You are on page 1of 14

Mazungumzo ya watu mbalimbali wakizungumza na sauti za pikipiki zikipita.

F:Ndio……mimi naitwa Justas Nsenga kutoka chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo….au wengine
tunasema…..wananiita Mwasenga.
P:Mwasenga…..Muhehe?
F:Aaaah….(kukataa)…..na….mimi….eeeeh(kushangaa)mimi Msukuma.
P:Msukuma!
F:Eeeeeh….(kukubali)
P:Msukuma?...na nyinyi mnatumia mwa….hiyo hiyo?
F:Nimee….nimepewahilo jina na Wahehe
P:Ooooh…(kushangaa)…Muhehe amekupa Mwasenga?
F:Eeeeh…(kukubali)
P:Aaaaaakh…..(kushangaa)
F:eeeh….(kukubali)
P:Aaaaah….(kukubali)..na sisi ndio tunaanziaga hivyo hivyo….mwa…mwa
F:Mwa…?
P:Eeeh….(kukubali)
F:Aaaaakh…..(kukubali)….na wewe unaitwa se….nani?
P:Semng’ong’o
F: Semng’ong’o?
P:Eeeeeh…(kukubali)
F:Jina lako la kwanza?
P:Christina
F: Christina!
P: Eeeh….(kukubali)
F:Wewe una….unaishi….umeanza kuishi hapa lini?......umezaliwa hapa hapa?
P:Mimi mzaliwa wa hapa hapa
F: Aaaaaakh…..(kushangaa)…..umezaliwa mwaka gani?
P:Mwka sabini na nne (74)
F:Nyumbani kwako wewe……mko wangapi?
P:Nyumbani?.....ninapoishi?
F: Eeeh….(kukubali)….wanakutegemea wewe
P:Nipo mimi na mume wangu na watoto wa…eeeeeh(kufikiria)….wa nne (4)
F:Watoto wako wa nne?
P: Eeeh….(kukubali)
F:Mzee nae ana miaka mingap?
P:Mzee?
F:Mmmh…(kukubali)….mmeo alizaliwa lini?
P:Alizaliwa mwaka sa…..sabini na sita(76)
F:Nani mkuu wa kaya?
P:Mume wangu
F:Naye alizaliwa hapa?...au…alii…
P: Eeeh….(kukubali)….wa hapa hapa
F:Wa hapa hapa?
P: Eeeh….(kukubali)
F:Kwenye mambo ya upandaji miti…..kuna….shughul nyingine mbali na hiyo ambayo
mnaifanya kwa ajili ya kupata mahitaji ya nyumbani…ama kama….kwa ajili ya kuendesha
maisha?
P:Aaaahk….(kukubali)….yeye ni mfanyabiashara wa…..
F:Mfanyabiashara?
P:Ndio
F:wa…?
P:wa mbao
F:Na wewe?
P:Mimi mkulima tu
F:Una…..una shamba lako mwenyewe….unamiliki la miti?
P:Shamba….ni shamba ambalo tunamiliki na mwenzangu
F:Huna la kwako….kama….kama wewe?
P:La kwangu mwenyewe?
F:Eeeehk…(kukubali)
P:Lipo
F:La kwako lipo?
P: Eeeehk…(kukubali)
F:Lina kama heka ngapi?
P:Kama heka moja …..lingine ndio la pamoja na mwenzangu
F:La kwako wewe lina heka moja?
P: Eeeehk…(kukubali)
F:Na lile ambalo….mna….mnamiliki…… ni kila mtu na shamba lake au ni hilo linguine linakuwa la
wote?
P:La wote tu
F:Ni lina heka ngapi?
P:Heka 3……we haya ni mashamba yale binafsi achana na yale ya kikundi
F:Ni binafsi
P:Aaaakh…(kukubali)
F:Kwa mfano hili la kwako wewe ulipata wapi?.....hii ardhi uliipata wapi?
P:Hii ardhi?
F: Eeeehk…(kukubali)
P:Nilipewa na wazazi wangu
F:Wakakugaia?
P: Eeeehk…(kukubali)
F:Au…..walikuazima tu ulimie alafu urudishe?
