You are on page 1of 5

S/N 4.

JINA LA MLALAMIKAJI Bw. Beatus Robert Mafuru

LALAMIKO /HOJA Aliomba nafasi ya kazi ya Afisa Tarafa na baadaye akaomba nafasi ya Afisa Mtendaji Kata daraja la II lakini hadi sasa hajapata taarifa yoyote.

MAJIBU YA HOJA Maombi ya nafasi ya Afisa Tarafa hukuitwa katika usaili kwa sababu hukuambatisha cheti cha shahada ya kwanza kwenye maombi yako ya kazi. Nafasi ya Afisa Mtendaji Kata daraja la II uliitwa kwenye mchujo tarehe 27 Oktoba, 2012 na ulipata alama ambazo hukustahili kuitwa kwenye usaili wa ana kwa ana. Mchakato wa kuwapata watendaji wakuu/watendaji waandamizi una taratibu zake hivyo endapo kama hutapata taarifa ya kuitwa ieleweke kuwa hukukidhi vigezo vya kuitwa katika usaili.

5.

Bw. Seleman T. Byarugaba

Aliomba nafasi za watendaji waandamizi za 1) Director of Finance, Personnel and Administration Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC). 2) Director Business Development Fisheries Education and Training Agency (FETA) 3) Director of Finance and Administration NEMC Anaomba kufahamishwa ni hatua gani imefikiwa

8.

Bw. Jerome Jerome

Anasema kuwa wao wanaishi vijijini. Ili watume maombi ya kazi ni lazima wasafiri hadi wilayani ili waweze kutuma barua hizo za maombi ya kazi. Je? Hakuna e-mail address ili waweze kutuma kwa mtandao?

Tumepokea ushauri wako hivi sasa Sekretarieti ya Ajira ina mpango wa kuanzisha e- Application. Utaratibu huu utawapa fursa waombaji wa fursa za ajira kutumia mtandao na maombi yao kufika kwa haraka zaidi. Aidha, suala la kupotea kwa barua za maombi halitakuwepo tena.

11.

Njiro student center Gharama zinazotozwa na Bodi Suala hili si la Sekretarieti ya Ajira, ya Ugavi ni kubwa kiasi kwamba malalamiko haya wasilisha katika Bodi ya wanapohitaji waombaji wenye Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB). sifa na waliosajiliwa na Bodi wao wanakosa sifa hizo kutokana kukosa fedha za kulipia gharama za utafiti na masomo. Liliacia Kimambo Aliomba kazi ya katibu mahsusi Daraja la I katika Taasisi zifuatazo: i) Taasisi ya Usimamizi wa fedha (IFM) ii) Chuo cha Maji (WDMI) Anasikitika hadi leo hajaitwa kwenye usaili na kwamba huenda ikawa haitwi katika usaili kutokana na yeye kuwa na Ajira katika Chuo cha Ustawi wa Jamii
2

12.

Napenda kukujulisha kuwa nafasi uliyoomba ya katibu mahsusi Daraja la I ni sawa na nafasi zilizotangazwa na IFM na WDMI. Hivyo unashauriwa kuomba tena endapo tu nafasi itakayokuwa imetangazwa ni ya cheo cha juu kuliko cheo ulichonacho hivi sasa. Pia mwajiri wako wa sasa Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii atapaswa apitishe barua yako ya maombi ya kazi. Vinginevyo ukienda kinyume na utaratibu huu maombi yako ya kazi hayatashughulikiwa.

17.

