You are on page 1of 1

A-One Products and Bottlers Limited

Nafasi za kazi ya Mauzo


Dar es Salaam, Arusha, Moshi, Tanga, Dodoma, Singida, Igunga, Manyoni, Mbeya, Kyela,
Morogoro, Mwanza, Musoma, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Bukoba, Mjombe / Makambako,
Songea, Iringa / Mafinga / Ilula, Lindi / Masasi / Mtwara, and Ifakara
Moja ya kampuni yetu, A-One Products and Bottlers Limited imeanzisha uzalishaji na mauzo ya
bidhaa za vinywaji vya Soda - ambavyo ni Mo Cola, Portello, Mo Chungwa, Mo Embe, Mo Bomba,
Mo Lemon, Mo Mint na aina mbili ya ladha Mo Malta. Tunahitaji watu wenye ujuzi na uaminifu kwa
ajili ya kuendesha shughuli za mauzo kwenye matawi yetu.
Afisa - Masoka (Sales Supervisors)
Afisa masoko wote watakuwa na jukumu la kuchukua oda zote, kusimamia usambazaji wa bidhaa
kwenda kwa wateja husika, na kuongeza na kupanua mauzo kwa kutumia njia za kiufasaha na
kiutaalamu na ubunifu za kuwahudumia wateja awe na elimu kuanzia Diploma na uzoefu wa miaka
mitano katika mauzo ya bidhaa aina ya vinywaji katika miji mikubwa, miji midogo ,na vijiji katika
eneo lake la kazi.
Wauzaji (Salemen / Salesgirls)
Kazi kubwa ni kuwahudumia wateja wote kulingana na mpangiliowa kazi na taratibu zitakazowekwa
na kiongozi wake, awe anajua kusoma na kuandika anaujuzi wa miaka 2-3 katika mauzo ya bidhaa
aina ya vinywaji vinavyotambulika nchini katika miji mikubwa, miji midogo na vijiji katika eneo
lake la kazi.
Madereva (Drivers)
Awe ana ujuzi wa kuendesha gari na leseni hai inayomruhusu kuendesha gari na uzoefu usiopungua
miaka mitatu. Awe anafahamu vizuri maeneo yote ya miji mikubwa, miji midogo na vijiji katika eneo
lake la kazi
Mwombaji atatakiwa awe na wathamini wawili ambao itabidi wawe watu wanaofahamika na
kupatikana iwapo Kampuni itawahitaji.
Tuma CV yako ndani ya siku 15 ya tangazo hili kupitia recruitment@metl.net au kwenye anwani
iliyopo chini
National Recruitment Cell
Mohammed Enterprises (Tanzania) Limited
P.O. Box 20660,Dares Salaam
Contact : 0715543608, 0765580073, 0682753764

You might also like