You are on page 1of 20

Uzalishaji bora wa

mahindi

Matumizi sahihi ya mbolea na mbinu nyingine za kilimo nchini Tanzania

Chapisho hili ni pato kutoka mradi unaofadhiliwa na AGRA nchini Tanzania uitwao:
Scaling up Minjingu phosphate utilization for balanced fertilization of crops in Tanzania
Mradi wa kukuza matumizi ya mbolea za Minjingu fosfati na matumizi sahihi ya mbolea mbalimbali, Tanzania
na msaada kutoka Africa Soil Health Consortium ambayo inaratibiwa na CABI

Chapisho hili limeandikwa na:


This publication has been written by:
1
J.M.R. Semoka, 1N. Amuri, 2C.P. Msuya-Bengesi, 3S.T. Ikerra na 4I. Kullaya
1. Idara ya Sayansi ya Udongo, S. L. P. 3008, SUA, Morogoro, Tanzania
2. Idara ya Elimu na Ushauri wa Kilimo, S. L. P. 3002, SUA, Morogoro, Tanzania
3. Mlingano Agricultural Research Institute, S. L. P. 5088 , Tanga, Tanzania
4. Selian Agricultural Research Institute,
2 S. L. P. 6024, Arusha, Tanzania

Udongo
Udongo una rutuba ya asili yaani virutubisho katika udongo, mboji (organic
matter), na viumbe mbalimbali vinavyoishi kwenye udongo. Rutuba ya udongo
inategemea sana hali ya udongo kikemia, kibiolojia na kifizikia.

Makundi ya udongo
Kuna makundi makuu matatu ya udongo, kutokana na ukubwa wa
chengachenga za udongo:
Kichanga (Sand soil) - una uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na
unyevunyevu. Hivyo, hukauka upesi.
Tifutifu (Loam soil) - unahifadhi maji vizuri na upatikanaji wa maji na
virutubisho kwa mimea ni mkubwa.
Mfinyanzi (Clay soil) - unahifahdi maji mengi zaidi, bali upatikanaji
wa maji na virutubisho kwa mimea ni mdogo.
Vipimo vinavyoonyesha hali ya rotuba ya udongo ni:
Tindikali ya udongo
Kiasi cha mboji
Kiasi cha Naitrojeni, Fosfati, Potashi, Salfa, Chokaa (Calcium) na
Magnesium. Vilevile kiasi cha zinki, shaba, manganese na boroni
vinapimwa.

pH ya udongo (Soil pH)


pH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo.
Udongo waweza kuwa tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko
7), au katikati (neutral) - ph ya 7. Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa
kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya
tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0).
Mahindi hustawi kwenye udongo wa tifutifu wenye tindikali ya wastani na
virutubisho vya kutosha.

Mbolea
Mbolea ni chakula cha mimea, ambayo ni mchanganyiko wa virutubisho
mbalimbali vinavyoongezwa kwenye udongo au vinavyowekwa moja kwa moja
kwenye mimea ili kuongeza ukuaji na uzalishaji wa mimea.
Virutubisho hivyo ni pamoja na madini muhimu kama vile naitrojeni, fosfati na
potashi. Madini mengine ni pamoja na salfa, chokaa (calcium), magnesium,
boroni, shaba, chuma, manganese, molybedenum na zinki. Haya madini kwa
asili, yanapatikana katika udongo kwa viwango tofauti. Yanapopungua
kutokana na kilimo, inabidi yaongezwe kwa kutia mbolea.