Bw. Godfrey Christopher

Aliomba kazi (hakutaja aina ya Tumepokea ushauri wako na tutaufanyia kazi aliyoomba) lakini wakati wa kazi. kuitwa katika usaili kupitia mtandao wa www.ajira.go.tz jina lake halikuonekana. Alishangazwa kupata taarifa kuwa jina lake lilisomwa katika chumba cha usaili. Inavyoonekana kulikuwa na makosa katika uchapaji wa jina lake. Hivyo basi anaomba tuwe makini wakati wa kuandaa majina husika. Alifanya usaili wa Civil Engineer (TANROADS) lakini mpaka leo hajabahatika kuitwa kazini. Alihoji kama ifuatavyo: Kutuma barua za maombi ya kazi kwa njia ya posta sio sahihi tuanzishe email address Ni kweli ulifanya usaili wa TANROADS lakini matokeo yako hayakuwa mazuri (yaani chini ya wastani unaotakiwa). Suala la matumizi ya e-Application lipo katika mchakato, hivyo mara baada ya kukamilika umma utajulishwa namna ya kutumia utaratibu huo.

18.

Bw. Mussa Madirisha

19.

Bw. F. S. Belleh

Kazi zote zenye uzoefu ni lazima Anapinga kutangaza kazi kwa masharti ya Tangazo yazingatie uzoefu kuzingatia uzoefu kwamba si na si vinginevyo. Kwani kazi hizi ni za sahihi. madaraka na sio kazi za viwango vya kuanzia. Mfano Mhandisi Daraja la II.
3

Halihitaji uzoefu. Sekretarieti ya Ajira inawapa vipaumbele vyuo vya Serikali tu na si vyuo binafsi. Hoja hiyo si sahihi, Sekretarieti ya ajira inasaili waombaji kazi wote wawe wa vyuo vya Serikali au vya binafsi. Kitu cha msingi ni lazima wawe na sifa na vyuo vyao viwe vinatambuliwa na Serikali Suala la vyeti feki sio gumu kulishughulikia. Suala hili litaendelea kuboreshwa kwa kutumia utaratibu wa e-Application ambapo mfumo utatambua mara moja Index Number za vyeti vilivyoghushiwa.

20.

Bw. Yesse Mwanjome

Analalamika kuwa: Muda wa maandalizi ya usaili ni mdogo hakutaja siku. Matangazo ya usaili yangepangwa mara tu mtu anapohitimu masomo kwani akikaa kwa muda mrefu anapoteza kumbukumbu ya alichojifunza. Amepata majina ya kuitwa kwenye usaili haelewi na anashangaa jina lake halipo.

Matangazo ya kuitwa katika usaili ni siku kumi na nne (14) kabla ya tarehe ya usaili. Hii ni kwa mujibu wa mwongozo na taratibu za Utumishi wa Umma Serikalini. Nafasi za kazi hutangazwa mara vibali vya ajira vinapopatikana. Hivyo, kutokana na wingi wa waombaji wa fursa za ajira kuwa wengi, wanasababisha kuwepo na ushindani mkubwa. Kama ulipata majina ya kuitwa katika usaili na jina lako halipo ieleweke kuwa hukufanikiwa.

21.

Bi. Mwasiti Iddi

Alihoji kuwa Je? Ni halali kuweka majina ya kuitwa katika Tovuti tarehe 05.12.2012 na usaili kufanyika tarehe 08.12.2012

Taarifa zilizotolewa katika tarehe hizo ni baada ya usaili wa mchujo ambao ulifanyika 03/12/2012 , hivyo wasailiwa walijulishwa kuwa majibu yatatolewa kuanzia tarehe 03/12/2012 05/12/2013 na usaili kufanyika tarehe 08.12.2012. Aidha kabla ya usaili wa mchujo waombaji wa fursa za Ajira walijulishwa mapema zaidi yaani siku kumi na nne (14) kabla ya usaili wa mchujo. Napenda kukujulisha kuwa Sekretarieti ya Ajira haifanyi kazi kwa utashi wa Taasisi fulani au mtu fulani. Sekretarieti ya Ajira inafanya kazi kwa kuzingatia Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma. Hivyo basi unashauriwa kuomba kazi kwa kuzingatia masharti yaliyotangazwa na Taasisi husika na si vinginevyo.

24.

Bw. Peter Simon Msuya

Analalamika kuwa, hapati kazi kutokana na Wakuu wa Taasisi fulani kutuma majina yao ili wao walisipate kazi. Kwani amekuwa akiomba kazi bila mafanikio yoyote.

You might also like