You are on page 1of 8

Na Clara Matimo, Mwanza 1 UKANDA WA ZIWA VICTORIA, una fursa tele za uchumi na biashara,lakini bado wananchi wake ni fukara

wanaoishi kwa kipato cha chini ya Dola moja kwa siku.( source ya taarifa hii?) Ziwa Victoria,linalobeba jina la ukanda huu,lina eneo ambalo ni takriban kilomita za mraba 69,000. Ni ziwa la pili kwa ukubwa (wapi?),nyuma ya Superior,huko Marekani na ni ziwa la kwanza kwa ukubwa hapa Afrika. Ni chanzo cha Mto Nile ambao ni mto wa pili kwa ukubwa hapa duniani,nyuma ya Mto Mississippi ulioko Marekani. Mbuga za Serengeti

Ziwa Victoria lina visiwa 500, kati ya hivi 200 hukaliwa na watu,katika nchi zote za Kenya,Uganda na Tanzania Katika Tanzania,ziwa Victoria hufikia katika mikoa ya

Kagera,Mwanza na Mara ambako kama wananchi wangewezeshwa vizuri,basi wangevua samaki kwa tija na kujipatia kipato cha kutosha kuwaondoa katika janga la ufukara. Jijini Mwanza pekee kuna viwanda zaidi ya vinane vya kusindika samaki(sangara) ambao husafirishwa Ulaya na Marekani. Sangara, ni samaki wanaopatikana ziwa Victoria pekee hapa duniani,lakini bado wananchi wa kawaida ambao ni wavuvi hawajanufaika vya kutosha.( unatoa maelezo tu bila kutoa mifano halisi. Je, viwanda hivyo havitowi masoko na ajira?) Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania(TTB), Peter Mwenguo, mikoa ya Kanda ya Ziwa ina vivutio tele vya utalii,ambavyo kama vitawezeshwa,vitazaa fursa za ajira na kipato kwa wananchi wa kawaida na kodi serikalini. Mkoa wa Mwanza una vivutio vya utalii kama ifuatavyo: Hifadhi ya Kisiwa cha Rubondo,Kisiwa cha

Saanane,Kijereshi pori la akiba,Mbuga za Serengeti ziko kilomita 100 tu kutoka jijini Mwanza,Makumbusho ya Bujora,mahali pa kihistoria,ambako watumwa walitunzwa kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar.(watumwa walipitia Bujora?) Magu,kuna kaburi la mpelelezi maarufu,Henry Stanley,(sio kweli!) kuna miamba ya Bismark,kuna mapango ya Hendebezyo iliyowahifadhi watu wakati wa vita vya kikabila huko wilayani Ukerewe. Katika kilima cha Isamilo,jijini Mwanza,ndipo mahali Speke(mpelelezi wa zamani) alisimama akitazama Ziwa Victoria na kutangaza kwamba ziwa hili lilikuwa chanzo kikuu cha Mto Nile. Ukara,kuna jiwe linalocheza dansi linapoimbiwa,kama lingetangazwa na kuhifadhiwa lingeweza kuwa kivutio na chanzo cha mapato cha watu na serikali za maeneo husika. MKOA WA MARA: umesheheni vivutio vingi vya utalii,kama fukwe za

Makoko, na kibara,visiwa vya Nyafuba,Lukuba na Nyamasanje ambako wanaishi wavuvi wa samaki. Kuna Mlima Mtiro,huko Masita,Majita ambao una dimbwi la maji yasiyokauka msimu mzima,kuna milima kama Kasino huko Tarime ambao una kreta, mlima Charibo uko Bunda,Bungaji una vifaa vya uhunzi na kuna mito yenye viboko wengi kama mto Mara, Rubana,Ikorongo na ngome za wajerumani kama Ikoma n.k Kuna kivutio cha makumbusho ya Butiama, mahali ambapo pia kuna kaburi la Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere. MKOA WA KAGERA. Mkoa wa Kagera una vivutio vingi vya utalii ambavyo pia vinaweza kuwa fursa za ajira kwa wananchi na chanzo cha mapato serikalini. Kuna nyumba ya Chifu Rukamba wa Kabale, mahandaki yaliyoko Bwanja,Kigarama na Katoke. Kuna maporomoko ya maji huko Kyamunene, nyumba