Aina za mbolea

Kuna aina mbili kuu za mbolea ambazo ni:


1. Mbolea za asili (organic fertilizers)
2. Mbolea za viwandani (inorganic or industrial fertilizers)

Mbolea za asili (organic fertilizers)


Hizi ni mbolea zinazotokana na wanyama na mimea. Mbolea za asili ni kama
vile:
Mbolea vunde: inajulikana pia kama biwi au compost. Hutokana na
mchanganyiko wa manyasi au mabaki ya mbao na samadi na majivu.
Samadi: kutoka kinyesi cha wanyama kama mifugo na ndege.
Mbolea za kijani: hutokana na kupanda mimea aina ya mikunde
ambayo hukatuliwa na kuchanganywa na udongo.
Majivu: ni mbolea ya asili yenye madini aina ya potashi kwa wingi,
fosfati, chokaa na magnesium.
Matandazo (mulch): ambayo baadaye yakioza huwa mbolea.

Mbolea za viwandani (inorganic fertilizers)


Hizi ni mbolea zinazotengenezwa viwandani kwa kutumia virutubisho mbalimbali kwa kufuata viwango
maalum vilivyowekwa ili kukidhi mahitaji ya mimea. Mbolea hizi zinatengenezwa kwa lengo maalum la
kupata aina na kiasi fulani cha kirutubisho/ virutubisho vinavyohitajika na mimea.

Mbolea za kupandia mahindi


Mbolea maarufu za kupandia katika soko la Tanzania ni: TSP, DAP, Minjingu Phosphate na Minjingu
Mazao. Lakini zile ambazo zimechaguliwa kwenye mradi wa Kukuza matumizi ya Minjingu Phosphate
ni DAP, Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao.

Diammonium Phosphate (DAP)


Ina virutubisho viwili - naitrojeni ambacho kiko kwa kiwango cha asilimia 18, na fosfati (P2O5)
ambacho kiko kwa kiwango cha asilimia 46. Inapatikana katika hali ya chengachenga (granules).

Minjingu Phosphate
Ina kiwango cha fosfati (P2O5) asilimia 29 na inatumika zaidi kwa kutoa
kirutubisho hiki. Lakini inaongeza vilevile kirutubisho cha chokaa (calcium)
ambacho kipo kwa kiwango cha asilimia 40. Chokaa inasaidia vilevile kukabili
tindikali (acidity) ya udongo.
Minjingu Mazao
Hii ni mbolea mpya inayotokana na Minjingu Phosphate lakini imeongezwa
virutubisho vingine vitano ambavyo ni naitrojeni (10%), salfa (5%), zinki (0.5%),
shaba (0.5%), boroni (0.1%), pamoja na chokaa (25% CaO) na magnesium
(1.5% MgO). Virutubisho vilivyoongezwa hususani naitrojeni na salfa ni vile
ambavyo vinakosekana katika aina nyingi za udongo.
Zinki, shaba na boroni vimeongezwa kwa tahadhari kwa sababu vinaonyesha
dalili za upungufu katika baadhi ya maeneo. Minjingu Mazao iko katika hali ya
chengachenga.

Jinsi ya kuchagua mbolea ya kupandia


Mbolea za kupandia hasa Minjingu Phosphate na Minjingu Mazao zinahitaji hali
maalum ya udongo ili ziweze kufanya kazi vizuri.
Kwa mfano hali ya tindikali ya udongo inabidi iwe chini ya 6.2 ili mbolea za
Minjingu ziyeyuke kwa kiwango cha kutosha. Kwa udongo wenye tindikali zaidi
ya 6.2, tumia DAP wakati wa kupanda. Ikiwa kuna upungufu wa potashi, tumia
mbolea zinazorejesha madini hayo.
Tumia mboji pamoja na mbolea za viwandani ili kuongeza mazao. Mboji huwa
haibebwi na mvua na faida yake hudumu kwa muda mrefu. Mboji husaidia
udongo kuhifadhi maji na virutubisho. Zinapowekwa kwenye mashimo ya
kupandia mbegu ni vyema kufukia mbolea kabla ya kuweka mbegu
(kutenganisha mbolea na mbegu).

