You are on page 1of 20

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.

com

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1181 SHAABAN 1436, IJUMAA , JUNI 12-18, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Guantanamo Dar!
Aljazeera Ukerewe yazima uzushi wa Jihad John-3
Waalikeni Polisi, 'Task Force' Misikitini wajione!
Mwenzao alisilimu baada ya kutesa Guantanamo
OCD Nansio ajionea. Sasa ahimiza Doria ya Nafsi

SHEIKH Farid Hadd.

MWANASHERIA Mkuu
Wa Zanzibar Saidi Hassan

Tafrani Segerea
Ustadh Salum Ally alala juu ya mti
Amtaka Mwanasheria Mkuu Zanzibar
Sheikh Farid aitwa kuepusha balaa

Vitabu hivi vichomwe moto


Soma zaidi Uk. 20

Kwa nini Wizara inaruhusu kutukanwa Waislam

HAIWEZEKANI Serikali
ya Ta n z a n i a i a c h i l i e
mambo haya yasomeshwe
katika shule za Tanzania.
Vipi mambo haya ya
kipropaganda yenye
khatari kubwa kwa
nchi nzima ya Tanzania

yaendelee kusomeshwa.
Kama nchi hii haina
Udini, muhimu kabisa
ni kupigwa marufuku
usomeshaji wa propaganda
za aina hii na vitabu vyote
vichomwe moto leo kabla
ya kesho. (Soma zaidi Uk. 7, 8)

Ushindi lazima Zanzibar


Woga ukizidi huzaa ujasiri

Usanii wa vitambulisho upo wazi

CCM wanaamini kuwa


wananchi wataendelea
kudumisha amani na
utulivu kwa kuwajaza
woga wa Babu Nshenga.
Lakini watambue kuwa
woga ukizidi sana, huzaa
BAADHI ya wafungwa katika gereza la Guantanamo wakiswali. Juu ni gereza hilo ujasiri usiotarajiwa wala
linavyoonekana kwa nje.
usiozuilika.

Na hapo ndipo
watakapoweza kuona kasi
na ghadhabu za nguvu ya
Umma wakati ukifika.
Tu o m b e a m a n i n a
u t u l i v u wa k w e l i n a
uchaguzi huru na wa haki!
(Soma Uk. 16)

Tahariri/Habari

2
AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786


Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Karibu Ramadhani
ZIMESALIA siku chache
sana kabla ya mwezi
mtukufu wa Ramadhwani
kuingia.
Huu ni mwezi
wa kufunga kama
ilivyobainisha Qur'an
iliposema:
Enyi mlioamini!
mmefaradhishiwa swawm,
kama waliyofaradhishiwa
waliokuwa kabla yenu ili
mpate kumcha Allah.
Na atakayekuwa
miongoni mwenu
mgonjwa au yumo safarini,
basi atimize hisabu katika
siku nyingine. Na wale
wasioweza, watoe fidia
kwa kumlisha masikini.
Na atakayefanya wema
kwa kujitolea, basi ni bora
kwake.
Na mkifunga ni bora
kwenu, kama mnajua.
Mwezi wa Ramadhaan
ambao imeteremshwa
humo Quran kuwa ni
uongofu kwa watu, na
hoja zilizo wazi za uongofu
na upambanuzi. Basi
atakayekuwa mjini katika
mwezi huu na afunge.
N a m we n ye k u wa
mgonjwa au safarini, basi
atimize hisabu katika
s i k u n ye n g i n e . A l l a h
anakutakieni yaliyo
mepesi wala hakutakieni
yaliyo mazito, na
mtimize hiyo hisabu, na
mumtukuze Allah kwa
kuwa amekuongoeni ili
mpate kushukuru. [AlBaqarah: 183-185].
Ni mwaka jana tu
tulikuwa na mgeni wetu
huyu tunayetarajia
kumpokea tena hivi
karibuni, Mwenyezi
Mungu akitujalia.
Tu l i k a a n a y e s i k u
zisizozidi thelathini na
baadaye akaondoka.
Huenda wengi wetu
mgeni huyo alifika
na akatuacha kama
alivyotukuta. Tulisahau
kuwa mgeni huyu kwetu
ni neema isiyofanana na
kitu chochote. Na kwamba
akija akaondoka bila ya
Muislamu kutakasika, basi
tena huyo yupo katika
hasara kubwa.
L a k i n i k wa h e k m a
zake Mwenyezi Mungu,
kila mwaka neema ya
mwezi wa toba hutufikia
na kupata fursa nyingine

ya kujitakasa kwa uchaMungu.


Kwa wale ambao
walikosea mwaka jana
wakaiwacha Ramadhani
ikaondoka zake bila
kuitendea haki, Basi
tusifanye makosa tena
k wa n i b a h a t i wa k a t i
mwingine haiji mara mbili.
Ni vyema tukajiandaa
mapema kuupokea
Ramadhani na mgeni wetu
huyo akija, tunahitajika
tufanye mambo muhimu
yafuatayo.
Kwanza ni kuwa
wapole, wenye huruma,
wanyenyekevu, kupendana
na kusaidiana.
Pili
ndani
ya
Ramadhani tunahitajika
kutubu madhambi yetu
kwa kumuomba Mola
atusamehe yale mabaya
na maovu tuliyoyatenda.
Tunafahamu kuwa kwa
udhaifu wa kibinadamu,
katika kipindi cha mwaka
mzima kama binadamu
tumekuwa ndani ya
dimbwi la maasi.
Ya p o
matendo
tuliyotenda kwa viungo
vyetu, kwa dhahiri au
kwa bahati mbaya, yawe
ya kutenda, ya kuona
au kusikia, yote haya
Ramadhani itatusaidia
tuyafuta kwa sharti kuwa
tuwe wakweli na tutubu
katika ukweli wa kutubia.
Hata tukishamaliza
kutubia, tumeahidiwa
kusamehewa na kuwa
huru na mbali kabisa na
madhambi. Muislamu
anakuwa msafi kama siku
ile ya kuzaliwa. Baada
ya h a p o m g e n i we t u
ataondoka, tunahitaji
neema gani kubwa zaidi
ya hii Waislamu.
Tuangalie, ni wangapi
tulikuwa nao na sasa
hawapo. Hawakupenda
kuondoka, lakini pia nao
walikuwa wamekusuduia
kuwa mwezi huu ukifika
wa t a f u n g a , wa t a t u b u
makosa yao, lakini Mola
keshawachukua.
Basi somo hilo litoshe
kwa Waislamu kujiandaa
kukutana na mgeni huyu.
Tu j i a n d a e k u m p o k e a
v ye m a n a k wa k u wa
tumeshajua kuwa mgeni
wetu ni mtakatifu na
anakuja na neema nyingi,
basi na sisi tujiandae

kupata mafunzo ndani


yake kitakatifu ili kuwa
wasafi wa mwili na roho
hata baada ya kuondoka.
Tusikubali ulaghai wa
dhana potofu za vunja
jungu zilizobeba nafsi ya
matamanio na uasi wa
kidunia, zilizopandikizwa
ili Waislamu wavunje imani
zao na kuwa na dhamira
mbaya za kuipokea
Ramadhani.
Dhana ambazo
zimebuniwa ili ziwafanye
Wa i s l a m u w a k u t a n e
na Ramadhani wakiwa
wachafu, tena uchafu wa
kukusudia kufanywa kwa
kuhofia kuwa ndani ya
Ramadhani hakutakuwa
n a n a f a s i ya k u f a n ya
uchafu huo.
Ni ushauri wetu
tujitahidi sana kuikwepa
dhana hiyo ya uasi, tusiige
tabia za ibilisi na shetani
aliyelaaniwa.

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015


Sote tunafahamu kuwa
Ramadhani ni ishara na
alama njema na fundisho la
kuwaunganisha Waislamu
ulimwenguni kote katika
ibada.
B a s i Wa i s l a m u
wote nchini, ni vyema
wakathamini somo hili,
wakaungana kwa umoja
wao na kusahau hitilafu
zao kupitia Ramadhani hii.
Ni muhimu sasa
Waislamu wakajikurubisha
kwa Mola wao, wakaandaa
sehemu zao za ibada,
masurufu ya futari na
daku, kuwaomba msamaha
wale wote uliowakosea,
wawakumbuke yatima,
wawakumbuke wagonjwa,
wa s i o j i w e z a , wa j a n e ,
wanaohitaji misaada, kutoa
s a d a k a , k u wa a o m b e a
waliotangulia mbele ya
haki na kila mara midomo
yetu iwe ni yenye kutoa
maneno safi na kumtukuza

muumba.
Shukrani zote ni zake
Muumba wa mbingu na
ardhi aliyetujaalia siku
chache za mgeni wetu
Ramadhan zinazompa
Muislamu nafasi ya
kujisafisha na kuwa Mcha
Mungu.
Tutoe tu indhari kwa
wa f a n ya b i s h a r a w o t e
nchini, hasa wa bidhaa
za vyakula kuwa katika
kipindi hiki cha mwezi
Mtukufu wa Ramadhani,
basi wawape tahfif
Waislamu kwa kuwauzia
bidhaa kwa bei ya haki, ili
kuwawezesha kutekeleza
ibada hii kwa wepesi.
Tukifanya baishara kwa
uadilifu tukitanguliza
mbele ucha-Mungu, utu
na huruma kwa waja wa
Allah, itakuwa na matokeo
bora zaidi kuliko kuweka
mbele tamaa ya kupata
hata kwa kuwakomoa
wafungaji.

Serikali ina nia mbaya-Wakili


Ni juu ya akina Sheikh Mselem
Mgomo wapamba moto Segerea

Na Bakari Mwakangwale

WA K I L I w a Wa i s l a m u
wenye tuhuma za Ugaidi,
Abubakari Salimu, amesema
Serikali ina nia mbaya dhidi
ya wateja wake kwa kuipiga
danadana kesi hiyo ili wateja
wake waendelee kusota
rumande.
Wakili huyo, ameyasema
hayo Jumatatu wiki hii
akiongea na An nuur, mara
baada ya Mahakama ya
Kisutu Jijini Dar es Salaam,
kuiahirisha kesi hiyo
inayowakabili Sheikh Farid
Had na wenzake 23, mapaka
Juni 18, 2015.
Alisema, kutokana na
mwenendo wa kesi hiyo
unavyo kwenda, wanaona
kama vile kuna nia mbaya
ya kutaka kuichelewesha
kesi hiyo kwa makusudi kwa
kutumia kigezo cha rufaa yao
(upande wa mashitaka) katika
Mahakama ya Rufaa.
Tunaona kama kuna nia
mbaya ya kuichelewesha
kesi hii, wanatumia kigezo
kwamba kwa sababu
wa m e k a t a r u f a a k a t i k a
Mahakama ya Rufaa, ili pia
na mambo mengine huku
yasimame na hawa Waislamu
waendelee kusota rumande.
Alisema Wakili Salimu.
Wakili Salimu, alisema
awali katika kesi hii ya
Masheikh na Waislamu,
Mahak ama Kuu ilisema
kwamba shauri hili lirudi
Mahakama ya Kisutu,
ili litolewe maamuzi, na
kwamba Mahakama isiseme
tu kwamba haiwezi kusema
chochote hivyo ikatakiwa

irudi ili Mahakama iseme


chochote na ambaye
hatoridhika ndipo akatwe
rufaa.
Cha ajabu, alisema kwa
upande wa Serikali, wao
wakasema wanakata rufaa
k wa m a a m u z i h a y o ya
Mahakama Kuu, akadai, hatua
hiyo wanaona ni kuwa na nia
mbaya ya kuchelewesha kesi
hiyo, kwani imekuwa (upande
wa mashitaka, Serikali)
kila wakifika Mahakamani
(Kisutu) wanasema kuna
rufaa katika Mahakama ya
Rufaa, kwa hiyo hawawezi
kuendelea na chochote.
Akifafanua kigezo hicho
cha upande wa Serikali,
Wa k i l i S a l i m u , a l i s e m a
rufaa hiyo haizuii kesi
hiyo kuendelea kwani kwa
vyovyote itakavyo kuwa,
hata Mahakama ikisema,
Mahakama Kuu ilikosea,
i t a b i d i f a i l i l i r u d i s h we
Mahakama ya Kisutu kwa
ajili ya kuendelea kusikilizwa,
na hata ikisema Mahakama
Kuu ilikuwa sahihi bado faili
litarudi Mahakama ya Kisutu,
akahoji kulikuwa na haraka
gani ya kukata rufaa.
Wakili huyo, akasema
kupigwa danadana kwa kesi
hiyo ya Waislamu ni jambo
la kusikitisha kwani hatua
ya Serikali kukata rufaa
maa muzi ya Mahak ama
Kuu, wao upande wa utetezi
wanaona sio sahihi, kwa
sababu zimeshakuwepo kesi
mbalimbali mfano wa hiyo,
na wala Serikali haikuta rufaa.
Kesi hizo zilikuwa ni za
tuhuma za ugaidi na zilitolewa
maamuzi na Mahakama Kuu

lakini upande wa Jamhuri


ya Muungano (serikali)
hawakukata rufaa, si hivyo
tu lakini hata nia ya kukata
rufaa hawakuionyesha, lakini
kwa hawa Waislamu hali
inakuwa hivyo, hali hii inatia
mashaka. Alisema.
Akirejea mfano wa kesi
hizo, alisema Mahakama
Kuu, ilishawahi kuamua moja
kwa moja kesi ya tuhuma za
Uagaidi ilikuwa ikimkabili
mwanasiasa Mh. Wilfred
Lwakatare, ambapo alidai
kuwa Mahakama hiyo ilifuta
tuhuma za Ugaidi dhidi yake,
lakini upande wa Jamhuri
(Serikali) haikutoa taarifa ya
kukata rufaa.
Lakini akasema mbali ya
kesi hiyo, aliitaja kesi iliyowahi
k u wa k a b i l i wa n a c h a m a
wa Chama Cha Chadema
Wilayani Igunga, Mkoani
Tabora, ambapo Mahakama
Kuu ilifuta mashitaka yao
lakini upande wa Jamuhuri
pia haikueleza nia ya kukata
rufaa.
Wakili Salumu, alisema
kutokana na danadana hiyo,
wanafuatilia suala hilo na
kwamba wameshawasilisha
maombi yao Mahakama ya
Rufaa, juu ya suala hilo.
Alisema, katika barua hiyo,
wameomba mambo mawili,
moja wapo ya mambo hayo,
kwanza izuie hiyo taarifa
ya kukata rufaa kwa maana
kuwa iondolewe, ama isipo
ondolewa basi rufaa husika
isikilizwe haraka ili kutoka
haki na mambo yaweze
kuendelea katika Mahakama
za chini.

Inaendelea Uk. 4

3
Na Mwandishi Wetu,
Mwanza
KITUO cha Kiislamu,
Aljazeera kilichopo Nansio,
Ukerewe, kimefungua
milango yake kwa kila
anayetaka kujua ukweli na
kuvunjilia mbali propaganda
chafu za kukibambikia
ugaidi.
Katika hatua hiyo,
iliandaliwa semina ya mwezi
mzima ambapo msimamo
na mafundisho ya Uislamu
juu ya haki na wajibu wa
Waislamu kwa binadamu kwa
ujumla ulifafanuliwa kwa
mapana na marefu.
M a s o m o ya l i y o t o l e wa
katika semina hiyo
iliyowajumuisha washiriki
181 kutoka mikoa ya Kanda
ya Ziwa, inafuta kabisa zile
propaganda na dhana potofu
kuwa Chuo cha Kiislamu
k a m a A l - J a z e e r a , k u wa
kinaweza kutumiwa kwa
namna yoyote kusomesha
na kuhimiza jambo la
kuwadhuru watu.
Ili kuliweka hilo
bayana kwa vyombo vya
Dola, kiserikali na kijamii,
walialikwa pia washiriki na
watoa mada kutoka taasisi
mbalimbali zisizo za kidini
wakiwemo Kamanda wa
Polisi wa Wilaya, Hakimu wa
Wilaya na maofisa wengine
wa serikali.
Huu ni ufunguaji milango
na uwazi ambao kwa hakika
ni wa kuhimizwa ufanyike
katika taasisi zote za
Kiislamu ili kuchoma moto
kichaka wanakojificha watu
wanaopiga propaganda chafu
dhidi ya Uislamu.
Maadhali mafundisho
ya Uislamu sio biashara
ya bangi, basi Waislamu
wasione vibaya kuwaalika
watu wengine, hasa mamlaka
za kiserikali na taasisi za
kijamii kuona wanachofanya
na hata kutoa elimu kama
alivyofanya OCD na Hakimu
wa Ukerewe.
I l i k u wa n i I m a m u n a
Khatibu Mkuu wa Msikiti
Mkuu wa Ijumaa Mwanza
Sheikh Hamza Mansour,
aliyehudhurisha mada
mintarafu muamala au
mahusiano baina ya Waislamu
na wale wasiokuwa Waislamu.
Katika mada hiyo, Sheikh
Hamza alionesha namna
Mtume alivyoamiliana na
wasio kuwa Waislamu kwa
wema kwa kuwafanyia insafu
na adala ya hali ya juu, hata
wale ambao walikuwa maadui
zake wa wazi kabisa.
Ni katika hali hiyo, washiriki
wa semina na Watanzania
k wa u j u m l a wa l i t a k i wa
kujiuliza: kama Mtume (s.a.w)
alikuwa akiwafanyia uadilifu,
hata wale waliomtangazia
uadui, vipi leo Waislamu
watangaziwe ugaidi ambao
tafsiri yake ni kuwadhuru
watu wasio na hatia.
Au vipi Chuo, Madrasa au
shule inayoitwa ya Kiislamu,
inayosomesha Uislamu,
ituhumiwe kuwa inasomesha
ugaidi.
S h e i k h
H a m z a

Habari

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Aljazeera Ukerewe wakomesha


propaganda za akina Jihad John
Waonyesha njia. Wamwita OCD, Hakimu
Waislamu wasijifungie kama wauza bangi
Kamanda wa Polisi ahimiza Doria ya Roho

akisherehesha mada yake


hiyo, aliwakumbusha
wanasemina na Waislamu
kwa jumla juu ya kisa cha
mateka, aliyekuwa adui
mkubwa sana wa Mtume
(s.a.w.).
M a t e k a h u y o a k i i t wa
Thumama ibn Uthali
aliyetangaza uadui dhidi
ya Mtume (s.a.w.) kabla ya
kukamatwa kwake kama
mateka wakati wa vita.
Baada ya kukamatwa
mateka, Thumama
alishikiliwa na Mtume (s.a.w)
kwa muda wa siku tatu
mtawalia msikitini kwake
ilhali akipatiwa chakula na
huduma zote za kibinadamu
kwa insafu na kwa uadilifu
wa hali ya juu na siku ya tatu
Mtume aliamuru aachwe
huru pasi kufanyiwa ubaya
wowote kwa siku zote tatu za
umateka wake.
Akifafanua kisa hicho,
Sheikh Hamza alisema kuwa
Thumama alielekea nyumbani
kwake baada ya kuachiwa
huru na siku iliyofuata
akarudi kwa Mtume (s.a.w)
kwa ajili ya kusilimu.
H a t a h i v y o , k a b l a ya
kumsilimisha, Mtume
(s.a.w) alimuuliza sababu
iliyomfanya asisilimu wakati
alipokuwa mateka na badala
yake akaja kutaka kusilimu
baada ya kuwa huru.
Kwa maelezo ya
Sheikh Hamza kama
yanavyopatikana katika
vitabu vya Tarikh ya Kiislamu,
Thumama alimjibu Mtume
kwa kumwambia kwamba
lau angelisilimu wakati akiwa
mateka, watu wangelidai
kwamba hakusilimu kwa
imani thabiti kutoka katika
moyo wake, bali amefanya
hivyo kwa kutaka aachiwe
huru kwa hofu ya kuchelea
kuendelea kuwa mikononi
mwa Waislamu akiwa mateka.
Na katika kujieleza,
Thumama akamweleza
M t u m e ( s . a . w ) k wa m b a
aliamua kusilimu kwa ridhaa
yake mwenyewe baada ya
kuachiwa huru kutokana na
uadilifu aliotendewa na yeye
mwenyewe yaani Mtume
(s.a.w.) na Maswahaba zake
(r.a.).
Alisema, hakutegemea
kabisa kufanyiwa wema ule

kutokana na uadui wake


a l i o k u wa n a o d h i d i ya
Uislamu na Mtume (s.a.w.).
Kwa hiyo kutokana na
utu na ubinadamu alioukuta
kwa Waislamu, wafuasi
wa M u h a m m a d ( s . a . w )
wa l i o m s h i k i l i a m a t e k a ,
ilimfanya atafakari juu ya Dini
ya Muhammad na akaamua
kusilimu.
Swali ambalo kila
mwanasemina alitarajiwa
kujiuliza ni hili:
Kama Uislamu unafundisha
kuwafanyia insafu, uadilifu,
utu na ubinadamu mateka wa
kivita, vipi jambo la kuuwa
na kujeruhi watu kigaidi
linasibishwe na Uislamu,
Waislamu na taasisi zao!
Kama haya yanayodaiwa
ya akina Jihad John na IS,
yangekuwa na muingiliano
wowote na Uislamu, basi
tungeyakuta wakifanyiwa
akina Thumama ibn Uthali na
mfano wao, wakati wa Mtume
(s.a.w).
Kwa upande wake
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa
wilaya ya Ukerewe, Bw. Ali
Muhammed alizungumzia
suala la Ulinzi na Usalama
ambapo aliwafahamisha
wanasemina juu ya dhima ya
Jeshi la Polisi katika suala la
Ulinzi na Usalama wa Raia
pamoja na mali zao.
L a k i n i
p i a
akawatanabahisha juu ya
dhima ya raia kuhusu masuala
hayo kwa upande mwingine.
Kamanda Ali aliwazindua
wanasemina juu ya suala la
haki na wajibu wao kwa Jeshi
la Polisi kwa upande wao
kama raia wa nchi hii.
Aidha, alitumia vyema
fursa hiyo kufafanua haki
na wajibu wa Jeshi la Polisi
kwa wananchi na kuwataka
Mashekhe na Waislamu kwa
jumla kudumu katika kile
alichokiita 'doria ya kiroho'.
Hiyo ni pamoja na
kuhakikisha kuwa wanajenga
hulka ya kunasihiana wao kwa
wao pamoja na kuwanasihi
wananchi wengine juu ya
kuamrishana mema na
kukatazana mambo maovu.
Kwa upande wao kama
Jeshi la Polisi aliahidi kwamba
wataendelea na 'doria ya

kimwili' katika kuhakikisha


wananchi na mali zao
wanakuwa katika hali ya
usalama na amani.
Kwa upande wake Hakimu
Mkazi wa Mahakama ya
Mwanzo Bukindo wilayani
humo Bw. Mrisho Abeid
alihudhurisha mada mbili
zikihusu 'Makosa ya Jinai' na
'Sheria ya Ardhi'.
M a d a ya ' M a k o s a ya
Jinai' ililenga kuwapatia
wanasemina mwangaza wa
ufahamu juu matendo ya
jinai ili waweze kuyatambua
na kujitahidi kuyaepuka,
hususan katika kipindi hiki
cha zama za ulimwengu
wa propaganda dhidi ya
Waislamu na Uslamu kwa
jumla.
Kwa upande wa mada
ya 'Sheria ya Ardhi
Tanzania', hii ililenga juu
ya k u wa t a n a b a h i s h a n a
kuwatolea ufafanuzi
wanasemina na Waislamu
kwa jumla juu ya masuala
mtambuka yahusuyo ardhi
kama vile tafsiri ya ardhi
kisheria, taratibu za kupata
ardhi, umiliki wa ardhi,
wajibu wa mmiliki wa ardhi,
haki za mmiliki wa ardhi, jinsi
ya kupoteza haki ya umiliki
wa ardhi, migogoro ya ardhi,
asili au chimbuko la migogoro
ya ardhi pamoja na utatuzi wa
migogoro ya ardhi.
Pa m o j a n a h a y o , B w .
Mrisho Abeid aliwahamasisha
Waislamu mmoja mmoja
na kama kundi wajitahidi
kadiri ya uwezo wao kutafuta
n a k u m i l i k i a r d h i , k wa
munasaba wa kisheria na si
kiholela au kimazoea, kwa
ajili ya maendeleo yao binafsi
ya kimakazi, kibiashara, kama
ilivyo kwa wananchi wengine
na kwa maendeleo yao kama
umma kwa ajili ya ujenzi
wa shule, hospitali, zahanati
pamoja na vitega uchumi
vingine.
Naye Afisa Biashara
wa wilaya ya Ukerewe,
B w . S a n g a r a r a Wa r i o b a
aliwafunda wanasemina na
Waislamu kwa jumla juu
ya suala la ujasiriamali
na umuhimu wake kwa
Waislamu na kwa wanajamii
wengine kwa jumla.

