You are on page 1of 1

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VY HABARI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO ) linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu


taarifa iliyoandikwa katika Gazeti la Mwananchi, la Tarehe 15 Juni, 2017
toleo no: ISSN 0856 -7573 NA. 6166 ukurasa wa 3 lenye Kichwa cha habari
Vifaa vya Mitambo ya Kinyerezi II hatarini kuuzwa , Taarifa hiyo si
sahihi na ni upotoshwaji, TANESCO inapenda kuufahamisha umma kuwa;

Mosi; Ujenzi wa Kituo cha kufua umeme kwa njia ya Gesi asilia cha Kinyerezi
II ambacho kinaendelea kujengwa, kinahusisha ununuzi na usairishwaji wa
mitambo mingi mikubwa kutoka nje ya Tanzania, kwa kutambua hilo
TANESCO imekuwa ikifuata taratibu zote za kisheria katika kufanya
manunuzi hayo ikiwa ni pamoja na kulipia kodi na usairishwaji wake hadi
kufika katika eneo la ujenzi wa mitambo hiyo.

Pili; Hadi kuikia MEI 2017 TANESCO tayari imekwisha pokea mizigo mingi
ikiwa ni pamoja na makontena zaidi ya 400 ambayo yamepokelewa katika
bandari ya Dar es salam tayari yamekwisha ikishwa katika eneo la
Kinyerezi, ili kuendelea na ujenzi. Mradi wa umeme wa Kinyerezi II
utapokea jumla ya makontena 900 na mizigo mingine mikubwa hadi kuikia
mwezi Agosti 2018

Uongozi wa TANESCO unapenda kuuhakikishia umma wa TANZANIA kuwa:


kazi nzuri ya Ujenzi wa Mitambo ya kufua umeme iliyozinduliwa na
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe
Joseph Magufuli, inaendelea kwa kasi kama ilivyo pangwa, pia ni matarajio
yetu kuwa Mitambo hii itakamilika kwa wakati ili kufanikisha azma ya
Serikali ya awamu ya Tano ya kuiikisha Tanzania katika uchumi wa kati wa
Viwanda.

Imetolewa na : OFISI YA UHUSIANO


TANESCO - MAKAO MAKUU.

You might also like