You are on page 1of 38

Shared by: Zechariah Wakili Msomi (Mwanafunzi wa sheria UDOM)

KESI YA JAMHURI NA MWALIMU RESPICIUS PATRICK MTAZANGIRA PAMOJA NA


HERIETH D/O GERALD, KWA LUGHA YA KISWAHILI (TAFSRI ISIYO RASMI)

THE REPUBLIC

VERSUS

1. RESPICIUS S/O PATRICK@ MTAZANGIRA


2. HERIETH D/O GERALD

SWAHILI VERSION.

TRANSLATED BY (IMETAFSIRIWA NA) ZECHARIAH LEARNING ADVOCATE


(Mwanafunzi wa sheria UDOM, CBSL).

Hii ni kesi inayohusu kupigwa hadi kuuawa kwa aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya msingi
Kibeta, Iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Sperius Eradius, na Mwalimu wa nidhamu
wa shule hiyo, kwa madai kuwa aliiba pochi.

Ambapo mtuhumiwa mmoja (Mwalimu Respecius) alikutwa na hatia ya mauaji na kuhukumiwa


adhabu ya kunyongwa mpaka kufa. Mtuhumiwa mwingine (Mwalimu Harieth) alikutwa bila
hatia na kuachiwa huru.

KESI AMBAYO IMEVUTA HISIA ZA WATU WENGI SANA. NAMI KWA KUGUSWA NA
KUONA UMUHIMU WA KESI HII, NIMEAMUA KUIFASRI YOTE KWA LUGHA YA
KISWAHILI, ILI IWAFIKIE WATU WENGI, HASA WAALIMU AMBAO NDO
WAHUSIKA WAKUU: (Hasa waalimu, Mwalimu yeyote husika tafadhali.). Tunafahamu
wanafunzi wanavyoadhibiwa huko mashuleni kinyume cha utaratibu, Fuateni utaratibu kabla
hayajawakuta

KESI HII IWE FUNZO (LESSON) KWA WAALIMU WOTE WENYE TABIA YA
KUADHIBU WANAFUNZI VIKALI KINYUME CHA SHERIA

Kwa kusoma kesi hii, utajifunza vingi, mfano, Ushahidi unaotakiwa Mahakamani ili
kushinda kesi, na jinsi ya kumbaini shahidi mwongo na mkweli​.
Utafahamu, ​kama maelezo yanayotolewa kituo cha polisi yanaweza kutumika kama
ushahidi Mahakamani na kuzingatiwa​?

Na ​nini kitatokea endapo mashahidi kwenye kesi wanatoa ushahidi ambao unatofautiana
kuhusu kitu kile kile kimoja (contradictions)​ kama ilivyokuwa kwenye hii kesi.

Pia, ​utajua NIA (INTENTION) inapimwaje au kutazamwa Mahakamani ili kujua kama
mtuhumiwa alikusudia kuua ama la! Vitu gani vinaashiria mtu alikusudia kuua?

Vilevile, ​Utafahamu utaratibu sahihi na kununi za kutoa adhabu ya viboko shuleni.


Wakati gani adhabu ya viboko hutolewa? Nani ana Mamlaka kutoa adhabu ya viboko?
Nini kitatokea Mwalimu asipofuata utaratibu sahihi wa kutoa adhabu ya viboko? Na kama
mwanafunzi akigoma hatua gani zitachukuliwa?​ Hayo na Mengine mengi, utayapata kwenye
hii kesi.

(KWA KUWA NI KESI NDEFU, UNAWEZA KUIKOPI AU KUHIFADHI SEHEMU


UNAYOWEZA KUIPITIA BAADAE UKASOMA TENA)

TAFADHALI USIBADILI MAUDHUI, (NARUDIA HII NI TAFSRI ISIYO RASMI,


LAKINI MAANA (TONE) NI ILE ILE, KILICHOBADILIKA NI LUGHA TU).

KARIBU:

Kesi ilikuwa kati ya JAMHURI na washtakiwa wawili ambao ni

1. RESPICIUS S/0 PATRICK@ MTAZANGIRA na

2. HERIETH D/O GERALD


22/2 & 6/3/2019

Kesi hiyo ilisikilizwa Mahakama Kuu ya Tanzania Bukoba Registry, mbele ya Judge L.M.
MLACHA, J.

FACTS:
Sperius Eradius, Mwanafunzi wa darasa tano, mtoto wa kuasiliwa (adopted) wa Mchungaji
Justus Balilemwa. Alienda shuleni asubuhi na mapema kama kawaida. Akapangiwa kusafisha
madarasa yeye na wenzake. Na wakafanya. Hakuna shaka kwamba, Alikuwa na afya njema, na
hakuna aliyefkri atakufa baadae siku hiyo.
Kijana Sperius Eradius, Sasa amefariki, na hii kesi imeletwa kuchunguza sababu za kifo chake
na kuwapa adhabu wale watakaobainika na mauaji hayo.

Taarifa ya kifo cha Sperius Eradius ilifika kituo cha polisi Bukoba siku hiyo hiyo majira ya saa
saba mchana. Ambapo ilikuja baadae kuhusishwa na waalimu wawili Respicius Patrick@
Mtazangira na Harieth Gerald katika kesi iliyofunguliwa mahakamani, ilidaiwa kwamba
Mwalimu Respicius Patrick @ Mtazangira na mwenzake Harieth Gerald wamemuua
Mwanafunzi Sperius Eradius tarehe 27/08/2018 katika shule ya msingi Kibeta iliyopo Manispaa
ya Bukoba mkoa wa Kagera.

Watuhumiwa walikana mashtaka

Kesi ilikuwa na mashahidi tisa (9) upande wa mashtaka/Jamhuri na Mashahid watatu upande wa
Watuhumiwa.

Vielelezo vilivyotolewa kama ushahidi mahakamani:

{I} Taarifa (Report) mbili za madaktari kuhusu uchunguzi wa mwili wa marehemu ili kujua
sababu za kifo chake. (Two postmortem reports) na

{II} Fimbo tatu kubwa au kuni.


(3 big sticks or fire woods.)

Kifo cha Sperius Eradius kimevuta hisia za watu wengi mno. Kwa sababu ni nadra kusikia
waalimu wameshtakiwa kwa kosa la kuua mwanafunzi.

Polisi walikuwa na kazi ngumu sana. Ndugu hawakuiamini report ya kwanza ya Daktari. Hii
ilipelekea kufanyika kwa uchunguzi mwingine wa mara ya pili.

Shule nzima iliweweseka. 27/08/3018 Ilikuwa ni kilio. Baadhi ya Wanafunzi na waalimu


walimlilia Sperius Eradius.

TWENDE KWENYE KESI KUANZA KUSIKILIZWA RASMI:

Hakimu alianza na upande wa Mashtaka (Jamhuri).

Shahidi namba moja (PW1) Benigius Benezeti, ambaye ni bodaboda aliiambia Mahakama kuwa,
alipigiwa simu na Mwalimu, Maadam Harieth Gerald, mteja wake wa siku zote, tarehe
27/8/2018, majira ya saa moja kamili asubuhi.
(Bodaboda) akaja akamchukua mpaka shule ya msingi Kibeta.

Ambapo Mwalimu (Harieth) alipokelewa na Wanafunzi. Mwalimu alikuwa na kikapu chenye


chupa ya chai, kipande cha kitenge, mtandio na koti.

Vyote hivyo vilichukuliwa na Wanafunzi ambao walikuwa wamekuja kumpokea.

Punde tu, Mwalimu Harieth akagundua pochi yake haipo. Akamtuma bodaboda afuatilie njiani
kuitafuta.

PW 1 (Bodaboda) akaenda ila hakuipata.


Baadae (bodaboda) akapewa taarifa na Mwalimu Harieth kwa njia ya simu kwamba, pochi
imeonekana na Mwanafunzi wa darasa tano.

Bodaboda akamwachia hilo suala mteja wake akaendelea na shughuli zake.

PW4 (Shahidi namba nne upande wa Mashtaka/Jamhuri), Goodluck Gilbert


ambaye Alikuwa kaka mkuu

na PW6 (Shahidi namba sita upande wa Mashtaka/Jamhuri) Mericiana Yohana, ambae Alikuwa
dada mkuu.

Wote, Wanafunzi wa shule ya msingi Kibeta

Ushahidi wao ambao pia uliungwa mkono na Shahidi namba 7 (PW 7) Enata Isidori (Mkuu wa
shule) na Shahidi namba nane (PW8) Sundi Elisha (Mkuu wa shule msaidizi)

Waliunga mkono ushahidi uliotolewa na bodaboda au shahidi namba moja (PW1)


Kwamba, Mwalimu Harieth alikuja na pikipiki (bodaboda) asubuhi na akapokelewa na
wanafunzi na darasa la pili ambao walibeba mizigo yake.

Baadae (Mwalimu Harieth) akaja asubuhi mstarini (SMART AREA), na akataka kujua kama
kuna mwanafunzi yeyote amemwona mtu aliyechukua pochi yake?

Hakuna aliyejitokeza kusema amemwona mtu yeyote. Wanafunzi wakaenda darasani.

Mwalimu Harieth akapiga hatua kwenda darasa la nne, ambapo mwanafunzi mmoja kwa jina
Elia alidai amemwona Sperius Eradius, Marehemu, akichukua pochi.
Sperius Alikuwa darasa la tano.

Mwalimu Harieth akaenda darasa la tano na kumchukua Sperius. Akataka kujua kama Sperius
alikuwa mwizi au alikuwa na tabia ya kutoroka shuleni?

Darasa wakasema HAPANA

Mwalimu Harieth akaondoka na Sperius akampeleka mpaka ofsini (staff room) na kumwuliza
kama amechukua pochi au la?

Sperius akasema HAPANA.


Mwalimu Harieth akamchapa Sperius fimbo tatu (3) kwenye mikono.

Kisha akaagiza kengele igongwe. Wanafunzi wakapanga mstari. Akawauliza kama kuna yeyote
alimwona Sperius akichukua pochi?

Wanafunzi wawili wa darasa la nne (Flora na Imelda) wakasema, ni Sperius ndiye aliichukua.
Wengine wakasema HAPANA.

Mwalimu Harieth akaagiza begi la Sperius na dada yake (Irene) yakaguliwe. Zoezi hilo
likafanyika ila pochi haikuonekana.

Kisha Mwalimu Harieth akamkabidhi Sperius kwa Mwalimu Respicius, mkuu wa nidhamu
(discipline master).

Shahidi namba nne upande wa Mashtaka/Jamhuri (PW4), Goodluck Gilbert (Kaka mkuu),
aliiambia Mahakama kuwa;

Mwalimu Harieth alimsimulia kwa ufupi Mwalimu Respicius (mkuu wa nidhamu), akisema
Wanafunzi wamemtaja Sperius kuwa amechukua pochi lakini Sperius anakana. Na kwamba
amemchapa fimbo tatu lakini bado, Sperius anasema Hapana.