Bwana Warioba alisisitiza


umuhimu wa kujikwamua
kiuchumi ili kujimudu kwa
chakula, makazi, mavazi na
kumudu kutekeleza ibada
maalumu zinazomhitaji
Muislamu kuwa na uwezo
wa kimali kama kutoa zaka
na kwenda kutekeleza ibada
ya hijja.
Akitoa nasaha zake katika
semina hiyo, Sheikh wa
wilaya ya Ukerewe Juma
Saidi aliwanasihi wanasemina
kuzingatia utendaji,
uelimishaji na uchungaji wa
mipaka ya Allah (s.w.).
Kuhusu utendaji, Sheikh
Juma Saidi aliwataka
wanasemina wawe mabalozi
wazuri katika jamii zao
walizotoka kwa kuyatia katika
vitendo yale yote waliojifunza
kupitia semina hiyo katika
maisha yao ya kila siku.
Kwa upande wa suala la
uelimishaji, Sheikh Juma
aliwahimiza wanasemina
wa wa f i k i s h i e Wa i s l a m u
wenzao na jamii kwa jumla
yale waliyojifunza pamoja
na kuwataka wao wenyewe
kuendelea kujifunza kutoka
kwa Waislamu wenzao.
Kwa kumalizia akawataka
wanasemina kuchunga
mipaka ya Allah (s.w.) popote
watakapokuwa.
Wa f a n y e h i v y o k w a
kushikamana na mafundisho
ya Qur-an na Sunna pamoja
na kuwaasa kujiepusha na
yale yote yanayopingana na
viwili hivyo.
Taasisi ya Al-jaziira Islamic
Centre ( JIC) ipo kijiji cha
Nebuye kata ya Ngoma
tarafa ya Mumbuga wilayani
Ukerewe mkoani Mwanza.
S e m i n a h i i ya m we z i
mzima ni ya kumi na nne
(14) ikiwa ni mwendelezo
wa semina kumi na tatu
zilizowahi kuratibiwa na
kuendeshwa huko nyuma na
taasisi hiyo kama mojawapo
ya sehemu ya programu zake
za kila mwaka.
Semina ilifanyika katika
Msikiti Mkuu wa Ijumaa
uliopo katikati ya mji wa
Nansio wilayani Ukerewe
na kuhudhudhuriwa na
Wa i sl a mu wa p a t a o 1 8 1 ,
wanaume wakiwa 98 na
wanawake 83, kutoka mikoa
ya kanda ya ziwa na mikoa
ya jirani.
Mafunzo katika semina
hiyo yaliendeshwa na
wataalamu mbalimbali wa
ndani na wa nje ya taasisi hiyo
waliohudhurisha mada kwa
nyakati tofauti kulingana na
ratiba iliyopangwa ambayo
ilijumuisha masomo ya elimu
ya mwongozo ambayo ni
Qur-an (Usomaji na Tafsiri),
H a d i t h , Ta u h i i d , F i q - h i
pamoja na Sira.
Semina ilifunguliwa
Ijumaa ya Mei nane (Mei 8)
hadi Jumapili ya Juni saba
(Juni 7, 2015).

4
Inatoka Uk. 2

Alisema, mpaka sasa


kutokana na hali hiyo,
wateja wake wanaoshikiliwa
k wa m u d a m r e f u s a s a
kwa kunyimwa dhamana,
inaonekana wamepoteza
muelekeo, kwani akasema
hata hatua wanazo zichukua
hivi sasa ni kutokana na
madhila wanayoyapata.
Alisema, hatua ya kugoma
kula gerezani na kugoma
kushuka katika gari kuingia
Mahakamani Jumatatu wiki
hii, ni miongoni mwa ishara
za kupinga kunyimwa haki
zao na kupigwa danadana
kwa kesi yao.
Leo (Jumatatu wiki hii)
wa t u h u m i wa wa m e f i k a
Mahakamani, lakini kuna
wengine hawakufika
kutokana na sababu
mbalimbali, wapo ambao
wanaumwa hawakuweza
kufika na wengine wapo
katika mgomo wametengwa,
hatujui kinachoendelea juu
yao. Alisema Wakili Salimu
na kuongeza,
N a h a wa wa l i o f i k a
Mahakamani hapa Kisutu,

Na Sheikh Al-sayed
Awadh Abduladhim
Shukrani zote anastahiki
Mwenyezi Mungu Rehema
na amani zimfikie Mtume
wa Mwenyezi Mungu.
Kwa hakika wamezingatia
wanachuoni funga kwa
u wa z i k u wa n i m a i s h a
ya kimaumbile hayawezi
kuendelea maisha hayo
isipokuwa kwa funga
kutokana na usawa na Afya ya
maumbile yetu yaliyokamili
n a k wa k i u m b e ye y o t e
hapana budi atakumbana na
ugonjwa ambayo yatamzuia
kula na kama hakufunga kwa
kutaka mwenyewe.
Hapa ndipo tunapoiona
miujiza ya Mwenyezi
Mungu kwa kuweka sheria
ya kufunga kuwa ni ibada,
funga husaidia viungo
katika kuvipumzisha kwa
chakula kidogo pamoja
na kuendeleza maisha
ya kawaida kama ilivyo
elimu ya kidaktari ya sasa
imethibitisha kuwa funga
ni kinga na ni tiba kubwa
ya magonjwa mbali mbali

Habari/Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Serikali ina nia mbaya-Wakili


nao hawakushuka, kutoka
katika gari la Magereza ni
mgomo mwingine tena huu
ukiacha ule wa kula chakula,
ambao ulianza na wachache
wiki iliyopita.
Alisema, migomo hiyo
miwili tofauti ina maana
t o f a u t i t o f a u t i k wa n z a
wanalamikia kuona kuwa
kesi yao inacheleweshwa bila
sababu za msingi, lakini pia
wanadai kuwa Mahakama
ya Kisutu haina uwezo wa
kusikiliza tuhuma zao kwa
hivyo haikuwa sahihi wao
kuletwa katika Mahakama
hiyo.
Lakini pia wametuambia
kuwa madai yao waliyokuwa
wakiyatoa siku zote
ya k u p a t i wa m a t i b a b u
hayatekelezwi pamoja na
haja yao ya kuonana na
Wanasheria Wakuu kutoka
Zanzibar na Bara haijatimizwa
kwa hiyo hawaoni sababu
ya kuendelea na kesi yao.
Alieleza kilio cha Masheikh

na Waislamu hao.
Kwa mujibu wa Wakili
h u y o , Wa i s l a m u h a o
wamedai kurejea Gerezani,
Segerea kwenda kuungana
na wenzao waliogoma kula,
tokea wiki iliyopita jambo
ambalo alidai inaongeza
idadi ya wanaogoma kula
kadiri siku zinavyozidi
kwenda mbele badala ya
kupungua.
Hata hivyo, Wakili huyo
a l i s e m a k u wa H a k i m u ,
amewataka wao kama
Mawakili wa watuhumiwa
hao, wanayo kila sababu ya
kufika gerezani kuwaona
watuhumiwa hao na kupata
uhakika wa kile kinachodaiwa
kugoma kula wakiwa humo
gerezani.
Kutokana na hii hali,
Hakimu ameshauri tutumie
nafasi yetu kwende kuonana
nao na wao kama Mahakama,
wa t a c h u k u a j u k u m u l a
kwenda kuwaona pia maana
k i s h e r i a wa n a r u h u s i wa

kufanya hivyo, ili


kujiridhisha na kujuwa ni
kweli watuhumiwa hao
wamegoma kula au ni taarifa
tu zinazushwa. Alisema
Wakili huyo.
Hata hivyo alisema, hatua
hiyo ya kugoma kula na
kuingia Mahakamani ni
utashi wao kutokana na
kuona kuwa hawatendewi
haki, hivyo ikiwa wameona
hiyo ndiyo njia ya kuweza
kutoa msukumu kwa ajili
ya kumaliza jambo lao, ni
maamuzi yao binafsi.
Sisi nafasi yetu ni
kuwashauri tu, kwamba
wasigome kula, wasigome
kushuka katika gari
wanapofika Mahakamani,
lakini kutekeleza inabaki
katika utashi wao ambao
hakuna ambaye ataweza
kuuingilia. Huwezi
kumlazimisha mtu mzima
kula, kama anasema hataki,
sasa wewe unafanyaje kwa
hiyo hili ni suala la mtu binafsi

kwa kile anachoamini


inafaa katika kupigania
haki yake, japokuwa sheria
hairuhusu kufanya hivyo.
Alisema na kufafanua.
Kwa mujibu wa Kamati
ya Maafa ya Shura ya
Maimamu, imeeleza kuwa
mpaka sasa (Jumanne wiki
hii) idadi ya Waislamu
waliogoma gerezani
imefika 18, na wote hao
wamewekwa katika selo
ya ndani ya gereza hilo.
Wa k a t i h u o h u o ,
imeelezwa kuwa
mtuhumiwa namba 22,
katika kesi hiyo, Ustadhi
Abdallah Saidi, ametolewa
katika selo ya mjumuiko
na wezake kutokana na
kile kilichoelezwa kuwa
yupo mstari wa mbele
kutoa Daawa gerezani
humo.
Taarifa hizo zimesema
kuwa Ust. Saidi,
alichukuliwa hatua hiyo
na uongozi wa Gereza hilo
tokea Juni 6, 2015,ambapo
ameunganishwa katika
selo maalumu ya Masheikh
Faridi Had na Sheikh
Mselem Ally.

ibada kwa ajili ya Mwenyezi


Mungu ni miongoni mwa
ibada tukufu nayo ni siri
kati ya mja na mola wake
na Mwenyezi Mungu ndiye
mlipaji wa funga amesema
kila matendo ya binadamu
ni yake isipokuwa funga
kwani hiyo ni yangu na mimi
ndiye nitakaye lipa imamu
Bukhari hapo huja manufaa
mwIngine yote kwa njia ya
kuifuata funga au ni ya ziada
tuu na moja ya manufaa hayo
ni ya kidunia na hukumu
ya m o l a m l e z i a m b a ye
wameanza kugundua juu
ya funga kwa uwazi katika
zama zetu hizi mpya nayo ni
kupatikana afya ya kimwili
na ya nafsi na badala ya
kumshukuru Mwenyezi
Mungu na kumshukuru juu
neema hizi zilizoongezeka
katika funga juu ya neema ya
kuabudu tumeanza tunajadili
juu ya uwezo wa funga katika
kutibu na magonjwa wakawa
baadhi wanazungumzia
kuhusu
kiwango
wanazungumzia kuhusu
kiwango cha kushindwa
kielimu katika kutibu kwa
kutumia funga na kwamba
ni tiba ya kila ugonjwa na
kama ni makusudi wengine
wanakanusha na wengi wao
ni wale wanaotumia mali
zao ovyo wao wanapinga
kuwa funga inanafasi
yoyote ya kitiba miongoni
mwa magonjwa na ni kati
ya kuvuka mipaka na
mapungufu akasimama
mgonjwa akiwa ameduaa
hajui juu ya hizi rai mbili ipi
aushike na kati ya kuvuka

mipaka au mapungufu
inasimama dini ya kiislamu
kwa ushupavu kwa ukati
na kati wake uliozoeleka ili
kuleta muongozo wake wa
ukati na kati kwa ajili ya uma
wa kati na kati katika hali
zake zote kama alivyosema
Mwenyezi Mungu mtukufu
na hivyo hivyo tumewafanya
uma wa kati na kati 143 Albakarat anasema mmoja wa
madoktari waislam pamoja
na kukiri kwangu kulikotimia
kama dokta muislam
kwamba funga husaidia
katika tiba katika baadhi ya
magonjwa isipokuwa mimi
Siwezi kuutani kielimu kuwa
ni hakika na ni maalum
wakati wa mtume kabla ya
zama zake kabla ya kuja
mtume na hakuja mtume
(S.A.W) kwa dalili ya wazi
inayojulisha nafasi ya funga
katika tiba na lililozuri na
tuseme kwamba miongoni
mwa hukumu za funga kuwa
zinasaidia tiba baadhi ya
magonjwa kwa masharti ya
kushikamana na mpango wa
chakula cha kiislam na amri
za daktari anayekutibu na
huu ndio muongozo wa ukati
na kati katika kuifanyia kazi
funga na hilo ndilo bora kwa
kufuata na kuepuka kuvuka
mikapa au mapungufu
ambayo hupelekea maadui
wa u i s l a m u k u wa u n a
upungufu na hauna utukufu
pale tutakapo waambia kuwa
katika funga kuna tiba ya
kila magonjwa tunawaambia
hakuna tiba katika funga ya
hivi hivi.

Funga ni chanzo cha afya ya binadamu

tena ya hatari magonjwa


ya sasa pamoja na kuwa na
kiasi kidogo cha chakula
kilichopo kwenye moyo
hujipanga pumzi na hufanya
kazi kwa kujipumzisha zaidi
na kwa mpangilio hujinyosha
m a p a f u m a w i l i b i l a ya
kikwazo na hupungua vizuizi
vya kukutana navyo moyoni
hupungua mapigo yake kwa
kutohitajika juhudi zote hizo
zilizokubwa kwa ajili ya
kusukuma damu kwenda
katika moyo kwa kuipeleka
msukumo wa kiasi kikubwa
cha chakula na kabla ya kila
kitu kwani viungo vingine
hupata raha ya lazima kwa
ajili ya kufanya upya wa
viungo vilivyoharibika
vipate uzima uliokamilika,
na kama ilivyokuwa
uwakilishi wa chakula na
u c h a f u wa k e h u r u h u s u
kipindi cha mapumziko
viungo kuwa huru hapo hua
upya yenyewe kwa yenyewe,
na miongoni mwa mambo
ambayo hayanashaka ndani
yake, kwamba kila sheria
katika uislam vina hukumu
yake na faida zake nyingi
kiasi haziwezi kudhibitiwa
na akili ya kibinadamu na
wala haiwezi kuwekwa
kwenye elimu isipokuwa
Mwenyezi Mungu ambaye
ni mjuzi wa hali zote za
viumbe na kwa yale yaliyo
mazuri kwao kwamba
alivyosema Mwenyezi
Mungu mtukufu kwani
anatu vile alivyoviumba naye
ni mpole ana habari (14)
Mulku lakini shina katika
hekima katika kila ibada
iwe kwa ajili ya kujisogeza
k wa M we n ye z i M u n g u
kama alivyosema Mwenyezi
Mungu sema hakika ya

swala yangu na ibada zangu


na uhai wangu na umauti
wangu kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu mtukufu mola mlezi
wa ulimwengu 162 An-aam.
amesema Mtume (S.A.W)
kwa hakika kila matendo
hutazamwa nia na kila mtu
ana alichonuia Bukhari na
kwa hivyo basi ni wajibu
wa kila muislam aweke
lengo lake katika kila ibada
ni kumridhisha Mwenyezi
Mungu kwanza na mwisho
na sio kupata faida ya kidunia
kama hivyo ndivyo huenda
ukafanikisha au usifanikishe
na funga ya Ramadhani
katika sheria ya kiislam ni
nguzo miongoni mwa nguzo
za kiislam ameifaradhisha
kwa hekima yake kubwa
kuziunganyisha nyoyo za
waislamu kwa ucha mungu
na si kwa manufaa ya kidunia
ya mpito na kwa hivyo
amesema enyi mlioamini
imelazimishwa kwenu funga
kama ilivyolazimishwa kwa
watu waliopita kabla yenu
ili mpate uchamungu 183
Al-bakarat funga katika
uislamu sio mazoezi ya
viungo, ambayo malengo
yake ni kupunguza uzito wa
mwili na kuiadhibu nafsi na
kuilazimisha ili iwe nyepesi
kukufuata na uitawale wala
sio mazoezi ya kiroho kwa
maana unaipa mazoezi
kama huko wanako fanya
mazoezi ya kihindi kwa lengo
la kuongeza uzingatio au
kukuza moyo au vinginevyo.
Miongoni mwa malengo
ya kidunia bali funga ni

5
Jeshi Lebanon
lawashukuru
Hizbullah kwa
kuwadhibiti
magaidi
KAMANDA Mkuu wa Jeshi
la Lebanon Jean Kahwaji
ametoa shukuran zake za
dhati kwa Wanaharakati
wa Kiislamu wa Hizbullah
nchini humo, kufuatia
juhudi walizozionyesha
katika kukabiliana na
makundi ya kigaidi
wakishirikiana wanajeshi
wa Lebanon katika
operesheni za pamoja katika
maeneo ya mpakani mwa
nchi hiyo na Syria.
Wa p a m b a n a j i wa
H i z b u l l a h wa l i a n z i s h a
operesheni za kuyasafisha
maeneo ya mpakani ya alQalamun yaliyopo katika
ardhi ya Syria tangu wiki
tatu zilizopita, ambapo
wamefanikiwa kuyasafisha
maeneo mengi yaliyokuwa
yamejaa makundi hayo.
K a t i k a h o t u b a ya k e ,
Kamanda Mkuu wa jeshi
la Lebanon Jean Kahwaji,
alisisitizia udharura wa
kuendelezwa mapambano
hayo kwa lengo ya
kuyasafisha kabisa maeneo
ya mpakani mwa taifa hilo,
huku akishiriautayari wa
jeshi la Lebanon katika
uwanja huo.
Kahwaji alisema kuwa
siasa za ndani ya Lebanon
zinaviunga mkono vikosi
vya jeshi hilo, ili liweze
kutekeleza majukumu yake
kwa namna iliyo bora zaidi.
Aidha alisisitizia udharura
wa jeshi la taifa hilo kuwa
makini na kuongeza
kuwa, uchunguzi wa duru
za usalama unaonyesha
kuwa, makundi ya kigaidi
yanakusudia kutekeleza
vitendo vya kigaidi katika
maeneo ya ndani mwa nchi
hiyo kufuatia kushindwa
huko mpakani.
Inaelezwa kuwa baada
ya mapigano makali katika
m a e n e o ya a l - Q a l a m u n
yaliyosababisha kusafishwa
maeneo mengine ya
kimkakati yenye ukubwa wa
zaidi ya kilometa za mraba
300, kwenye miinuko ya
mpakani mwa nchi mbili
za Syria na Lebanon, hali
ya usalama bado ni ya kutia
wasiwasi katika miji na vijiji
vya maeneo hayo kutokana
na uwepo wa wanachama
wa m a k u n d i ya D a e s h
na Jabhatu Nusra katika
miinuko ya miji ya Arsal,
Kaskazini Mashariki mwa
Lebanon ambao wanaweza
kufikiria kulipa kisasi.
Ni katika mazingira hayo,
ndipo Katibu Mkuu wa
Hizbullah, Sayyid Hassan
Nasrullah alisema kutokana
na mazingira nyeti ya sasa
ya taifa hilo la Kiarabu na
eneo zima la Mashariki ya
Kati, aliwataka viongozi na
makundi ya siasa ya nchi hiyo
kutambua mazingira hayo na
kuisaidia serikali na jeshi
katika kutekeleza majukumu
yao ya kuimarisha usalama
nchini.

Habari za Kimataifa

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Watoto wanamalizwa Palestina

Mikutano ya
Israel imeua watoto 980 Gaza siri Saudia na
Israel ni hofu
JESHI la Utawala wa Israel
limewaua watoto wapatao
kwa Iran?
980 katika hujuma zake
za hivi karibuni katika
Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa Kituo
cha Habari cha Palestina,
i m e k u wa n i j a m b o l a
kawaida kwa utawala
wa Kizayuni wa Israel
kukiuka sheria zote za
kimataifa kuhusu kulinda
haki za watoto katika vita
vyake dhidi ya Gaza.
Taarifa iliyotolewa na
Jumuiya ya Kimataifa
ya Kuwatetea Watoto
Wapalestina, kwa mnasaba
w a S i k u y a Wa t o t o
Wasio na Hatia ambayo
huadhimishwa Juni 4,
imesema kuwa mwaka
2014 ndio uliokuwa
mbaya na mgumu zaidi
kwa watoto wa Gaza,
kwani zaidi ya watoto 530
waliuawa katika hujuma
za katili za jeshi la Israel.
Aidha taasisi hiyo
i l i s e m a k u wa k a t i k a
mwaka huo, kwa wastani
watoto 196 Wapalestina
walikuwa wakikamatwa
kila mwezi na vikosi vya
Israel. Kwa ujumla zaidi
ya Wapalestina 2,100,
wengi wao wakiwa raia,
waliuawa katika hujuma
ya kutisha za utawala wa
Kizayuni wa Israel huko
Gaza mwaka 2014.
Wakati huo huo taasisi
za Umoja wa Mataifa
zimeafikiana na taasisi
za Palestina kuwa idadi
ya kushtusha ya watoto
waliuawa katika hujuma
ya Israel huko Ghaza
mwaka jana. Katika ripoti
ya s i r i ye n ye k u r a s a
22 iliyovujishwa kwa

WAZAZI wa Kipalestina wakiwa wamebeba maiti


za watoto wao waliouliwa na majeshi ya Israel huko
Gaza.
vyombo vya habari, Jeshi wamepata hifadhi hapo
la Israel limetajwa kuwa ni waliuawa shahidi.
mtenda jinai mahiri dhidi
Imedokezwa kuwa
ya watoto.
Katibu Mkuu wa Umoja
Ripoti hiyo pia imetaja wa Mataifa Ban Ki-moon,
namna jeshi la Israel yuko chini ya shinikizo la
lilivyodondosha mabomu Marekani kutoiweka Israel
katika shule saba za Umoja katika orodha ya nchi
wa Mataifa katika vita vya zinazokiuka haki za watoto
mwaka jana Gaza, ambapo kama ilivyopendekezwa
w a t u 4 4 w a l i o k u w a katika ripoti hiyo.irib.