Dalili ya upungufu wa
virutubisho mbalimbali
1. Upungufu wa naitrojeni (Nitrogen)

Kwa ujumla mmea unakuwa mdogo, mwembamba na hutoa suke dogo, na


mwishowe hutoa mazao kidogo (picha A). Kama upungufu ni mkubwa sana
mmea unaweza usitoe mhindi kabisa.
Kupungua kwa kasi ya ukuaji wa mmea - ambayo husababisha
mmea kudumaa.
Rangi ya kijani kwenye mmea hufifia na kugeuka taratibu kuelekea
kwenye njano. Upungufu ukiwa mkubwa sana, majani hugeuka
rangi ya njano kutoka pembeni. Majani yaliyokomaa ndio huanza
kugeuka.
Majani ya mwanzo hukauka mapema kwenye mimea yenye
upungufu kuliko ile yenye naitrojeni ya kutosha.

2. Upungufu wa fosfati (Phosphorus)

Dalili ya kwanza ni kupungua kwa kasi ya kukua na mashina kuwa


membamba.
Upungufu ukiwa mkubwa, mmea unakuwa na rangi ya zambarau
(picha B). Rangi hii inaanzia pembeni mwa majani na kwenye
mashina na baadaye husambaa kwenye jani lote. Rangi inaonekana
vizuri zaidi upande wa chini wa jani.
Majani ya mwanzo hukauka mapema na mizizi haikui vizuri kwenye
mimea yenye upungufu kuliko ile yenye fosfati ya kutosha.

B
7

3. Upungufu wa potashi (Potassium)

Kupungua kasi ya ukuaji wa mimea, ambayo inasababisha mmea


kudumaa (picha C).
Upungufu ukiwa mkubwa rangi ya kijani inafifia na mwisho
kutoweka kabisa na sehemu iliyoathirika inakauka (necrosis)
kwenye mazao mengi km mahindi, mazao mengine ya nafaka na miti
ya matunda. Kutoweka kwa rangi ya kijani na kukauka
kunaanzia pembeni mwa majani na kwenye ncha. Majani yanakuwa na
michirizi ya manjano na vinundu nundu kama migongo ya bati
(yellowish streaks and corrugated).
Majani ya mwanzo hukauka mapema kwenye mimea yenye
upungufu kuliko ile yenye potashi ya kutosha.

Jinsi ya kuchagua mbolea ya kutumia

Kuandaa shamba, kupanda


na kupalilia
1. Kuandaa shamba, kusafisha, kulima/kutifua

Ni vyema mashamba yaandaliwe mapema kabla ya msimu wa kupanda


haujaanza ili kumpa mkulima fursa ya kupanda kwa wakati unaotakiwa.
Kuna njia mbalimbali zinazotumika kuandaa mashamba. Kati ya njia hizi ni
pamoja na kufyeka, kungoa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa
kutumia:
i). Jembe la mkono - wengi wanatumia
ii). Jembe la kukokotwa na wanyama kama ngombe
iii). Power tillers
iv). Matrekta
Matumizi ya trekta, power tillers na jembe la kukokotwa na wanyama
yanapunguza nguvu kazi kwani vinachimbua udongo na kuufanya kuwa tifutifu
(kufanya isiwe na mabonge makubwa, wala isiwe vumbi vumbi). Hii husaidia:
i). Mizizi ya mimea kupenyeza ardhini kirahisi
ii). Udongo kuweza kuhifadhi maji
iii). Udongo kuwa na hewa inayohitajika na mimea
iv). Ukuaji mzuri wa mimea hivyo kuongeza mavuno

2. Kupanda

Mbegu bora
Matumizi ya mbegu bora ni muhimu katika upatikanaji wa mavuno mengi na
bora. Kuna makundi mawili makuu ya mbegu ambayo ni:
i). Mbegu za asili: Ni zile ambazo zimetumika miaka mingi katika historia
ya kilimo
ii). Mbegu zilizoboreshwa: Hizi ni zile zilizoboreshwa kutoka mbegu za
asili. Kundi hili linagawanywa kwenye makundi mawili - composite
varieties na mbegu chotara (Hybrids).
9

