Professional Documents
Culture Documents
Brochure Swahili 2
Brochure Swahili 2
Mei, 2005
Makala ya Habari kwa Umma
UTANGULIZI
Katika Kipeperushi Na.1 cha Habari Kwa Umma, zilitajwa faida mbalimbali za mifuko
ya uwekezaji wa pamoja. Faida hizo ni pamoja na ukusanyaji rasilimali, kutawanywa
kwa hatari za uwekezaji, kupunguzwa gharama za uwekezaji na kuwezeshwa wawekeza-
ji wadogo wadogo.
Mfuko huu umebuniwa kuwezesha ushiriki wa Watanzania wa aina zote yaani mtu
mmoja mmoja na taasisi mbalimbali za kijamii ( zilizosajiliwa nchini na wanufaika wake
wote ni Watanzania) iwe kipato chake ni kidogo au kikubwa na vilevile kwa Watanzania
walioko ndani au nje ya nchi.
Kampuni kwa kawaida inaundwa kwa watu kununua hisa kwa mujibu wa katiba ya kam-
puni (Memorandum and Articles of Association). Kampuni inasajiliwa na Wakala wa
Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Baada ya kampuni kusajiliwa inakuwa kama
mtu kisheria hali inayoitofautisha na wana hisa wake. Mali ya kampuni si mali ya wana
hisa. Mali hiyo ni ya kampuni. Wana hisa wanazo haki zao kufuatana na katiba ikiwa
ni pamoja na haki ya gawio kutokana na faida, kuhamisha [kuuza] hisa, kupiga kura, na
Awali ya yote, kupata gawio kutoka kwenye kampuni inategemea mambo mawili; kwan-
za gawio linatolewa iwapo kampuni imepata faida na pili gawio linapatikana kulingana
na sera ya gawio (Dividend Policy) kama inavyokuwa imeamuliwa na Bodi ya
Wakurugenzi wa kampuni. Inawezekana kwa mfano; Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni
kuamua kuwa faida ibakizwe ndani ya kampuni kwa ajili ya kukuza shughuli za kam-
puni fulani.
Jambo la pili muhimu ni kwamba, kwenye kampuni Bodi ya Wakurugenzi ndiyo yenye
wajibu na madaraka ya kuendesha kampuni. Kwa hiyo, Bodi ya Wakurugenzi ndiyo
inayoteua watendaji wa kila siku wa shughuli za kampuni na yenyewe kubakia na wajibu
wa kutoa na kuratibu sera za kampuni.
Serikali imekubali kutoa asilimia mbili (2%) ya hisa za Kampuni ya Bia Tanzania na asil-
imia moja ( 1%) ya hisa za Kampuni ya Sigara Tanzania kama mtaji kwa ajili ya Mfuko
wa Umoja. Thamani ya hisa hizo zote hapo tarehe 08 Machi, 2005 ilikuwa kiasi cha shs.
11,571,609,600/=
Licha ya kukubali kutoa hisa zake kwenda kwenye Mfuko wa Umoja, Serikali pia imepi-
tisha uamuzi wa kutoa punguzo la asilimia thelathini (30%) kwenye thamani ya mwan-
zo ya vipande vya Mfuko wa Umoja. Thamani ya mwanzo ya vipande vya Mfuko wa
Umoja ni shs. 100/= kwa kila kipande. Lakini, kwa ajili ya punguzo linalotolewa na
serikali la 30%, mauzo kwa kila kipande yatakuwa kwa bei ya shs 70/=.
Kiwango cha chini cha vipande ambacho mtu anaweza kununua katika kipindi cha
mauzo ya awali ni 50 amabvyo vitamwezesha mwekezaji kuweza kuingia kwa kiwan-
go cha chini cha shs. 3,500/=. Hakuna kiwango cha juu. Hata hivyo maombi yote
yatatathiminiwa na Meneja kulingana na malengo ya mpango kwa kutumia vigezo
vitakavyopitishwa na Mamlaka.
Ili kuhakikisha kuwa punguzo la bei linawanufaisha Watanzania pekee, watu na taasisi
zilizotajwa hapa chini ndio wanaoruhusiwa kuwekeza wakati wa kipindi cha toleo la
kwanza la Mfuko wa Umoja.
(a) Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea wanaoishi nchini au nje
ya nchi.
(e) Vyama vya Ushirika, Taasisi za Kijamii, Taasisi za Misaada, Taasisi za Kidini
na Vyama/vikundi vya uwekezaji viliyosajiliwa Tanzania ambavyo wanufaika
wake wote ni Watanzania.