TELEVISHENI ya Marekani
ya CNN imefichua kuwa,
Wizara ya Mambo ya Nje ya
nchi hiyo imewapa mafunzo
magaidi wa Daesh.
Te l e v i s h e n i h i y o y a
Marekani imesambaza
mkanda wa video kupitia
Intaneti, ambapo ndani ya
mkanda huo anaonekana
Kanali Gulmurod Khalimov,
Mkuu wa zamani wa Jeshi la
Polisi la Tajikistan ambaye
hivi sasa amejiunga na kundi
la la Daesh akisema kuwa,
yeye binafsi ameshiriki mara
tatu katika mafunzo ya kijeshi
ndani ya ardhi ya Marekani
na moja ya mafunzo hayo
ameyapata kwenye jimbo la
Louisiana la Marekani.
Hata Wizara ya Mambo
ya Nje ya Marekani imekiri
jambo hilo. Msemaji mmoja

wa Wizara ya Mambo ya
Nje ya Marekani ameiambia
televisheni ya CNN kwamba
Kanali Khalimov, alipata
mafunzo ya kijeshi katika
vipindi vitano tofauti nchini
Marekani na Tajikistan baina
ya mwaka 2003 hadi 2014.
Alisema, mafunzo hayo
yalitolewa na kusimamiwa na
Wizara ya Mambo ya Nje ya
Marekani kwa kile alichodai
ni kupambana na ugaidi.
Licha ya viongozi wa
Marekani kukiri mara
kwa mara kuwa ndio
waliolianzisha na kulipa
mafunzo kundi la Daesh,
lakini hivi sasa wameunda
muungano wa kulipiga vita
kundi hilo.
Wachambuzi wa mambo
wanasema kuwa huo ni
mchezo wa kisiasa tu wa

RIPOTI imefichuka kuhusu


mikutano kadhaa ya siri
baina ya wawakilishi wa
Saudi Arabia na Israel kwa
lengo la kujadili misimamo
yao kuhusu Iran.
Kwa mujibu wa tovuti
ya Bloomberg, mikutano
hiyo imefanyika mara tano
katika kipindi cha miezi 17
iliyopita, ambapo maafisa
hao wa Saudia na utawala
wa Israel wamekutana kwa
nyakati mbalimbali huko
India, Italia na Jamhuri ya
Czech.
Tovuti hiyo imemnukuu
Jenerali mstaafu katika
Jeshi la Israel, aliyeshiriki
katika moja ya vikao hivyo
akisema, "Tuligundua kuwa
tunakabiliana na matatizo na
changamoto za pamoja na pia
baadhi ya majibu ya pamoja."
Aidha Alhamisi iliyopita
m a a f i s a m a s h u h u r i wa
zamani wa Saudia na Israel
walikutana katika taasisi za
Council on Foreign Relations
huko Washington.
Kikao hicho kilihudhuriwa
na Anwar Majed Eshki,
Mshauri wa zamani wa
serikali ya Saudia na Dore
Gold, balozi wa zamani wa
Israel ambaye nimtu wa
karibu sana wa Waziri Mkuu
wa Utawala wa Kizayuni
Benjamin Netanyahu.
Israel na Saudia zote
kwa pamoja zinapinga kile
zinachosema ni kuenea
ushawishi wa Iran katika
eneo la Mashariki ya Kati.
Aidha pande mbili hizo
zimetangaza wazi kupinga
mapatano ya nyuklia baina ya
Iran na madola sita makubwa
duniani.
Hivi karibuni gazeti moja
la Uingereza lilisema Israel
imetangaza kuwa tayari
kuipa Saudia makombora
katika vita vyake dhidi ya
watu wa Yemen.

CNN yafichua namna US inavyowapa mafunzo Daesh


M a r e k a n i n a k wa m b a ,
Washington na washirika

wake hawana nia ya kweli


ya kupambana na kundi hilo.

JOHN Mcain aliyekuwa mgombea Urais wa Republican


Marekani amekuwa kinara wa mawasiliano kati ya kundi
la Daesh na Serikali ya Marekani nchini Syria.

TANGAZO

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE


KIRINJIKO ISLAMIC TEACHERS COLLEGE - SAME, KILIMANJARO

KOZI YA UALIMU WA LUGHA YA KIARABU, KIINGEREZA,


KISWAHILI NA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU NGAZI YA CHETI

Muda wa Kozi ni miaka miwili


SIFA ZA MUOMBAJI:
(a) Awe Muislamu.
(b) Awe amefaulu masomo manne (4) au zaidi kwa kiwango cha D au zaidi katika Mtihani wa Kidato cha 4.
(c) Atakayekuwa na ufaulu wa kiwango cha D au zaidi katika Lugha ya Kiarabu, Kiingereza, Kiswahili na Elimu ya Dini ya Kiislamu
atapewa kipaumbele zaidi.

Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 15 JULAI, 2015.


Fomu za maombi zinapatikana kwa gharama ya Shilingi 5,000/= (elfu tano) katika Tovuti:www.ipcorg.tz na katika vituo vifuatavyo:
ARUSHA: Ofisi a Islamic Education Panel,
Jambo Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala
na Msikiti Mkuu wa Bondeni, Simu: 0783
552414/0762 817640.

KILIMANJARO-Moshi: Msikiti wa Riadha:


0712216490 Same Juhudi Studio mkabala
naBenki ya NBC Same: 0757013344.
Same: Kirinjiko Islamic Secondary
School: 0784 296424/0655 676075.
Usangi: Falhum Kibakaya: 0787 142054.
Ugweno: Kifula shopping Centre: Yusuph Shanga:
0784 585776.
TANGA: Twalut Islamic Centre - Mabovu Darajani:
0715 894111
Uongofu Bookshop: 0784 982525.
Korogwe: SHEMEA SHOP: 0754 690007.
Lushoto: Mandia Shop: 0782 257533
Handeni: Mafiga - 0782 105735/0657 093983.
MWANZA: Nyasaka Islamic Secondary School: 0717
417685/0786 417685.
Ofisi ya Islamic Education Panel, Mtaa wa Rufiji
mkabala na Msikiti wa Al-Amin: 0785086770/0714
097362.
MUSOMA: Ofisi ya Islamic Education Panel Mtaa wa
Karume, Nyumba Na. 05: 0765024623.

SHINYANGA: Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa


SONGEA: Kwa Kawanga karibu na Msikiti wa Nuru
ya Shinyanga Mjini: 0752 180426.
- 0713 249264/0683 670772.
Kahama: Ofisi ya AN-NUUR na Msikiti wa Ibadhi: 0753
Mkuzo Islamic High School: 0717 348375.
993930/0688 794040.
DAR ES SALAAM: Ubungo Islamic High School:
0756584625/0657 350172.
Ofisi ya Islamic Education Panel, Temeke - Msikiti wa
Nurul Yakin: 0655144474, 0787119531.
MOROGORO: Ramadhani Chale-0715704380
DODOMA: Hijra Islamic Primary School: 0716
544757/0718661992.

MBEYA: Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini0785 425319.


Rexona Video mkabala na Mbeya RETCO, 0713
200209/0785 425319.
RUKWA: Sumbawanga: Jengo la Haji Said - Shule ya
Msingi Kizwike 0717 082072.

SINGIDA: Ofisi ya Islamic Education Panel, karibu na


Nuru Snack Hotel:0786425838/0784 928039.

TABORA: Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566,


0787 237342.
Nzega: Dk. Mbaga 0754 576922/0784 576922.

MANYARA: Ofisi ya Islamic Education Panel-Masjid


Rahma: 0784 491196.

IRINGA: Madrastun-Najah: 0714 522 122

KIGOMA: Msikiti wa Mwandiga: 0714 717727


Kibondo: Marubona Isl. SS. 0714 710802.

PEMBA: Wete Islamic Sch. 0777 432331/0712772326


UNGUJA: Madrasatul - Fallah: 0777 125074

LINDI: Wapemba Store: 0784 974041/0783


488444/0653 705627.

Pandu Bookshop: 0777 462056 karibu na uwanja wa


Lumumba.

MTWARA: Amana Islamic S.S. 0715 465158/0787


231007.

MAFIA: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na Msikiti Mkuu:


0773 580703.

Kwa maelezo zaidi piga simu: 0787 188964, 0784 267762 na 0654 613080

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU - WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Propaganda za udini shuleni Tanzania-6

Profesa Ibrahim Noor Shariff

Z I N A Z O F U AT A n i
picha nambari 6.10 na
6.11 ambazo zimewekwa
pamoja katika ukurasa
wa 80 wa kitabu cha
History for Secondary
S c h o o l s , F o r m Tw o ,
2012. Kwanza ziangalie
picha zenyewe, ikisha
tutazungumzia juu ya
propaganda iliyotumika:
M a a n a ya m a e l e z o
yaliyoandikwa kwa
Kiingereza chini ya picha
ya kwanza yanasema
Mtumwa akipigwa
mboko na maelezo ya
pili yanasema Mtumwa
anyongwa na aachiliwa
afe.
Kwa mtu yoyote
mwenye kutumia akili
yake, ataelewa moja kwa
moja kuwa kuziweka
pamoja picha hizi mbili si
jambo la sudfa, bali ni la
kukusudiwa. Ya kwanza
inaonesha huyo khabithi
anayemcharaza mboko
mtumwa ni Mwarabu na
kuiweka ya pili ubavuni
m wa k e n i k u m f a n ya
mtazamaji mwenyewe
amalize kwa fikra ya
kwamba waliomnyonga
mbavuni huyo mtumwa
wa Kiafrika na kumwacha
afe kwa maumivu mapevu
ya kikatili, si wengine bali
ni Waarabu Waislamu.
Sasa tuangalie mchezo
mchafu wa kipropaganda
we n ye k u t u m i a d i n i
kama ni kisingiziyo
ulivyochezwa.
Kwanza, inasikitisha
kuona kuwa waandishi wa
kitabu hicho cha historia,
kughushi mchoro wa yale
yaliyotendeka Suriname
Amerika ya Kusini, nchi
ambayo ilikuwa ni koloni
la Wadachi na wala sio
Afrika Mashariki na
wa k h u s i k a wa l i k u wa
Wazungu Wakristo wala si
Waarabu Waislamu. Sasa

angalia tena hizo picha na


zile za asili na ujiamulie
mwenyewe namna na
kadiri ya mchezo muovu
u n a o c h e z wa n a wa l e
wenye siasa kali za kidini
Tanzania.
Picha ya kwanza ya
upande wa kushoto ni
ya asili, nayo imetokana
na masimulizi ya John
Gabriel Stedman. Picha
hii, kwa tafsiri, imeitwa
Mnegro aliyetundikwa
a k i wa m z i m a k a t i k a
mbavu zake kwa ajili ya
kunyongwa Mchoro huo
umetokana na maelezo
ya alieshuhudia kitendo
hicho huko Suriname
mwaka 1773. Mtumwa
huyo pichani alishindiliwa
shazia au ndoana kubwa
mbavuni mwake na
kutundikwa kwa ndoana
hiyo. Katika tukio hilo,
mtundikwa alikaa siku
tatu akisononeka kabla ya
kufa baada ya kupigwa
rungu. Hapana shaka
hayo yalikuwa mateso
makubwa sana.
Suala ambalo linafaa
tujiulize hapa ni hili: Picha
hii inakhusiana nini na
Afrika Mashariki, kitendo
ambacho hakina ushahidi
wowote kuwa Mwarabu
wala Mswahili kafanya
Afrika Mashariki?
Kwa mtu yoyote
anayeelewa asili ya
picha hizi na anayeweza
kuitumia akili yake
kiuadilifu, hataacha kujua
kuwa hapa hapajatumika
uadilifu na uelezaji wa
kweli, bali zimetumika
siasa kali za udini
zinazotokana na Vita
vya Msalaba ili kuuficha
ukweli wa waliyoyafanya
Waafrika na Wazungu
Wakristo na kuwatupia
uchafu wao Waislamu.
Nawauliza tena,
kwanini ndugu Perazia
Kaloly, Ferix Kiruthu
na Cloudy Chatanda
wameyafanya haya na nani
waliowapa rukhsa hiyo ya
kutumia propaganda hizo
kuwasomeshea watoto
wetu shuleni?
Tuangalie sasa wapi
imetokea na hiyo picha
ya pili:
Je, kuna shaka yoyote ile
kuwa mchoraji wa picha
ya juu amenyakua fikra
hiyo ya kupigwa mnyonge
wa Kiafrika kutokana na
picha ya kamera ilioko
chini yake?
Katika picha hii ya
kamera, tunayemwona

Kuadhibu Watumwa

Picha hizi mbili zimechorwa kuonesha ukhabithi wa Waarabu Waislamu. Lakini


kweli picha hizi zinatokana na matokeo waliyoyafanya Waarabu? Au zote mbili
zimeibiwa kutoka kwingineko na za asili hazikhusiani na Waarabu?

Picha hii ya kushoto ya asili inakhusu ukhabithi uliofanywa Suriname, Amerika,


na Wazungu Wakristo 1773. Hii ya pili ya kulia imekopiwa ili kuzua (na kupiga
propaganda chafu kuwasingizia uovu) Waislamu Tanzania.

Picha ya kwanza ni ya kuchora inazua ukhabithi ati walioufanya Waarabu Tanzania,


kumbe ukweli ni kuwa inatokana na picha ya kamera inayoonesha ukhabithi
walioufanya Waafrika Kongo kwa amri ya watawala wa Kibiligiji.
ni Mwafrika ndiye
anayempiga mboko
Mwafrika mwenziwe, na
tokeo hilo limetendeka
Kongo chini ya utawala
wa wakoloni wa Kibiligiji

Wa z u n g u Wa k r i s t o .
Imeandikwa kwingi
na hadi kuna kanda za
filamu zinazoonesha na
kuzungumzia ukhabithi
wa Mfalme wa Wabiligiji,

Leopold II (1835-1909).
Mfalme huyu na
Wabiligiji walipoitawala
Kongo, waliwalazimisha
Wa a f r i k a k u wa f a n y i a
Inaendelea Uk. 8

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Propaganda za udini shuleni Tanzania-6

Inatoka Uk. 7
kazi kama ni watumwa
wa o n a wa n a h i s t o r i a
wanatuelezea kuwa
Wabiligiji waliwauwa
Waafrika wasiopungua
millioni kumi na
k u wa m a u wa j i h a y o
yanatambulikana kama ni
maafa makubwa. Mauwaji
ya k h a l a i k i ya wa t u
ambayo kwa Kiingereza
huitwa genocide.
Iangalie tena picha
ya asili ya kamera
iliyotangulia na utaona
kuwa Mwafrika aliyekuwa
kibaraka wa Kibiligiji,
ndiye aliyetumwa
kumpiga mboko mtumwa
wa Kiafrika. Mzungu
Mkristo haonekani
pichani, kwa hivyo
lawama kubwa anatupiwa
nokoa wa Kiafrika kwa
kutekeleza amri za
Mzungu za kumtendea
mtumwa ukhabithi.
Lakini picha ya kuchora
inaonesha kuwa khabithi
huyo mwenye kumtandika
mboko mtumwa wa
Kiafrika, ni Mwarabu
mwenyewe, ingawa hao
makhabithi wa Kiarabu
pia waliwatuma manokoa
wao kutekeleza amri zao.
Kwa hivyo, katika picha hii
tunapooneshwa moja kwa
moja kuwa ni Waarabu
Waislamu wenyewe ndio
waliowafanzia ukhabithi
watumwa wa Kiafrika,
lawama zetu zinawashukia
Waarabu Waislamu bila ya
kizuizi.
Kama nilivyoelezea,
picha hii ni ya kuchora, si
ya kamera kama ya chini
yake. Kwa hivyo inatokana
na fikra za mchoraji.
Je, unadhani mchoraji
hakukusudia mtazamaji
aone uchungu na ahisi
chuki juu ya Mwarabu
Mwislamu na hatimae
kuwachukia Waislamu
na Uislamu wenyewe?
Kila kitu kimepangwa na
wenye siasa kali za udini
na wachoraji wao. Hakuna
kilichochorwa kwa bahati
mbaya.
Picha na asili
zake tumeziona. Je,
wanapropaganda za
udini walidhani kuwa
k u l e k u g h u s h i k wa o
hakutatambuliwa?
Haisikitishi tu, bali
inaliza kuiona hali
ya masomo ya historia
iliyojaa chuki dhidi ya
Waislamu Tanzania ilivyo,
huku wanajua fika kuwa
Tanzania ina Waislamu

Katika maandishi
yao pia wametumia
propaganda kubwa kwa
mwenye kuelewa lugha
ilivyotumiwa. Kwa mfano,
katika sehemu waliyoiita
The psychological effect of
slavery on its victims yaani:
Athari ya kisaikolojia ya
utumwa kwa waathiriwa,
mna mengi yaliyokusudia
kuficha ukweli na kuleta

ya Kizungu. Kwa nini


hawakuainisha wazi kwa
kuandika Wazungu, au
anataka kuwaficha?
Ingekuwa waandishi
hao wana nia nzuri ya
kufundisha, wangelitumia
majina yanayofahamika
kwa wengi, na ikiwa kama
waandishi wameamua
kutumia majina ya
kiethonolojia kwa nini

Picha hii inaonesha Wabiligiji na watumwa wao ambao


wameshikishwa viganja vya watumwa waliokataa
kufanya kazi bure na kukatwa viganja hivyo kutiwa
adabu ili pia kuonesha mifano kwa wengine nini
watafanywa wakikataa kuwa watumwa wa Wabiligiji.

Wabiligiji waliwatia mpaka watoto wadogo wa


Kiafrika utumwani, Kongo.

Angalia na hii picha ya kuchora ya kerekecha inayoonesha


vipi Mfalme Leopold II wa Ubiligiji alivyowazonga na
kuwatia kabare Waafrika wa Kongo kama chatu.

Mwafrika kutiwa adabu na Wazungu amekatwa


kiganja.
wengi sana ambao
wameshaanza kuelewa
upotoshaji huo ulivyo.
Hii ni khatari kubwa
sana kwa usalama wa
nchi, na wa kulaumiwa
hawatakuwa wengineo, ila
ni wale waliojitosa katika
propaganda za siasa kali
za udini zinazotokana

na Vita Vya Msalaba na


kujitwika bendera ya vita
hivyo visivyowakhusu
ndewe wala sikio. Wakulaumiwa pia ni Serikali
ya Tanzania iliyozifumbia
macho propaganda hizo
na kuziachilia zisomeshwe
katika shule na kutia chuki
katika bongo za vijana.

chuki, wameandika
Perazia Kaloly na Ferix
Kiruthu yanayofuata:
The Arab slave traders
and the Caucasians slave
owners looked down upon
dark-skinned people.
Ta f s i r i : Wa f a n y a
biashara ya utumwa wa
Kiarabu na Wakaukasian
wamiliki wa watumwa
waliwadharau watu wenye
ngozi nyeusi.
Angalia ibara hio
ilivyoandikwa, kwanza
katajwa Mwarabu kwa
dhambi kubwa ya
k u f a n ya b i a s h a r a ya
utumwa, khalafu katajwa
Caucasian kwa dhambi
ndogo ya kumiliki.
Je, wewe unawafahamu
nani wamekusudiwa kwa
jina la Caucasian?
Hilo ni jina la
kiethonolijia ambalo
halifahamiki kwa wengi
isipokuwa wasomi. Walio
kusudiwa hapo ni wa jamii

basi wasitumie kwa


wote badala ya kuandika
wafanya biashara wa
Kiarabu wakaandika
wa f a n ya b i a s h a r a ya
utumwa wa Kisemiti.
Kwa nini waighushi
picha hiyo? Kwa nini
wachezee maneno? Au
kwa kuwataja Wazungu
ingelitambulikana kuwa
wao walikuwa pia ni
madhalimu wakubwa
na walikhusika katika
udhalimu huo.
Angalia picha zote
mbili na utafakari ibara
hiyo khalafu uhukumu
nini agenda ya Perazia
Kaloly na Ferix Kiruthu,
na historia itawakumbuka
kwa hayo.
Wa l i c h o k i f a n ya
wa a n d i s h i wa v i t a b u
vya historia Tanzania na
wachoraji wao ni kunyakua
picha zenye kuonesha
ukhabithi uliotendwa
Inaendelea Uk. 12

9
Na Bakari Mwakangwale
UKIFIKA wanakuambia
k a b i s a k u wa h a p a s i o
Mahabusu. Hapa sio
Gerezani wala hapa
sio Selo ya Polisi. Hii ni
Guantanamo.
Niliwaambia hata
mkiniuwa msidhani kwamba
mtakuwa mmefanikisha
lengo lenu. Sisi mnatukamata
si kwa kuiba, au tumefanya
ovu lolote huko uraiani, bali
mnatutuhumu kwa dhana tu,
labda mseme kosa ni imani
yetu na Uislamu wetu.
WAISLAMU waliokamatwa
kwa tuhuma za Ugaidi,
wa m e f i c h u a k u wa i p o
Guntanamo isiyo rasmi
n c h i n i wa n a y o i n g i z wa
watuhumiwa kuteswa kabla
ya kufikishwa Mahakamani.
Aidha, imedaiwa kuwa
Guantanamo hiyo ipo
chini ya kikosi maalumu
kinachojulikana kama Task
Force ambacho kinafanya
kazi nje ya utaratibu wa
kawaida wa kipolisi.
Hayo yamebainishwa na
mmoja wa watuhumiwa
hao, akiongea na An nuur,
a k i d a i k u wa Wa i s l a m u
wanafanyiwa dhulma kubwa
wa n a p o k u wa m i k o n o n i
m wa wa t u h a o a m b a o
wanajiita Task Force na
kwamba unaweza usiamini
ukielezwa unachofanyiwa
pindi wanapokuhoji watu
hao.
A l i p o u l i z wa k wa n i n i
analeta mfano wa
Guantanamo, alieleza kuwa
ni maafande hao, wanaoitaja
sehemu hiyo kwa jina hilo
mbele ya watuhumiwa, tena
kwa majigambo na kwamba
sehemu hiyo ipo maeneo
ya Mikocheni, Jijini Dar es
Salaam, na wanaeleza wazi
kuwa hapo sio Polisi.
Hili neno ni wao
wanalitamka mbele
yetu, wanapaita hapo ni
Guantanamo, na ukifika
wanakuambia kabisa kuwa
hapa sio Mahabusu, hapa sio
Gerezani wala hapa sio Selo
ya Polisi, bali wanasema hii
ni Guantanamo ya Serikali.
Alisema Muislamu huyo.
Alisema, kabla ya
kukamatwa na aliposikia
madai ya Masheikh
waliofanyiwa vitendo vya
kinyama, ilikuwa ni vigumu
kuamini kama kweli kuna
askari ndani ya Tanzania hii
wanaweza kufanya mambo
hayo.
Lakini anasema, baada ya
kuwa mikononi mwa watu
hao, na mwenendo wao
wa kuwahoji na kuwatesa
watuhumiwa wa ugaidi,
alibaini kuwa hawashindwi
kukufanyia unyama wa aina
yoyote.
Guantanamo
ni
Mahabusu/gereza, lililopo
Marekani, ambalo Taifa
hilo hulitumia kuwahifadhi
watuhumiwa wa ugaidi
kutoka nchi mbalimbali
kabla ya kuchukuliwa hatua
za kisheria.
Alisema, kuwa katika

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Guantanamo Dar es Salaam!!!