Ushauri wa matumizi ya mbegu zilizoboreshwa unatofautiana kutoka eneo moja na lingine kwa
sababu ya:
i). Mwinuko kutoka usawa wa bahari
ii). Kiasi cha mvua katika eneo husika
iii). Muda unaotumia mbegu hadi kukomaa
Mbegu za mahindi zilizoboreshwa ni kama TMV1, TAN 250, TAN 254, Staha, Situka na zingine zote
zinazoanza na herufi H kama vile H 250, H 251 na H 615.

Jinsi ya kuweka mbolea za kupandia


Mbolea hizi zinawekwa shambani kabla ya kupanda/kusia mbegu. Zinawekwa kwa njia mbalimbali
kama vile kusambaza kwenye eneo husika na kuchanganya na udongo, au kuweka kwenye mistari au
mashimo ya kupandia. Ni bora zaidi kuchanganya mbolea za Minjigu Phosphate au Minjingu Mazao
na udongo kuliko kutia kwenye shimo la kupandia. Pia kuchanganya mbolea na udongo huondoa
athari za mbolea kwenye uotaji wa mbegu, hasa kama kuna uhaba wa unyevunyevu.
Viwango vya mbolea za kupandia
Kiwango cha mbolea za kupandia kilichopendekezwa ni kilo 20 fosfati (P) kwa hektari ambayo ni
sawasawa na kiasi cha aina mbambali za mbolea za kupandia kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali
namba 1.
Jedwali na. 1: Kiasi cha mbolea za kupandia kwa inayopendekezwa kwa eneo (hektari au ekari)
Aina ya mbolea za

Idadi ya mifuko ya kilo 50

Idadi ya mifuko ya kilo 50

kupandia

kwa hektari

kwa ekari

DAP

Minjingu fosfati

Minjingu Mazao

10

Viwango kwa kila shimo

Nusu kizibo cha soda


Kizibo kimoja cha soda
Kizibo kimoja na nusu cha soda

Muda wa kupanda
Muda wa kupanda unatofautiana kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na majira ya mvua. Kwa
mfano katika wilaya ya Morogoro tarehe za kupanda ni kuanzia februari 15 hadi Machi 15. Mkulima
anashauriwa afuate kalenda ya muda wa kupanda kama anavyoshauriwa na bwana shamba wake.
Kupanda kwa nafasi
Kupanda kwa nafasi ni kati ya njia bora za kilimo inayomwezesha mkulima kupata mazao bora. Hivyo
ni muhimu sana kuzingatia kupanda kwa mistari na kufuata nafasi zinazoshauriwa na wataalamu wa
kilimo. Kwa mfano nafasi zifuatazo zinaweza kutumika katika upandaji wa mahindi:
Nafasi

Idadi ya mbegu kwa kila shimo

Kiwango cha mbolea kutumia kizibo cha chupa

90 sm X 30 sm

90 sm X 25 sm

90 sm X 50 sm

* Nafasi hizi zote hutoa mimea 44,000 katika heka.

11

3. Kupalilia

Ni muhimu shamba lipaliliwe baada ya mimea kuota ili kuondoa magugu. Magugu ni mimea hivyo
hushindana na mimea iliyopandwa na mkulima kwa kunyonya virutubisho ardhini. Magugu yanaweza
pia kuhifadhi wadudu na magonjwa yanayoweza kushambulia mimea iliyopandwa na hivyo
kupunguza mavuno.