P:Hamna walinigaia…..mmmmh(kukubali)….yani kila wazazi baada ya muda fulani walipita, wanagaia
kila mototo shamba la kulima mahindi…..mmmh(kukubali)….baada ya kuona shamba lile limechoka sasa
….mmmmh(kukubali)…..ndio nikapanda miti
F:mmmmmmh…....(kukubali)na hizi heka 3 mnazomiliki kama familia nazo mlizipataje?
P:Hizi?.....mmmmh(kukubali)….tulinunua na mwenzangu
F;Mlinunua?
P: Eeeehk…(kukubali)
F: (Kelele za makaratasi)…..naaa…..mmeanza kupanda miti mwaka gani?....kwa mfano wewe umeanza
kupanda miti kwenye shamba lako hili mwaka gani?
P:Mimi?......mmmmh(kukubali)….miti yangu ina miaka…mii….miaka miwili
F:Mmmmkh….(kushangaa)
P:Eeeeh….(kukubali)
F:Na hili shamba ambalo mna….mnamiliki wote na mzee?
P:Miaka mitano
F:Miaka mitano!....hamjawahi kuvuna hata shamba moja?
P:Hatujawahi
F: Mmh….(kushangaa)
P: Eeeeh….(kukubali)
Sauti za makaratasi na watu wakizungumza kwa mbali.
F:Kwanini labda wewe….wewe una shamba na yeye ana shamba….isiwe tu labda zote mkasema ziko
pamoja hapa tunazimiliki wote?
P:aaakh…(kukataa)….yaani hiyo nimeongea kwa maana kwamba mimi wakati hilo shamba napewa
lilikuwa bado lipo mikononi mwa…shamba la familia …..aaaaah(kushangaa)….eeeeh(kukubali)….baada
ya mimi kuishi na yeye ndio pa….tukatafuta ardhi yetu wote kwa pamoja…..eeeeeeh(kukubali)….lakini
hata hilo shamba pia shughuli za shambani tunazofanya wote ka pamoja hata kama lip…..ni la kwangu
mwenyewe
F: Eeeeh….(kukubali)
P: Eeeeeeeh….(kukubali)
F:Na nini kilicho…kusukuma wewe kuwa na shamba la miti?
P:Mimi!
F: Eeeeh….(kukubali)…au nyinyi kama familia kuwa mnapanda miti?
P:Kupanda miti inafaida ….mmmmmh(kukubali)….faida yake hasa baada ya kuuza mnapata hela ya
kusomeshea watoto
F:Mmmh..(kushangaa)….sasa faida mmeijuaje na wakati mbona bado hamjaa….hamjauza?
P:Faida!....mmmmh(kukubali)…yani faida ninayoipata mimi kwenye hilo shamba
yani….mmmh(kukubali)….,kwa mfano hata waelimishaji wanaokuja kuelimisha juu ya upandaji wa
miti…..mmmmh(kukubali)…..wao wanapata nafasi….sehemu ya kwenda kujjifunzia shambani
kwako…..mmmmh(kukubali)…. kwamba miti wanapandaje …kuliko kwenda kwenye shamba mwingi
P:Eeeeh….(kukubali)
F:mmmmmh…(kukubali)….Naaa….mbegu wewe unapata wapi za kupanda kwenye shamba
lako?,…unapata wapi?
P:Mbegu!
F:mmmmh(kukubali)
P:Nawatika kitalu kidogo binafsi nyumbani
F:Mmmmh….(kukubali)
P: Eeeeh….(kukubali)
F:Mbegu za dukani au za wapi?
P:Aaaaaakh…(kushangaa)……mbegu tunatoa kwenye miti mingine….ambayo ishakomaa
F:Mmmmh….(kukubali)….naa…kwenye mgawanyo wa kazi ….mmmmh(kukubali)….sasa sijui
unafanyaje ….wewe kwenye shamba lako …..una shamba lako mwenyewe,shamba la familia,shamba la
chakula…. mgawanyo nani anapanga hapo ratiba….. nani afanye kazi wapi?