Mwalimu Respicius (Mkuu wa nidhamu) akamuuliza Sperius kama amechukua pochi au la!
Sperius akakataa.

Mwalimu huyo wa nidhamu (Respicius) akamchukua mwanafunzi (Sperius) mpaka ofsini kisha
akachukua fimbo.
Akamuuliza tena mara ya pili swali lile lile. Sperius akasema HAPANA.
Akamchapa Sperius mguuni, mgongoni na kichwani. Akampiga Sperius fimbo nyingi nyingi
kabla ya kumwamuru apige magoti.

Kisha akauliza tena, "wewe umechukua pochi?" Sperius akasema HAPANA.

Mwalimu Respicius (mkuu wa nidhamu) akamwagiza PW4 (Goodluck Gilbert, Kaka mkuu),
achukue fimbo kutoka kwenye kuni (fire woods) ambazo zilikuwepo nje ya ofsi, huku
akimuonesha kipande fulani cha kuni.

PW4 akaona kile kipande ni kikubwa mno. Akachukua fimbo ndogo na kumpelekea Mwalimu

Mwalimu Respicius akampiga nayo mgongoni huku akisema, hiyo haikuwa ile anayotaka

Akamwagiza awaite Wanafunzi wa darasa la nne ambao walikuwa na mapanga. Walipokuja


akawaagiza kuleta vipande sita vya kuni (six (6) pieces of fire woods) na waviweke tayari kwa
kazi (and prepare them for the job.)

Wakaleta vipande sita na kumkabidhi.


Akachagua vitatu kati yake, vile ambavyo vilikuwa vimenyooka vizuri. Kisha akabeba kimoja
akamfuta Sperius na kumwagiza avue kaptura zake na viatu

Sperius akavua akabaki na “pensi” & “bukta”

Kisha Mwalimu Respicius akaanza kumpiga na fimbo. Akampiga kwenye viungo (joints) vya
miguu na mgongoni.

Sperius akakubali kuwa yeye ndo ana pochi. Mwalimu Respicius akawatuma PW4 (Goodluck
Gilbert, Kaka mkuu) na wanafunzi wawili wa darasa la saba kwenda na Sperius kuleta pochi.

Wakaenda na Sperius lakini hawakuipata.

Sperius Akawaambia kwamba, alikuwa amekubali ili asiendelee kupigwa zaidi.


Wakamrudisha tena kwa Mwalimu Respicius, ambae alipatwa na hasira na kusema “ngoja
niwaonyesheni kazi ya jiwe”.

Mwalimu Respicius, akasogea darasa la saba na kuchukua BIKARI. Kisha akarudi kwa Sperius
na kusema, “Nitakuwekea alama ambayo utamuwekea hadi mjukuu”.
Akaingiza BIKARI kwenye kidole cha Sperius kwenye kucha na kuvuta kucha kuja juu.
Akafanya hivyo, huku akisema, “Niambie waleti ilipo”

Sperius akasema NO.

Mwalimu Respicius akavuta juu kucha.

Sperius akasema “sina”. Mwalimu Respicius akaendelea kumpiga kwa kutumia fimbo

Hali ya Sperius ikabadilika na kuwa mbaya. Kisha (Sperius) akasema “acha niwapeleke pochi
ilipo”

Wanafunzi wakaambatana na Sperius kwenda kutafuta pochi. Wakiwa na Mwalimu wao.


Wakafika ile sehemu ila hawakuipata.

Mwalimu Respicius akaendelea kumpiga Sperius, ambapo alianguka wakiwa njiani wakati
wanashika barabara kutoka vichakani.

Mwalimu Respicius akaendelea kumpiga Sperius huku akisema “huu ni usanii, hivi sivyo
wanavyozimiaga”

Wakasimama pale kwa muda. Sperius akapata nguvu. Akasema kwamba hawezi kutembea na
akaomba kubebwa

Mwalimu Respicius akampiga tena akisema huo ulikuwa ni “usanii” kama mpango (plan) wa
kutoroka. Akaagiza Wanafunzi wavue masweta yao Kisha wampepee apate hewa. Wanafunzi
wakafanya hivyo.

Sperius akapata nguvu kiasi. Wakaelekea jengo la chekechea kutafuta pochi. Lakini hawakuweza
kuipata. Mwalimu Respicius akampiga kichwani. Sperius akaanguka chini. Akapiga kifua
kwenye jiwe. Akaishiwa nguvu.

Mwalimu Respicius akaita bodaboda. Wakapanda pikipiki na Sperius na kuondoka.

PW4 (Goodluck Gilbert, Kaka mkuu) alielezea muda na kusema kipigo kilianza saa mbili kamili
(8:00 AM) asubuhi na kuendelea mpaka saa tano kamili (11:00 AM) asubuhi.
Ushahidi wa (Shahidi namba sita upande wa Mashtaka/Jamhuri) PW6 Mericiana Yohana, ambae
Alikuwa dada mkuu unafanana na huo wa PW4 (Goodluck Gilbert, Kaka mkuu) in all material
areas.

Shahidi namba 7 (PW 7) Enata Isidori (Mkuu wa shule) alitoa ushahidi kuwa, alikuja ofsini
mapema siku hiyo.

Yeye na Mratibu Elimu wa kata (Ward Education Coordinator) walikuwa na mpango wa kwenda
kutafuta Wanafunzi watoro wa darasa la saba.

Walipanga wawarudishe shule ili kujaza form za TSM9 ili waweze kufanya Mitihani yao ya
mwisho

Hiyo ilikuwa pia ni wiki ya Mitihani na shule ilikuwa tayari kwa ajili ya Mitihani.

Akiwa ofsini, majira ya 7:15 AM, Mwalimu Harieth akaja na kusema kwamba pochi yake
imepotea.

Wakawa na majadiliano kadhaa. (Mkuu wa shule) Akamshauri Mwalimu Harieth, afuatilie njiani
hadi nyumbani kwake. Mwalimu Harieth akaomba ruhusa na kuondoka.

PW7 Enata Isidori (Mkuu wa shule) akampangia Mwalimu Alpinensia kuendelea na majukumu
ya Mwalimu Harieth, ambayo ilikuwa ni kusimamia Mitihani ya darasa la pili.

PW7 (mkuu wa shule) akaondoka na kumwachia uongozi wa shule PW8, Mwalimu Sundi
Elisha, Mkuu wa shule msaidizi

Shahidi namba nane upande wa Mashtaka/Jamhuri, PW8, Mwalimu Sundi Elisha, Mkuu wa
shule msaidizi alitoa ushahidi kwamba, aliwasili shuleni siku hiyo na pikipiki na kuelekea moja
kwa moja kwenye ofsi ya mkuu wa shule kusaini daftari la mahudhurio.

Akamkuta Mwalimu Harieth Ofsini. Wakasalimiana kila mmoja. Mwalimu Harieth akamwomba
amzuie dereva pikipiki (bodaboda) asiondoke, akisema kwamba alikuwa amepoteza pochi yake.
Na akataka kutoka nje.

Akamtaka bodaboda asubiri. Bodaboda akabaki na Mwalimu Harieth.

Kisha PW8, Mwalimu Sundi Elisha, Mkuu wa shule msaidizi aliachiwa uongozi wa shule na
Mkuu wa shule kama ilivyoelezwa hapo awali.
PW8, Mwalimu Sundi Elisha, Mkuu wa shule msaidizi alitoa ushahidi wake kwamba Mwalimu
Harieth alikuja baadae na kusema hajafanikiwa kuipata pochi njiani.

Aliwauliza Wanafunzi wa darasa la pili kama wameiona pochi, wakasema HAPANA.


Akaondoka na baadae akaja na Sperius akasema baadhi ya wanafunzi wamemwona na pochi.

PW8, Mkuu wa shule msaidizi akamtahadharisha kuwa sio vizuri kuwaamini sana Wanafunzi.
Akamshauri kutafuta uthibitisho zaidi.

Wakawaita wanafunzi. Mwalimu Harieth akaahidi kutoa Tsh 5, 000 kwa mwanafunzi ambae
angeweza kumwonesha aliyechukua pochi.

Baadhi wakasema kwamba walimwona Sperius anaichukua, wengine wakasema HAPANA

PW8, (Mkuu wa shule msaidizi) Akamshauri Mwalimu Harieth kutafuta uthibitisho zaidi.
Mwalimu Harieth hakuweza kupokea ushauri wake.

Mwalimu Harieth akamchapa Sperius fimbo tatu kwenye matako.

Sperius alishika fimbo wakati Mwalimu Harieth anaenda kupiga fimbo ya nne

Sperius akaenda kwa PW8 (Mwalimu Sundi Elisha, Mkuu wa shule msaidizi), akisema,
“Naomba msaada”.

Mwalimu Harieth akamjibu PW8 akisema “Kwani wewe ndio umemtuma hiyo walet?”

Kisha Mwalimu Harieth akamchukua mwanafunzi huyo na kumpeleka kwa mwalimu wa


nidhamu (discipline master).

Kwa kuwa ulikuwa muda wa Mitihani, PW8 akaelekea darasani kuendelea kusimamia Mitihani
ya MEMKWA, akawaachia mgogoro huo Mwalimu Harieth na Mwalimu Respicius (Mwalimu
wa nidhamu)

PW8 anashuhudia kuwa, alipata taarifa ya kupigwa kwa mwanafunzi kutoka kwa Mwalimu
Claudia Modest.

PW8, alikuwa Kwenye darasa la MEMKWA wakati huo.


Wakaenda hima ofsini ambapo alimwona Mwalimu Respicius anampiga mwanafunzi kwa
kipande cha ukuni. Akamsukuma Mwalimu Respicius pembeni, akachukua kipande cha ukuni na
kukirusha mbali. Kisha akamtoa Sperius nje ya ofsi

Hali ya Sperius ilikuwa mbaya.


Mwalimu Respicius akamwambia kwamba, Sperius tayari amekiri kilichobaki ni kwenda na
kuleta pochi.

PW8, Akamwamuru Mwalimu Harieth waende na (Mwalimu wa nidhamu) hadi eneo husika.
Wakaondoka pamoja, ila Mwalimu Harieth akarudi muda si mrefu, huku akisema kwamba
Mwalimu Respicius alikuwa amemruhusu arudi wakiwa njiani na kumwambia kuwa ataenda
peke yake.

PW8 hakujua kilichoendelea kwa Sperius, alikuja kujua baadaye.

PW8 akamsimulia PW7, Enata Isidori (Mkuu wa shule) alipokuja baadaye siku Hiyo, kwamba
Mwalimu Respicius amempiga Sperius sana na kuondoka naye kwenda kusikojulikana.

