You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu: 255-22-2114512, OFISI YA RAIS,


2116898 IKULU,
E-mail: press@ikulu.go.tz 1 BARABARA YA
Tovuti : www.ikulu.go.tz
BARACK OBAMA,
Faksi: 255-22-2113425
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha


Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Desemba, 2017
amekutana kwa mara ya kwanza na kamati maalum aliyoiunda kwa lengo la
kuhakiki mali za chama hicho, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kamati hiyo aliitangaza tarehe 20 Desemba, 2017 Mkoani Dodoma na inaongozwa


na Dkt. Bashir Ally.

Katika Mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli amewataka wajumbe wa kamati


hiyo kufuatilia na kuhakiki mali zote za chama, kumhoji mtu yeyote ambaye
atahitajika kutoa taarifa juu mali za chama na kubaini thamani ya mali, mahali
zilipo, makusanyo ya mapato na wanaozishikilia ama kutumia mali hizo.

Mhe. Rais Magufuli pia ametoa wito kwa wanachama wa CCM na wananchi
wengine kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zote zinazohusu mali za chama kwa
kamati hiyo, na watakaoitwa kuhojiwa waitikie wito huo.

“Nataka mali za chama zikinufaishe chama, nataka mkamhoji mtu yeyote,


awe kiongozi, awe mwanachama, awe mfanyabiashara, mtu yeyote.
Mkazihakiki mali zote ili chama kipate haki yake” amesema Mhe. Rais
Magufuli.

Akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo, Dkt. Bashiru Ally amesema kamati
imeanza kazi rasmi na ametoa wito kwa wanachama, wananchi na wote
wanaozitumia mali za chama kutoa ushirikiano watakapoitwa kuhojiwa.

“Tumezungumza na Mwenyekiti kwa karibu saa mbili, katueleza matarajio


yake, sababu za kuunda tume hii, kazi zake na faida zake kwa chama na
kwa nchi, kwa hiyo ametukabidhi vitendea kazi na taarifa mbalimbali na
ametueleza kazi yetu ni kuhakiki mali zote za chama kwa kushirikiana na
wanachama na wale wanaoshirikiana na chama kuzitumia hizo mali kama
vile wapangaji, wasimamizi, nakadhalika” amesema Dkt. Bashiru Ally.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Desemba, 2017

You might also like