You are on page 1of 2

1

WAREMBO WA MISS UNIVERSE TANZANIA 2014 WAANZA KAMBI



Warembo wa Miss Universe Tanzania 2014 wameanza rasmi kambi katika hoteli yenye hadhi
ya kipekee Golden Tulip Hotel. Hii ni kwa ajili ya kujiandaa na fainali ya Miss Universe Tanzania
2014 itakayofanyika tarehe 02 mwezi Octoba.
Miss Universe Tanzania pia imeandaa mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kuwapa warembo ili
kujitambua kama vijana na kama wanawake. Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa na wataalamu
mbalimbali toka katika Nyanja tofauti.
Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ndio Mkurugenzi na
Muandaaji mkuu wa Kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai amesema usaili wa
mwaka huu umefanyika katika mikoa mitano ya Tanzania na warembo zaidi ya 70 walisajiliwa
kwa mashindano haya.
Kambi ya Miss Universe Tanzania 2014 imekamilishwa na warembo 12 kutoka mikoa mitano ya
Tanzania ambayo ni Arusha , Mwanza, Mbeya, Iringa na Dar es Salaam, pamoja na mrembo
mmoja kutoka Zanzibar.
Tumechagua warembo ambao wameonyesha uwezo wa kujitambua na kuelewa umuhimu wa
kushiriki katika mashindano makubwa kama haya. Tuna wanafunzi wa vyuo wanaosomea
udaktari, uhandisi,uhasibu na pia tuna akina dada wajasiriamali . Tunafurahi kuona kila mwaka
warembo wetu wanazidi kujitambua na kazi yetu kubwa ni kuwaendeleza alisema Sarungi
Pamoja na zawadi ya fedha taslimu, mshindi wa Miss Universe Tanzania 2014 atapata fursa ya
kutangaza bidhaa mbalimbali na kufanya kazi za kijamii. Pia kama ilivyo ada kwa mwaka wa 4
sasa, mshindi atapewa nafasi (scholarship) ya kusoma New York Film Academy , Marekani. Hivi
2

sasa washindi wa mwaka 2011 na 2012, Nelly Kamwelu na Winfrida Dominique wako New York
masomoni.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo wake wa
kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na kuliletea sifa Taifa bali pia amepata
mafanikio makubwa katika fani ya ulimbwende kwa kuwa mwanamitindo wa kimataifa. 2008
Miss Universe Tanzania iliwakilishwa na Amanda Ole Sulul,2009 Illuminata James ,2010 Hellen
Dausen , 2011 Nelly Kamwelu, 2012 Winfrida Dominique,2013 Betty Boniface ambaye ndiye
anakabidhi taji kwa mshindi wa mwaka huu.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yamedhaniwa na Insignia, MeryLight , Golden Tulip,
Compass Communications, AzH Photography, Adams Digicom, Opulence, Missie Popular blog,
Seif Kabelele blog, Urban Rose Hotel, RichBoys Entertainment (TZ) Ltd na New York Film
Academy.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mwanakombo Salim: 0655441165

You might also like