You are on page 1of 2

HOJA BINAFSI YA MHE KABWE ZUBERI ZITTO (MB) YA KUTAKA BUNGE LIJADILI HALI YA ZAO LA MKONGE NCHINI NA KUAZIMIA

KWAMBA MWAKA 2012 NI MWAKA WA KUPANDA MKONGE (Chini ya Kanuni ya 54(1) ya Kanuni za Bunge,Toleo la 2007)

Kwa kuwa Tanzania imekuwa katika mipango mbalimbali ya kuongeza mauzo ya bidhaa nje na kuongeza ajira kwa raia wake; na kwamba mazao ya kilimo yana mchango mkubwa sana katika kukuza uchumi wa nchi na hivyo kuondoa umasikini kwa Watanzania. Na kwa Kuwa Zao la Mkonge limeonekana ni zao linaloweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza mauzo nje ya nchi, kuongeza ajira na kuondoa umasikini; ukizingatia kwamba Tanzania imewahi kuwa mzalishaji mkubwa wa Mkonge Duniani na kwamba Tanzania imedhamiria kurejea katika hali hiyo; Na kwa kuwa Faida za Zao la Mkonge ni nyingi na zitakazosaidia kukuza uchumi wa nchi yetu na kwamba Tanzania imedhamiria kuboresha maisha ya wananchi wake, Na kwa kuwa Serikali ya Tanzania imetangaza Kilimo kuwa ni kipaumbele kwa kupitia kaulimbiu ya KILIMO KWANZA; Ninaliomba Bunge lako Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wake wa Tano wa Bunge la Kumi liazimie yafuatayo: 1. Kwamba Mwaka 2012 utakuwa mwaka wa kupanda Mkonge na hivyo Serikali kupitia Taasisi zake ijiandae inavyopaswa kutekeleza azma hii kwa kuhamasisha wakulima wadogo kupata Ardhi ya kulima Mkonge. Kampeni ya kupanda Mkonge ihusishe wadau mbalimbali. 2. Kwamba Serikali itaweka miundombinu ya kifedha kuwezesha kufikiwa kwa lengo la kupanda Hekta 200,000 za Mkonge na hivyo kusaidia wakulima wadogo na wakubwa kupata mikopo nafuu kutoka katika taasisi za kifedha, 1

3. Kwamba Sheria ya Mkonge ya mwaka 1997 ipitiwe upya kwa lengo la kuipa nguvu Bodi ya Mkonge katika kusimamia tasnia nzima ya Zao la Mkonge (upstream, midstream and downstream). Vile vile kuweka masharti ya Matumizi ya Bidhaa za Mkonge hapa nchini. 4. Kwamba Serikali ichukue hatua madhubuti kulinda bidhaa za Mkonge dhidi ya ushindani usio halali. 5. Serikali ichukue hatua ya kuwanyanganya wawekezaji walioshindwa kuendeleza mashamba ,kuyapangia matumizi mengine ikiwwemo kuyagawa kwa wananchi ambao watayaendeleza. 6. Kwamba Serikali ipige marufuku kuuza nje ya nchi bidhaa ghafi zinazozlishwa hapa nchini. 7. Kwamba ufanyike utafiti na mpangilio utakaobainisha ni ardhi ipi ya mashamba ya Mkonge yaendelee kutumika kwa zao la mkonge yaendelee kutumika kwa zao la mkonge na yepi yatumike kwa mazao mengine na shughuli nyingine.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. Kabwe Zuberi Zitto, Mb Jimbo la Uchaguzi -Kigoma Kaskazini 09.02.2012

You might also like