You are on page 1of 24

Soko La Hisa La

Dar es Salaam

LIJUE SOKO LA HISA LA


DAR ES SALAAM

Machi, 2015
SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

YALIYOMO

KURASA

1.

DIRA

2.

AZMA 4

3. UTANGULIZI

4.

NAFASI YA MASOKO YA MITAJI KWENYE MFUKO WA FEDHA

KATIKA UCHUMI

5.

MFUMO WA USIMAMIZI WA KISHERIA

6.

MAJUKUMU YA SOKO LA HISA

7.

WANACHAMA

8.

MUUNDO WA UONGOZI WA SOKO

9.

KANUNI ZA KUORODHESHA HISA NA DHAMANA

10.

ADA ZINAZOTOZWA NA SOKO

11

11.

MAKAMPUNI YALIYO ORODHESHWA

14

12.

MFUMO WA MNADA

17

13.

KUHAMISHA MILIKI YA HISA

17

14.

USIMAMIZI WA SOKO

17

15.

ULINZI KWA WAWEKEZAJI

17

16.

ELIMU KWA UMMA

17

17.

VIVUTIO VYA USHIRIKI KWENYE MASOKO YA HISA

17

18.

Washiriki wa soko la hisa

19

18.

ANUANI YA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

22

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

1.0 DIRA
Kuwa soko endelevu la mitaji ambalo ni injini ya kukuza uchumi wa Tanzania.
2.0 AZMA
Kutoa huduma bora ya soko la mtaji lenye kuwezesha maendeleleo ya uchumi wa nchi na
kuwezesha wananchi kiuchumi.
3.0 UTANGULIZI
Ili kuyaelewa masoko ya mitaji na majukumu yake kwenye uchumi, ni muhimu kuelewa nafasi
ya masoko haya kwenye mfumo mzima wa fedha katika uchumi; muundo wa masoko ya mitaji,
mfumo wa kisheria na namna masoko haya yanavyofanya kazi. Inakubalika kuwa hakuna
uchumi wa kisasa ambao ukajengeka bila ya kuwa na mfumo imara wa fedha. Mfumo imara wa
fedha kwenye uchumi unaweza kufananishwa na mafuta ya kulainisha injini katika gari. Kama
ambavyo injini ya gari huweza kulainishwa na mafuta ili ifanye kazi vizuri, vivyo hivyo mfumo wa
fedha huwezesha uchumi kufanya kazi kwa kukutanisha pande mbili, zile zenye mitaji ya ziada
inayotafuta sehemu za kuwekeza na zenye kuhitaji mitaji hiyo. Pande hizi mbili hukutana kupitia
masoko ya fedha, mitaji huwekezwa na kutoa faida kwa pande husika na hivyo kuwezesha
ufanisi wa matumizi ya mitaji.
4.0

NAFASI YA MASOKO YA MITAJI KWENYE MFUMO WA FEDHA KATIKA UCHUMI


(i) Maana ya Mfumo wa fedha katika Uchumi
Mfumo wa fedha katika uchumi unajumuisha masoko ya fedha, taasisi zinazohusika
na usimamizi wa mfumo wa fedha, sheria, kanuni na taratibu ambazo zinasimamia
uuzaji na ununuzi wa hatifungani, hisa na dhamana nyinginezo zinazohusika, na
hatimaye faida (yield) hubainika.
(ii) Masoko ya fedha
Masoko ya fedha yanajumuisha masoko yote yenye kuhusika na mitaji ya muda mfupi,
kwa kawaida pungufu ya mwaka mmoja, (money markets) na yale yenye kuhusika na
dhamana za muda mrefu, zaidi ya mwaka mmoja ambayo ni masoko ya mitaji (capital
markets). Kwa hiyo, masoko ya fedha ni masoko ya dhamana za muda mfupi na mrefu.
(iii) Masoko ya mitaji
Masoko ya mitaji ni mfumo na taasisi zinazowezesha wenye mitaji kuiwekeza kwenye
vitega uchumi vyenye kuzalisha na kupata faida. Masoko ya mitaji huwezesha wenye
fedha za ziada kuzitoa kwa wenye kuzihitaji kwa kuilipia kwa bei iliyo sahihi. Masoko
ya mitaji yamegawanyika kwenye mafungu mawili:
Soko la awali; na
Soko la pili.
(iv) Soko la awali
Haya ni masoko ya mitaji yanayoshughulika na mauzo ya dhamana kwa mara ya
kwanza. Mfano ni kama kampuni inapouza hisa au hatifungani zake kwa umma kwa
mara ya kwanza. Hisa na hatifungani hizi baadaye huuzwa kwenye soko la pili.
(v) Soko la pili
Haya ni masoko yanayoshughulika na hisa na hatifungani zilizoko mikononi mwa
wawekezaji waliozinunua kwenye soko la awali. Soko la Hisa la Dar es Salaam

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

nimojawapo ya taasisi za soko la pili la mitaji. Wawekezaji kwenye soko la pili


hukutanishwa na madalali kwa ajili ya kuuza na kununua dhamana zilizoorodheshwa.
Soko la Hisa la Dar es Salaam ni mojawapo ya taasisi muhimu kwenye mfumo wa
fedha wa Tanzania.
5.0 MFUMO WA USIMAMIZI WA KISHERIA
Usimamizi wa kisheria wa masoko ya mitaji umejengwa kwenye nguzo kuu tatu za kisheria.
(i)

Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya Mwaka 1994 (Cap 79) kama


ilivyorekebishwa
Hii ndiyo sheria mama inayoratibu na kusimamia masoko ya mitaji hapa Tanzania.
Mamlaka ya masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ndiyo taasisi inayosimamia
utekelezaji wa sheria hii.

