You are on page 1of 6

Kelele za makaratasi na milio ya viti kama vikisogezwa

F:huwa wanawakodisha au?

P:hata huwa wanatoa bure tu lakini tulifoji tukapanda malezi wakati wa…wa….wanakataa malezi

F:hawataki malezi …kwanini?

P:aaa…wanasema ina athari kwa mmea wao kwasababu mnapanda…..wewe unapanda malezi na wao
wanapanda mti hapo hapo….mmmh(kushangaa)……. Sasa wanasema kuna madhara kwenye nanilii…yao

F:aaaah..(kushangaa)…wanataka mpande nini?

P:mahindi tu peke yake

F:mahindi tu!....au……mnatatizo gani maana sijajua ….sababu nikiangalia mahindi na malezi ni kama
vinafanana

P:aaah wanasema wana….wanahashiria kuwaleta wadudu ambao wanashambulia…eee…mt… mti wa


mpaina

F:eeeeeh(kushangaa)…..kaaa…kwahiyo hawakugundua kuwa nyinyi mmeweka hiyo wangewafukuza

P:aaaaah(kufikilia)….waligunduaga yameota

F:(kicheko)

P:kwa sababu tulipanda miaka 2 sasa meneja aka…sasa akaja…mmmh(kushangaa)… akatoa taarifa rasmi
kwamba kule hakuruhusiwi kupanda mmea wowote wa aina nyingine ni mhindi
tu…mmmh(kushangaa)…wale ambao wamepanda mahindi…wamepanda malezi mwenzao wamenipa
adhabu ya kupewa warning

F:aaaaakh..(kushangaa)

P:mmmh(kuitika)….sasa kwa namna hiyo hata muacha huyu atakaye panda


mwakani…mmmh(kushangaa)…kwa sababu anaonekana yeye ndio aliyepewa adhabu hiyo sasa kupewa
adhabu kwa niaba ya mtu mwingine….eeeeh(kukubali)….naona yeye hataipendelea

F:aseee mzee Kule hapa mpo kwenye kata yako hapa …..mko watu wangapi?

P:tuko watu 5

F: wa 5

P:eeeh(kukubali)

F:wanakutegemea wewe?.....au wengine wanajitegemea wenyewe?

P:hao ndio wanao nitegemea mimi

F:wa 5

P: eeeh(kukubali)

Kelele za makaratasi
F:binafsi una miaka mingapi mzee Kule?

P:nina miaka 64

F:na mama?

P:ana miaka 57

F:na hao wengine wa 3 nii…?....wakike wangapi na wakiume wangapi?

P:wa…kike 1

F:1

P:mmmmh(kukubali)

F:yeye ana miaka mingapi?

P:eeeeeeeeh…..aaaaaah…(kufikilia)….amemaliza sasa hivi…..anamaliza sasa hivi mwaka huu

F:ina maana anasoma?

P: eeeh(kukubali)….alikuwa anasoma

F:na hao wa kiume?

P:wana miaka kumi na minane

F: eeeh(kukubali)…….wote au…..mwingine,

P:hata mwingine ana miaka 15

F: eeeh(kukubali)……wameshamaliza shule hawa?

P:mmoja anasoma sekondari

F:mmoja wa miaka 15

P: eeeh(kukubali)

F:naaa…hapa wewe mzee Kule una….shamba la miti heka ngapi?

P:aaaaa….nina heka 2 tu

F:heka 2

P: eeeh(kukubali)

F:naaa….shamba hili wewe ulipata wapi hili?....ulilipataje?

P:aaaa ….hili shamba baada ya kuletwa operasheni sogeza….. mmmmh(kushangaa)…..tulikuwa


tunagawiwa kila nyumba hekari 3…….mmmh(kushangaa)….kwa sababu tuliacha mmm…masikani kwetu
huku tukaja huku….. mmmmmh(kushangaa)….huku tuliletwa tu

F:khaaaa….(kushangaa)…
P:mmmmh(kukubali)….

F:hekari 3….mmmh(kukubali)…kwahiyo katika 3 hizi ukapanda 2 mahindi….nanii…..miti 1 ndio unalima


mazao lakini ya chakula

P:eeeee..hizi ni….hizi 2 naa naa….nizopznda maa…na…nanii miti….eeeh(kuitika)…..2 katika hizi


nilizopewa ndio hizo na nalima mahindi nikichanganya na nyingine za huko tulikoamia…tulikohama

F:aaaakh..(kushangaa)…

P:mmmh(kukubali)….

