You are on page 1of 12

Bulletin

News
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali
kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
http://www.mem.go.tz
HABARI ZA
NISHATI &MADINI
Toleo No. 39 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - Oktoba 24-30, 2014
Kituo cha Kinyerezi kukamilika Machi mwakani Uk2
<
Hakuna Siasa
katika Gesi-
Masele
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele
2 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
NISHATI/MADINI
Hakuna Siasa katika Gesi-Masele
Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga (kulia) akizungumza na Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini (hawapo pichani) kuhusu hatua iliyofikiwa ya
ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi kilichopo jijijni Dar es Salaam
Na Greyson Mwase,
Dar es Salaam

N
aibu Waziri wa
Nishati na Madini
anayeshughulikia
masuala ya madini
Stephen Masele amesema
kuwa Serikali imedhamiria
kuendesha sekta ya gesi na
mafuta kitaalamu zaidi na sio
kisiasa kama inavyodhaniwa.
Masele aliyasema hayo
kwenye kongamano la mafu-
ta na gesi lililoambatana na
maonesho ya siku mbili lililo-
fanyika jijini Dar es Salaam
kuanzia Oktoba 21 hadi 22,
2014. Kongamano hilo lililoan-
daliwa na Wizara ya Nishati
na Madini kwa kushirikiana
na Mamlaka ya Usimamizi wa
Huduma za Nishati na Maji
(EWURA), Shirika la Maende-
leo ya Petroli Nchini (TPDC)
na Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) lilikutanisha
wadau mbalimbali kutoka se-
hemu mbalimbali nchini lengo
likiwa ni kujadili changamoto
katika sekta mpya za gesi na
mafuta, pamoja na kuzipatia
ufumbuzi
Masele alisema Serikali
imejipanga katika kuhakikisha
kuwa inazalisha wataalamu
watakaosimamia vyema sekta
mpya ya gesi na mafuta hivyo
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Stephen Masele (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Rais wa Taasisi ya
Wahandisi Nchini Mhandisi Dkt. Malima Bundara (kulia) mara alipotembelea banda la taasisi hiyo kwenye maonesho yaliyoambatana na
kongamano la mafuta na gesi jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 22 Oktoba, 2014
nchi kunufaika na uwepo wa
rasilimali hiyo.
Akielezea mikakati ya seri-
kali katika kuimarisha sekta
mpya ya gesi, alisema kuwa
Serikali imeanza kupeleka
wataalamu wake nje ya nchi
katika kozi mbalimbali kuhu-
siana na mafuta na gesi ili
waweze kusimamia sekta hiyo.
Tunataka kwa mwaka an-
galau tupeleke wanafunzi 20
kwenda kusoma nje ya nchi
ambao watakuja kuwa wasi-
mamizi wazuri wa sekta hii
mpya ya gesi, alisema Masele.
Masele aliendelea kusema
kuwa mikakati mingine iliyo-
fanywa na Serikali ni pamoja
na kuanzisha kozi za gesi na
mafuta katika vyuo vikuu vya
Dar es Salaam na Dodoma.
Suala la gesi na mafuta
linahitaji utaalamu wa hali ya
juu, halihitaji siasa kamwe,
ndio maana serikali imeamua
kuwekeza nguvu zake zote
katika utaalamu wa gesi na
mafuta ili nchi ifanikiwe ka-
tika usimamizi wa sekta hizi
muhimu, alisisitiza Masele
Alisema kuwa mikakati
mingine iliyofanywa ni pamo-
ja na kujifunza kutoka katika
nchi mbalimbali zilizoanza ku-
zalisha gesi na mafuta mape-
ma.
Aliendelea kusema ni-
shati ya umeme ni muhimu
katika ukuaji wa uchumi wa
nchi na kusisitiza kuwa tayari
wawekezaji wengi kutoka nje
ya nchi wameanza kuonesha
nia ya kuwekeza katika vi-
wanda vikubwa hali itakay-
opelekea nchi kutoka kwenye
orodha ya nchi masikini duni-
ani na kufikia kipato cha kati
ifikapo mwaka 2025 kama
dira ya maendeleo ya taifa ina-
vyoeleza.
Kituo cha Kinyerezi kukamilika Machi mwakani
Na Greyson Mwase,
Dar es Salaam

K
ituo cha kufua
umeme kwa njia ya
gesi asilia chenye
uwezo wa kuzalisha
megawati 150 cha Kinyerezi 1
kilichopo jijini Dar es Salaam
kinatarajiwa kukamilika mape-
ma mwezi Machi, mwakani,
imeelezwa
Hayo yamesemwa na
Kamishna Msaidizi wa Nisha-
ti- Umeme Mhandisi Innocent
Luoga katika ziara ya Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Ni-
shati na Madini, mara ilipo-
fanya ziara yake katika kituo
hicho ili kujionea maendeleo
ya ujenzi wake.
Akielezea hatua ya ujenzi
iliyofikiwa katika ujenzi wa
kituo hicho, Mhandisi Luoga
alisema kuwa kituo hicho am-
bacho kinajengwa na kampuni
ya Jacobsen ya kutoka nchini
Norway kiko katika hatua
za mwisho za ukamilishwaji
wake na kuongeza kuwa vifaa
vyote kwa ajili ya kukamilisha
ujenzi wa kituo hicho vime-
shawasili kama ilivyopangwa.
Alisema kuwa ujenzi wa
kituo hicho unagharimu Dola
za Marekani milioni 183 na
kusisitiza kuwa mpaka sasa
Serikali imekwishalipa kiasi
cha Dola za Marekani mil-
ioni 150
Aliendelea kusema
kuwa lengo la kituo hicho
ni kuongeza uzalishaji wa
umeme hadi kufikia Megawa-
ti 3,000 ifikapo mwaka 2015
na kuongeza kuwa ujenzi wa
kituo hicho ni moja ya miradi
29 iliyopo kwenye Mpango
wa Matokeo Makubwa sasa
(BRN)
3
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
MAONI
Tahariri
MEM
Na Badra Masoud
FIVE
PILLARS OF
REFORMS
KWA HABARI PIGA SIMU
KITENGO CHA MAWASILIANO
BODI YA UHARIRI
MHARIRI MKUU: Badra Masoud
MSANIFU: Essy Ogunde
WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase
Teresia Mhagama, Nuru Mwasampeta , Leonard Mwakalebela,
Mohamed Saif
INCREASE EFFICIENCY
QUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICE
SATISFACTION OF
THE CLIENT
SATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF
SHAREHOLDERS
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Kila la kheri Kongamano
Jotoardhi!!!
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Hakuna fidia REA
Awamu ya Pili
Na Greyson Mwase,
Mkuranga Pwani
Naibu Waziri wa Nishati na
Madini anayeshughulikia nisha-
ti Charles Kitwanga amesema
kuwa hakutakuwepo na fidia
katika utekelezaji wa mradi
wa usambazaji wa umeme vi-
jijini Mkuranga unaofadhiliwa
na Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) awamu ya pili.