Kama ilivyokwishaelezwa hapo awali, Serikali tayari imekwishatenga hisa kwa ajili ya
Mfuko wa Umoja. Uwekezaji utafanywa kwenye dhamana za serikali, hatifungani za
makampuni, akaunti za muda maalum na hisa nyinginezo zitakazokuwa zimeorodhesh-
wa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam. Kiwango kitakachowekezwa kwenye hisa
hakitakiwi kuwa zaidi ya asilimia thelathini (30% ) ya mseto mzima wa uwekezaji wa
mfuko.
Mfuko wa Umoja unazo aina mbili kubwa za uwekezaji ambazo zinalenga kukidhi
malengo ya wawekezaji, aina hizo ni mpango wa mapato (income distribution) na mpan-
go wa kukua (Re-investment).
MPANGO WA MAPATO
MPANGO WA KUKUA
Chini ya mpango wa kukua hakuna gawio litakalotolewa, badala yake mapato yatabak-
izwa kwenye mfuko na wawekezaji watapewa vipande vya nyongeza, idadi ya vipande
itapatikana kwa kuchukua gawio alilotakiwa kupata mwekezaji na kugawa kwa thamani
halisi ya kipande kwa wakati wa mgao. Wawekezaji vijana wanashauriwa kufuata utarat-
ibu huu kwani unawawezesha kukuza rasilimali zao katika uwekezaji kwa ajili ya maisha
ya baadaye.
Mazingira haya yanaongeza urahisi kwa wawekezaji kubadili kutoka utaratibu mmoja
kwenda mwingine.
KIELELEZO III
SURA YA SHUGHULI ZA MFUKO WA UMOJA
Kuna njia mbili ambazo vipande vya Mfuko wa Umoja vinaweza kununuliwa. Vipande
vinaweza kununuliwa wakati wa kipindi cha toleo la kwanza (yaani vinapouzwa kwa
mara ya kwanza - IPO) na hivyo kufaidika na punguzo la asilimia thelathini (30%).
Vilevile vinaweza kununuliwa wakati wowote baada ya kipindi cha kizuizi cha mwaka
mmoja kinachoishia tarehe 31 Julai, 2006. Hii ni kwa sababu Mfuko wa Umoja ni mfuko
wa wazi unaoruhusu wawekezaji kuuza vipande vyao kwa Dhamana ya Uwekezaji
Tanzania na kuvinunua tena wakati wowote wanapokuwa na fedha za kuwekeza.
Baada ya kipindi cha kizuizi, vipande vinaweza kununuliwa (siku za kazi) katika kipin-
di cha mwaka mzima isipokuwa kipindi kisichozidi siku saba ambapo daftari la wana
vipande litakuwa limefungwa.
(a) Matawi ya; CRDB Bank Limited, National Microfinance Bank, Shirika la
Posta, Benki ya Posta (Tanzania Postal Bank) na Akiba Commercial Bank
Limited.
Malipo kwa ajili ya ununuzi ya vipande katika kipindi cha mauzo ya awali na baada ya
kipindi cha kizuizi yanaweza kufanywa kwa fedha taslim, au hundi za benki kupitia kwa
wakala yoyote kati ya waliotajwa. Hundi iandikwe “ Mfuko wa Amana ya Kikundi cha
Umoja” (Umoja Unit Trust Scheme). Wawekezaji wanatahadharishwa kwamba malipo
ya kununua vipande vya mfuko yasifanywe kwa mtu au taasisi nyingine zaidi ya
mawakala waliotajwa ambao wanatambulika na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania.
(iii) Taarifa za nusu mwaka zinatakiwa zitumwe kwa wenye vipande si zaidi
ya miezi miwili ya vipindi husika.
(d) Ili mtu akubali kuwekeza kwenye mfuko, inabidi taarifa muhimu zenye
kuhusiana na mfuko huo ziwe zimetolewa kwake. Taarifa hizo ni pamoja na
mambo ya msingi yahusuyo mfuko, sera ya uwekezaji, n.k. Mabadiliko yoyote
ya msingi kuhusiana na taarifa hizo yataweza kufanyika iwapo tu wawekezaji
watakuwa wameruhusiwa kuuza vipande vyao kwa thamani ya wakati huo na
taarifa hizo kuwa zimewekwa kwenye magazeti ya Kiswahili na kiingereza
yenye mzunguko mkubwa hapa nchini.
(a) Wenye vipande wote wana haki ya kupata hati za kumiliki vipande kulingana na
idadi ya vipande walivyonunua.
(a) Mwenye vipande ambaye jina lake limesajiliwa kwenye daftari la mpango siku
itakayotangazwa kuwa ya kugawa mapato, na ambaye hayuko kwenye mpango
wa kukua atakuwa anastahili kupata mgao wa fedha taslim.