(ii) Sheria ya Makampuni ya 2002 (Cap. 212)



Sheria hii inasimamia mambo kadhaa yanayohusu makampuni ikiwa ni pamoja
na uanzishwaji wa kampuni binafsi na za umma, uuzaji wa hisa, haki za wanahisa,
yanayotakiwa kuwepo kwenye nyaraka za matarajio,majukumu ya wakurugenzi na
uongozi wa kampuni. Mtekelezaji wa sheria hii ni Msajili wa Makampuni.
(iii) Kanuni na taratibu zilizotungwa na Mamlaka na pia Soko la Hisa

Masoko ya mitaji ni dhana inayohitaji uelewa maalum na ambayo usimamizi wake
hubadilika mara kwa mara. Ili kuweza kwenda sanjari na maendeleo na mabadiliko
hayo ya mara kwa mara bunge kupitia sheria ya Masoko ya Mitaji limetoa fursa kwa
Mamlaka na Soko kutunga kanuni za kusimamia masoko haya. Soko la Hisa nalo
limeandaa taratibu maalum za usimamizi wa soko ambayo ziko katika Kitabu cha
Kanuni cha Soko. Maelezo zaidi yatapatikana kwenye Kitabu cha kanuni.
6.0

MAJUKUMU YA SOKO LA HISA


Soko la dhamana zilizoorodheshwa
(i) Huwezesha wauzaji na wanunuzi kushiriki kwa kuuza na kununua dhamana
zilizoorodheshwa. Soko la Hisa linatoa fursa ya kutoka na kuingia kwenye vitega
uchumi kwa urahisi.
(ii) Utambuzi wa bei

Soko la Hisa huwezesha kupatikana kwa bei ya hisa na dhamana zilizoorodheshwa
kwenye Soko la Hisa. Bei hupangwa na nguvu ya soko, na sio Soko wala dalali
anayepanga bei ya hisa na dhamana.
(iii) Huwezesha uwazi

Kanuni za soko kuhusu utoaji taarifa muhimu hulazimisha kampuni zilizoorodheshwa
sokoni kutoa taarifa zao mapema iwezekanavyo. Taarifa hizi huwezesha wawekezaji
kuweza kufikia uamuzi wa kuuza ama kununua wakiwa na taarifa zote muhimu
kuhusu kampuni.

Taarifa hutolewa kwa ngazi mbili, wakati hisa zinatolewa kwa mara ya kwanza
ambapo kampuni inatakiwa kutimiza masharti maalum na wakati ikishaorodheshwa
hutakiwa kufuata masharti ya kudumu ya kutoa taarifa zote muhimu wakati wote

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

inapokuwa bado imeorodheshwa. Soko la Hisa linakuwa kama kituo cha taarifa kwa
makampuni na wawekezaji.

(iv) Kuwezesha ubinafsishaji na umiliki mpana wa hisa za makampuni
yanayobinafishwa

Soko la Hisa limewezesha ushirikishwaji wa wananchi wengi zaidi katika umiliki
wa yaliyokuwa mashirika ya umma ambayo hisa zake zimeuzwa na Serikali kwa
wananchi kupitia Soko la Hisa.
(v) Huwezesha upatikanaji wa mitaji

Soko la Hisa huwezesha makampuni kuuza hisa na hivyo kuyawezesha kupata mitaji
kwa gharama nafuu. Uzoefu umeonyesha kuwa wawekezaji walio wengi wako tayari
kulipia hisa bei kubwa na kukubali riba ndogo kwa hatifungani pindi makampuni
husika yanapokuwa yamekidhi masharti ya kuingia Soko la Hisa, kuliko hisa na
hatifungani za makampuni mengine ambayo hayafahamiki ama kuorodheshwa
kwenye Soko, ambayo wawekezaji hulipia bei ndogo na wakopeshaji hudai riba
kubwa kutokana na hatari au hasara ya uwekezaji kuwa kubwa kwenye makampuni
hayo.
(vi) Huwezesha kujenga utajiri

Masoko ya mitaji yanatoa faida halisi kubwa kwa wawekezaji kwa sababu hisa kwa
ujumla hufunika mfumuko wa bei na zimeweza kufanya hivyo kwa muda mrefu.
Faida itokanayo na uwekezaji kwenye hisa imekuwa kubwa kuliko mfumuko wa
bei na kumpatia mwekezaji faida inayoweza kufidia kupungua thamani ya fedha,
ikilingwanishwa na amana za mabenki ambazo riba yake ni ndogo kuliko mfumuko
wa bei. Na pia kwa kuwekeza kwenye hisa mitaji hukua baada ya muda tofauti na
kuweka fedha kwenye amana za mabenki.
(vii) Kuchangia kukuza utamaduni wa uwekaji akiba

Soko la Hisa lilipoanzishwa miaka tisa iliyopita, sio Watanzania wengi waliokuwa
wanajua kuhusu masoko ya hisa. Kwa sasa, wengi wameshaelewa na wana shiriki
kwenye masoko hayo. Ushiriki wao umewezeshwa na Soko la Hisa kutoa maelezo
na elimu kwa umma kuhusu masoko ya mitaji. Lengo la Soko la Hisa ni kuendelea
kutoa elimu kwa umma ili Watanzania wengi zaidi washiriki kwenye masoko ya hisa
na umiliki wa hisa kama njia mojawapo ya kujiwekea akiba.

7.0

WANACHAMA WA SOKO LA HISA

Wanachama wa Soko la Hisa la Dar es Salaam wamegawanyika kwenye mafungu makuu mawili:
Madalali; na
Wanachama washiriki.
Madalali:
Hawa ni wanachama walioruhusiwa kushiriki kwenye minada ya Soko la Hisa inayofanyika kila
siku za Jumatatu hadi Ijumaa. Madalali wanashiriki kwenye Soko la Hisa kwa kuuza na kununua
hisa kwa niaba ya wateja wao au kwa ajili yao wenyewe.

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

Wanachama washiriki:
Hawa siyo madalali, lakini wana maslahi na kukua kwa masoko ya mitaji hapa Tanzania.
Wanachama hawa ni pamoja na kampuni zilizoorodheshwa katika Soko, zenye wasifu wa
kuorodheshwa, wawekezaji wakubwa, Taasisi za kitaaluma na pia mtu mmoja mmoja. (Maelezo
zaidi yanapatikana kwenye Kitabu cha Kanuni cha Soko la Hisa).
8.0 MUUNDO WA UONGOZI WA SOKO
Soko la Hisa ni kampuni iliyoandikishwa mwaka 1996 chini ya Sheria ya Makampuni 2002
(Cap 212) kama kampuni iliyo na dhima ya udhamini bila ya kuwa na mtaji. Uongozi wa Soko
umejengwa kwenye nguzo kuu tatu.
Nguzo ya kwanza ni Mkutano Mkuu wa wanachama ambao hukutanisha wanachama wote.
Nguzo ya pili ni Baraza la Soko (the Council) ambalo huteuliwa kwa mujibu wa Katiba ya
Kampuni. Majukumu yote ya uongozi yamekabidhiwa kwa Baraza la Soko. (Maelezo zaidi yapo
kwenye Kitabu cha kanuni).
Nguzo ya tatu ni Uongozi wa Soko (Management), chini ya Mtendaji Mkuu. Uongozi wa Soko
umeundwa na Mtendaji Mkuu na Mameneja ama Wakuu wa Vitengo. Uongozi unawajibika kwa
Baraza la Soko.
9.0 KANUNI KORODHESHA HISA NA DHAMANA
Katika kuorodhesha hisa na dhamana, Soko la Hisa limegawanyika katika sehemu kuu mbili:
Soko Kuu
Soko la kukuza Ujasiriamali
NAMBA KIGEZO
SOKO KUU

SOKO LA KUKUZA
UJASIRIAMALI

1.
Historia ya
Angalau miaka mitatu.

bishara



Hakuna. Iwapo kamuni hainza


historia ya kufanya biashara,
inatakiwa kuonyesha kuwa ina
mtaji wa kutosha kuanzisha
mradi uliofanyiwa utafiti na
gharama zake kujulikana.