Kitwanga aliyasema hayo ka-
tika mkutano wake na wananchi
wa kijiji cha Mwalusembe wilay-
ani Mkuranga katika mkoa wa
Pwani. Kitwanga alifanya zi-
ara mwishoni mwa wiki katika
wilaya ya Mkuranga ili kujionea
maendeleo ya utekelezaji wa mi-
radi ya umeme vijijini inayofa-
dhiliwa na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) awamu ya pili.
Kitwanga aliongeza kuwa
katika awamu ya kwanza ya
utekelezaji wa miradi ya usam-
bazaji wa umeme vijijini iliyo-
fadhiliwa na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA), wananchi wal-
ipewa fidia hali iliyopelekea
changamoto ya fedha nyingi
kutumika kama fidia kwa wa-
nanchi waliotoa maeneo yao
kwa ajili ya kupitishwa kwa ngu-
zo za umeme kuliko gharama ya
mradi halisi.
Alisema ili kukabiliana na
changamoto ya kutoa fedha
nyingi kama fidia, Serikali
ikaamua kutoa punguzo maalum
la shilingi 27,000 kama gharama
ya kuunganishiwa umeme huku
wananchi wenye kupenda ku-
unganishiwa umeme kijitolea
sehemu ndogo ya maeneo yao
kwa ajili ya kuwekwa nguzo
za umeme na kuanza kufaidi
umeme ili kujiletea maendeleo.
Umeme ni nishati muhimu
kipaumbele chetu kama Serikali
ni kuweka umeme hasa katika
maeneo yale ambayo wananchi
wake wanahitaji kuunganishi-
wa umeme pasipo kudai fidia,
na kwa wale wanaodai fidia ni
vyema wakasubiri tukimaliza
kwa wasiohitaji fidia. Alisisiti-
za Kitwanga.
Kitwanga alisema lengo ni
kupunguza gharama kubwa
inayotumika kama fidia na kui-
peleka katika maeneo men-
gine yenye kuhitaji umeme na
kusisitiza kuwa Serikali imeji-
panga kuhakikisha kuwa kasi
ya usambazaji wa umeme vi-
jijini ni kubwa ili kuendana
na dira ya maendeleo ya taifa
ya mwaka 2025 yenye kuitaka
Tanzania kuwa nchi yenye ki-
pato cha kati ifikapo mwaka
huo na kuondoka katika kundi
la nchi masikini duniani.
Kitwanga aliwataka wa-
nanchi kuanza kuweka miun-
dombinu ya umeme katika ny-
umba zao ikiwa ni pamoja na
kujaza fomu ili waweze kuun-
ganishiwa umeme.
Naibu Waziri wa
Nishati na Madini
anayeshughulikia
masuala ya
nishati Mhe.
Charles Kitwanga,
(aliyesimama)
akielezea mikakati
ya Serikali katika
kufikisha umeme
vijijini katika kikao
kilichoshirikisha
Mkuu wa Mkoa
wa Pwani
Mwantum Mahiza
na watendaji
wa Tanesco,
wataalamu
pamoja na
waandishi wa
habari.
u
Wiki ijayo Tanzania kupitiaWizara ya Nishati na Madini
itakuwa mwenyeji wa kongamano la wadau wa Jotoardhi
duniani ambalo litajadili masuala mbalimbali yanayohusu
uendelezaji wa vyanzo vya jotoardhi katika nchi zilizo katika
Bonde la Ufa.
Kongamano hilo limepangwa kufanyika katika ukum-
biwa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) kuanzia 29
hadi 30 Oktoba, mwaka huu huku ukitanguliwa semina ya
mafunzo kwa siku mbili kuanzia Oktoba 27 hadi 28, mwaka
huu ambapo jumla ya washiriki wapatao 500 wanatarajiwa
kuhudhuria kongamano hilo.
Washiriki katika kongamano hilo watatoka sehemu mbal-
imbali duniani wengi wakiwa wataalamu wa nishati, watoa
maamuzi pamoja na viongozi mbalimbali wa mashirika ya
kimataifa kama UNEP.
Pamoja na nchi yetu kuwa na vyanzo vingi vya jotoardhi
lakini bado hatujaanza kutumia jotoardhi kwa ajili ya kuzali-
sha umeme au matumizi mengine ikiwemo katika viwanda.
Jotoardhi ni rasilimali muhimu inayotokana na majimoto
yanayotoa mvuke chini ya ardhi (200C) ambayo hupatikana
umbali wa kuanzia km 2.5 hadi 3.
Mara nyingi hupatikana katika maeneo yanayopitiwa na
Bonde la Ufa.
Aidha, Jotoardhi ni moja ya vyanzo mbadala vya nishati.
Hivyo, Jotoardhi hutumika kuzalisha umeme na pia kwa
matumizi mengine kama kilimo (green houses- unyevunye-
vu), kukaushia mazao kama tumbaku (temperature kubwa
vyumbani), mahotelini (kuosha vyombo) na viwanda vya
saruji (kukaushia). Chanzo hiki hakichafui mazingira.
Hata hivyo nchi yetu bado haijaanza uzalishaji wa umeme
kwa kutumia jotoardhi lakini utafiti unaonesha kwamba kuna
maeneo zaidi ya 50 yenye dalili ya chanzo hicho. Kati ya vy-
anzo hivyo, eneo lililofanyiwa utafiti wa kitaalam ni Mbeya
(100MW au zaidi). Uchimbaji unaweza kufanyika wakati
wowote. Maeneo mengine ni Uyoi, Manyara, Natron haya-
jafanyiwa utafiti wa kutosha. Hazina inayokadiriwa kuwepo
nchini ni zaidi ya MW 5,000.
Hivi sasa Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini
imedhamiria kuendeleza chanzo hiki na ipo katika programu
mbalimbali za kitaifa na Kimataifa kwa ajili ya uendelezaji
huo. Baadhi ya wafadhili wameanza kuonyesha nia kusaidia
katika masuala ya utafiti wa awali na pia kujenga uwezo wa
wataalam.
Aidha, Serikali inaendelea na maandalizi ya mkakati, ka-
nuni na muundo wa kitaasisi ili kusimamia uendelezaji huo.
Kampuni ya Jotoardhi imeanzishwa Desemba, 2013 na im-
eanza kazi rasmi Julai, 2014.
Tunaamini Kongamano hili litachochea na kuhamasisha
matumizi ya nishati jadidifu ili kuchangia katika upatikanaji
wa nishati kwa nchi zilizopitiwa na bonde la ufa ikiwamo
Tanzania.
Vivyo hivyo kongamano hilo litumike kubadilishana
uzoefu na uelewa na watalaam kutoka katika nchi mbambali
hususan zenye uzoefu pamoja na kuimarisha uhusiano ka-
tika uendelezaji wa nishati ya jotoardhi.