Aljazeera Ukerewe yazima uzushi wa Jihad John


Alikeni Polisi Msikitini waone ghala la mabomu!
Mwenzao alisilimu baada ya kutesa Guantanamo
OCD Nansio ajionea. Sasa ahimiza Doria ya Nafsi

majumba hayo (Guantanamo)


kuna watu wapatao tisa
mpaka 12, ambao alidai kuwa
ni Maafisa wa Polisi na wale
wa Usalama, na kwamba hiyo
ni timu maalum inayojiita
Task Force.
A l i s e m a , u k i i n g i z wa
humo, unawekwa mbele yao
kisha wanakuuliza maswala
mbalimbali kila mmoja swali
lake kuhusiana na wewe
binafsi pamoja na masuala

ya Waislamu na Uislamu kwa


ujumla.
Muislamu huyo,
a l i ye m we n ye j i wa n j e
ya Jiji la Dar es Salaam,
aliyeshikiliwa kwa muda
wa siku 20, akiwa mikononi
mwa Task Force kabla ya
kufikishwa Mahakamani,
alibainisha kuwa, Waislamu
wanaokamatwa ndani na nje
ya Jiji wengi wao hufikishwa
k wa n z a M a k a o M a k u u

ya Jeshi la Polisi Jijini Dar


es Salaam (Central) kisha
hupelekwa Mikocheni
(Guantamano).
Alisema, jamaa hao
wanauliza maswali ambayo
wanajua kabisa kuwa huna
majibu, lakini wanataka wewe
uwajibu vile wanavyotaka
wao jambo ambalo mwisho
wa siku watakuingiza katika
kipigo tu.
Kama ukiwaambia hujui

Kwenu yaweza kuwa


kosa mimi kulisilimu
Lakini mimi Terry Holdbrooks sio msaliti
Ni aibu kuwa na kitu kama Guantanamo

Terry Holdbrooks Jr., ni


mmoja wa Polisi Jeshi (MP)
(Military Police), waliokuwa
wakiwalinda, kuwatesa na
k u wa h o j i wa t u h u m i wa
wa ugaidi kule Kambi ya
Guantanamo (Camp Delta,
JTF Guantanamo Bay).
Akiwa amefanya kazi hiyo
mwaka 2003 na 2004.
Ilikuwa ni katika usiku
mmoja wa mwezi Desemba
2003 ambapo Terry anasema
alikuwa tayari kuwa
M u i s l a m u k wa k u s o m a
maneno yaliyoandikwa kwa
Kiingereza, yakisomeka:
There is no god but
God, and Muhammad is the
messenger of God.
Anasema, aliandikiwa
maneno hayo katika karatasi
ngumu na mfungwa mmoja
yakiwa yametafsiriwa kutoka
lugha ya Kiarabu kwa sabbu
i l i k u wa v i g u m u k wa k e
wakati huo kuyasema kwa
Kiarabu.
Anasimulia Kay Campbell
kuwa Terry alisilimu baada
ya kuusoma Uislamu kwa
wafungwa wa Guantanamo,
Uislamu ambao awali
aliambiwa ni dini ya vurugu
na maangamizi, lakini
akakuta kumbe ndiyo dini
yenye nidhamu na amani
aliyokuwa akiitafuta katika
maisha yake.
Akisimulia safari ya Terry
kusilimu, mwandishi Kay

Campbell anasema kuwa


kijana Terry Holdbrooks
wakati huo akiwa na umri wa
miaka 29 alikuwa mmoja wa
vijana wengi wa Kimarekani
waliojiunga na jeshi baada
ya Septemba 11, wakiwa na
hasira ya kwenda kupambana
n a Wa i s l a m u b a a d a ya
kupigwa propaganda kuwa
Waislamu ndio waliolipua
majengo pacha ya World
Trade Centre (WTC) na
kuuwa zaidi ya Wamarekani
4000 wasio na hatia.
Holdbrooks walked into
an Army recruiters office in
Arizona a year after 9/11 saying
he wanted to join the Army,
go kill people and get paid for
it (then he) signed up for
military police because it offered
a bonus.
Anasimulia mwandishi
Campbell akimaanisha
kuwa Terry aliingia jeshini
katika kikosi cha MP mwaka
mmoja baada ya Septemba
11 akiwa na shauku ya
kuwa muuwaji wa kulipwa,
akikusudia kuuwa Waislamu
waliohusika na Septemba 11.
Anasema kuwa kabla ya
kupelekwa Guantanamo,
walipigwa darasa na
Kamanda wao wakiambiwa
kuwa wanakwenda kukutana
na magaidi hatari sana,
magaidi wa kimataifa na
h i v y o wa we m a k i n i n a
wasiwe na chembe ya huruma

juu yao.
Remember what Muslims
did to us. Remember who youre
protecting.
Anasema Terry, kuwa hayo
yalikuwa maneno ambayo
kamanda wao aliyekuwa na
cheo cha sergeant alikuwa
akiyarudia mara kwa mara
kama kuwakumbusha kuwa
wanakwenda kukabiliana na
watu waliouwa Wamarekani
4000 katika September 11 na
hivyo hawastahiki kuonewa
hata chembe ya huruma kwa
sababu ni magaidi katili.
So Holdbrooks arrived at
the hot, seared base expecting
hulking killers in every cell.
Anasimulia Campbell.
H a t a h i v y o Te r r y
anasema, alipofika huko na
kila masiku yalivyokuwa
yakienda, alikuja kuona
kuwa aliyokuwa ameambiwa
na makamanda wake na hali
halisi, ni mambo mawili
tofauti kabisa. Ni kama
mbingu na ardhi.
Akitaraji kukutana na
mijitu iliyobobea katika
medani ya kijeshi na kivita,
alisema alikuja kukuta
k u wa wa t u a l i o k u t a n a
nao walikuwa madaktari,
walimu wa skuli na madrasa,
wakulima na wafanya
biashara, maimamu wa
Misikiti, madereva wa tax
(tax drivers) na maprofesa wa

Inaendelea Uk. 10

wanachokuuliza, utasikia
wanasema mpeleke gereji,
huko ndio kuna mateso
m a k u b wa , h u m o g e r e j i
moja ya zana wanayoitumia
k u wa a d h i b u Wa i s l a m u
(watuhumiwa) ni mipini ya
majembe, sio bakora, wala
hupigwi kwa makofi, ni hiyo
mipini na vifaa vingine vizito
ndivyo vinavyotumika.
Kuna watu wa miraba
minne wanafanya shughuli
hiyo, na anapoanza
kukuadhibu anachojoa shati,
anapiga miguuni katika
nyayo, mgogoni mpaka
anatoka jasho kwa kupiga
mwanadamu mwenzake.
Amesema Muislamu huyo.
Alisema, kwa kawaida
ukitoka Sentro, kwenda
Guantanamo, unatoka ukiwa
u n a t e m b e a m we n ye we ,
lakini ukirudi jioni kutoka
huko unaitafutia miguu
pa kukanyaga, kutokana
na kuvimba na wakifika
hapo Polisi, wanakutupa tu
kama mnyama hamna cha
matibabu wala huduma ya
kwanza.
Alisema, mara nyingi
walipokuwa wakirudishwa
Sentro katika hali hiyo
ya maumivu, alikuwa
akiwafariji wenzake kwa
kuwapa mawaidha na
kuwajenga kiimani kutokana
na hali mbaya wanayorudi
nayo kutoka Mikocheni,
jambo ambalo lilisababishwa
kuhamishwa selo na
kupelekwa kituo kingine
cha Polisi.
Anasema, awali akiwa
Guantanamo alipigwa sana
na watu hao wanaojiita Task
Force lakini wakashangaa
hakuwa analia wala kupiga
kelele, jambo ambalo
liliwashangaza na kudai
kuwa yeye ni sugu.
Hata hivyo alidai kuwa
aliwajibu kwamba, wasidhani
n j i a h i y o wa n a y o t u m i a
ya kuwatesa Waislamu ni
kuwakomoa.
Niliwaambia hata
mkiniuwa msidhani kwamba
mtakuwa mmefanikisha
lengo lenu, kama mnadhana
hivyo, muelewe kuwa kwa
Muislamu haiko hivyo,
sisi mnatukamata si kwa
kuiba, au tumefanya ovu
lolote huko uraiani, bali
mnatutuhumu kwa dhana tu,
labda mseme kosa ni imani
yetu na Uislamu wetu.
Najua nipo hapa kwa
ajili ya Uislamu wangu,
kwa hiyo napata faraja
kila mnalonifanyia. Mimi
na Waislamu wenzangu,
kwetu ni kheri zaidi kuliko
mnavyodhania, zaidi
mnatuzidishia imani.
Alisema akirejea kauli yake
mbele ya Task Force.
Alisema, kufuatia kauli
yake hiyo, kuna afande
aliunga mkono, akisema
anachosema huyo Ustadhi
ni sahihi, akiwafafanulia
msimamo wa Waislamu wa
Libya na Palestina, ambaye
alidai amejifunza kutoka
kwao alipokuwa masomoni

Inaendelea Uk. 11

10
Inatoka Uk. 9

vyuo vikuu, huko watokako.


Katika hao wanaodaiwa kuwa
magaidi hatari, Terry anasema
alikuwepo mtoto wa miaka 12 na
mzee wa miaka zaidi ya 70 aliyekaribia
kukata roho kwa maradhi ya TB
(tuberculosis) iliyokuwa imefikia
kilele kwa kukosa tiba stahiki.
Hali hiyo ilimchanganya MP Terry
ambaye alikuwa kazi yake ni kuwatoa
wafungwa kutoka katika sero zao
na kuwapeleka katika vyumba
vya mahojiano na kuwarejesha.
Aidha alikuwa pia katika zamu ya
kuwalinda usiku na mchana.
Kilichomshanganza zaidi anasema,
watu hao hawakuonekana kuwa na
fadhaa wala kukata tamaa, bali wenye
moyo, ucheshi, furaha na nidhamu ya
kuchunga muda wa swala.
The detainees read their Qurans.
They kept the daily schedule of prayers.
They remained undiscouraged under
horrendous pressure.
Mtu anakuwaje mahali pa mateso
kama hapa Guantanamo lakini abdo
unamuona anatabasamu?
Ni moja ya maswali yaliyokuwa
yakimsumbua MP Terry alivyokuwa
akiwaona wafungwa wake Waislamu
walivyokuwa na mioyo ya kutokukata
tamaa, wakiwa wenye furaha na
tabasamu kila akiongea nao.
Unakuwaje mahali pa mateso
kama hapa, halafu bado unaamini
kuwa kuna Mungu anayekujali,
wakati anakuacha unateseka hapa
Guantanamo?
N i s wa l i j i n g i n e l i l i l o k u wa
l i k i m s u m b u a Te r r y a k i wa o n a
Waislamu wale kila ikifika muda wa
swala utawakuta wanatawadha na
kuswali. Nidhamu waliyokuwa nayo
katika ibada zao na kudumu katika
kusoma Quran.
Hili ni jambo jingine
lilimchanganya MP Terry. Akawa
karibu nao na kuwa akiongea nao
mara kwa mara kujua walikotoka na
maisha yao yalivyokuwa. Ni kupitia
mazungumzo hayo, alikuja kuwajua
kuwa wengi wao ni baba na waume
wema katika familia zao, wasomi,
lakini pia raia wema na wafanyakazi
wasio kuwa na matatizo walikotoka,
halikadhalika wanaolaani tukio
la September 11 na kusema kuwa
waliofanya uharamia na ugaidi ule
ni watu katili, shambulio ambalo
halikubaliki kabisa katika Uislamu.
Unapowasikiliza watu hawa
na kutizama mienendo yao, kutwa
nzima, you start thinking, Was I lied
to?
Anasema Holdbrooks kwamba
lazima itakujia kuwa ulidanganywa
kuwa unakwenda kukutana na majitu
magaidi katili.
Hali hiyo ilimpa hamu Terry ya
kusoma juu ya Uislamu kupitia
internet na kisha kupata hamu
ya kujua nini kipo katika Qurna
ambapo alipewa Quran ya tafsiri ya
Kiingereza ambayo alitumia muda
wa siku tatu tu kuisoma yote.
It took Holdbrooks three nights to
read it. As a restless seeker in his teens,
he had studied Christianity, Buddhism,
Judaism, and never saw much sense in
them. In the Quran, for the first time,

Makala

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Kosa kulisilimu?

Terry Holdbrooks Jr.

WAANDAMANAJI wakimchagiza Rais Barack Obama kuifunga


Guantanamo.
he found a religious text that meets his
logical criteria.
Ndivyo anavyosimulia mwandishi
Kelly kuwa kwa mara ya kwanza
Terry alikuwa ameona ndani ya
Quran mafundisho yenye mantiki
na yanayoingia akilini tofauti na
aliyokuwa akisoma katika Ukristo,
Ubudha na Uyahudi.
It made sense from beginning to
end. It doesnt contradict itself. Theres
no magic. Its just a simple instruction
manual for living.
N d i v y o a n a v y o e l e z a Te r r y
Holdbrooks mwenyewe kuwa ndani
ya Quran ni vitu vyenye mantiki

AN-NUUR

mwanzo mwisho, wala hukutani


na vitu vyenye kujikoroga. Hakuna
uchawi na mkanganyiko, bali ni
maelekezo mepesi ya kueleweka juu
ya maisha.
Hata hivyo, mambo hayakuwa
m e p e s i k w a Te r r y b a a d a y a
kusilimu. Alikuja kufukuzwa jeshini
ikidaiwa kuwa kachanganyikiwa.
Mkewe naye akamkimbia. Alifikia
kupachikwa tuhuma ya usaliti
jambo lililompelekea kuandika kitabu
alichokipa jina Traitor?, chenye
kurasa 164.
I may have become a Muslim, but I
am not a traitor.

Anasema Terry katika kitabu hicho


kinachopatikana online kupitia www.
GtmoBook.com.
Kwamba anaweza kushutumiwa
kwa kusilimu kwake, lakini labda
kwa wengine huko kusilimu ndio
kosa, lakini yeye sio msaliti wa
Marekani.
Kinyume chake anasema, ni aibu
kwa taifa linalojinadi kwa ustaarabu
kama Marekani kuwa na kambi ya
mateso Guantanamo. Anasema hapo
ni mahali panapofanyika mambo
ambayo hutarajii afanyiwe hata
mnyama, ndio maana inafikia mahali
hata wafungwa pamoja na ustaarabu
wao wanafikia mahali pa kugoma
kula. Anataja kisa cha wafungwa 102
ambao waligoma kula kwa zaidi ya
siku 100.
I tell this story and I wrote the book
so idiot-simple that anyone could read
and understand that the existence of
Guantanamo is something to be ashamed
ofI just want to share information with
people in depth and then let them make
up their mind.
Anasema Holdbrooks
akitukumbusha kuwa wakati sisi
tunajinadi kuwa tuna Guantanamo
zetu huku, tujue kuwa huko kwa
walimu na wakufunzi wetu, serikali
inachagizwa kuifunga kwa sababu
ni jambo la aibu, ushenzi, fedheha na
ukosefu wa utu.
Watu wengi wenye heshma zao
katika jamii na kimataifa, wakiwemo
wasomi, wanasheria, wapigania haki
za binadamu, wanasiasa, watu wa
dini, wameandika vitabu, makala na
kufanya mihadhara kumtanabahisha
Rais Barack Obama kuifunga
Guantanamo kwa sababu ni jambo
la kifedhuli, aibu, ushenzi lisilofaa
kufanywa na watu wastaarabu.
Akizungumzia hali ya Waislamu
hivi sasa ulimwenguni, Terry ametoa
wito kwa Waislamu wasiufanye
Uislamu kuwa kama biashara ya
bangi.
You cant be afraid to be a Muslim
in public. Tell your neighbors youre
Muslim. Invite them into your home.
Invite them to visit the masjid to see our
secret bomb factories. If its time to pray
pray. The whole world is an acceptable
place to pray.
Kwamba, Waislamu wasiogope
kuweka Uislamu wao hadharani.
Kama ni majirani zako wajue kuwa
wewe ni Muislamu (na wanufaike na
wema wa jirani Muislamu). Waalike
nyumbani kwako. Waalikeni wasio
kuwa Waislamu Msikitini waone
(ili kukomesha propaganda kuwa
kuna) viwanda vya mabomu ya
kufanyia ugaidi. Ukifika wakati wa
swala, swali. Ardhi yote ni mahali
pa kuswalia.
Akitoa wito rasmi kwa Waislamu
wa Marekani, Terry anasema kuwa
anataka lau anakuja Mtume (s.a.w)
leo, basi akute Waislamu bora kabisa
wapo Marekani.
Kwa hivyo wajitahidi kwa kusoma
na kuwa watu wenye kufanyiana
wema miongoni mwao na kwa
walimwengu, kuanzia ndani ya
Marekani na nje. Kwamba Waislamu
wa Marekani wana wajibu wa kufuta
picha mbaya ambayo inajipaka nchi
yao hivi sasa kwamba ni taifa la
kibabe na mauwaji dunia nzima tena
kwa watu wasio na hatia.

11

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Mafundisho ya Quran

Fethullah-Gulen
NA wape habari njema
wale ambao wameamini
na wakatenda matendo
mema kwamba wana wao
mabustani inapita ndani
yake mito kila wanapopewa
humo katika matunda
chakula wanasema: Hiki
ndicho tulichopewa huko
nyuma na wanakiletewa
hali ya kuwa kinafanana na
wana wao humo wake walio
takaswa na wao humo ni
wenye kuishi mielele. [AlBararah 25]

Hakika aya hii Na


wanakiletewa hali ya
kufanana, inaashiria
kwenye kufanana, katika
mtizamo wa kupata neema,
na uwezesho kutoka kwa
Mwenyezi Mungu.
Kufuatana na ufananizaji
wa Al-Ustadh Saeed A-Nursi,
neema hizi zenye kufanana
huenda zikawa ni katika
m i s a a d a ya M w e n y e z i
Mungu ya hapa duniani au
ni katika misaada ya akhera.
Kwa mfano: Mtu anamsifu
Mwenyezi Mungu hapa
duniani, maana anasema:
Al-Hamdulillah anazikuta
sifa hizo zinatengeneza
tunda huko akhera- maana
kila takbira na kila tasbihi
na kila tahlili hapa, iko
katika nafasi ya kokwa na
mbegu zilizotawanywa na
zilizopandwa katika udongo,
zinazaa neema mbalimbali
huko peponi.
I s i p o k u wa k u n a p a s a
kuashiria kuonyesha kitu
muhimu sana katika jambo
hili, nalo ni kwamba sisi
hatuelewi uhusiano kati ya
haya mambo mawili kwa

Inatoka Uk. 9
katika nchi hizo kwa nyakati tofauti
kuwa Muislamu wa kweli hana
anachopoteza dhidi ya imani yake.
Akielezea aliyohojiwa, alisema
zaidi ilikuwa ni kuhusiana na harakati
zake kwa kujishughulisha katika
masuala ya Waislamu na Uislamu
akihutubia mara kwa mara kuwa
wanaonewa na kudhulumiwa.
Walinieleza kuwa naonekana
kila sehemu katika mikusanyiko
ya Waislamu na katika Misikiti
mbalimbali katika mikoa mbalimbali,
sasa wakataka kujua mimi ni dhehebu
gani, uwezo wa kuwepo huko kote na
upata wapi.
Niliwajibu kuwa uwezo wangu
unatokana na michango ya Waislamu
ndiyo inanifanya niwepo kila
mahali.Alisema.
Alisema, amebaini kuwa
Serikali haipendi kuona viongozi
wanaokubalika kwa Waislamu, hasa
wale ambao wanawaunganisha
Waislamu wawe kitu kimoja katika
jamii.
Akasema, hao ndio huandamwa
kwa kutafutiwa tuhuma zisizo za
kweli na ukitoka inakuwa bahati yako
na sio tatizo kwao kukuzuia kama
unavyoona hali ilivyo kwa Masheikh
wa UAMSHO na wengine.
Alisema, akiwa huko, pia aliulizwa
kuhusu Sheikh Hudhaifa, kwamba
anamfahamu vipi akadai, aliwajibu
kwa kuwaeleza kuwa huyo alikuwa
ni kiongozi wa Taasisi ya Kiislamu
lakini pia alikuwa mwalimu wake.
Lakini pia wakaniluliza
namfahamu vipi Sheikh Qassim
Mafuta, nikawaambia namjua kwa
sababu tumesoma chuo kimoja,
wakaniuliza vipi mawaidha yake,
nikawaambia kwa mazingira ya
sasa kwa Waislamu na Uislamu,
mawaidha yake hayana lengo la
kumtoa Muislamu katika dhulma
inayotukabili hivi sasa Waislamu.

ujuzi uliyokamilika.
Kwa hakika ni kwamba
sisi tunakitazama kila kitu
katika ujumla wake na kwa
sababu hiyo, tutabakia ndani
ya mipaka ya taathira na
makusudiwa yake wakati
wa kusimama kwetu na
uchambuzi na uundaji wa
kifikra. Ila kuna mambo

mengi sana yanayozuka


katika ulimwengu wa
sababu hizi kwa sifa ya
kwamba zinasimama kwa
kuudhihirisha uhakika huu
ambao unatajwa na aya hii
mbele ya macho yetu kwa
nguvu zote.
Kwa mfano hajasimamapo
mtu yeyote kuvuna shairi

Guantanamo Dar es Salaam!!!


Alisema.
Alidai, aliulizwa pia juu ya
M a s h e i k h wa n a o h u b i r i k u wa
kusoma ni ukafiri na kuwaghilibu

watoto wa Kiislamu kuacha shule


na vyuo ambapo aliwajibu kuwa
lengo la mawaidha ya watu hao ni
kutaka kuwaacha Waislamu katika

MMOJA wa watuhumiwa akionesha kovu alilolipata akiwa mikononi


mwa polisi kutokana na mateso ya maafande hao kabla ya kufikishwa
mahakamani.

katika shamba ambalo


alipanda ngano pamoja na
kuwa shairi na ngano ni
katika jinsi moja. Na hatuvuni
peasi kutoka katika mti wa
tufaa wala tini kutoka katika
mti wa zabibu.
Alikuwa Mtume (s.a.w.)
unamjia wahyi anayafahamu
yale anayoyasema Jibril (A.S.),
hawakuwa wale waliyokuwa
karibu yake wanasikia kitu
chochote hata kitu kidogo
kilicho kama kelele za nyuki.
Ni hivyo hivyo kushuka
k wa M we n ye z i M u n g u
mtukufu katika thuluthi ya
mwisho ya usiku kwenye
mbingu ya dunia na mamia
ya mambo mbalimbali. Jee,
tunaweza kusema kwamba
sisi tunafahamu, mfano wa
mambo haya katika fremu ya
sababu na matokeo?
Ni kama alivyosema
Al-Imamu Al-Ghazali:
Kwa hakika sisi hatuwezi
kufahamu kwa akili zetu
z a k i d u n i a m a a n a k wa
akili za kimaisha, maana
k wa a k i l i z e t u a m b a z o
tunazitumia katika maisha
yetu, mfano wa mambo
haya yenye kufungamana
na akhera, tukayafahamu
vizuri, isipokuwa wakati
tutakapoandaliwa huko
Inaendelea Uk. 13

matatizo na kuendeleza mgawanyiko


miongoni mwa Waislamu kutokana
na maudhui ya mawaidha yaliyo na
lengo la kutaka kuwafanya Waislamu
waendelee kuwa wajinga.
Akasema, alifafanua kwamba
mausatadhi hao ndio mfano wa
Masheikh ambao wanaowataka
Waislamu wasisome elimu nyingine
zaidi ya dini, na wanawataka
Waislamu wasishiriki katika harakati
za kijamii na kisiasa wala wasipige
kura.
Alidai, katika kujibu na kueleza
kuwa masheikh wanaohubiri imani
za ki-Boko Haram (kuwa kusoma ni
ukafiri), hawafai na ni wapotoshaji wa
Uislamu, alishushiwa kipigo, jambo
ambalo lilimfanya ajiulize maswali
mengi.
Hata hivyo, alidai kuwa kwa sasa
ana hakika kuwa hizi kampeni za
kuwataka Waislamu wasisome na
wasijihusishe na siasa na mambo
mbalimbali ya kijamii, ni mpango
maalumu wa maadui wa Uislamu
na Masheikh waliobeba agenda
hiyo wana kazi maalum dhidi ya
Waislamu.
Katika masiku ya hivi
karibuni, Masheikh na Waislamu
wanaoshikiliwa kwa tuhuma za
Ugaidi, walitoa malalamiko ya
kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji
wakiwa mikononi mwa vyombo vya
dola.
Wa i s l a m u h a o , w a m e t o a
malalamiko hayo, mbele ya
Mahakama ya Kisutu, wakidai
kuwa walihojiwa wakiwa uchi kama
walivyozaliwa, kuingiliwa kinyume
cha maumbile, kushindiliwa vitu
vigumu sehemu ya haja kubwa.
Je, huu ndio utaratibu wa
upelelezi mnaowafanyia ndugu zetu
huku bara? Au huwa wanafanyiwa
Waislamu tu.
Alilalamika Sheikh Farid, wakati
akitoa malalamiko yao juu ya unyama
waliofanyiwa kabla ya kupelekwa
gerezani.