2.
Historia ya

kupata faida

Hakuna.

Kuwa na faida baada ya kodi


kwa ngalau miaka miwili kati ya
mitatu ya historia ya biashara
ya kampuni.

3.
Mtaji wa
Angalau 1 bilioni TZS
kampuni
uliokwisha

kulipiwa

Angalau TZS 200 milion

4.
Kusajiliwa


Kampuni imesajiliwa Tanzania


kama kampuni ya umma, au
kama ni kampuni inayojisajili
kutoka nje ya Tanzania, sheria ya

Kampuni imesajiliwa Tanzania


kama kampuni ya umma, au
kama ni kampuni inayojisajili
kutoka nje ya Tanzania, sheria

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

ya makampuni iwe inafanana na makampuni iwe inafanana na ya


ya Tanzania.
Tanzania.

5.
Mali halisi ya

kudumu

Kampuni iwe na angalau 50%


ya mali ya kudumu ndani ya
Tanzania.

Kampuni iwe na angalau 50% ya


mali ya kudumu ndani ya
Tanzania.

6.
Aina ya
Makamuni yote kutoka sekta

kampuni
yoyote yanaruhusiwa

yanayoruhusiwa kuorodheshwa.
kuorodheshwa

7.
Njia ya kutoa
Toleo kwa umma, kudhamini au

hisa kwa umma njia zote mbili.

Makamuni yote kutoka sekta


yoyote yanaruhusiwa
kuorodheshwa.

8.
Shughuli za
Kampuni inatakiwa kuwa na

biashara
mradi maalum

inayoushughulikia na kumilikiwa

na kampuni inayouza hisa kwa

umma.


Maelezo ya kina yanayohusu


biashara husika ikiwa ni pamoja
na: Mpango wa biashara wa
miaka mitano, riporti ya
uchambuzi yakinifu kwa
makampuni yaliyokuwa na
uzoefu kwenye biashara wa chini
ya mwaka mmoja.

9.
Umiliki wa
Angalau 25% ya hisa zote

umma
zilizoorodheshwa. Wawekezaji

binafsi hawaruhusiwi kuwa na

zaidi ya 1% ya hisa zote na

taasisi 5% ya hisa zote.

10. Idadi ya
Isipungue 1000 ukiondoa

wanahisa baada wafanyakazi wa kampuni.

ya kutoa hisa

kwa umma na
kuorodheshwa.

11. Kipindi cha
Sio lazima.

kizuizi.

Angalau 10% ya hisa kumilikiwa


na umma.

12. Matumizi ya

mtaji

uliopokelewa.

Kutoa maelezo ya kiasi


kitakachopokelewa (baada ya
kutoa gharama) ikibainishwa
matumizi ya kila sehemu mtaji
huo utakakotumika.

Kutoa maelezo ya kiasi


kitakachopokelewa (baada ya
kutoa gharama) ikibainishwa
matumizi ya kila sehemu mtaji
huo utakakotumika.

Endapo makusanyo hayatatosha Endapo makusanyo

Toleo kwa umma, toleo kwa


wawekezaji wachache,
kudhamini au njia zote tatu.

Angalau wanahisa 100.

Ikiwa kampuni haina historia ya


miaka mitatu, waanzilishi
hawarhusiwi kuuza hisa zao kabla
ya mwaka mmoja.

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM


kuanzisha mradi uliokusudiwa,

kampuni itatakiwa kuonyesha ni

wapi itapata mtaji wa ziada na

kiasi kilichopungua.


Endapo matumizi halisi

hayafahamiki kwa kiwango

chochote cha makusanyo,

kampuni itatakiwa kutoa

maelezo ya ujumla ya matumizi

ya mtaji utakaopatikana

utakapowekezwa. Kampuni pia

itatakiwa kutoa maelezo ni kiasi

gani cha chini kitakachokubaliwa

kama mtaji wa kuwekeza kwenye

kampuni endapo toleo halitaleta

mtaji uliotarajiwa.

hayatatosha kuanzisha mradi


uliokusudiwa, kampuni itatakiwa
kuonyesha ni wapi itapata
mtaji wa ziada na kiasi
kinachopungua.

13. Washauri
Sio lazima.

maalum.

Ni lazima kampuni iwe na


Mshauri Maalum kwa kipindi
chote wakati imeorodheshwa.

14. Wakurugenzi na Maelezo kuhusu umri, sifa na



viongozi
uzoefu wa miaka mitano.
waandamizi

Kuwepo na viongozi wenye


uzoefu maalum wa mwaka
mmoja kabla ya kuorodheshwa.

15. Mahesabu ya

kampuni




Lazima yatayarishwe kwa


kuzingatia viwango vya
mahesabu vya kimataifa na
kukaguliwa na mkaguzi
aliyeidhinishwa na bodi ya Taifa
ya wahasibu na wakaguzi wa
hesabu.

Lazima yatayarishwe kwa


kuzingatia viwango vya
mahesabu vya kimataifa na
kukaguliwa na mkaguzi
aliyeidhinishwa na bodi ya Taifa
ya wahasibu na wakaguzi wa
hesabu.

Endapo matumizi halisi


hayafahamiki kwa kiwango
chochote cha makusanyo,
kampuni itatakiwa kutoa
maelezo ya ujumla ya matumizi
ya mtaji utakaopatikana
utakapowekezwa. Kampuni pia
itatakiwa kutoa maelezo ni kiasi
gani cha chini kitakachokubaliwa
kama mtaji wa kuwekeza kwenye
kampuni endapo toleo halitaleta
mtaji uliotarajiwa.

16. Wakaguzi wa
Wawe wameandikishwa na bodi

hesabu
ya Taifa ya wakaguzi wa hesabu

na kuidhinishwa na Mamlaka ya

Masoko ya Mitaji na Dhamana.

Wawe wameandikishwa na
bodi ya Taifa ya wakaguzi wa
hesabu na kuidhinishwa na
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na
Dhamana.

17. Uongozi
Angalau miaka miwili kabla ya

usiobadilika
kuorodheshwa.

Hakuna haja. Mkazo umewekwa


kwenye uzoefu wa viongozi
hawa.

