You are on page 1of 12

KAMBI TAKATIFU

(shida)
1. Camera inaonyesha tukiwa katika shamba
tunalima kikosi kizima huku walinzi
wametusimamia.
2. Jackson ni kijana ambae anapendwa sana
na mkuu wa kikosi hicho,hivyo
tunaonyeshwa akiwa na mkuu katika
mazingira tofauti anapokuwa kiongozi
huyo.
3. Camera inaonyesha Jackson akiwa na
wafungwa wengine wanalima,KAMANDA
mkuu wa kikosi anakuja kukagua shamba,
anamuona jack, analima kwa bidii
anaingiwa na huruma na kukumbuka
alivyowaua wazazi wake bila jack
kujua,anamchukua katika gari yake na
kuondoka naye mpaka nyumbani.
4. Camera inaonyesha Mkuu akiwa na Jack
nyumbani kwake akiongea nae maneno ya
faraja na kuonyesha zaidi upendo kwake.
5. Camera inaonyesha Jack akiwa anaenda
shambani peke yake, ghafla anaona
walinzi wanavyo mkimbiza mateka 1
aliyejaribu kutoroka kulingana na mateso
wanayo yapata.

6. Camera inaonyesha mateka huyo aliye


jaribu kutoroka akiwa amefungwa kwa
kuninginizwa huku mkuu akiamuru
apigwe kwa kosa alilotenda la kutoroka.
7. Camera inaonyesha wafungwa wote
wakiwa wamekusanyika wakiwa katika
ulinzi mkali sana na mda huo kiongozi wao
anakuja kuhutubia kutokana na alicho
fanya m1 wao kutoroka.
8. Camera inaonyesha wale viongozi katika
kambi hiyo wakikaripiwa na mkubwa wao
kwa kuzembea katika ulinzi na
kusababisha wafungwa kutaka kutoroka,
kiongozi wa ulinzi anavuliwa cheo na
kupewa mtu mwingine, na Jack
anakabidhiwa funguo kuwa dereva wa
mkuu.
9. Camera inaonyesha mkuu anapiga
kengere ya kuita kambi nzima,haraka
wanafika na kuanza utambulisho wa
uongozi mpya.
10.
Camera inaonyesha wafungwa wakiwa
wanapelekeshwa zaidi ya mwanzo,na kwa
mateso makali sana
11.
Camera inaonyesha Jack akiwa na
kiongozi wa ulinzi akimuonya kuwa
uongozi sio kuwa tesa watu bali ni kuwa

peleka taratibu lengo watimize wajibu


wao,lakini kwa kutokusikia ushauli
anafoka na kusema asifuatiliwe yeye
anataka kutenda kazi yake impasavo
kutenda. Mda wote wa maongezi hayo
yupo mzee nyuma yao anawasikiliza
mazungumzo yao.
12.
Camera inaonyesha Jack akiwa na
kiongozi mkuu akimwambia alivyofokewa
na mlinzi huyo hataki kusikiliza ushauri
13.
Camera inaonyesha kiongozi mkuu
akiwa na uongozi mzima wa kambi hiyo na
kuwaeleza kuhusu kambi iliyvo na uongozi
na kila mtu anatakiwa kumheshimu
mwenzake ili waweze kuongoza vizuri. Na
anatangaza kuwa kuanzia leo kila
atakachoongea Jack lazima asikilizwe na
kumtii.
14.
Camera inaonyesha Yule mzee
akiomba ruhusa ili aweze kuonana na Jack
lakini anazuiliwa,Yule mzee kwa huruma
anaanza kukumbuka jinsi wazazi wa jack
walivyouliwa kikatili na mkuu wa kambi.
15.
Camera inaonyesha mkuu wa kambi
akitoa maagizo waende polini kutafuta
kuni kwa ajili ya kambi.

16.
Camera inaonyesha wakiwa
wamekusanywa wafungwa wote na walinzi
wakijipanga kuondoka, mkuu wa kambi
anafuatia nyuma taratibu na gari yake.
17.
Camera inaonyesha wakiwa wamepaki
pembeni wanasubiri warudi ili waondoke
lakini Jack anatoka kwenye gari na kuingia
polini kufuatilia kinachofanyika.
18.
Camera inaonyesha wafungwa wakiwa
wanakata kuni mara Yule babu anamuona
Jack na kumwendea ghafla wanatokea
walinzi wakitaka kumpiga lakina Jack
anawazuia,babu anashukuru sana
amesaidiwa.
19.
Camera inaonyesha wakiwa wanatoka
polini na magogo ya kuni, Jack anaingia
kwenye gari na kuondoka
20.
Camera inaonyesha Jack akiwa
amepitiwa na usingizi lakini cha ajabu
anamuota Yule mzee akaimwambia Kija
nimeshakutafuta mara mbili kuna jambo la
msingi nataka nikuambie lakini kumekuwa
na ukuta mkubwa , nakuja mara ya mwisho
nikishindwa basi anatoka usingizini na
kuliwazia jambo hilo.
21.
Camera inaonyesha Jack akienda
kambini,anawaona wafyeka majani, Yule

