asilimia 50. (Tazama Jedwali Na. 3) Jedwali Na. 3 Uchambuzi wa Ustahimilivu wa Deni la Taifa
Kiashiria Deni la Taifa Pato la Taifa 23.7tr 44.7tr = 0.53 0.53x100 = Matokeo (asilimia) Ukomo

53.02%

50

Chanzo: Uchambuzi wa Kambi ya Upinzani

Utata katika Deni la Taifa (Fungu 22) Mheshimiwa Spika, mfumo wa sasa wa kuweka pamoja malipo ya Deni la Taifa na malipo kutoka mfuko mkuu wa Hazina hauweki uwazi wa kutosha. Jambo lenye utata katika fungu 22 - Deni la Taifa - ni kwamba fungu hilo linajumuisha huduma za Mfuko Mkuu wa Hazina (Consolidated Fund Services - CFS). Kwa mujibu wa Randama ya Wizara ya Fedha, Idara ya Mhasibu Mkuu, Fungu 22 Deni la Taifa - jumla ya shilingi 870,717,882,000 zimetengwa ndani ya
Page 14 of 52

Mfuko Mkuu wa Hazina (ambazo zimechanganywa pamoja na Deni la Taifa) kwa ajili ya ajili ya malipo mbalimbali kama ilivyooneshwa kwenye jedwali Na 4. Jedwali Na 4. Bajeti kwa ajili ya CFS Others
S/N NDANI YA CFS OTHERS KUNA MATUMIZI YAFUATAYO FEDHA ZILIZOTENGWA 2013/2014 1. Mishahara ya Majaji, Makamishna wa Tume ya Haki za 6,311,772,000 Binadamu na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali 2. 3. 4. Mafao ya Wastaafu wanaofanya kazi kwa Mkataba Stahili za Majaji Serikali za Mitaa kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. 5. Malipo ya Pensheni kwa ajili ya wastaafu hai, Mirathi, 213,498,000,000 watumishi walio katika Mikataba Serikalini na Stahili za Majenerali kwa kila mwezi 6. 7. 8. Gharama za Huduma za Benki (bank charges) Ada ya Usimamizi wa Amani za Serikali 6,400,000,000 1,700,000,000 3,757,060,000 1,844,840.000

Michango ya Mwajiri kwa Watumishi wa Serikali Kuu na 556,809,310,000

Riba ya Mapungufu kati ya Mapato na Matumizi (Interest on 80,000,000,000 net deficit position)

Gharama za usafiri na malazi na posho kwa ajili ya uhakiki 396,900,000 na usuluhuishi wa taarifa za madeni. JUMLA 870,717,882,000

Chanzo: Randama ya Wizara ya Fedha (Fungu 22) uk. 17

Page 15 of 52

Mheshimiwa Spika, mbali ya hayo fungu 21 kasma 290700 contingencies non-emergency kasma ndogo 290704: Domestic Debts - Sh 436,721,151,000 ambayo matumizi yake yanaonyeshwa kama: gharama za upigaji kura za maoni, kuhuisha Daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi ujao, kulipia madeni ya wakandarasi na watumishi, gharama za Bunge la Katiba, deni la HESLB kwa mfuko wa PSPF, mfuko wa maendeleo ya Jimbo, Ukaguzi wa shule za msingi na Ssekondarina mengine mengi. Kambi Rasmi ya Upinzani inaona kuwa matumizi haya hayana mtiririko unaoeleweka. Kambi inaamini kuwa kuna uwezekano mkubwa fungu hili likatumika kuweka fedha ambazo badaye zitakuja kukwapuliwa na wajanja. Hivyo basi, inamtaka Mheshimiwa Waziri wa Fedha atoe uchambuzi wa gharama ya kila kimoja kwani kurundika mambo yote kwenye kapu moja kunaweza kusababisha jambo moja kulipwa hata mara kumi na kusiwepo ushahidi wake wa malipo na pia watu wakikosa ushahidi wa kuhoji. Mheshimiwa Spika, kitendo cha kuchanganya deni la taifa na matumizi haya ya fedha yanayohusu Mfuko Mkuu wa Hazina kunaweza kutoa mwanya mkubwa wa ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kisingizio cha Deni la Taifa. Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inataka mambo makubwa mawili yafanyike kama kama ifuatavyo:

Page 16 of 52

1. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanye ukaguzi maalum (Special Audit) katika kitengo cha Deni la Taifa (fungu 22) ili tuweze kujua mikopo hii tunayoichukua kila wakati inatumika kufanyia nini, na miradi iliyotekelezwa kama ni miradi ya kipaumbele kwa mujibu wa mpango wa taifa wa maendeleo. Aidha, ukaguzi huu maalum utatuwezesha kama taifa kujua kiwango halisi cha Deni la Taifa ambalo tunadaiwa. 2. Serikali itenganishe haraka iwezekanavyo deni halisi la Taifa na matumizi mengine yanayohusu Mfuko Mkuu wa Hazina (Consolidated Fund Services Others) ili kuziba mianya ya ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kisingizio cha Deni la Taifa. Tunapendekeza kwamba Fungu namba 22 liwe la Deni la Taifa pekee na Fungu lingine litengenezwe kwa ajili ya CFS.

3.0 UCHAMBUZI WA BAJETI YA SERIKALI. 3.1 KODI KWENYE MAFUTA Mheshimiwa Spika, Waziri wa Fedha ameendeleza utaratibu wa kila mwaka wa kupandisha kodi kwenye bidhaa zile zile ikiwemo mafuta bila kutilia maanani kuwa kufanya hivyo kunahatarisha maisha ya wananchi kwani kutaongeza gharama ya karibu kila kitu. Hotuba ya
Page 17 of 52

bajeti iliyowasilishwa na Serikali haijalenga kabisa katika kukuza ustawi wa wananchi badala yake imejikita katika kuongeza mzigo mkubwa wa umasikini kwa wananchi, kuongeza mfumuko wa bei na kuzorotesha uchumi wa Tanzania kama nitakavyoelezea hapa chini. Wakati Bajeti ya mwaka 2012/13 ililenga kupunguza gharama za maisha kwa mwananchi, Bajeti ya Mwaka 2013/14 kwanza haina malengo mahususi na pili inafuta mafanikio yote yaliyopatikana katika sera ya Bajeti ya mwaka uliotangulia. Mheshimiwa Spika, moja ya vyanzo vipya vya mapato kwa mujibu wa hotuba ya bajeti ya Waziri wa Fedha ni pamoja na ongezeko la ushuru wa mafuta kama ifuatavyo. i. Ushuru wa Dizeli umeongezwa kutoka shilingi 215 kiwango cha sasa kwa lita hadi shilingi 217. ii. Ushuru wa Petroli umeongezwa kutoka shilingi 339 kiwango cha sasa kwa lita hadi shilingi 400, ikiwa ni ongezeko la shilingi 61. Mheshimiwa Spika, Bajeti imeongeza pia tozo kwenye mafuta (fuel levy). Kwa mujibu wa maneno ya Waziri kwenye hotuba yake ni kwamba ameongeza tozo kwenye petroli peke yake lakini ukweli ni kwamba, ongezeko hilo litaiathiri pia bei ya dizeli na hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta Sura 220 (the Road and Fuel Tolls Act). Neno fuel limetafsiriwa kama petroli aina ya supa, au kawaida, na dizeli kwa matumizi ya kuendeshea gari
Page 18 of 52

