You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
Simu Na: +255 (026) 2963630 Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Nukushi: +255 (026) 2963629 na Utawala Bora,
Barua Pepe: ps@utumishi.go.tz Jengo la Taaluma Na. 1,
Tovuti: http://www.utumishi.go.tz Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
Barabara ya Mkalama,
S.L.P. 670,
40404 DODOMA.

TAARIFA KWA UMMA

WAAJIRI NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA MGAWANYO SAHIHI WA


RASILIMALIWATU

Waajiri nchini wametakiwa kuzingatia mgawanyo sahihi wa Rasilimaliwatu


katika Utumishi wa Umma ili kuwa na utendaji bora na wenye matokeo katika
utumishi wa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala


Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na
Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es
Salaam.

Mhe. Kairuki amesema mwajiri anapoomba kibali cha kuajiri watumishi ni vema
akazingatia mahitaji kulingana na majukumu yaliyopo ili kuondoa ziada ya
watumishi wa umma wasio na kazi kuendana na fani walizosomea kwa lengo
la kuwa na utendaji mzuri.

Ni vizuri sana wakati tunaomba vibali vya kuajiri watumishi wa umma


tukazingatia mgawanyo sahihi wa rasilimaliwatu katika maeneo yetu kulingana
na majukumu ya watumishi tunaowahitaji badala ya kuomba watumishi wengi
ambao wanasababisha kuwa na ziada ambayo haitumika ipasavyo Mhe.
Kairuki amesema.

Waziri Kairuki amesema katika vibali 10,184 vilivyotolewa hivi karibuni na Ofisi
ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa Mamlaka
za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala za Serikali, pamoja na
Taasisi na Mashirika ya Umma ili kujaza nafasi zilizoachwa na watumishi wa
umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, Halmashauri ya Manisapaa ya
Ubungo imetengewa jumla ya nafasi 140.

Aidha, ameongeza kuwa, Halmashauri hiyo imetengewa jumla ya nafasi za


ajira mpya 397 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hivyo zitendewe haki kwa
kuhakikisha watumishi watakaoajiriwa wanafanya kazi kwa mujibu wa mpango
uliopo.

Mhe. Kairuki yuko katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es salaama kwa
lengo la kukutana na watumishi wa umma na kusikiliza malalamiko, ushauri na
changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia
kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili kufikia malengo
yaliyopangwa na Serikali.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI


OFISI YA RAIS-UTUMISHI
17.07.2017

You might also like