You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA

Anuani ya Simu MKUUPOLISI Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,


Simu : (022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556 S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM .

18/ 07/ 2017

TAARIFA YA KWA VYOMBO VYA HABARI


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro, amefanya
mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni pamoja na
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa


Kinondoni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Suzan
Salome Kaganda amekuwa Mkuu wa kitengo cha Mafao na Fidia
Makao Makuu ya Polisi, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo ambaye alikuwa
kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga.

Aidha, Nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga


imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Simon Sylverius
Haule, ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu wa Polisi wa Mkoa wa Mara.

Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la


Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Imetolewa na:
Barnabus D. Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.

You might also like