Mwisho tunaamini kongamano hilo litajenga uelewa kwa
viongozi, watoa maamuzi, watunga sheria na wananchi kwa
ujumla kuhusu faida za jotoardhi hivyo kwa pamoja tunalita-
kia kila la kheri Kongamano hilo la Jotoardhi, mkoani Aru-
sha.
4 Bulletin News
http://www.mem.go.tz

TOTAL waonesha nia kutafti Ziwa Eyasi
Waziri wa Nishati
na Madini Profesa
Sospeter Muhongo
(katikati) akisisitiza
jambo wakati
alipokutana na
wawakilishi wa
Kampuni ya kutafiti
na kuchimba
gesi na mafuta
ya TOTAL OIL.
Wengine katika
picha ni baadhi
ya watumishi
wa Shirika la
Maendeleo ya
Petroli Tanzania
(TPDC) na
watumishi wa
Wizara ya Nishati
na Madini.
u
Na Asteria Muhozya, Dar es
Salaam
K
ampuni ya kutafiti na kuchimba
mafuta ya TOTAL OIL imeone-
sha nia ya kutafiti gesi na mafuta
katika Ziwa Eyasi.
Wawakilishi wa Kampuni hiyo wali-
yasema hayo walipokutana na Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo mwishoni mwa wiki na kuoe-
nesha nia ya kuwekeza katika sekta hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho,
Waziri Muhongo alieleza kuwa, zipo
fursa nyingi za uwekezaji katika sekta
ya mafuta na gesi na kuitaka kampuni
hiyo kuangalia namna inavyoweza ku-
fanya kazi na Tanzania kupitia Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC), ikizingatia uzoefu wake katika
masuala hayo.
Kuna fursa nyingi za uwekezaji,
mafuta yakigunduliwa ni biashara. Seri-
kali ina mipango madhubuti ya kupanua
bandari zake nchini ikiwemo bandari ya
Mbegani, Tanga na Dar es Salaam kwa
hivyo, suala la usafirishaji halitakuwa
tatizo,.
Aidha, Profesa Muhongo aliongeza
kuwa, Tanzania inahitaji wawekezaji
makini na inataka ushindani wa kibi-
ashara katika sekta ndogo ya mafuta na
gesi na kuitaka kampuni hiyo kuangalia
fursa za kibiashara kupitia gesi na mafu-
ta zilizopo nchini.
Tunataka ushindani, tunataka
kampuni nyingi katika sekta hii. BP ni-
mewaambia na ninyi njooni, tunakari-
bisha ushindani, alibainisha Muhongo.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) James Andilile, (wanne kutoka kulia) akieleza jambo wakati wa kikao baina ya Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Wizara na Kampuni ya TOTAL OIL
5
Bulletin News
http://www.mem.go.tz

Kitwanga aagiza
Tanesco kuunganishia
wateja umeme ndani
ya siku moja
Bodi mpya ya Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) ikiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya
GST, (waliokaa - katikati) ni Mwenyekiti wa Bodi,Profesa Justine Ntalikwa, wa kwanza kushoto (walio-
kaa) ni Katibu wa Bodi, Profesa Abdulkarim Mruma.
GST yapongezwa
Na Priscus Benard
Dodoma
M
wenyekiti wa Bodi mpya ya
Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST), Profesa Justine Nta-
likwa amempongeza Mtendaji
Mkuu wa Wakala huo Profesa
Abdulkarim Mruma kwa utekelezaji mzuri wa
majukumu ya GST, hususan utekelezaji mzuri
wa Mradi wa Uendelezaji Endelevu wa Rasili-
mali Madini (SMMRP).
Profesa Ntalikwa, aliyasema hayo katika
ofisi za GST-Dodoma wakati wa kikao kati ya
Bodi hiyo na Uongozi wa Wakala kilicholenga
katika kuwakaribisha wajumbe wapya wa Bodi
ya Ushauri ya Wakala wa Jiolojia Tanzania.
Pamoja na kutoa pongezi hizo kwa niaba
ya wajumbe wa Bodi, Profesa Ntalikwa aliahidi
kuwa Bodi hiyo itakuwa ikitoa ushauri wa mara
kwa mara kwa Wakala huo ili uweze kutekeleza
majumu yake ipasavyo na hivyo kuchangia ka-
tika juhudi za serikali za kupunguza umaskini.
Awali, akisoma ripoti ya utekelezaji wa ma-
jukumu ya GST, Mtendaji Mkuu wa Wakala
huo, Profesa Mruma, aliwaeleza wajumbe hao
kuwa asilimia 92 ya eneo lote la nchi (Tanzania
Bara) limeshafanyiwa utafiti wa kijiolojia na
asilimia 18 ya eneo lote la nchi limeshafanyiwa
utafiti wa jiofizikia kwa kutumia ndege (High res-
olution Airborne Geophysical Survey) na utafiti
wa jiokemia.
Aliongeza kuwa asilimia 100 ya eneo lote
ya nchi limefanyiwa utafiti wa jiofizikia kwa
kutumia ndege (Low Resolution Airbone Geo-
physical Survey).
Aidha, Profesa Mruma aliwaeleza wajumbe
hao wa Bodi kuwa GST kupitia Wizara ya Ni-
shati na Madini imeendelea na juhudi zake za
kutafuta wahisani ili kutekeleza jukumu la ku-
hakikisha taarifa za jiosayansi zenye ubora zina-
patikana na kuwafikia wadau kwa wakati, hivyo
kutokana na juhudi hizo, GST kupitia Wizara
kwa kushirikiana na Serikali ya Finland itafanya
utafiti wa miaka miwili katika eneo la Naching-
wea (Nachingwea block) ili kubaini madini ya
aina mbalimbali yakiwemo madini ya kimkakati
ya metali (strategic metals).Utafiti huu unatarajia
kuanza Mwezi Februari Mwaka 2015.
Akizungumzia utekelezaji wa Mradi wa
Uendelezaji Endelevu wa Rasilimali Madini
(SMMRP) ambao unafadhiliwa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki
ya Dunia, Mtendaji Mkuu alisema kuwa kupi-
tia mradi huo GST imenuifaika katika masuala
mbalimbali ikiwemo wataalam kupata mafunzo
mbalimbali, kupatiwa vifaa vipya na vya kisasa
vya kazi ambavyo vimepelekea ubora wa hudu-
ma na bidhaa zitolewazo na Wakala kuendelea
kuimarika.
Kupitia mradi huu, maabara ya kisasa ya
jioteknolojia imeanzishwa, na baada ya kukamil-
isha zoezi la kufunga vifaa na mashine mbalim-
bali za uchunguzi, maabara hiyo itakuwa moja
ya maabara kubwa katika Afrika Mashariki na
Kati na hivyo kutekeleza lengo la Wizara na
Serikali la kuongeza maduhuli, alisisitiza Prof.
Mruma.
Profesa Mruma aliongeza kuwa sehemu
kubwa ya mradi wa SMMRP imekamilika na
wataalam wapo kwenye hatua za mwisho za
kukamilisha uchoraji wa baadhi ya ramani za ji-
osayansi na wengine wanajiandaa kwenda kwe-
nye mafunzo juu ya uendeshaji na matumizi ya
vifaa vipya vilivyonunuliwa.