P:Ratiba inapangwa na mwenzangu, lakini naye anajua kwamba kuna shamba lingine lipo
pembeni….mmmmh(kukubali)….kwahiyo kazi zote zinakwenda kwa pamoja
F:Mmmmh…(kukubali)….we shambani kwako,kwa mfano kwenye wakati ule unaandaa shamba huwa si
tunaanza kwanza kufyeka … Eeeeh….(kukubali)…..nani alifyeka shambani kwako?
p:(sauti ya pikipiki)….niliweka watu kutusaidia kufyeka,nilimwambia kwanza mwenzio kwamba nina
shamba ambalo nimepewa….mmmmh(kukubali)….na familia akasema basi tuweke watu wafanye
nini…mmmh(kukubali)…..waandae hilo shamba
Kelele za kuandika kwenye makaratasina mazungumzo ya watu mbalimbali yakiendelea
F:mmmmmh…(kuguna)…kwenyeee…ukishafyeka…..labda ya kwenye kuchimba mashimo na kupanda
nani alifanya hiyo kitu ?
P:Tuli….tulifanya wote kwa pamoja na mwenzangu
F:Mlipanda wenyewe?
P: Eeeeh….(kukubali)
F:Watoto
P:Watoto wanakuwa wapo shuleni mara nyingi
F:(sauti ya pikipiki)….naa..kule ku..na..nii….ukishapanda kuna kazi gani nyingine?....mnafanyaga
kwenye shamba lenu la miti?
P: Tukishapanda!....Eeeeh….(kukubali)…..lazima kutengenezea visahani nini
F:Kutengenezea visahani!
P: Eeeeh….(kukubali)
F: Kutengenezea visahani hivi…nani anatengeneza?
P:Visahani….. Eeeeh….(kukubali)….tunatengeneza wenyewe
F:Wewe unashiriki kwenye kutengeneza visahani?
P: Eeeeh….(kukubali)
F:Mzee?...naye anashiriki?
P:Naye anashiriki kama anakuwa hajaenda …hajapata dharura ya kwenda labda
kazini….mmmh(kukubali)….au wapi tunakuwa wote
F:Naaa….kazi gani nyingine ambayo inafanyika kwenye shamba la miti humu….baada ya kutengeneza
visahani,inayofatia ni kazi gani?
P:Inayofatia ni kupruni miti
F:Kupruni?.... Eeeeh….(kukubali)…..kwenye kupruni anafanya nani?
P:Kwenye kupuni….Eeeeh….(kukubali)….ana…yani kwa mfano labda yeye ameenda kazini kwenye
biashara zake hizo…. Eeeeh….(kukubali)…..basi anatafuta mtu anaenda kupruni miti
F:Kazi gani nyingine inafatia?
P:Baada ya kupruni miti!
F:Eeeeh….(kukubali)…ile…. Hamna ile kutengeneza fire breaks sijui boundaries
P: Eeeeh….(kukubali)…ndio hiy fire break
F:Eeeeh….(kukubali)….anafanya nani…..anatengeneza hiyo?
P:Tunatengeneza wenyewe
F:Na mzee?
P: Eeeeh….(kukubali)
F:Watoto wanashiriki kwenye hii?
P:Watoto!...mmmh(kukubali)….siku ambazo,kwa mfano zile siku za likizo wana….tunashirikiana nao
pamoja
F:mmmmh…(kukubali)
P:mmmmh….(kukubali)
F:Naa….(sauti za kugonga kitu)….kuna…bado bado hatujaanza bado bado hatujaweza kuuza …si ndio/
P: Eeeeh….(kukubali)….bado
F:Na nini ambacho,kwa mfano kazi zile za kwenye shamba linguine ambalo
mnamilikiwote….mmmh(kukbali)…nalo utaratibu wake ukoje?...nani anayefanya kazi kule?
P:Yani hizo kazi… Eeeeh….(kukubali)…….wote mnazifanya kwa pamoja
F:kwa pamoja!
P:lakini wakati mwingine yeye akiwa labda ndio yuko safarini nini…mmmmh(kukubali)….inakuwa ni
vigumu nafanya kazi mimi mwenyewe
F:unafanya wewe mwenyewe?
