Professional Documents
Culture Documents
A
E
I NV
RONM EN TA LN
ET
DO D O M
RK WO
D O N E T
MWONGOZO WA MWANANCHI JUU YA KUZIFAHAMU NA KUZIJUA SERA NA MIONGOZO KATIKA SEKTA YA MAZINGIRA, ARDHI NA MISITU
1
1.
a)
UTANGULIZI
Viumbe hai
Neno mazingira linajumuisha viumbe hai na visivyo hai na mfumo wa maisha ya binadamu na viumbe vinginevyo. Kwa maana nyingine Neno mazingira hujumuisha hewa, ardhi na maji; uhai wa mimea na wanyama ukiwemo uhai wa binadamu; hali za jamii, Viumbe kijamii, kiuchumi na ustawi wa maisha ya visivyo hai wanadmau na jumuia zao, shughuli za wanadamu pamoja na ama sehemu moja, au mchanganyiko wa mahusiano ya vyotevilivyotajwa hapo juu.
b)
Neno Sera linatafsiliwa kama ni matamko ya jumla ya serikali au taasisi au chama yanayotoa mwelekeo au dira na majukumu ya washirika au wadau. Hivyo kila sera ina lengo kuu au lengo la jumla ambalo halina budi kuzingatiwa wakati wa kuainisha madhumuni ya sekta inayohusika na sera hiyo
c)
Maisha ya watanzania wote ni yenye uhusiano wa karibu sana na mazingira. Ni lazima tujitahidi kusiamamia mazingira na maliasili zake kwa namna inayotoa nafasi ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo yanayojihimili kwa vizazi vya sasa na kwa vizazi vijavyo. Watanzania hatuwezi kufumbia macho athari za kimsingi za uharibifu wa mazingira zitokanazo na shinikizo za shughuli za maendeleo. Matatizo yatokanayo na uharibifu wa mazingira ni halisi na si uzushi, na yanatuhusu sisi sote. Kuna Uhusiano tegemezi kati ya uharibifu wa mazingira na umasikini. Uharibifu wa mazingira hasa husababishwa na kuenea kwa umasikini; vivyo hivyo, umasikini mara nyingi husababisha uharibifu wa mazingira. Matatizo yatokanayo na maendeleo duni kama umasikini, afya duni, na mengineyo ambayo huikabili idadi kubwa ya watanzania, kwa kiasi kikubwa yana uhusiano na mazingira kwa maana ya kwamba ni ya kimaendeleo.
4
d)
Shughuli za kila siku za binadamu mara nyingi hutegemea uwepo wa eneo ambalo ni sehemu moja wapo ya mazingira. Katika tafiti mbalimbali zimeonyesha ya kuwa hali halisi ya mazingira ya Tanzania inatia wasiwasi. Uchambuzi umebaini matatizo sita yanayohitaji suluhisho la haraka. Matatizo haya ni:
Uharibifu wa ardhi (kutokana na matumizi mabaya) Kutopatikana kwa maji safi kwa wakazi wa mijini na vijijini Uchafuzi wa mazingira Upotevu wa makazi ya viumbe pori na bioanuwami Uharibifu na makazi ya viumbe wamajini; na Uharibifu wa misitu
5
Cont.