Alieleza kuwa kutokana na utekelezaji
mzuri wa mradi huo, Benki ya Dunia imekubali
kuongeza fedha zaidi ili kukamilisha baadhi ya
maeneo ambayo hayakufikiwa na mradi.
Wajumbe wa Bodi mpya ya Wakala wa Ji-
olojia (GST) ni Prof. Justine W. Ntalikwa (Mwe-
nyekiti), Prof. Abdulkarim Mruma (Katibu),
Prof. Shukrani Manya, Dk. Savinces J. Maron-
ga, Dk. Medard Kalemani, Bibi. Bertha Sambo,
na Bw. Augustine Ollal.
Kiwira
Na Greyson
Mwase, Pwani
Ili kuhakikisha wananchi wa-
nanufaika na nishati ya umeme
na kuchochea kasi ya ukuaji wa
uchumi, Serikali kupitia Wizara
ya Nishati na Madini ime-
agiza Shirika la Umeme Nchini
(Tanesco) kufanya kazi kwa
weledi na ufanisi lengo likiwa
ni kuwaunganishia wateja wake
umeme ndani ya siku moja
mara baada ya kukamilika kwa
taratibu za malipo.
Hayo yameelezwa na Naibu
Waziri wa Nishati na Madini
anayeshughulikia masuala ya
nishati Charles Kitwanga
alipokutana na mkuu wa mkoa
wa Pwani Mwantum Mahiza
na watendaji wa Tanesco katika
ziara yake ya kutembelea miradi
ya umeme inayofadhiliwa na
Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) awamu ya pili.
Waziri Kitwanga alisema kuwa
ili kuendana na kasi ya ukuaji
wa uchumi wa nchi, shirika la
Tanesco linatakiwa litoe huduma
kwa ubora wa hali ya juu, wa
kuridhisha na kwa wakati.
Inabidi ifikie mahali iwapo
mteja atalipia umeme kabla
ya saa nne asubuhi na ambaye
haitaji nguzo, basi aunganishiwe
umeme ndani ya siku hiyo hiyo,
na hili linawezekana. Alisema
Kitwanga.
Kitwanga aliendelea kusema
kuwa kwa wateja wanaohitaji
huduma ya nguzo za umeme,
shirika linatakiwa liwe limewaun-
ganishia umeme kwa kipindi cha
siku tatu.
Waziri Kitwanga aliongeza kuwa
Tanesco linatakiwa kuondoa
mfumo wa wateja kulipa madeni
yao kwa foleni badala yake,
walipe kwa kufuata mfumo
wa kielektroniki ili kurahisisha
ulipaji wake na wananchi kupata
huduma kwa wakati.
Aidha, Kitwanga aliongeza
kuwa ili kuondokana na adha
ya kukatika kwa umeme mara
kwa mara kutokana na sababu za
matengenezo ya miundombinu
ya umeme, Tanesco inatakiwa
kubuni mifumo mbadala ya
kuwezesha huduma ya umeme
kuendelea kupatikana wakati
matengenezo yakiendelea pasipo
kukwamisha shughuli za
uchumi.
Inatakiwa ifike mahala umeme
uwe ni kama oksijeni katika
mwili wa binadamu, mwili wa
binadamu ukikosa oksijeni kwa
muda mfupi unapoteza uhai,
tukielewa umuhimu wa umeme
kwa mantiki hii, zitatumika mbi-
nu mbadala za kuzuia kukatika
umeme wakati wa matengenezo
hivyo kupelekea uchumi wa
nchi kukua kwa kasi. Alisisitiza
Kitwanga.
Naibu Waziri aliendelea kusema
kuwa Serikali kupitia Wizara
ya Nishati na Madini imeji-
panga kuhakikisha kuwa nishati
ya umeme inachangia katika
kutimiza lengo la Dira ya Maen-
deleo ya Taifa ya Mwaka 2025
ya kuhakikisha kuwa ifikapo
mwaka 2025 nchi ya Tanzania
inaondoka kwenye kundi la nchi
masikini duniani na kuwa nchi
ya kipato cha kati.
Alisema kuwa katika nchi nyingi
zilizopiga hatua kubwa katika
ukuaji wa uchumi wake, nishati
ya umeme imechangia kwa kiasi
kikubwa mno na kusisitiza kuwa
Wizara ya Nishati na Madini
imejizatiti kuhakikisha kuwa
uchumi wa nchi unakua kupitia
mchango wa sekta ya nishati.
Wakati huo huo akielezea hali ya
umeme katika mkoa wa Pwani,
Meneja Mwandamizi wa Tane-
sco Kanda ya Dar es Salaam
na Pwani Mhandisi Mahende
Mugaya alisema kwa kipindi cha
kuanzia Januari hadi Septemba
mwaka huu Shirika la Tanesco
lilifanikiwa kuwaunganishia
umeme wateja 10, 100 katika
mkoa wa Pwani na kufikisha
asilimia 21.3 lengo likiwa ni
kufikisha asilimia 30 ifikapo
mwaka 2015.
Mhandisi Mahende aliongeza
kuwa kwa sasa shirika la
Tanesco linaendelea na zoezi la
ukarabati wa miundombinu ya
umeme iliyochakaa na kuongeza
kuwa ifikapo Februari mwakani
tatizo la kukatika umeme mara
kwa mara litakuwa limekwisha
kabisa.
Akielezea changamoto Shirika
la Tanesco linalokumbana nazo
katika shughuli zake katika
mkoa huo, Mhandisi Mahende
alitaja kuwa ni pamoja uchakavu
wa miundombinu ya umeme
na kusisitiza kuwa ukarabati
bado unaendelea katika maeneo
yaliyoathirika.
Mhandisi Mahende aliendelea
kusema kuwa changamoto
nyingine ni pamoja na madeni
sugu kwa wateja na kuongeza
kuwa hadi sasa Shirika linadai
shilingi bilioni 16 wateja mbalim-
bali na kusisitiza kuwa Tanesco
imepanga mikakati mipya ya
ukusanyaji wa madeni hayo.