12

MASHAIRI/MAKALA

MTUKUFU RAMADHANI
Kwa jina lako Rahimu,naanza kusimuliya
Mola wetu Mkarimu,Ya Rabi nijaaliya
Nikadiri kukhitimu, haya nalokusudiya
Niusifu mwezi mwema,mtukufu Ramadhani
Rabi peleka salamu, zende kwa wetu Nabiya
Mtume wetu Adhimu, Muhamadi Hashimiya
Na Swahaba Akiramu, na Isilamu jamiya
Niusifu mwezi mwema, mtukufu Ramadhani
Ya Rabi tupe mwafaka, tufunge bila udhiya
Saumu yenye Baraka, kwako twaitaradhiya
Tuifunge huno mwaka, na mwakani kwa afiya
Tuufunge mwezi mwema, mtukufu Ramadhani
Karibu wetu mgeni, kwa hamu twakungojeya
Ulotukuka yakini, nuru ulivyo eneya
Mtukufu Ramadhani, karibu twakupokeya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Mtakatifu adhimu, sote twakukongoweya
Mwezi uliye muhimu, Mola metutunukiya
Twafurahi Isilamu, kila pembe ya duniya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Mtukufu mwezi mwema, wa sisi kunyenyekeya
Mwenye kuyatenda mema, bila ya kufanya riya
Tamswamehe Karima, madhambi kumfutiya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Mwezi wa nyingi faida, metukuzwa na Jaliya
Mwezi mwema wa Ibada, na imani kutungiya
Huondoka zote shida, nafusi zikatuliya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Mwezi huno wa maana, ameusifu Nabiya
Ni bora wajulikana, kwa kheri nyingi kungiya
Mwezi wa neema sana, baraka hutushukiya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Mwezi mwema wa swiyamu, wa mema kujichumiya
Milango ya Jahanamu, Rahimu huifungiya
Na ya Janatu Naimu, wazi hutufunguliya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Ni mwezi wa Quraani, mwanzo kuteremkiya
Alipokuja pangoni, Jibirili kwa Nabiya
Ilikiuwa Ramadhan, wahayi alipokeya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Mashetani makafiri, wawi wa kuharibiya
Hawawezi kuathiri, wasiwasi kututiya
Huwafungia Qahari, mbali wakatokomeya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Imo Lelatil Qadri, usiku huo kungiya
Bora sana mashuhuri, kuliko elifu moya
Miezi inayo jiri, ya taqwimu Hijiriya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Na hushuka Malaika, mbinguni wakatokeya
Kwa amri ya Rabuka, duniyani kufikiya
Amani hunawirika, hadi swabahi kungiya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Usiku mwema kipita, wakati huo kungiya
Na ukija kukukuta, Ibadani umengiya
Hakika utaipata, Rehema yake Jaliya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Haya basi Isilamu, mgeni ashaingiya
Natutimize saumu, tuifungeni kwa niya
Swala zote tuzikimu, za suna na faridhiya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Mashekhe na masharifu, wahimizeni jamiya
Hima tufungeni safu, Tarawehe kuqimiya
Tumlekee Raufu, kwa kuomba na kuliya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Darasani tuhimize, wenzetu kuhudhuriya
Kwa wakati tufulize, misikitini kungiya
Mawaidha tusikize, atatujazi Jaliya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Haya shime muombeni, Mola kumnyenyekeya
Quraani isomeni, kila siku juzu moya
Mukiweza ongezeni, muzidi kukaririya
Kongo mwezi wetu mwema, mtukufu Ramadhani
Na akhiri nimefika, beti nalokusudiya
Chache naloziandika, tosha kumi na tisiya
Namshukuru Rabuka, shairi limetimiya
La kuswifu mwezi mwema, mtukufu Ramadhani
Amina Rabi Dayani, Dua yetu kubaliya
Ya Ilahi tuauni, tuepushe na udhiya
Tuifunge Ramadhani, kwa furaha na afiya
Twaomba yake neema, mtukufu Ramadhani
SWALEH SUHEIL ABEID

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Propaganda za udini shuleni Tanzania-6

Inatoka Uk. 10
na Wazungu Wakristo

na vibaraka wao wa
Kiafrika na kuwatupia
lawama Waarabu na
Waswahili Waislamu.
Hakuna shaka yoyote
kuwa uelekezaji wa
makombora yao wenye
siasa kali za udini
kuwalenga Waswahili
na Waarabu, ambao
ni Waislamu, kuwa
kumefanywa kwa
makusudi. Lengo hili
la kipropaganda za
siasa chafu za udini,
linakwenda vipi na
siasa rasmi za Tanzania
zinazojigamba kila leo
kuwa Tanzania haina
dini?
Haiwezekani
Serikali ya Tanzania
iachilie mambo haya
yasomeshwe katika
shule za Tanzania, ila
pawe na watu wenye
nguvu kubwa ya
kuilazimisha Serikali
kuwaachilia waendelee
kuyasomesha hayo ya
kipropaganda yenye
khatari kubwa kwa
nchi nzima ya Tanzania
katika siku za usoni.
La muhimu kabisa
ni kupigwa marufuku
usomeshaji wa
propaganda za aina
hii na vitabu vyote
vichomwe moto leo
kabla ya kesho.
Kusema tungoje
mpaka tuchapishe
vingine venye kuelezea
ukweli kamili, ni
kuendeleza usomeshaji
wa kipropaganda na
dhulma kubwa katika
nchi inayojinata kuwa
inaziheshimu dini zote
kisawasawa na haina
mapendeleo.
Wasiyoyazungumzia
wenye
siasa kali za udini
Tanzania
Maudhui haya ya
utumwa na biashara
yake, khasa kukhusiana
na Zanzibar, si mambo ya
kuyafanyia maskhara.
Kwa nini? Kwa sababu
ni moja katika jambo
lililotumiliwa vibaya
sana: Kwanza, na
Wamishinari na wafuasi
wao katika kuupiga
vita Uislamu katika
Afrika Mashariki.
Pili, kama tulivyotaja
kabla, wanasiasa fulani
Waislamu Zanzibar, pia

Askari watumishi wa Wabiligiji, Kongo akiwalinda


watumwa wa kike (wakiwa wameachwa uchi wa
mnyama).

waliyatumilia vibaya
sana katika majukwaa ya
siasa na kuwanyooshea
vidole Waarabu peke
yao kama kwamba ni
Waarabu peke yao ndio
walioyafanya maovu
yote ya utumwa.
Zilikuwa ni siasa za
chuki zilizopindukia
m i p a k a . H a t i m a ye ,
tumeshuhudia
namna roho za watu
zilivyoangamizwa 1961
na kwa wingi zaidi 1964
na kuendelea.
Ni wajibu wetu
tuzinduane ili tuelewe
vizuri matokeo
yaliyowafikisha
Wa z a n z i b a r i h a p a
wa l i p o . I n a f a a p i a
tusomee zaidi ukweli
u l i v y o wa t a a r i k h i
inayokhusiana na
biashara ovu ya
utumwa ili kuelewa
yasiyokuwa ya kweli
wanayoyakhubiri na
k u ya a n d i k a we n ye
lengo la siasa kali za
udini zisizokhusiana
na mafunzo ya Yesu.
(Hawa wenye) lengo
la siasa zenye kutaka
kuwapiga vita Waislamu
na kuwakhasamisha
na Wakristo katika
Afrika Mashariki na
kwingineko. Na katika
hawa wamo pia wale
Waislamu wenye kupiga
debe bila ya kuujua
mchezo unaochezwa.
Au Wanajua, lakini
wanaona kuwa ni siasa

zenye natija kwao.


We n ye s i a s a k a l i
za udini hawaelezi
chochote kukhusu
maovu waliyoyafanya
baadhi ya Wazungu
Wakristo. Huwaoni
kuzungumzia ya
Waafrika 10,000,000
(milioni kumi)
waliouliwa Kongo na
Wabiligiji wakisaidiwa
na askari wa Kiafrika. Na
(hawazungumzii pia)
mamilioni waliotiwa
utumwani kufanya kazi
mashambani, lakini
wakati huo huo hujaribu
kuchora picha mbovu
sana juu ya Waislamu
na kuwasingizia
hata yale waliokuwa
hawakuyatenda
Waislamu na kuficha
mazuri waliyoyafanya.
Angalia baadhi ya picha
za utumwa uliofanywa
Kongo ambako
ukhabithi mkubwa sana
ulitendwa:
Fungua mwenyewe
mtandao uandike kwa
mfano Congo Slavery
na utastaajabu kuona
makala yalivyokuwa
mengi kukhusu
utumwa huko Kongo
ilipotawaliwa na
Wa b e l i g i j i . K a t i k a
Yo u t u b e p i a
kumejaa maelezo
ya filamu kukhusu
unyama uliofanywa na
Wabeligiji.

13

MAKALA

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

'Vunjajungu' na hatma ya funga zetu (1)


Na Abuu Nyamkomogi

'VUNJAJUNGU', kama
dhana na kwa maana
ninayoikusudia katika
makala haya, ni istilahi
isiyo rasmi inayotokana na
maneno rasmi mawili ya
lugha yetu adhimu na aushi
ya Kiswahili ambayo ni
'vunja' na 'jungu'. Maneno
ambayo yamehulutishwa
a u k u a m b a t i s h wa a m a
kujumuishwa pamoja na
hatimaye kuzalisha istilahi
h i y o i s i y o r a s m i , k wa
muktadha wa makala haya,
ambayo ni 'Vunjajungu'.
Aghalabu matumizi ya
istilahi hii hushika kasi zaidi
katika kipindi hiki cha mwezi
wa nane ujulikanao kwa jina
la Shaaban kwa mujibu wa
Kalenda ya Kiislaamu. Kwa
maneno mengine, istilahi hii
hutamkwa na husikika zaidi
katika mwezi huu kuliko
mwezi mwingine wowote
katika mwaka kupitia
matangazo yarushwayo
na vyombo vya habari vya
umma na vya watu binafsi
na katika mazungumzo
ya kawaida ya baadhi ya
wanajamii.
Ni nadra kusikia neno
hili likitumika au kutumiwa
katika miezi mingine ya
mwaka kama vile Muharram,
Swafar, Rajab, Ramadhaan,
shawwaal kwa kutaja
michache; na pale inapotokea
kutumiwa au kutumika
kwake katika miezi hiyo
niliyoitaja au hata katika ile
mingine ambayo sijaitaja
mbali na Shaaban, matumizi
hayo aghalabu hurejelea ama
kilichojiri au kilichotarajiwa
kujiri katika kipindi cha
mwezi wa Shaaban kwa
kukifungamanisha au
kukihusisha na dhana
yenyewe ya 'Vunjajungu'.
Naam, tukirejelea mada
ya msingi ya makala haya
ya leo neno 'vunjajungu'
japo linaweza; kwa maana
ya kilugha au ya msingi
wa maneno yaliyotumika
kuunda neno hilo; kufasiliwa
kwa maana ya 'haribu chungu
kikubwa' au 'uharibifu wa
chungu kikubwa' ingawa
hii si maana tunayoikusudia
katika makala haya.
Aidha, maana rasmi ya
kikamusi neno 'vunjajungu'
kama kidahizo limefasiliwa
kuwa ni mdudu aina ya panzi
mwenye kiuno chembamba
na macho makubwa na hula
wadudu wadogo.
Maana ninayoikusudia
katika makala haya, si maana
hiyo ya msingi ya neno husika
kama ilivyodokezwa hapo
juu na katika fasili ya kabla
yake bali ni ile ya kimuktadha
au ya kimazingira ambamo
neno hilo hutumika au
hutumiwa hususan katika
kipindi hiki tulichomo.

AMIR wa Baraza Kuu, Sheikh Mussa Kundecha akizungumza katika moja ya


makongamano mengi yaliyofanyika ya kuwaelimisha Waislamu kuujua Uislamu
wao vilivyo na kuutekeleza.
'Vunjajungu' ni dhana
inayotumiwa kumaanisha
kipindi maalumu; kabla
ya m we z i M t u k u f u wa
Ramadhani au kwa maneno
mengine kipindi cha mwezi
wa Shaaban; kitumiwacho
n a Wa i s l a m u h a s a
wasiojitambua kukithirisha
kufanya maasi pamoja na
kujikita zaidi katika ushiriki
wa starehe zisizo halali kwa
hofu ya kutoweza kufanya
hivyo katika mwezi Mtukufu
wa R a m a d h a n i n a k wa
kutambua kwamba kufanya
hivyo ndani ya mwezi huo
kutawasababishia waruke
patupu (habaan manthuura)
katika swaumu au funga zao
watarajiazo kufunga katika
mwezi huo.
Ijapokuwa, kwa muktadha
wa m a d a h i i , k i l a m t u
anaweza kuwa na fasili au
tafsiri yake hiyo haitakosa
kulihusisha suala hili na
utendaji wa maasi au maovu
fulani kwa namna moja au
nyingine.
Kama ilivyo desturi au
ada katika kipindi hiki,
kama nilivyodokeza huko
nyuma, nidaa au matangazo
kuhusu 'vunjajungu'
yamekwishaanza, na naamini
yataendelea, kutolewa hadi
mwisho wa mwezi huu
(Shaaban) yakiwavutia na
kuwaraghibisha Waislamu
wa sampuli niliodokeza
katika fasili ya 'vunjajungu'
hapo juu, wahamasike katika
kuunga mkono kwa kushiriki
'vunjajungu' kwa kumuasi
Allah (s.w.), kadri ya uwezo
wao, katika kipindi hiki cha
kuelekea mwezi Mtukufu wa
Ramadhani.
Kauli kama vile zile za

'Karibuni au Mnakaribishwa
katika disko la 'vunjajungu'
la kukata na shoka!'au 'Njoo
uvunje jungu la mwaka nasi
hadi majogoo!' na kadhalika,
ni sehemu tu ya ya kaulimbiu chache kati ya nyingi
zitumikazo au zitumiwazo
na vyombo vya habari na
magari ya matangazo katika
kuwashajiisha, aina ile ya
Waislamu niliyodokeza huko
nyuma, kushiriki katika
mradi wao huo haramu!
Ni katika kipindi hiki,
kwa machombezo ya
matangazo kama hayo,
ndipo ambapo baadhi ya
Waislamu wasiojitambua
hunasa kirahisi mtego huu
k wa k u g h u r u r i k a k wa
k u j i i n g i z a n a h a t i m a ye
kuzama katika laghwu na
mambo mengine kedekede
ya hawaa nafsi ikiwa ni
pamoja kujiingiza katika
madisko ya 'vunjajungu',
uzinzi pamoja na ulevi kwa
kutaja machache.
Itoshe tu kusema
kwamba maasi au maovu
yanayotendwa kipindi hiki
si hayo tu bali nimeyataja
hayo matatu kwa sababu
aghalabu ndio hukithiri kwa
kiwango kikubwa katika
utukiaji au utendekaji wake
katika kipindi hiki cha
kuelekea mwezi Mtukufu
wa Ramadhani.
Naam, wafungaji-tarajali
wa s wa u m u ya m w e z i
Mtukufu wa Ramadhani
wanaotanguliza mambo
ya hawaa nafsi kama hayo
yaliyodokezwa hapo juu na
mithili yake, ni vigumu sana
kuufurahia ujio wa mwezi
Mtukufu wa Ramadhani;
japo vinywa vyao vinaweza

kudai hivyo lakini matendo


yao yanakataa; kwa kuhisi
kuwa Ramadhani ni jela au
kifungo kitakachowanyima
'uhuru' wao wa kutenda
watakalo kama walivyozoea.
Ndio maana, kwa kipindi
hiki, Waislamu wa sampuli
hii watajitahidi kadiri
wawezavyo kujikita zaidi
katika kutenda yale maovu
ambayo huhisi hawatapata

fursa wala wasaa wa


kuyatenda katika 'Jela ya
Ramadhani'!
Kwa mantiki hiyo, yumkini
kabisa watu hawa hutamani
mioyoni mwao 'kifungo'
kiishe haraka iwezekanavyo
mara baada ya 'kuanza
kwake' ili waendelee kuwa
'huru' katika uzinzi, ulevi,
madisko na kadhalika.
Kumaizi ukweli wa hili
hakuhitaji mtu kuwa na
Stashahada au Shahada au
kuwa Daktari au Profesa
bali kwa kutumia akili yake
ya kawaida tu (common
sense) na kutumia macho
yake; mara tu baada ya
mwandamo wa mwezi
Shawwal kama taashira ya
kukamilika kwa mwezi wa
Ramadhani; atatambua hili
kwa kuwaona wafungaji wa
aina hiyo wakiuaga mwezi
huo kwa cherekochereko ya
madisko yao usiku huohuo
wa mwandamo wa Shawwal
kwa kukesha hadi majogoo,
na kuusindikiza mchana
wake kwa ulevi na hatimaye
kurudi uzinzini kama
ilivyokuwa ada yao kabla ya
Ramadhani.
Huu ni msiba. Na ndio
maana tunaona watu
wamekuwa wakifunga, lakini
lile lengo la kufunga ambalo
ni kuwa wacha-Mungu,
halifikiwi.
(Mwandishi wa makala
haya ni msomaji wa muda
mrefu wa gazeti la ANNUUR anayeishi jijini
Mwanza.)

Mafundisho ya Quran

Inatoka Uk. 11
akhera kwa akili ya akhera.
Wa k a t i h u o u t a w e z a
kufahamu uhusiano kati ya
kusema Subhanallah na
kati ya kuyala matunda ya
peponi, kwa sababu kila kitu
kitapita huko.
Kufuatana na kanuni za
ghaibu na za nyuma ya tabia
(Metaphysical), tunaona na
tutafahamu kwa uwazi wote,
uhusiano wa kisababu kati
ya malipo na neema ambazo
zinapatikana huko na kati ya
kutenda hapa duniani.
Kanuni za uhakika za
Kifizikia zinazopatikana hapa
haziishii hapa, zinafanya
kazi huko. Kwa mfano,
anasema Mtume (s.a.w.)
kwamba swala zetu zitakuwa
mliwazaji wetu na rafiki yetu
katika makaburi yetu na
kwamba mtu ataingia peponi
kupitia milango yake minane
ambayo ni mbalimbali na
kwamba Quran itasimama
ili iwe muombezi wa msomaji
wake.
Hakika neema yoyote ile,
neema hiyo ama ni malipo

ya matendo fulani au ni
kusimama kwa malipo hayo
au ni kwamba uwezesho wa
milele huko. Ni mashuke ya
mbegu za matendo mema
hapa duniani.
Kwa sababu hiyo, hayo
mawili kwa mazingatio haya,
yanafanana katika undani
wake. Ama kwa mazingatio
ya vipeo vya peponi, pana
tofauti kubwa kati ya mawili
hayo. Inakunjuka dunia na
inavuka, kwa sababu moja
lau ni matunda ya uwezo.
Moja lao linabeba sifa ya
umilele na jingine ni la muda.
Vipeo vya ladha ya milele na
jingine vipeo vya mwili. Moja
lao ni wema kwa ngazi ya
jicho la yakini na jingine,
upole wa Mwenyezi Mungu
katika kilele cha Haki ya
yakini.
(Imenukuliwa kutoka
Kitabu: Miyangaza ya Quran
katika mbingu ya hisia,
cha Muhammad Fethullah
Gullen kilichotafsiriwa
kwa Kiswahili na Sheikh
Suleiman Amran Kilemile)

14

Makala

Mchango wa Waislmau katika maendeleo ya Dunia - 14


Na Ben Rijal
Na Ben Rijal
K AT I K A m a k a l a
hizi za Mchango wa
Wa i s l a m u k a t i k a
maendeleo ya dunia,
katika sehemu nyingi
nilikuwa namtaja Ibn
Sina na ujuzi wake
wa utabibu. Aidha
na mchanganyiko wa
fikra zake katika asili
ya maisha. Nitajaribu
kuandika makala mbili
tafauti juu ya Ibn Sina.
Kwa watu wa Ulaya
ni Avicenna katika
kuficha kuwa sio
Muislamu aonekane
kuwa ni Mzungu
kutokana na kazi
kubwa za kitaaluma
alizozifanya kuanzia
utibabu, falsafa, ilimu
ya nyota, fizikia n.k.
Jina lake khasa ni Abu
Ali al-Husayn ibn Sina,
yeye ni mzaliwa wa
Afshana katika maeneo
yaliokaribu na Bukhara,
kaandika maandiko
mengi ya kupigiwa
mfano lakini kati ya
kazi zake kubwa ni ile
ijulikanayo kama alQanun fil-Tibb kitabu
c h a m u o n g o z o wa
utibabu kilichotumika
Ulaya na Marekani
n a U l i m we n g u wa
Kiislamu hadi katika
karne za karibuni.
Aidha aliandika kitabu
juu ya kupona maradhi
na kukiita al-shifa
ambacho kiliwaathiri
wengi khasa khasa
Thomas Aquinas katika
karne ya 13 mwaka wa
1274.
I b n
S i n a
alisumbuliwa sana na
matatizo ya metafizikia

-metaphysical ikiwa
falsafa ya kuchunguza
chanzo cha uhai na
maarifa, udhanifu,
aliathiriwa pakubwa
na kazi za Aristotle
na Plato. Alijisomesha
vya kutosha kuweza
kuelewa juu ya utanzu
wa uhai. Inakadiriwa
a l i t u m i a m u d a wa
mwaka na nusu
akitaabika katika
k u t a k a u e l e wa j u u
ya hili. Huko mbele
tutakuja kuona namna
alivyokuja kuyakamata
ya Aristotle na wengine
kueleza kuwa alikuwa
na imani dhaifu na hata
wengine kufika kusema
alikuwa murtad.
Nitajaribu kuziweka
hoja za wasomi
mbalimbali juu yake
na kufahamu ukweli
wa imani yake ulikuwa
vipi?
Katika falsafa, Ibn
Sina alijaribu kufanya
kila aliwezalo kuiweka
falsafa iende na
mwenendo mzima wa
dini ya Kiislamu na
hapa ndipo kina Imam
Ghazali walipokuwa
hawaafikiani nae.
Maisha yake katika
k u m b u k u m b u
zilizoandikwa na
wanafunzi wake
kama Wahid Juzjani,
kuna maandiko
yanaonyesha namna
alivyokuwa akijadiliana
na wanafunzi wake alMubahathat na hata
yale maandishi ya Ibn
al-Qiftis Tarikh alhukama juu ya historia
ya falsafa. Aidha Zahir
al-Din Bayhaqis katika
Tatimmat Siwan alhikma wamemuweka
wazi
alikuwa
anakwendaje na
ulimwengu wa falsafa.
M s o m i
w a
U l a ya
G u t a s
anatutahadharisha
kuwa ili kuijua falsafa
aizungumzayo Ibn Sina,
inabidi tujifunze falsafa
kisha ndio tumsome na
kumtolea hoja. Farabi
alimvutia mno kwani
kumsoma Al-Farabi
aliweza kuwaelewa
akina Aristotle na
kina Plato na kuweza
kujenga hoja zake

Fatilia
kuandama kwa Mwezi
Leo Ijumaa ni tarehe 24 Shaaban 1436

AH sawa na tarehe 12 Juni 2015.


Tutaangalia kuandama kwa mwezi wa
Ramadhani tarehe 17 June 2015 siku ya
Ijumatano.
Kutoka leo Ijumaa ya tarehe 12 Juni 2015
hadi kufika Ramadhani tumebakisha
siku 6 tu.