18. Kamati za

ukaguzi


Ni lazima kuwa na kamati ya


ukaguzi kama inavyopendekewa
na miongozo ya Mamlaka ya
masoko ya mitaji kuhusu utawala
bora.

Ni lazima kuwa na kamati ya


ukaguzi kama inavyopendekewa
na miongozo ya Mamlaka ya
masoko ya mitaji kuhusu utawala
bora.

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

19.


Mtaji wa
kutosha wa
kufanyia
biashara

Wakurugenzi kutoa maoni yao


kuhusu kuwepo kwa mtaji wa
kutosha wa kuendesha biashara
kwa angalau kipindi cha miezi 12.

20.



Barua ya
Kampuni kuleta barua ya
uthibitisho
uthibitisho kutoka kwa
kutoka kwa
wasimamizi yake wa kisheria.
wasimamizi wa
kisheria

Wakurugenzi kutoa maoni yao


kuhusu kuwepo kwa mtaji wa
kutosha wa kuendesha biashara
kwa angalau kipindi cha miezi 12.
Kampuni kuleta barua ya
uthibitisho kutoka kwa
wasimamizi yake wa kisheria.

21. Katiba ya

kampuni






Katiba kuwa na kipengele chenye


kuonyesha kuwa kampuni
inaruhusiwa kutoa hisa kwa
umma, kulinda maslahi ya
wawekezaji wadogo, kuhamisha
umiliki wa hisa, majukumu ya
wakurugenzi kwenye kukopa, na
kanuni za utawala bora wa
kampuni

Katiba kuwa na kipengele chenye


kuonyesha kuwa kampuni
inaruhusiwa kutoa hisa kwa
umma, kulinda maslahi ya
wawekezaji wadogo, kuhamisha
umiliki wa hisa, majukumu ya
wakurugenzi kwenye kukopa, na
kanuni za utawala bora wa
kampuni

22. Wajumbe wa

bodi ya
wakurugenzi

23. Waraka wa

matarajio

kupitishwa na
Mamlaka

24. Kutimiza

masharti ya

utawala bora



Kampuni kuwa na angalau 1/3 ya Kampuni kuwa na angalau 1/3 ya


wakurugenzi wasio watendaji
wakurugenzi wasio watendaji

Waraka wa matarajio ni lazima


upitishwe na mamlaka.

Waraka wa matarajio ni lazima


upitishwe na mamlaka.

Kampuni kuweka nadhiri ya


kutekeleza masharti ya utawala
bora kama yanavyotakiwa na
kanuni za utawala bora za
Mamlaka ya masoko ya mitaji
(CMSA) kama zitakavyotolewa
mara kwa mara.

Kampuni kuweka nadhiri ya


kutekeleza masharti ya utawala
bora kama yanavyotakiwa na
kanuni za utawala bora za
Mamlaka ya masoko ya mitaji
(CMSA) kama zitakavyotolewa
mara kwa mara.

25. Sera ya gawio


Kampuni kutoa sera bayana ya


gawio.

Kampuni kutoa sera bayana ya


gawio.

26.

Kampuni inatakiwa kutoa


muhtasari wa waraka wa
matarajio kwenye magazeti.

Kampuni inatakiwa kutoa


muhtasari wa waraka wa
matarajio kwenye magazeti.

Kutoa taarifa
kwenye
magazeti

* (Kanuni zote hizi zinapatikana kwenyue kitabu cha kanuni cha soko la hisa).

10

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

10.0

ADA ZINAZOTOZWA NA SOKO

(a) ADA YA KUORODHESHA


(i) Hisa

SOKO KUU
SOKO LA KUKUZA
UJASIRIAMALI
Kuorodhesha hisa kwa mara Asilimia 0.2% ya
Asilimia 0.1% ya thamani
ya kwanza (kampuni
thamani ya soko ya
ya soko ya hisa
inapoorodheshwa kwenye
hisa zilizoorodheshwa, zilizoorodheshwa,
soko la hisa kwa mara ya
kiwangi cha chini
kiwangi cha chini kikiwa
kwanza)
kikiwa ni TZS 2 milioni ni TZS 1 milioni na cha juu

na cha juu kikiwa ni
kikiwa ni TZS 10 milioni.

TZS 20 milioni.

Ada ya kuorodhesha hisa za Asilimia 0.1% ya
Asilimia 0.05% ya thamani
ziada (hulipwa na kampuni
thamani ya soko ya
ya soko ya hisa
yenye hisa zilizoorodheshwa hisa zilizoorodheshwa, zilizoorodheshwa,
yenye kuongeza hisa zaidi
kiwangi cha chini
kiwangi cha chini kikiwa
kwenye soko la hisa)
kikiwa ni TZS 2 milioni ni TZS 1 milioni na cha juu

na cha juu kikiwa ni
kikiwa ni TZS 10 milioni.

TZS 20 milioni.

Ada ya mwaka ya
Asilimia 0.05% ya
Asilimia 0.025% ya
kuorodheshwa (hulipwa na thamani ya soko ya
thamani ya soko ya hisa
kila kampuni iliyoorodheshwa hisa zilizoorodheshwa, zilizoorodheshwa,
kwenye soko la hisa)
kiwangi cha chini
kiwangi cha chini kikiwa

kikiwa ni TZS 2 milioni ni TZS 2 milioni na cha juu

na cha juu kikiwa ni
kikiwa ni TZS 20 milioni.

TZS 20 milioni.
(ii) Hatifungani
Kuorodhesha hatifungani kwa mara ya
kwanza (kampuni inapoorodheshwa
kwenye soko la hisa kwa mara ya kwanza)

Asilimia 0.05% ya thamani ya soko ya


hatifungani zilizoorodheshwa, kiwango
cha chini kikiwa ni TZS 500,000/= na
cha juu kikiwa ni TZS 5 milioni.

Ada ya kuorodhesha hatifungani za ziada


(hulipwa na kampuni yenye hatifungani
zilizoorodheshwa yenye kuongeza
hatifungani zaidi kwenye soko la hisa)

Asilimia 0.025% ya thamani ya soko ya


hatifungani zilizoorodheshwa, kiwango
cha chini kikiwa ni TZS 250,000/= na
cha juu kikiwa ni TZS 2.5milioni.

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

11

Ada ya mwaka ya kuorodheshwa


(hulipwa na kila kampuni
iliyoorodheshwa kwenye soko la hisa)

Asilimia 0.0125% ya thamani ya soko


ya hatifungani zilizoorodheshwa,
kiwangi cha chini kikiwa ni TZS
500,000/= na kiwango cha juu kikiwa ni
TZS 2.5 milioni.