Alibainisha changamoto
nyingine kuwa ni pamoja na
wizi wa umeme, na madai
ya fidia katika utekelezaji wa
mradi wa umeme wa awamu ya
kwanza uliokuwa unafadhiliwa
na Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) na kuongeza kuwa wa-
nanchi walidai fidia iliyokuwa
kubwa kuliko gharama za mradi.
nNi kwa utekelezaji mzuri mradi wa SMMRP
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati
Mhe. Charles Kitwanga, akisisitiza jambo katika kikao. Kulia ni Mkuu wa Mkoa
wa Pwani, Mwantumu Mahiza
6 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Matukio pichani
Mbunge wa viti maalumu Singida Martha Mlata akichangia jambo katika kongamano hilo
Mkurungenzi Msaidizi- Gesi
Asilia kutoka Shirika la
Maendeleo ya Petroli Nchini
(TPDC) Joyce Kisamo
akichangia mada katika
kongamano la Tatu la Mafuta
na Gesi lililofanyika hivi
karibuni jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu kutoka kampuni ya
BG Fred Kibodya (kushoto)
akimwonesha Naibu
Waziri wa Nishati na Madini
anayeshughulikia Madini
Stephen Masele (katikati)
moja ya machapisho ya
kampuni hiyo. Wa pili kutoka
kulia ni Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini
Mhandisi Ngosi Mwihava
u
ABG kuongeza
kiwango cha malipo
kwa Halmashauri
Na Veronica Simba Dar
es Salaam
K
ampuni ya African Bar-
rick Gold (ABG) itaanza
kulipa asilimia 0.3 ya ma-
pato yao kwa Halmashauri
husika badala ya kiwango
kinacholipwa sasa na Makampuni ya ma-
dini cha Dola za Marekani 200,000 kwa
mwaka.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni
na Afisa Mtendaji Mkuu wa ABG,
Bradley Gordon wakati wa kikao baina
ya uongozi wa juu wa kampuni hiyo na
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo kilichofanyika Makao
Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam.
Gordon alisema ABG itaanza kulipa
kiwango hicho kipya kuanzia mwaka huu
wa fedha kwa Halmashauri za Wilaya za
Tarime, Kahama na Bulyanhulu ambako
kampuni hiyo inamiliki na kuendesha
migodi mikubwa ya North Mara, Buzw-
agi na Bulyanhulu, kufuatia makubaliano
yaliyofikiwa kati ya ABG na Wizara ya
Nishati na Madini.
Akizungumzia usimamizi wa
matumizi ya fedha hizo ili kuhakikisha
zinawanufaisha walengwa ipasavyo,
Waziri Muhongo alisema malipo husika
yatafanyika hadharani yakishuhudiwa na
Wizara pamoja na wananchi wenyewe.
Wananchi watashirikishwa kucha-
gua vipaumbele vya matumizi ya fedha
zao, alisema Waziri Muhongo na
kuongeza kuwa matumizi ya fedha hizo ya-
takaguliwa kwa kufuata taratibu za Serikali.
Akizungumza katika kikao hicho,
Makamu wa kwanza wa Rais wa ABG,
Deo Mwanyika alisema kampuni hiyo imed-
hamiria kufanya mabadiliko kadhaa yanay-
olenga kuboresha utendaji na hivyo kupata
ufanisi zaidi katika biashara ya madini.
Alitaja moja ya mabadiliko yatakay-
ofanyika hivi karibuni kuwa ni kuhamisha
Makao Makuu ya ABG kutoka Johannes-
burg Afrika Kusini na kuyahamishia Dar es
Salaam, Tanzania.
Kazi zote kubwa za ABG zitafanyika
hapa nchini japokuwa tutaendelea kuwa na
tawi la Ofisi zetu hapo Johannesburg, alise-
ma Mwanyika.
Mwanyika alisema mojawapo ya mi-
kakati ya ABG ni kuboresha utendaji kazi
ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya
wataalamu wazalendo badala ya wageni pale
kila itakapowezekana.
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na
Madini imekubaliana na Makampuni yote
yanayomiliki migodi mikubwa ya dhahabu
hapa nchini kulipa asilimia 0.3 ya mapato
yao kwa mwaka kwa Halmashauri husika
badala ya Dola za Marekani 200 ambazo
inalipa sasa.
Uongozi wa juu wa Kampuni ya African Barrick Gold (ABG)
(kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo (katikati) katika kikao baina ya kampuni hiyo
na Waziri hivi karibuni. Walioketi Kushoto kwa Waziri ni Viongozi
na Maafisa mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
n Sasa kulipa 0.3% ya mapato yake
kwa mwaka
7
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao cha kazi cha Idara ya
Madini wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa katika kikao hicho.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Alfred Shayo (katikati) akifungua
rasmi kikao cha Kazi cha Idara ya Madini kilichofanyika hivi karibuni katika hoteli
ya Kings Way ya Mkoani Morogoro. Kushoto ni Kamishna wa Madini, Mhandisi
Paul Masanja na kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini- Uratibu, Mhandisi John
Shija.
Wajumbe wa Bodi mpya ya Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) wakielezwa
jinsi maabara inavyoandaa sampuli katika maabara ya uchenjuaji madini
iliyopo Mbwanga nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Kamishna wa
Madini, Mhandisi
Paul Masanja
(kulia) akieleza
jambo kabla ya
ufunguzi wa Kikao
cha Kazi cha
Idara ya Madini.
Katikati ni Katibu
Tawala wa Mkoa
wa Morogoro,
Bw. Alfred Shayo
ambaye alikuwa
Mgeni Rasmi
katika kikao hicho.
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakala Jiolojia Tanzania
(GST), Profesa Justine Ntalikwa akiongoza kikao cha
bodi kilichofanyika ofisi za Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST).
Wajumbe wa Bodi mpya ya Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) wakioneshwa kazi zinavyofanyika
katika maabara ya uchenjuaji madini iliyopo Mbwanga nje kidogo ya mjini wa Dodoma.
8 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Geothermal: Solution to Africas Energy Needs
29 -31 October, 2014 AICC Arusha, Tanzania
Hosted and organized by the Government of the United Republic of Tanzania in collaboration with UNEP and other partners, Endorsed by the International Geothermal Association.
Na Veronica Simba
Dar es Salaam
N
chi za Tanzania na Fin-
land zinapanga kush-
irikiana katika sekta za
umeme jua, madini na
makazi kupitia mradi wa
uvumbuzi unaounganisha utafiti wa
kitaaluma na maendeleo ya kibiashara
unaoendeshwa na Chuo Kikuu cha
Aalto kilichoko Finland.
Akizungumza hivi karibuni katika
kikao baina yake na Ujumbe kutoka
Chuo Kikuu cha Aalto uliofuatana na
Balozi wa Finland hapa nchini Sinikka
Antila, Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo alisema
ushirikiano baina ya pande hizo mbili
utahusisha kufanya tafiti mbalimbali
pamoja na mafunzo katika sekta zi-
lizoainishwa.
Katika kikao hicho, Waziri
Muhongo aliwaagiza Wataalamu ku-
toka Wizara ya Nishati na Madini,
Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
Shirika la Umeme Tanzania (TANE-
SCO), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) na Shirika la Maendeleo la
Taifa (NDC) kukutana na Ujumbe
huo kutoka Chuo Kikuu cha Aalto ili
kujadiliana jinsi ya kushirikiana katika
sekta ya umeme jua.
Vilevile, Profesa Muhongo aliagiza
kufanyike kikao kingine kujadili ush-
irikiano wa pande hizo mbili katika
sekta ya madini. Alisema kwa upande
wa Tanzania, kikao hicho kinapaswa
kuwashirikisha wataalamu wa madini
kutoka Wizarani, Idara ya Madini ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo
cha Madini Dodoma (MRI), Wakala
wa Jiolojia Tanzania (GST), Shirika
la Maendeleo la Taifa (NDC) pamoja
na Wakala wa Ukaguzi wa Madini
(TMAA).