Ibn Sina

IBN Sina
katika metafizikia
Babake Ibn Sina
a l i k u wa m s o m i n a
inadhaniwa alikuwa
mwenye kufwata
madhehebu ya Ismaili.
Mzee wake huyu
alikuwa mtaalamu kwa
hio alipewa kibarua
cha kuwa Gavana
wa Samanid. Akiwa
na umri mdogo, Ibn
Sina alikuwa na kiu ya
kusoma kwa hio aliomba
ahame na familia yake
na kuelekea Bukhara
na alipofika hapo
alisoma na kufwata
madhebebu ya Abu
Hanifa (Hanafi) chini
ya mwalimu Ismaiil
Zahid. Aidha alisoma
juu ya utibabu kwa
walimu mbalimbali.
Samanid inaaminika
kuwa ilikuwa na
maktaba iliojaza
vitabu vya kila aina na
hapo ndipo Ibn Sina
akenda kujisomea juu
ya taaluma ya utibabu
na kuwa anajisomesha
mwenyewe na kujaribu
kuyatumia yale
alioyasoma.
Alianza kujulikana
alipotimu umri wa
miaka 18 kutokana na
kuwa ashabobea katika
taaluma mbalimbali
ikiwemo ya utabibu na
hilo likamfanyia wepesi
kuweza kupata kibarua
katika mahkama ya
Samanind ikiwa chini
ya kiongozi Nuh
ibn Mansur na hapo
alikuwa akifanya kazi
ya kutibu wagonjwa.
Alipofariki baba
ya k e a l i p a n d i s h wa
cheo lakini Samanid

h a k u m u w e k a
aliondoka na kuhamia
Gurganj iliopo
K h a wa r z a m , k i s h a
akarudi Bukhara katika
mwaka wa 999 ambako
alikutana na aliokuja
k u wa m wa n a f u n z i
wake Juzjani. Baada
ya m wa k a a k a f i k a
Buyid na kupata kazi
ya utabibu na kuandika
kitabu kwa lugha ya
Kifursi Danishnama-yi
AlaI ikiwa ni kitabu
cha maarifa.
Wa s o m i
wa
nyakati hizo walipata
misukosuko mingi
kutokana na kupewa
kazi na watawala
na
watawala
wa n a p o b a d i l i k a a u
kuondolewa na wao
hujikuta matatani. Ibn
Sina katika maisha
yake ya mji wa
Hamdan kulikuwa na
mapambano makali
baina ya dola ya Isfahan
na Hamdan. Hapa Ibn
Sina akufungwa baada
ya Isfahan kushinda Ibn
Sina alibaki Hamdan
kwa muda lakini
baadaye alikimbilia
Isfahan. Kwa muda
wa miaka 10 hadi 12,
Ibn Sina alibaki katika
utumishi wa Amiri wa
Isfahan, Abu Yafar
Alaa ad-Dawlah akiwa
daktari wake.
Somo la uanzilishi
ndio lilomsumbua
sana Ibn Sina na kufika
kusema kuwa dunia
haina muumba na haina
mwanzo, hapo alikuja
kugombana na wasomi
we n g i n e k u m we k a
kuwa murtad. Lakini
juu ya hayo, Ibn
Sina baadaye alikuja
kuandika kuthibitisha
kukuwepo kwa Mungu,
huku kulimchukua
katika mkondo mmoja
kisha ukamvuta katika
mkondo mwengine, juu
ya hayo bado wasomi wa
wakati wake na wakati
huu bado wanamuona
Ibn Sina kateleza na
kumhesabu ndani ya
hukumu zao kuwa ni
Murtad na kumuelezea
zaidi kuwa akipenda
pombe na mabibi.
Starehe hizi
zilimfanya apatwe na
ugonjwa wa msokoto
wa t u m b o a m b a y o
inafikiriwa ndio
aliomfanya aage dunia.
Hapa ndipo nitajaribu
kupatizama zaidi
kuwa jee tunaweza
kumhukumu mja
au mja uhukumiwa
na Allah? Ibn Sina
katika nyakati tafauti
alishauriwa aache anasa

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

na kila akikatazwa
kushikamana na anasa
akisema :
Napendelea maisha
mafupi ya upana kuliko
membamba yenye
urefu.
M a r a d h i
ya l i v y o m z i d i h u k u
akiwa kitandani alijuta,
a k a t o a v i t u v ya k e
kwa masikini, akatoa
vitu alivyopata kwa

dhuluma, akaacha huru


watumwa na kuanza
kusikiliza kwa kisomo
cha Qur-aan mpaka
alipoaga dunia.
Kama mwanadamu
usiokamilika, jee
utakuwa na lipi la
kumhukumu?
Makala ijayo
nitammurika zaidi
Ibn Sina na kuweza
kumuelewa.

Jee Unajua?

1.
Maji yaliokuwa sio salama yanauwa watoto
wafikao 200 kila saa duniani kote.
2. Takwimu za duniani zinaonyesha kuwa
wanawake wanakuwa na umri mrefu kuliko
wanaume, wastani wa umri wenye kikomo kwa
wanawake ni miaka 69 na kwa wanaume ni miaka
64.
3. China ndio nchi yenye idadi kubwa ya
watu, ikifwatiwa na India. China ina idaidi ya watu
wafikao bilioni 1.35 huku India ikiwa na idadi ya
watu wafikao bilioni 1.21. Nchi ya China na India
kwa pamoja ukizichanganya zina idadi ya watu
wafikao asilimia 37% ya wakazi wote waliopo
duniani.
4. Inasemekana vita vilivyopiganwa kwa
muda mfupi vilipiganwa katika mwaka wa 1896
wakati Ufalme wa Zanzibar uliposalimu amri kati
yake na mkoloni Muiengereza, vita baina ya pande
mbili hizo vilichukua dakika 38.
5. Mabomu yaliozikwa kwenye ardhi
huchukua roho za watu 24,000 kila mwaka.
6. Nchi moja peke yake duniani isiokuwa na
jeshi wala matumizi ya kijeshi nchi hio ni Iceland.
7. Mabara ya Asia na Pacific ndio yanaongoza
kwa utapio mlo ikiwa na idadi ifikiayo watu milioni
553 na nchi ambazo zinaongoza ni Indonesia na
Philippines.
8. Katika nchi zilizo kusini ya jangwa la
Sahara ina idadi ya watu wafikiao idadi ya milioni
227 wapo katika hali ya kukosa chakula zikiwemo
nchi za Ethopia, Niger na Mali.
9. Wasiwasi na kuogopa ni khulqa ya
mwanadamu, hata mwanadamu akiwa ana ushujaa
wa aina gani huwa ana kitu anaogopa, kwa mfano
Napoleon, Mussolini na Hitler walikuwa na
ugonjwa ujulikanao kwa kimombo Ailurophobia
ikiwa ni khofu ya kuogopa paka.
10. Inaaminika kuwa mwanadamu anatumia
asilimia 33% ya maisha yake akiwa amelala, hio ni
sawa na miaka 25.

UWANJA WA VIJANA - JIONGEZEE MAARIFA

CHEMSHA BONGO namba 10

Weka duara kwenye jawabu Ilio sawa. Jawabu


kamili wiki ijayo.
B
A
Q
Q
R
A
L
2:9

M
F

A
2
E
F
G
N
A
N
A
U

D
9
A
N
H
D
Y
T
K
T

R
O
O
K
A
I
L
A
K
A

U
I
E
I
P
O
A
R
A
R

1:3

3
U
R
A
T
A
S
I

A
0
P
O
N
A
U
W
M
N

S
R
S
H
A
F
L
E
A
A

D
D
F
O
T
U
Q
H
D
D

3
3
Y
U
I
O
A
E
I
A

1
0
Z
C
B
I
D
P
N
K

F
C
V
B
N
M
R
H
A
U

1.
Taja Sura inayoelezea mwezi wa Ramadhani.
2.
Vita gani Waislamu walipigana katika mwezi
wa Ramadhan.
3.
Ratio baina ya Waislamu na Makafiri katika
vita vya mwanzo waliopigana Waislamu ilikuwa 1:3,
1:6, 2:9.
4.
Sala gani inayosaliwa katika mwezi wa
Ramadhani tu.
5.
Katika mwezi wa Ramadhan kuna milo miwili
inatakiwa kuliwa moja jua linapokuchwa na mwengine
kabla ya kuingia alfajiri, milo hio ni :,

6.
Ramadhani una usiku mtukufu unaitwaje?
7.
Mwezi wa Hijra huandama biana ya na

8.
K u f u n g a k wa m w e z i wa R a m a d h a n
kulifaradhishwa katika mji gani?
9.
Asio balighi ana wajibika kufunga? Ndio au
Hapana.
10. Ramadhani humtakasa mja ..

15

TANGAZO

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

16

MAKALA

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Wimbo wa Amani na Utulivu na Uchaguzi Mkuu


Na Yussuf Hamad

ENZI zile za utoto wangu,


kijijini kwetu alitokezea
kuwapo babu mmoja aliye
akiitwa Babu Nshenga.
Babu huyu hakuwa babu
kwa maana ya kuwa
akitembelea fimbo,
alikuwa babu kwa sababu
alishakuwa na wajukuu,
na wengi wa wajukuu zake
hao, walikuwa marika yetu.
Babu Nshenga, alikuwa
miongoni mwa watu wazima
wachache mno ambao, kwa
nilivyonikisikia na baadaye
kujionea mwenyewe, kuwa
akiheshimiwa sana na kila
mtu, mkubwa na mdogo, wa
kike kwa wa kiume.
Awali sikufahamu
kwa kina sababu ya
kuheshimiwa kwake kule
kukubwa kulikopitiliza.
Utoto haupimwi kwa kuwa
na akili ndogo na maungo
a m b a y o h a ya j a p e v u k a
tu: utoto hupimwa kwa
kuwa na uwezo mdogo
wa kuchanganua mambo,
kujua siri za dunia na
malimwengu na uhaba wa
elimu waliyo nayo watu
wengi wazima: wawe
wasomi au mburumatari
kama mie, mradi ni watu
wazima kuna kitu lazima
watakuwa wamekutangulia
kukijua.
Nilipokuwa mkubwa
na kupata uwezo wa
kuchanganua mambo,
nilikuja kutambua kuwa
Babu Nshenga alikuwa
haheshimiwi kwa heshima
tu: alikuwa akiogopwa.
Akiogopwa kwa sababu
akitisha. Tena akitisha kama
magonjwa yasiyo kinga wala
tiba! Heshima ya aina hii
haifai kuitwa heshima kwa
sababu ni heshima ya woga.
Haina ukweli wowote wala
uhalisia.
Wa t u wa l i k u wa
wakimuogopa Babu
Nshenga kwa kuwa
kwanza alikuwa mchawi,
muokosi na hasidi wa kila
kitu akionacho. Nshenga
akiitumia elimu yake
kudhuru watu wasio hatia,
kuwaumiza wanaompinga,
wasiomuamini, na hata watu
anaohisi kuwa watakuja
kuwa tishio kwake. Elimu
ya k e n a u t a wa l a wa k e
ulimpa shauri la kuwa rai
mujarabu ya kuleta heshima
na utulivu ni kuwaadhibu au
kuwaondoa wale wote weye
kuleta dalili za kukupinga au
kukusumbua.
CCM ndani ya miaka
yote hamsini ya Utawala
wake, haipishani sana na
historia ya Babu Nshenga,
kusema kweli. Haipishani
kwa sababu licha ya mateso
wa ya p a t a y o wa n a n c h i
kutona na utawala wao:
kuanzia elimu duni,

HAYATI Mwalimu J.K.


Nyerere.

RAIS mstaafu Benjamin


William Mkapa.

RA I S J a k a ya M r i s h o
Kikwete.

RAIS wa Zanzibar, Dkt.


Ali Mohamed Shein.

huduma mbovu za afya,


miundo mbinu duni, umeme
usioaminika, huduma mbovu
za kijamii, ufisadi uliopita
mipaka, utawala wa mabavu
na kinyapara na mengineyo
mengi inashangaza kuwa
bado tu nchi hii inajisifia
kuwa ina amani na utulivu!
Hiki ni kituko kwa kweli.
I n g a wa wa l i o w e n g i
wataamini kuwa nchi
yetu ina amani na utulivu.
Ukweli ni kuwa amani na
utulivu uliopo ni ule ule wa
Babu Nshenga na watoto
wa kijijini, na sio amani na
utulivu mwingine. Leo hii
utajisifiaje amani na utulivu
ikiwa mvua ya siku moja
inajaza maji majumbani na
kuharibu kila kitu na hakuna
lolote linalofanywa ama
kujikinga na wala kufidia
maafa hayo?
Tu n a j i s i f i a a m a n i n a
utulivu wakati leo hii wenye
haki ya kusema na kujieleza ni
wachache huku walio wengi
wakijieleza hukabwa koo na
kudhihakiwa? Yuko wapi
Said Ali wa JUVICUF? Wako
wapi UAMSHO? Yaliwafika
yapi wanachama wa CUF
walio wakirudi mkutanoni
Makunduchi? Unajua hatua
gani zilichukuliwa dhidi ya
waliowahujumu wana CUF
waliojeruhiwa? Hakipo, hilo
ndilo jibu. Sasa basi fikiri, hivi
nchi hii ina amani na utulivu
kweli?
Amani na Utulivu wa
kweli hupatikani mahali
ambapo hapana chuki wala
dhana ya visasi. Hupatikana
mahali ambapo pana upendo
na matumaini ya kweli. Kama
haya ni ya kweli, tutajivuniaje
amani na utulivu wakati
jamii yetu imejazwa siasa za
chuki: chuki za umajimbo,
udini, na uvyama kwanza
badala ya utaifa?
Leo hii kuna Wapemba
ambao wamefanywa
wahanga wa siasa za
kibaguzi hapa nchini. Leo
hii kuna Waislamu ambao ni
mbuzi wa kafara wa mfumo
ulioshika hatamu nchini
ilhali tukiaminishwa nchii

hii haina dini.


Hivi leo CUF na UKAWA,
ambao licha ya kukubalika
na wananchi walio wengi,
wamekuwa wakifunikwa
kifuu dume ili wasione
wala wasitoe mwanga wa
matumaini kwa wananchi
waliokwisha kata tamaa na
maisha chini ya utawala wa
Babu Nshenga na warithi
wake.
Ukiacha hayo, ni wangapi
kati yetu wanauguza majeraha
yaliyosababishwa na Serikali
tawala? Ni wangapi kati yetu
wametenganishwa na aila
zao baada ya watawala na
serikali zao kuwatia nguvuni,
vizuizini? Katika hali kama
hii bado tuna thubutu ya
kudai kwetu kuna amani?
Amani na utulivu uko
wapi wakati kila mwaka
wa uchaguzi lazima mmoja
wetu adhulumiwe? Tena
adhulumiwe hadi kufikia
watu kupoteza roho kwa
kudai haki zao za msingi?
Tumeona yaliyojiri 1995,
2000 na 2005 kasoro ya 2010.
Hakukuwa na amani kitu
wala utulivu jambo! Ilikuwa
vurugu mechi tu, mpata
mpataye mkosa ujingawe.
Sheria ya msituni ikatawala!
Kinachokera zaidi, amani
inapovurugwa na utulivu
ukapotea, wale wanaoleta
uharibifu huwalaumu wale
walioathiriwa na uharibifu
wao huo kuwa ndio
waharibifu kwani kwao wao,
wafanyalo ndio sahihi tu hata
wakiuwa mtu.
Wakati muda wa uchaguzi
ukikaribia kubisha hodi,
nahisi tena kuwa kuna kila
dalili za uvunjifu wa amani
au wa kutaka amani ivunjike,
ukifanywa. Tuache yale
ya kupigana mapanga na
kuzuiana kwenda kufanya
mikutano mashamba. Kuna
ya vitambulisho vya ukaazi
na zoezi zima la kuandikisha
wapiga kura. Kinachofanyika
sasa, ni kuwa wananchi
walio wengi wenye haki
ya kupatiwa vitambulisho,
hawapatiwi. Ukiuliza kwa
nini, majibu utaambiwa

vitambulisho vipo zaidi ya


laki mbili havijachukuliwa na
wahusika. Tusiamini jambo
hili, nawanasihi sana.
Ukweli ni kwamba
watu wanapokwenda
kudai vitambulisho vyao
huambiwa njoo kesho mpaka
wakachoka kufuatilia na
kupiga kalenda kwa sababu
kesho huwa haifiki wala
haiko. Mwisho, huchoka.
Wakaamua kuviacha tu huko.
Huu, kwa lugha nyepesi,
ndio unaoitwa usanii wa
CCM, kwa taarifa yako. Na
huu ndio ukweli ingawa
wenyewe akina ahlilmaknuush(watu wa
kukanusha kila jambo)
watakanusha kila siku hadi
kiama kiwafikie! Ila swali
linabakia pale pale. Je, kwa
hali kama hii amani na
utulivu upo kweli au kuna
amani na utulivu wa woga
tu?
Umuhimu wa kitambulisho
cha Mzanzibari unaeleweka
na kila mtu kwa sasa. Kubwa
zaidi la umuhimu huo ni vile
kupata haki ya kuandikishwa
katika daftari la wapiga kura.
Ila wakati zoezi hili muhimu
likisonga mbele, kuna
taarifani kuwa Wazanzibari
walio wengi wenye haki hii
kwa hakika wamo hatarini
kuikosa. Tena kuikosa kwa
vitimbi tu na usanii wa dola.
Wa k a t i Wa z a n z i b a r i
wenye sifa ya kuandikishwa
wakinyimwa haki yao
hiyo kwa kunasibishwa na
upinzani wa umajimbo,
kuna jopo la wageni kutoka
bara ambao hawana sifa
z a u k a z i wa Z a n z i b a r
wameandikishwa. Hadi
kufikia sasa, inakadiriwa
kuwa zaidi ya wapiga kura
haramu laki moja kutoka bara
wameshaandikishwa. Na hao
yawezekana ni robo tu ya
walioandikishwa hadi sasa
kama sehemu ya makununu
ya kujijengea mazingira ya
ushindi wa kishindo kama
si wa gharika, yarabi salama,
Mungu mwema!
Kuna ithibati ya
vitambulisho vya ukazi na
hata video inayoonyesha
wapiga kura feki hawa.
Ingawa Mheshimiwa Samia
Suluhu anabisha, kuna taarifa
na ushahidi wa kutosha
unaonyesha mamluki hao
wa kibara wakiandikishwa

ndani ya kambi za jeshi hapa


visiwani.
S u a l a h i l i wa p i n z a n i
wameshalizungumza sana na
kuitaka Serikali ichukue hatua
zinazofaa bila matumaini
ya jambo hili kupatiwa
ufumbuzi. Wakiambiwa
kuhusu kadhia hii, huitikia
mbele ya nyuso za wadaio,
wa k i g e u k a h u wa c h e k a
visogo na kuwapuuza kama
vile madai yao yale haya
maana yoyote.
Ninachoshangaa, wakati
haya yakitendeka au
yakitendwa kwa makusudi,
Serikali haionyeshi dalili
yoyote ya kuchukua hatua
zaidi ya kukanusha. Tena
kukanusha bila kujua kuwa
kufanya hivyo sio kinga wala
tiba ya tatizo. Mradi maslahi
yao yanakuwa, basi hakuna
haja ya kutafuta ufumbuzi wa
tatizo linalolalamikiwa.
Na iwe iwavyo, lakini ni
kweli kabisa kuwa kuna
hujuma nyingi zinazofanywa
ili kuuvuruga uchaguzi na
kuvuruga amani na utulivu
nchini. Baya zaidi, hujuma
hizi zinafanywa na wale
wale wanaohubiri amani
na utulivu kila wapandapo
majukwaani kuwahutubia au
tuseme kuwatia woga wale
wanaowaamini wasipate ari
ya kuhoji huku maslahi yao
yakiwaendea sawa.
Ninachoonya katika hali
kama hii, matukio haya na
mengine yanayofanywa
n a ya l e ya n a y o p a n g wa
kufanywa ili kuhakikisha ile
dhana ya ushindi lazima
inafikiwa, hayatamalizia
kwenye amani na utulivu tu.
I k i wa C C M i n a a m i n i
kuwa wananchi wa nchi
hii wataendelea kudumisha
a m a n i n a u t u l i v u k wa
kuwajaza woga wa Babu
Nshenga, basi watambue
kuwa woga ukizidi sana,
huzaa ujasiri usiotarajiwa
wala usiozuilika. Na hapo
ndipo watakapoweza kuona
kasi na ghadhabu za nguvu
ya Umma wakati kufika.
Tuombe amani na utulivu
wa kweli na uchaguzi huru
na wa haki!

