You are on page 1of 15

"Tubadili Jiji la Dar es Salaam: Kuna Zaidi ya Mafuriko" Nimetafuta hotuba ya video ama sauti ya Mh.

Rais Jakaya Kikwete wakati akifungua Bunge kwa mara yake ya kwanza kama Mkuu wa Nchi mwaka 2005 lakini nimeikosa. Nitaendelea kuitafuta. Kuna maneno mahususi nilitaka niyarejee ninapoandika ujumbe huu kwake ili kuongeza mantiki ya ninachotaka kumshauri. Pamoja na kukosa hotuba yake ile muhim sana katika historia ya nchi yetu, bado nakumbuka alivyoitoa maana nilimwangali na kumsikiliza tangu aliposimama hadi alipokaa. Kumbukumbu zangu zinaniambia alikua amevaa suti ya rangi kama ya bluu hivi huku akionekana kama Kijana mcheshi, mpole, mtaratibu na aliyejipanga kuweka kumbukumbu vema juu ya mipango yake ya kuingozoza nchi kwa siku ambazo angepata kibali kwa Mugnu na kwa Watanzania. Ninakumbuka baadhi ya maneno aliyotakua anayatamka lakini nakosa ukamilifu wa sentensi zake bila kumsikiliza upya. Hata hivyo kumbukumbu hii inanipa ujasiri wa kutosha wa kuandika ujumbe huu ili uifikie serikali na Rais wangu kuwashirikisha mawazo yangu ya muda mrefu niliyonayo juu ya UKARABATI, UBANGAJI, UBORESHAJI, UENDELEZAJI na MENEJIMENTI ya JIJI LA DAR ES SALAAM LENYE SURA YA UKISASA, KUVUTIA NA HUDUMA STAHIKI ZA KIJAMII. Kumbukumbu zangu zinanionesha kuwa, wakati uongozi wa muungano wa vyama vya upinzani Kenya uliojulikana kama NARC ulipoingia madarkani mwaka 2002, Nairobi ilikuwa moja ya miji korofi na hatari zaidi barani Afrika na
1

duniani. Pamoja na mambo mengine mji huu ulijaa vibaka wa kutisha maarufu kwa jina la Chokoraa huku wengine wakiwa wamezaliwa na kukua katika mazingira hayohayo kwa zaidi ya miaka 30. Pamoja na kuwa miongoni mwa majiji makubwa zaidi katika ukanda huu wa Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara na kuwa kitovu cha ofisi za kimataifa na mashirika mengi makubwa, Nairobi ulikua mji mchafu sana katika maeneno mengi huku ukikumbwa na tatizo kubwa la msongamano wa magari na watu kutokana na ufinyu wa miundombinu hasa ya barabara na kukosekana kwa usafiri mbadala wa reli. Mitaa mingi hasa ya watu maskini (slums) ya Kibera na kwingine yaliongeza sura mbaya ya mji wa Nairobi. Kwa ujumla Nairobi kulitisha na nina kumbukumbu ya kupita barabarani mchana huku mtu anabwaka na hapakua na wa kumsaidia maana hakuna aliyekua tayari kuhatarisha maisha yake. Serikali ya Rais mstaafu Kibaki ilipoingia madarakani mwaka 2002, pamoja na mambo mengine, walikuja na mkakati wa kurudisha hadhi ya mji wa Nairobi. Muda hautoshi kueleza ni mipango au miradi gani mahususi iliyowekwa na serikali lakini mengi yalifanyika ikiwa ni pamoja na mkakati wa kujenga makambi ya kuwahifadhi maelfu ya Chokoraa (for rehabilitation process) waliokua wamejaa mjini. Hadi Kibaki anamaliza ungwe ya kwanza ya uongozi wake, mji wa Nairobi ulikua umeanza kujengeka taswira mpya yenye matumaini na maeneno kadhaa yakiwa yamebadilishwa kutoka kua Slums na kuwa na mwenekano
2

