You are on page 1of 1

Mwanzo wa safari yangu Kutoka enzi za Mambo ya Walawi mpaka sasa.

Hesabu ya miaka yote ipo kwenye Kumbukumbu la Torati ambalo Yoshua aliwakabidhi Waamuzi. Nikisafiri pamoja na Ruthu na Samweli tulikutana na Wafalme wawili wakijadili Mambo ya Nyakati za uhai wa Ezra kabla ya Nehemia kujenga Kuta za Yerusalemu. Wakati tukiwasikiliza, mara akaja Esta na taarifa za Ayubu aliyekuwa taabani. Ikabidi tumtafute Daudi aje kupiga kinubi, Kuimba Zaburi na kutoa Mithali zilizompa ahueni. Baadaye, tukawa tukimsikiliza Mhubiri huku Wimbo Ulio Bora ukipiga taratibu. Tukaendelea mbele na kufika kwa nabii Isaya akiwa na Yeremia katika Maombolezo ya Ezekieli aliyepotelewa na nduguye Danieli aliyekuwa Mateka. Wakati huo Hosea, Yoeli na Amosi walikuwa wanatusubiri nyumbani kwa Obadia ili tukasikilize ushuhuda wa Yona aliyemezwa na Samaki. Ibada Hiyo ilikuwa Ikiendeshwa na Mika akisaidiwa na Nahumu. Ushuhuda uligusa maisha ya wengi na kupelekea Habakuki na Sefania kujitoa kikamilifu katika kumtumikia BWANA. Naye Hagai akaongeza ujumbe mfupi kwamba Fedha na Dhahabu ni mali ya bwana, baada ya kusikia hivyo Zekaria akafanya hima kuleta Zaka zote na Matoleo kwa Malaki. Safari ikaendelea, Mathayo na Marko wakaungana nasi mpaka kwa Dokta Luka, ambaye kwa wakati huo alikuwa na Yohana akiandika habari za Matendo ya Mitume ili kutuma kwa kanisa la Warumi na Wakorintho. Tukawasihi watupatie nakala nasi tufikishe kwa kanisa la Wagalatia. Waefeso wakapata taarifa za waraka huo, wakatusihi sana tuwafikishie wao pamoja na Wafilipi. Tukaona ni vema pia tuufikishe katika makanisa ya Wakolosai na Wathesalonike. Tukikaribia mwisho wa safari tukakutana na Timotheo aliyetupokea na kutukutanisha na Tito ndugu yake Filemoni katika kanisa la Waebrania. Siku hiyo Yakobo alikuwa akieleza kuhusu ujio wa Petro. Mara wakaingia Yohana na Yuda wakiwa na Kitabu kikubwa kinachoelezea Ufunuo wa Yohana.

You might also like