ya kijadi ya chifu Kasusura,michoro katika mapango ya Busota na vifaa vya uhunzi. Mkoani Kagera pia kuna Pori la akiba la Rumanyika na Biharamulo,kuna nyumba ya Chifu Rumanyika ambayo ilitumiwa pia kufua vyuma,kuna chemichemi za Mtagata,nyumba ya kijadi ya Chifu Bahamba na urithi wake,kuna mapango ya Yerusale,maporomoko ya Rusumo na Pori la akiba la Burigi. Nyumbu,katika mbuga za Serengeti Katika maeneo mengi ya Kanda ya Ziwa kuna madini mengi ambayo kama wazawa wangewezeshwa kiuchumi na kukopeshwa zana za uchimbaji na elimu ya ujasiliamali, wangeweza kuondokana na umasikini. Mji wa Mwanza ambao ni kitovu cha nchi za Maziwa Makuu,ungeweza kukua haraka na kuwa kituo kikuu cha biashara katika nchi hizo,kama ungekuwa na mahoteli ya nyota tano na sita. Jiji la Mwanza, hadi sasa lilikuwa na mahoteli ya hadhi

ya nyota nne, ambayo hayakuwa na hadhi ya kuweza kuhifadhi wakuu wa nchi. Miaka michache iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alimwalika Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni, kufanya mazungumzo jijini Mwanza. Kwa kuwa Rais Kikwete alichelewa kidogo kutua jijini Mwanza, kwa sababu alikuwa na kazi Dar es salaam, Rais Museveni alipowahi kuja Mwanza ,ndege yake ilishindwa kutua Mwanza kwa kuwa asingeweza kupata mahali pa kupumzika jijini Mwanza,yeye na ujumbe wake. Mwanza, kwa muda mrefu, hakukuwa na hoteli yenye uwezo wa kumhifadhi mkuu wa nchi, "Presidential Suit" na Rais Museveni asingeweza kwenda Ikulu ya Mwanza,wakati bado mwenyeji wake alikuwa hajafika! Miji ya Mwanza,Musoma,Bukoba na Geita,licha ya kuwa katika eneo lenye vivutio vingi vya utalii,bado haina mahoteli yenye hadhi ya kitalii ambayo yangejengwa katika visiwa na fukwe za Ziwa kubwa la pili duniani na la kwanza kwa ukubwa hapa Afrika, watalii wengi

wangefikia Kanda ya Ziwa. Hivi leo watalii wengi hufikia katika miji ya Arusha na Nairobi,nchini Kenya,licha ya kwamba Mwanza ni mji uliopo kilomita 100 tu kutoka lango la kuingilia Serengeti,Ndabaka Gate. Jiwe la Bismark jijini Mwanza MWISHO Clara, Kwa bahati mbaya hii sio habari ya kitafiti wala yakichunguzi. Kimsingi inatoa maelezo elezo ambayo hayana lolote jipya. Kazi yako ilipasa kulenga sababu/ kwa nini fursa hazitomiki. Mbaya zaidi ina facts zisisosahihi Stanley hakuzikwa Magu! Fanyia utafiti hilo. Story yako ina uhaba wa sources wakuongelea matatizo ulioainisha. Sasa kazi yako nikutafiti kwa nini fursa hazitumiki kikamilifu. Lenga fursa moja uitafiti kwa kina ( mahoteli, utalii, uvuvi?) ongea na watalaamu, wafanyabiashara na wananchi wakawaida.

Kopoka

You might also like