PW7 (mkuu wa shule) akampigia simu Mwalimu Respicius ambaye alirudi baadaye peke yake
bila Sperius, na kuwaambia kwamba hakupata ushirikiano kutoka kwa wazazi wa Sperius na
kwamba amemwacha Sperius nyumbani.

Muda si mrefu polisi wakafika pale shuleni na kuwaambia kuwa Sperius amefariki.

Siku ikageuka kuwa mbaya kwa waalimu na wanafunzi kwa vilio.

Mwalimu Respicius akatafutwa lakini hakuonekana. Alikuja kukamatwa baadae kutoka


kichakani ambapo alikuwa amejificha, akatiwa pingu na kupelekwa kituo cha polisi.

PW7, PW8 na Mwalimu Harieth, nao pia walipelekwa kituo cha polisi kuhojiwa.

Na kuhusu kilichoendelea pale, baada ya kuondoka kwa Mwalimu Respicius na Mwanafunzi


Sperius

Kuna ushahidi wa Shahidi namba mbili upande wa Mashtaka/Jamhuri, PW2 Happiness


Tinkaligale ambaye ni mama (Mlezi) wa Sperius na Shahidi namba tatu upande wa Mashtaka,
(PW3) Simon Samson.
PW2, mama (Mlezi) wa Sperius, aliiambia Mahakama kuwa, alipata taarifa kwamba Sperius
alikuwa kando ya njia hajiwezi.

Akachukua pikipiki na kuelekea hilo eneo. Akamkuta Sperius eneo linaitwa Radio Vision. Huku
kukiwa na watu kibao. Akamwona na Mwalimu Respicius amesimama ameshikilia fimbo.

Sperius alikuwa amelazwa chini hajiwezi na haongei. Mama (Mlezi) wa Sperius akataka kujua
kipi kimetokea kwa mwanae.

Mwalimu Respicius akajibu kwa kifupi kwamba “Amekwapua”. Sperius hakuwa na kaptura
wala viatu. Shati lake lilikuwa limevaliwa nusu upande.

Mama wa Sperius akaomba msaada watu waliokuwepo pale na kumpeleka Sperius Hospital ya
mkoa apate msaada.

Mwalimu Respicius, akachukua pikipiki nyingine wakati huo na kukimbia. Sperius aliwekewa
Oxygen, lakini muda si mrefu ikatangazwa amefariki.

Taarifa zilitumwa polisi na PW3, Simon Samson. PW3 pia ni miongoni mwa waliowachukua
Sperius na mama yake na kuwapeleka hospitali. Ushahidi wake unafanana na huo wa PW2
(mama wa Sperius) katika kila kitu.

Alisimulia kuwa Sperius alikuwa amevimba miguu na kichwa. Pia aliona alama za kupigwa
kwenye mbavu.

Mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na Dr. Kahima Jackson, Daktari wa magonjwa


kutoka Hospital ya Rufaa Bugando

Huu ulikuwa ni uchunguzi wa mara ya pili ambao ulifuatia, baada ya uchunguzi wa awali
uliofanywa na Dr. Otieno (DW3).

Dr. Kahima alitoa maelezo ya uchunguzi. Ambapo alifanya vipimo vya nje na ndani.

Vipimo vya nje vilionyesha baadhi ya majeraha yaliyotofautiana ukubwa, urefu na upana.
Majeraha hayo yalikuwa kichwani, usoni, mashavuni, nyuma ya shingo, mabegani, mikononi,
kifuani, mgongoni, tumboni, matakoni, na kwenye miguu yote miwili.
Alisema kwamba 95% ya majeraha yalikuwa ni alama (makovu) zilizosababishwa na kitu
kisichokuwa na ncha kali (butu). Pia akaongeza kuwa, kulikuwa na aina mbalimbali za alama
(makovu) kichwani na mikononi.

Na kwamba kulikuwa na alama kidoleni zilizowekwa na kitu chenye ncha kali (Kama kuchoma).

Alifungua kichwa, kifua na tumbo ila hakuweza kuona tatizo ambalo lilisababisha kifo. Alitaja
sababu ya kifo kuwa Neurogenic shock iliyotokana na kitu kisichokuwa na ncha kali (blunt
object).

Taarifa yake ya uchunguzi ilipokelewa Mahakamani kama kielelezo P1.

Shahidi namba tisa upande wa Mashtaka/Jamhuri PW9, Inspekta msaidizi Christopher Kapela
ndiye alikuwa mpelelezi wa kesi. Alielezea namna alivyopata taarifa, na kwenda shule kukamata
mtuhumiwa na akakusanya ushahidi.

Ambapo alichora ramani mbili za eneo la tukio, pale shuleni (Kielelezo P2) na eneo ambapo
Sperius alikutwa na kuchukuliwa na mama yake. (Kielelezo P3). Vilevile aliwasilisha vipande
vitatu (3) vya ukuni (Kielelezo P4) ambavyo inadaiwa vilitumika kutekeleza uhalifu.

KUSIKILIZWA KESI UPANDE WA MTUHUMIWA/MSHTAKIWA:

Mtuhumiwa alikuwa na haya ya kusema katika kujitetea.

Shahidi namba moja DW1, Respicius Patrick Mutazangira (51) (Mtuhumiwa mwenyewe)
aliiambia Mahakama kwamba, alienda shuleni mapema siku hiyo na kuanza kufundisha
wanafunzi wa darasa la saba.

Yeye ni Mwalimu wa hesabu na Sayansi. Alikuwa na kipindi maalum cha hesabu siku hiyo
ambacho kilianza saa 7:00 AM. Alifundisha mpaka 8:40 AM, akaondoka na kwenda ofsini (staff
room) kusahihisha makaratasi.

Punde, Mwalimu Harieth akamjia na kusema kwamba pochi yake imeibiwa na Mwanafunzi.
Akamtaja huyo mwanafunzi kuwa ni Sperius, marehemu.

Akawaita wanafunzi wa darasa la sita na darasa la saba karibu na Ofsi. Akamtuma Amimu
Haruna awaite wazazi wa Sperius. Pia akawaagiza wanafunzi kwenda na kumleta Sperius. Ila
muda si mrefu, Mwalimu Harieth akaja na Sperius staff room na (Mwalimu Harieth)
akamwomba (Mwalimu Respicius) amsadie.
Akataka kujua Sperius alikuwa wapi. Sperius akanyamaza. Akampiga fimbo tatu mikononi kwa
kosa la kuondoka nje ya shule bila ruhusa.

Kisha akagundua kuwa Sperius alivaa kaptura nne (4). Hiyo ilikuwa tabia mbaya. Akamwamuru
avue kaptura tatu (3). Akabaki na kaptura ya shule, bukta na nguo ya ndani (pants). Akampiga
fimbo tatu miguuni kwa hilo kosa.

Mwalimu Sundi Elisha (PW8) Mkuu wa shule msaidizi, akafika wakati huo, akachukua fimbo na
kuitupa mbali.

DW1, Respicius Patrick Mutazangira (mtuhumiwa). Aliilezea fimbo hiyo kuwa ni fimbo ya
mwanzi na sio ukuni kama walivyosema PW4, PW6 and PW8.

DW1 (mtuhumiwa) akaendelea kusema kwamba, alimchukua mwanafunzi (Sperius) kwa nia ya
kwenda kuwaona wazazi wake nyumbani. Na kwamba, hakuweza kutembea sana kwa sababu
alikuwa na matatizo ya kiafya. Akachukua pikipiki

Wakaondoka na Sperius. Ila wakati wako njiani, kukazuka mabishano kati yake na dereva wa
pikipiki, kuhusu kiasi cha nauli anachotakiwa kulipa.

Bodaboda alitaka 3,000/= akisema eneo wanakoenda ni mbali sana. Wakashindwa kuelewana.
Akamlipa 1,000/= akashukia njiani. Akiwa pale, akatokea mwanamke fulani na kuuliza kipi
kilikuwa kinaendelea. Akamwambia kuwa, anawatafuta wazazi wa Sperius.

Yule mwanamke akachukua simu yake na kumpigia mtu fulani. Akaja mwanamke mmoja na
kupiga yowe akisema “unamuua mwanangu!”

Watu wengi wakaja. Yule mwanamke akamchukua mwanafunzi akaondoka. Na yeye


(mtuhumiwa) akachukua pikipiki na kurudi shuleni.

Akapigiwa simu na Mkuu wa shule akiwa njiani. Akafika shuleni na kuwasimulia waalimu
kilichotokea. Kisha akondoka shuleni kwenda kutafuta simu yake. Ambapo ilimchukua takribani
masaa mawili (2) kwa sababu kulikuwa na mvua kubwa. Akiwa anarudi shuleni, aliwekwa chini
ya ulinzi.

(Mtuhumiwa) Alikana kumpiga mwanafunzi, isipokuwa tu kwa zile fimbo sita za mwanzi.
DW2, Shahidi namba mbili (Mshitakiwa/mtuhumiwa mwingine), Harieth Gerald Sahini ( 47),
Aliiambia Mahakama kwamba, aliwasili shuleni siku hiyo na kupokelewa na wanafunzi wa
darasa la tano, la nne na la pili. Akafungua pochi yake na kumpa bodaboda Tsh 1,000/=

Alikuwa na kikapu, pochi, koti, kitenge na mtandio wa kichwani, ambavyo aliwapa wanafunzi.
Akabaki mikono tupu. Akaelekea Ofsi ya Mkuu wa shule kusaini daftari la mahudhurio.

Kisha akaenda staff room kukagua mizigo yake. Kila kitu kilikuwepo isipokuwa pochi. Akarudi
kwenye Ofsi ya Mkuu wa shule na kumwambia kwamba pochi yake imepotea.

Mkuu wa shule akamwelekeza afuatilie kwa wanafunzi waliompokea. Akaenda kwa wanafunzi
wa darasa la pili. Wakamwambia aliyeichukua ni Sperius, mwanafunzi wa darasa la tano. Pia
aliambiwa kwamba Flora, Imelda na Elia walikuwepo pia.

DW2 (mshitakiwa) Harieth Gerald, akaendelea kusema kwamba, alienda darasa la tano ila
hakuweza kumpata Sperius.

Akaripoti suala hilo kwa Mwalimu wa nidhamu (Mwalimu Respicius) na akamwachia


alishughulikie. Yeye akaenda darasa la pili kusimamia Mitihani.

(Mshitakiwa) Harieth Gerald alikana kuhusu kurudi nyumbani kutafuta pochi siku hiyo. Alikana
kuongea na bodaboda (PW1) kwenye simu kuhusu pochi. Pia Alikana kumpiga mwanafunzi
(Sperius).

Akitaja vilivyokuwemo kwenye pochi, Mshitakiwa (Harieth Gerald) alisema, Pochi ilikuwa na
simu, vitambulisho (Kitambulisho cha kazi, cha Taifa na
cha kura) na Tshs. 75,000/=.