("fuel" means petrol, whether super or regular, and diesel for use in the propulsion of a vehicle). Mheshimiwa Spika, kwa mapendekezo hayo ya Serikali, shilingi 63 kwa lita inaongezeka kwenye gharama za mafuta. Hii itaathiri bei ya mafuta ya dizeli na petroli, na si petroli peke yake. Hata hivyo, hilo si ongezeko peke. Kuna ongezeko zaidi lipo kwenye mapendekezo ya Serikali kupitia hotuba ya Waziri wa Fedha Ukurasa wa 77 la ushuru wa Petroli (petroleum levy) wa kiwango cha shilingi 50 kwa lita. Mheshimiwa Spika, ni vyema Bunge lako tukufu na wananchi wakaelewa kwamba petroleum inahusisha nishati zote za mafuta katika hali ghafi kwa kuwa aina nyingine zote za mafuta zinatengezwa kutokana na petroleum), ikiwa ni pamoja na gesi katika hali kimiminika (liquid gas), grisi (grease), parafini (paraffin) dizeli, mafuta ya taa, mafuta ya ndege. Na kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi wa Petroleum - the Petroleum (Conservation) Act, Sura ya 392, Petroleum imetafisiriwa kama ("petroleum" includes any inflammable liquid or liquid gas made from petroleum, coal, schist, shale, peat, or any other bituminous substance or from any product of petroleum). Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa hotuba hiyo, majumuisho ya maongezeko mahusui ya moja kwa moja ya ushuru katika mafuta ya dizeli, petroli, na mafuta ya taa, na ongezeko la ujumla la petroleum yanatoa jumla inayoonekana kwenye jedwali hapa chini.
Page 19 of 52

AINA

YA ONGEZEKO FUEL LEVY MAHUSUSI (shilingi) (shilingi) 63 63 -

ONGEZEKO (shilingi) 50 50 50

LA JUMLA (shilingi) 115 174 50

MAFUTA

JUMLA(PETROLEUM)

Dizeli Petroli Mafuta ya taa

2 61 -

Mheshimiwa Spika, ongezeko hili ni dhahiri kuwa linakwenda kuongeza gharama za usafirishaji mali, gharama za usafirishaji chakula, gharama za uzalishaji malighafi na bidhaa kwenye viwanda vidogo na vikubwa, yanaenda kuongeza mfumuko wa bei, na matokeo yake kupaisha gharama za maisha kwa jumla yake na kudumisha umasikini nchini. Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inapinga kubadilisha sheria ya Petroli sura 392 na kuongeza kitu kinaitwa Petrolium Levy kwa ajili ya kuongeza shilingi 50 kwa kila lita ya mafuta na ziweze kupelekwa REA. Kiasi ambacho kitakusanya kupitia ushuru huu ni shilingi bilioni 123.725 kwa mwaka ujao wa fedha.

Page 20 of 52

Hatupingi wazo la kuongeza fedha kwa ajili ya REA, siku zote kambi ya Upinzani imekuwa ikitaka REA kuwezeshwa zaidi ili kubadilisha maisha ya wananchi vijijini kwa kuwapa nishati ya Umeme. Fedha hizi zingeweza kupatikana kwa njia nyingine ambazo hazimuumizi mwananchi. Serikali imekwepa jukumu la kupunguza matumizi yasio ya lazima ili kupata fedha za miradi ya maendeleo na badala yake inakwenda kwenye njia rahisi lakini zenye kumuumiza mwananchi. Ikumbukwe kwamba mwaka 2012/13 Bunge lilitenga zaidi ya shilingi bilioni 300 kwa ajili ya umeme vijijini lakini fedha zote hizo hazikwenda REA na badala yake zikaenda kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya kukodi ili kuzuia mgawo wa umeme. Hakuna dhamana yeyote kuzuia fedha hizi zitakazopatikana kutokana na kuongeza ushuru wa mafuta kwenda kuwanufaisha asilimia 18 tu ya Watanzania ambao wameunganishwa kwenye mtandao wa umeme. Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Bajeti Mheshimiwa Waziri amependekeza kufanywa kwa marekebisho ya sheria ya ushuru wa mafuta na kuongeza kodi ya fuel levy kutoka shilingi 200 kwa lita hadi shilingi 263 kwa lita kiasi ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia 31.5. Waziri wa Fedha amesema hatua hii inalenga kuiongezea serikali mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 155.893 katika mwaka ujao wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara. Kambi ya Upinzani Bungeni inapinga nyongeza hii kwani itaongeza gharama za maisha kwa mwananchi.
Page 21 of 52

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba Bunge likatae mapendekezo yote ya kuongeza kodi kupitia The Road and Fuel Tolls act Sura ya 220, Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura 147 eneo la Ushuru za bidhaa za Petroli na Sheria ya Utafutaji Mafuta, sura ya 392. Mapendekezo haya ya Serikali yataongeza gharama za maisha kwa mwananchi masikini. Mapato yatakayopotea kutokana na kukataa mapendekezo haya yatafidiwa na hatua za kiutawala na kikodi tutakazopendekeza ikiwemo kupunguza matumizi, kupunguza misamaha ya kodi na kuzuia utoroshaji fedha.

3.4 SHERIA YA KODI YA MAPATO sura 332 NA USHURU WA BIDHAA SURA 147 Mheshimiwa Spika, Serikali inapendekeza mabadiliko kwenye sheria ya kodi ya mapato ikiwemo kupunguza kiwango cha chini cha kulipa PAYE na kuanza kutoza kodi kwenye huduma za kusafirisha fedha kwa kupitia simu za mkononi. Vile vile Serikali inataka kubadilisha sheria ya ushuru wa bidhaa kwa kuwalipisha kodi wananchi asilimia 14.5 kwenye huduma zote za simu za mkononi (all mobile phone services) na kwamba asilimia 2.5 ziende kugharamia elimu nchini. Mheshimiwa Spika, ushuru wa bidhaa huu ni janga jingine kwa wananchi, kwani mpaka sasa wananchi wamekuwa wakitozwa
Page 22 of 52

pesa nyingi na kampuni kugharamia simu za mkononi, huku kampuni zikikwepa kodi kwa kutokutoa taarifa sahihi juu ya kiasi gani cha faida yanapata, na wakati huo Serikali haina uwezo wa kujua ni kiasi gani hasa cha simu zinazopigwa na faida halisi ambayo kampuni hizi zinaipata. Mheshimiwa Spika, Kilio cha wananchi ni kampuni za simu kulipa kodi ya mapato na sio kuhamisha ulipaji kodi na kuwabebesha watumiaji. Serikali badala ya kupambana na kampuni zenye nguvu kwa kuweka utaratibu wa kudhibiti matumizi yao ya uwekezaji, imeamua kumlalia mwananchi mnyonge kwa kuongeza ushuru na hivyo kuongeza gharama za mawasiliano. Mheshimiwa Spika, Serikali inapanga pia kutoza kamisheni ya asilimia 10 kwa mawakala wa huduma za mihamala ya pesa kwa njia ya simu (mobile money transfer/transactions) kama njia ya kuongeza mapato. Katika hotuba ya msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia tuliitaka Serikali itoze kodi na ushuru kwenye pesa kwa njia ya simu, lakini tulitahadharisha kwamba mzigo huo wa kodi usibebeshwe kwa wananchi bali kampuni za simu. Kwamba kampuni zilipe kutokana na faida zinazozipata kwa sababu kwa mujibu wa sheria (the Banking and Financial Institutions Act, 2006). Lakini cha ajabu Serikali hii ya CCM imendelea kuziogopa kampuni za simu na imezua pendekezo ya kuwatoza asilimia 10 mawakala, huku ikiziacha kampuni zikipeta.
Page 23 of 52