P: Eeeeh….(kukubali)
F:au mnatumia utaratibu huo wa kutafuta vibarua tena…. Eeeeh….(kukubali)….kama huku
P:una tafuta mtu tena ananisaidia
F:manake nilikuwa naona kama una shamba lako… Eeeeh….(kukubali)…na una shamba la familia,…
Eeeeh….(kukubali)…mgawanyo wa kazi unaendaje hapo?…..nilikuwa najaribu kuona
inakuwaje?.......unawezaje hizi shughuli zote kuzimudu na shamba la chakula?
P;zaidi zaidi….mmmh(kukubali)….kabisa ndio huwa tunaomba watu tunasaidiana na mmi mwenyewe na
watoto….mmmh(kukubali)….naa…tunatafuta kijana mwingine yoyote yule aka….tusaidia
F:kwenye shamba lipi?
P:kwenye hilo shamba la pamoja
F:la pamoja!
P: Eeeeh….(kukubali)
F:naaa…labda…kuna miezi gani ambako unakuwa na kazi nyingi sana….,za miti hapo nyumbani kwako
na mambo ya shamba labda zinagongana?
P:kuanzia mwezi wa…kuanzia mwezi wa pili ule….mmmmh(kukubali)…kuna kuwa na kutengenezea
visahani,…mmmmh(kukubali)…kufyekelea mshamba ya miti na kupalilia shambani mahindi yanakuwa
muda tayari wa kupalilia
F:mmmmmh…(kukubali)
P: Eeeeh….(kukubali)…hapo kazi zinakuwa zipo nyingi
Sauti za watoto wakilia na mazungumzo ya watu kwa mbali
F:mmmmh…(kukubali)…kwa hiyo sasa hapo kazi zikiwa nyingi huwa mnafanya nini?......mnafanyaje
kukabiliana nah ii kitu?
Jibu lilichelewa kidogo kutolewa;
F:huwa mnafanyaje?
P:tunaenda nazo hivyo hivyo kiugumu ugumu
F:mmmmh…(kushangaa)
P:mmmh…(kukubali)
F:kiugumu ugumu?.... Eeeeh….(kukubali)…..kiugumu ugumu ndio unaa….
P:kiugumu ugumu kwamba yani unafanya kazi hapa kidogo,mara unaenda uta….uta… leo utapalilia siku
mbili tatu…mmmh(kushangaa)….unaacha tena kupalilia unaenda hata kwenye miti hivyo
hivyo….mmmmh(kushangaa)….unatafuta mtu unampa ….unampa hela kidogo anakusaidia
F:huku hakuna ile….migohe?
P:aaaakh….(kukataa)…migohe sahizi …mmmh(kushangaa)…ilikuwa zamani siku hizi haipo migohe
kweli
F;kwanini hamna?
P:sielewi,sijui ni kwa nini….naona hiyo sahizi inazidi kupotea migohe,lakini miaka ya nyuma kulikuwa
na migohe
F:mmmh….(kushangaa)
P:eeeeh…(kuitika)
Mazungumzo ya watu yanaendelea kwa mbali na watoto wakipiga kelele
F:kwanini?....kwa sababu ya nini?.....(jibu lilichelewa kutolewa)…..unafikiri ni kwa sababu gani
imeondoka migohe,hatuitumii?.....mmmmmh(kushangaa)…..imekufa lini hii migohe?....(ukyima wa
kutoa majibu ukazidi kuendelea)…..eti dada Christina?.....eeh(kuitika)…..migohe umeona …miaka
ganiilikuwa ipo,miaka gani imepotea?
P:migohe kwenye kumbukumbu yangu mimi….kuanzia miaka….miaka ya…95
ile…mmmhh(kushangaa)…96….97 migohe ilikuwepo…lakini huku miaka ya huku mbele naona migohe
inazidi inazidi kufanya nini….mmmmh(kushangaa)…inazidi kupotea na wazee wetu wa zamani ndio
walikuwa wanaitisha zaidi migohe….mmmh(kukubali)…sahizi hivi….vijana yani….. walio….huu ni
wakati nani….hawaitishi migohe
F:mmmmh (kukubali)…naaa kwenye utaalam wa kilimo cha miti….eeeeh(kuitika)….kwa mfano
kutengeneza hiyo nini?
