You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

NAFASI ZA AJIRA KWA MADAKTARI, MADAKTARI WA MENO, TABIBU, TABIBU WASAIDIZI NA WATAALAMU WA MAABARA Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, inawatangazia Wahitimu wa taaluma zilizotajwa hapo juu kuwa zipo nafasi za kazi katika Mikoa na Halmashauri zote nchini isipokuwa Mkoa wa Dar es Salaam na Halmashauri zake. Waombaji wanatakiwa kuambatanisha nyaraka zifuatazo katika maombi yao:1. Vyeti vya Elimu ya Sekondari. 2. Cheti cha Kuhitimu mafunzo ya taaluma husika. 3. Kwa wale wanaotakiwa Kwa mujibu wa sheria kufanya mafunzo kwa vitendo, wawasilishe cheti cha kuhitimu mafunzo hayo. Mwisho wa kupokea maombi ni wiki mbili kuanzia tarehe ya tangazo hili kutoka. Aidha, juu ya bahasha iandikwe nafasi inayoombwa. Majina ya watakaopangiwa vituo vya kazi yatatangazwa kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz Maombi hayo yatumwe kwenye anuani ifuatayo:KATIBU MKUU, WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII, S.L.P. 9083, DAR ES SALAAM.

You might also like