(b) USHURU KWENYE SOKO LA PILI


(i) Manunuzi ya Hisa
Kiwango cha
Ada ya
Ada ya soko
Mfuko wa Jumla ya
mauzo
madalali
na Mamlaka
fidia
ghamara kwa

mwekezaji
Mauzo hadi
1.70 0.28 0.02
2.00
TZS 10 milioni
Mauzo hadi
TZS 40 milioni

1.50

0.28

0.02

1.80

Mauzo yoyote zaidi


0.80 0.28 0.02
1.10%
ya TZS 50 milioni

(ii) Manunuzi ya Hatifungani


Thamani ya mauzo

Ushuru unaotozwa

Hadi TZS 40 milioni

1/16%

Kiasi chochote zaidi ya TZS 40 milioni

1/32%

Kiwango cha chini cha ushuru

TZS 5,000

(c) Ada za hifadhi ya hisa


(i) Kwa mwekezaji
Namba Aina ya ada

Soko kuu

Soko la kukuza ujasiriamali

(i)

TZS 1,000

TZS 1,000

TZS 1,000

TZS 1,000

Ada kwa kila manunuzi

(ii) Kuunganisha umuliki wa hisa


(iii)

Kudurufu hati ya hifadhi (kila hati)

TZS 2,000

TZS 2,000

(iv)

Kuhamisha miliki bila kuuza

TZS 1,000

TZS 1,000

(v)

Taarifa kuhusu umiliki

TZS 5,000

TZS 5,000

TZS 25,000

TZS 25,000

TZS 1,000

TZS 1,000

(vi)

Kutoa hisa kwenye hifadhi

(vii)

Kuweka na kutoa hisa rehani

12

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

(ii) Kwa makampuni


Namba Aina ya ada
Soko kuu

Soko la kukuza
ujasiriamali

(i)

TZS 1,000

TZS 1,000

Asilimia 0.5% ya thamani


ya soko ya hisa
zilizoorodheshwa, kiwango
cha chini kikiwa ni TZS 2
milioni na cha juu kikiwa ni
TZS 10 milioni

Asilimia 0.25% ya thamani


ya soko ya hisa
zilizoorodheshwa,
kiwango cha chini kikiwa
ni TZS 1 milioni na cha
juu kikiwa ni TZS 5 milioni

Hifadhi ya Hisa

(ii)
Kutayarisha hati za hifadhi

wakati wa mauzo ya hisa

ya awali


(ii) Ada za ISIN


Namba Ada

Kiasi

(i)

Ada kwa hisa na hatifungani zilizo orodheshwa


kwenye soko (ada ya mara moja tu)

TZS 300,000

(ii)

Ada ya matoleo ya ziada ya hisa na hatifungani

TZS 150,000

(iii)

Ada kwa kwa hisa na hatifungani ambazo hazija


orodheshwa kwenye soko (ada ya mara moja tu)

TZS 150,000

(iii) Ada ya Uanachama wa Soko La Hisa


Namba

Aina ya ada

Kiasi

(i)

Ada ya kiingilio

TZS 2,000,000

(ii)

Ada ya mwaka

TZS 1,000,000

(iv) Ada ya Uanachama wa Hifadhi ya Hisa (CDS)


Namba

Aina ya ada

(i)

Ada ya kiingilio

TZS 1,000,000

(ii)

Ada ya mwaka

TZS 2,000,000

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

Kiasi

13

11.0

MAKAMPUNI YALIYOORODHESHWA

(a) Hisa
(i) Kampuni za kitanzania

Jina lakampuni
Tarehe ya

kuorodheshwa

Idadi ya Hisa Aina ya biashara


zilizo tolewa

TOL Gases Ltd.


15 Aprili, 1998
55,835,490
(zamani ikiitwa TOL Ltd.)
(TOL)

Uzalishaji na usambazaji wa
gesi, vifaa vya kuchomelea
na hospitali.

Tanzania Breweries Ltd.


9 Septemba,
294,928,463
(TBL) 1998

Uzalishaji na uuzaji wa bia

Tanzania Tea Packers Ltd. 17 Disemba,


18,657,254
(TATEPA)
1999

Kilimo cha chai, usindikaji,


uuzaji na usambazaji wa chai

Tanzania Cigarette Co. Ltd. 16 Novemba,


100,000,000 Uzalishaji na usambazaji wa
(TCC)
2000 tumbaku
Tanga Cement Co. Ltd.
(SIMBA)

26 Septemba,
63,671,045
2002 saruji

Uzalishaji na usambazaji wa

Swissport Tanzania Ltd.


26 Septemba,
36,000,000
(zamani ikiitwa DAHACO) 2003

Kutoa huduma kwenye


viwanja vya ndege

Tanzania Portland Cement 29 Septemba,


179,923,100
Co. Ltd. (TWIGA)
2006

Uzalishaji na usambazaji wa
saruji

Dar es Salaam Community 16 Septemba,


Bank Ltd (DCB)
2008

67,827,897

Benki ya Biashara

National Microfinance
Bank Ltd (NMB)

6 Novemba,
2008

500,000,000

Benki ya Biashara

CRDB Bank Plc (CRDB)

17 Juni, 2009

2,176,532,160 Benki ya Biashara

Precision Air Services Plc

21 Disemba 2011 160,469,800

Usafiri wa anga

Maendeleo Bank (MBP)

1 Novemba 2013 9,066,701

Benki ya Biashara

Swala Gas and Oil

11 Agosti 2014

Madini Gesi na Mafuta

Mkombozi Bank

29 Desemba 2014 20,615,272

14

99,954,467

Benki ya Biashara

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

(ii)

Makampuni ya nje

Jina lakampuni

Tarehe ya
kuorodheshwa

Idadi ya Hisa
zilizo tolewa

Aina ya biashara

Kenya Airways Ltd


1 Oktoba, 2004
1,496,469,034
(KA)

Usafirishaji wa abiria na
mizigo kwa njia ya anga
sehemu mbalimbali duniani

East African Breweries 29 Juni, 2005


790,774,356
Ltd. (EABL)


Kampuni mama ya
makampuni kadhaa zenye
kuhusika na Uzalishaji na
uuzaji wa bia nchini Kenya,
Uganda na Mauritius.