P:visahani
F:visahani….eeeh alafu kutengeneza fire brake…una…unapanda kwa mistari au unapandaje?
P:napanda kwa mstari
F:unatumia mbali gani?
P:umbali!.... Eeeeh….(kukubali)…kati ya mti hadi mti?…. Eeeeh….(kukubali)….ni kama
hatuaaa….kuanzia tano sita….
F: Eeeeh….(kukubali)
P: Eeeeh….(kukubali)
F:na mstari kwa mstari?
P:nayo ndio hatua kamaaaa…sita hivi au saba
F:mmmh….(kukubali)
P: Eeeeh….(kukubali)
F:ulijifunzaje hizi mbinu?
P:hizi mbinu!.... mmmh….(kukubali)….tunakuja tunafundishwa na
wataalamu….mmmmh(kushangaa)….mbalimbali baada ya kujiunga na
vikundi….mmmmh(kushangaa)….ndio wanatuelekeza jinsi ya upandaji wa miti
F:(Kelele za makaratasi)…wataalamu kutoka wapi?
P:hawa wataalamu wanatokaaa….kikundi hichi cha….cha naniiii…UWAMIKE
F:UWAMIKE!..... Eeeeh….(kukubali)…UWAMIKE..sii…
P:iii….eeeh(kushtuka)….aaaakh(kukataa)…nishasahau jina hili…
F:wanao wafundisheni huu utaalamu ni watu gani?
P:hao wapanda miti wa…wataalamu wa wapanda miti…kikundi kinaitweje sijui hiki….wanafika hapa
wanatuitisha
F; au ndio hao wa FDT….wanaowafundisheni?
P:saa ingine ndio hao…wanaokuja wataalamu wengi wengi mpaka
tunasahau…mmmh(kukubali)….tunasahau majina wanakuja wengi wengi nao kutufundisha
F:na wewe ni mwanachama wa UWAMIKE?
P:alikuwa mwanachama mume wangu….mmmh(kuitika)…baada ya yeye kuwa na shughuli nyingi ndio
naudhuria mimi?
F:mmmmh(kukubali)
P: Eeeeh….(kukubali)
F:kuna utaalamu gani ambaooo…..umeweza kujifunza lakini unashindwa kuutumia….huutumii kwenye
mashamba yako ya miti?....na kwanini labda?
P:utaalamu ambao nimejifunza,jinsi ya kutengeneza nanii… ya kutengeneza barabara ya
moto….mmmh(kukubali)….wanasema tuwe tunachukua hatua 10…mmmmh(kukubali)….
Eeeeh….(kukubali)lakini sasa wakati mwingine unaweza kuwa labda afya yako….una afya mgogoro na
ile hatua ni kubwa..mmmh(kuitika)…unaweza labda uweke hata watu wakusaidie saa ingine hela
inakuwa hamna….mmmh(kukubali)…ya kuwalipa
F:kwa hiyo unatumiaga umbali gani?…..Eeeeh….(kuitika)…unatumiaga umbali gani wa barabara ya
moto?
P:ndio hivyo hivyo na…na…natengeneza hivyo hivyo kadri walivosema lakini sichukui ule…yaani
nafanya kazi kidogo…..
F:mmmh(kaitika)….
P:Eeeeh….(kukubali)
F:hakuna utaalamu mwingine?..…ambao unafikiri umefundisha lakini unashindwa kuutumia?
P:hamna
P:hakuna?
P: mmmhh….(kukubali)
F:na labda ungependa kujifunza zaidi….mmmmmh(kuitika)…utaalamu gani kwenye mambo haya ya
miti?
P:kwenye mambo ya miti!....mmmmh(kukubali)…..(sauti ya pikipiki)…labda tu hatua za upandajiwa miti
vizuri
F:kwani kwenye na nii hamfundishwi?
P:tunafundishwa
F:mmmh(kukubali)…sasa una…
P:na…na watekaji wa…wataalamu wa watekaji wa miti
F:mmmmh(kuguna)…..