Mheshimiwa Spika, Tozo hili jipya kwenye usafirishaji wa fedha ni tozo linayobagua (discriminatory) kwa misingi kwamba wanaotuma fedha kwa njia za mabenki hawatozwi kodi kama hii. Ni dhahiri mabenki yanapiga vita mobile money transfer na hivyo Serikali imeshawishiwa na mabenki kuongeza gharama za utumaji fedha ili kuua sekta hii inayokua kwa kasi na inayohudumia wananchi masikini kabisa. Katika Azimio la Bunge kuhusu Watanzania wanaotorosha fedha na kuzihifadhi nje ya nchi, Bunge liliazimia kwamba Serikali ianzishe kodi ya financial transaction tax ili kuweza kusimamia vizuri utumaji na upokeaji wa fedha katika njia za mabenki. Kambi ya pinzani inapendekeza kuwa tozo hili jipya kwenye mobile money transfer litumike iwapo tu tozo kama hili litawekwa kwenye utumaji fedha kwa njia za benki na njia nyinginezo. Vingenevyo tozo hili ni la kibaguzi na linapendelea watu wenye uwezo mkubwa dhidi ya wanyonge na hivyo tunatoa wito kuwa pendekezo hili lisikubaliwe na Bunge. Aidha, tunaendelea kupinga ongezeko hili la ushuru kwa kuwa sekta hii ya mawasiliano ndio inaongoza katika kuchangia fedha nyingi kwenye pato la taifa kuliko sekta nyingine yeyote hapa nchini. Sekta hii huchangia asilimia 36.5 ya pato la taifa. Kwa mfano kwa mwaka 2012/2013 sekta hii ilichangia shilingi bilioni 287 wakati pombe, hasa bia, ikichangia shilingi bilioni 214 na sigara shilingi bilioni 99.
Page 24 of 52

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza mabadiliko ya Sheria ya Mawasiliano (EPOCA) ya mwaka 2009 ili kuipa TCRA mamlaka ya kufanya ukaguzi wa uwekezaji unaofanywa na kampuni za simu hapa nchini kwa lengo la kuzuia ukwepaji kodi unatokana na kudanganya gharama za uwekezaji. Kupitia TMAA ianyokagua migodi Serikali imeweza kuokoa kodi nyingi sana. Hivyo tunataka TCRA ifanye kazi hiyo ya kukagua gharama za uwezekaji zinazofanywa na kampuni za simu. Kambi ya upinzani Bungeni inatarajia kuwa sekta ndogo ya mawasiliano itaweza kuchangia sio chini ya asilimia 10 ya mapato ya ndani. 3.4.1 PAYE Mheshimwia Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kushusha PAYE kutoka asilimia 14 ya sasa mpaka asilimia 9 na kiwango cha chini cha kutoza PAYE kiwe ni Sh 250,000 kwa mwezi. Hii itawezesha wananchi wa kipato cha chini kubakia na fedha za kutosha na kutumia kwenye matumizi ili kuchochea uzalishaji nchini. Uamuzi wa Serikali wa kushusha PAYE kwa asilimia moja tu (sawa na shilingi 1,900 kwa mwezi) ni kiini macho na haina maana yeyote na kwa kweli ni matusi kwa wafanyakazi wa Tanzania. 3.4.2 Tax Returns Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba kwa kuwa utaratibu wa vitambulisho vya taifa umeanza na tayari sehemu fulani ya wananchi wamepewa vitambulisho na kwa kuwa kwa
Page 25 of 52

kupitia mfumo wa TIN na usajili wa magari kuna watanzania wengi sana wana rekodi za kikodi ni vema sasa sheria ya kodi ya mapato sura 332 ifanyiwe marekebisho ili kulazimisha kila mwananchi ajaze tax return awe au asiwe na kipato. Hii itawezesha sana kupanua wigo wa kodi kwa kuongeza idadi ya walipa kodi hapa nchini ili kufikia lengo la anagalua Watanzania milioni 4.5 ambao wanalipa kodi kutoka milioni moja wa sasa. 3.4.3 Kodi ya Ongezeko la thamani (VAT) Mheshimiwa Spika, Serikali inapendekeza mabadilko kadhaa

kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani VAT ikiwemo kuondoa ushuru wa gharama sifuri kwenye viwanda vya nguo na kuweka unafuu wa VAT (kutoka jedwali la kwanza kwenda jedwali la tatu). Pia Serikali inapendekeza kufanya mabadiliko kwa kuondoa msamaha wa VAT kwenye sekta ya Utalii. Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba mfumo mzima wa zero rating uondolewe na badala yake kwa bidhaa zenye umuhimu na zilizopo kwenye jedwali la kwanza zipelekwe jedwali la tatu kama special relief. Pendekezo hili linatokana na ukweli kwamba mfumo wa zero rating hauonyeshi mafanikio makubwa, hupoteza mapato kwa sababu ya kutumika vibaya na kuwa na tatizo la cash flow kwa wazalishaji wengi. Nchi jirani ya Kenya, katika muswada wake wa sheria ya VAT, imependekeza kuondoa mfumo mzima wa zero rating.
Page 26 of 52

4.0 UWEKEZAJI NA MISAMAHA YA KODI Mheshimiwa Spika, Kwa muda mrefu sana tumekuwa tukijadiliana kuhusu misamaha ya kodi kama kivutio cha uwekezaji nchini. Serikali kupitia sheria ya uwekezaji nchini hutoa nafuu lukuki kwa wawekezaji ili kuleta mitaji yao nchini. Tanzania inatoa pia nafuu za kisekta, mathalani kilimo kinapata nafuu ya asilimia ishirini (20%) ya mtaji kwa kuandaa mashamba. Kampuni za uchimbaji madini zinazochimba madini ya dhahabu, shaba, makaa ya mawe, lime, nickel n.k yanapata nafuu ya asilimia mia moja (100%). Utalii inapata nafuu ya asilimia kumi (10%). Mheshimiwa Spika, pamoja na uvutiaji wa uwekezaji toka nje kupitia motisha za kikodi; bado fursa za ajira ni ndogo, bado hakuna urari wa biashara, bado maendeleo ni kidogo sana katika teknolojia. Na hii ni tasfiri kwamba motisha za kodi zinazotolewa kwa wawekezaji hazitoi matunda yanayokusudiwa, badala yake zimeendelea kuinyima mapato serikali. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali ya CCM ifahamu kuwa si motisha za kodi peke yake zinazoweza kuwavutia wawekezaji, bali hali ya utulivu wa kiuchumi na kisiasa, uwepo wa rasilimali za asili na rasilimali watu, utulivu wa soko la ndani, uimara wa pesa ya ndani (local currency), uwazi na kutokuwepo kwa rushwa, ni vigezo ambavyo kwa pamoja vinawavutia wawekezaji.
Page 27 of 52