e)
Hatua mbalimbali zimechukuliwa na serikali ya Tanzania katika kuimarisha ustawi mzuri wa maisha ya wananchi wake pamoja na kuwaletea maendelea katika sekta zote za kijamii na kiuchumi. Juhudi zinafanyika ili kuubalisha mfumo wa uchumi ili uwe uchumi wa soko huria, ambapo sekta binafsi inapewa nafasi kubwa zaidi. Ongezeko la uwekezaji katika sekta mbalimbali za Kiuchumi yatasababisha mabadiliko ya mfumo mzima wa uchumi. Aidha yatathiri shughuli kubwa za kiuchumi, mgawanyo na matumizi, na mazingira kwa ujumla
Cont....... Katika mabadiliko haya ya kiuchumi, mtazamo wa serikali utakuwa katika sekta za kilimo na viwanda, hususani Utalii,madini na miundo mbinu ya usafirishaji, kama vichocheo muhimu vya kukuza uchumi. Serikali inatambua kwamba, kuendelza sekta ya kilimo, kunaweza kuleta athari kubwa na mbaya kwa maliasili na mazingira, hivyo kudhoofisha zaidi ukuaji wa kilimo. Upanuaji wa kilimo unamaanisha upanuzi wa mashamba katika maeneo ambayo ni misitu na yika, maeneo ya wanyama pori; kukaushwa kwa matindiga, kupanua kilimo cha umwagiliaji unaosababisha maji yatuame na yaongeze chumvichumvi ardhinini, na ongezeko kubwa la matumizi ya madawa ya kilimo, uchafuzi wa maji yaliyo chini ya ardhi kutokana na madawa yatumiwayo vibaya mashambani, na kadhalika. Vivyo hivyo serikali inatambua kwamba kupiga jeki sekta ya utalii, viwanda na miundo mbinu kunaweza kusabababisha mabadiliko katika matumizi ya maliasili na kwa mazingira
2.
a)
Malengo ya jumla juu ya Sera ya Taifa ya Mazingira Malengo ya haya yameainishwa kama ifuatavyo:
Kuhakikisha upatikanaji, ulizi na matumizi sawa ya rasilimali katika mahitaji muhimu ya vizazi vya sasa na vijavyo Kuzuia na kudhibiti uharibifu wa ardhi, maji, mimea, na hewa Kuhifadhi na kuimarisha urithi wetu wa ssili, na usio wa asili, ikiw apaojana bioanuwani zilizo katika mfumo wa kiikolojia Kuboresha hali na uzalishaji wa maeneoo yanayoharibiwa ikiwa ni pamoja na makazi ya vijijini na mijini ili watanzania waishi katika mazingira safi, mazuri na yenye kuzalisha Kuongeza utambuzi na ufahamu wa uhusiano katika ya mazingira na maendeleo, kuendeleza ushirikishwa wa watu binafsi na jumuiya katika maswala ya mazingira Kukuza ushirikiano wa kimataifa katika agenda ya mazingira na kupanua ushirikishwaji na kutoa mchango kwa mashirika na programu baina ya pande mbili, kikanda, na kimataifa ikiwa ni paoja na kutekeleza mikataba iliyowekwa.
10
b)
3.
Jitahadi nyingi zimefanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutoa sera mbalimbali katika kukabilina na matatizo yanayokabilina na mazingira, ikiwa ni pamoja na Sera ya Misitu ya Mwaka 1998, na Sera ya Ardhi ya mwka 1999. sera zote hizi zilitanguliwa na sera ya kilimo ya mwaka 1983 na ile ya mifugo ya mwaka 1984. Zote zinasisitiza umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwa na mipango na matumizi bora ya ardhi na mazingira kwa ujumla.
11
a)
SEKTA YA ARDHI
Historia ya uchumi wa nchi yetu inaonyesha kuwa muda mrefu kabla na baada ya uhuru pato la wananchi wengi linaendelea kuwa dogo. Na hii imetokana na kuwa na mfumo ya kisiasa na kuchumi ambayo haikuweza kuleta maendeleo makubwa kwa jamii. Kutokana na dhana hiyo serikali imetayarisha sera inayoeleza masuala ya usimamizi wa ardhi. Sera hii imetayarishwa kwa kuzingatia maoni na mapendekezo ya wadau (washiriki) wote, ikiwemo serikali yenyewe, taasisi mbalimbali zinazojihusisha au kutumia ardhi, na wananchi wa wote wa Tanzania
12
Cont..