Mazungumzo ya watu mbalimbali yakiendelea na sauti ya pikipiki
F:Naaa….utaalamu huu unafikiri ingekuwa rahisi kujifunza kwa kutumia mfumo gani ambao rahisi wewe
kujifunza?....tutumie mfumo gani wa wewe kujifunza?
P:(kelele za pikipiki na watu wakizungumza kwa nguvu)…hata mfumo wa vikundi kwa pamoja
F:kwanini unafikiria wa vikundi?
P:mfumo wa vikundi kwa pamoja kwa sababu naweza nikawa mimi sii…mimi bado sielewi na mwingine
tena akawa haelewi kwahiyo inakuwa faida ya wote….mmmmh(kukubali)…hata kama unakuwa
umesahau kwenda kujifunza kwa mwenzio kwenda kukumbuka siku ile walifundisha nini…unakwenda
kuangalia mwenzako amefanya nini
F:naaaa…kwa mfano kwenye kuuza miti kwa uzoefu wako unaonaje watu …hivi nani huwa anaamua
kwamba sasa katika kaya labda kwa uzoefu anayesema sasa nauza mti inafanyika kwa kukaa pamoja au
anaamua baba tu anauza au inakuwaje?
P:hiyo….mmmh(kuitika)….hata kama bado hatujauza na ninavyojua mimi mawasiliano ya wote wawili
ya baba na mama …mmmmh(kukubali)….kutokana na lile hitaji
linalohitajika….mmmmh(kukubali)…labda watoto wako shuleni inabidi makae kuwa tuuze miti
….mmmmh(kukubali) tupeleke ada ya watoto shuleni
F:mmmmh(kukubali)…
P: Eeeeh….(kukubali)
F:naa… wengi hapa wanauza kama mbao…. au kama miti au kama shamba?
P:walio wengi wanauza kama miti kama yaani miti tu ipo shambani wanamuuzia mteja
F:mmmmh…(kuitika)
P: Eeeeh….(kukubali)
F:naaa…wengi wanauza katika umri gani miti yao?
P:hapo kuna makundi mawili….mmmmh(kushangaa)….kuna wengine wanauza miti ya kufuga ile
amepatwa tatizo la dharura, miti bado michanga anauza….mmmh(kushangaa)….wengine tayari
imeshatimia kuvuna anauza
F:ile imetimia kuvuna kama miaka mingapi?
P:kuanzia miaka 7
F:naaa…labda kwa kuangalia nini ambacho unaona kama….kama kimekuwa kama changamoto kwa sisi
waa..wakulima wa miti hapa kwetu?
P:changamoto ni kwamba yaani miti inaungua…
F:mmmmh(kushangaa)….inasababishwa na nini?
P:inasababishwa tu na moto ambao hatujui moto umetoka wapi….moto tu yaani
unaanza…mmmmh(kushangaa)…..hata hatujui sababu moto umeanzeje….mmmmh(kushangaa)…na
mashamba mengine hayajatengenezwa naniliii…mmmmh…….(kushangaa)…zile barabara za moto…
F:mmmmh…(kushangaa)…..naaa…kwa kina mama wengine labda wanafikiri nini ambacho
kinawakwamisha na wao wasiwe kama wewe ambao wana…wanapanda miti?......kwa mfano ukiangalia
katika wamama 10 ….mmmmh(kaitika)…unaweza kukuta wangapiwanamashamba yao ya miti hapa
kwetu Kifanya?
P:kuna wengine hawapandi miti…sasa kwa mfano hivi mimi yaani tuseme niii….sijui ni elimu ya mtu
au…mwingine akiona moto unavyowaka utasikia mimi siwezi kupanda miti…mmmh(kushangaa)…kama
hivi mashamba yanaungua ungua mbona hasara ….mmmmh(kushanga)…niafadhali niache kupanda miti
F:wewe sasa mbona ulikuwa jasiri sasa ukaamua upande miti?
P: basi ndio hivyo sababu unapanda ikiungua basi ndio hvyo bahati nasibu unaweza
ukashangaa…mmmmh(kuitika)…shamba lako halijapitiwa na moto
F:hakuna sababu nyingine inayowafanya waogope ku…kushiriki kwenye …kuwa na mashamba yao?