Na kwamba hakuweza kuipata pochi hadi sasa. Alikana kuhusika kwenye mauaji ya mwanafunzi
(Sperius). Alikubali kuwa, yeye pamoja na waalimu Wengine walipelekwa kituo cha polisi
baadaye siku hiyo, kama ilivyotangulia kuelezwa huko juu.

(Daktari) kama Shahidi namba tatu, upande wa utetezi/Defence (Washtakiwa), DW3 Dr. Felix
Otieno aliiambia Mahakama kwamba,

Alifanya uchunguzi wa kwanza wa mwili wa marehemu (first Post-Mortem


examination) siku hiyo hiyo 27/08/2018. Akaona alama/makovu mbalimbali ya zamani usoni,
mikononi, miguuni, mgongoni na tumboni. Akafunua tumbo ila hakuona chochote kisichokuwa
cha kawaida.Taarifa yake ilipokelewa kama kielelezo D4.
DW3 Dr. Felix Otieno alielezea sababu ya kifo kuwa, majeraha ya kimwili (physical injury.)

Upande wa utetezi (washtakiwa) ulikuwa na vielelezo vingine vitatu, ambavyo ni maelezo


yaliyotolewa polisi na Simon
Samson (PW3), Goodluck Gilbert (PW4) na Mericiana Yohana (PW6).

Vielelezo hivi vilitolewa na kupokelewa kwa ajili ya kulinganisha maelezo.

Washtakiwa walitaka kulinganisha kilichosemwa kituo cha polisi na kilichosemwa Mahakamani,


hususani kwenye maelezo yanayohusu pochi.

Wawakilishi (Mawakili) wa pande zote mbili walipewa nafasi kuongea na Mahakama katika
uwasilishaji wao wa mwisho.

Mr. Kabunga na Ms. Aneth Lwiza waliwakilisha upande wa utetezi (washtakiwa) huku Mr.
Hashimu Ngole PSA (Wakili mkuu wa Serikali) akiwakilisha upande wa Mashtaka (Jamhuri)

Upande wa utetezi (Washtakiwa), walidai kwamba Washtaki (Jamhuri) wameshindwa


kuthibitisha kesi pasipo na shaka na wakaiomba Mahakama iwaachie huru watuhumiwa.

Wakairejesha Mahakama kwenye kesi ya Nathaniel Alphonce Mapunda and another v. R [2006]
TLR 395 wakisema ni heri kuwaachia huru watu 100 wenye hatia kuliko kumfunga kimakosa
mtu mmoja asiye na hatia.

Wakasema, kesi ya Jamuhuri ina mkanganyiko (Utata) unaopelekea iwe dhaifu. Wakarejea kesi
ya Christian Kale and Another v. R [1992] TLR 302 kuunga mkono hoja yao kwamba,
Watuhumiwa mbele ya Mahakama wasifungwe kwa sababu tu ya udhaifu wao katika kujitetea
ila kwa sababu ya ushahidi wenye nguvu wa upande wa Mashtaka (Jamhuri).

Waliwasilisha kuwa, Mkanganyiko (Utata) na kutofautiana kwa maelezo ya mashahidi upande


wa Jamhuri, vimeharibu uaminifu wa mashahidi wa msingi wa Jamhuri, ambao ni PW4, PW6 na
PW8.

Wakasema kwamba, kule kuwepo tu kwa watuhumiwa shuleni siku hiyo ya tukio, kusichukuliwe
kuwa wao ndio waliomuua marehemu. Wakarejerea kesi ya Damian Petro v.R [1980] TLR 260
kuunga mkono hii hoja yao.
Pia upande wa utetezi waliirejesha mahakama kwenye kesi ya Salum Mhando v.R [1993] TLR
170, Crospery Ntalinda v R CAT Criminal Appeal No.312 of 2015, Goodluck Kyando v R
[2006] TLR 363, Michael Aeshi v R [1992] TLR 92 and Kibwana Salehe v R [1968] TLR 391
kuonesha kwamba, kukiwa na mkanganyiko (Utata), ushahidi huo lazima ukataliwe.
Wakaongeza kuwa, uaminifu wa mashahidi umeharibiwa.

Upande wa utetezi (washtakiwa), ukaonesha maeneo yafuatayo kama sehemu zenye


(mkanganyiko) utata;

Moja, ushahidi kuhusu pochi.


pili, ushahidi kuhusu idadi ya kengele zilizolia siku hiyo.
Tatu, ushahidi kuhusu kutolewa kwa kucha na
Nne, ushahidi kuhusu sehemu ambayo Mwalimu Harieth alimpiga Sperius fimbo.

Pia waliongezea kwa kutaja maeneo mengine mawili;

Kwamba, upande wa Mashtaka umeshindwa kumuita Mwalimu Alipensia athibitishe kuwa yeye
ndo alisimamia Mitihani siku hiyo, kitu ambacho kinawabeba. (A fact which give an advantage
to them).

Wakaielekeza Mahakama kwenye kesi ya Aziza Abdalah v R [1991]TLR 71, wakidai kwamba
kushindwa kumleta Shahidi muhimu, kunaipa Mahakama haki ya kuja na tafsri yoyote kuhusu
jambo husika kwenye kesi. (Entitle the court to an
adverse inference to the prosecution on the point.)

Pia walidai kwamba, ushahidi wa uchoraji ni wa kukuzwa (kutiwa chumvi mno) hivyo unapaswa
kupuuzwa. (Evidence on feinting is an exaggeration which should be neglected.)

Wakizungumzia (Sheria ya) Education No. 24 of 2002, upande wa utetezi, walidai kwamba,
haiwafungi wateja wao, kwa sababu kulikuwa na ushahidi unaoonyesha kuwa, mshtakiwa
(mtuhumiwa) namba mbili (Mwalimu Harieth) hakumpiga mwanafunzi, na zile fimbo sita
alizochapa mtuhumiwa namba moja (Mwalimu Respicius) zilikuwa zimehalalishwa na baraza la
shule (had justification from the school committee).

Wakielezea yaliyomo kwenye mkanganyiko (Utata), upande wa utetezi (washtakiwa), walisema,


ushahidi wa PW4 na PW6 ambao unaonesha kwamba Mwalimu Harieth hakuja na pochi shuleni
hauendani na maelezo yao waliyotoa polisi (Vielelezo D2 na D3) hivyo kuufanya ushahidi huo
uwe wa uongo.
Wakasema, hao mashahidi wamekana kile walichosema kituo cha polisi, hii inawafanya kuwa
waongo na wasioaminika.

Kuhusu kengele, utetezi upande wa washtakiwa waliwasilisha kuwa, PW8 hakusikia kengele
nyingi Kama ilivyodaiwa na PW4 and PW6 hii inawafanya kuwa waongo na wasioaminika.

Wakaendelea kusema kwamba, PW4 ni mwongo kwa sababu ushahidi wake unahitilafiana na
ule wa Daktari kwenye kipengele cha kutolewa kucha.

Upande wa utetezi ukaialika mahakama kutazama kwamba ushahidi wa PW4 na PW6


Unahitilafiana na ule wa PW8 kuhusu eneo ambapo fimbo za Mwalimu Harieth zilichapwa.

Wakasema, wakati PW8 alisema kwamba fimbo zilichapwa matakoni, PW4 na PW6 wakasema
kwamba, Mwalimu Harieth alimchapa Sperius mikononi. Hii inawafanya PW4 and PW6 kuwa
waongo na wasioaminika

Upande wa Mashtaka (Jamhuri) ukiwakilishwa na Mr. Hashimu Ngole, PSA (Wakili mkuu wa
Serikali), wakasema kwamba neno (kirai) BEYOND REASONABLE DOUBT (Iliyothibitishwa
pasipo na shaka yoyote) sharti itafsiriwe vizuri ipasavyo (properly).

Akailekeza Mahakama kwenye kesi ya Magendo Paul and Another v R [1993] TLR 125,
ambayo (kesi hii) ilifuata maamuzi ya House of Lords (Mahakama ya juu kuliko zote Uingereza)
katika kesi ya Millar v Minister of Pensions ambapo (Judge) Lord Denning alinukuliwa akisema

Sheria itashindwa kuilinda jamii, kama Mahakama itaruhusu tofauti ndogo ndogo zichukue
nafasi ya haki.

Akasema kwamba, kutofautiana huwa kupo mara zote kwenye kesi, cha muhimu ni kuchunguza,
Je! hizo tofauti zinafika kwenye kiini au mzizi wa kesi au la!

Mr. Hashimu Ngole akawasilisha kwamba, mzizi mkuu kwenye kesi iliyopo Mahakamani ni
kupigwa na kifo kilichotokana na kupigwa huko. Hivyo vipengele vingine ni vitu vidogo vidogo
tu. Alisema.

Upande wa Mashtaka (Jamhuri) uliwasilisha kuwa, mashahidi wake walikuwa wazi kabisa na
thabiti (very specific and firm) kuhusu namna marehemu alivyopigwa na kufariki.
Akiongelea maelezo yaliyotolewa polisi, PSA (Wakili mkuu wa Serikali), alisema kwamba
maelezo yanayotolewa polisi na mtuhumiwa sio ushahidi (police statements are not evidence),
hivyo yasiingizwe kwenye kesi kuichanganya Mahakama. Na Pia hayo (maelezo) sio sehemu ya
ushahidi wao.

Isitoshe, maelezo hayo hayaoneshi kama yalisomwa kwa mashahidi (baada ya kuandikwa).

Akaendelea kuwasilisha kwamba, mashahidi wake wamekana kuhusu kutoa maelezo kama hayo
kituo cha polisi Wala
Hawakutoa maelezo mbele ya PW9.

The Principal State Attorney (Wakili mkuu wa Serikali), akasema kwamba, haoni uzito wa huo
utata (mkanganyiko) kati ya PW5 and PW4 kuhusu kucha kwa sababu suala sio kwamba kucha
haikutoka, ila suala au hoja ni kwamba Bikari ilitumika kumwadhibu mwanafunzi.

Aliuchukulia huo mkanganyiko (utata) kama kitu kidogo na akaiomba Mahakama iupuuze.

Akanukuu kesi ya Marando Slaa Hofu and 3 others v R CAT Criminal Appeal No.246 of 2011,
Chrisant John v R CAT Criminal Appeal No. 313 of 2015, Elia Nshambwa Shapwata and
another v R CAT Criminal
Appeal No. 92 2007, Edson Simon Mwombeki v R CAT Criminal Appeal No. 94 of 2016,
Lusungu Duwe v R CAT Criminal Appeal No.76 of 2014 na R v
Golda (1960) I WLR 1169 Kuunga mkono hoja kwamba, mkanganyiko (utata) mdogo unatakiwa
kupuuzwa

Mr. Ngole akairejesha Mahakama kwenye kesi ya R v Golkadas Karia (1951) EACA 211 kuhusu
doctrine of common intention (nia moja ya kutimiza kusudio lisilo halali).