Cont
b)
SEKTA YA MISITU
Katika sekta ya Misitu Sera ya Taifa ya Misitu imetungwa kwa kuzingatia mfumo wa jumla wa kiuchumi, kimazingira na kijamii. Sera ya misitu ina madhumuni yanayolenga kupiga vita umasikini na ufukara ili kuboresha hali ya maisha ya wananchi. Kimazingira sera inalenga kuhakikisha upatikanaji, ulinzi, na maamuzi sawa ya rasilimali kwa ajili ya mahitaji muhimu ya vizazi vya sasa na baadae bila kuharibu mazingira na kuhatarisha afya na usalama wa binadamu.
Neno Misitu lina maana ya ardhi yote yenye uoto wa mimea na uwingi wa miti ya kimo chochote kile ivunwayo, na isiyovunwa na iliyo na uwezo wa kuota mbao na mazao mengine yenye kurekebisha hali ya hewa au mfumo wa vyanzo vya maji, au yenye kuhifadhi mifugo au wanyama pori.
15
Cont
16
Lengo na Madhumuni ya Sera ya Misitu Lengo: Lengo kuu sera ya Taifa ya misitu ni kuimarisha mchango wa sekta ya misitu kwa maendeleo endelevu ya Tanzania kwa kuifadhi na kusimamia misitu yake kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo Madhumuni: Madhumuni ya sekta ya misitu kwa kuzingatia lengu kuu ya Taifa ni: Kuhakikisha upatiakanaji endelevu wa mazao na huduma ya misitu kwa kuwa na maneno ya kutosha ya misitu iliyohifadhiwa chini ya usimamizi madhubuti Kupanua ajira na kuendeleza pato kutokana na maendeleo endelevu ya viwanda vilivyijikita kwenye misitu na biashara Kuimarisha mifumo ya ikolojia kwa kuhifadhi bionuwai ya misitu, maeneo lindimaji na rutuba ya udingo Kukuza uwezo wa Taifa kusimamia na kundeleza sekta ya misitu kwa wadau (washirika wengine)
17
Cont
Kulingana na madhumuni hayo Sera inaelekeza yafuatayo ili kuwa na maendeleo endelevu ya misitu na uhifadhi wa mazingira
a) Matumizi mazuri ya rasilimali za misitu na programu za upandaji wa miti ili kukidhi mahitaji ya ndani na ya nje ya nchi b) Hifadhi ya ardhi kwa kuifanika kwa uoto itaendelezwa kwa kupanda miti c) Usimamizi utaimarishwa na sheria zianzohusika zinazohusika zitatekezwa kwa kupanda miti d) Misitu asilia yenye thamani kubwa za kibiolojia itahifadhiwa. e) Wakulima, wafanyabiashara, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs/ CBOs), shule na vikundi vingine vitahamasishwa kujishughulisha na upandaji miti.
18
4.
USHIRIKI/ NAFASI YA SERIKARI, VIKUNDI AU JUMUIYA ZA KIRAIA KATIKA UHIFADHI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Mazingira ni urithi wa kiasili na wa kiutamaduni. Kwa hiyo, vizazi vya sasa vinaweza kunufaika. Ni lazima kutambua utaratibu iliopo wa uendeshaji na kufikia njia na namna ambazo uratibu wa, na ushirikino kati ya vyombo mbalimbali vya kitaasisi vyenye majukumu yanayolingana, unavyoweza kuimarishwa. Aidha kuna haja ya kuunganisha dhamira na kazi za vyombo hivyo Baraza la Mawaziri ndilo kamati kuu na ya kudumu yenye jukumu la kuratibu na kutung asheria ambazo wizara mbalimbali huwasilisha malengo y aSera, mipango ya utekelezaji na vipaumbele
19
a)
20
Cont......