17
Na Ben Rijal
NENO mazingira
limechukua nafasi kubwa
katika maisha yetu ya kila
siku, mazingira yamepewa
umuhimu mkubwa
kutokana na maisha
yetu yote yanategemea
mazingira na kila mazingira
yakichafuka na kuharibika
mwanadamu na viumbe
m b a l i m b a l i v i n a k u wa
katika matatizo na shida.
Tujiulize kwanza nini
m a z i n g i r a ? M a i s h a ya
viumbe na mwahali
wanapopatikana tutasema
mazingira au tutasema
mazingira ni maingiliano
baina ya viumbe hai na vile
vilivyowazunguka yaani vitu
vilivyokuwa sio hai, ikiwa
udongo, mchanga, milima,
mazingira ni viumbe hai na
yale yote yaliowazunguka
n.k.
Mazingira yanachafuliwa
kwa kila namna mfano, ukataji
wa misitu, umwagaji wa
maji machafu kwenye mito,
maziwa na bahari, utowaji
wa moshi usiochujwa kutoka
viwandani na kuelekea
angani, kunyesha kwa mvua
ya tindi kali, kutosafishwa
kwa maji machafu na
kuachiwa kuingia katika
bahari na mito, kuvunjwa
kwa matumbawe kwa njia
mbalimbali ikiwa pamoja na
kutumia uvuvi haramu wa
kutumia mabomu n.k.
Uislamu unafunza utunzaji
wa mazingira na uhifadhi wa
mazingira kupitia kitabu
kitukufu Quran na Hadithi
za Mtume SAW.
Quran inatufunza kuwa
maisha yote yapo katika
uwiyano, mizani na Allah
amejaalia uwiyano huo,
huku mwanadamu anakuwa
mstari wa mbele katika
kuyachafua mazingira.
Kwa hakika Sisi
tumekiumba kila kitu kwa
kipimo. (54:49).
Allah amejalia kila kitu
kuwemo kwenye mizani na
mizani hio haina shaka na
ni yeye Allah aliokamilisha
kuiweka dunia katika mizani
iliokamilika.
Mwenyezi Mungu
anajua mimba abebayo
kila mwanamke, na
kinacho punguka na kuzidi
matumboni. Na kila kitu
kwake ni kwa kipimo. (13:8).
Katika vyote alivyoumba
Allah na kumleta duniani
mwanadamu, Allah
aliikamilisha mizani.
Na mbingu ameziinua,
na ameweka mizani. (55:7).
Tunapoiangalia dunia,
tunakuta kuna vitu vya
kila aina na kila kimoja
kinakuwepo kutokana na
kushikamana na kengine.
Maisha yetu yanategemea
jua kwa kuwa jua ndio
linaungana na majani katika
miti na kufanya chakula
na wanadamu na viumbe
mbalimbali kutegemea
vyakula kutokana na miti,
ingawa kuna wanyama hawali
majani lakini wanakula wale
wanyama wanaokula majani.
Hapa unaiona dhana nzima
ya kitu kimoja kuungana
na kutegemeana na kitu
chengine. Maisha yote
yanashikana na sehemu moja
ya mazingira. Allah ndio
yeye mwenye kuviendesha
na hakuna kitu kimoja

MAKALA

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Uhifadhi wa Mazingira na Uislamu

Mazingira yanayopendeza

Mazingira yalioharibiwa
kinachojiendea wenyewe bila
ya uwezo wa Allah. Hapa mja
anatakiwa kuwa mwangalifu
kwa kujuwa kaumbwa na
aliomuumba ameviweka
vitu tuvitumie kama vile
alivyoviweka katika mizani
yake.
Je! Huoni kwamba
Mwenyezi Mungu
vinamtakasa vilivyomo
katika mbingu na ardhi, na
ndege wakikunjua mbawa
zao? Kila mmoja amekwisha
jua Sala yake na namna
ya kumtakasa kwake. Na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye
kuyajua wayatendayo.
(24:41).
Tu j u w e k u w a A l l a h
ameumba kila kitu kiwe
alama na maana kamili na
kuweza kufahamika utukufu
wake na sababu ya kuviumba
vitu hivyo.
Ambaye amekufanyieni
ardhi kuwa tandiko, na
akakupitishieni humo njia,
na akakuteremshieni kutoka
mbinguni maji. Na kwa hayo
tukatoa namna mbalimbali za
mimea. (20:53).
Kuleni, na mchunge
wanyama wenu. Hakika
katika hayo zipo ishara kwa
wenye akili. (20:54)
Allah ameiumba dunia
sio kwa bahati nasibu au
kwa kukosea, bali ameiumba
dunia tupate mazingira yalio
salama na yalio endelevu.
Na hatukuziumba
mbingu na ardhi na
vilivyomo baina yake kwa
mchezo. (44:38)
Hatukuviumba hivyo ila
kwa Haki, lakini wengi wao

hawajui. (44:39)
Quran inatufahamisha
na inatuongoza kuelewa
kuwa Allah ameviumba
a l i v y o v i u m b a k u wa n a
thamani ndani yake na hivyo
alivyoviumba ameviumba
viweze kumtumikia
kwa kuwa ni yeye Allah
ameviweka kuwa kila
kimoja kati ya alivyoviumba
viwe vinategemeyana na
kisha baada ya kuviumba
mwishowe hutoweka, kisha
akatoa vitu kutokana na
nje ya uhai kisha vitu hivyo
vikawa ndio uhai autegemayo
mwanadamu.
Hakika Mwenyezi Mungu
ndiye mpasuaji mbegu na
kokwa, zikachipua. Humtoa
aliye hai kutoka maiti, naye
ni mtoaji maiti kutokana
na aliye hai. Huyo ndiye
Mwenyezi Mungu. Basi vipi
mnageuzwa? (6:95)
Allah ameumba mauti na
atampa jaza yule ambaye
kati ya wanadamu akatenda
mema. Allah ameumba
uhai na mauti kwa sababu
zake na ufisadi autendao
mwanadamu afahamu
kuwa katika maisha ya
baadaye hatokuwa katika
waliofuzu. Kwa mantiki hii
mwanadamu anatakiwa
mara zote awe mwangalifu
katika maisha yake ya kila
siku kwa viumbe vyengine
na rasilimali ziliomo kwenye
mazingira anayoishi.
AMETUKUKA ambaye
mkononi mwake umo
Ufalme wote; na Yeye ni
Mwenye uweza juu ya kila
kitu. (67:1).

Ambaye ameumba mauti


na uhai ili kukujaribuni
ni nani miongoni mwenu
mwenye vitendo vizuri zaidi.
Na Yeye ni Mwenye nguvu
na Mwenye msamaha. (67:2)
Maisha yamo ndani ya
mazingira na maisha kuweza
kuwa endelevu, yanategemea
mazingira, mwanadamu ni
sehemu kubwa ya dunia
tunayoishi, mwanadamu
yupo juu ya viumbe
mwandamu na uhusiano
baina yake na mazingira
yameelezwa kwa kina katika
Quran tukufu na Hadithi za
Mtume SAW.
Tu n a p o z u n g u m z i a
maendeleo endelevu
huzungumza matumizi
ya rasilimali ziliopo pasi
kuzimaliza na kuzibakisha
kwa vizazi vijavyo na huku
ndipo Allah alipotuelekeza
kuwa tutumia pasi na kufanya
ufisadi na ubadhirifu.
Katika Saheeh Al-Bukhari
t u n a f a h a m i s h wa k u wa
Kazi njema aitendayo
mwanadamu haipo kwake
peke yake, bali inaendelezwa
mpaka kwa viumbe vyengine
na kuna malipo kwa kila jema
ulifanyalo kwa kila kiumbe
kilichokuwa hai. (Saheeh
Al-Bukhari)
K a t i k a h i k m a k u b wa
alioifanya Allah ni kumjaalia
mwanadamu kuwa na akili
na kuwa juu ya viumbe
vyote. Nikusema kumfanya
kiongozi katika dunia na
kuwa sehemu muhimu ya
dunia na kuwa mtekelezaji
wa ya l e A l l a h a m e t a k a
ayatekeleze akiwa kama
kiongozi ambao mwanadamu
ameletewa ujumbe kupitia
kwa Mitume asiwe mwenye
kufanya uharibifu.
Bahati mbaya mwanadamu
amekuwa mharibifu na
kuyaharibu yale mazingira
ambayo yanamzunguka kwa
kuchafua vianzio vya maji,
kutoa uchafu viwandani na
kumwaga kwenye vianzio
vya maji na kwenye mito
na bahari, kukata misitu na
kusahau kupanda miti na kila
iana ya ufisadi. Mwanadamu
huyo huyo ametengeneza
aina mbalimbali za silaha
a m b a z o z i n a p o t u m i wa
katika maeneo ambayo
m a b o m u ya n a p o t u p wa
maisha huangamia, sio
kuuwawa kwa mwanadamu
tu lakini mazingira yote
kuwa sio salama na ardhi
hizo kutoweza kuendelea
kupandwa kwa miti na
kukuweko kwa wanyama.
Dunia ni nzuri na
ipo kijani, hakika Allah
ametukuka na kumfanya
mwanadamu kiongozi
na ndio yeye aliojaaliwa
tuwe huru na wenye kuwa
wadilifu. (Saheeh Muslim).
Allah amekiweka kila
kitu sawa ili tusiwe katika
mashaka, lakini ujuwaji wetu
wanadamu katika kuyasarifu
mazingira ndio hujitia
taabuni.
Na akaweka humo milima
juu yake, na akabarikia humo
na akakadiria humo chakula
chake katika siku nne. Haya
ni sawa kabisa kwa wanao
uliza. (41:10)
Uislamu umeweka

wazi matumizi endelevu


ya maliasili na haki ya kila
kiumbe kuweza kuishi kwa
usalama na amani, bahati
mbaya mwanadamu kwa
uroho aliokuwa nao amekuja
kutaka kuuweka uwiyano na
mizani ya maisha katika nje
ya utaratibu aliotutaka Allah
tuutekeleze.
Kila mmoja wetu
anatakiwa kuwa anatumia
rasilimali zilizopo
duniani kwa uangalifu na
kuhakikisha anazitumia yeye
na vizazi vinavyokuja na
hivyo vizazi nao kubakisha
kwa vizazi vyenginevyo. Kasi
ya mwanadamu wa leo ilivyo
na matumizi ya rasilimali,
amekuwa anatumia rasilimali
zilizomo kwa kipundukia au
tuseme nje ya matumizi yake.
Shirika la uhifadhi la The
Convention for International
Trade in Endangered
S p e c i e s o f Wi l d F a u n a
and Flora (CITES) limo
katika kudhibiti biashara
ya viumbe wasiopungua
33,000 kwa Marekani na
nchi za Marekani ya Kusini
kwa khofu viumbe hivyo
kutoweka na kutoonekana
tena mfano wa Dinosaur au
ndege aliokuwa akipatikana
kisiwani Mauritius aitwayo
Dodo.
Matumizi ya kupindukia
kwa rasilimali ziliomo kwenye
mazingira yaliotuzunguka na
idadi ya watu inayoongezeka,
hayendi sambamba yanatoa
shindikizo maisha kuwa ya
taabu kila kukicha.
Viumbe vyote vina
haki ya kutumia rasilimali
ziliomo kwenye mazingira
yalituzunguka kutokana na
zawadi aliotupa Allah lakini
matumizi haya yawe katika
uangalifu na kutumia kwa
njia ambayo inakubaliana
na ule msemo wa zamani
kula na kubakisha, kwani
Allah ametuumba tuwe na
uwiyano wa matumizi ya
rasilimali zilizomo duniani
pasi kuzifuja.
Na kina Thamud
tuliwapelekea ndugu yao
Saleh. Akasema: Enyi
watu wangu! Muabuduni
Mwenyezi Mungu. Nyinyi
hamna Mungu ila Yeye. Yeye
ndiye aliye kuumbeni katika
ardhi, na akakuwekeni humo.
Basi mwombeni msamaha,
kisha mtubu kwake. Hakika
Mola wangu Mlezi yupo
karibu, anaitikia maombi.
(11:61).
Allah ametuumba na
k u t u we k a k a t i k a a r d h i
sio kuja kufanya fujo na
uharibifu. Katuumba na
kutuleta duniani tumuabudu
na kutii maamrisho yake
pindipo tukiyatekeleza hayo
hapa duniani, tutaishi kwa
amani na maisha ya akhera
yatakuwa ya wale waliofuzu.
Mtume SAW katutataka
tupande miti Atakayepanda
miti na katika mti huo
wakafaidika wanadamu,
ndege na wanyama ajuwe
hio kwake itakuwa sadaka
(Saheeh Al-Bukhari, Saheeh
Muslim).
Maisha endelevu
yatatokana na kuweko kwa
miti na ndipo wajuzi wa
mabadiliko ya tabia nchi
wanasisitiza tujikite na
MKUHUMI, Mkakati wa
upandaji miti ya misitu na
kupunguza hewa ukaa.
Inaendelea Uk. 18

18
Na Alhaj Abdallah
Tambaza
MWEZI kama huu miaka
minne iliyopita, Rais Jakaya
Kikwete ilibidi akatishe
ziara nchini Botswana na
kurudi nyumbani kuongoza
maelfu ya waombolezaji
jijini Dar es Salaam katika
mazishi ya mmoja wa watu
mashuhuri kupata kutokea
katika ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati. Alikuwa
bingwa wa usomaji Quran;
bingwa wa unajimu; bingwa
wa tiba asilia; mtaalamu wa
nyota (horoscope) na pia
mwanasiasa nguli. Endelea
na sehemu ya tatu ya makala
haya.....
Katika utabiri, alianzia
kwenye kutabiri mpira kabla
ya kutoa utabiri wa nyota
magazetini, wakati huo
ambapo hakukuwa na mtu
mwengine aliyeijua fani hiyo
hapa nchini.
Kwa mara ya kwanza,
tulimshuhudia Sheikh
Yahya akitabiri mpira katika
m a s h i n d a n o m a k u b wa
ya Sunlight Cup (baadaye
Taifa Cup) yaliyokuwa
yakishindanisha timu za
mikoa yote ya Tanzania Bara.
Vipeperushi vyake
alivyokuwa akivitawanya
k a b l a ya m c h e z o p a l e
uwanja wa Karume, si tu
kwamba vilionyesha ni
timu gani itaibuka mshindi,
bali pia nambari za
wachezaji na dakika mabao
yatakapofungwa.
Nakumbuka mwaka
mmoja kwenye miaka
ya 1960s, mashindano ya
Gossage (sasa Challenge
Cup) kwa nchi za Afrika
M a s h a r i k i , ya l i f a n y i k a
jijini Dar es Salaam. Sheikh
alikuwa akitoa utabiri wa
michezo ile kadri ilivyokuwa
inaendelea.
Siku moja kulikuwa na
mchezo baina ya Kenya
na Uganda na hapo
aliitabiria timu ya Kenya
kuibuka mshindi akitaja pia
dakika na idadi ya mabao
yatakayopatikana.
Alibashiri pia wachezaji
wa Kenya Joe Kadenge,
Chege Ouma, Livingstone
Madegwa na John Ambani
n d i o w a t a k a o n g a r a
mchezoni.
Wa t u wa K e n ya ,
wakiwamo viongozi wa nchi
ile, walianza kumfuatilia
k wa k a r i b u ; h a s a p a l e
alipotabiri Kenya ndiyo
wa t a k a o c h u k u a k o m b e
mwisho wa mashindano.
Utabiri ulipotimia;
aliletewa mwaliko maalumu
na Serikali ya Kenya kwenda
Nairobi kwenye sherehe za
ushindi.
Huo ukawa ndio mwanzo
wa Sheikh Yahya kufungua
ofisi katika jiji la Nairobi,
wa t e j a wa k e wa k u b wa
wakiwa wanasiasa na
viongozi mashuhuri nchini
Kenya.
Kadri siku zilivyoenda,
Sheikh alipanuka na
a k a wa n a o f i s i k u b wa

KUMBUKUMBU

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Sheikh Yahya Hussein-3

AL-MARHUUM Sheikh Yahya Hussein.


pale Government Road,
Nairobi na akanunua
jumba la kifahari maeneo
ya Kileleshwa, nje kidogo
(suburb) ya Nairobi.
K i l e l e s h wa n i k a m a
vile Beverly Hills, Laguna
Beach ama Bel Air kule Los
Angeles, California, ambako
huishi watu maarufu na
we n ye u we z o m k u b wa
(celebrities). Kamwe huwezi
kupafananisha na Masaki,
sijui Mbezi Beach ama
Oysterbay ya hapa kwetu.
Siku moja, katika miaka
ya 1970s, nikiwa mfanyakazi
pale Nairobi kwenye
Jumuiya ya Afrika Mashariki
ya zamani, kulifanyika
maonyesho makubwa ya
All Africa Trade Fair katika
viwanja vya Ngong.
Maonyesho hayo, kidogo
yanafanana na maonyesho ya
Sabasaba hapa kwetu. Rafiki
yangu, Alhaj Mohamed Said
(mwanahistoria maarufu
nchini) na mimi, tulitembelea
maonyesho yale na tukafika
hadi kwenye banda la Sheikh
Yahya.
Tu l i m k u t a S h e i k h
akitoa maelezo namna
anavyotabiria watu kuhusu
maisha yao kufuatana na
michoro ilivyo kwenye
viganja vyao vya mikono
(palmistry). Ghafla akapaza
sauti kuniita mimi nipande
pale jukwaani, ehe! Njoo
hapa we Mswahili, njoo.
N i l i i n g i wa n a w o g a
sana, nikajifanya sikusikia,
maana sikujua nini anataka
kunifanya mnajimu yule.
A l i p o n g a n g a n i a s a n a
ikabidi niende. Alichukua
mkono wangu akaunyanyua
juu na kuanza kuelezea nini
maana ya ile michoro iliyo
kiganjani mwangu.
Hii inaonyesha wewe
eh! utasafiri nchi za mbali na
kufika katika makontinenti
mengi duniani na utazuru

s e h e m u t a k a t i f u h a ya
nenda zako,alisema.
Niliondoka zangu na
kuyaacha nyuma matabiri
yale ya Sheikh Yahya. Wakati
huo sikuwa najua nchi au
mji wowote zaidi ya Nairobi
na Dar es Salaam kwetu
nilikozaliwa.
Miji kama vile Tanga na
Morogoro kwangu ilikuwa
ni miji ya mbali tu. Lakini
miaka kadhaa baadaye,
nilikuja kugundua tayari
nimeshatembelea sehemu
nyingi duniani na hivyo
kujiuliza, ala kumbe utabiri
ule umetimia!
Kwa schorlaship kutoka
ICAO, yaani Shirika la
Umoja wa Mataifa la Usafiri
wa A n g a , m wa k a 1 9 8 4
nilipelekwa katika Chuo cha
Usalama wa Anga (LENAC)
kule Toulouse, Ufaransa.
Nilipokuwa huko, nilipata
fursa iliyoniwezesha kufika
kwenye kituo kikubwa
cha setelilaiti duniani
kilichojulika kama SARSATCORPAS (Search and Rescue
Satelite).
Nilipanda pia ule mnara
wa kihistoria jijini Paris,
unaoitwa le Tourefel na pia
kuyashuhudia maonyesho
m a k u b wa ya m a d e g e
duniani ya Le Burget Air
Show.
Kama hiyo haitoshi,
mwaka 1988 mwandishi
alipata nafasi ya kujiunga na
Chuo Kikuu cha California
pale Los Angeles, na hivyo
kufika sehemu nyingi
maarufu kule California
ikiwamo Hollywood,
Beverly Hills, Las Vegas
pamoja na DisneyLand.
Nilikuwapo pia pale Rose
Bowl Stadium, Pasedina
kushuhudia fainali za
kihistoria za Kombe la Dunia
baina ya Brazil na Italy na
kumwona Robberto Baggio
akipaisha juu penati.

Nilitembelea pia nchi za


Mexico, Belgium Uingereza,
Spain, Sweden na Germany.
Lakini utabiri wa Sheikh
Yahya sikuanza kuuhisi,
hadi pale nilipojiona
nimesimama viwanja vya
Arafat pale Mecca kwa Ibada
ya Hijja. Sikuamini macho
yangu kwamba na mimi ni
miongoni mwa umati ule
uliokuwapo pale, mahali
ambapo baba yetu Adam
ndipo alipoungana tena na
mama Hawa tukazaliwa sisi
binadamu.
Sheikh Yahya hakuwa
mnajimu wa Afrika
Mashariki peke yake.
Alikuwa na ofisi London,
Lusaka na kule Mbabane
Swaziland, ambako mmoja
wa wateja wake alikuwa ni
mfalme Sobhuza aliyekuja
kumpa uraia wa heshima
wa nchi hiyo mnamo
mwaka 1990. Hii inaelezwa
na Hassan Yahya Hussein
aliyekuwa kaambatana na
babake nchini humo kikazi.
K a t i k a k u i s h i k wa k e
K e n y a , S h e i k h Ya h y a
aliishi kifahari sana hata
ikasababisha baadhi
ya wabunge wa nchi
i l e k u m w o n e a n g o wa .
Wa l i a n z i s h a m j a d a l a
bungeni wa kutaka Sheikh
Yahya afukuzwe nchini
kwao.
Hii mutu kutoka pande
ya Tandhania anatengeneza
pesa mingi sana na kunyonya
watu ya Kenya si akwende
kwao walisikika wabunge
wa Kenya wakilalamika.
Sheikh Yahya yalimfika
hayo kutokana na maisha
ya anasa aliyokuwa akiishi,
ikiwamo kuendesha magari
mapya mapya ya kifahari

(fleet of luxurious cars) na


namna alivyokuwa akiweka
mwilini mwake designer
suits (Pierre Cardin, Yves
Saint Lorrane, na mguuni
akiwa na kiatu cha Kitaliano
Bruno Magli) zilizokuwa
zikimkaa kwelikweli.
Sheikh Yahya alikuwa
mtu mkarimu na mwenye
huruma (compassionate) pia.
Kila asubuhi pale nyumbani
kwake Magomeni, alikuwa
akikutana na kuwasaidia
watu wasiojiweza misaada
mbalimbali ya kujikimu
kimaisha.
Daima dumu, wakati
akiwa jijini Dar es Salaam,
S h e i k h Ya h ya a l i k u wa
akifika katika hoteli maarufu
ya Shibam pale Magomeni
au Seiyun Hotel iliyoko
Kariakoo, ili kusalimiana na
watu. Akiwa hapo mara zote
huwa analipia watu wote
vyakula walivyokula.
Eh! eh! Waache wende
zao, wache wende tu
tutalipa, tutalipa sisi, hapan
shaka, Sheikh alikuwa
akisema, kumwambia
mwenye hoteli.
Hivyo, wakati huu
ambapo tunakumbuka na
kuenzi maisha na nyakati
za mtu huyu mashuhuri
ambaye ametangulia
mbele za haki na kutuachia
haiba (legacy) nyingi
sana, nashindwa kuelewa
ilikuwaje kiongozi wa serikali
akatoa amri na tingatinga
wa t u wa k a l i v u n j e v u j e
kaburi lake ati kazikwa
eneo la serikali ni ujahili
na majahili tu wanaoweza
kufanya ushenzi ule!
Tuseme tu: Allahuma
ghufirlahu; waarhamu;
wamaskanahu filjannah!
(Eh! Molla, mghufirie na
umsamehe madhambi yake;
umrehemu na peponi iwe
ndio maskani yakeAmeen.
(Mwandishi anapatikana
kwa Simu: 0715 808 864.)

Uhifadhi wa Mazingira na Uislamu

Inatoka Uk. 17
Ikiwa Waislamu tutaweza
kushikana na upandaji
wa miti, tutaiokoa dunia
pakubwa na janga la
mabadiliko ya tabianchi
kutokana na idadi yetu ya
watu bilioni 1.2 robo ya
idadi hii ikishikamana na
upandaji wa miti tutakuwa
tumeitendea haki dunia.
Khalifa wa Nne katika
Uislamu Syd Ali ibn AbiTalib katika kuuhisha maisha
na kujali mazingira aliwataka
waumini waungane naye
katika kuihuisha ardhi
i l i o k u wa h a i z a l i s h i n a
k u i g e u z a k u wa y e n y e
kuzalisha na kuwa endelevu.
Katika kulifanikisha
hilo alisema maneno haya
Shiriki kwa furaha ikiwa
wewe ni mwenye kufaidika
na matumizi ya rasilimali,
usiwe mwenye kufisidi
kuwa mwenye kupanda
vipando wala usiwe mwenye
kuangamiza.
Uislamu umesisitiza
p a k u b wa m a t u m i z i ya
rasilimali na mazingira

kuwa katika uangalifu wala


sio kati ya wale wafujaji,
maendeleo endelevu ndio
muongozo aliokuja nao
Mtume SAW ila Waislamu
wameupa mgongo,
k u n a h i t a j i k a Wa i s l a m u
kujizatiti katika matumizi
ya rasilimali tulizonazo kwa
uangalifu na hata zile P3
ikiwa Reduce, Recycle na
Reuse ikamanisha Punguza
matumizi, zirejeze mabaki
ya maliasili ulizozitumia
na uendelee kutumia vitu
ambavyo utaweza kuvitumia
bada ya kuvitupa.
Utapousoma Uislamu na
ukazama, utakuta maisha
yote yapo katika kujitakasa
na kujikurubisha kwa Allah
na kila ukiwa karibu na
Allah utakuwa sio mroho,
sio mharibifu wa kuleta
ufisadi na kuwa katika
upendo wa hali ya juu na
vilivyokuzunguka.
Tuyatunze mazingira kwa
kuweza kufanikiwa duniani
na akhera, Ameen.

19
MAMBO
matatu
yanapendekezwa kwa
mwenye kufunga: La
Kwanza, kuharakisha
kufuturu, baada ya
k u h a k i k i s h a k u wa j u a
lishatua. Hii ni kwa qauli ya
Mtume wetu Mpenzi s.a.w.:
" Wa t u h a w a t a a c h a
kuwa katika kheri wakiwa
wanaharakisha kufuturu".
(Imehadithiwa na Al
Sheikhan).
Na ameeleza Ibnu Hibbaan
kwamba:
"Alikuwa (Mtume wetu
Mpenzi s.a.w.) akiwa
kafunga, hasali mpaka
apelekewe tende mbichi
au maji, ale (tende-mbichi)
au anywe maji, ikiwa siku
za baridi; hasali mpaka
tumpelekee tende au maji".
Kutokana na Hadithi
hii, inapendekezwa siku za
baridi kufungua kinywa kwa
tende au maji, na siku za joto
kwa tende-mbichi au maji.
Hivi ni kwa vile kitu kitamu
kinatia nguvu mwilini na
maji yanasafisha mwili.
Na amesema Al Rauyany:
"Asipopata tende, basi kwa
kitu kitamu chochote kwani
Saumu inapunguza nguvu
za macho, na tende hurejesha
nguvu za macho, basi kitu
kitamu huwa mahala pa
tende".
La Pili, kuakhirisha
(kuchelewesha) kula daku.
Hivi ni kwa Hadithi ya
Mtume wetu Mpenzi s.a.w.:
"Hakika kuakhirisha daku
ni miongoni mwa sunna za
Mitume". (Imehadithiwa na
Ibnu Hibbaan).
Na imepokewa pia
kwamba:
"Hautaacha umati wangu
kuwa katika kheri wakiwa
wanaharakisha kufuturu na
wanaakhirisha kula daku".
(Imehadithiwa na Ahmad).
Hikma ya kuakhirisha
kula daku ni kumpa mtu
anaefunga nguvu za kufanya
ibada, katika kutafuta riziki
na ibada nyengine za kutwa.