Kwa upande wetu, tunataka ku-
wasaidia wachimbaji wadogo, hivyo
pamoja na mambo mengine mtakay-
opendekeza katika ushirikiano huo,
msiwasahau wachimbaji wadogo, ali-
sisitiza Profesa Muhongo.
Aidha, kwa upande wa sekta ya
makazi, Waziri Muhongo alishauri
wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha
Ardhi, Shule ya Uhandisi ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam na wadau
wengine husika kukutana na Ujumbe
kutoka Finland ili kujadili namna ya
kushirikiana katika sekta hiyo.
Awali, akiwasilisha mada katika
kikao hicho iliyohusu kukitambulisha
Chuo Kikuu cha Aalto, Meneja wa
Mradi wa uvumbuzi unaounganisha
utafiti wa kitaaluma na maendeleo ya
kibiashara wa Chuo hicho, Sara Linde-
man alisema dhumuni la Mradi huo ni kuendesha utafiti wa hali ya juu ambao
utanufaisha jamii husika kutokana na uchunguzi unaojumuisha mambo mbalim-
bali ya kimaendeleo.
Alisema awamu ya kwanza ya Mradi huo itafanyika mwaka 2014 hadi 2015
ambapo kwa mwaka 2014 Mradi unalenga nchi za India, Mexico na Tanzania,
na utapanuka kuelekea katika nchi zinginezo mwaka 2015.
Tanzania, Finland kushirikiana katika sekta za nishati na madini
Meneja wa Mradi wa uvumbuzi unaounganisha utafiti wa kitaaluma na
maendeleo ya kibiashara unaosimamiwa na Chuo Kikuu cha Aalto kutoka
Finland, Sara Lindeman akiwasilisha mada ya utambulisho wa chuo hicho
kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na wataalamu
mbalimbali wa Wizara.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo akimpa mkono wa pongezi Balozi wa
Finland nchini, Bi Sinikka Antila mara baada ya
kikao baina ya Waziri na Ujumbe kutoka Chuo
Kikuu cha Aalto kilichoko Finland kilichofanyika
hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara, Dar es
Salaam. Katika kikao hicho, Tanzania na Finland
zilikubaliana kukutanisha wataalamu wake ili
kupanga namna ya kushirikiana katika sekta za
umeme jua, madini na makazi.
9
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
WIZARA YA NISHATI NA MADINI INAPENDA KUWATAARIFU WANANCHI WOTE KUWA:
TANZANIA ITAKUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA TANO WA KIMATAIFA WA JOTOARDHI
UTAKAOFANYIKA KUANZIA TAREHE 27 OKTOBA HADI TAREHE 2 NOVEMBA, 2014 KATIKA KITUO
CHA MIKUTANO CHA KIMATAIFA CHA ARUSHA (AICC).
WASHIRIKI WA MKUTANO HUO NI WANACHAMA WA NCHI ZILIZO KATIKA BONDE LA UFA (RIFT
VALLEY) YAANI ERITREA, ETHIOPIA, KENYA, RWANDA, TANZANIA NA UGANDA. VILEVILE, NCHI
KADHAA ZA AFRIKA, ULAYA, MAREKANI NA ASIA, ZIKIWEMO: BURUNDI, COMORO, JAMHURI YA
KIDEMOKRASIA YA KONGO, MSUMBIJI, DJIBOUTI, ZAMBIA, MALAWI, ICELAND, NEW ZEALAND,
MAREKANI, CANADA, ITALIA, INDIA, JAPANI, UJERUMANI NA INDONESIA ZITASHIRIKI.
MKUTANO HUO UTAONGOZWA NA KAULI MBIU ISEMAYO
JOTOARDHI NI SULUHISHO LA MAHITAJI YA NISHATI KATIKA AFRIKA (Geothermal: Solution
to African Energy Needs).
JOTOARDHI NI MOJAWAPO YA VYANZO VYA NISHATI ITOKANAYO NA MVUKE UNAOTOKA
ARDHINI, HUSUSAN KATIKA MAENEO YALIYO KATIKA BONDE LA UFA (RIFT VALLEY).
MGENI RASMI KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO HUU ANATARAJIWA KUWA MAKAMU WA RAIS
WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. MOHAMED GHARIB BILAL. AIDHA,
MKUTANO HUO UTAFUNGWA NA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
MHE. MIZENGO PETER PINDA.
MKUTANO HUO UMEANDALIWA NA SERIKALI YA TANZANIA KUPITIA WIZARA YA NISHATI
NA MADINI KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINALOSHUGHULIKIA
MASUALA YA MAZINGIRA (UNEP) PAMOJA NA WADAU WENGINE WAKIWEMO; UMOJA WA NCHI
ZILIZO KATIKA BONDE LA UFA (ARGeo), GEF, SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA
(TPDC), SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO), SHIRIKA LA MAENDELEO LA KIMATAIFA
LA ICELAND (ICEIDA), NDF, KAMPUNI TANZU YA JOTOARDHI (GDC), FEDERAL INSTITUTE FOR
GEOSCIENCES AND NATURAL RESOURCES (BGR), POWER AFRICA, KAMISHENI YA UMOJA WA
AFRIKA (AUC), BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB), EAST AFRICAN REGIONAL BRANCH
(EARB) OF INTERNATIONAL GEOTHERMAL ASSOCIATION (IGA) NA CHUO KIKUU KINACHOTOA
MAFUNZO YA KUENDELEZA JOTOARDHI (UNU-GTP).
KWA TAARIFA ZAIDI NA USAJILI TEMBELEA TOVUTI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI
(www.mem.go.tz) NA TOVUTI YA KONGAMANO LINALOANDALIWA (c5.theargeo.org).
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
MKUTANO WA TANO WA KIMATAIFA WA JOTOARDHI

TANGAZO
10 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Mkuranga kupata umeme
wa uhakika Juni mwakani
Na Greyson Mwase,
Mkuranga, Pwani

W
ilaya ya
Mkuranga na
vitongoji vyake
inatarajiwa ku-
pata umeme wa
uhakika ifikapo Juni mwakani,
imeelezwa
Hayo yamesemwa na
mkandarasi kutoka kampuni ya
MBH Power Limited kutoka In-
dia Bw. Narinder Kumar mbele
ya Naibu Waziri wa Nishati na
Madini anayeshughulikia nishati
Charles Ktwanga alipofanya zi-
ara katika wilaya hiyo ili kujionea
maendeleo ya miradi ya umeme
inayofadhiliwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) awamu ya
pili.
