You are on page 1of 2

25th Sept, 2012. Kumb: NCS/FILE No 18/01/02/12. Erick Mukulungi, S.L.P.. Dar Es Salaam. Ndugu, YAH.

MAREJESHO YAKO YA MWEZI JUNE, JULAI NA AUGUST 2012 UNAYODAIWA. Kichwa cha habari hapo juu chahusika sana. Ofisi ya Ndugumbi Community SACCOS, inakutaka kufanya marejesho yako matatu ambayo hujafanya hadi hivi sasa, yaani rejesho la tarehe 13/06/2012, 13/07/2012 na 13/08/2012, jumla ya shilingi za kitanzania 2,280,000/= ikiwa ni :Mkopo wa Tshs 500,000/= x3 1,500,000/= Riba ya Tshs 120,000/= x3. 360,000/= Akiba ya Tshs 50,000/=x3.150,000/= Adhabu ya Tshs 90,000/=x3.270,000/= JUMLA2,280,000/= Ofisi imefikia hatua hii baada ya kufanya jitihada za kukutaka kurejesha pasipo utekelezwaji wowote. Ofisi inakupa siku saba (7) kuanzia tarehe ya barua hii kutekeleza agizo hili, tofauti na hapo ofisi itachukua hatua za kisheria dhidi yako, kwa mujibu wa sheria na kanuni za Saccos yetu. Ni matumaini yetu kwamba utekelezwaji wa agizo hili utafanyika kwa haraka sana ili kuepusha usumbufu na adha yoyote ile itakayoweza kujitokeza . Ahsante sana. Wako katika ujenzi wa Taifa, Eva Dominick Mushi. Nakala kwa; 1) Charles Lucas Mgonja [Mdhamini]. 2) Kamati ya mikopo - Taarifa. - Taarifa. (Manager).

You might also like