You are on page 1of 1

Siku ya 16: Jumanne, Januari 21, 2014 OMBI LA 1: SHUKRANI Baba, tunakushukuru kwa kuwa utafanya kila mahali

panapowazunguka watu wako kuwa Baraka na kutakuwa na mvua za Baraka juu ya kila mshindi mwaka huu (Eze. 34:26). (4:40-4:46pm). OMBI LA 2: KAZI ZA KIMUUJIZA Baba, kwa kupita fikira za kila mmoja, mpatie kila asiye na kazi kibali kisicho cha kawaida kwa kazi yoyote ya kimuujiza anayoitarajia mwaka huu (Zab. 37:25). (4:46-4:52pm). OMBI LA 3: KUHARIBU NGUVU ZA VIZUIZI Baba, haribu kila nguvu zinazoleta vizuizi na kudorora katika maisha ya kila mshindi mwaka huu wa Neema Inayozidi na mfanye kila mmoja kwa uweza wako akapate matendo ya ajabu (Zab. 144:1-3). (4:52-4:58pm). OMBI LA 4: MGUSO MKUU KUPITIA HUDUMA ZETU ZA UTANGAZAJI Baba, acha mguso wa huduma zetu za utangazaji kama vile huduma za kwenye mtandao, Redio Domi, Nyaraka katika magazeti n.k ukawe mkuu na kuleta shuhuda za ajabu mwaka huu (Mith 4:18). (5:10-5:16pm). OMBI LA 5: TAIFA LETU Baba, mtaabishe kila anayelitesa taifa letu, na kila matendo maovu yakawarudie wao na watoto wao (2Thes. 1:6). (5:16-5:22pm).
OMBI LA 6: MAKANISA YETU YOTE KUWA MALISHO YA MAJANI MABICHI Baba, tuma neno lako likiwa na nguvu mwaka huu, na kufanya makanisa yetu yote ulimwenguni kuwa malisho ya majani mabichi mahali ambapo kondoo watasitawi vema na kuimarishwa. (Mdo 6:7). (5:22-5:28pm).

You might also like