You are on page 1of 1

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

Simu ya Upepo : N G O M E
Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463
Sanduku la Posta 9203,
Telex
: 41051
DAR ES SALAAM, 21Julai,
2015.
Tele Fax
: 2153426
Barua pepe
: ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti
: www.tpdf.mil.tz
Taarifa ya kifo kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika
kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali Dismas Stanslaus Msilu
(mstaafu) kilichotokea tarehe 19 Julai, 2015 katika Hospitali Kuu ya
Jeshi Lugalo.
Brigedia Jenerali Dismas Stanslaus Msilu (mstaafu)
alizaliwa tarehe 24 September 1938 katika kijiji cha Mlolo, Kata ya
Tanangozi, Wilaya ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa.
Alijiunga na
masomo ya Shule ya msingi na Sekondari na kuhitimu mwaka 1959.
Marehemu Brigedia Jenerali Dismas Stanslaus Msilu
alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 01 Julai
1975. Alistaafu utumishi Jeshini tarehe 23 September 1993.
Marehemu Brigedia Dismas Stanslaus Msilu ameacha mke
na watoto. Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe
22 Julai 2015 kuanzia saa 1:30 hadi 2:00 asubuhi katika Hospitali Kuu
ya Jeshi Lugalo na mazishi yatafanyika Mkoani Iringa tarehe 23 Julai
2015.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
BRIGEDIA JENERALI DISMAS STANSLAUS MSILU (MSTAAFU)
AMINA
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756 342279

You might also like