F:kule ulikohama unapanda nini?

P:aaaaa kule huwa nalima tu mahindi

F:mahindi

P:mahindi,njegere,ngano hii inayosemwa tunalinga….eeeh(kuitika)…..ngano huko huko….

F:eeeeh(kuitika)…kule hukupanda miti uliko hama?

P:aaaa kuna sehemu tu kidogo nimepanda Selejina

F:se…se…inaitwajwe?

P:mlingo

F:aaaah(kukubali)…

P:mlingoti mwekundu

F:mlingoti mwekundu……mmmmh(kukubali)…..kama heka ngapi?

P:aaaaa kama heka 1 tu

F:huu mlingoti mwekundu unakomaa baada ya muda gani?

P:aaaa kwa kweli kukomaa kwake sisi hiyo tunategemea nguzo zaidi za
umeme……aaah(kushangaa)…..miaka 7 hivi 10 lakini ya kupasua kwakweli inaweza ikachukua mpaka
miaka 20 hivi….eeeeeh(kushangaa)…ndio uwe mti umekomaa…..lakini hata hiyo hiyo miaka 7
wanapasua …..mmmh(kushangaa)….lakini sehemu kubwa sisi tunang’ang’ania nguzo

F:mmmh(kuitika)…..kwahiyo hizi heka 2 hizi umepanda miti gani?

P: hiyo mipaini tu

F: mipaini….mmmh(kukubali)…. mbegu unafata wapi?

P:aaaa mbegu hii niliyopanda nilikuwa nawa

F:unakitalu chako?
P:aaaa nilikuwa nakitalu lakini mwaka huu si…sina kitalu…(Sauti ya mtoto akiimba)….nina kitalu cha hiyo
miti milingoti miyekundu…….mmmmh(kukubali)….sasa kwa sababu pale mlikuwa mnazungumzia mipaini
hiyo mimi sina….

F:aaaa pamoja na..ni miti tu paini na hii milingoti…aaaah(kukubali)….lakini sehemu kubwa inajitokeza
paina ndio wengi wamepanda

P:aa wengi wamepanda paini

F:mmmmh(kukubali)…

P:tumeanza kugundua sasa kwamba tulichelewa kupanda mlingoti …mmmh(kushangaa)…..nao ndio


wenye pesa kwa sasa

F:kweli?

P:kweli

F:mnawauzia wa…. Tanesco mnamuuzia nani?

P:kuna watu wanakuja wanaangua wanakwenda….mmmh(kushangaa)….kumuuzia ku…. pamoja na…na


Sawiu huko anakiwanda cha kuchemsha manguzo hayo….mmmh9kushangaa)….waku treat tuchukue
kutreat

F:ku treat eeeh….(kukubali)….

P:sasa watu wanapita wanalangua…..aaaaahk(kushangaa)…sas ukiona ukiangalia na paini


havi…havi…hambatani hivitunaona tuliharibu kabisa kupanda paini kupanda seleju

F:mmmh…(kushangaa)…

P:mmmh…(kukubali)…lakini unaokuwa ni mlingoti mwekundu..mmmh(kushangaa)…huu mweupe haukui


kwa haraka

F:mmmh…(kuitika)…hizi heka 2 anamiliki nani za miti?

P:naam

F:hizi heka 2 za miti nani mmiliki?

P:aaa tulipanda mimi na mwenza

F:eeee…..lakini ardhi shamba la nani?

P:shamba hilo ndio nililosema tulipewa na serikali ya vijiji wakati tulipoamishwa

F:eee lipo kwenye jina la nani?...Mzee Mkulule

P:Mzee Mkulule

F:mmmh(kuguna)… na….labda mama yeye hana ploti yake ya miti?

P:ya kwake binafsi?

F:mmmh(kuitika)…
P:eee anayo

F:anayo…yeye ana heka ngapi?

P:yeye ana nusu heka tu

F:kaanza kupanda lini?

P:mmmh(kufikilia)…yeye amepanda 2014

F:kapanda paina?

P:mmmmh(kukubali….

F:nini kilichomsukuma akaamua kupanda?

