Professional Documents
Culture Documents
ARTICLE 13-(a-c);16(1-6)
Maeneo ya matumizi yameelezwa kwa kutajwa vipengele mbalimbali.Hata hivyo
napendekeza kuwe na sekta za kipaumbele za matumizi ya pesa
inayokusanywa(priority sectors) inayolandana na mpango wa miaka 5 wa
ARTICLE 17(2-A,B)
Muswada unapendekeza pia kususpend fiscal rules za pesa zinazotokana na
mafuta na gesi pale ambapo kutakuwa na matukio ya majanga na baadaye
kuripoti katika bunge matumizi hayo.
Hii ni hatari sana kwa kuzingatia kuna scandal nyingi sana zimetokea hapa nchini
kwa pesa kutumika vibaya kwa visingizio vya usalama waTaifa na hata majanga ya
njaa.Kuripoti bungeni sio njia nzuri ya kudhibiti matumizi haya bali kudhibiti nani
anaidhinisha ndio njia nzuri Zaidi.Hata kama majanga huwa ni ya dharura
napendekeza kamati ya bunge mojawapo(mfano:ya huduma za jamii) ndio ipewe
mamlaka ya kujadili na kupendekeza jambo flani kuwa limekidhi kigezo cha kuwa
janga na kukubali matumizi yafanyike.
Bila kufanya hivyo ni kutoa mwanya kwa matumizi mabaya na baadae zitaletwa
ripoti zilizojaa ufundi wa kupikwa na pesa zitakuwa zimeshaliwa wakati huo na
pekee kitakachofanyika ni kujiuzulu kwa viongozi wakati Taifa litakuwa
limeshapata hasara kubwa sana.
ARTICLE 18(4,5)
Taarifa zimeeleza zitachapishwa katika gazeti la serikali na pia kupatikana katika
mitandao ya serikali na wizara ya fedha.Ni muhimu kuwa wazi kuwa taarifa hizi
zitachapishwa kila baada ya muda gani au wakati gani mfano:Kila mwisho wa
mwaka wa fedha au kila baada ya miezi mitatu baada ya bodi kukutana.
Bila kufanya hivyo ni kutoa mwanya wa kisheria kwani hata wakikaa mwaka
mzima hawajachapisha na wakaisoma bungeni tu mwananchi wa kawaida
ananyimwa nguvu ya kudai taarifa hiyo.Tukumbuke kuwa kufichwa kwa taarifa
ndio imekuwa nguzo kuu ya kuficha maovu hapa nchini.Sheria iweke muda
maalumu wa kuchapishwa taarifa hizo ili wananchi tuweze kuzidai.
ARTICLE 20(1-5)
Napendekeza utaratibu wa ukaguzi wa mahesabu uhusihe kamati ya PAC pia.Hii
itasaidia kama kamati maalumu ya bunge kupata nafasi ya kupitia kwa undani(to
scrutinize) mapato na matumizi hayo kabla hayajafikishwa bungeni.Kuwasilishwa
ukaguzi huo mara baada ya kupitia kwa waziri peke yake ni kutoa muda finyu wa
kujadili na kupata mambo kwa undani.
Napendekeza kutokana na umuhimu wa mapato haya ripoti yake ipitie utaratibu
kama wa mashirika ya umma kwa kuzingatia kuwa hizi ni pesa za umma
zinazotokana na rasilimali zetu.Kamati ya PAC ihusike na yenyewe ndio iwasilishe
taarifa hiyo bungeni na sio waziri husika kama ilivyo katika utaratibu wa
uwasilishwaji wa hesabu za mashirika ya umma.
Naomba Kuwasilisha,