Mbolea za kukuzia
Ni mbolea zinazotumika baada ya mimea kuota kwa lengo la kuikuza mimea ili itoe mavuno bora.
Mara nyingi mbolea hizi zinatoa kirutubisho cha naitrojeni. Mbolea maarufu za kukuzia katika soko la
Tanzania ni kama:
AIna ya mbolea

Kiwango cha kirutubisho cha naitrojeni

Urea

46%

Calcium Ammonium Nitrate (CAN)

23%

Sulphate of Ammonia (SA)

21%

12

Urea inakirutubisho cha naitrojeni (N) kwa kiwango kikubwa na watu wengi wanauzoefu nayo. Vilevile
bei yake ni nafuu ikilinganishwa na mbolea zingine za kukuzia. Mbolea hii iko katika hali ya
chengachenga za mviringo (granules) za rangi nyeupe. Kiwango cha urea ni nusu kizibo cha soda kwa
kila shina.
Mbolea hizi hazidumu kwenye udongo kwa muda mrefu kwa hiyo huwekwa shambani wakati mimea
inapokuwa na mahitaji makubwa ya kirutubisho cha naitrojeni na wakati udongo una unyevunyevu na
shamba halina magugu.
Mbolea za kukuzia huwekwa kuzunguka kila shina la mimea au pande mbili au tatu au nne za kila
shina. Cha muhimu ni kwamba mbolea isirundikwe sehemu mmoja.

13

Viwango vya mbolea za kukuzia vinavyoshauriwa


Kiwango kinachopendekezwa ni kilo 60 naitrogeni kwa hektari, ambacho ni sawasawa na kiasi kama
inavyoonyeshwa kwenye jedwali namba 2. Mbolea inayotumika mara kwa mara ni Urea. Hata hivyo
mbolea zingine kama SA inaweza kutumika kama kuna mahitaji ya salfa. CAN inaweza kutumika kama
kuna mahitaji maalum ya nitrate na ammonium. Kwenye mahindi mbolea ya kukuzia inawekwa baada
ya palizi ya kwanza ambayo ni kama wiki tatu mpaka wiki nne baada ya kupanda.
Jedwali na. 2: Kiasi cha mbolea za kukuzia kwa inayopendekezwa kwa eneo (hektari au ekari)
Idadi ya mifuko ya

Idadi ya mifuko ya

kilo 50 kwa hektari

kilo 50 kwa ekari

Urea

Nusu kizibo cha soda

CAN

Kizibo kimoja cha soda

SA*

Nusu kizibo cha soda

Aina ya mbolea za kukuzia

Viwango

* Kiwango kilichowekwa hapa ni kwa ajili ya kupata kirutubisho cha salfa kinachosha - ambacho ni kilo 20 ya salfa kwa hektari. Na kupata sehemu
ya mahitaji ya naitrojeni ambyao ni kilo 21. Hii ina maana kwamba kilo 39 za naitrojeni inabidi ziwekwe kama Urea au CAN.

14

Mambo muhimu ya kuzingatia


Kuweka mbolea: Sehemu za nchi ambazo muda wa kukua mahindi ni mrefu (zaidi ya miezi mitatu),
ni vyema kuweka mbolea za kukuzia mara mbili, yaani nusu ya kiwango kinachopendekezwa baada
ya mwezi mmoja, na kurudia tena (kutumia nusu iliyosalia) baada ya wiki tatu.
Kupalilia: Katika kilimo cha mahindi, ni muhimu shamba lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea
kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda. Wataalamu wanashauri kwamba katika
kilimo cha mahindi, shamba lipaliliwe mara 2-3, kufuatana na hali ya magugu katika shamba.
- Utafiti unaonyesha kwamba, shamba la mahindi ambalo halijapaliliwa linaweza kupunguza
mavuno kwa asilimia 60 hadi 100 ya mavuno yanayotarajiwa. Hata kama mkulima atatumia
mbegu bora, aina na kiasi cha mbolea zinazoshauriwa, kupanda kwa mstari pamoja na mbinu
nyingine bora zinazoshauriwa, bila kupalilia hali hii itaathiri mavuno yake.