mzee kwa furaha anamkimbilia lakina


walinzi wanamzuia ghafla anakumbuka ile
ndoto, na kuamuru wamuache.
22.
Kumbukumbu tunaona mkuu wa
kambi akiteka ile familia, baba analeta
ubisha anapigwa risasi kichwani wakati
huo mama akiwa katika kukimbia
anapigwa risasi mgongoni na kumalizia
kichwani, anabaki Jack akiwa haelewi kitu
mchanga sana ndipo anabebwa na
kupelekwa kwa kiongozi wa kambi.huvi
ndivyo ilivyokuwa. KWA HIYO MIMI
NILIWEZA KUKUA VIP? na baada ya hapo
wewe ulipelekwa kwa kiongozi mkuu wa
kambi mpaka leo ndipo unaishi, mwanangu
sisi tuliteseka makazi yetu yakaharibiwa
tukapoteza ndugu lakin kwa ukatili
tunaofanyiwa na ulinzi alioweka
tunashindwa kutoka kambini hapa.
23. Camera inaonyesha Jack akiwa katika
gari anarudi nyumbani huku akitafakari
yale maneno na kulinganisha yote
anayoyaona,anagundua kuwa ni kweli,

BAADA YA WIKI 2
24. Jack anataka maongezi na kiongozi wa
kambi, ana muuliza Hivi mzee wazazi

wangu wako wapi? Umefika wakati nataka


kujua nikawatembelee. Kwa mstuko
mkubwa sana, ananyamaza kidogo kasha
anamjibu Jack wazazi wako walipata ajali
ya gari wakapoteza maisha wote, Jack
anaendelea kuhoja maswali.
25. Camera inaonyesha siku iliyofuata
mkuu wa kambi alikuja sasa kumuweka
selo Jack maana kaisha jua ukweli anaweza
kusumbua, walifika na kumfunga kamba
na kumuweka chumba maarumu nnje
wakawekwa walinzi wa2
26. Camera inaonyesha akiwa
ameninginizwa anaanza kukumbuka
maneno ya babu pia alivyojibiwa na
kiongozi huyo, anajua kuwa ni gaidi sana
anaanza kufikilia njia ya kujiokoa ili
atoroke.
27. Camera inaonyesha baada ya mda
mfupi anakuja kiongozi wa kambi na
walinzi wake ili kumuhoji kupata ukweli
anajua nini kuhusu baba yake, Jack anakaa
kimya wanaamriwa apigwe, wanampiga
kasha wanaondoka na kumuacha akiwa
ameninginia juu.

28.

Akiwa pale hajiwezi anafikilia kipigo


alichopewa ongeza na alivyoambiwa na
babu anapata hasira sana na kuchukua
hatua ya kujifunua mwenyewe.
29. Camera inaonyesha wakipanga
mipango jinsi ya kufanya ili wampoteze
Jack kama alivyotokea kwa baba yake, kwa
sababu ameanza kufuatilia ataharubu
kaqzio na wanaruhusiwa kwenda na
kumfyeka.
30. Camera inaonyesha anagonga mlango
kwa ndani mlinzi anafungua kutazama nani
anagonga mlango, anapewa kichapo na
kutoka njee kimya kimya na kutoroka.
31. Camera inaonyesha wakati wanatoka
nnje kwenda chumba maarum alipo Jack,
wanamuona akichukua gari la kiongozi wa
kambi na kupotea.
32. Camera inaonye kiongozi wa ulinzi
akitoa ripoti kwa mkuu kuwa Jack
ametoroka. Anapewa amri kuwa waende
mpaka warudi nae ra sivyo adhabu kari juu
yao.
33. Camera inaonyesha Jack amefika
njiani kamkuta dada mmo1 kasimama na
gari yake akimsubiri mwenzake anafika na