Jubilee Holdings Ltd


20 Disemba, 2006 59,895,000
(JHL)


Kampuni mama ya
makampuni kadhaa zenye
kuhusika na huduma za
bima nchini Kenya, Uganda
na Tanzania

Kenya Commercial
17 Disemba, 2008 2,970,340,000 Benki ya Biashara
Bank Ltd (KCB)

National Media Group 21 Februari 2011
188,542,286
Kampuni ya utangazaji na
Plc habari
Acacia Mining Plc
7th Disemba, 2011 410,085,499
Kuchimba na kuzalisha
dhahabu
Uchumi Super Market 15 Agosti 2014
364,965,594
(USL)

Maduka ya bidhaa
mbalimbali (supamaketi)

(iii) Historia ya Manunuzi ya hisa


Jina la
Bei ya Idadi ya Hisa
Thamani ya
Mtaji
Kiasi
Idadi ya
kampuni
Hisa
zilizo
Mauzo ya
uliopatikana
cha walionunua

kipindi
tolewa
hisa
mtaji
Hisa

cha uliopat
kuorod- ikana
heshwa

TOL1
500
7,500,000 3,750,000,000 3,598,086,000 96
10,500
550 23,594,277 12,976,852,350 9,630,874,000 74
23,000
TBL2
TATEPA 330 1,584,912 523,020,960 571,461,000 109 2,000
TCC
410 19,500,000 7,995,000,000 9,394,125,000 118
7,508
SIMBA
300
20,693,090 6,207,927,000 24,210,915,300 390
14,228
SWISSPORT 225
17,640,000 3,969,000,000 31,196,340,000 786
41,025
TWIGA
435
53,975,900 23,479,516,500 86,419,680,855 368
18,300
NICOL
300 50,000,000 15,000,000,000 5,601,735,000 37
2,987

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

15

DCB
275
5,454,546 1,500,000,150 3,704,094,900
NMB
600
105,000,000 63,000,000,000 224,999,340,000
CRDB
150 125,429,692 18,814,453,800 50,719,410,000
PRECISION 475
58,841,750 27,949,831,250 12,091,030,000
TBL3
2,060
58,985,693 121,510,527,580 297,593,326,800
MAENDELEO
BANK
500
9,066,701
4,000,000, 000
4,533,350,500
SWALA
500
9,600,000 4,800,000,000 6,643,900,000
MKCB
1000 5,000,000 5,000,000,000 3,776,820,000

247
357
270
43
245

5,446
27,303
21,282
7,057
2,081

113
138
76

2528
1867
2618

(b) HATIFUNGANI ZA MAKAMPUNI


KAMPUNI

AINA YA
TAREHE YA RIBA
HATIFUNGANI TOLEO

KUIVA

ALAF LTD.





Hatifungani zenye 24 Februari,


thamani ya TZS
2008
15.07 bilioni zisizo
na dhamana,
toleo la kwanza
zitakazoiva
mwaka 2015

Kurejeshwa kikamilifu
mwisho wa
hatifungani tarehe
17 Disemba 2015

Wastani wa Faida
wa dhamana za
siku 182 za serikali
za karibuni na
Malipo
zikiongezewa
riba

BANK M
Hatifungani zenye 4 Februari, Riba isiyobadilika
LIMITED
thamani ya TZS
2011
ya 15% kwa

14.5 bilioni zisizo
mwaka inayolipwa

na dhamana na
kuanzia 4

kuiva mwaka 2016
Februari 2012

hadi tarehe ya

kupevuka pamoja

STANDARD
Hatifungani zenye 22 Octoba, Riba isiyobadilika
CHARTERED
thamani ya TZS
2010
ya 11%, Faida
BANK LTD.
10 bilioni zisizo na
hadi kuiva

dhamana, toleo la
inayolipwa mara

kwanza zitakazoiva
mbili kwa mwaka

mwaka 2015

Kurejeshwa kwa
pamoja tarehe
4 Februari, 2016

Kurejeshwa kwa
awamu 10 tofauti
za kiwango cha
1,000,000,000 kila
moja pamoja na
riba hadi tarehe 21
Octoba 2015

PROMOTION
Hatifungani zenye 8 Novemba, 1. Wastani wa Faida Kurejeshwa kwa
OF RURAL
thamani ya TZS
2015
wa dhamana za
awamu 6 tofauti za
INITIATIVES
14.5 bilioni zisizo
siku 364 za serikali kiwango sawa kila
AND
na dhamana na
za karibuni na
moja kila baada ya
DEVELOPMENT kuiva mwaka 2015
malipo
miezi 6 kuanzia
ENTERPRISES
zikiongezewa riba Novemba 2012
LTD (PRIDE)
kwa 2% juu ya

kiwango kilichopo

2. Riba isiyobadilika

ya 11.75% kwa
mwaka
16

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

12.0

MFUMO WA MNADA
Mnada unafanyika kwenye mtandao wa kompyuta (ATS). Kupitia mtandao huu madalali
wa Soko wanauziana hisa na hatifungani wakiwa kwenye ofisi zao.

Mfumo huu unategemewa kuwezesha kusaidia huduma kuwafikia Watanzania walio nje
ya Dar es Salaam siku za karibuni.

13.0 KUHAMISHA MILIKI YA HISA



Uhamishaji miliki ya hisa na hatifungani hufanyika kupitia mfumo wa kompyuta wa
kusimamia uhamisho wa miliki ulioanza tangu mwaka 1999. Mfumo huu husimamia
uhamishaji wa miliki unaotokana na mauzo na manunuzi, hisa kutolewa kama zawadi
na kurithisha hisa kutoka kwa marehemu. Mfumo huu huwezesha kuhamisha miliki kwa
muda mfupi (ndani ya siku 3 kwa hisa na siku moja kwa hatifungani baada ya mauzo).
14.0

USIMAMIZI WA SOKO
Mamlaka na Soko la Hisa kwa pamoja husimamia mnada ili kubaini kama kuna
udanganyifu, upotoshaji na ushiriki wenye mgongano wa maslahi. Soko la Hisa
linawajibika na usimamizi wa moja kwa moja ambapo wataalam wa Mamlaka husimamia
kwa kuangalia jinsi mnada unavyoendelea wakiwa ofisini kwao.

15.0

ULINZI KWA WAWEKEZAJI


Kwa mujibu wa Sheria ya masoko ya Mitaji na Dhamana, Soko la Hisa limeanzisha Mfuko
wa Fidia utakaotumika kufidia wawekezaji watakaopata hasara kutokana na udanganyifu
au matumizi mabaya ya fedha zao na madalali wa Soko. Mfuko huu hutunzwa na Soko
la Hisa. Mfuko pia hutumika kufidia hasara itokanayo na uzembe wa madalali. Fidia
inayolipwa kwa sasa haizidi Shilingi 100,000/= kwa hasara apatayo mwekezaji.

16.0 ELIMU KWA UMMA



Elimu kwa wawekezaji hutolewa na Soko la Hisa kupitia semina zinazoandaliwa na Soko la
Hisa, kupitia taasisi nyinginezo na pia kupitia mafunzo kwa wawekezaji wanaotembelea
Soko la Hisa ili kuona mnada unavyoendeshwa.

