You are on page 1of 5

1

PRESS 15/9/2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI ITAKAYOTOLEWA NA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM
SULEIMAN KOVA TAREHE 15, SEPTEMBA 2014 KATIKA UKUMBI
WA MIKUTANO WA KANDA MAALUM
UTANGULIZI
Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam ina utaratibu wa kufanya
mazungumzo na wananchi kwa kupitia vyombo vya habari vya aina
mbalimbali kwa lengo la kuwapasha habari wananchi kuhusu hali ya
usalama jijini na hatua zinazochukuliwa na Polisi Kanda Maalum ya Polisi
Dar es salaam katika kukabiliana na changamoto za uhalifu jijini na
mafanikio yaliyopatikana katika kipindi husika.
Katika kipindi cha wiki mbili tangu tulipokutana mara ya mwisho
yametokea matukio ya uhalifu ya hapa na pale ambayo wananchi
ambao ni walaji wa huduma za ulinzi na usalama wanatakiwa kupewa
taarifa ili kwa pamoja tushirikiane kupunguza uhalifu jijini au
kuutokomeza kabisa.

TAARIFA YA MAFANIKIO KATIKA UTENDAJI
Matukio yaliyojitokeza katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ni haya
yafuatayo


2

OPERATION MALUM YA KUZUIA KUPAMBANA NA MATISHIO YA
UHALIFU KUFANYIKA DSALAAM.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum linaanzisha operesheni maalum ya
kupambana na vitendo mbali mbali vya uhalifu ambayo vimejitokeza na
kuashiria uvunjifu wa amani na kuleta tishio kwa wakazi wa Dsalam.
Matukio yaliyojitokeza kwa matishio ni kama yafuatayo:-
1. Ujambazi wa kutumia silaha
2. Dawa za kulevyaa za viwandani na mashambani
3. Majambazi wanaoteka na kufanya uhalifu dhidi ya watu
wanaosafirisha fedha taslim kiholela
4. Majambazi wanaovizia katika mabenki na maduka ya kubadilishana
fedha (Bureau De Change)
5. Vikundi vinavyojihusisha na itikadi kali kwa kutumia mwavuli wa
Dini, siasa au wahalifu wanaofanya vitendo vinavyoashiria na
kujielekeza katika kufanya ugaidi.
6. tutapambana na kero ambazo ni vyanzo vya uhalifu ambavyo ni
maeneo yanayojihusha na kusambaza na kuuza dawa za kulevya,
upishi wa pombe haramu ya gongo, baa na grocery yanayokesha
na katika pamoja na wateja wao wakilewa kucha na wale
wanaopiga mziki usiku katika mtaa bila kujali maisha au
mapumziko kwa raia wengine wanaoishi jirani.
Operesheni hiyo imezingatia kumbukumbu za uhalifu ambazo
zimeanza kujitokeza wakati wa mchana na usiku ambapo kama
mwenendo huo hautadhibitiwa hali ya utulivu katika jiji la DSalaam
utavurugika na wananchi wataanza kuishi katika hali ya hofu. Aidha
yapo mawasiliano ya karibu kati ya Polisi Kanda Maalum na
Makamanda katika mikoa ya mipakani ili kuhakikisha kwamba silaha
zote zinazoingia DSalaam hazivushwi kiholela kwa njia za panya
katika mikoa hiyo na hatimaye kutumika kwa uhalifu katika jiji la
DSalaam.
Operesheni hii kali ya aina yake inataendeshwa kwa awamu tatu hadi
mwishoni mwa mwaka huu. Tunatoa wito kwa wananchi waendelee
3

kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili mafanikio makubwa zaidi
yapatikane dhidi ya uhalifu.
MTANDAO WA WAHALIFU WANAOTUMIA TEKNOLOJIA YA
MAWASILIANO (IT) WAKAMATWA JIJINI DA ES SALAAM

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam limewakamata
watu wawili wanaojihusisha na mtanda wa uhalifu kwa kutumia
Teknolojia ya Mawasiliano (IT) ambapo taarifa za kiintelijensia
zilionyesha kwamba lengo lao ni kuwasaidia wahalifu wa aina mbalimbali
ikiwa ni pamoja na wale wa kutumia silaha. Pia imebainika kwamba
watuhumiwa hawa huwasaidia watu walioiba simu kwa kubadilisha
kumbukumbu zao ili wasiweze kukamatwa na Polisi.

Watuhumiwa hawa walikamatwa tarehe 11/09/2014 huko Kariakoo
katika mtaa wa Agrey wakijifanya ni mafundi wa kawaida wa simu
ambapo wamesomea teknolojia ya mawasiliano (Information
Technology) katika vyuo vilivyopo jijini Dar es Salaam kwa sasa ni
mafundi wa simu za mikononi ambao hujihusisha na vitendo vya
KUFLASH SIMU, KUFUNGUA PASS WORD, na kupoteza IMEI NAMBA za
simu wanazoletewa na wahalifu kwa lengo la kubadilisha utambulisho
(IDENDIFICATION) na uhalisia wa simu husika.
Majina ya watuhumiwa ni kama ifuatavyo:-
1. EDSON S/O KENNEDY NDEIKYA, miaka 27, fundi simu mkazi wa
Mabibo Kanuni.
2. IBRAHIM S/O MUHDINI KASUKU, miaka 23, fundi simu, mkazi wa
Keko Magurumbasi.
MAJAMBAZI SUGU WAWILI WAKAMATWA NA SMG JIJINI
DAR ES SALAAM

Jeshi la Polisi Kanda Maalum limeendelea na oparesheni zake
kuwatafuta na kuwakamata majambazi wote wanaofanya uhalifu wa
kutumia silaha na uhalifu mwingine ili sheria ichukue mkondo wake.
Katika oparesheni hiyo yamekamatwa majambazi wawili kwa kosa la
kumiliki silaha kinyume cha sheria na kuitumia katika matukio ya
ujambazi.

