You are on page 1of 3

SALA ZENYE THAWABU KUBWA MNO!

Ni siku ya Alkhamisi kuamkia Ijumaa Ina jumla ya Rakaa Mbili tu. Zinasaliwa kwa mpango ufuatao -: Unanuia Nawaitu Uswali Sunnat Lailat Jumaa Rakaa teen Lillahi Taala Allahu akbar.

Rakaa ya kwanza soma Surat Fatiha mara moja na Idhazulzilat mara 15 na Rakaa ya Pili soma Surat Fatiha mara moja na Idhazulzilat mara 15 baada ya kutoa salaam utasoma uradi huu:Yaa hayyu ya Kayyum Yadhaljalali wal ikram mara 100 Unamsalia Mtume s.a.w kwa idadi unayotaka Kisha unamaliza kwa kusoma surat Fatiha. FAIDA ZAKE KWA UCHACHE Mtume (S.A.W) amesema mtu (muislam) mwenye kutimiza sala na uradi huo Mwenyezi Mungu (S.W.) mwenyewe anamchukulia dhamana mtu huyo ya kumuepusha kutokana na adhabu zote za kaburi lake kama vile giza kali,wadudu, kutoulizwa maswali na malaika wawili (Munkar na Nakir) kaburi hupanuliwa pande zote kwa dhiraa 70 kaburi hujaa nuru tukufu, siku ya Kiyama mwili wa mtu huyo wote utang'aa kwa nuru kali ya kuwashangaza waumini wenzie (ambao hawakuweza kuifikia ibada hiyo ya usiku wa manane). Hapa duniani mtu huyo haumfikii umauti wake mpaka mwenyewe ALLAH ahakikishe ya kwamba tayari amekamilisha kumwandalia makazi mazuri ya Akhera yake yote kaburini,

Yeyote anayesema yafuatayo pale anapomwendea mkewe: Bismillahi, Allahumma jannibnash sh-shaytaana wa jannibish shaytaana maa razaqtana (Kwa jina la Allah, ewe Mola wangu niepushe na shetani na ukiepushe na shetani kile utakacho turuzuku). Basi wakipata mtoto shetani hatomdhuru kabisa milele (Al Bukhariy kutoka kwa Ibn Abbaas .)

HAKI ZA MUME KUTOKA KWA MKE

1. Mke ajue umuhimu wa kumtii mume wake kuwa ni jambo muhimu na kutokumtii ni jambo la hatari kwani hadithi inasema:

(())
Mtume kasema: Kama ningeliweza kumuamrisha mtu amsujudie binaadamu mwenzake, ningeliamrisha mwanamke amsujudie mume wake kwa jinsi haki ya mume ilivyo tukufu kwa mke wake. [Tuhfat Al-Ahwadhi 4.323 kutoka Tafsiyr ya Ibn Kathiyr]

2. Mke inampasa kumtimizia haja ya mumewe wakati wowote anapomhitajia kujimai naye, kwani kuna hatari kwa kutokumtii mumewe katika jambo hili kama ifuatavyo:

(())
Mume atakapomwita mkewe kitandani na akikataa mke, basi malaika watakuwa wanamlaani huyo mke mpaka asubuhi [Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy]

3. Kumhudumia mumewe kwa upole (yaani bila ya kujikalifisha zaidi ya uwezo wake)

4. Haimpasi mke kutoa sadaka kitu chochote bila idhini ya mumewe. Kasema Mtume

)) " ( (( - )
Asitoe sadaka mwanamke kitu chochote kutoka nyumbani ila kwa idhini ya mumewe. Wakasema ewe Mjumbe wa Allaah hata chakula? Kasema hicho ni

mali bora yetu. [Hadiyth imepokelewa na Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy kasema ni Hasan.] Ama mwanamke anayo haki kutoa sadaka katika kipato chake mwenyewe kisicho cha mumewe. Katika Hadiyth nyingine sahihi inatujulisha kuwa mwanamke anaweza kutoa sadaka ikiwa anatambua kuwa hatoghadhibikiwa na mumewe.

)) (( -
Kutoka kwa Hamaam kasema: Nimemsikia Abu Hurayrah kwamba Mtume kasema: Mwanamke akitoa sadaka kutoka katika kipato cha mumewe bila ya amri yake basi na yeye atapata thawabu nusu yake. [AlBukhaariy]

5. Haimpasi mwanamke kutoka nyumbani kwake bila ya idhini ya mumewe (hata kwenda kwa wazazi wake)

6. Haimpasi mwanamke kumfanyia ujeuri, ufedhuli au usafihi mumewe

) (
Kutoka kwa Abdur-Rahman Ibn 'Awf kasema: Kasema Mtume : Atakaposwali mwanamke Swalah zake tano, akafunga mwezi wake (wa Ramadhaan), akahifadhi sehemu zake za siri (asifanye uzinifu), akamtii mume wake, ataambiwa ingia peponi kupitia mlango wowote autakao. [Swahiyh at-Targhiyb]

Bila ya shaka baada ya kutimiza haki hizi, ndoa itakuwa yenye kudumu bila ya kuwa na matatizo makubwa ya kuiharibu au kuivunja.

You might also like