Mkurugenzi wa mazingira ana jukumu la Kuratibu vyama, vikundi au tasisi zote, ikiwemo serikali, katika maswala yote yanayohusiana na mazingira. Kuishauri serikali katika maswala ya kisheria yahusianayo na mazingira kwa kushirikisha mahusiano ya kimataifa, na usimamizi mzima wa serikali katika mazingira. c) Bazara la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (National Environment Management Council) NEMC
Baraza hili lina jukumu la kutoa Ushauri, na kusimamia utekelezaji wa maamuzi yanayohusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira na kufanya kazi ya usuluhishi wa kitaalamu katika kushughulikia tathimini ya athaliza uharibifu wa mazingira. Pia lina kazi ya kuaratibu na kufanya tafiti mbalimbali zihusianazo na uhifadhi wa mazingi kwa kuzishirikisha taasisi zote za umma na binafsi.
21
Cont....
d)
Serikali za Mitaa Serikali za mitaa zinawakilisha sehemu yenye uwezo mkubwa katika mfumo mzima wa serikali. Hiki ni chombo muhimu katika kuamua na kufanikisha malengo ya sera za mazingira. Zina wajibu wa kujenga, kuendesha na kuendeleza miundombinu kiuchumi, kijamii na kimazingira Serikali za mitaa zitawajibika kusimamia michakato y amipango na kuanzisha sera na sheria ndogondogo kuhusu mazingira kwenye maeneo yao,pamoja na kutekeleza dhima muhimu ya kuelimisha, kuhamashisha na kuitikia maoni y awatu wake kwa shabaha ya kutekeleza malengo ya mazingira.
22
Cont.....
e)
Kazi za kamati ya mkoa ya Sera ya mazningira itasaidiwa na Kamati za wilaya, Kata na Vijiji na zitafadhiliwa na mabaraza ya wilaya, kata na vijiji. Kamati hizo zitawajibika kuratibu nakutoa ushauri kuhusu vikwazo kweney utekelezaji wa Sera na programu za mazingira; kuongeza mwamko au utambuzi kuhuz mazingira, utoaji habari, ukusanyaji na utawanyaji habari zinazohusu mazingira katika wilaya, kata au vijiji vyao.
23
f) Vikundi vya kijamii Vikundi vya kijamnii vinaweza saidia uhifadhi wa mazingira kwa kuwa na miradi/ shughuli kuu mbili:
Shughuli za kiuchumi
Ambazo ni Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Usindikaji, Viwanda vidogovidogo na vikundi vya akiba na mikobo. Shughuli hizi za kiuchumi mara zote hulenga kuongeza kipato. Ambapo uzalishaji wa bidhaa hutegemewa kuwa wa juu na baadae kuzwa na kupata fedha ambazo zitatumiwa na wanakikundi.
Shughuli za kijamii
Miradi ya kijamii hulenga kuboresha upatikanaji wa hudumu mbalimbali kwa maeneo yao (kama vile mahitaji ya viwanda, Elimu, Afya n.k) huduma zinapokuwa karibu hupelekea kupunguza gharana za upatikanaji.
24
Cont.......
25
5. HITIMISHO
Kutokana na kero ya umasikini wa wananchi na uharibifu wa mazingira wananchi kwa kushirikiana na serikali na taasisi/ asasi/ wadau mbalimbali wanapaswa kuamka na kuamua kwa pamoja kupambana na uharibifu wa mazingira unaopelekea umaskini katika jamii zetu. Hivyo basi kwa kujatilia mkazo haya mkazo unatakiwa zaidi katika upangaji wa matumzi ya ardhi kwa kuwashirikisha wananchi wenyewe ili hatimaje waweze kutekeleza mipango na sera kikamilifu. Na mwongozo huu unaweka wazi mambo muhimu yakufanywa na kutekelezwa ikiwa sera na sheria zitatekelezwa ipasavyo.
26
ANSTENI
Imeandaliwa na
Lameck Batimo Sebyiga Project Officer/ Liaison Officer Dodoma Environmental Network (DONET) P.O.Box 1414 Cell: +255 713 285290/ +255 757 395662 Email: lansebys@gmail.com Dodoma, Tanzania
27