You are on page 1of 2

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Samsung Tanzania yapata Ongezeko la wateja Kusajili bidhaa kwa zaidi ya 30% Dar es Salaam, Tanzania Kampuni ya Samsung Tanzania imeelezea ongezeko la wateja kujisajili katika mfumo wa dhamana ya ziada kwa zaidi ya asilimia 30 ikiwa ni ongezeko kubwa kwa kampuni hiyo mara baada ya kuzinduliwa kwa promosheni ya Pambika na Samsung iliyoanza mwanzoni mwa mwezi Novemba na kumalizika wiki iliyopita iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wateja kununua na kusajili bidhaa halisi za Samsung nchini kote. Mapema akiwasilisha muhtasari wa ripoti ya promosheni ya Pambika na Samsung katika kuonyesha mafanikio ya kampeni hiyo, Bw. Sylvester Manyara ambae ni Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania alieleza jinsi promosheni ya Pambika na Samsung iliyodumu kwa wiki saba ambavyo haikuongeza tu mauzo ya bidhaa za Samsung bali pia iliongeza ufahamu wa wateja juu ya kununua bidhaa halisi pamoja na kusajili bidhaa katika mfumo wa dhamana wa zaida ambalo ndio lilikuwa lengo kuu. Tunafuraha kutangaza kwamba promosheni yetu ya Pambika na Samsung imeleta mafanikio makubwa, tumeshuhudia ongezeko la wateja zaidi ya asilimia 30 wakisajili kwa hiari katika mfumo wetu wa dhamana ya miezi 24. Ikionyesha mafanikio ya kampeni yetu kama sehemu ya mipango ya muda mrefu ya Samsung katika kuondoa tatizo la bidhaa feki Tanzania pamoja na kuongeza ufahamu juu ya umuhimu wa kununua bidhaa halisi. Huku kampeni yetu ikifikia kikomo wiki iliyopita tunaimani kwamba huu utamaduni wa kununua bidhaa halisi utaendelea hata baada ya kumalizika kwa promosheni alisema Bw. Manyara Malengo ya muda mrefu ya Samsung kama mdau mkubwa wa bidhaa za kielektroniki nchini Tanzania ni kutengeneza ukaribu na ushirikiano kati ya mamlaka za nchi zinazosimamia sheria, wateja, wazalishaji na jumuiya za kibiashara kupigana na tatizo la bidhaa feki nchini Tanzania, tunawaomba Watanzania kusimama imara na wadau wote katika vita hii dhidi ya bidhaa feki na kuendeleza utamaduni wa kununua bidhaa halisi hata kama si bidhaa ya Samsung. Taarifa hii iliyotolewa na Samsung Tanzania wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhitimisha mwisho wa promosheni ya msimu wa sikukuu inayojulikana kama Pambika na Samsung ambayo ilianza Septemba 7, 2013 kabla ya kufikia tamati Desemba 23, 2013. Promosheni hiyo ililenga kuwazawadia wateja wa Samsung vitu mbalimbali mara baada ya kununua na kusajili bidhaa halisi. Jumla ya wateja 90 waliibuka washindi wakati mfanyabishara mkazi wa Dar es Salaam Bw. Juma Musa Ramadhani (46) aliibuka mshindi wa jumla kwa kujinyakulia gari jipya aina ya Mitsubishi Double Cabin ikiwa ni zawadi kubwa ya promosheni. Bw. Manyara alisema kwamba kuuzwa kwa bidhaa halisi kwa wingi ni chanzo cha ajira hapa nchini. Bidhaa halisi zinaponunuliwa, nafasi za ajira nazo zinatengenezwa na kuimarika nchini

Tanzania. Hata hivyo bidhaa feki zinaleta ile hali ya kutakuwa na usawa wa ushindani katika soko hasa kwa wazalishaji wa ndani na wafanyabiashara, pia inaua viwanda na kuongeza tatizo la ajira nchini Tanzania. Tungependa kuwashukuru watu wote walioshiriki katika promosheni ya Pambika na Samusung na bado tunaendelea kuwahimiza wateja wetu kutumia bidhaa zetu halisi. Kuongezeka na kuimarika kwa mauzo kwa bidhaa zetu kunaleta ongezeko la ubora na thamanani kwa bidhaa zetu. Bado tunajivunia ongezeko kubwa la wateja katika bidhaa zetu zote na bado tunaendelea kuongeza teknolojia mpya kila siku katika kuvumbua bidhaa mpya zitakazorahisisha maisha ya Watanzania. Lakini pia tunaimarisha kitengo chetu cha huduma kwa wateja ili wateja wote wafaidike na huduma ya dhamana ya zaida alimalalizia Bw. Manyara.

You might also like