(b) Mgao wa mapato utafanywa kwa kuhamisha fedha kwenda kwenye akaunti za
wawekezaji ambao watakuwa wametoa taarifa kwa Dhamana ya Uwekezaji
Tanzania mahali akaunti zao zilipo au kwa kutoa hawala za fedha.
(c) Kuweka fedha kwenye akaunti na kutuma hawala ya fedha kutafanywa katika
kipindi kisichozidi siku tano za kazi.
(e) Wenye vipande walio katika mipango yote miwili ya kukua na mapato
watapata taarifa ya akaunti kwa ajili ya vipande vilivyoongezeka na fedha
taslim kutokana na mgao wa mapato.
(f) Katika kipindi kisichozidi siku kumi baada ya tarehe ya mgao wa mapato,
Dhamana ya Uwekezaji Tanzania itatuma taarifa za akaunti kwa wenye vipande
ambao watakuwa wamepata vipande kutokana na kuwekezwa mapato yao.
Vipande vya Mfuko wa Umoja vinaweza kuwa dhamana au rehani (pledged or mort-
gage)
Iwapo itatokea mwenye vipande amefariki, madai ya mirathi yatakuwa kama ifuaatavyo;
• Iwapo vipande vinamilikiwa na watu wawili kwa pamoja basi mrithi atakuwa ni
yule aliyebaki.
Thamani ya kila kipande inaweza kupatikana kwa kugawanya idadi ya vipande vya
mfuko kwa wakati huo ambayo kama ilivyotamkwa awali, mfuko wa Umoja utakuwa ni
mseto wa mizania wenye rasilimali za aina tofauti. Kwa wakati wowote ule, rasilimali
hizo lazima thamani yake ijulikane. Kwa kufanya hivyo, thamani ya rasilimali zote
kwenye mfuko zitajulikana. Madeni ya mfuko inabidi yatolewe ili kupata thamani halisi
ya mpango (Net Asset Value). Kwa hiyo, thamani halisi ya mpango inapatikana kwa
kuchukua thamani ya rasilimali za mfuko na kutoa madeni ya mfuko na wakati huo huo
bila kusahau mapato ambayo yameishajulikana japo hayajapokelewa na gharama
ambazo zinakisiwa (accruals and provisions)
Licha ya kufahamu thamani ya mfuko mzima, thamani ya kila kipande pia inaweza kuta-
futwa, thamani ya kila kipande inapatikana kwa kugawana thamani ya Mfuko kwa idadi
ya vipande vya Mfuko kwa siku hiyo ambayo hesabu hizo zinafanyika.
Ni wazi kuwa uthamini wa mali za Mfuko ni shughuli ngumu na yenye kuhitaji utaalam
; pamoja na hayo, mwongozo uliopo ni kuwa uthamini unafanyika kwa kuzingatia
thamani zinazotambulika kutoka kwenye soko.
MAMBO YA KUZINGATIA
b) Kuna “kipindi cha kizuizi” (lock-in-period) cha mwaka mmoja. Baada ya kipindi
hicho cha kizuizi, mfuko utaweza kuuza na kununua vipande kutoka kwa
wawekezaji. Bei ya kununulia na kuuzia itategemea thamani halisi ya wakati huo
(Net Asset Value) baada ya kutoa au kuongeza gharama ya huduma ambayo ni
asilimia moja (1%)
.
c) Kiwango cha chini cha kuwekeza wakati wa toleo la mwanzo ni sh 5,000/=
(shilingi elfu tano tu) kwa ajili ya kununua kiwango cha chini cha vipande
hamsini. Kutokana na punguzo la bei lililotolewa na Serikali, wawekezaji
wanaweza kuingia kwenye Mfuko wa Umoja kwa gharama ya sh. 3,500/=
. Wawekezaji hawatatozwa gharama zozote wakati wa mauzo ya mwanzo.
g) Mauzo na manunuzi yatakuwa wazi kila siku ya kazi isipokuwa wakati wa kipindi
cha kizuizi (lock-in-period) na kipindi ambacho daftari la orodha ya wanavipande
litakuwa limefungwa kama itakavyotangazwa na Dhamana ya Uwekezaji
Tanzania.
k) Inaruhusiwa kwa mwekezaji kuuza sehemu ya vipande vyake ili mradi salio la
vipande atakavyokuwa anamiliki wakati wowote lisiwe chini ya vipande kumi.
Manunuzi vile vile yatafanyika katika mafungu ya vipande kumi.
l) Hakutakuwa na riba itakayolipwa kwa mwenye kuuza vipande kwa kipindi amba
cho muuzaji atakuwa hajatumiwa fedha zinazotokana na mauzo ya vipande vyake.
