You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII S.L.

P 9083 DAR ES SALAAM

Simu ya Mdomo: 2120261/7 Fax No. 2139951 Barua zote ziandikwe kwa Katibu Mkuu Unapojibu tafadhali taja Kumb. Na..JB.138/322/02/1 Waganga Wakuu wa Mikoa, Waganga wa Kanda za Mafunzo, Waganga Wakuu wa wilaya, Tanzania Bara.

14th August, 2013

YAH: MITIHANI YA MASOMO YA KUJIENDELEZA KATIKA FANI YA UUGUZI KWA NJIA YA MASAFA Ninapenda kuwafahamisha kuwa kutakuwa na mafunzo ya kujiendeleza katika fani ya Uuguzi Daraja la B (Enrolled Nurse kuwa Registered Nurse) kwa njia ya MASAFA. Mafunzo haya yatatanguliwa na mitihani ya kujiunga na mafunzo. 1.0 Mafunzo hayo yataendeshwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na AMREF Tanzania. 2.0 NURSING Wauguzi daraja la B kuwa Registered Nurse. 3.0. VYUO VITAKAVYOENDESHA MAFUNZO Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na AMREF Tanzania imeteua vyuo vifuatavyo : . a) Chuo cha Uuguzi Mbeya b) Chuo cha Uuguzi Muhimbili c) Chuo cha Uuguzi Ifakara d) Chuo cha Uuguzi KCMC e) Chuo cha Uuguzi Shirati f) Chuo cha UuguziBugando g) Chuo cha Uuguzi Hubert Kairuki h) Chuo cha Sayansi Zanzibar Maelezo zaidi kuhusu mafunzo haya yatatolewa katika magazeti ya Daily News na Nipashe wiki ya tarehe 19/08/2013 na wiki ya tarehe 26/08/2013.

Taarifa hizi na maelezo ya ziada unaweza kupata kutoka tovuti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. www.moh.go.tz na tovuti ya AMREF Tanzania www.amref.org. Pia unaweza kupata taarifa kutoka kwa wauuguzi wakuu wa mikoa na wilaya viliko vyuo. 4.0 TAREHE ZA MITIHANI Kutakuwa na mitihani ya kuandika na mahojiana ya ana kwa ana itakayofanyika katika vyuo vitakavyoendesha mafunzo kuanzia tarehe 23/09/2013 5.0. Wafanyakazi wote wanaopenda kujiunga na mafunzo haya ya elimu kwa njia ya masafa watume maombi yao na kujaza fomu ya maombi hayo kwenye shule husika wakiambatanisha vivuli vya vyeti halisi vya kumaliza elimu ya secondary, kuhitimu mafunzo ya awali na leseni ya kufanya kazi (Licence to practice). Utaratibu huu utatuwezesha kuandaa na kutuma majina na namba za mitihani kwa wahusika mapema. Mafunzo haya hayatahusiana na wale waliojiorodhesha kwa Waganga Wakuu kwa ajili ya kujiendeleza kwa kukaa chuoni (full time), aidha mwombaji wa mafunzo haya ya Masafa (e-Learning) anaweza kuomba hata kama alijiorodhesha kwa ajili ya full time iwapo atapenda. Napenda ieleweke wazi kuwa mafunzo haya yanaratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na AMREF Tanzania. Kwa wale ambao wataomba kwenye vyuo vya serikali (Mirembe na Mbeya) wanapaswa kulipa ada kwenye akaunti ya Wizara: Health Service Funds Account No. 0111-030-12059, NBC (National Bank of Commerce) Corporate Branch. Risiti Halisi ni lazima iambatanishwe na maombi. 7.0 Waganga Wakuu wa Wilaya mnakumbushwa kuhakikisha kuwa taarifa hii inawafikia watoa huduma katika vituo vya Serikali, Taasisi binafsi na vituo vya Mashirika ya dini vilivyo katika wilaya zenu, mapema iwezekanavyo. Nawatakia utekelezaji mwema wa zoezi hili

DK. Gozibert Mutahyabarwa K.n.y. KATIBU MKUU Nakala: Mkurugenzi wa Huduma za Afya/Afisa Utumishi Mkuu JWTZ Makao Makuu, S.L.P 9203, DSM. Mkurugenzi- Christian Social Services Commission, S.L.P 9433, DSM Waratibu wa Kanda za Mafunzo Wakuu wa vyuo vya Mafunzo ya Fani ya Uuguzi Mkurugenzi, AMREF Tanzania.

You might also like