You are on page 1of 1

Wanafunzi 208 wafundishwa na walimu wawili

http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=33451

HABARI MPYA

LA JANA

MATANGAZO

BEI ZETU

WASILIANA NASI

TUMA HABARI

jumatatu, 8 agosti 2011

1:02:38 PM

Yaliyopita

Pekua Tovuti

Wanafunzi 208 wafundishwa na walimu wawili

na Francis Godwin, Ludewa

MWALIMU mkuu na makamu wake katika shule ya msingi Mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Iringa wamelazimika kufundisha wanafunzi 208 wakiwemo wasichana 90 na wavulana 118 kutokana na tatizo la upungufu wa walimu. Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa habari za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP ) mkoani Iringa ulibaini tatizo hilo hatua ambayo inawapa wakati mgumu wanafunzi wa kike hasa wakati wanapougua na kuhitaji msaada. Ilielezwa kuwa upungufu mkubwa wa walimu katika shule hiyo ambayo inadaiwa kujengwa juu ya madini ya Mchuchuma na Linganga imechangia kusababisha wanafunzi wengi kufaulu huku baadhi ya wanafunzi wakilazimika kuacha shule. Mzazi Augustino Haule alisema kuwa pamoja na kusomesha watoto wawili katika shule hiyo, mtoto wa kike alilazimika kuacha shule kutokana na muda mrefu kutumia mitaani kutokana na walimu kutofundisha mara kwa mara. Haule alisema kuwa mbali ya walimu hao kuwa wachache, mazingira ya shule hiyo yanachangia watoto kuacha shule kutokana na muda mwingi kufanya kazi za kupika na kuchota maji ya walimu umbali wa zaidi ya kilomita 2 kutoka katika shule hiyo. Alisema kuwa ni vema serikali ikaifunga shule hiyo hadi pale itakapopata ufumbuzi juu ya tatizo la upungufu wa walimu kuliko serikali kuendelea kuwaacha wanafunzi zaidi ya 200 kufundishwa na walimu wawili pekee. Mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Joseph Lugome alithibitisha uhaba huo wa walimu katika shule hiyo na kuwa hadi sasa kwa zaidi ya wiki mbili anafundisha mwalimu mmoja kutokana na mwenzake kupata matatizo ya kiafya. Alisema kuwa katika shule hiyo wanafunzi 47 ni darasa la saba ambao wanangoja kufanya mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya msingi na kati ya wanafunzi hao wasichana ni 24 na wavulana ni 25 huku wanafunzi wa darasa la nne katika shule hiyo ni 10 pekee wasichana wakiwa 11 na wavulana 8. Afisa elimu wa wilaya ya Ludewa Robert Hyella alithibitisha kuwepo kwa tatizo la uhaba wa walimu katika shule za msingi ndani ya wilaya hiyo na kuwa shule zinazoongoza kwa upungufu wa walimu ni zile zilizopo pembezoni mwa wilaya hiyo.

juu

Habari Mpya

Matangazo

Bei zetu

Wasiliana nasi

Tuma habari

Webmaster

Copyright 2011 FreeMedia Ltd.


Wasomaji free media limited 2011 mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania simu +255-22-2126233 faksi +255-22-2126234 selula 0713 296570

hit counter

1 of 1

8/8/2011 1:02 PM

You might also like