You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA)

TAARIFA KWA WAKANDARASI WANAOTEKELEZA MIRADI


YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI
Juni 16, 2017
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatambua kuwa baadhi ya wakandarasi
wanaotekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini hawajakamilisha miradi kwa
mujibu wa MIKATABA waliyosaini na Wakala (REA). Aidha, kuna baadhi ya
wakandarasi wamekamilisha miradi lakini hawajakabidhi rasmi miradi hiyo na vifaa
au hawajafanya marekebisho kasoro zilizobainishwa na wasimamizi wa miradi
kutoka (TANESCO na REA).

Kwa tangazo hili, Wakala unawataarifu wakandarasi wote ambao hawajakamilisha


matakwa hayo ya kimikataba kufanya hivyo mara moja. Wakandarasi
watakaoshindwa kutimiza masharti hayo hawataruhusiwa kushiriki katika zabuni
zitakazotangazwa na Wakala (REA) baada ya TANGAZO hili na hatua nyingine
zitachukuliwa juu yao kwa mujibu wa mikataba hiyo.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la Mawasiliano, Ghorofa ya 2
Barabara ya Sam Nujoma, 14414
S. L. P 7990
Dar es Salaam, Tanzania
Barua Pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003
Nukushi: +255 22 2412007

You might also like