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kitabu cha utafiti wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (Lessons From Selected Cases of Tax Simplification Reforms and Tax Expenditure Budgeting) cha mwezi Machi 2012, Tanzania ni moja nchi zenye huruma katika kulipisha kodi vyanzo vyake kiasi cha kuzorotesha uwezo wake wa kukusanya mapato yake ya ndani na hivyo kushindwa kutekeleza miradi yake ya maendeleo. Kwa mujibu wa taarifa za TRA (TRA Monthly Revenue Report) misamaha ya kodi kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Ushuru wa Forodha (custom) peke yake imeipotezea Tanzania wastani wa asilimia 4.3 (4.3%) ya Pato la Taifa kati ya mwaka 2006/2007 - 2010/2011. Mheshimiwa Spika, asilimia 4.3 (4.3%) ya pato la Taifa ni sawa na Shilingi za kitanzania trillion moja, bilioni mia tisa ishirini na mbili, milioni mia nane hamsini na tisa, kaki tano na tisa elfu (1,922, 859, 509,000/). Wakati Serikali inapoteza fedha zote hizi kama misamaha ya kodi, Serikali hiyo hiyo inakwenda kukopa Uchina kiwango kama hicho cha fedha kwa ajili ya kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam. Mheshimiwa Spika, kiasi hicho cha pesa kingetosha kulipa deni la Shilingi 33,442,156,55, madai yote ya walimu ya malimbikizo ya mishahara, likizo, uhamisho, masomo, matibabu, kujikimu, ajira mpya, na mengineyo na kubaki kiasi cha Shilingi 1,919,515,293,345 pesa ambazo zingeweza kutumika kulipa askari polisi wote nchini, madaktari na watabibu, askari magereza wote.
Page 28 of 52

Mheshimiwa Spika, kiasi hicho kingeweza, kama mbadala, kutumika kujenga shule, kununua vitabu, kujenga zahanati na kununua dawa, kujenga viwanda na hivyo kupanua ajira. Kuboresha maisha ya wakulima na wafugaji, kupeleka nishati ya umeme vijijini n.k. Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba misamaha yote ya Kodi iwekwe wazi na ikaguliwe na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Ikumbukwe kwamba misamaha ya kodi ni ruzuku ya Serikali kwa wanaofaidika na misamaha, hivyo ni matumizi kama matumizi mengine yeyote ya Serikali na hivyo ni lazima yakaguliwe na ukaguzi wake kuwekwa wazi kama taarifa nyingine za CAG. Mheshimiwa Spika, Suala la kuweka wazi misamaha ya kodi na kufanyiwa ukaguzi lilishughulikiwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Mamlaka ya Mapato Tanzania ambapo suala hili lilikubalika na Waziri wa Fedha alipaswa kuliwekea utaratibu wa kisheria kwenye Sheria ya Fedha mwaka huu. Jambo la kushtusha ni kwamba Serikali imekaa kimya kabisa kuhusu jambo hili na hivyo kuonyesha kwamba Serikali imewekwa mfukoni na wanaofadika na misamaha hii. Hakuna namna nyingine ya kueleza zaidi ya kusema kwamba Serikali imeshindwa nguvu na makampuni, taasisi na watu binafsi wanaopinga mabadiliko kwenye mfumo wa misamaha ya kodi, wanaopinga uwazi na wanaopinga ukaguzi wa misamaha yao.
Page 29 of 52

Kama si hivyo, basi ni vema Mheshimiwa waziri wa Fedha akalibainisha suala hilo katika Sheria ya fedha na aeleze hivyo kinaga ubaga katika majumyuisho yake.

4.1 UKWEPAJI KODI Mheshimiwa Spika, Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zenye tatizo kubwa la ukwepaji wa kodi unaofanywa na kampuni kubwa za kimataifa zilizowekeza, kampuni za ndani na watu binafsi. Watu na kampuni wanaokwepa kodi hutoa taarifa za uongo juu ya mauzo na faida zao, na kuonyesha kwa udanganyifu kuwa wamepata hasara. Tafiti nyingi ikiwemo Ripoti ya Benki ya Dunia (2008) zinaonyesha kuwa ukwepaji kodi ni tatizo kubwa Tanzania kuliko nchi tunazopakana nazo. Kwa mujibu wa ripoti Benki ya Dunia kampuni nyingi Tanzania hutoa taarifa kwa kiwango cha asilimia 69 tu ya mauzo yake, ukilinganisha na asilimia 77 nchini Uganda, na asilimia 86 huko Kenya. Kampuni hapa nchini zinakuwa na vitabu viwili vya hesabu; kimoja wanaandika hesabu za kweli na kingine wanaandika taarifa za uongo kwa madhumuni ya kupunguza kodi. Lakini hiyo ni njia moja tu. Mheshimiwa Spika, njia nyingine inayotumika na kampuni hizo kukwepa kodi ni kutotoa taarifa za mauzo ya nje, kufanya biashara
Page 30 of 52

nje ya nchi kimagendo (kupitia njia za panya). Kwa mujibu wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (East African Business Council) mwaka 2008 kiasi cha biashara ya thamani ya Dola za Marekani milioni 602 ($ 602 Milioni) zilifanyika kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania, pale Namanga peke yake. Mheshimiwa Spika, mfano mmoja dhahiri wa ukwepaji kodi kwenye mauzo ya nje umeonyeshwa na utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia katika Bandari ya Dar es Salaam na Bandari nyingine hapa nchini kuhusu mauzo nje ya zao la korosho ghafi. Mwaka 2011 Tanzania iliuza kwenda nchini India korosho kiasi cha tani 80,000 kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania na Benki Kuu ya Tanzania. Hata hivyo, idara ya Forodha ya India inaonyesha katika mwaka huo, nchi hiyo ilikuwa imenunua tani 120,000 za korosho kutoka Tanzania. Hii maana yake ni kwamba jumla ya tani 40,000 ya korosho ambazo ni sawa na theluthi moja ya korosho zote zilizopaswa kuwa zimeuzwa nchini India na nusu ya korosho zilizoripotiwa kuwa Tanzania imeuza nchini India hazikuripotiwa na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa sana kiwango cha kodi ambacho serikali ilipaswa kukusanya. Pia, tofauti hiyo ilipunguza urari wa mauzo nje. Mheshimiwa Spika, hivi karibuni tumeshuhudia taarifa za ukwepaji mkubwa sana wa kodi ya forodha kufuatia wafanyabiashara wasio waaminifu kutumia vibaya mfumo wa kutoa mizigo. Ikumbukwe kwamba Bunge lako tukufu katika mwaka wa fedha wa 2008/09
Page 31 of 52

lilipinga mfumo wa kuruhusu wafanyabiashara wakubwa kutoa mizigo yao bila kukaguliwa. Bidhaa nyingi zilizoagizwa hazikulipiwa kodi kwa sababu ama hazikuwa zimeorodheshwa kwenye nyaraka zilizowasilishwa idara ya forodha au kulifanyika udanganyifu wa aina ya bidhaa. Kwa mujibu wa taarifa za TRA, ukaguzi wa mizigo uliofanyika kati ya Aprili na Juni 2013 unaonyesha kwamba jumla ya shilingi bilioni nne ziliokolewa. Mheshimiwa Spika, kuna mtandao mzito wa wafanyabiashara wakubwa hapa nchini kwa kushirikiana na maafisa wa forodha wanafanya njama za kukwepa kodi. Kumekuwa na vita vya kibiashara miongoni mwa wafanyabiashara, vita ambayo imewagawa maafisa wa forodha wasio waaminifu na kujikuta kufanya kazi za wafanyabishara wakubwa. Kumekua na uonevu mkubwa dhidi ya wafanyabiashara wadogo na wanaoibukia unaofanywa na wafanyabaishara wakubwa na wa muda mrefu. Hakuna haki kabisa katika ukaguzi wa mizigo jambo linalosababisha wafanyabiashara wadogo wengi wa Kariakoo kuumizwa kutokana na hila za wafanyabishara wakubwa wanaoshirikiana na maofisa wa idara ya forodha. Mheshimiwa Spika, hii inathibitishwa na Taarifa ya ukaguzi wa thamani ya Fedha (Value for Money Audit Tanzania Revenue Authoritys New Customs system) iliyotayarishwa na Bert Cunningham kutoka Canada. Taarifa hiyo inaonyesha kuwa maofisa
Page 32 of 52