kupaki pembeni na kuingia kwenye gari


yao, anawaamuru waingie anaondoa gari
kwa speed.
34. Camera inaonyesha wakati wale
walinzi wanafika pale waliona gari
ikipotelea kwa mbali,wanarudi kambini na
kutoa ripoti kuwa hawajaweza
kumkamata,tunaona akiwa na hali ya
kuchanganyikiwa huyo kiongozi wao.
35. Camera inaonyesha akiwa amezidiwa
anapewa huduma ya kwanza kasha
kupelekwa hospitalikwa maumivu
aliyopata kutokana na kupigwa.
36. Camera inaonyesha Baada ya siku 3,
Jack anaruhusiwa na kupewa utaratibu
kuwa anatakiwa kufanya mazoezi ili apate
nguvu vizuri wanaondoka mpaka
nyumbani.
37. Camera inaonyesha Jack akiwa na
wale wadada pale nyumbani wakimuuliza
kilichompata mpaka anakuwa vile.
38. Camera inaonyesha Jack akiwa katika
mazoezi ya viungo vya mwili wake ili
aweze kurudia hali yake.
39. unganisha Camera inatuonyesha
baada ya wiki moja Jack sasa akifanya

mazoezi kwa bidii zote na akikumbuka


mambo aliyotendewa, na akiwa
amekomaa.
40.
Camera inaturudisha kambini tunaona
wakiwa na mkutano walinzo wote
wakipanga jinsi gani wataweza mkamata
Jack popote alipo, wanateuliwa watakao
fanya kazi ya kumtafuta mjini.
41.
Camera inaonyesha maaskali
waliotumwa wapo mjini wakijaribu
kumtafuta Jack kila mahali, siku ya kwanza
inaisha bila kufanikisha.
42.
Camera inaonyesha Jack akiwa na
matembezi mjini mara anapishana nao bila
yeye kujua lakini wao wanamuona na
kumfahamu, wanaanza kumfuatilia ili
wajue anapoishi.
43.
Camera inaonyesha warudi kambini na
kutoa taarifa kuwa Jack kaonekana , na
wamepaona anapoishi, bila kupoteza muda
wanaamuliwa waende na kumleta mara
moja iwezekanavyo.
44.
Camera inaonyesha wale walinzi
wakija, wakati huo Jack nae anawaaga
dada zake na kutoka. Wanafika na

kumuulizia Jack wanaambiwa katoka


wanatekwa na kufungwa kamba wana
ondoka na mmo1 kati yao wanaacha
maagizo.
45.
Camera inaonyesha Jack akiwa njiani
anarudi nyumbani kabeba zawadi kufika
nyumbani anakuta hali tofauti, dada yake
analia, kafungwa na mwingine hayupo,
anamfungua kamba kisha anambiwa
mqaagizo aliyopewa.
46.
Camera inaonyesha dada Jack
aliyetekwa akiwa amefungwa kamba
katika chumba alipokuwa amefungwa
Jack,akiombwa namba za simu ya
nyumbani na kutaja. Simu inapigwa
anapokea Jack anaambiwa unatakiwa
kambini haraka sana kabla ya siku tatu (3)
hazijatimia na kama hautafanya hivyo,
dada yako yupo hatarini na wewe
utafuatia sim inakatwa.
47.
Camera inaonyesha Jack akifanya
mazoezi kwa hasia kali na huku
akikumbuka maneno ya kwenye simu
aliyoambiwa na nah ii siku ya 2

48.
Camera inaonyesha siku ya tatu,Jack
anachukua namba ya simu iliyotumika
kumpigia, anavalia mavazi kazi,na kuaga
kwa dada yake anaingia kwenye gari
anaondoka.
49.
Camera inaonyesha yakiwa yamebaki
masaa 4 anapigiwa simu kuwa mda si
mrefu kazi hatoweza kumuona dada yake
tena,tunaona akishuka kwenye gari na
kuanza kukimbia kuelekea kambini
50.
Camera inaonyesha dada Jack aliyeko
nyumbani amepata ramani ya KAMBI
TAKATIFU anaamua kwenda huko ili atoe
msaada kwa ndugu zake, anaenda mpaka
Jack alipoacha gari analiona na
kulifahamu,anaingia na kuendelea na
safari.
51.
Camera inaonyesha akianza
maagamizi kwa walinzi mmo1 mmo1
anapigana anafanikasha kufika maeneo ya
ndani huku akiendelea kupambana, zikawa
zimebaki dakika 2 anakutana na vikwazo
lakin anapenya anaingia mpaka chumba

alipo dada yake anaona akinyooshewa kisu


kuchinjwa mara anampiga risasi katika
mikono yote gafla anaingia mlinzi wake
anapambana na Jack lakini anashinda
mwishi Jack anafanikisha kuangamiza
kambi mzima na kutoka na dada yake kwa
Ushindi.anaenda kuwa fungulia wafungwa
wanamshukuru sana.
52.
Camera inaonyesha Jack akijikokota na
dada yake mara wanaona gari inakuja
kumbe dada yao, wanaingia kwenye gari
na kuondoka.

MWISHO

You might also like