P:aaaa…unajua mimi huyu mmama nilimrithi…aaahk(kushangaa)….alikuwa mke wa marehemu mdogo


wangu…mmmh(kushangaa)…sasa marehemu mdogo wangu alikuwa na shamba akaamua kupanda hata
anapoaga dunia…mmmh(kushangaa)…wameendelea kuvuna miti ya marehemu mdogo
wangu…mmmh(kuitika)….sasa hii ndicho kilichomvutia baada ya kuona….mmmh(kuitika)….ni faida miti
lakiniasingekuwa amegundua aliyeanzisha ni marehemu mdogo wangu

F:mmmh(kuitika)….

P:mmmmh….(kuitika)…

F:na wewe ulianza kupanda lini miti?

P:aaaa…nimevuna zaidi ya mara 1…… sasa sijui unasema hii niliyopanda?

F:kuanza kabisa kupanda miti ulianza muda gani?

P:aaaa kuanza kupanda miti mimi nimeanza mwaka efu moja na…na….tisini na tisa

F:ndio ukaanza kupanda miti kwenye mashamba yako?

P:eeeeh(kukubali)…hiyo niliyoanza nilisha…nilishavuna mda mrefu sana

F:ulishavuna eee

P:mmmh(kukubali)

F:na nini kilichikufanya wewe miaka hiyo ukaamua kuwa unapanda miti na usipande vitu vingine?

P:aaaa walipokuja hawa wenzetu wa misitu…mmmmh(kukubali)….eee walikuwa wanashauri tupande


miti….mmmh(kuitika)…..na kama huna mbegu walikuwa wanatoa bure unakwenda
bustanini….mmmh(kushangaa)….wanabustani pale kwenye shule ya sekondari ya …ya
Ifwagi…mmmh(kuitika)…ndio ilipokuwa bustani unakwenda…unakwenda wanakugawia miti wanasema
na wewe upande ……mmh(kushangaa)…lakini hatukujua manufaa tumekuja kugundua baadae,baada ya
kuona ina nunuliwa..mmmh(kushangaa)….wao walikuwa wanatushauri tu kupanda lakini hatukuwa
tunajua faida yake kwa kweli

F:mmmmmh(kushangaa)…..naaa..na labda wewe baada ya kuanza na hizo heka kwanini hujaongeza


labda ukawa na heka nyingi zaidi ya hizi… za miti?
P:ardhi kwa sasa hakuana….mmh(kushangaa)…hata kama unanguvu ya kupanda…mmmh(kuitika)…labda
uwe umepata chanzo cha kupata pesa kwa sababu wapo wenye hali duni ya maisha wanaamua
wauzee….mmmh(kuguna)…pale alipo…mmmh(kuitika)….na ukiangalia kwetu sisi kama kijiji hiki aridhi
imepungua…mmmh(kushangaa)…iko kwa watu…wamilikaji wakubwa sisi wa dogo kwa kweli tumeuza
sehemu kubwa aliyonayo mashamba ni wachache kabisa hata kama anayo labda ana heka 1,kanusu
heka basi shamba kama shamba

F:kwani wewe ulikuwa nayo alafu pia ukauza?

P:aaaa mimi sijauza…mmmh(kuitika)…kwangu mimi kwakweli sijauza

F:kwa mfano kule kwenye mahame yako kule mlipo hama

P:eeee huko ndio sijagusa ndio ninakolima

F:sasa mbona kule hujapanda miti sasa

P:aaa kule sasa tumetenga kwa ajili ya kulima mahindi

F:mmmmh(kukubali)

P:eeeeh(kuitika)

F:aaakh na hii miti unayopanda umepanda wapi?

P:hii nimeipanda kwa nyuma hapa kidogo

F:aaakh(kushangaa)..

P: eeeh(kukubali)

F:kwanini sasa ukalime kule mbali mahindi,naniu… ngano alafu hapa karibu ukapanda miti?

P:aaaa huku rotuba baada ya kuona imechoka…mmmh(kushangaa)…ndio tukaamua kupanda miti

F:aaakh(kushangaa)..

P: eeeh(kukubali)….kule tulikuwa tumeacha hata kulima tulikuwa hatulimi limi…..mmmh(kuitika)….sasa


tumeamua kwenda kulima baada ya huku sasa kuwa kama ardhi haipo tumepanda miti kama unavyoona
huku ukigeuka hukaoni kanafasi kakubwa ni kanafsi kadogo kadogo kanakoonekana hakako hakana mti

F: F:aaakh(kushangaa)….na yeye labda sijui inakuwaje kwa yeye kwenye miti

P: eeeh(kukubali)

You might also like