wa forodha wanashirikiana na mawakala wa mizigo na wafanya biashara (Clearing and Forwarding Agents) kuonyesha kiwango kidogo cha mizigo inayoingizwa nchini au thamani ndogo ya mizigo kwa lengo la kukwepa kulipa kodi stahiki. Kutokana na ukosefu wa maadili, rushwa na uzembe wa maafisa wa forodha, Taifa hupoteza mapato ya zaidi ya asilimia 15 ya kiwango kinachokusanywa na Idara ya Forodha kwa mwaka. Katika mwaka wa Fedha 2012/13 jumla ya shilingi bilioni 477 zimepotea kupitia idara ya forodha peke yake. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina mashaka makubwa sana kwamba ukwepaji kodi kwenye eneo la kodi ya forodha ni mkubwa mno kuliko inavyoripotiwa hivi sasa. Vyombo vya habari vinavyoandika habari hizi, vinaandika kutokana na taarifa ambazo zimekipata kuitoka kwa chanzo chao ambacho aghalabu huwa hakina taarifa zote na za kina. Hivyo, ni dhahiri kuwa kinachoandikwa ni sehemu tu na ukweli wote hausemwi. Kambi ya Upinzani Bungeni, kwa mujibu wa kanuni ya 117 italeta hoja Bungeni kutaka kuundwa kwa kamati teule ya Bunge kuchunguza Mfumo wa Forodha na ukwepaji kodi katika idara ya Forodha ya Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa lengo la kuhakikisha ukwepaji kodi unadhibitiwa na wahujumu wote wanachukuliwa hatua stahili za kisheria.

Page 33 of 52

Mheshimiwa Spika, suala la ukwepaji wa kodi linahusu pia wanasiasa wakiwamo Wabunge. Ni dhahiri wabunge wana stahili za kisheria za kupata msamaha wanapoagiza magari yao nk. Tunatoa wito kwa wabunge ambao ni wafanyabiashara waliosajili biashara zao katika Kituo cha Uwekezaji yaani TIC na kupata vyeti vya misamaha ya kodi wawe wa kwanza kuhakikisha kuwa hawatumii misamaha hiyo vibaya. Hatuwezi kuwa mbele kukemea misamaha ilhali sisi wenyewe tunaitumia vibaya misamaha hiyo. Ni dhahiri kabisa kwamba inapaswa kuwa ni aibu kwa mbunge kutumia msamaha wa kodi aliopata kununua kitanda, magodoro na mambo kama hayo. Sisi wabunge tutembee kwenye maneno yetu ikibidi hata kwa kukataa misamaha hii mikubwa ya kodi tunayopewa. Natumai baada ya CAG kuanza kukagua misamaha ya kodi kama matumizi mengine yeyote ya Serikali tutashuhudia aibu kubwa tutakayopata kwa kutumia vibaya misamaha ya kodi. Mheshimiwa Spika, hivi sasa dunia ipo kwenye ajenda ya kuzuia utoroshaji mkubwa wa fedha kupitia tax havens ambapo licha ya kwamba kuna fedha zinazotokana rushwa katika utoroshaji huu lakini pia kuna fedha nyingi zinazotokana na ukwepaji wa kodi (Tax evasion and tax avoidance). Taarifa ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (The joint report from the African Development Bank (AfDB) and Global Financial Integrity (GFI)) iliyotolewa jijini Marrakech nchini Morocco inaonyesha kuwa jumla ya dola za Marekani trilioni 1.4
Page 34 of 52

zimetoroshwa kutoka Afrika kati ya mwaka 1980 mpaka 2009 na hivyo kulifanya bara hili kuwa net creditor kwenye dunia. Sehemu kubwa ya Fedha hizi ni kodi inayokwepwa na kampuni kubwa zinazowekeza katika bara la Afrika. Sehemu nyingine ya fedha hizi zinatokana na udanganyifu katika akaunti ya Deni la Taifa ambapo madeni na riba za uwongo hulipwa kutoka Afrika. Mheshimiwa Spika, wakati dunia nzima ipo kwenye kampeni kubwa dhidi ya ukwepaji kodi unaofanywa na kampuni kubwa duniani zinazowekeza kwenye nchi zinazoendelea, Tanzania ipo kimya kabisa kana kwamba hakuna linalotokea. Licha ya kwamba Bunge la Tanzania ni Bunge la Kwanza katika nchi za SADC kupitisha Azimio kuchunguza utoroshwaji wa Fedha (Azimio la Bunge namba 9/2012), Serikali ya Tanzania imekaa kimya kabisa kupaza sauti yake kuhusu ukwepaji kodi mkubwa. Tanzania inapoteza mapato ya ndani sawa na asilimia tano (5) ya Pato la Taifa kupitia kodi za kimataifa ambayo ni sawa na shilingi trilioni mbili kila mwaka. Uchunguzi unaonyesha kwamba katika orodha ya walipa kodi wakubwa 10, kampuni saba zinatumia tax havens kukwepa kodi. Katika kampuni kubwa tatu za simu hapa nchini kampuni mbili zimesajiliwa tax havens za Uholanzi na Luxembourg na hivyo kukwepa kodi mbalimbali hapa nchini. Kampuni moja kubwa ya madini hapa nchini ina kampuni dada tisa (9) katika offshore hali kadhalika kampuni moja kubwa ya kutafuta mafuta na gesi hapa nchini. Katika mahojiano na gazeti la Financial
Page 35 of 52

Times la Uingereza la mwezi June, 2013 kampuni ya African Barrick Gold imetangaza kufunga baadhi ya kampuni zaidi ya 24 iliyoyasajili maeneo kama Cayman Islands. Mheshimiwa Spika, bila Serikali ya Tanzania kuamua kwa dhati kusafisha nyumba yake, hata juhudi kubwa zinazofanywa na asasi za kiraia kama Oxfam, ActionAid, Tax Justice Network nk katika kupambana na ukwepaji kodi na utoroshaji wa fedha hazitafua dafu. Wakati nchi za G8 zinaweka mipango ya kutusaidia na sisi kama nchi tuweke mipango yetu wenyewe. Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza hatua za awali zifuatazo zichukuliwe ili kukabiliana na utoroshaji mkubwa wa fedha unaotokana na ukwepaji wa kodi; (i) Tanzania ijiondoe kabisa katika mfumo wa kodi

unaopendekezwa na OECD (OECD model treaty) kwani mkataba huu wa kikodi unalinda kampuni kubwa za nje dhidi ya nchi changa kama Tanzania. (ii) Tanzania ijondoe katika mikataba yote ya kikodi na nchi ambazo ni tax havens kama Mauritius, Uingereza (City of London and British overseas territories), Luxembourg, Netherlands n.k. (iii) Kampuni yoyote ya ndani na nje yenye kampuni dada

zilizosajiliwa kwenye tax havens zitangaze bayana na kuweka

Page 36 of 52

wazi hesabu zao kwa miaka mitano iliyopita kwa ukaguzi wa TRA na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. (iv) Bunge litunge sheria kudhibiti matumizi ya tax havens

yanayofanywa na kampuni za uwekezaji na haswa kwenye sekta za Mawasiliano, Madini, Mafuta na Gesi na nyinginezo.