Kabla ya kukamatwa kwa bunduki hiyo watuhumiwa walikuwa
wamepanga kufanya tukio la ujambazi katika maduka ya MPESA na
4

TIGO PESA yaliyopo maeneo ya Sinza Madukani. Majambazi hao
waliahirisha kufanya tukio baada ya kushtukia mtego wa polisi.

Mnamo tarehe 10/09/2014 majambazi hao walikamatwa baada ya Polisi
kupata taarifa kuwa yamejipanga kufanya tukio la uhalifu maeneo ya
YOMBO DOVYA na kisha kuweka mtego katika nyumba ya ASIA D/O
ALLY KASHINDE anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 iliyopo
maeneo ya Yombo Makangarawe (M) wa Kipolisi wa Temeke. Baada ya
kuwakamata majambazi hao walipekuliwa katika chumba wanacholala
ndipo ilipopatikana silaha aina ya SMG yenye namba IC 5740 ikiwa na
risasi 07 ndani ya magazine. Bunduki hiyo imekatwa mtutu na kitako.
Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kuwezesha kuwakamata wengine
wanaoshirikiana katika genge hili la ujambazi.

Majina ya watuhumiwa wa ujambazi waliokamatwa ni kama ifuatavyo:
1. KHAMIS S/O AMBA, Miaka 40, Mkazi wa Yombo Makangarawe.
2. OMAR S/O KHAMIS, Miaka 43, Mkazi wa Masasi Nyasa Mtwara


KUKAMATWA KWA TIKETI BANDIA 424 ZA MECHI YA NGAO YA
HISANI KATI YA YANGA NA AZAM

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda linawashikilia na kuwahoji
watu wawili kwa kosa la kupatikana na tiketi bandia za mchezo wa mpira
wa miguu wa kuwania NGAO ya JAMII uliofanyika mwishoni mwa wiki hii
kati ya timu za YANGA na AZAM zote za jijini Dar es Salaam.

Watu hao walikamatwa usiku wa tarehe 13/09/2014 maeneo ya Mission
Quarter, mtaa wa Masasi, Kata ya Kariakoo (M) wa Kipolisi Ilala Dare es
Salaam baada ya polisi kupata taarifa juu ya kuwepo watu hao eneo la
tukio. Polisi waliweka mtego na kufanikiwa kuwakamata BARAKA S/O
MZEE, Miaka 34, Mkazi wa Magomeni na NASSIB S/O KULWA,
Miaka 37, Mkazi wa Temeke Mwisho. Walipopekuliwa walikutwa na tiketi
bandia za mchezo huo wa ngao ya hisani kati ya timu ya Yanga na Azam
zote za jijini Dar es Salaam.

KUPATIKANA KWA SILAHA AINA YA PISTOL NA RISASI SITA (6)
Jeshi la Polisi limefanikiwa kupata silaha aina ya pistol glock yenye
namba TZ CAR 10315 yenye magazine moja na risasi 6 baada ya genge
5

la wahalifu kukurupushwa na Polisi walipokuwa wakipanga kufanya tukio
la unyanganyi wa kutumia silaha huko maeneo ya Tegeta Msichoke kata
ya Kunduchi wilaya ya Kipolisi Kawe.
Tukio hilo lilitokea tarehe 3/9/2014 baada ya majambazi kukimbia na
kutelekeza begi baada ya kupekuliwa na polisi walikuta sina hiyo pamoja
na vitu vingine kama jeki moja, shoka ndogo moja, mkasi mmoja wa
kukatia waya, tindo moja ya kutobolea ukuta, kisu kimoja kidogo na saa
ya mkononi. Pia ilikamatwa pikipiki moja yenye namba T.412 CXV aina
ya King Lion rangi nyekundu ambayo imeachwa na wahalifu hao.
HITIMISHO
Kwa kuwa ili uhalifu utokee ni lazima pawe na fursa zinazoshawishi
kutendeka kwa uhalifu. Miongoni mwa mazingira rafiki kwa ajili ya
kufanyika kwa matukio makubwa hasa ya unyang`anyi wa kutumia
silaha au nguvu ni uendeshaji wa shughuli za uuzaji wa vileo bila
kuzingatia sheria, upigaji wa muziki kwa sauti ya juu wakati wa usiku bila
kikomo na kuendesha shughuli za biashara usiku bila ya kuwa na mfumo
mzuri wa ulinzi na usalama.
Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es salaam inatoa wito kwa wananchi,
wafanyabiashara, wanahabari na makundi mbalimbali kushirikiana na
Jeshi la Polisi kwa hali na mali sambamba na kutoa taarifa za mitandao
ya uhalifu ili Jeshi la Polisi liweze kujipanga vizuri kukabili vitendo vya
kihalifu na kuifanya jamii ya Dar es salaam iweze kuishi bila hofu ya
uhalifu.
Pia tunasisitiza wafanyabiashara kuheshimu masharti ya yaliyopo katika
leseni za biashara zao sambamba na kuimarisha ulinzi katika maeneo
yao ya biashara.

S.H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM YA POLISI
DAR ES SALAAM.

You might also like