You are on page 1of 3

MAISHA MAGIC BONGO

IMEFIKA!
CHANELI MPYA INAYOZINDULIWA NA M-NET
KUWALENGA WATANZANIA.
Kampuni inayoongoza kwa burudani barani Afrika, M-Net inazindua chaneli
mpya yenye kulenga watanzania, itakayokuwa na burudani mbali mbali
zenye hadhi ya Kitanzania, ni MAISHA MAGIC BONGO itakayoanza
kuonekana hewani Octoba 1 saa 10 Alasiri. Moja ya madhumuni ya M-Net
ni kuhakikisha inalifikia soko la wateja wake ikiwemo kuingiza maudhui
wanayopenda wateja wake. Chaneli hii mpya inategemea kukidhi mahitaji
ya soko la wateja wa Tanzania.
Ikihusisha vipindi zaidi ya 6 vitakavyokuwa vikiruka kila siku, MAISHA
MAGIC BONGO itakuwa inapatikana kwa wateja wote wa Afrika Mashariki
kupitia chaneli 160. Mbali na kuonyesha filamu kali kutoka Bongo Muvi na
tamthilia za Kiswahili zinazopendwa na kufatiliwa nchi nzima, chaneli hii
pia itakuwa ikionyesha vipindi vya maisha ya wa Tanzania, Muziki
ukiwemo Bongo Flava , Maisha ya Mastaa na vipindi vya majadiliano ya
moja kwa moja , bila kusahau sinema kali za kihindi kutoka Bollywood
zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.
Akizungumza juu ya uzinduzi wa 'MAISHA MAGIC BONGO, Mkurugenzi wa
M-Net kwa Afrika Mashariki Theo Erasmus anasema, " Tumefurahi kufunua
mkondo huu mpya na kwa kuendelea mbele tunatarajia chaneli hii
itakuwa moja ya chaneli pendwa zaidi Tanzania kwa msaada wa
watazamaji wetu wa Tanzania ambao daima wamekuwa waaminifu kwetu
na ndio sababu M-Net leo tumeamua kuwaletea chaneli hii mahususi kwa
ajili yao.
Tunashukuru zaidi tumeweza
kupata baadhi ya vipindi bora kutoka kwa wazalishaji wakubwa kutoka
ndani ambao wanashirikiana nasi, pia tunaangalia namna ya kupanua
ushirikiano wetu zaidi na wazalishaji hawa wa filamu na vipindi vya
runinga ili kuhakikisha kwamba mafanikio yao yanakuwa makubwa zaidi.
Ni mwezi sasa, tangu DStv ilipotangaza kwenye maonyesho ya maudhui
nchini Mauritius, MAISHA MAGIC BONGO ipo tayari kuzinduliwa, na baadhi
ya vipindi vitakavyokuwemo kwenye chaneli hii ni:

Filamu za kibongo zitaonyeshwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa


saa 17:00 jioni, pia Jumamosi na Jumapili saa 19:30 usiku. Wakati
1

huo huo Filamu za kihindi zilizotafsiriwa kwa Lugha ya Kiswahili


zitakuwa zinaonyeshwa kila siku ya Ijumaa saa 19:30 usiku. Baadhi
ya Bongo Muvi maarufu zilizopo kwenye ratiba sasa ni Hard Price,
Jimmy, Nampenda Motika na Nusra, na baadhi ya za kihindi ni I am
24, Jimmy, Anwar na Amar Akbar Anthony.

Upande wa Tamthilia , jiandae kupata Talaka ( Jumanne saa 19:00


usiku ), usikose Mtaro ( Jumatatu saa 19:00 usiku) Isiyopitwa na
muda Siri ya Mtungi ( Jumamosi na Jumapili saa 18:00) na ya vijana
zaidi Dunia Tambara Bovu ( Ijumaa saa 19:00 usiku). Wasanii wenye
vipaji waliopo kwenye tamthilia hizi ni kama vile Hamis Korongo ,
Alafa Arobain , Paulo Francis, Juma Rajab Rashid, Hidaya Maeda,
Daudi Michael, Caroline Hussein na Habibu Seif na wengine wengi,
hakika hii si ya kukosa!

Bila shaka, MAISHA MAGIC BONGO pia itakuletea vipindi viwili vya
muziki, Mzooka (Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 Alasiri) itakupa
burudani ya video mpya kali kutoka Bongo, wakati kipindi cha Sifa
Mix kitakuwa kikikujia ( kila Jumapili saa 11:00 asubuhi) ikikuletea
muziki laini wa nyimbo za Dini.

Pia kuna vipindi majadiliano utaviona kwenye chaneli hii, kama vile
Mkasi ( kila Jumapili saa 16:00 EAT ) ambazo inazungumzia maisha
ya wasanii wakubwa Tanzania, kisha hakikisha hauachi kumfuatilia
Mboni (Jumamosi saa 15:00 EAT) Mboni Masimba akifanya
mahojiano na watu mashuhuri , wajasiriamali, viongozi wa jamii na
siasa , kujadili mada mbalimbali kuanzia utamaduni wa kiuchumi.

Pia kwenye MAISHA MAGIC BONGO, usikose kuangalia kipindi cha


Ajabu, kinachoburudisha na wakati mwingine kuogopesha lakini
muda wote kitakuburudisha (Jumatano saa 19:00 Usiku).

Kwa kusherehekea uzinduzi wa Maisha Magic Bongo, DStv inafurahi


kuwatangazia punguzo la bei kwenye vifaa vyake kuanzia tarehe 1 Oktoba
2015. Vifaa vya DStv sasa vitapatikana kwa Tshs 79,000 tu, vigezo na
masharti kuzingatiwa.
Hii ni kuwawezesha waTanzania kuangalia chaneli mpya ya Maisha Magic
Bongo itakayopatikana kwenye vifurushi vyote, ikiwemo kifurushi cha
Bomba ambacho ni Tshs 23,500 tu kwa mwezi.
Hivi pamoja na vingine kibao ambavyo si vya kukosa kwenye chaneli hii
mpya, hakikisha unaangalia MAISHA MAGIC BONGO kuanzia usiku wa leo!
Tembelea tovuti www.maishamagic.tv kwa maelezo zaidi.
Mwisho.
Wasiliana na:
Barbara Kambogi
Meneja Uhusiano
2

MultiChoice Tanzania
Barua Pepe: Barbara.Kambogi@tz.multichoice.com
Simu: +255784818797

You might also like