Huku akirejea kesi hiyo, akasema kwamba, (common intention) sio lazima kwenye kila kesi,
kwamba lazima watu wawili wakutane na kukubaliana kufanya uhalifu. Maafikiano ya kufanya
uhalifu yanaweza kuonekana kutokana na vitendo.

Na kwa mtazamo wake, vitendo vya mtuhumiwa namba moja na mtuhumiwa namba mbili,
kwenye hii kesi, inaonesha kuwa, walikuwa na dhamira au nia moja (common plan) ya kumuua
Sperius.

Anasema kwamba, mtuhumiwa (mshitakiwa) namba mbili (Mwalimu Harieth) aliyakataa


maneno ya wanafunzi kwamba Sperius hakuwa na tabia ya wizi.
Mwalimu Harieth aliwapuuza wanafunzi na kuendelea kumpiga Sperius na mwisho kabisa
akamkabidhi Sperius kwa Mwalimu Respecius, ambaye alimpiga mpaka akafa.

Kwake yeye, (Wakili mkuu wa Serikali, Mr. Ngole), hii inaashiria kwamba, wahalifu hao wawili
walikuwa na nia moja ya kumwua mwanafunzi.

Mr. Ngole akaendelea zaidi na kuiambia Mahakama kwamba, kuna ushahidi unaoonyesha
kwamba Watuhumiwa wameongea uongo ili kujitetea.

Akasema kwamba, kwa kuwa Watuhumiwa hawana jukumu la kuthibitisha unyofu wao
(kutokuwa na hatia kwao), ila kama wakisema uongo, msimamo wa kisheria ni kuwa, uongo wao
unaithibitisha kesi ya Jamhuri.

Akitoa mfano, alisema kwamba, mtuhumiwa namba mbili (Mwalimu Harieth) alidanganya pale
aliposema kwamba hajampiga marehemu (Sperius) wala kutoka nje ya shule.

Akaielekeza Mahakama kwenye kesi ya Pascal mwita and another v R [1993]TLR 295 na Musa
Timotheo and another v R [1993] TLR 125 kisha akaialika Mahakama itamke kwamba huo
uongo wa Watuhumiwa unaithibitisha kesi ya Jamhuri.

Na kuhusu Nia ya uwovu (malice aforethought), Mr. Ngole aliirejesha Mahakama kwenye
kifungu 200 cha sheria ya kanuni ya adhabu (Penal Code), kesi ya Chrisant John na kesi ya
Enock Kipela v R CAT Criminal Appeal No. 150 of 1994.

Upande wa Mashtaka ukawasilisha kwamba, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba Mwalimu


Respicius alimpiga mwanafunzi (Sperius) mno, na akaongezea kwamba, namna kupigwa huko
kulivyofanywa kuliashiria kwamba alidhamiria kumwua Sperius.

Akaielekeza Mahakama kwenye Education Circular (sheria) ambayo inataja fimbo nne tu, kisha
akaendelea kusema kwamba, marehemu alipigwa fimbo nyingi bila ushahidi wa kuiba pochi.

Akaikataa hoja ya upande wa utetezi kwamba Mwalimu Respicius alikuwa na mamlaka kutoka
baraza la shule kuchapa zaidi ya fimbo nne, akidai kwamba, baraza halikuwa na mamlaka ya
kufanya hivyo.

Akaiomba Mahakama ikubali kuwa, Jamhuri imethibitisha kesi yake pasipo na shaka, (beyond
reasonable doubts) dhidi ya Watuhumiwa wote hivyo Mahakama iwatie hatiani kama
walivyoshtakiwa.
Waheshimiwa wazee wa baraza (assessors/Wasaidizi wa Jaji) wawili walishawishiwa na
ushahidi kama ulivyoainishwa hapo juu pamoja na sheria husika, kwa umakini kabla
hawajaulizwa kutoa maoni yao.

assessors wawili wakawatia hatiani kwa mauaji, Watuhumiwa wote wawili.

(JUDGE ANAENDELEA KUONGEA)

Wakaniambia kwamba, kulikuwa na ushahidi mzuri unaoonyesha kwamba Sperius alikufa


kutokana na kupigwa na Mwalimu Respicius.

Wakaendelea kusema kwamba, Mwalimu Harieth naye aliweka mkono wake, kwa sababu yeye
ndiye aliyemkabidhi Sperius kwa Mwalimu Respicius.

Pia (Mwalimu Harieth) aliukataa ushauri wa Mkuu wa shule msaidizi, kuhusu kufanya utafiti
zaidi ili apate uhakika, na badala yake akampeleka Sperius kwa Mwalimu Respicius ambaye
alimpiga Sperius mpaka akafa.

(Assessors) wakaongeza kuwa, Mwalimu Harieth hakuweza hata kujitokeza kuzuia kilichokuwa
kinaendelea, anaonekana kuunga mkono kile kilichokuwa kinaendelea.

Assessor mmoja aliungana na wenzake katika maamuzi yao kuhusu Mwalimu


Respicius, ila akakataa kuunga mkono uamuzi wa kumtia hatiani Mwalimu
Harieth.

Alitoa wazo (hoja) kwamba, ushahidi wa kumpiga Sperius ambao unamhusisha Mwalimu
Harieth unahitilafiana. Ambapo PW4 na PW6, walisema kwamba alimpiga Sperius mikononi.
PW8 ambaye pia alikuwepo, akasema kwamba, alimchapa matakoni.

Amewapa fursa ya kumtilia shaka Mwalimu Harieth na kumkuta asiye na hatia.

(UCHAMBUZI/MTAZAMO WA JUDGE MWENYEWE RASMI):

Nilipata fursa ya kupitia ushahidi na maoni kwa makini.

Baada ya kupitia ushahidi na maoni ya pande zote kwa makini, Nimebaini kuwa, Fact 12
hazijakanwa
Moja, Watuhumiwa hawajakana kumjua marehemu. Wote walisema walikuwa wanamjua
marehemu Sperius Eradius vizuri kabisa, mwanafunzi wa darasa la tano.

Pili, Watuhumiwa hawakukana kwamba, Sperius Eradius alikuwepo shuleni asubuhi katika afya
njema

Tatu, Watuhumiwa hawakani kwamba, Sperius alituhumiwa kuiba pochi na

Nne, Watuhumiwa hawakani kwamba, Sperius Eradius kwa sasa amefariki.

Tano, Watuhumiwa hawakani kwamba, mwili wa Sperius Eradius ulikutwa na majeraha


mbalimbali kuzunguka mwili mzima.

Sita, Mwalimu Harieth anakubali kwamba, alipokelewa na Wanafunzi ambao walichukua kikapu
chake na vitu vingine alivyokuwa navyo

Saba, Mwalimu Harieth anakubali kwamba, alienda kwenye Ofsi ya Mkuu wa shule ambapo
aliwakuta PW7 and PW8.

Nane, Mwalimu Harieth anakubali kwamba, aliwaambia PW7 and PW8 kuwa pochi yake
ilikuwa haionekani.

Tisa, Mwalimu Harieth anakiri kwamba, alimshirikisha Mwalimu Respicius kulishughulikia


tatizo kwa uwezo wake kama Mwalimu wa nidhamu.

Kumi, Mwalimu Respicius anakubali kwamba alimpokea mwanafunzi kutoka kwa Mwalimu
Harieth na kumpiga fimbo sita

Kumi na moja, Mwalimu Respicius anakubali kwamba, alionwa na PW8, Mkuu wa shule
msaidizi, akimpiga mwanafunzi.

Kumi na mbili, Mwalimu Respicius anakubali kwamba, alionwa na Mwanafunzi na PW2 and
PW3 kando ya njia ambae (Sperius) hao (PW2 na PW3) walimchukua.

Maswali makubwa muhimu ya kutafutia ufumbuzi sasa ni haya,

Nani alisababisha majeraha mbalimbali kwa mwanafunzi (Sperius)?

Na alikuwa na dhamira (nia) gani?


Haya maswali yatajibiwa kwa ushahidi.

Ushahidi wa PW4, PW6 and PW8 unaonesha kuwa mwanafunzi (Sperius) alipigwa fimbo tatu
kutoka kwa Mwalimu Harieth (akitumia fimbo za kawaida za shule) kabla hajakabidhiwa kwa
Mwalimu Respicius ambaye alimpiga mno kuanzia 8:00 AM mpaka 11:00 PM.

Zaidi, Ushahidi unaonyesha kwamba, (Mwalimu Respicius) alitumia Fimbo za kawaida za shule,
lakini baadaye akabadili na kutumia kipande cha ukuni. Na kwamba alimvua kaptura zake na
viatu kabla ya kumpiga.

Inaonekana zaidi kwamba, alimpigia staff room na maeneo mbalimbali nje ya Ofsi.
Alimpiga (Sperius) mikononi, miguuni, mgongoni, shingoni na kichwani.

Pia alitumia Bikari kuchoma kwenye kidole cha Sperius.

Huu ushahidi unaendana na taarifa ya uchunguzi ya Dr. Kahima, PW5 na unaungwa mkono pia
na ushahidi wa Dr. Otieno, DW3. Bado unazidi kuungwa mkono na Ushahidi wa PW2 na PW3
ambao wamlichukua mwanafunzi (Sperius) kando ya njia na kumpeleka hospitali

Kwa upande mwingine, Mwalimu Harieth alikana kumpiga Sperius.

Mwalimu Respecius alikubali kumpiga Sperius ila akasema kwamba, ilikuwa kidogo, viboko
vitatu vya kawaida tu.

Sasa nani mkweli?

Nilichukua muda kupitia ushahidi kwenye kipengele cha kupigwa, na azimio (nia) ya kupiga,
kwa umakini.

Nikiwa nafanya hivyo, Nikarejea kauli ya Kibiblia ya Pontio Pilato, wakati aliposema, Ukweli ni
Kitu gani? (Meaning, what do we mean by the truth?)

Hakuwa anajua maana ya Ukweli na hilo lilikuwa ni tatizo katika kuamua kesi iliyokuwa mbele
yake.

Mimi sina tatizo kama Hilo hapa kwangu.


Tatizo langu ni hili; Ni kwa nini watu hawataki kusema ukweli Mahakamani Hata kwa vitu
vilivyo wazi kabisa?
(My problem is this; why is it that people do not want to say the truth in court
even on obvious things?)

Kila anayekuja Mahakamani anasema, “Sio kweli Mheshimiwa”, (meaning it is not true your
honour). Kwa nini?

Nikavuta pumzi na kuwaza sana kuhusu hilo.