Na Mussa Ame
RAMADHAN huingia
kwa kuonekana mwezi 29
Shaaban au kumaliza siku
thelathini za Shaaban.
Amesimulia Ibnu Umar
(r.a) kutoka kwa Mtume
(s.a.w) amesema, Msifunge
mpaka uonekane mwezi na
msifungue mpaka uonekane
mwezi (Muttafaq SB 1906
SM 1080).
Hadithi Muttafaq ni ile
iliyokubaliwa na Bukhari
kwa kuwemo katika Sahihi
Bukhari (SB) na Muslim
kwa kuwemo kwenye Sahihi
Muslim. (SM).
Amesimulia Abii Hurayra
(r.a) amesema Mtume (s.aw.),
Fungeni kwa kuonekana
mwezi na fungueni kwa
kuonekana mwezi, na kukiwa
na mawingu timizeni siku
thelathini (SM1081).
Amesema Ibnu Hajari
Asqalaany katika sherhe ya

Makala

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Yenye kupendekezwa katika Saumu

Sunna ya daku hupatikana


kwa kula kitu kidogo au hata
maji. Imehadithiwa na Ibnu
Hibbaan kwa Hadithi ya
Mtume wetu Mpenzi s.a.w.:
"Pateni sunna ya (kula)
daku, japo kwa funda la
maji".
Wakati wa daku ni tangu
baada ya nusu ya usiku
mpaka kabla ya alfajiri.
La Tatu, kujiepusha na
maneno machafu. Ikiwa
m a n e n o h a y o ya t a m t i a
kwenye madhambi, basi
ni haraam kuwa nayo, na
ni waajib kujiepusha nayo,
kama vile kusema watu,
kusengenya, kusema
uwongo, na ya mfano wa
haya. Yote haya ni maneno
machafu na yanapoteza
thawabu. Hivi ni kwa Hadithi
ya Mtume wetu Mpenzi
s.a.w. yenye maana kama hii:
"Asiewacha maneno
machafu na kuyatumia, basi
Mwenyezi Mungu Mtukufu
hana haja ya yeye kuwacha
chakula chake na maji yake".
Na Hadithi nyengine ya
Mtume wetu Mpenzi s.a.w.
(inasem):
"Huenda ikawa aliyefunga
a s i we n a k i t u ( a s i p a t e
thawabu) katika Saumu
yake hiyo isipokuwa njaa, na
huenda anayesimama usiku
(kusali) asiwe na kitu (asipate
thawabu) katika kisimamo
c h a k e h i c h o i s i p o k u wa
kukesha". (Imehadithiwa na
Al Haakim).
Siku Zenye Kuharamishwa
Kufunga
Inaharamishwa kufunga
siku ya Idi-l-fi'tri na siku ya
Idi Al-Adh-ha (Idi ndogo
na Idi kubwa)". Hivyo ni
kwa mafunzo ya Mtume
wetu Mpenzi s.a.w. kama
ilivyoelezwa hapa:
"Amekataza Mtume wetu
Mpenzi s.a.w. kufunga katika
siku mbili - siku ya 'Idi Alfi'tri

na siku ya 'Idi-l-adh-ha".
Kufunga katika siku
mbili hizi ni haraam, sawa
ikiwa ni Saumu ya fardhi,
au ya sunna, au ya kafara,
au ya nadhiri. Vilevile
imeharamishwa kufunga
siku za (tashriiq), nazo ni
siku tatu baada ya siku ya
kuchinja. Siku ya kuchinja
ni mwezi kumi wa mfunguo
tatu. Kwa hivyo siku za
"tashriiq" ni mwezi kumi na
moja, kumi na mbili na kumi
na tatu wa mfunguo tatu.
Mtume wetu Mpenzi s.a.w.
amekataza kufungu siku
hizi kwa sababu hizi ni siku
za furaha (siku za idi), siku
za kula, kunywa na kuzidi
kumtaja na kumshukuru
Mwenyezi Mungu Mtukufu
kwa nema zake juu yetu.
Kwa yule mtu aliefanya
(Hija tamatu'i) ni mtu
kufanya 'Umra kisha akatoka
katika ihraam akapumzika,
kisha akahirimia Hija. Huyu
anatakiwa atoe sadaqa kwa
kuchinja, akiwa hana uwezo
wa kuchinja afunge siku
tatu wakati yuko Makka na
siku saba akirejea nchini
kwao. Yeye inajuzu kufunga
katika hizi siku za tashriiq
kama ilivyokuja kwa Qauli ya
Mwenyezi Mungu Mtukufu:
", basi mwenye
kujistarehesha kwa kufanya
Umra kisha ndio akahiji,
basi achinje mnyama aliye
mwepesi kumpata. Na asiye
pata, afunge siku tatu katika
Hija na siku saba mtakapo
rudi, hizi ni kumi kaamili
". (Al Baqara : 196).
Na katika Hadithi za Imam
Al Bukhary r.a. kutokana na
Hadithi ya Sayyidah 'Aisha,
Mama wa Waumini r.a. na
Ibni 'Amri r.a. wamesema:
"Haikuruhusiwa kwenye
siku za tashriiq kufunga
isipokuwa kwa yule aliyekosa
mnyama wa kuchinja".

Qauli hii ameichukuwa


Imam Al Nnawawy r.a. na
kuitumia.
Kufunga Siku ya Shaka
Siku ya shaka ni mwezi
ishirini na tisa Shaabani
kuingia ama mwezi mosi
Ramadhani, au mwezi
thalathini Shaabani.
Imeharamishwa kufunga
siku hii sunna isiokuwa na
sababu. Vilevile ni haraam
kufunga siku hii kuwa ni
Ramadhani; hivi ni kwa qauli
ya 'Ammaar bin Yaasir r.a.:
"Mwenye kufunga siku
ya shaka, amemu'asi Abal-Qaasim, yaani (Mtume
wetu Mpenzi s.a.w.)".
(Imehadithiwa na Al
Bukhary).
Na kama ataweka nadhiri
kufunga siku ya shaka, basi
haitasihi. Lakini hii siku
ya shaka ikisadifu ikawa
ni katika siku anazofunga
sunna zake za kawaida,
basi haiharamishwi kwake
yeye kufunga hio siku yenye
kusadifu kuwa ni siku ya
shaka. Hivi ni kwa qauli ya
Mtume wetu Mpenzi s.a.w.:
"Msiitangulizie
Ramadhani kwa kufunga
siku moja au siku mbili,
isipokuwa kwa mtu ambaye
anakuwa akiifunga siku
ile, yeye naaifunge siku
ile". (Imehadithiwa na Al
Sheikhan).
Vilevile kwa yule mwenye
kuunganisha ile siku ya shaka
na siku ya kabla yake, hivi
haiwi kafunga siku ya shaka.
Hukumu ya Kuingilia
Mchana wa Ramadhani
Kwa mwenye kuingilia
mchana katika mwezi wa
Ramadhani, inalamzim
k a f a r a k u b wa , n a y o n i
kuwacha huru mtumwa
Muislamu, asipopata, afunge
miezi miwili mfululizo, ikiwa
hawezi alishe masikini sitini
chakula cha kawaida cha nchi

na Mashekhe wake na Ibn


Mundhir na Jamhuur ya
Maulamaa wameona kuwa,
ukithibiti kuonekana mwezi
wa Ramadhani nchi moja ni
wajibu wa Waislamu wote
duniani wafunge, kwa vile
hadithi zimekuja kwa wingi
wa watu, yaani fungeni
kwa kuonekana mwezi, na
mwenyewe Mtume (s.a.w)
aliamrisha watu kufunga
kwa kuonekana mwezi na
bedui, mtu wa mbali wala
hakuzingatia masafa.
Amesimulia Ibnu Umar
(r.a) waliuona watu
mwezi, nikampa khabari
Mtume (s.a.w) kwamba
mimi nimeuona mwezi,
alifungua na akaamrisha
watu kufungua.(D 23342)
Na hoja hii ya kuandama
mwezi popote na wakafunga

watu wote, ndiyo hoja ya


M a u l a m a a we n g i z a i d i
( Jamhuur ) na urahisi wa
m a wa s i l i a n o k wa s a s a ,
unaipa hoja hii nguvu zaidi,
kwani Abdallah Ibnu abbas
(R.A), katika hoja yake,
hakuitaja hiyo hadithi ya
M t u m e ( s . a . w ) wa l i v y o
amrishwa, alisema tu hivi
ndivo tulivyoamrishwa.
Inasihi kwa mwezi
wa kufunga Ramadhani,
ushahidi wa mtu mmoja
muadilifu, kwa hadithi ya
Mtume (s.a.w) kwamba
alikuja bedui akasema mimi
nimeuona mwezi, akasema
Mtume (s.a.w) unashuhudia
kwamba hapana mola ila
Allah (s.w)?, unashuhudia
kuwa Muhammad (s.a.w)
ni Mtume wake?, akasema
naam , akasema Mtume
( s . a . w ) e we B i l a l i ( r . a )
waamrishe watu wafunge
kesho. (T691 D2340 Mj 1652
). Hadithi hii ameisahihisha
Hakim na Ibnu khuzaymah

Kuingia Ramadhani
Bukhari hadithi (SB 19061911).
Wa m e k h i t a l i f i a n a
Maulamaa kuhusu watu
wa nchi za mbali kufunga,
kwa kufuata muandamo wa
nchi nyengine Kundi moja
limesema kila nchi wauone
mwezi wa mji wao nao ni
Kassim, Ikrimah, Salim na
Ishaaq. Na ameitoa hadithi
Imamu Tirmidhy ya kisa cha
Qurayb inayotoa ushahidi
wa hoja hiyo, pale Abdillah
Ibni Abbas(r.a) alipokataa
mwandamo wa mwezi wa
Sham yeye akiwa Madina,
na akasema hivi ndivyo
tulivyoamrishwa (SM1087
D 2332 T 693).
Na kundi jengine ni
kundi la Malik , Ahmad bin
Hambal, baadhi ya watu
wa Shafiy, Imaam Qurtubiy

alioko. (Atafanya hivyo,


yaani kulisha masikini,
kwa kutoa thamani ya
chakula hicho). Haya
ni kwa qauli ya Mtume
we t u M p e n z i s . a . w .
kama ilivyoelezwa na Al
Sheikhan:
"Mtu alikwenda kwa
Mtume wetu Mpenzi s.a.w.
akasema: "Nimeangamia".
A k a u l i z wa n a s . a . w . :
"Nini kimekuangamiza"?
Akajibu: "Nimemuingilia
mke wangu katika
Ramadhani". Mtume
s.a.w. akamuuliza:
"Unacho cha kukombolea
mtumwa"? Akajibu: "Sina".
Akaulizwa: "Unaweza
kufunga miezi miwili
mfululizo"? Akajibu:
" S i we z i " . A k a u l i z wa :
"Unacho cha kuwalisha
masikini sitini"? Akajibu:
"Sina". Kisha akakaa
kitako akaja Mtume
wetu Mpenzi s.a.w. na
kikapu ndani yake mna
tende, akamwambia towa
sadaqa hii. Akasema yule
mtu: "Nitowe kumpa alie
faqiri kuliko sisi, Wallahi!
Hakuna karibu na kwangu
nyumba yenye kuhitajia
hizi tende zaidi yetu sisi".
Mtume wetu Mpenzi s.a.w.
akacheka mpaka magego
yake s.a.w. yakadhihiri,
kisha akamwambia:
"Nenda kawape ahli yako
wale".
H a d i t h i
h i i
imetufahamisha ya
kwamba faqiri mwenye
kulazimikana na kutoa
kafara inajuzu kuitumia
kafara hio kwa kuwapa
watu wake wa nyumbani.
(Imenukuliwa kutoka Kitabu
cha Fiqhi Iliyowepesishwa
kilichoandikwa na Farouk
Abdalla Al-Barwani.)
na ikadhaifishwa na Albany ).
Amesema Tirmidhy
kuwa Maulamaa wengi,
wa m e k u b a l i a n a j u u ya
ushahidi wa mtu mmoja kwa
kufunga, na hivyo ni kauli
ya shafi, Ahmad na Abuu
Hanifa na Ibnu Mubarak na
ndiyo kauli ya Jamhuur ila
Ishak anasema pasifungwe
ila kwa ushahidi wa watu
wawili.
Ama mwezi wa kufungua
(mfunguo mosi), itathibiti
sikukuu kwa kuonekana
mwezi, kwa watu wawili
waadilifu, kwa hadithi sahihi
kuwa walikhitilafiana watu
mwisho wa Ramadhani
wakaja mabedui wawili,
wakashuhudia mbele ya
Mtume (s.a.w) kuuona
mwezi jana jioni na
akaamrisha Mtume (s.a.w)
watu wafungue na waende
katika viwanja vya kusali
Iddi. ( D.2339 amesahihisha
Albany).

AN-NUUR

20

MAKALA

20

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Tafrani Segerea

AN-NUUR

SHAABAN 1436, IJUMAA JUNI 12-18, 2015

Safari ya Hijja Hijiria 1436

Tanzania Muslim Hajj Trust, uandikishaji unaendelea,


gharama za Hijja ni US Dollar 4400, tarehe za Safari ni:
11 na 13 Septemba, kurudi 7 Oktoba, 2015.
Wahi kujiandikisha sasa
Kwa mawasiliano: +255 222 182370
0754 261910; 0717 000065
+255 222181577
0784 272723
0786 383820
website-www.hajjtrust.or.tz
0713 764636

E-mail:info@hajjtrust.or.tz

Ustadh Salum Ally alala juu ya mti


Amtaka Mwanasheria Mkuu Zanzibar
Sheikh Farid aitwa kuepusha balaa

Na Bakari Mwakangwale
K AT I K A h a l i i s i y o ya
kawaida, mtuhumiwa wa
kesi ya Ugaidi, Ustadh
Salum Ally, amepanda
juu ya mti mrefu uliopo
eneo la ndani ya gereza la
Segerea, Jijini Dar es Salaa
na kugoma kushuka.
Haikuweza kufahamika
mara moja iwapo lengo la
mtuhumiwa huyo lilikuwa
kujirusha afe au nini.
Hata hivyo alipoulizwa
alisema kuwa haoni tena
sababu ya kuishi katika
mgongo wa ardhi kutokana
na mambo machafu
aliyofanyiwa akiwa
mikononi mwa vyombo vya
Dola.
Mtuhumiwa huyo aliye
m s h i t a k i wa n a m b a 1 4 ,
amechukua uamuzi huo
Jumanne wiki hii majira ya
mchana na kuleta tafrani
ndani na nje ya gereza hilo
kufuatia taarifa kuenea
kupitia simu na mitandao
ya kijamii.
Akiongea kwa njia ya
simu akiwa eneo la tukio
hilo, Katibu wa Kamati
ya M a a f a ya S h u r a ya
Maimamu, Ustadhi Ally
Mbaruku, alisema juhudi
za kumshawishi ashuke
z i l i g o n g a m wa m b a n a
kwamba mpaka anaondoka
eneo hilo majira ya saa 12,
jioni alikuwa bado hajashuka.
Ust. Mbaruku, alisema
u s h a w i s h i wa k u m s i h i
ashuke kutoka juu ya mti
s i k u h i y o ya J u m a n n e ,
ulishindikana na kuamua
kumuacha na kusubiri
majaliwa yake atakapoamua
mwenyewe.
Naye mjumbe wa Kamati
hiyo, Ust. Hassan Kayagali,
alisema, walifika gerezani
hapo katika kawaida yao
ya kuwapelekea mahitaji
Waislamu hao, lakini hali
waliyoikuta hapo iliwastua.
Tulipofika tuliambiwa
mmoja kati yao, Salum Ally
Salum, ameamua kupanda
juu ya mti uliopo ndani ya
eneo la Gereza la Segerea, hali
ambayo imewastua na juhudi
za kumshusha kwa kutumia
nasaha zimeshindikana.
Alisema Ust. Kayagali.

Alisema, mtuhumiwa
huyo, amekuwa akisema
kuwa hana haja ya kuendelea
kuishi katika mgongo wa
ardhi kutokana na mambo
aliyofanyiwa na namna kesi
yao inavyocheleweshwa bila
sababu za msingi.
Kwa mujibu wa Ust.
Mbaruku, ameelezwa
gerezani hapo kuwa huenda
Ust. Salum, ameamua
kuchukua hatua hiyo ikiwa
ni muendelezo wa migomo
inayoendelea miongoni
m wa wa t u h u m i wa h a o
kushinikiza madai yao
mbalimbali ambayo tayari
wameshayatoa.
Hata hivyo imeelezwa
kuwa Ust. Salumu, ameshuka
Jumatano (wiki hii) kufuatia
juhudi za Sheikh Farid Hadi,
kufanya kazi ya ziada ya
kumnasi ashuke mtini baada
ya kupewa fursa ya kwenda
katika eneo la mti huo.
Ni kwamba, Ustadhi
Salum, alilala juu ya mti, jana
(jumanne) aligoma kabisa
kushuka, lakini asubuhi ya
leo (Jumatano) ameshuka,
baada ya Sheikh Farid,
kumnasihi sana. Alisema
Ust. Mbaruku.
Alisema, wakati anashuka,
Ust. Salum, alieleza kuwa
anashuka kwa heshma ya
kiongozi wake ambapo
baada ya kushuka, Sheikh
Farid aliwanasihi Waislamu
kuendelee kuwa na subra,
nasaha ambazo ziliungwa
mkono na Mama mzazi
wa Ustadh Salum, ambaye
alifika mapema asubuhi
Gerezani hapo.
M a m a ya k e a l i k u j a
gerezani asubuhi na
a l i k u t a n a n a m wa n a e ,
ambapo alimnasihi kwa
kumtaka awe na subira
kuliko kuchukua maamuzi
ya kujidhuru, kwani Allh
(SWT) yupo pamoja naye.
Alisema, Ust. Mbaruku,
akirejea nasaha za mama
Salum.
Ust. Mbaruku, alisema
miongoni mwa madai
wanayodai Waislamu hao
n i k u p a t i wa m a t i b a b u
sambamba na kufanyiwa
uchunguzi wa kina wa afya
zao kutokana na mambo
wa l i y o f a n y i wa wa k i wa

mikononi mwa maafisa wa


Polisi.
Aliyataja madai mengine
kuwa ni kutaka kuonana
na Mwanasheria Mkuu
wa Zanzibar pamoja na
Mwanasheria Mkuu wa
Tanzania Bara.
Ust. Salim amechukua
hatua hiyo, siku moja baada
ya siku ya Jumatatu wiki hii
akiwa na wenzake wengine
kugoma kushuka katika
gari la Magereza kuingia
ndani ya Mahakama ya
Kisutu, wakidai kuchoshwa
na kupigwa danadana kwa
kesi yao, hatua iliyofanya
kesi hiyo kusomwa wakiwa
nje ya Mahakama.
Matukio hayo mawili
yametanguliwa na kwenda
sambamba na mgomo wa
kula chakula kwa baadhi ya
watuhumiwa wa kesi hiyo
gerezani humo.

SHEIKH Farid Hadd.

MWANASHERIA Mkuu
Wa Zanzibar Saidi Hassan

Wakati huo huo, kesi ya


Sheikh Ponda Issa Ponda,
imeahirishwa hadi Juni 25,
2015, katika Mahakama ya
Mjini Morogoro, ambapo
baada ya kusimama kwa
muda mrefu sasa itaanza
kusikilizwa tena.
Aidha, kesi inayomkabili
Imamu Hamza wa Jijini
Mwanza, nayo imeahirishwa
mpaka Juni 25, 2015,
itakaporudi katika hatua ya

kusikiliza shahidi, upande


wa mashitaka.
Imamu
Hamza
anakabiliwa na mashitaka
matatu, shitaka la kwanza
likiwa ni uchochezi, la
pili anadaiwa kutoa kauli
inayoumiza imani nyingine,
kwa kusema tunakoelekea
ni kuzuri kuja kuuwana na
Makafiri na shitaka la tatu
ni kushawishi kutenda kosa.

semina ya pamoja kati ya


viongozi wa dini, jeshi la
polisi, Tume ya Uchaguzi
katika semina iliyofanyiwa
Wa w i K i s i wa n i Pe m b a
iliyoandaliwa na Jumuiya
ya M a i m a m u Z a n z i b a r
JUMAZA na UKUEM kwa
ufadhili wa Mtandao wa
Kimataifa wa Kidini kwa
Watoto (GNRC) ambayo
imewashirikisha watu 45
kutoka wilaya zote za Pemba.
Akisoma maazimio
walioafikiana katika
semina hiyo, Sheikh Said
Omar Said kutoka UKUEM
Pemba amesema viongozi
hao wametaka dini zipewe
nafasi na heshima yake
inayostahiki ili kujenga jamii
tulivu inayoishi kwa amani
na kuheshimu tofauti zilizo
miongoni mwa raiya wote
nchini.
Wamesema, uchaguzi ni
mchakato unaojumuisha
taasisi nyingi ikiwemo Tume

ya Uchaguzi, Taasisi hizo


zitambue kuwa ni zenye
jukumu (masul), hivyo
zitende haki na zionekane
zikifanya hivyo.
Kwa upande mwingine,
Jeshi la Polisi lilipongezwa
na wanasemina na kuombwa
lisirudishwe linakotoka kwa
kutumiliwa bali liendelee
kulinda Usalama wa Raiya,
kama ambavyo limekuwa
likifanya siku za karibuni.
Sheikh Said amesema,
washiriki hao wamesema
imani ya wananchi
kwa viongozi wa dini ni
kubwa hivyo basi Taasisi
za kidini zipewe nafasi
inayotambulika ili zifuatilie
mwenendo mzima wa
uchaguzi mkuu na kutoa
ushauri unaofaa kila dalili
zikiashiria kuhitajika ushauri
huo kwani kinga ni bora
kuliko tiba.

Masheikh Zanzibar waihimiza


serikali kutenda haki kwa wote
Na Salma Alghaithiyyah,
Zanzibar

VIONGOZI wa Dini ya
K i i s l a m u wa m e i o m b a
serikali kutenda haki na
uadilifu katika kutoa haki
k wa wa n a n c h i b i l a ya
ubaguzi wa aina yoyote.
Wa m e s e m a k w a m b a
amani haipatikani bila ya
haki, hivyo basi ni wajibu
haki kupewa nafasi yake
kwani kutambua haki na
wajibu walionao raiya kwa
nchi yao, ni moja katika sifa
muhimu za viongozi.
Viongozi wa Dini ya
Kiislamu Pemba wanaiomba
S e r i k a l i ya M a p i n d u z i
Zanzibar kuwapatia
wananchi haki zao za msingi
ikiwemo vitambulisho vya
Mzanzibari Mkaazi, na haki
ya kushiriki katika kupiga
kura ili kuepusha dhulma
kwa wanao stahiki.
Hayo yameelezwa katika

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

You might also like