15

Kudhibiti magonjwa na wadudu


wanaoshambulia mahindi
Magonjwa yanayoshambulia mahindi
i) Maize streak virus (picha A)
Dawa/Kudhibiti: Mbegu bora inayostahimili ugonjwa, kupanda mapema,
kungoa mimea iliyoathirika ama kunyunyiza dawa za kuua vectors kama vile
inzi weupe (white flies).

ii) Smut (Fugwe) (picha B).


Dawa/Kudhibiti: Tumia Helerat ukifuata maagizo kamili.
iii) Cob rot (kuoza kwa mhindi) (picha C)
Dawa/Kudhibiti: Tumia mbegu zinazostahimili kuoza.

Wadudu na wanyama wanaoshambulia mahindi


i) Stalk borer (picha D)
Dawa/Kudhibiti: Tumia Malathion, sumithion, vumbi ya cymbush au Sevin 5G
na ufuate maagizo kamili.

ii) Cutworms (Vikata Shina) (picha E)


Dawa/Kudhibiti: Tumia Dragnet FT na ufuate maagizo kamili.
iii) Wanyama waharibifu (picha F)
Kudhibiti: Kuwatishia na kuwafukuza wanyama.

Ili mkulima aweze kupata mazao mengi na bora inashauriwa kutumia dawa za
kuzuia magonjwa na wadudu washambuliao mimea na njia zinginezo.

16

Kuvuna, kukausha, kusafisha


na kuhifadihi
Kuvuna

Mahindi yako tayari kuvuna wakati kikonyo kimekuwa dhaifu na mahindi


yanaangalia chini. Mahindi yakishakauka vizuri yanatenganishwa na bua halafu
majani ya mhindi kutolewa.

Kukausha

Kama mahindi hayajakauka vizuri hukaushwa zaidi katika juani siku 3-4 ili
kupunguza unyevunyevu kufikia kiwango kinachofaa kwa kuhifadhi (14%). Ni
muhimu mahindi yakauke vizuri ili yasioze yakiwekwa ghalani.
Ili kujua kama mahindi yamekauka vizuri, tia mahindi kadhaa kwenye chupa ya
soda iliyokauka na uongeze kiganja kimoja cha chumvi. Tingisha chupa halafu
uwache itulie kwa dakika tatu. Chumvi ikikwama kando ya chupa, basi mahindi
haijakauka vizuri.

Kusafisha
Mahindi yaliyokauka vizuri hupepetwa na vilevile mahindi mabovu huondolewa.

Kuhifadhi

Mahindi safi huchanganya na dawa za kuua wadudu kama vile Actellic Super
ambayo ni vumbi nyeupe na kisha kuhifadhiwa kwenye ghala.

17

Manufaa ya matumizi
ya mbolea
i). Kuongeza mavuno
ii). Ubora wa mazao
iii). Kuhifadhi rutuba ya udongo
iv). Kuongeza kipato kutokana na mavuno mengi na bora

Mambo muhimu ya kuzingatia

Ni muhimu kutumia mbolea za viwandani katika kilimo cha mahindi ili kumuwezesha mkulima kupata
mavuno mengi. Lakini ikumbukwe kwamba matumizi ya mbolea ni lazima yaambatane na matumizi ya
mbinu nyingine bora za kuzalisha mahindi, kama vile:
Kuandaa shamba
Matumizi ya mbegu bora
Kupalilia
Kupiga madawa ya kuzuia na kuua wadudu na magonjwa
Kuvuna kwa wakati unaostahili
Kuhifadhi vizuri mahindi

Kwa maelezo zaidi, muone au wasiliana na:


1. Bwana/bibi shamba wako.
2. Muuza pembejeo aliye karibu nawe.
3. Kitivo cha Kilimo, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, na taasisi zingine vya utafiti wa
kilimo kama Katrin, Ilonga, Mlingano na Selian (SARI).