wenye mvuto. Mwaka 2007, Kibaki aliporudi madarakani na kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa, mradi wa kubadilisha Nairobi haukusimama. Pamoja na changamoto za kiuongozi walizokua nazo na madhara ya machafuko ya baada ya uchaguzi, Kenya waliendeleza mradi wa kubadili Nairobi. Kulipa uzito jukumu la ubadilishaji taswira ya Jiji wa Nairobi; mwaka 2008 serikali ya Kibaki na Raila iliunda wizara mpya maalumu kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa mji wa Nairobi (The Ministry of Nairobi Metropolitan Development). Pamoja na kuonekana kuwa wizara hii iliundwa tu kwa lengo la kutatua changamoto ya kugawana madaraka ndani ya serikali ya Umoja wa Kitaifa, ukweli ni kuwa kulikua na kazi ya kufanya iliyoendana na dhamira njema ya Serikali kubadili mandhari ya Jiji la Nairobi iliyokua haiendani na hadhi yake. Sio lengo la makala hii kuelezea uzuri au kazi nzuri iliyofanywa kuboresha Jiji la Nairobi, lakini kwa wale waliokua wanaijua Nairobi miaka ya 1990 na 2000 mwanzoni, wanaweza kuelezea vema maendeleo na mabadiliko makubwa yalifanywa na serikali ya Kenya ikishirikiana na wadau wake wa maendeleo na mashirika ya kimataifa kama UN Habitat hasa ilipokua chini ya Pro. Mama Tibaijuka. Pamoja na kuwa Nairobi bado sio mahali salama sana, lakini leo mtu unaweza kwenda kutembea tu mjini kama mtalii na ukijionea mengi ya kupendeza macho na kufurahisha moyo wako huku ukijipumzisha kwenye bustani nzuri ya Uhuru wakati wa mchana.

Yapo maswali mengi ambayo mtu angeweza kuwa nayo kuhoji maamuzi ya seriakli kuunda wizara ya kushughulikia Jiji moja badala ya kutumia rasilimali hizo kuboresha kilimo, elimu na huduza zingine za jamii kama afya. Lakini ukweli ni kuwa Kibaki na wenzake kuna vitu waliona kama viongozi na walifanya maamuzi ya kiutekelezaji bila kujali maswali na hoja hizi zenye uzito na ukweli. Walijua umuhimu wa mji wa Nairobi katika nchi yao, uchumi wao, uchumi wa Afrika Mashariki , uchumi wa Afrika na nafasi (strategic position) ya mji wao kidunia. Kwa wale wasiojua, kulingana na Encyclopedia zilizo Maktaba, wakati sisi tunapata uhuru miaka ya 1960 na Dar es Salaam ukiwa mji mdogo sana, Nairobi tayari ilishakua na hadhi ya Jiji chini ya wakoloni. Kutangulia kwake huko, kumeifanya Nairobi kuwa kitovu cha mashirika na huduma nyingi za kimatafa. Katika ukanda huu wa Afrika Kusini mwa Jangwa la (kutoa tu miji ya Afrika Kusini), Nairobi ndio mji wenye matawi na huduma nyingi kubwa za kimataifa za viwango vya juu kuliko mji mwingine wowote ule. Wageni wengi hasa toka nchi za Ulaya na Marekani wanofanya kazi hapa nchini au wanaokuja kutalii, hufuata huduma muhim kama afya na elimu Nairobi. Kwa mfano; ukisoma ushauri wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani dhidi ya raia wao walioko Dar es Salaam, wanashauriwa wanapohitaji huduma za afya hata za immergency, warushwe na ndege kwenda Nairobi maana hakuna huduma ya kuaminika Tanzania!!! Sina haja ya kuelezea na kusisitiza sana umuhim wa Jiji la Dar es Salaam kwa watanzania maana ni jambo la wazi. Bila hata kuangalia takwimu za TRA, kumbukumbu zangu
4