Kampuni ya MBH Power
Limited ni kampuni iliyopewa
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantum Mahiza (kulia) akisisitiza jambo katika kikao. Katikati ni Naibu Waziri wa
Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga. Kushoto ni Meneja Mwandamizi
wa Tanesco Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Mahende Mugaya.
n Ni baada ya kukamilika kwa mradi wa REA awamu ya pili
kazi ya utekelezaji wa miradi ya umeme
vijijini katika wilaya ya Mkuranga.
Akielezea hatua iliyofikiwa ya utekeleza-
ji wa mradi huo, Bw. Kumar alisema mpaka
sasa kampuni imeshaanza kazi ya kusimika
nguzo katika maeneo yote umeme utaka-
popita na kusisitiza kuwa jumla ya nguzo
6,000 za umeme wenye msongo mkubwa
wa umeme na nguzo 6,000 za umeme we-
nye msongo mdogo wa umeme zinahita-
jika ili kukamilika kwa mradi huo.
Aliendelea kusema kuwa vifaa ving-
ine kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu
ya umeme ikiwa ni pamoja na transfoma
vinatarajiwa kuwasili mapema Novemba
mwaka huu.
Alisema wananchi wengi wameonekana
kufurahishwa na maendeleo ya mradi huo,
hususan wakati wakishuhudia nguzo zikisi-
mikwa katika maeneo yaliyo karibu na ny-
umba yao.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga
Mercy Silla alisema kuwa REA imeleta
mabadiliko makubwa sana hali iliyopelekea
wilaya ya Mkuranga kupanuka na kuanza
kuwa mji.
Awali wilaya ya Mkuranga ilikuwa
ni kama kijiji, lakini baada ya Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) kuanza kusambaza
umeme, wahamiaji wamekuwa ni wengi
sana hali inayoashiria kuwa uchumi wa
wilaya ya Mkuranga inakua. alisema Silla
Silla aliendelea kusema kuwa thamani
ya ardhi imeendelea kupanda kila kukicha
kutokana na wahamiaji wengi wanaohamia
maeneo ambayo yameanza kuonesha dalili
za kuwekwa miundombinu ya umeme.
Aliendelea kusema kuwa wawekezaji
wengi wameanza kuonesha nia ya kujenga
viwanda hali itakayoongeza ajira na kupan-
ua biashara katika wilaya ya Mkuranga
Wakati huohuo Naibu Waziri wa Ni-
shati na Madini anayeshughulikia nishati
Charles Kitwanga alimtaka Meneja wa
Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) wilaya
ya Mkuranga kushirikiana kwa karibu
na halmashauri ikiwa ni pamoja na ku-
wasilisha ripoti ya maendeleo ya miradi ya
umeme kila baada ya wiki mbili kwa mkuu
wa wilaya hiyo.
Wakandarasi wasiowajibika kunyanganywa tenda na kufutiwa usajili Kitwanga
Na Greyson Mwase,
Mkuranga, Pwani
N
aibu Waziri wa Nishati
na Madini anayeshu-
ghulikia masuala ya ni-
shati Charles Kitwanga
ameyataka makampuni
yaliyopewa kazi ya kusambaza umeme
vijijini kukamilisha kazi hiyo kwa
wakati na katika kiwango kinacho-
takiwa vinginevyo watanyanganywa
tenda zao pamoja na kufutwa kabisa
katika Bodi ya Usajili ya Wakandarasi
Nchini (ERB)
Kitwanga aliyasema hayo mara
baada ya kutembelea miradi ya umeme
vijijini inayofadhiliwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) awamu ya pili
ili kujionea maendeleo yake pamoja na
kuzungumza na wananchi.
Kitwanga alisema kuwa imekuwa
ni kawaida ya baadhi ya wakandarasi
kutokukamilisha kazi za kusambaza
umeme vijijini kulingana na mikataba
waliyowekeana na Serikali hivyo kuk-
wamisha malengo ya Wizara katika
kuhakikisha kuwa asilimia kubwa ya
wananchi waishio vijijini wananufaika
na huduma ya umeme na hivyo ku-
changia katika ukuaji wa uchumi wa
nchi.
Alisema kuwa Wizara itahakiki-
sha inafuatilia maendeleo ya kila mradi
pamoja na kuangalia utekelezaji wa
mikataba waliyosaini na itakapobaini-
ka kampuni imeshindwa kufanya kazi
kwa ufanisi na kukwamisha maende-
leo ya miradi hiyo, itanyanganywa
tenda pamoja na kufutwa kabisa katika
Bodi ya Usajili ya Wakandarasi Nchini
(ERB)
Katika hili hatutakuwa na upen-
deleo kabisa, iwe ni kampuni ya kitan-
zania au ni ya kigeni, iwapo imeshind-
wa kazi itanyanganywa tenda na
kufutwa kabisa kwenye Bodi ya Usajili
ya Wakandarasi Nchini (ERB) Alise-
ma Kitwanga.
11
Bulletin News
http://www.mem.go.tz
TANZIA
Mapato ya Gesi kuinua
sekta nyingine Masele
Asteria Muhozya na
Greyson Mwase, Dar es
Salaam
N
aibu Waziri wa Nishati na
Madini anayeshughulikia
madini Stephen Masele
amesema kuwa mara baada
ya kuanzishwa kwa mfuko
wa mapato ya gesi, fedha hiyo itatumika
kwa ajili ya kuwezesha sekta nyingine na
kuinua uchumi wa nchi.
Masele aliyasema hayo kwenye kon-
gamano la mafuta na gesi lililoambatana
na maonesho la siku mbili lililofanyika
jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba
21 hadi 22, 2014 lililokutanisha wadau
mbalimbali nchini lengo likiwa ni kujadili
changamoto katika sekta mpya za gesi na
mafuta pamoja na kuzipatia ufumbuzi.
Masele alisema kuwa mara baada ya
kuanzishwa kwa mfuko huo, fedha zi-
tatumika kwa ajili ya shughuli maalumu
za maendeleo baada ya kuidhinishwa na
bunge na kuepusha matumizi yasiyo ya
lazima kama kulipana posho za vikao na
makongamano.
Fedha hizi sio kwa ajili ya posho,
makongamano, sherehe, bali ni kwa ajili
ya maendeleo ya uchumi. Lengo ni kua-
cha uchumi imara mara baada ya gesi ku-
malizika kabisa katika miaka ya baadaye,
alisisitiza Masele.
Masele aliendelea kusema kuwa
iwapo fedha hizo zitatumika vyema kui-
marisha sekta nyingine za kiuchumi kama
vile kilimo taifa la Tanzania litakuwa
limepiga hatua kubwa kabisa na kufuta
kabisa umaskini.
Wakati huo huo akielezea mikakati ya
Serikali katika ushirikishwaji wa wananchi
katika uchumi wa gesi Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
Mhandisi Ngosi Mwihava alisema Serika-
li imepanga kuhakikisha kuwa inapeleka
wataalamu na wanafunzi wanaofanya vi-
zuri kusoma katika vyuo vilivyopo nje ya
nchi kusomea jinsi ya kusimamia sekta
mpya ya gesi na mafuta lengo likiwa ni
kuzalisha wataalamu zaidi watakaoshiriki
katika uchumi wa gesi.