5.0 MAENDELEO YA MICHEZO Mheshimiwa Spika, maendeleo mazuri ya michezo katika taifa lolote, ni utambulisho mzuri wa taifa hilo katika mataifa mengine kutokana na ushirikiano wa kimichezo na mataifa hayo. Pamoja na mambo mengine, michezo katika nchi yetu inaweza kutumika kutengeneza fursa za kiuchumi kwa kuitangaza nchi yetu duniani katika sekta za utalii na uwekezaji. Ukiacha mbali suala la manufaa ya kiuchumi yanayoweza kupatikana kupitia michezo, michezo pia inawajengea vijana wetu afya na hivyo kuwa na taifa la watu wakakamavu. Kwa upande mwingine, michezo pia ni ajira. Inasikitisha kwamba katika hotuba nzima ya Waziri wa Fedha, hapakuwa na mpango wowote wa kukuza michezo hapa nchini bila hata kujali kwamba timu yetu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ipo katika nafasi nzuri sana hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote katika kuweza kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia mwakani.

Page 37 of 52

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika barua yake ya tarehe 5/4/2013 iliomba Kamati ya Bajeti kuangalia namna ya kusaidia kupata fedha za kujenga michezo na hasa kusaidia Taifa Stars katika juhudi zake za kuelekea kufuzu kwenye michuano ya kombe la Dunia huko Brazil. Hata hivyo Wizara ya Fedha haikutoa hata senti tano kwa ajili hiyo. Kamwe hatuwezi kufanikiwa kwenye michezo bila kuwekeza na kutegemea juhudi za dharura za kamati za kusaidia ushindi. Tukitaka tungae kwenye michezo ni lazima tuwekeze sana na kuwekeza ni gharama, gharama ambayo thamani yake ni kubwa sana kwa nchi. Mheshimiwa Spika, licha ya michezo kuliingizia taifa mapato kupitia asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) inayotokana na viingilio katika michezo mbalimbali, hakuna uwekezaji wowote wa maana uliofanyika kwenye michezo jambo ambalo ni hatari kwa uhai na maendeleo ya michezo hapa nchini. Aidha hakuna mipango madhubuti ya muda mrefu kuhusu maendeleo ya michezo hapa nchini. Kutowepo kwa mipango madhubuti na ya muda mrefu,

kumeshababisha timu zetu kufanya vibaya katika mashindano mengi ya kimataifa na hivyo kulifanya taifa letu lionekane kuwa ni taifa dhaifu au kichwa cha mwendawazimu kama alivyopata kusema Rais Mstaafu was Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi. Kambi Rasmi ya Upinzani, inatoa angalizo kwa Serikali kwamba, kamwe hatuwezi kufanikiwa katika michezo kwa mipango ya
Page 38 of 52

kukurupuka. Aidha ni aibu kwa Serikali kukusanya kodi kutokana na michezo, halafu vijana wetu wanakosa fedha ya nauli kwenda nchi nyingine kwa mashindano ya michezo mpaka wafanye harambee ya kukusanya fedha kwa wahisani. Hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inapendekeza mambo yafuatayo yafanyike ili kunusuru tasnia ya michezo hapa nchini; 1. Timu yoyote itakayowakilisha taifa katika mashindano yoyote ya kimichezo igharamiwe na Serikali kwa asilimia 100. 2. Viwanja vyote vya Michezo hapa nchini viundiwe Wakala wa Serikali, Wakala wa maendeleo ya michezo (Sports Development Agency). Wakala huo uwe na majukumu ya kujenga viwanja vipya na kusimamia viwanja hivyo kwa niaba ya Serikali. Viwanja vyote vya michezo vilivyoporwa na CCM kama Lake Tanganyika Kigoma, Ali Hasan Mwinyi - Tabora, Kirumba Mwanza, Maji Maji Songea nk virejeshwe Serikalini mara moja chini ya Wakala wa Viwanja vya Michezo. Wakala pia ujenge academies za michezo maeneo kama vile Mbeya, Tanga, Mtwara, Mwanza, Manyara na Dar es Salaam ili kukuza vipaji vya watoto na vijana. 3. Mashirika yote ya Umma, hasa mashirika makubwa yawe na timu za michezo. Ushauri uliotolewa na IMF na Benki ya Dunia dhidi ya Mashirika ya Umma kuwa na timu ulikuwa
Page 39 of 52

ushauri usio wa maana. Wenzetu Uganda kwa mfano, Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) wana timu katika ligi Kuu, ambayo ni moja ya timu mahiri katika ukanda huu wa bara la Afrika. 4. Serikali ianzishe Mfuko Maalum wa Michezo (Sports Fund). Pia, Serikali ianzishe Kodi ya Maendeleo ya Michezo (Sports Development Levy). Kodi hii ipatikane kama ifuatavyo: Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilimia 18 iliyokuwa ikikatwa kwenye viingilio katika michezo mbalimbali iondolewe na badala yake kiasi hichohicho kiingizwe kwenye Mfuko wa Michezo (Sports Fund) utakaoanzishwa. 5. Matumizi ya Mfuko wa michezo yawe kama ifuatavyo: i. Asilimia 50 ya fedha zitakazokusanywa zitumike kujenga miundombinu ya michezo (Sports Infrastructure) kupitia kwa Wakala wa Maendeleo ya Michezo na Academies. ii. Asilimia 50 inayosalia itumike kuhudumia maandalizi ya timu za Taifa.

6.0 UKUSANYAJI WA MAPATO YA ZIADA. 6.1 BANDARI YA DAR-KAMA KICHOCHEO CHA UCHUMI Mheshimiwa Spika, Bandari ya Dar es Salaam ni mlango mkuu wa biashara kwa asilimia 90 kwa nchi sita zisizokuwa na bandari za
Page 40 of 52

Zambia, Malawi, Rwanda, Burundi, Uganda na eneo la Mashariki ya nchi ya DRC. Toleo la tatu la taarifa ya Benki ya Dunia (Tanzania Economic Update) la mwezi Mei, 2013 inaonyesha kwamba Bandari ya Dar es Salaam inapoteza fedha na muda mwingi sana kwa watumiaji wa bandari hiyo kwa kulinganisha na Bandari yoyote katika mwambao wa Afrika ya Mashariki. Mheshimiwa Spika, taarifa hiyo ya Benki ya Dunia inasema kwamba familia za kawaida zingeweza kuepuka matumizi ya takriban dola za Marekani 147 au asilimia 8.5 kwa mwaka kama Bandari ya Dar es salaam ingekuwa inafanyakazi kama inavyofanyakazi Bandari ya Mombasa. Mheshimiwa Spika, kutokana na utafiti ni kwamba kama Bandari ya Dar es Salaam itaboreshwa na kubadili mtizamo (mind set) wa watendaji wake katika uwajibikaji ni dhahiri kwamba bandari ina fursa za kuongeza mapato ya Serikali yapatayo dola za Marekani bilioni 1.8 au shilingi trilioni 2.93 kwa mwaka au ongezeko la asilimia saba la pato la Taifa. Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza kuimarisha ufanisi wa Bandari kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014 na kufikia ufanisi wa asilimia hamsini (50%) jambo ambalo litawezesha kuongeza mapato ya ndani ya kiasi cha shilingi trilioni 1.46 6.2 Kudhibiti misamaha ya kodi
Page 41 of 52

Mheshimiwa Spika, katika mapendekezo ya namna bora ya kuongeza mapato ya serikali, Kambi Rasmi ya Upinzani tunapendekeza yafanyike marekebisha katika Sheria ya Uwekezaji na kuweka udhibiti wa thabiti katika kutoa misamaha na nafuu za kodi, tofauti na hali ilivyo sasa ambapo asilimia 4.3 ya pato la taifa linapotea kwa misamaha ya kodi. Kiwango hiki ni sawa na shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia tisa ishirini na mbili, milioni mia nane hamsini na tisa, Laki tano na tisa elfu (1,922, 859, 509,000/-). Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA

inapendekeza kudhibiti misamaha hiyo ili kuishusha na kufikia asilimia moja (1%) ya pato la taifa. Jambo hilo ni muhimu lifanyike kwa sababu kwa kufanya hivyo nchi itakuwa imeokoa shilingi Trilioni moja, Bilioni mia tano arubaini na tano, milioni mia sita themanini na mbili, laki nane na elfu sabini na tisa (1,545, 682, 879, 000). 6.3 Kodi ya Mauzo na Manunuzi ya Bidhaa kutoka Nje Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA inapendekeza kuanzishwa kwa kodi maalumu (Special Railways development levy) ya manunuzi na mauzo ya bidhaa nje. Tunapendekeza tozo ya asilimia moja (1 %) ya bei ya bidhaa zinazoagizwa toka nje na asilimia 0.5 (0.5%) ya thamani ya bidhaa kwa zile zinazouzwa nje. Mapato ya tozo hii maalumu yote yatumike kujenga miundombinu ya Reli hapa nchini.

