You are on page 1of 2

MTANDAO WA MASHIRIKA YANAYOTETEA USAWA WA KIJINSIA NA HAKI ZA

BINADAMU(FemAct) NA WANAHARAKATI NGAZI YA JAMII (GDSS)


UTEUZI WA BARAZA LA MAWAZIRI
TAARIFA KWA UMMA
19TH DECEMBER 2015
Sisi Mashirika tuanaotetea usawa wa kijinsia, demokrasia na maendeleo na wanaharakati ngazi ya jamii (GDSS)
tuanapenda kutumia nafasi hii kuwapongeza Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa rais wa
awamu ya tano na makamu wake Mheshimiwa Samia Suluhu kuwa makamu wa rais wa kwanza mwanamke.
Kadhalika tunampongeza Mh. Raisi kwa jitihada anazozionesha za kudhibiti matumizi mabaya ya rasilimali za
umma ikiwa ni pamoja na kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri.
Pamoja na hayo kama wanaharakati wa masuala ya jinsia tumeguswa na uteuzi wa baraza la mawaziri. Tunatarajia
kwa kupunguza baraza la mawaziri na kubana matumizi, fedha hzo zitatumika kuendelea kuboresha na kuimarisha
huduma za jamii ikiwemo maji, elimu na afya ya uzazi. Ijapokuwa ni jambo jema kupunguza idadi ya mawaziri
kama sehemu ya udhibiti wa matumizi ya serikali, tulitarajia kuwa uteuzi huu ungezingatia usawa wa kijinsia kwani
kati ya mawaziri 15 na manaibu waziri 15 walioteuliwa hadi sasa, wanawake ni wa 3 tu na manaibu wanawake ni
wa 5 tu sawa na asilimia 26.6 idadi ambayo imeshuka ukilinganisha na baraza lililopita.
Ikumbukwe kuwa Tanzania ni moja kati ya Mataifa yaliyosaini mikataba mbalimbali ya Kimataifa na Kikanda
inayoweka misingi ya usawa kwa binadamu ikiwemo haki na usawa katika ushiriki kwenye uongozi wa ngazi zote.
Moja kati ya Mikataba hiyo ni Tamko la Umoja wa Matifa la Haki za Binadamu(UDHR:1948), Mkataba wa
Kimataifa wa Kutokomeza aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW: 1979, Articles 7: a, b na c),
Mpango Kazi wa Beijing (1995), Mkataba wa Ziada wa Maputo, na Mkataba wa Nyongeza wa jinsia na Maendeleo
kusini mwa Africa (SADC Gender Protocol,) ambayo inaelekeza serikali husika kuhakikisha wanawake wanapewa
nafasi sawa na wanaume katika ngazi mbalimbali za uongozi.
FemAct na GDSS tunatoa rai yetu kwa Mhe. Rais kuwa, kwa kuwa bado zimebaki nafasi chache za uteuzi ili
kukamilisha baraza la mawaziri, uteuzi wa nafasi zilizobakia utazingatia usawa wa kijinsia ili kupunguza pengo
lililopo kuelekea usawa wa 50/50 katika nafasi za uongozi.
Aidha tunaendelea kuhimiza kuzingatiwa kwa usawa wa kijinsia katika teuzi nyingine zozote zijazo. Nafasi
nyinginezo ni pamoja na uteuzi wa Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya,
Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali, Wakurugenzi na Wakuu wa taasisi na
mashirika ya umma kadhalika uteuzi wa bodi mbalimbali katika mashirika na taasisi hizo bila kusahau teuzi katika
mhimili ya mahakama. Ni matarajio yetu kuwa, mamlaka za kiuteuzi ikiwa ni pamoja na Rais, Waziri Mkuu na
Mawaziri wa wizara mbalimbali zitazingatia kikamilifu usawa wa kijinsia katika uteuzi wowote utakaofanyanyika.
Kadhalika, tutahakikisha kuwa tunafuatilia kwa karibu teuzi zitakazofanyika.
Pili kama wananchi wa Tanzania tunathamini na kupongeza jitihada mbalimbali ambazo serikali inaendelea
kuzifanya katika kuboresha utendaji wake hususan kudhibiti matumizi mabaya ya kodi za wananchi kwa kupunguza
matumizi ya kawaida, safari za nje za watendaji wa serikali, kupambana kuziba mianya ya rushwa na kuongeza
juhudi za ukusanyaji wa kodi kutoka katika vyanzo mbalimbali vya ndani vya mapato.Hatua hii ni ya muhimu
katika kuleta maendeleo endelevu ya Taifa na hivyo kuwezesha watanzania wote kunufaika na rasilimali za nchi.
Pamoja na pongezi hizi, tunapenda kutoa angalizo kuwa jitihada hizi zitakuwa na manufaa kwa Taifa na
kuwanufaisha makundi yote ya kijamii endapo mianya yote ya rushwa na ukwepaji kodi itazibwa, na dhana za
uwazi na uwajibikaji wa watumishi wa umma na serikali zitasimamiwa na kutekelezwa ipasavyo kwa
kuwashirikisha wananchi. Tunasisitiza kuwa masuala hayo yafanyike kwa misingi ya haki na usawa. Hivyo
1

tunamtaka Mhe. Raisi kuhakikisha kuwa jitihada alizoanza zinakuwa endelevu hata baada ya muda wake wa kukaa
madarakani kwa kutengeneza mifumo mizuri ya uwajibikaji na uwajibishwaji wa watumishi wa serikali na wauma
kama ambavyo ameanza kufanya sasa.
Mwisho kama wanaharakati katika ngazi mbalimbali tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya tano
katika kuleta maendeleo ya Taifa letu na wananchi wake kwa ujumla, na tunamtakia Mh. Raisi na Makamu wake
pamoja na baraza la mawaziri mafanikio katika kipindi cha uongozi wao.

Imetolewa na,
Abdullah Othman
Mwenyekiti FemAct

Lilian Liundi

Seleman Bishagazi

Mkurugenzi Mtendaji, TGNP Mtandao

Mwakilishi wa Semina za Jinsia na Maendeleo

Mratibu, FEMACT

Kwa Niaba ya;


9.

1.

Life Skills Association (LISA)

2.

Tanzania Education Network (TENMET)

3.

Tanzania
(TCIB)

4.

Citizens

Information

Bureau

Journalists Environmental Association of


Tanzania (JE T)

Women Fighting
(WOFATA)

AIDS

in

10. Mburahati Queens FC


11. Youth Partnership Country Wide (YPC)
12. NETWO+
13. Taaluma Women Group (TWG)

5.

Binti Leo

6.

African Youth

7.

African Life Foundation

8.

Pwani - DPA

14. Sahiba Sisters Foundation


15. FORDIA

Tanzania

You might also like