Hata hivyo aliwataka wananchi kuji-
andaa na ushiriki katika uchumi wa gesi ili
waweze kunufaika.
Alisema mara gesi itakapoanza ku-
zalishwa wananchi watashiriki katika ku-
toa huduma muhimu kama vile vyakula
mbalimbali, malazi pamoja na kujiajiri ili
kuongeza kipato.
Akielezea mikakati ya Serikali katika
kuhakikisha wananchi wananufaika na
uchumi wa gesi Mhandisi Mwihava alise-
ma kuwa Serikali imepanga kuyawezesha
makampuni ya kitanzania kutoa huduma
katika makampuni ya wawekezaji na ku-
wezesha vyuo vya ndani kutoa mafunzo
yatakayoendana na mahitaji ya makam-
puni ya gesi na mafuta.
Tunataka ifike mahali tuwe na
makampuni yatakayoweza kushindan-
ishwa na makampuni ya kimataifa na
ikiwezekana hata kutoa huduma nje ya
nchi, alisema Mhandisi Mwihava.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Stephen Masele
akifunga rasmi kongamano hilo
Uongozi wa Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST) kwa niaba ya Wizara ya Nishati na Madini
inatoa pole kwa familia ya ndugu wa Marehemu
Samwel Simon Mhalata aliyefariki dunia mnamo
tarehe 19/10/2014 mkoani Dodoma
Marehemu alikuwa akitumikia Wakala
huo kutoka tarehe 03/10/1983 mpaka mauti
yalipomkuta.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la
Bwana lihimidiwe,
Amina.
12 Bulletin News
http://www.mem.go.tz
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofsi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Na Mohamed Saif
W
izara ya Nishati
na Madini kupitia
Idara ya Madini
imepongezwa kwa
juhudi zake za kuwaendeleza
wachimbaji wadogo kwa kuwa-
patia ruzuku pamoja na kutenga
maeneo maalumu ya uchimbaji
madini kwa wachimbaji hao.
Pongezi hizo zimetolewa na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mo-
rogoro, Bw. Alfred Shayo wakati
wa ufunguzi wa kikao kazi cha
Idara ya Madini kinachofanyika
katika hoteli ya Kings Way ya
mkoani Morogoro.
Bw. Shayo amesema kuwa kil-
io cha muda mrefu cha wachim-
baji wadogo kuhusu ukosefu wa
mitaji ya kutosha kuendeshea
shughuli za uchimbaji madini
kimesikika na sasa Wizara ya Ni-
shati na Madini imeanzisha uta-
ratibu maalumu wa kutoa ruzuku
kwa wachimbaji hao.
Ninafarijika kusikia kuwa
moja ya masuala yatakayojadili-
wa katika kikao hiki ni utaratibu
mpya na bora zaidi wa utoaji wa
ruzuku kwa wachimbaji wa-
dogo, na ni matumaini yangu
kuwa kikao hiki kitatoka na uta-
ratibu bora na unaotekelezeka
wa namna ya kutoa ruzuku kwa
wachimbaji wadogo sambamba
na utaratibu wa kuwapa elimu
itakayowezesha kuwapa ujuzi wa
kufanya shughuli zao kwa ufani-
si, alisema Katibu Tawala.
Aidha, Bw. Shayo aliipongeza
Wizara ya Nishati na Madini
kwa kutekeleza mkakati wa
kutenga maeneo maalum kwa
ajili ya wachimbaji wadogo na
kueleza kuwa Wizara iendelee
kutenga maeneo zaidi kwa ajili ya
wachimbaji hao ili watanzania
wengi waweze kushiriki katika
shughuli za uchimbaji madini.
Naye Kamishna wa Madini,
Mhandisi Paul Masanja alisema
kuwa Idara ya Madini katika
Wizara ya Nishati na Madini, im-
ejipanga vyema kuhakikisha sek-
ta ya madini inaongeza mchango
wake katika pato la taifa.
Tumejipanga vizuri kuhakik-
isha sekta hii ya madini inachang-
ia katika kukuza uchumi wa
taifa hili la Tanzania, alisisitiza
Mhandisi Masanja.
Vilevile Mhandisi Masanja
alibainisha kuwa miongoni mwa
juhudi zinazofanywa na Serikali
kupitia Wizara ya Nishati na Ma-
dini katika kuhakikisha Sekta ya
Madini nchini inaimarisha ushiri-
ki wa Wananchi kwenye shughuli
za madini, inaongeza mchango
wake kwenye pato la Taifa,ni
kurasimisha shughuli za wachim-
baji wadogo, kuimarisha usi-
mamizi na udhibiti wa shughuli
za utunzaji wa mazingira kwenye
maeneo ya migodi na pia na ku-
fungamanishwa kwa sekta hiyo
na sekta nyingine za kiuchumi
ili kuchangia katika kupunguza
umasikini.
Kikao kazi hicho kimehud-
huriwa na Makamishna Wa-
saidizi wa Madini, Afisa Madini
Wakazi pamoja na wataalamu
kutoka Wakala Wa Jiolojia Tan-
zania (GST), Wakala wa Ukaguzi
wa Madini Tanzania (TMAA),
Shirika la Madini la Taifa (STA-
MICO) na Kitengo cha Uthamini
wa Almasi na Madini ya Vito
(TANSORT).
Pamoja na kujadili na ku-
fanya maamuzi juu ya masuala
yanayohusu utaratibu wa utoaji
ruzuku kwa wachimbaji wado-
go nchini, kikao kazi hicho pia,
kimejadili kuhusu mgawanyo wa
majukumu baina ya Wizara na
Taasisi zake katika kutoa elimu
kwa wachimbaji wadogo, taratibu
za kupata na kutenga maeneo ya-
nayofaa kwa ajili ya wachimbaji
wadogo, mkakati wa kuimarisha
ukusanyaji wa maduhuli, na mfu-
mo mpya wa kupokea maombi ya
leseni za madini na malipo kwa
njia ya mtandao.
UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII UJUMBE WA WAZIRI WIKI HII
WAFANYAKAZI WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, KAMPUNI NA
TAASISI ZETU TUENDELEE KUCHAPA KAZI KWA UMAKINI, UADILIFU NA
UBUNIFU MKUBWA SANA KWA KUSUDIO LA KUFUTA UMASIKINI NCHINI
MWETU. TUTASHINDA, TUSIKATISHWE TAMAA.
Kamishna wa Madini,
Mhandisi Paul Masanja
(wanne kutoka kushoto,
waliokaa) akiwa katika
picha ya pamoja na
washiriki wa kikao
cha kazi cha Idara ya
Madini kilichofanyika
hivi karibuni katika
Hoteli ya Kings Way
ya Mkoani Morogoro.
Kushoto kwake ni
Katibu Tawala wa
Mkoa wa Morogoro,
Bw. Alfred Shayo
ambaye alikuwa Mgeni
Rasmi katika kikao
hicho.
u

You might also like