Soko la Hisa linaendesha elimu ya uwekezaji na utunzaji fedha kwa wanafunzi wa vyuo
vya elimu ya juu nchini ambapo wanafunzi hupewa nafasi ya kushiriki kwenye shughuli
za mafunzo wa vitendo kwa kuuza na kunua hisa kwa kipindi cha miezi mitatu.

Majarida yanayotoa maelezo kuhusu Soko la Hisa huchapishwa mara kwa mara na Soko la
Hisa yakilenga kutoa maelezo kuhusu uwekezaji na wakati wa kampuni mpya inapokuwa
imeorodheshwa Sokoni.

17.0 VIVUTIO VYA USHIRIKI KWENYE MASOKO YA HISA



Serikali imetoa vivutio muhimu vya kuwezesha ushiriki mpana kwenye masoko ya mitaji.
(a) VIVUTIO KWA MAKAMPUNI
(i) Kodi ya makampuni imepunguzwa kutoka 30% hadi 25% kwa kipindi cha miaka
3 iwapo kampuni itamilikiwa kwa 35% na umma. Punguzo hili litaendelea kwa
miaka 5 baada ya kuorodheshwa kwa kampuni hiyo katika Soko la Hisa.

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

17

(ii) Punguzo la kodi ya makampuni kutoka 30% hadi 25% kwa makampuni yote
yaliyoorodheshwa katika soko la hisa na ambayo yametoa angalau 30% ya hisa
zao kwa umma.
(iii) Gharama za kuuza hisa kwa umma zinazokubaliwa na Mamlaka ya mapato
Tanzania (TRA) kama gharama za uendeshaji kwenye ukokotoaji wa faida na
hasara ya kampuni kwa ajili ya kutafuta kodi ya mapato.
(iv) Kodi ya zuio kwenye mapato yatokanayo na vyombo vya uwekezaji wa pamoja
ni kodi ya mwisho. Wawekezaji wa mifuko hii hawalipi kodi tena.
(b) VIVUTIO VYA WAWEKEZAJI
(i) Hakuna kodi ya ongezeko la mtaji, ikilinganishwa na 10% kwa kampuni ambazo
hazijaorodheshwa.
(ii) Hakuna ushuru wa stempu kwenye mauzo ya hisa zilizoorodheshwa,
ikilinganishwa na 6% kwa kampuni zisizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa.
(iii) Kodi ya zuio kwenye gawio ni 5% ikilinganishwa na 10% kwa kampuni
zilizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa.
(iv) Hakuna kodi za zuio kwa mapato ya riba yatokanayo na jhatifungani
zilizoorodheshwa zenye kuiva baada ya miaka mitatu na zaidi.
(v) Kodi ya zuio kwenye mapato ya mfuko wa uwekezaji imeondolewa.
(vi) Mapato ya wawekezaji kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja yamesamehewa
kodi.

18

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

18.0 WASHIRIKI KATIKA SOKO LA HISA


(a) MADALALI
CORE securities Ltd
Orbit Securities Co. Ltd
Rasilimali Ltd
Ghorofa ya Nne Jengo la Elite City, Ghorofa ya Nne,
Ghorofa ya Saba,
Kwenye kona ya barabara za
Jengo la PSPF Golden Jubilee Jengo la Samora Towers
Samora na Morogoro
Towers, Barabara ya Ohio,
Barabara ya Samora,

Dar es Salaam
Dar es Salaam
Simu: +255 (22) 2123103,
Nukushi:+255 (22 2122562
Simu: +255 (22) 211 1758
Simu: +255 (22) 211 1711
Barua Pepe: info@coresecurities.co.tz; Nukushi: +255 (22) 211 3067 Nukushi: +255 (22) 212 2883
Tovuti: www.coresecurities.co.tz
Barua Pepe: orbit@orbit.co.tz Barua Pepe:
rasilimali@africaonline.co.tz
Tanzania Securities Ltd
Vertex International
Solomon Stockbrokers Co. Ltd
Ghorofa ya Saba, Jengo la IPS,
Securities Ltd
Sakafu ya ardhini,
Kona ya barabara za
Jengo la Annex- Ubalozi
Jengo la PPF House, kona ya
Samora na Azikiwe, Dar es Salaam
Zambia, Kona ya
barabara za Samora na Morogoro,

barabara za Sokoine
Dar es Salaam
Simu: +255 (22) 211 2807
na Ohio, Dar es Salaam
Nukushi: +255 (22) 211 2809
Simu: +255 (22) 211 2874
Barua Pepe:
Simu: +255 (22) 211 6382
Nukushi: +255 (22) 213 1969
info@tanzaniasecurities.co.tz
Nukushi: +255 (22) 210387
Barua Pepe:

Barua Pepe:
solomon@simbanet.net
vertex@vertex.co.tz








ZAN Securities Ltd


Ghorofa ya Pili,
Jengo la VIVA Towers,
Barabara ya Ali Hassan Mwinyi
Dar es salaam
S.L.P 2138
Ghorofa ya kwanza,
Muzammil Centre, barabara
ya Malawi, Zanzibar

Simu: +255 (22) 2126415,


Nukushi: 255 (22) 2126414
Simu ya rununu:
+255 (786) 344767 /
(755) 898425

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

19

(b) Washauri Wateule


Enterprise Growth Marker Advisors Ltd
Ghorofa ya kwanza
Jengo la Alfa House ploti ya 25
Barabara Mpya ya Bagamoyo
S.L.P. 79807
Dar es Salaam

Simu: +255 22 2760145, +255 759 191 093
Simu ya mkononi: +255 754 222 450
Barua pepe: info@egma.co.tz

TSL Investment Management Ltd


Ghorofa ya sita, Jengo la IPS
Mtaa wa Samora na Azikiwe
S.L.P. 9821
Dar es Salaam

ARCH Financial & Investment


Limited
Ghorofa ya Pili, Wingi ya C, Jengo la NIC Life
Mtaa wa Sokoine na Ohio
S.L.P 38028
Dar es Salaam

Exim Advisory Services Ltd. Advisory


(Fund Manager)
Ghorofa ya 8, Jengo la Ofisi ya Academy
Plot ya 2385/12, Mtaa wa Azikiwe
S.L.P. 3219,
Dar es Salaam.