Kisha nikagundua ugumu wa kuwa Jaji na Hakimu. Ni kazi inayotaka akili itulie.
na kujitolea kwa ajili ya haki na msaada kutoka kwa Mungu.

(It is a job which needs peace of mind, commitment towards justice and assistance from God.)

Inawataka (Majaji) kuwa makini sana kwenye kutathmini (kuchambua) ushahidi, vinginevyo
watashindwa na hatari ya kupotezwa (kudanganywa)

Kwa hiyo nitajaribu kuwa makini sana katika kuuchambua ushahidi wa kila Shahidi ambaye
amefika hapa Mahakamani.

Nitaanza kuongelea uaminifu wa mashahidi.

‘Bahati nzuri hiki sio kipengele kisichokuwa na mifano (authorities)’ [mfano ​kesi za nyuma].
Emphasis added.

Tuna mifano mingi. (We have many authorities.) Baadhi imeshanukuliwa kwangu na Mawakili.

Kwenye kesi ya Edson Simon Mwombeki (supra), mahakama ya rufaa ilifuata uamuzi wake wa
awali wa kwenye kesi ya Goodluck Kyando V.R, [2006] TLR 363.

Na ilikuwa na haya ya kusema; Kila Shahidi ana haki ya kukubalika na lazima aaminiwe na
Ushahidi wake ukubaliwe, labda kama kuna mantiki na sababu njema ya kutomwamini Shahidi
(Imetafsiriwa.)

(“​Every witness is entitled to credence and must be believed and his testimony accepted
unless there are good and cogent reasons for not believing a witness​”)

Mahakama (ya rufaa) ikaendelea kusema yafuatayo katika ukurasa wa 16. Ikasema kwamba;-
Sababu nzuri za kutomwamini Shahidi ni pamoja na ukweli kwamba, Shahidi ametoa ushahidi
usio yakinifu (improbable) au usio na mashiko (implausible) au ushahidi umehitilafiana kwenye
sehemu muhimu (materially contradicted) na Shahidi au mashahidi wengine. Soma kesi ya
Mathias Bunda/a V. R, Criminal Appeal No. 62 of 2004).

Kwa maneno mengine, lazima kuwepo na sababu nzuri (njema) kabla ya kuukataa ushahidi wa
Shahidi.

Sababu hizo nzuri zinazoweza kupelekea Mahakama iukatae ushuhuda wa Shahidi ni zifuatazo;

Pale ambapo Shahidi anaongea jambo au kitu ambacho hakina maana (unreasonable), kitu
ambacho hakiwezekani kabisa (not probable) katika mazingira ya kesi husika.

(Anaongea) kitu ambacho kinadhoofisha (defeat) au hakina mantiki (logic). Au kitu ambacho
kinapingana au kuhitilafiana na ushahidi uliotolewa na Mashahidi wengine.

Mwingine anaweza kuuliza swali, vipi kuhusu kuhitilafiana (utata) kwenye ushahidi?

Je! Inawezekana kusema kwamba, pale ambapo kuna utata na/au kuhitilafiana (kutofautiana)
katika ushahidi, ushahidi wa Shahidi lazima utiliwe shaka na kukataliwa?

Ikizungumza kuhusu utata na kuhitilafiana (kwa ushahidi), mahakama ya rufaa ilikuwa na haya
ya kusema kwenye kesi ya Chricant John (supra) ukurasa wa 19-20

Kwamba, ‘Utata (kutofautiana) kwa shahidi mmoja yeyote au miongoni mwa mashahidi
hakuwezi kukwepeka au kuzuilika kwenye kesi yeyote ile. Japo, katika kuzingatia aina, idadi na
madhara ya utata (kutofautiana), lazima kila mara, ikumbukwe kwamba, mashahidi hawawezi
kila muda kukumbuka kwa kina maelezo ya kila kitu kilichotokea.

(It must always be remembered that witnesses do not always make a blow by blow mental
recording of an incidence.)

Kwa hiyo kutofautiana kusichambuliwe bila kuwekwa kwenye muktadha wake sahihi, kama
jitihada za kutafuta uzito wake. Ili kujua, kama (kutofautiana) kunaenda mpaka kwenye mzizi wa
kesi au la, ama badala yake unaharibu uaminifu wa wahusika kwenye kesi.

Mahakama ilifuata maamuzi yake ya awali kwenye kesi ya Elia Nshamba Shapwata and Another
(supra), ambapo ilisema kwamba;
Katika kuchambua utofauti (discrepancies), contradictions (utata) na maneno yaliyoachwa
(omissions), haipendezi kwa Mahakama kuchukua sentensi kadhaa na kuzitumia peke yake huku
wamezitenganisha mbali na maelezo mengine yaliyobaki

Mahakama sharti iamue, Je! huo utofauti na utata ni kidogo sana (minor) au unaingia kabisa
kwenye kiini au mzizi wa kesi?

Mahakama ya rufaa iliweka bayana kwamba kutofautiana (kuhitilafiana) kidogo tu (minor


contradictions) ambako hakufiki kwenye kiini au mzizi wa kesi kunaweza kupuuzwa.

Lakini pale mbapo utata au kutofautiana kunafika mpaka kwenye mzizi au kiini cha kesi,
kutapelekea kukosa imani na Shahidi na ushahidi wake.

Uchunguzi kuhusu kutofautiana (Utata wa ushahidi) lazima viende sanjari (pamoja) na


uchunguzi wa mwenendo wa Shahidi.
Viwili hivyo, vina uhusiano wa karibu.

Mtindo wa kuchunguza mwenendo wa mashahidi unaweza kutofautiana kutoka Jaji au Hakimu


mmoja na mwingine.

Lakini kwa mtazamo wangu (Judge), uchunguzi huu unaweza kufanyika kama ifuatavyo;

Uchunguzi kwa njia ya kupima namna ambavyo Shahidi anaonekana (mwonekano wa Shahidi)
kizimbani.

Namna anavyoongea na kujibu maswali aliyoulizwa na Wakili wake wakati wa examination in


chief na namna anavyojibu maswali wakati wa cross examination.

Kama Shahidi hawezi kuongea sawasawa, anashindwa kusimama imara kwenye sehemu
muhimu (key areas), ana uso wa kutetemeka, anashika kichwa kama vile anataka kukumbuka
hadithi aliyoambiwa na mtu fulani.

Hicho kinaweza kuwa kiashiria kwamba, mwenendo wa Shahidi huyo unajenga maswali.

Lakini kama Shahidi anasimulia maelezo thabiti kabisa na anazidi kutetea msimamo wake kwa
nguvu zote, wakati wa cross
examination, hatetemeki (isipokuwa kwa ile kawaida ya kuogopa Mahakama kwa baadhi ya
watu), pia yuko tayari kuomba radhi pale ambapo hakumbuki vizuri kitu fulani.
Huyo ndiye Shahidi ambaye mwenendo wake hautakiwi kutiliwa mashaka. Katika kesi nyingi,
huyu ndiye Shahidi wa ukweli.

Nilipata muda kuwachambua mashahidi wote kwa makini. Sikuweza kutilia mashaka mwenendo
wa PW2, PW3, PW4, PW5, PW6 and PW8.

Wote walionekana imara na thabiti. Ushahidi wao ulikuwa na mpangilio wa mantiki na


unashabihiana wote katika vipengele vyote muhimu.

Sikuweza kugundua hisia zozote za uongo katika ushuhuda wao kwenye kipengele muhimu cha
kupigwa.

Nawaona kama watu waliokuwa hawasemi kitu, isipokuwa ukweli tu.

Kwa upande mwingine, mwenendo wa DW1 (Mwalimu Respecius) na DW2 (Mwalimu Harieth)
ulionekana kuwa hafifu kilipofika kipengele cha kupigwa kwa mwanafunzi. Walionekana kama
kuna kitu wanaficha.

Hawakuwa wazi. Wote walikuwa wanatetemeka wakati walipokana kumpiga mwanafunzi


(Sperius)

Ushahidi wao haukuwa na mantiki katika hatua fulani.

Haukuwa unaaminika, mathalani, kuamini maneno ya DW1 (Mwalimu Respecius) kwamba,


alimpiga marehemu fimbo ndogo sita tu, wakati Shahidi wake DW3 (Daktari) ambaye aliufanyia
uchunguzi (vipimo) mwili wa marehemu masaa 2.30 baadae, alisema kwamba kulikuwa na
majeraha mbalimbali.

DW1 (Mwalimu Respecius) hakusema nani alieongezea kipigo. Ikiwa mwanafunzi (Sperius)
alipigwa kidogo tu shuleni kama (Mwalimu Respecius) anavyotaka tuamini, nani tena alikuja
hapo katikati na kuongeza majeraha mbalimbali ambayo yalionekana na Shahidi wake Dr.
Otieno?

Je, Inawezekana kusema kwamba, mama yake (Sperius) PW2 na PW3 ndio waliompiga wakiwa
njiani kwenda hospitali?
Na ikiwa Sperius alikabidhiwa kwa mama yake akiwa katika hali nzuri kama DW1 (Mwalimu
Respecius) anavyotaka tuamini, ni kwa nini mama yake alipiga yowe ambalo lilivuta watu
wengi?

Na kama alipigwa kidogo, kwa nini alikufa punde tu baada ya kufika hospitali?

Maswali haya hayana majibu! Yanaenda kuharibu mwenendo wa DW1 (Mwalimu Respecius).
Yameuhafifisha ushahidi wake. Hii pia inamaanisha kwamba, aliongea uongo wakati amekula
kiapo.

Uongo wake unaithibitisha kesi ya Jamhuri. (Tazama kesi ya Felix Lucas Kisinyala v. R CAT
Criminal Appeal No. 129 of 2002 na Salum Yusufu Liundi v. R CAT Criminal Appeal No.26 of
1984).

Kwa hiyo, ni hitimisho langu kuwa, Mwalimu Respicius ndiye aliyempiga mwanafunzi (Sperius)
na kwamba alimpiga kwa namna ilivyoelezewa na PW4, PW6 and PW8.

Ni hitimisho langu pia kwamba, majeraha yaliyoonwa na PW3, PW5 na DW3 yalisababishwa
na DW1 (Mwalimu Respicius).

Mwenendo wa DW2 (Mwalimu Harieth) haukuwa pia mzuri. Naye alisema uongo, usiohitajika
wakati mwingine. (She also spoke lies, sometimes very uncecessary).

Alidanganya Pale aliposema kwamba hakuondoka shuleni siku hiyo asubuhi, na kwamba
alipitiliza kwenda darasa la pili kusimamia Mitihani.”

Uso wake haukuweza kuakisi (kuendana na) maneno yake kizimbani wakati akiwa anayaongea
hayo.

Sauti yake ilipungua (fifia), kumaanisha kwamba, alikuwa anapingana na dhamira yake.

