You are on page 1of 2

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Samsung yakabadhi rasmi gari kwa Mshindi wa promosheni ya Pambika na Samsung Mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Juma Musa Ramadhan (46) amekabidhiwa rasmi zawadi yake ya gari aina ya Mitsubishi Double Cabin toka kwa Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya gari hilo yaliyofanyika jijini Dar es salaam. Hatua hiyo imekuja mara baada ya droo kubwa ya Pambika na Samsung iliyochezeshwa siku ya Jumatatu ya wiki hii na kumtangaza Bw. Juma Musa Ramadhani amabe ni mfanyabiashara kuwa mshindi wa Jumla wa promosheni hiyo iliyodumu kwa muda wa wiki sita toka Novemba 7, 2013 mpaka Desemba 23, 2013. Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa gari hilo rasmi, Bw Juma alisema kwamba gari hilo limekuja wakati muwafaka ambapo atalitumia katika shughuli zake za biashara ambazo zinaanza rasmi mwakani. Nipo katika michakato ya mwisho ya kufungua duka langu kubwa maeneo ya Tabata Segerea ambako ndiko ninapoishi, na duka hilo limeshakamiliko kwa asilimia kubwa hivyo natarajia lianze kutoa huduma mwakani, hili gari kwangu naona kama baraka toka kwa Mwenyezi Mungu na mwanzo mzuri wa biashara yangu kwani limekuja wakati muwafaka, Asante sana Samsung kwa kuwajali wateja wenu haikuwa raisi kuamini mara pale tu nilipopokea simu lakini sasa naamini kweli nimeshinda gari hili alisema Bw Juma mara baada ya kukabidhiwa garii lake. Akizungumzia jinsi alivyoshiriki kwenye promosheni hiyo Bw. Juma alisema kwamba Nilinunua simu ya Samsung na kisha kujisajili katika mfumo wao maalum wa dhamana ambapo nilitambulishwa kwamba simu yangu ni halisi na imesajiliwa na Samsung Tanzania, hilo lilinipa furaha kwa kununua simu halisi lakini sikuwa najua kama nimeingia kwenye droo ya Pambika na Samsung, hivyo hata nilipopigiwa simu hii haikuwa rahisi mara moja kuamini nilichokuwa nikisikia toka upande wa pili. Akikabidhi gari hilo mara baada ya kuwasili dukani kwa mshindi huko Tabata Segerea Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania Bw Sylvester Manyara alisema kwamba promosheni hiyo aliandaliwa maalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa Watanzania juu ya athari zitokanazo na manunuzi ya bidhaa feki zilizoenea sokoni lakini pia kuhamasisha wananchi kununua bidhaa halisi na kuzisajili kwa mawakala walioidhinishwa.

Napenda kuwashukuru wale wote walioshiriki katika promosheni hii, kupitia promosheni ya Pambika na Samsung kumekuwa na ongezeko la zaidi ya asilimia 30 la wateja walionunua bidhaa halisi na kujisajili hivyo ni ishara njema kwamba kama wadau kushirikiana na mamlaka husika nchini Tanzania tukiungana pamoja kupambana na bidhaa feki basi tunaweza fanikiwa vita hiyo kwa asilimia kubwa. Ni matumaini yetu kwamba bado manunuzi ya bidhaa halisi yataenedelea hata mara baada ya kuisha kwa promosheni hii alisema Bw. Manyara Jumla ya washindi 90 wamepatikana katika kipindi cha wiki sita toka kuanza kwa promosheni ambapo katika droo za kila wiki walikuwa wanatoka washindi 15 waliokuwa wakijishindia bidhaa mbalimbali za kila wiki huku zawadi kubwa ikiwa ni gari jipya aina ya Mitsubishi Double Cabin iliyokuwa imesheheni bidhaa mbalimbali toka Samsung

You might also like