You are on page 1of 2

TAARIFA KWA UMMA

Yah: WATANZANIA TUTAMBUE AMANI YETU NI FAHARI


YETU (KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI)
Ofisi
ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, pamoja na
majukumu yake ya msingi, inayo pia jukumu la kuhakikisha
ukuaji wa demokrasia unakuwepo kulingana na sheria, kanuni
na taratibu zilizowekwa kikatiba. Ukuaji wa
demokrasia
hauwezi kuwepo kama wananchi ambao ndio wafuasi wa
vyama vya siasa wanakuwa na uelewa mdogo juu ya ushiriki
wao kwenye siasa za kistarabu na zenye staha.
Ndugu Watanzania, mbali na tahadhari zinazotolewa katika
kipindi hiki cha kampeni kumekuwepo na viashiria vya uvunjifu
wa Amani miongoni mwa jamii yakiwemo baadhi ya makundi
ya wanachama, wafuasi na mashabiki wa vyama vya siasa.
Makundi hayo yanadiriki Kutoa maneno ya kejeli, matusi,
kuvamia, kupigana hata kujeruhi makundi mengine ambayo
siyo ya upande wao. Hali hii budi iachwe mara moja ili kuiweka
nchi yetu ya Tanzania katika hali ya amani na kuiepusha nchi
yetu kuingia kwenye vurugu, mfarakano
na machafuko
yasiyokuwa na ulazima wa kutokea.
Ni vyema Watanzania tutambue kwamba utofauti wa itikadi wa
vyama ndio ukomavu wa demokrasia nchini hivyo ni jambo la
busara kuvumiliana na kufanya siasa za kistaarabu. Kipindi hiki
ni cha mpito tu tusikiruhusu kikavuruga amani yetu kwani kuna
maisha baada ya uchaguzi na mwisho wa uchaguzi huu ndio
mwanzo wa chaguzi zingine kama hizi.
Kila mmoja wetu kwa nafasi yake hajachelewa kuhakikisha
kuwa nchi yetu inabaki salama. Kutovumiliana kwa utofauti
wetu wa itikadi za kisiasa kunaweza kuleta madhara makubwa
kwa jamii itakayopelekea idadi kubwa ya watanzania kupata
athari ikiwemo ulemavu, vifo, ukimbizi, njaa na maradhi.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inaamini kuwa, Viongozi wa
kisiasa wanao ushawishi mkubwa kwa wafuasi na mashabiki wa
vyama vyao. Tumieni nafasi hii kusisitiza Amani. Dhamana ya
nchi hii iko mikononi mwenu, ushawishi wenu kuhusu amani
katika kipindi hiki ndio utakaoliokoa taifa letu la Tanzania ama

italiingiza taifa katika vurugu na mfarakano. Nawaasa na


kuwataka viongozi wote wa Vyama vya Siasa kutoa kauli na
maelekezo kwa wafuasi na wanachama wa vyama vyao
kutoshiriki katika aina yoyote ile ya uvunjifu wa Amani. Tumieni
vyema dhamana ya uongozi mliopewa na mwenyezi Mungu
kuivusha salama Tanzania yetu.
Natoa rai kwa Waaandishi wa Habari, tumieni kalamu zenu
vyema kuhubiri Amani. Epukeni kuandika habari za uchochezi
bali
wasaidieni
Watanzania
kupata
taarifa
sahihi
zitakazowasaidia kufanya maamuzi kuchagua viongozi wao.
Msikubali kalamu zenu zikawa chanzo cha mfarakano na vurugu
bali ziwafanye muwe mabalozi wazuri wa amani.
Mwisho natoa wito kwa watanzania wote. Dumisheni Amani na
kamwe tusijiingize kwenye siasa zinazoleta mfarakano na
uvunjifu wa Amani. Kumbuka kuna maisha baada ya uchaguzi
na Amani ya Nchi yetu ni fahari yetu sote.
Mungu ibariki Tanzania

You might also like