P:san asana labda kwenye mambo ya mimi ninavvyojua miche nitapata
wapi?....mmmmh(kuitika)….nikiwa na shamba nitapata wapi miche ya kupanda?
F::ardhi?......sio tatizo?
P:hata aridhi ni tatizo….wengine wanakuwa hawana ardhi…
F:mmmmh(kukubali)….kwanini sasa wanaume ndio wengi wanapanda miti?....kwanini iwe tofauti kwa
sisi wengine?....kwa mfano hawa wanaouza miti sasa hivi ile hela unafikiri….kwa uzoefu wako ile hela
wanaa..ukishauzwa wana…wanagawiana kila mmoja…mama nawe shika hii,mtoto shika hii au utaratibu
huwa unakuwaje?
P:hapo siwezi jua kwa watu wengine ….mmmmh(kukubali)…sababu mtu unavyokuwa unauza lile
shamba unakuwa na malengo…unavyouza ile miti unakuwa na malengo Fulani….
F:mmmmh(kukubali)…..naaaa…
P:unakuwa na malengo ya kupeleka shuleni ada…mmmh(kukubali)…..au mnamalengo ya kujenga
F:mmmmmmh(kukubali)…..lakini wewe huwa unafikiri nani huwa ana…anafaidika
zaidi?....eeeh(kuitika)….katika kaya
P:baba, baba ndio anakuwa ana faidika zaidi
F:kwanini?
P:(kicheko)…..
F:eeeeh…(kuitika)
P:saa ingine ile hela anakaa nayo yeye …..eeeh(kuitika)…..bwana tumeuza miti hela hii
hapa…mmmmh(kuguna)…..eeeeh(kaitika)….anaweza akakaa nayo yeye bwana tatizo nini shuleni ada hii
hapa anakupa hela nyingine uende ukalipa ada nini shuleni yeye si ndo baba anakwambia hela nyingine
naendeshea shughuli nyingine….
F:mmmh(kushangaa)…kwa mfano wewe shamba lako sasa siku ukivuna itakuwaje?
P:shaamba langu mimi!.....eeeh(kukubali)….nitamshirikisha sababu yeye ni baba
….mmmmh(kukubali)…..hata kama ni shamba langu …eeeh(kukubali)….na shughuli zote tunafanya
pamoja….
F:eeeeh(kukubali)…. Naa…ukiuza ile hela mtafanyaje?
P:ni lazima nitamuuliza kwanza tuuze…tuuze miti na shughuli gani?……mmmh(kukubali)…sababu
huwezi kwenda kuuza tu miti hela ukaweka ndani….mmmh(kukubali)…lazima kuna jambo mnakuwa
mmelipanga bora tuuze tufanyie nini …..
F:eeeeeeh(kukubali)….na hela itakaa wapi?
P:hela!...mmmmh(kukubali)…..tutaielekeza kwanza kwenye lile jambo ambalo tumelipanga
F:lakini sasa si ukishauza kwani utafanya jambo hilo hapo hapo kama labda unajenga au nini si inabidi
ikae labda mkonono kwa mmoja labda nani anakaa nayo hiyo hela?
P:tunapeleka SACCOS kwanza
F:kwenye akaunti ya nani?
P:akaunti yetu
F:akaunti ya nani?....SACCOS iko akaunti ya kwako au..?
P:kuhusu katika kitabu cha familia
F:cha familia!
P:eeeh(kukubali)
F:kwahiyo unaweza ukatoa wewe hela au akatoa baba hela?
P:eeeh…(kukubali)….hata yeye anatoa pia hata mimi natoa
F:mmmmh(kukubali)….naaa…labda kuna kitu kingine umekiona kwenye kupanda miti kama kinaleta
athari …..miti inaleta athari, kuna athari yoyote ambayo miti inaleta kutokana na kupanda miti
P:zaidi zaidi mambo ya moto haya…..mmmmh(kushangaa)….ndio yanayotuathiri zaidi
F:hakuna kitu kingine kimekuja kujitokeza sasa….kuna baadhi ya miti wengine wanasema kwa mfano
inaleta….aaaa…ardhi inachakaa au labda pale yakii….wanasema nyani wanakuja sababu ya kupanda
miti wanaleta athari au labda chakula……uzalishaji wa chakula umepungua wewe unaonaje katika hilo?