zinaniambia kuwa zaidi ya 75% ya mapato ya kodi nchini, yanatoka Jiji la Dar es Salaam. Kila mmoja anajua kuwa Dar es Salaam ndiko kumesheheni huduma nyingi za kuaminika (angalau kwa viwango vya kibongobongo) kuliko mahali pengine popote pale nchini. Dar unasemekana ni mji wa tatu kati ya miji inayokua (ingawa kiholela) kwa kasi zaidi Afrika. Kulingana na taarifa ya Intelligence Unit (The Economist, Octoba 2013), Dar ni miongoni mwa miji 25 Afrika inayokua kwa kasi na ambayo makampuni makubwa ya kimataifa yanashauriwa kuingalia kwa jicho la kifursa kubwa ya kibiashara na uwekezaji. Sote twajua kuwa Dar ni lango kubwa la Bahari lenye fursa ya kuwa na bandari kubwa na yumkini nzuri kuliko Bandari zote za mwamboa mwa Bahari ya Hindi na inategemewa na nchi nyingi tilizopakana nazo zisizo na bandari. Taarifa ya sensa ya mwaka 2012, inaonesha kuwa jiji ya Dar lina karibu 10% ya idadi ya watu wote nchini. Haya ni makao Makuu ya Rais wa Jamuhuri, mabalozi, mabanki, wizara na makampuni mengi ya kibiashara. Pamoja na umuhimu huu wa Dar es Salaam kitafa na kimataifa, mji huu unakosa mvuto kwenye macho ya wenyeji na wageni na unakabiliwa na mapungufu mengi sana. Pamoja na jitihada nyingi zinazofanywa na serikali kisekta kuboresha baadhi ya huduma, Jiji la Dar es Salaam bado linakabiliwa na changamoto kubwa sana ambazo dalili inaonesha kabisa kuwa ama zimeshindikana kutatatulika; kumekosekana uongozi na menejimenti tahiki; au njia na mipango iliyoko sio sahihi na imeshindwa kutatua changamoto zilizoko na kukabiliana nawingi wa
5

zinanazokuja zinazosababishwa na ukuaji wa Jiji kwa njia nyingi. Tafiti zilizofanywa mwaka jana zilionesha watanzania ni katika ya raia wa nchi za duani amao wana msongo mkubwa wa mawazo (stress) hivyo hawana fuaraha. Sikumbuki uchambuzi wa utafiti huu kwa undani lakini nadhani waliangalia zaidi watu wa Dar es Salaam. Ndani ya Jiji letu ni ngumu kuwa na furaha siku nzima kwani mtu huna hakika ya kufika kazini au kokote uendako kwa wakati; unalala kwa kuchelewa sana na kuamka mapema sana kukabiliana na foleni; huna hakika ya kupata maji ya kuogoa na kunywa; huna hakika umeme utawaka hadi saa ngapi bila kukatika au kama umekatika hujui utarudi muda gani; huna hakika ya gari na nyumba yako kama viko salama muda wote; huna hakika ya kupata usafiri hata kama una nauli; na huna hakika kama njia uipitayo utafika mwisho bila kupigwa kabali na kuvuliwa hadi viatu ulivyovaa. Jiji letu limekua mji wa Stress na kila mmoja anamwongezea mwingine machungu ya stress zake na kusababisha uhaba wa haiba yenye furaha na kuridhika. Miongoni mwa changamoto hizi kubwa za jiji letu ni : 1. Tatizo la maji safi (hata kama sio salama ) na ya uhakika matumizi yoyote yale 2. Tatizo la uduma duni na zisizotosheleza mahitaji za usafiri (barabara, baharini na reli) 3. Tatizo kubwa la mifumo wa maji taka na njia ya mirefeji ya kupitisha maji wakati wa mvua 4.Tatizo kubwa la umeme usiokidhi mahitahi na usio wa uhakika 5. Tatizo kubwa la uchafu uliokithiri katika maeneo mengi
6

6.Tatizo kubwa la makazi holela. Sehemu kubwa ya jiji ina makazi/majengo mengi yaliyojengwa bila kufuata taratibu za mipango miji. 7. Majengo mengi ya thamani kubwa yamejengwa katika maeneno ambayo hayatambuliki kisheria, hayana hati, na hakuna miundombinu ya lazima inayoendana na hali ya ujenzi 8. Tatizo kubwa la usalama linalokua kila siku. Usalama wa raia na mali zao ni kati ya mambo yanayoongeza wasiwasi wa maisha ya watu wa Dar es Salaam kila. Hata yale maeneo yaliyokua yanajulikana kama salama, sasa yanakua hatari zaidi kwa uhai na mali 9.Tatizo kubwa la wahamiaji (kutoka vijijini na miji mingine) na wengi hawana shughuli maalumu kutokana na ugumu wa maisha na matumaini yanayoonekena Dar es Salaam 10. Tatizo la msongamano wa magari uliokithiri 11. Tatizo la njia, utaalamu, maeneo na rasilimali watu kwa ajili ya kukabiliana na majanga mbalimbali yanapotokea 12. Tatizo la mfumo mkubwa wa maisha utokanao na kupanda ovyo kwa bei ya vyakula na huduma 13. Tatizo la huduma za afya (kwa maana ya hospital za kisasa na kuaminika) ambazo haziendani na uhitaji wa jiji na nchi kwa ujumla wake 14. Tatizo kubwa la kutokujali kwa wale waliopewa dhamana ya kusimamia mambo mbalimbali 15. Na mengine mengi