(i) kununua vipande katika kipindi cha kizuizi kinachoishia tarehe 31 Julai,
2006;
(iii) katika kipindi kisichozidi siku saba kwa wakati mmoja, au vipindi vingine
kama itakavyoamuliwa na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania wakati ambapo
daftari la orodha ya wenye vipande litakuwa limefungwa.
KODI
Kodi ni sehemu muhimu katika shughuli za uwekezaji, kwa hiyo ni muhimu kwa
wawekezaji kwenye Mfuko wa Umoja kufahamu baadhi ya masuala ya kodi. Taarifa
inayotolewa katika kipeperushi hiki ni kwa ajili ya ufahamu wa jumla .Inashauriwa
kwamba wawekezaji wawasiliane na wataalam mbalimbali wa maswala ya kodi ili
kufahamu kodi watakazolipa kutokana na kushiriki kwao kwenye Mpango huu.
• Mapato ya mfuko yanatozwa kodi kwa kiwango cha kawaida cha makampuni.
Mawakala wa Kupokea
Hizi ni taasisi ambazo katika kipindi cha mauzo ya awali zitashiriki; kutoa fomu za
maombi, kusaidia wawekezaji kujaza fomu na kuchukua fedha kutoka kwa wawekezaji
ili kuziwasilisha kwenye Dhamana ya Uwekezaji Tanzania.
Mpango wa Kukua
Ni mojawapo ya utaratibu ambao wawekezaji wanaweza kuufuata ili badala ya kupokea
fedha taslimu (kama gawio la faida) wapewe vipande vya nyongeza kwa thamani ya
wakati huo.
Punguzo
Hiki ni kiasi cha pesa kinachopunguzwa kutoka kwenye thamani ya mwanzo ya vipande
vya Mfuko wakati wa kipindi cha mauzo ya awali
Mauzo ya Awali
Mauzo ya vipande au hisa yanayofanywa na mpango wa uwekezaji wa pamoja au kam-
puni kwa mara ya kwanza.
Mauzo ya Mwanzo
Hii ni sawa na mauzo ya awali ila hutumika kutofautisha zoezi lenyewe na mauzo ya
baadaye ya vipande ambayo kwa utaratibu wa Mfuko wa Umoja yatafanywa baada ya
kipindi cha kizuizi cha mwaka mmoja.
Mseto wa Uwekezaji
Huu ni mchanganyiko wa dhamana/rasilimali ambazo mfuko wa umoja utawekeza.
Mauzo
Haya ni mauzo ya vipande yanayofanywa na mfuko. Inawezekana yakawa ni mauzo ya
awali au mauzo yanayofuata baada ya kuisha kwa kipindi cha kizuizi.
Mdhamini
Mdhamini ni taasisi inayoanzisha Mpango, kwenye Mfuko wa Umoja, mdhamini ni
Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT).
Taarifa ya Akaunti
Hii ni aina maalum ya taarifa ya akaunti inayotolewa na mfuko kwa mwenye vipande
ikionyesha idadi ya vipande anavyomiliki kwenye mfuko. Ni kama taarifa ya akaunti ya
benki ambayo huonyesha salio kwenye akaunti ya mteja.
Mauzo Baadaye
Kama ilivyoelezwa hapo juu, haya ni mauzo ya vipande vya mfuko baada ya kipindi cha
kizuizi (lock –in –period)
Waraka wa Makubaliano
Huu ni waraka unaothibitisha kusajiliwa kwa dhamana ambayo ni mpango wa uwekeza-
ji wa pamoja. Waraka wa Makubaliano unatamka kuanzishwa kwa Mpango, wajibu wa
pande zinazohusika (Meneja na Mwangalizi), haki za wenye vipande n.k. Waraka wa
Makubaliano kwa kuanzia unawahusisha Meneja na Mwangalizi. Kila mwenye kipande
anakuwa sehemu ya Waraka wa Makubaliano anapojiunga na mpango.
Kipande
Hiki ni kipande kinachotolewa na mfuko kikiwakilisha haki alizonazo mwenye kipande
kutokana na mali na mapato ya mfuko kulingana na uwekezaji wake. Ni kama hisa
kwenye kampuni ingawa haki za wenye hisa zinatofautiana kiasi fulani na haki za wenye
vipande kama ilivyoelezwa katika kipeperushi hiki.
Hati ya Vipande
Hii ni hati anayopewa mwenye vipande ikiwa ni ushahidi wa kumiliki vipande katika
mfuko.
Mwenye Kipande
Ni mtu au taasisi inayokubaliwa na mfuko kama mmiliki halali wa vipande vya mfuko.