You are on page 1of 2

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa kuwa Kamati Kuu ya
Chama, chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, itakutana Mei 34, katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama.
Katika kikao hicho cha siku mbili kitakachofanyika jijini Dar es
Salaam, pamoja na masuala mengine ya kitaifa kuhusu hali ya
kisiasa nchini kwa ujumla na mengine mahsusi yanayohusu
uendeshaji wa chama, KK itapokea taarifa, kujadili na kufanya
maamuzi kuhusu;
1. Maandalizi ya Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika
Oktoba mwaka huu.
2. Taarifa ya ziara ya mafunzo kwa timu za kampeni, viongozi wa
serikali za mitaa na chama, kukiandaa chama kushinda dola na
kuongoza serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
3. Taarifa za utendaji wa chama kupitia kanda zote 10,
Tanganyika na Zanzibar.
4. Taarifa ya maendeleo ya mikakati ya kushiriki uchaguzi mkuu
kwa kushirikiana na vyama 4 vinavyounda UKAWA.
5. Taarifa za mwenendo wa shughuli ya uandikishaji wa wapiga
kura (upya) katika daftari la kudumu kwa teknolojia ya
Biometric Voters Registration (BVR) na hatma ya Uchaguzi
Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Imetolewa leo Jumamosi, Mei 2, 2015 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara a Habari na Mawasiliano- CHADEMA

You might also like