Ukweli ambao uko wazi, ni kwamba aliondoka kwa muda mfupi hiyo asubuhi.

Vilevile alifanya jitihada kadhaa kutafuta pochi na wanafunzi kama ilivyoainishwa na PW4 and
PW6.

Uongo wake kwenye kipengele hiki, unaithibitisha kesi ya upande wa Mashtaka (Jamhuri),
kwamba, alienda na wanafunzi kwa muda fulani kutafuta pochi huku akiwaacha wanafunzi wa
darasa la pili na Mwalimu Alipensia.
Vipi kuhusu upigaji kwa upande wa Mwalimu Harieth?

Nina ushahidi wa PW4 na PW6 ambao walisema kwamba, Mwalimu Harieth alimpiga
mwanafunzi (Sperius) fimbo tatu mikononi, ndani ya ofsi, akitumia fimbo za kawaida

Pia nina ushahidi kutoka kwa PW8 ambaye alisema kwamba, (Mwalimu Harieth) alichapa fimbo
tatu matakoni.

Swali sasa ni Je! Huu mkanganyiko (utofauti) ni mdogo au mkubwa (muhimu)?

Nimeufkria sana kwa makini. Nadhani huu ni utofauti wa msingi (muhimu) kwa sababu unafika
mpaka kwenye kiini/mzizi wa kesi.

Upigaji, sio kama utofauti wa kwenye pochi, huu (utofauti kwenye upigaji) unaenda mpaka
kwenye mzizi wa kesi.

Upo uwezekano mkubwa sana kwamba mashahidi waliokuwepo nje hawakuweza kuona vizuri,
kutokana na umbali (hadi ndani ya ofsi) lakini nadhani huu utofauti (utata) usichukuliwe
kiwepesi.

Inaonekana kwamba, hakuna ushahidi mzuri (wa kutosha) kutoka upande wa Mashtaka
(Jamhuri) kuthibitisha pasipo na shaka kwamba Mwalimu Harieth alimchapa marehemu viboko
vitatu

Nakubaliana na upande wa utetezi na mmoja kati ya wazee wa baraza (assessors) kwamba,


ushahidi kwenye kipengele hiki, hauaminiki

Nitaendelea kuchambua utata/tofauti zingine.

Utata kwenye pochi na kengele haufiki kwenye mzizi wa kesi. Huu nauchukulia kama mdogo
sana hivyo naupuuza.

Utata kuhusu kuondolewa kucha, unagusa kipengele cha kupiga, lakini unaonekana
kusababishwa na umbali na mshtuko.

PW4 alikuwa anamwangalia Mwalimu (Respicius) kutokea nje ya ofsi, na alikuwa katika hali ya
mshtuko baada ya kuona kilichokuwa kinaendelea na baada ya yeye mwenyewe kupigwa ​(wakati
ameambiwa alete ukuni fulani yeye akaleta fimbo nyingine).​ Emphasis added.
Anaweza kuwa aliona damu baadhi zinatoka kidoleni kutokana na kutumika kwa Bikari kisha
akafkri kwamba kucha ilikuwa inatolewa

Hicho ni kitendo cha kawaida ambacho kinaweza kutokea kwa Shahidi yeyote hususani pale
ambapo yuko kwenye mshituko kama ilivyokuwa kwenye hii kesi.

Nauchukulia utofauti huo kama mdogo sana, kwa sababu hiyo naupuuza.

Utata kutokana na maelezo yaliyotolewa kituo cha polisi, nao hauwezi kutiliwa maanani kwa
sababu tatu;

Moja, ulikuwa unahusu pochi na sio kupiga.

Mbili, maelezo hayo hayaoneshi kama yalisomwa kwa mashahidi baada ya kuyachukua. Na

Tatu, kama ilivyowasilishwa kiusahihi kabisa na Wakili mkuu wa Serikali, maelezo


yanayotolewa polisi sio ushahidi.
Hayawezi kuushinda ushahidi uliotolewa kwa kiapo.

Kazi yake ni kuondoa imani na Shahidi, ambapo kwa mtazamo wangu yameshindwa kufanya
hivyo, kutokana na uthabiti na mpangilio wa maelezo uliotolewa na PW4 and PW6.

Hilo limetajwa na limeisha.

Ngoja sasa nielekee kweye kuchambua Kanuni ya adhabu ya viboko (Corporal Punishment
Regulations made under Section 60 (o) of the Education Act, Cap. 353 R.E. 2002.

Nitaziandika kwa kirefu kurahisisha usomaji. (Kanuni hizo) zinasomeka kama ifuatavyo;
(Anaongea Muheshimiwa Jaji)

“THE EDUCATION (CORPORAL PUNISHMENT) REGULATIONS, GN.


294 OF 2002.”

1. Kanuni hizi zitaitwa the Education (Corporal Punishment) Regulations.


(These regulations may be cited as the Education (Corporal Punishment) Regulations.)

2. Katika kanuni hizi, labda kama mazingira yanaruhusu vinginevyo, “Adhabu ya viboko”
inamaanisha adhabu kwa kumchapa mwanafunzi kwenye mikono yake au kwenye matako huku
akiwa amevaa nguo zake za siku zote, kwa kutumia fimbo nyepesi na inayonyumbulika, lakini
(adhabu ya viboko) haijumuishi kumchapa mtoto na kifaa chochote au kuchapa sehemu nyingine
yoyote ya mwili.

“(Corporal punishment” means punishment by striking a pupil on his hand or on his normally
clothed buttocks with a light, flexible stick but excludes striking a child with any other
instrument or on any other part of the body).

“Mkuu wa shule” inamaanisha Mwalimu yeyote aliyeteuliwa na mamlaka husika kuwa


msimamizi wa shule ya msingi au sekondari na inajumuisha mtu yeyote ambaye anamwachia
majukumu yake

“(head of school”* means any teacher appointed by the relevant authority to be in-charge of
primary or secondary schools and includes any person to whom he delegates his duties.)

“Mwanafunzi” inamaanisha mtoto yeyote aliyeandikishwa katika shule yeyote ya msingi au


sekondari lakini haijumuishi mtoto aliyeandikishwa chekechea au chuo cha ualimu

(“Pupil” means any child enrolled in any primary or secondary school but does not include a
child enrolled in a pre-primary school or teachers' college)

“Mamlaka ya shule” inamaanisha waalimu wote ila haijumuishi wahusika (wanachama) wengine
kwenye ofsi.

“(school authority” means all teachers and does not include other members of staff.)”

3-(1). Adhabu ya viboko inaweza kutolewa endapo kutatokea utovu wa nidhamu uliokithiri ama
kwa makosa makubwa yaliyotendeka ndani ama nje ya shule yenye muelekeo wa kuishushia
shule heshima.

(Corporal punishment may be administered for serious breaches of school discipline or for grave
offences committed whether inside or outside the school which are deemed by the
school authority to have brought or are capable of bringing the school into disrepute.)

(2) Adhabu ya viboko iwe na uwiano, sharti izingatie ukubwa wa kosa, umri, jinsia na afya ya
mtoto na isizidi viboko vinne kwa wakati mmoja.
(Corporal punishment shall be reasonable having regard to the gravity of offence, age, sex and
health of the pupils and
shall not exceed four strokes on any occasion.)

4. (1) Mkuu wa shule kwa busara zake, anaweza kutoa adhabu ya viboko au kukasimisha
mamlaka yake katika maandishi kwa Mwalimu yeyote aliyechaguliwa kwa umakini mkubwa
kutoka ofsini kwake. Na huyo Mwalimu aliyechaguliwa atakuwa na mamlaka ya kutoa adhabu
pale tu atakapopata idhini ya mwalimu mkuu katika tukio husika

(The head of the school in his discretion may administer corporal punishment or may delegate
his authority in writing to a carefully selected member of his teaching staff provided that the
authorized member of staff may act only with the approval of the head of the school on each
occasion with corporal punishment is administered.)

(2) Mwanafunzi wa kike anapaswa kupewa adhabu ya viboko na mwalimu wa kike tu isipokuwa
kama shule haina mwalimu wa kike, ambapo ikitokea hivyo, Mkuu wa shule anaweza
mwenyewe kutoa adhabu au kumruhusu kwa njia ya maandishi Mwalimu wa kiume kutoa
adhabu ya viboko.

(A female pupil may only receive corporal punishment from a female teacher except where there
is no female teacher at the school in which case the head of school may himself administer
corporal punishment or authorize in writing a male teacher to administer corporal punishment.)

5. -(1) kila adhabu ya viboko inapotolewa kwa mwanafunzi kumbukumbu ya kutolewa kwa
adhabu hiyo sharti iwekwe katika kitabu kilichotengwa kwa kusudi hili, ikitaja jina la
mwanafunzi, kosa alilolifanya, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu.

(On every occasion when corporal punishment is administered it shall be recorded in writing in a
book kept for this purpose and such record shall state in each instance the name of the pupil, the
offence or breach of discipline, the number of strokes and the name of the teacher who
administered the punishment.)

(2) Na kumbukumbu hizo lazima zisainiwe na mkuu wa shule.

(Every entry in the book shall be made and signed by the head of the school.)

6. Kukataa kukubali adhabu ya viboko kwa Mwanafunzi au mzazi kwa niaba yake,
kunaweza kupelekea kusimamishwa masomo kwa mwanafunzi, kwa mujibu wa kanuni za
kusimamisha na kufukuza wanafunzi shuleni za mwaka, 2002.
(A refusal to accept corporal punishment either by a pupil or by a parent on the pupil's behalf
may lead to the exclusion of the pupil in accordance to the Expulsion and Exclusion of Pupils
from Schools
Regulations, 2002.)

7. Hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kupitia sheria ya Tume ya utumishi wa waalimu ya


mwaka 1989, dhidi ya Mkuu wa shule au mamlaka ya shule, kama utaratibu wa kutoa Adhabu ya
viboko umekiukwa

(A disciplinary action shall be instituted under the Teachers Service Commission Act, 1989 as
against a head of school or school authority if the administration of corporal punishment is
violated)

8. (Revokes the Education (Corporal Punishment Regulations.)

Kanuni zinaonyesha mambo muhimu yafuatayo;

Moja, Adhabu ya viboko inatolewa kutokana na utovu wa nidhamu shuleni uliokithiri ama kwa
makosa makubwa (grave offences)

Pili, Inatolewa na Mkuu wa shule au


Mwalimu yeyote aliyechaguliwa kwa umakini mkubwa kutoka ofsini, ambaye ameruhusiwa na
Mkuu wa shule kwa njia ya maandishi.

Tatu, (Adhabu ya viboko) Inatolewa kwa kumchapa mwanafunzi kwenye mikono yake au
kwenye matako huku akiwa amevaa nguo zake za siku zote, kwa kutumia fimbo nyepesi na
inayonyumbulika, lakini haijumuishi kumchapa mtoto na kifaa chochote au kuchapa sehemu
nyingine yoyote ya mwili.