Mambo haya yameufanya mji wa Dar es Salaam kupoteza mvuto ambao ulitakiwa kuwa nao na kushindwa kustahimili mahitaji wa wakazi wake na wageni wanakuja kwa muda mrefu na mfupi. Pamoja na ukubwa na umuhim wa Jiji la Dar es Salaam; 1. Kutokana na tafiti za wageni katika miji mikubwa Afrika, Dar es Salaam ni kati ya miji mikubwa Afrika ambayo haipati wageni wengi hasa wanaokuja kwa shughuli za kitalii. 2. Huduma za hoteli na huduma zingine za starehe/kujiliwaza ni ghali sana na hazikidhi mahitaji ukilinganisha na miji mingi Afrika 3. Ni mji wa 16 kwa ughali zadi wa maisha barani Afrika (The Economist, 2013) 4.Ni mji wa 13 Afrika kwa matatizo ya ulevi, uvutajiwa wa sigara na maovu mengine 5. Tofauti na miji mingi mikubwa Afrika na duniani, ni ngumu kuona watalii (wa ndani na wa nje) katika ya jiji na viunga vyake (katika muonekano wa kitalii) kutokana na kukosekana vivutio vya kitalii na mipango mibaya. Zaidi ya maeneno ya beach, jiji halina maeneno salama na yenye mvuto kwa shughuli za kitali. Ukionekana wapiga picha katikati ya Jiji la Dar, watu ama watakushangaa au kukucheka na walinzi kukukamata 6.Hakuna maeneo mazuri na ya kutosha kwa mapumziko kwa wasio na nafasi majumbani kwao au ya kifedha 7. Mji hauna vivutio zaidi ya majengo marefu ambayo mengi hayafanani na mazingira yalimo
8

8. Hakuna ramani nyepesi zipatikanazo kwa ajili ya wageni na watalii maana sio sehemu ya mandhari ya jiji 9.Biashara zinafanyika kila kona, kila mtaa, kila barabara na kila eneo hata pembeni na Ikulu ya nchi 10. ....na mapungufu mengine mengi 11. Hakuna hata huduma moja ya kijamii ambalo mtu anaweza kusema kwa hili dar es Salaama hakuna shida kila kitu kiko vizuri maana hata bahari tuliyopewa bure na Mungu, tumeshindwa kuifanya kuwa safi na ya kupendeza kwa matumizi yetu Kwa mtazamo wangu, naona kuwa mfumo wa uongozi/utawala/uendeshaji wa jiji ulioko, hauwezi kukidhi uhitaji wa kukabiliana na matatizo yanayolikabili jiji la Dar es Salaam. Hakuna kiashiria chochote kinachoonesha kuwa hali ya jiji hili na huduma zaidi itabadilika ndnai ya kipindi kifupi kijacho. Mabadiliko yaliyoko yamekua ni madogo sana na hayaendani na mahitaji na ukuaji wa jiji hili. Baadhi ya maboresho yamekua na madhara makubwa kwa upande mwingine na mfano wake ni ujenzi wa majengo makubwa usioendana na hali ya miundombinu iliyoko na hivyo kusababisha matatizo makubwa ya mifumo ya maji taka na mafuriko yasiyo lazima wakati wa mvua za masika. Hata Rais Kikwete alilitaja hili mwaka 2005 katika hotuba yake ya kwanza. Hivyo basi, ni ushauri wangu kuwa wakati umefika sasa kwa serikali (labda niseme Rais) kuona ulazima wa kufanya mabadiliko makubwa ya kiutawala kwa kuunda kitengo
9