Simu: 255 (22) 21 12807


Nukushi: 255 (22) 21 12809
Barua Pepel: info@tim.co.tz

Simu. +255 22 732922396


Nukushi +255 22 732928489

20

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

(c) WASHAURI WA UWEKEZAJI


FTC Consultants Limited
Ghorofa ya pili,
Jengo la Osman Towers,
mtaa wa Zanaki
Dar Es Salaam, Tanzania

Simu: +255 (77) 467 6676
Nukushi: +255 (22) 213 0519
Tovuti: www.ftc-tz.com

Orbit Securities Co. Ltd


LJK Konsulting Limited
Ghorofa ya Nne, Jengo la
Plot No. 294, Regent Estate
PSPF Golden Jubilee Towers,
S.L.P. 20651
Mtaa wa Ohio,
Simu/Nukushi +255 (22) 2124383
S.L.P. 31831, Dar es Salaam
Barua Pepe:
Simu: +255 (22) 211 1758
info@mekonsult.co.tz.
Nukushi: +255 (22) 211 3067
Barua Pepe: orbit@orbit.co.tz
Tovuti: www.orbit.co.tz

Gem Consulting Limited


Trident East Africa Limited
Sifa Advisory Limited
Ghorofa ya Nane,
Ghorofa ya Tatu,
S.L.P 412338028
Jengo la Office
Maktaba Complex
Dar es Salaam
Academy Scheme,
(Jengo la Tanzania
Simu. +255 (22) 2137570
Plot 2385/12, mtaa wa Azikiwe, Library Services)
Nukushi: +255 (22) 2136570
Dar es Salaam
Barabara ya Bibi Titi,
Tovuti: www.sifacapital.com

Dar es Salaam

Barua Pepe:
info@tridentealtd.com
River Capital Partners
ARCH Financial &
Skylink Financial Services
Ghorofa ya 10,
Investment Limited
Jengo la Amani Place
Advisory Limited
Ghorofa ya 4, Amani Place,
mtaa ya Ohio
Ghrofa ya Pili, Wing C,
Opposite Serena Hotel,
Simu: +255 22 2126050
Jengo la NIC Life House
Mtaa wa Ohio
Nukushi: +255 (22) 21216049 Kona ya barabara ya Sokoine Dar es Salaam.

Drive na mtaa Ohio

Dar es Salaam
Simu: +255 (22) 2115381

Simu: +255 (22) 732922396
Nukushi: +255 (22) 2112786/

Nukushi: +255 (22) 732928489 2114562

Barua Pepe: info@
skylinkfinancialservices.com
Exim Advisory Services Ltd
Solomon Stockbrokers Co. Tanzania Securities Ltd
(Fund Manager)
Ltd
(Fund Manager)
Ghorofa ya nane,
Ghorofa la Chini,
Ghorofa ya Sita,
Jengo la Office Academy
Jengo la PPF House,
Jengo la IPS,
Scheme Building
kona ya barabara za Samora Kona ya barabara za
Plot 2385/12, Mtaa wa Azikiwe na Morogoro,
Samora na Azikiwe,
Dar es Salaam
Dar es Salaam
Dar es Salaam

Simu: +255 (22) 211 2874
Simu: +255 (22) 211 2807

Nukushi: +255 (22) 213 1969 Nukushi: +255 (22) 211 2809

Barua Pepe:
Barua Pepe:

solomon@simbanet.net info@tanzaniasecurities.co.tztz

Tovuti: www.solomon.co.tz
Tovuti:

www.tanzaniasecurities.co.tz

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

21

Standard Chartered Bank


Rasilimali Ltd
Consultants for Resources
Tanzania Limited
Ghorofa ya Saba,
Evaluation Limited (CORE)
Jengo la International House
Jengo la Samora Towers
Ghorofa ya Nne
Barabara ya Garden Avenue
Barabara ya Samora
Jengo la Elite City,
Dar es Salaam
Dar es Salaam
Kwenye kona ya barabara
Simu: 255 (22) 2122160 /
za Samora na Morogoro
2122162
Simu: +255 (22) 211 1711
Tovuti: 255 (22) 2122089
Nukushi: +255 (22) 212 2883 Simu: +255 (22) 2123103,

Barua Pepe:
Nukushi:+255 (22) 2122562

rasilimali@africaonline.co.tz
Barua Pepe:
info@coresecurities.co.tz;

Tovuti: www.coresecurities.co.tz
Unit Trust of Tanzania
Ernst &Young Advisory
Enterprise Growth Market
(Fund Manager)
Services
Advisors Limited (EGMA)
Ghorofa ya 3, Jengo la Sukari,
Jengo la Utalii House
Ghorofa la kwanza,
Kona ya Mtaa wa
36 Barabara ya Laibon,
Jengo la Alfa House, ploti ya 25
Sokoine na Ohio,
Oysterbay,
Barabara Mpya ya Bagamoyo,
Dar es Salaam
Dar es Salaam
S.L.P 79807
Simu: + 255 (22) 212 8460
Dar es Salaam.
Nukushi: + 255 (22) 213 7593
Simu: +255 (22) 266 6853 /
Simu: +255 22 2760145,
Barua Pepe:
266 7659
+255 (759) 191093
uwekezaji@utt-tz.org
Nukushi: +255 (22) 266 6869 Nukushi: +255 (22) 2126414
Tovuti: www.utt-tz.org
Barua pepe: EYAS@tz.ey.com Barua pepe: info@egma.co.tz

Bank M Tanzania Limited
Equity for Tanzania Ltd.
NBC Bank Limited
Money Centre Namba 8,
(EFTA)
Kona ya barabara ya Sokoine na
barabara ya Ocean Road,
S.L.P 1747 Moshi.
mtaa wa Azikiwe,
Dar es Salaam.
Simu: +255 (27) 2750657
S.L.P 1863,

Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 (22) 2127824
Nukushi: +255 (22) 2127825
Simu: +255 (22) 2199793/
Tovuti: www.bankm.co.tz
+255 768 980 191

Nukushi: +255 (22) 2112887/
2113749

Barua pepe:
contact.nbc@nbctz.com

Tovuti: www.nbctz.com

19.0

ANUANI YA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM


Afisa Mkuu Mtendaji, Soko la hisa la Dar es Salaam,
Ghorofa ya 14, Jengo la PSPF - Golden Jubilee Tower,
Mtaa wa Ohio, S.L.P 70081, DAR ES SALAAM.
Simu: 255 (22) 2128522/2135779/2123983
Nukushi : 255 (22) 2133849
Barua pepe: info@dse.co.tz
Tovuti: www.dse.co.tz

22

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

Soko la Hisa la Dar es Salaam,


Ghorofa ya 14, Jengo la PSPF Golden Jubilee
Towers, Mtaa wa Ohio,
S.L.P 70081, DAR ES SALAAM
Simu: 255 22 212 8522 / 213 5779 / 2123983
Nukushi: 255 22 213 3849
Barua pepe: info@dse.co.tz
Tovuti: www.dse.co.tz
24

SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

You might also like