P:kama ni kitu gani kingine kingeweza kutusaidia?
F:aaaah….(kukataa)…yaani kuona miti imeleta nini….. wengine kuna magomvi pia nasikia kwa sababu
ya upandaji miti nyie hayajawahi kutokea hayo?
P:mmmmh…(kukubali)….ipo mambo ya ardhi yanaleta ugomvi ….
F:mmmmmh(kukubali)….nyinyi mmeshapata kesi kama hizo?
P:hatujawahi pata ila tunaona tu kwa watu wengine….mmmmh(kushangaa)….kesi kama hizo
F:shida inakuwa ni nini?
P:kwamba labda amepanda miti eneo lisilokuwa la kupanda miti labda ni viwanja yeye anapanda
miti….mmmh(kushangaa)….anaambiwa toa hii miti….mmmh(kushangaa)…kwenye eneo la kiwanja
F:mmmmh(kushangaa)….na pia nimesikia wengine wanapanda hata eneo la chakula kulima hamna
P:wengine wana mashamba yote anapanda miti….shamba la kulima mahindi ….mmmh(kushangaa)….
kwa hiyo inabidi ukate miti ulime mahindi
F:mmmmh…(kushangaa)…nyinyi hilo halijajitokeza kama changamoto kwenu?
P:huku!..
F:kwa mfano
P:lipo watu wanasema na wanaopanda mashamba yote miti wanaacha mashamba ya mahindi
…mmmmh(kushangaa)…..wanatakiwa….serikali ishazuia sa hizi
F:mmmmmh…(kukubali)….kwamba msipande miti
P:inatangaza kila siku kwamba unavyopanda miti hakikisha una panda nini….unakuwa na shamba la
mahindi
F:mmmmh…(kukubali)…au kuna magomvi pia yanayotokea baada ya kuuza miti familia ndani baba na
mama kunaa… inajitokeza migogoro hiyo?
P:wapo inayo…jitokeza tatizo kama hilo…mmmmh(kushangaa)….naona kuto kule kushirikiana
kushirikishana….mmmmh…(kukubali)…baba anaenda kuuza miti hamshirikishi mke
wake…..mmmmh(kuitika)…..yapo hayo mabo mtaani….
F:mmmmh(kukubali)….aaaah…unafikiri labda kwa…uzoefu wako nini ambacho umekiona kama,kama
umejifunza kutokana na shughuli yakoya upandaji miti….umejifunza kama uzoefu wakokwa kupitia
uzoefu wakonini ambacho umejifunza kutokana na na kilimo cha miti
P:nilichojifunza juu ya kilimo cha miti…..mmmh(kukubali)….ni upandaji wa miti kwa muda
unaotakiwa…mmmmh(kukubali)…na kuhudumia lile shamba vizuri ……..zaidi zaidi kutengeneza
barabara za moto ili kuepukana na mambo ya moto…mmmh(kukubali)….kwa sababu kama shamba
hujatengenezea barabara ya moto….mmmh(kukubali)…..ni rahisi kuungua lakini ukitengenezea
utashangaa mashamba ya wenzio yanaungua huko wewe la kwako linafanyaje…lisiungue
F;ookay lakini kutengeneza kinyungu…mmejifunza chanzo cha moto ……kwenye kinyungu?
P:eeeeh…(kukubali)…kama sa hizi vile ndio watu wanalima vinyungu moto unatoroka….
F:mmmmh(kukubali)….sawa dada Christina mimi nafikiri nimemaliza maongozi na
wewe….mmmh..(kukubali)…nashukuru,…labda kama kuna amebaki mtu mmoja ambaye sijaongea nae
sijui
P:sijuii atakuwa ameshatoka ……ngoja nimangalie hapa
F:huyu baba anaitwa nani?....mwenye koti jekundu?
P: huyu mwanasayansi
F;eeeh…(kukubali)…mwanasayansi
P:ngoja nimuite
F:eeeh…(kukubali)….hebu niitie nije nimuulize hapa mtu gani mwingine amaemuandaa
P:mwanasayansi

You might also like