18

Jedwali 1. Tafsiri ya matokeo ya vipimo vikuu vine vya upimaji wa udongo kwa ajili ya kilimo
Kipimo

pH ya udongo

Naitrojeni (N)
(%)

Kiwango

Ufafanuzi/tafsiri

Ndogo kuliko 5.5

Tindikali kali

5.5 hadi 7.0

Weka chokaa au tumia mbolea zisizo za tindikali kama


Minjingu fosfati au Minjingu Mazao kwa kiwango
kinachoshauriwa

Tindikali ya wastani Mimea mingi hushawi vyema katika udongo wenye pH


hadi katikati (neutral) hizi

7.0 hadi 7.5

Nyongo ya watani

Kubwa kuliko 7.5

Nyongo kali

Weka madini ya salfa

Ndogo kuliko 0.2

Kiasi kidogo

Kiasi hiki hakitoshelezi mahitaji ya naitrojeni kwa mimea.


Ni lazima kuweka mbolea ya kupandia yenye naitrojeni
kidogo (<20%N) na pia ni lazima kuweka mbolea za
kukuzia

0.2 hadi 0.5

Kiasi cha wastani

Kiasi hiki hakitoshelezi mahijaji ya naitrojeni kwa mimea


kwa msimu mzima. Mbolea za kukuzia zinahitajika ili
kukidhi mahitaji ya naitrojeni kwa uzalishaji mzuri

Kubwa kuliko 0.5

Kiasi kikubwa

Ndogo kuliko 15

Kiasi kidogo

15 hadi 25

Kiasi cha wastani

Chaweza kutosheleza mahitaji ya mimea kwa msimu


mmoja tu. Weka mbolea za kupandia kwa kiwango
kinachoshauriwa ili kuwa na uhakika wa mavuno mengi

Kubwa kuliko 25

Kiasi kikubwa

Haihitaji mbolea za kupandia kwa misimu miwili na


kuendelea kutegemea na wingi wa fosfati kwenye
udongo. Waweza kuweka kiasi kidogo tu cha mbolea za
kupandia (kwa mfano nusu au robo ya kiwango
kinachoshauriwa)

Ndogo kuliko 0.2

Kiasi kidogo

Weka mbolea za kupandia au kukuzia zenye potashi kwa


kiwango kikubwa (NPK 10-20-18 au 10-24-18)

0.2 hadi 0.4

Kiasi cha wastani

Kubwa kuliko 0.4

Kiasi kikubwa

Fosfati
(mg/kg)

Potashi
(cmolc/kg)

Mapendekezo/Ufafanuzi

Mimea mingi hushawi vyema katika udongo wa pH hizi

Kiasi hiki kinaweza kutosheleza mahitaji ya naitrojeni


kwa msimu mmoja. Mbolea za kukuzia zaweza kuwekwa
kwa kiwango kidogo
Weka mbolea za kupandia kwa kiwango
kinachoshauriwa

Kiasi hiki kinaweza kutosha kwa misimu miwili kama


mabaki ya mazao yataachwa shambani
Haihitaji mbolea ya potashi

*Ufafanuzi ni kutoka Landon (1991)

19

Chapisho hili ni pato kutoka mradi unaofadhiliwa na AGRA nchini Tanzania uitwao:
Scaling up Minjingu phosphate utilization for balanced fertilization of crops in Tanzania - (Mradi wa AGRA - 2009 SHP 016)
Mradi wa kukuza matumizi ya mbolea za Minjingu fosfati na matumizi sahihi ya mbolea mbalimbali, Tanzania
na msaada kutoka Africa Soil Health Consortium ambayo inaratibiwa na CABI
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,
Idara ya Sayansi ya Udongo
P. O. Box 3001, Morogoro, Tanzania
Tel.: +255 23 260 4 649
ISBN 978-9987-9673-5-3

Kufanya kazi kwa pamoja na wadau/wabia kutayarisha taarifa zinazohusu mbinu husishi za afya ya udongo

20

You might also like