maalumu ambacho uwajibikaji wake uko katika kuboresha Jiji la Dar es Salaam. Kitengo hiki kinaweza kuundwa kwa mfumo wowote ule lakini msisitizo mkubwa uwe ni kazi na majukumu ya kubadili Jiji. Kwa mtazamo wangu wa haraka, naweza kushauri kuwa iundwe wizara maalumu na ndogo kwa ajili ya kumeneji Jiji la Dar es Saalam na kusimamia miradi maalum itakayobadilisha hali iliyoko. Ninaelewa vema uwepo wa mfumo wa serikali za mitaa na tawala za mikoa nchini ambao hata Jiji hili ndio unatumika. Hata hivyo, nina hakika kuwa serikali ina uwezo na mamlaka ya kisheria kubadili muundoa na mfumo wa utawala ili kutekeleza mambo maalumu kama uwepo wa kitendo ninachopendekeza ili kutekeleza majukumu maalum ya kubadili mji wa Dar es Salaam bila kuingiliana na TAMISEMI. Nina habari za uhakika kuwa Mkoa wa Dar es Salaam uko mbioni kuanzisha wilaya zingine kadhaa kama namna ya kurahisisha utawala na utoaji wa huduma za jamii. Kwa mtazamo wangu, wilaya hizi haziendi kubadilisha chochote zaidi ya kutengeza nafasi mpya za kazi na gharama za utawala maana zkishaanzishwa, zinakwenda kufanya kazi zilezile za wilaya zilizoko; kwa utaratibu uleule na kwa malengo yaleyale ndani ya mfumo uliozoeleka. Ninaelewa kuwa umapendekezo yangu ya kuwa na kitengo au wizara maalum ya uboreshaji, uendelezaji na utengenezaji wa Jiji la Dar es Salaam unaweza kukabiliana na upinzani kwa maelezo kuwa unaongeza gharama za kiutawala na kuwapa watu vyeo. Hoja hii inaweza kuwa na sehemu ya ukweli lakini kwa mtazamo wangu, tunahitaji chombo cha ziada ili kipewe
10

majukumu ya ziada iliyoshindikana.

ya

kubadili

hali

ya

jiji

hili

Nimeanza makala yangu kwa kueleza kilichotokea na kinachoendelea Nairobi (hata kama hawajafikia ukamilifu). Hata hivyo, Nairobi sio mfano pekee. Miji mingi mizuri inayovutia watu duniania kama DUBAI, miji ya Malyasia, Indonosia, India, China na kwingine, haikufanikiwa kwa mifumo ya kawaida ya kiutawala (Routine Administrative Bureaucracy) bali waliunda miradi na Task Forces maalumu chini ya mifumo yao kusimamia miradi hii ya uboreshaji na uendelezaji wa majiji yao. Ni ushauri wangu kwa Rais na Watendaji wake kuwa waone sasa umuhim wa kuanzisha kitengo maalumu (eg. Dar es Salaam Metropolitan Development Project) na wa wakipe majukumu yanayoweza kufanana na haya: 1. Kutengeneza mpango Mkakati wa muda mrefu na mfupi wa uboreshaji wa Jiji na kusimamia utekelezaji wake mara moja 2. Kutengeneza Masterplan Mpya inayoonesha nini kinatakiwa kibadilishwe kukidhi mpango sahihi wa jiji utakaokidhi mahitaji ya karne nyingi zijazo bila ulazima wa kurudiarudia 3. Kwa kushirikiana na sekta binafsi, wubuni vivutio vya kitalii (iwe majengo, museum, beaches, miundombinu, bustani, minara, nk) sehemu mbalimbali za mji ili kukuza utalii wa ndani na wa nje na kuongeza mapato 4.Kuweka mpango mkakati na kusimamia utekelezaji wake katika kufanya kila kona ya Jiji la Dar es Salaam kuwa safi na la kuvutia (muda mfupi wa kubadili hali ya usafi wa sasa na muda
11

mrefu kuendeleza na kujenga tabia ya usafi wa jiji na na kutunza vivutio vyake) 5. Kubuni njia mbalimbali za usafiri wa reli, barabara na maji vyenye kukidhi mahitaji ya muda mrefu na huku vikiwa sehemu ya vivutio vya kitalii (kuachana na kasumba ya mradi liende....mradi njia inapitika) 6.Kushirikiana na sekta binafi na mashirika mengine kujenga huduma za kisasa za kijamii zenye viwango vya kimataifa kama vile Hospital zenye Specialized Health Services; mashule; hotels; viwanja vya michezo mbalimbali, nk: kama namna ya kuboresha huduma za jamii ndani ya nchi na kuingizia nchi mapato kwa watakaokuja kupata huduma kwetu 7. Kwa kushirikiana na sekta/wizara zingine, Kuweka mpango mkakati na kusimamia utekelezaji wake katika kukuza na kuboresha usafiri wa ndege, huduma za maji, huduma ya umeme na usafiri wa ndani ya Jiji 8. Kuboresha makazi katika ujumla wake na kuwa na mfumo bora zaidi wa kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhim za kijamii 9.Kuboresha hali ya usalama Jijini na kuufanya mji kuwa wa amani na utulivu kama lilivyo jina lake 10. Kutengeneza ajira kwa wakazi wa jiji na kuwa na mfumo mzuri wa kumeneji uhamiaji 11. Kutengeneza miji midogo nje ya mji mkuu kukidhi mahitaji ya kimataifa 12. Kuhakikisha matumizi ya mifumo ya kisasa ya mawasiliano hasa Internet vinakua sehemu ya
12