Page 42 of 52

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa mwaka 2012 Tanzania iliagiza bidhaa kutoka nje ya nchi zenye thamani ya dola za Marekani milioni 10,324.9 ambazo ni sawa na shilingi 16,519,840,000,000 (bei ya kubadilisha dola 1 ni sawa na shilingi 1,600). Kwa maana hiyo, asilimia moja ya mapato ya manunuzi yote ya nje ni shilingi bilioni 165.2. Mauzo ya bidhaa nje ya nchi kwa mwaka 2012 yalikuwa dola za Mmarekani milioni 5,912.3 ambazo ni sawa na shilingi trilioni 9.456 na asilimia 0.5 ya kiasi hicho ni shilingi bilioni 47.298. Mheshimiwa Spika, kutokana na kodi hii ya mauzo na manunuzi ya bidhaa kutoka na kwenda nje ya nchi, iwapo tozo hiyo ingekuwepo, serikali ingekusanya kiasi cha shilingi bilioni 212.498 mwaka 2012. 7.0 VIPAUMBELE VYA BAJETI YA MATUMIZI 2013/2014 Mheshimiwa Spika, kutokana na mapendekezo tuliyoyatoa, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inapendenkeza kuwa vipaumbele vya Bajeti ya mwaka ujao wa fedha vingekuwa kama ifuatavyo: (i) Kujenga Mazingira ya ukuaji wa uchumi vijijini (rural growth) kwa kuboresha na miundombinu ya ya umeme, barabara, maji miundombinu umwagiliaji.

Tunapendekeza kutumia shilingi bilioni 450 kila mwaka katika eneo hili. Fedha hizi zitasimamiwa na Mamlaka ya Maendeleo Vijijini (Rural Development Authority to be established) itakayokuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Page 43 of 52

(ii)

Kukarabati Reli ya Kati na matawi yake ya Tanga - Arusha na Mpanda. Tutatenga Tsh 212.498 bilioni kwa RAHCO kwa ajili ya Reli. Fedha za ujenzi wa Reli zitakuwa ni fedha endelevu kutoka Elimu na Railways Afya Development hasa kwa Shule Fund na itakayotokana na tozo maalumu tunayopendekeza.

(iii)

Kuboresha

Zahanati/Vituo vya Afya vya Vijijini kwa kutoa motisha kwa wafanyakazi wa Sekta hizi walio kwenye Halmashauri za Wilaya. Tunapendekeza posho za Mazingira ya Vijiji sawa na mara moja na nusu ya Mishahara yao. (iv) (v) (vi) Kuongeza Kima cha chini cha Mshahara kwa Wafanyakazi wa Umma mpaka Tsh 315,000 kwa Mwezi Kuanzisha Pensheni ya uzeeni kwa Wazee wote nchini wenye umri wa zaidi ya miaka 60. Kupunguza mzigo wa matumizi ya magari ya Serikali kwa kupiga mnada baadhi ya mashangingi na kuweka mfumo wa kukopesha Magari kwa watumishi wote wa umma wanaostahili magari. (vii) Kuanzisha Chuo Kikuu cha Mtwara (Mtwara University for Petroleum Studies) ili kuzalisha wataalamu wa kutosha wa Sekta ya Mafuta na Gesi na kuliandaa Taifa kuwa na wasomi mahiri wa maeneo hayo na hivyo kufaidika na Utajiri wa Mafuta na Gesi uliopo nchini kwetu.

Page 44 of 52

8.0 SURA YA BAJETI MBADALA KWA MWAKA 2013/14 Mheshimiwa Spika, kambi rasmi ya upinzani bungeni katika kupanga bajeti yake imezingatia heshima ya taifa kwa kuhakiki nchi inaweza kutumia vema rasilimali zake na kufuta utegemezi. Naomba kunukuu maneno ya Abraham Lincoln anayesema; You cannot help people permanently by doing for them, what they could and should do for themselves. Kwa tafsiri ya haraka haraka anamaanisha kuwa hauwezi kuwasaidia watu kwa kuwafanyia, wakati wote, kile ambacho wanaweza na wanapaswa kukifanya. Leo hii, kama nchi tunategemea kuendelea kusaidiwa na mataifa wahisani kwa vitu ambavyo tunauwezo wa kuvifanya na tunapaswa kuvifanya. Pia tunajenga taifa tegemezi lisilo na heshima mbele ya dunia na kujipa matumaini ya kuwa bado tunao uwezo wa kukopesheka. Ni lazima kuongeza wigo wa kodi ili kuondokana na utamaduni wa kupandisha kodi zile zile kila mwaka na hivyo kuonekana kana kwamba hatuna ubunifu wowote. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia heshima ya taifa letu kambi rasmi imependekeza bajeti mbadala ya mwaka 2013/2014 yenye jumla ya makusanyo ya ndani ya shilingi billion 15,698.937 kwa kujikita katika kupanua wigo wa mapato ya ndani na kuachana na mikopo yenye masharti ya kibiashara ili kupunguza mzigo mkubwa ulioingizwa katika deni la taifa. Asilimia 75.8 ya bajeti nzima ni mapato ya ndani ikijumuisha mapato ya halmashauri. Hivyo ni
Page 45 of 52

asilimia 24.2 tu ya bajeti ndio itatukana na misaada ya kibajeti na mikopo isiyo na riba za kibiashara. Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani bungeni inapendekeza kuondoa kabisa mikopo yenye masharti ya kibiashara na kupendekeza vyanzo mbadala vya mapato ili kuondokana na adha ya madeni na kukusanya mapato yetu ya ndani kugharimia uendeshaji wa bajeti, pia kupunguza matumizi yasio ya lazima na fedha hizo kuelekezwa katika miradi ya maendeleo. Mheshimiwa Spika, kutokana na ongezeko kubwa la matumizi yasiyo ya lazima katika bajeti ya serikali, kambi rasmi ya upinzani imependekeza kupunguza asilimia 30 ya gharama za posho za vikao, semina, usafiri, viburudisho, mafuta na vilainishi. Kwa mwaka 2012/2013 serikali inatumia shilingi billion 681 kwa matumizi yasiyo ya lazima na 2013/2014 imepanga kutumia shilingi bilioni 714 (kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Sikika) sawa na ongezeko la asilimia tano kinyume na kauli ya Waziri Mkuu ya kupunguza gharama za matumizi yasiyo ya lazima. Hivyo kambi imedhamiria kuwepo na punguzo hilo la shilingi bilioni 214 kutoka katika eneo hili ambazo zitaelekezwa katika miradi ya maendeleo.

JEDWALI LA VYANZO VYA MAPATO MBADALA.