huduma muhim zinazopatika kwa wenyeji na wageni 13. Kuanzisha sheria za usafi wa Jiji na kuzisimamia bila aina yoyote ya uzembe, rushwa, uzungushaji na uonevu 14. Waimarishe ulinzi wa jiji na mitaa yake ili kupafanya pawe mahali salama kwa wenyeji na wageni 15. Kingine chochote kile ambacho kitaonekana kinaweza kuwekwa chini ya ufuatiliaji na utendaji wa Team hii. Ili kuondoa dhana kuwa mapendekezo ya kitengo hiki ni ulani na busines as usual, nashauri yafuatayo kuzingatiwa: 1. Timu hii ipatikane kitaalamu kulingana na mahitaji na kuwe na rekodi sahihi ya utendaji wenye tija kwa watumishi wake 2. Timu hii ipewe muda maalumu ya utekelezaji wa kila mradi chini ya mkakati wa uboreshaji wa jiji. 3. Mahitaji muhim (resources) ya utekelezaji wa miradi chini ya timu hii yapatikane kwa wakati na bila mizengwe ili kuepuka ucheeweshaji wa miradi 4. Timu ipewe muda maalumu ambapo watatakiwa kuwa wanazalisha/wanapata mapato chini a miradi yao kwa ajili ya uendeshaji wa miradi mikbwa ya jiji 5. Miradi hii ifanywe na wenyeji kwa 100% huku wakipata ushauri na utaalamu mahusus toka kwa wataalum wenye historia ya kubadili miji katika nchi zingine- hasa nchi za Asia

13

6. Timu ifanye kazi kwa mfumo wa miradi (projects) badala ya mazoea (routine) ili iwe rahisi kupima utendaji dhidi ya malengo na gharama ya kila mradi 7. Watendaji wakuu wa timu walipwe kwa uzalishaji ( Paid per Performance and deliverables) na kwa mikataba maalum badala ya kulipwa kwa mazoea 8. Timu ipewe uhuru wa kisheria kufanya kazi na miradi yake kwa njia bora na ya haraka isiyofungwa na mifumo migumu ya umma na yenye gharama kubwa kama ile ya sheria ya manunuzi ya ummma 9. Timu iwajibike kwa Rais au ofisi/bodi/tume nyingine atakayoona ina nguvu ya kutosha kufikisha maono yanapotakikana ikiwa ni pamoja na kuwajibisha watendaji wapaoshindwa kutekeleza majukumu yao Ni maono yangu kuwa, wakati umefika watanzania tuache kuwa watu wa kushangaa kila nchi tunayokwenda. Tuache tabia ya kila mtanzania akipanda ndege kutoka nje ya nchi, anaanza kushangaa kila kitu anachokutana nacho kuanzia ndege yenyewe, viwanja, barabara na miji wanayokwenda. Wakati umefika sasa tuache kusimulia tu uzuri, mipango na utalii wa miji ya wengine huku kwetu pakionekana ni pango la wanyanganyi. Umefika wakati viongozi wetu wakose appetitite ya kusafiri nje kutafuta huduma kwa kigezo kuwa Dar es Salaam tunazo zaidi ya mahitaji yetu. Ifike mahali tuone kuwa hata sisi tunaweza kujitengenezea mbingu yetu wenyewe badala ya kila wakati kuwa watu wa kunukuu na kurejea mifano ya mafanikio ya Malyasia, Indonesia, India, China, Rwanda na Nairobi. Wakati umefika tuache kulalamika, kulaumu na kunyooshea watu vidole. Tunaweza kazi hii bila msaada wa wageni maana ni kwetu.
14

Tuanze sasa na Tuanze na Jiji la Dar es Saalam Mwalimu MM mathewmndeme@gmail.com

15

You might also like