Page 46 of 52

CHANZO CHA MAPATO. Kuongeza Ufanisi wa bandari ya Dar Es Salaam Marekebisho ya kodi za misitu Kupunguza misamaha ya kodi Kodi ya 0.5% kwenye Mauzo na ya 1% manunuzi ya nje kwa ajili ya kujenga Reli Kuzuia ukwepaji kodi unaofanywa na Kampuni za kimataifa Jumla

MAKISIO SHILINGI BILIONI 1,465.000 220.416 1,545.000 212.498

718.500

4,161.414 SURA YA BAJETI MBADALA YA MWAKA 2013/2014.

MAPATO A Mapato ya ndani i)Mapato ya Kodi (TRA) ii)Mapato yasiyo ya Kodi B C D Mapato ya Halmashauri Mikopo na misaada ya Kibajeti Mikopo na Misaada ya miradi ya maendeleo ikijumuisha MCA (T)
Page 47 of 52

SHILINGI BILIONI 15,315.485 13,855.851 1,459.634 383.452 1,163,131 2,692,069

Mikopo ya ndani Jumla ya Misaada na mikopo.

1,156,400 5,011.600

JUMLA YA MAPATO YOTE

20,710.537

MATUMIZI E Matumizi ya Kawaida (i) Deni la Taifa (ii) Mishahara (iii) Wizara Mikoa Halmashauri H Matumizi ya Maendeleo (i)Fedha za ndani (ii)Fedha za Nje JUMLA YA MATUMIZI YOTE. 6,537.467 1,040,949 20,710.537 Matumizi Mengineyo 3,319.156 5,706.399 4,106.566 3,352,316 49,701 704,549 7,578.416 13,132.121

Page 48 of 52

TOFAUTI KATI YA BAJETI YA SERIKALI NA BAJETI MBADALA YA KAMBI RASMI YA UPINZANI. BAJETI MBADALA YA KAMBI YA UPINZANI 2013/2014 BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2013/2014

Bajeti yenye kuondoa mikopo Bajeti yenye mikopo ya shilingi yenye masharti ya kibiashara ili 1.156 trilioni yenye masharti ya kulipunguzia madeni. Bajeti yenye wa kujikita katika Bajeti inayopingana na utekelezaji mpango wa mpango wa maendeleo wa na wa matakwa serikali ya taifa mzigo wa kibiashara

maendeleo kwa kutenga zaidi taifa kwa kutenga asilimia 22.4 ya asilimia 41 ya mapato ya kinyume ndani kugharimia miradi ya mpango maendeleo. michezo Kulipa wote na wakala kwa ambao

unahitaji asilimia 35. wa kipaumbele chake isiyo na mfumo wa

Imeanzisha kodi maalum ya Haijali michezo na wala sio maendeleo ya michezo pensheni kuanzia wazee Bajeti 60 miaka na pensheni kwa wazee. wafanyakazi, (PAYE) kodi ya

kuendelea. Kushusha kiwango cha chini Haijali kutoka 14% mpaka 9% cha kodi ya mapato (PAYE) mapato imeendelea

kuwa kubwa 13%

Kupunguza matumizi yasiyo ya Ina matumizi yasiyokuwa ya


Page 49 of 52

lazima kwa kuondoa 30% ya lazima kiasi cha shilingi bilioni OC kwenye wizara na idara . Bajeti inayojitegemea ya mapato punguzo makusanyo Bajeti 214 tegemezi kwa asilimia ya 37.8 kutokana na kukopa kwa kiwango kikubwa. la Bajeti yenye misamaha ya kodi (sawa na shilingi trilioni 1.922) na Bajeti isiyozingatia mfumuko wa kwa Bajeti

ndani ya asilimia 75.8 yenye

misamaha ya kodi na kufikia 1% kiasi cha 4.3% ya pato la taifa ya pato la taifa Bajeti muhimu Bajeti yenye maslahi bora kwa Bajeti iliyo na kima cha chini wafanyakazi kima chini kwa cha kuongeza cha shilingi 170,000 mshahara kisichoendana na gharama za maisha kwa sasa. itakayokabiliana

mfumuko wa bei kwa bidhaa bei

kuanzia 315,000

Bajeti inayofuta ongezeko la Bajeti inayoongeza kodi kwenye kodi kwenye mafuta ya dizeli na mafuta, dizeli 6.1% na petroli petroli 8.5% inayoongeza kwa 10% bei na ya wa hivyo Bajeti inayoondoa ongezeko la Bajeti kodi kwenye ngano na hivyo ngano

bidhaa za ngano kama mikate, kutowajali bei Inafuta ongezeko la

wananchi

maandazi, chapati kutopanda kipatyo cha chini wanaotumia bidhaa hizi kwa wingi kodi Inaongeza kodi kwenye simu za
Page 50 of 52

kwenye matumizi ya simu za mkononi mkononi kutakiwa

na

hivyo kulipa

mtumiaji kodi

/tozo/ushuru wa 36.5%

9.0 HITIMISHO. Mheshimiwa Spika, wakati waziri wa fedha alipokuwa anawasilisha hotuba yake ya bajeti wiki iliyopita wapo wabunge ambao walikuwa wanapiga makofi kuashiria kuwa waliridhika na hotuba ya bajeti na walikuwa wanaiunga mkono. Aidha, baada ya mawasilisho yake hayo wananchi wa kada mbalimbali kuanzia wasomi, wafanyakazi, wanasiasa, wakulima na wafanyabiashara pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu wamekuwa wakipaza sauti zao kuhusiana na jinsi ambavyo bajeti ya serikali itakavyokwenda kuongeza gharama za maisha na kuwafanya waendelee kuogelea kwenye wimbi la umasikini katika nchi yenye rasilimali za kutosha. Mheshimiwa Spika, ni rai yangu na ya kambi rasmi ya upinzani kuwa sisi wabunge wote bila kujali itikadi zetu tusikilize kilio cha watanzania wenzetu hawa na tuwe na huruma juu ya maisha yao na tutakapokuwa tunajadili bajeti hii tuangalie maslahi ya taifa letu na wananchi wetu kwa kuhakikisha kuwa tunatimiza wajibu wetu wa kuisimamia serikali ili itimize wajibu wake wa kutoa huduma kwa wananchi wake. Nawashauri waheshimiwa wabunge wenzangu
Page 51 of 52

kuwa kamwe tusikubali kuwaongezea wananchi mzigo wa gharama za maisha kwa kukubaliana na serikali katika kupandisha kodi kwenye bidhaa za mafuta, ngano, matumizi ya simu za mkononi, malighafi za sabuni na kodi zozote ambazo zitawaumiza wananchi wetu. Tuiambie serikali itumie vyanzo vingine vya mapato kwa ajili ya kupata fedha za kujiendesha bila ya kuwaumiza wananchi wetu. Sote tutimize wajibu wetu kwa taifa letu. Njia hizo zipo na baadhi tunmezipendekeza kupitia hotuba yetu hii na hotuba zilizopita. Ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa inayachukua mapendekezo haya na kuyatekeleza kwa ajili ya kumwokoa mwananchi masikini. Imeshajidhihirisha kuwa pale ambapo serikali imeyachukua mapendekezo yetu na kuyatekeleza kwa ufanisi, kumekuwepo na mabadiliko chanya. Serikali isione aibu kuyachukua mapendekezo yetu na kuyatekeleza kwa sababu tunayatoa kwa moyo wa uzalendo wa kulisaidia taifa letu na watu wake. Sisi si wabinafsi. Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo kwa niaba ya kambi ya upinzani naomba kuwasilisha.

Page 52 of 52

You might also like