Nne, lazima iwe na uwiano, sharti izingatie ukubwa wa kosa, umri, jinsia na afya ya wanafunzi
na isizidi viboko vinne kwa wakati mmoja.

Tano, sharti iingizwe kwenye kumbukumbu kwa njia ya maandishi, katika kitabu kilichotengwa
kwa kusudi hili, na kumbukumbu hiyo sharti itaje kwa kila tukio, jina la mwanafunzi, kosa
alilolifanya, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu.

Sita, Mwanafunzi wa kike anapaswa kupewa adhabu ya viboko na mwalimu wa kike tu


isipokuwa kama shule haina mwalimu wa kike, ambapo ikitokea hivyo, Mkuu wa shule anaweza
mwenyewe kutoa adhabu au kumruhusu kwa njia ya maandishi Mwalimu wa kiume kutoa
adhabu ya viboko.

Saba, Mwanafunzi ambaye anagoma kupewa Adhabu ya viboko anaweza kufukuzwa shuleni

Na nane, Mwalimu ambaye atashindwa kuenenda sawasawa na hizi kanuni, anaweza


kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Turudi kwenye kesi yetu sasa, Hakuna shaka kwamba, wizi lilikuwa ni kosa kubwa. Ila ushahidi
unaonyesha kwamba, hapakuwa na uthibitisho kwamba Sperius ndie alihusika kuiba (pochi).

Wanafunzi watatu tu walisema kwamba, Sperius ndiye alikuwa amechukua pochi. Wengi
walisema sio yeye, na wakaongezea kwamba (Sperius) hakuwa na tabia kama hiyo.

PW8 alimtahadharisha Mwalimu


Harieth kuhusu hicho kitu. Hakuamini kwamba Sperius ndiye alikuwa ameichukua.

Pamoja na hayo yote, Sperius alipigwa kama kibaka (street hard core criminal). Alipigwa mno!
Maskini. (He was beaten heavily! Poor boy!)

Mwalimu Respicius hakuwa na ruhusa kutoa Adhabu ya viboko. Hakupata ridhaa ya PW7 au
PW8 (Mkuu wa shule na mkuu msaidizi)

Aliendelea kumpiga mwanafunzi (Sperius) pamoja na kuingilia kati kwa bosi wake, PW8.
Akionesha tabia yake halisi.

Mwalimu Respicius hakutumia fimbo za kawaida za siku zote, kuchapa viboko vinne kwenye
matako kama ilivyoelekezwa na sheria.

Alitumia kipande cha ukuni kumpiga mwanafunzi (Sperius) huku akirudia rudia.

Bado hakukumbuka pia kunakili kumbukumbu ya Adhabu kwenye kitabu maalum.

Hii inaashiria kwamba, kilichofanywa na Mwalimu Respecius sio tu jinai, bali pia ni uvunjifu wa
Kanuni za Elimu (Education Regulations).

Mwisho nitaenda kuchambua nia ovu (Malice) na nia moja ya kutenda kusudio lisilo halali
(common intention).
Nitaanza na nia ovu (malice), Dhamira (nia) ya kuua.

Kesi kuu ya kutuongoza hapa ni maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kwenye kesi ya Enock kipela
v. Republic, (supra).

Mahakama ya rufaa ilisema kwamba;

Mara nyingi mshambuliaji hawezi kutangaza nia yake ya kuua au kusababisha majeraha ya
mwili. Kutambua kama alikuwa amedhamiria au la, lazima uangalie mazingira kadhaa,
yakiwemo yafuatayo;

Usually an attacker will not declare his intention to cause death or grievous bodily harm.
Whether or not he had that intention must be ascertained from various factors, including the
following:

1: Aina na ukubwa wa silaha, kama ipo, iliyotumika katika shambulizi. (The type and size of the
weapon, if any, used in the attack)

(2) Kiwango cha nguvu iliyotumiwa kwenye shambulizi. (The amount of force applied in the
assault;

(3) Sehemu za mwili ambapo pigo au shambulizi lilielekezwa au kupigwa (The part or parts of
the body the blow were directed at or inflicted on)

(4) Idadi ya mapigo (shambulizi), japo pigo au shambulizi moja, itategemea na kilichotokea
kwenye kesi husika, linaweza kutosha kabisa (kuonesha dhamira).

(The number of blows though one blow may, depending on the facts of a particular
case, be sufficient for this purpose)

(5) Aina ya madhara yaliyopelekewa (kusababishwa).


(The kind of injuries inflicted).

(6) Kauli au Maneno ya mshambuliaji, kama yapo, ambayo aliyatoa kabla, wakati na baada ya
mauaji. (The attackers utterances, if any, made before, during or after the killing) na

(7) Mwenendo wa mshambuliaji kabla na baada ya mauaji (The conduct of the attacker before or
after the killing).
Tazama pia kesi ya Saidi Ali Matola @ Chumila v. Republic, CAT Criminal Appeal
No.129 of 2005.

Ushahidi unaonyesha kwamba Mwalimu Respicius alitumia fimbo za kawaida, lakini


akabadilisha baadae na kuanza kutumia kuni

Mazingira hayaoneshi kwamba (Mwalimu Respicius) alitumia nguvu kubwa, ila inaonesha
kwamba alimpiga mwanafunzi (Sperius) mara nyingi (kwa kurudia rudia) huku akitamka
maneno makali.

Alitumia fimbo na kuni (kupiga) mwili mzima - Miguuni, mikononi, mbavuni, mgongoni,
mabegani, usoni, shingoni na kichwani.

Marehemu alipata alama (makovu) mwili mzima pamoja na majeraha makali

Ushahidi unaonyesha kwamba Mwalimu Respicius alitamka maneno yafuatayo wakati wa


shambulizi; “Ngoja niwaonyeshe kazi ya jiwe” (literally meaning let me fix him properly.)

Kisha akaongezea kwamba, “nitakuwekea alama ambayo utamuonyesha hadi mjukuu”

Na wakati mwanafunzi alipoanguka chini, Mwalimu wa nidhamu (Mwalimu Respecius)


alinukuliwa akisema; “Huu ni
usanii, hivi sivyo wanavyozimiaga”

Alisimama kwa muda kisha akaendelea na zoezi.

Tabia au mwenendo wa Mwalimu Respicius was that of a very rough and harsh teacher.
(Mwalimu jeuri na katili sana).

Alitoa Adhabu kwa masaa matatu kwa mwanafunzi ambaye alikuwa nusu uchi na ambaye
alikuwa akirudia rudia kusema kwamba hajachukua pochi.

Aliukataa ushauri wa Mkuu wa shule msaidizi ambaye alisitisha kupigwa.

Alimrudisha Mwalimu Harieth, wakati alipoomba waende wote na akaendelea na zoezi peke
yake

Kisha akarudi shule na kuwaongopea waalimu kwamba amemkabidhi mwanafunzi (Sperius) kwa
wazazi wake, akiwa salama kabisa
Alificha Ukweli kwamba, mwanafunzi (Sperius) alikuwa kwenye hali mbaya.

Na mwisho, wakati askari wamekuja shuleni, alikimbia na kwenda kujificha kwenye kichaka cha
karibu.

Yote haya kwa mtazamo wangu, yanaonesha kwamba Mwalimu Respicius alidhamiria ama
kumjeruhi au kumwondoa kabisa mwanafunzi (Sperius)

Alijua alichokuwa anakifanya na aliamua kukifanya mpaka mwisho.

Alikuwa na nia ovu yote inayohitajika kuwepo kwenye kesi ya mauaji. (He had the necessary
malice needed in a murder case.)

Hoja yake ya kujitetea kwamba, alikuwa tu anamwadhibu mwanafunzi kawaida, Haikubaliki.

Vipi kuhusu Mwalimu Harieth?


Ushahidi unaonyesha kwamba Mwalimu Harieth alipoteza pochi yake.

Kisha akamshuku (kumuhisi) Sperius Eradius kuwa ndiye mwizi, ambaye alimkabidhi kwa
Mwalimu wa nidhamu, kwa hatua zaidi.

Ushahidi unaonyesha pia kwamba, alienda huko na huku kutafuta pochi akisindikizwa na
wanafunzi

Mbali na kwenda na kumkabidhi mwanafunzi (Sperius) kwa Mwalimu wa nidhamu (Mwalimu


Respecius), hakuna ushahidi mwingine unaomuunganisha na upigaji ambao ulifuatia.

Apart from moving around and handling over the boy to the discipline master
there is no other evidence connecting her with the beatings which followed.

Kuna kiashiria cha kujizuia kama ilivyoainishwa na wazee wa baraza (assessors).

Kwamba hakuchukua hatua yotote kuzuia kupigwa (kwa Sperius). Hicho kiashiria kipo.

Lakini, hata hivyo, sidhani kwamba, kinatosha kuwa nia moja ya kutimiza kusudi lisilo halali
(common intention) kama inavyomaanisha kwenye kifungu cha 23 cha Sheria ya Kanuni ya
Adhabu na kwenye mazingira ya hii kesi.
Sioni uhusiano wowote kati yake.

Kwa hiyo ni hitimisho langu kuwa, hapakuwa na ushahidi mzuri kuhusu upigaji kwa upande
wake au nia moja ya kutenda kusudio lisilo halali yenye uzito kumwuunganisha na
kilichofanywa na DW1 (Mwalimu Respecius)

Na kama ilikuwepo nia yoyote, ilikuwa inalenga au inaishia kurudisha pochi yake na si
kumwondoa kabisa mwanafunzi (Sperius)

Baada ya kusema na kumaliza hilo, Nahitimisha na kuamua kwamba, upande wa Mashtaka


(Jamhuri) umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi ya mtuhumiwa namba mbili (Mwalimu Harieth)*
kikamilifu kabisa pasipo na shaka, ambaye namkuta bila hatia na kumwachia huru.

Kesi dhidi ya mtuhumiwa namba moja Respicius Patrick @ Mutazangira ilithibitishwa


kikamilifu pasipo shaka yoyote. Namkuta mtuhumiwa namba moja Respicius Patrick @
Mutazangira, kuwa na hatia ya mauaji kinyume cha kifungu namba 196 cha sheria ya kanuni ya
adhabu sura ya 16 Iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, hivyo namtia hatiani kama ipasavyo.

L. M Mlacha.

Judge

6/3/2019

HUKUMU:

Kuna adhabu moja tu ya kosa la mauaji ambayo ni kunyongwa mpaka kufa.


(There is only one sentence for murder which is death by hanging).

Nakuhukumu wewe mtajwa RESPICUS PATRICK @ MUTAZANGIRA kunyongwa mpaka


kufa.

I sentence you the said RESPICUS PATRICK @ MUTAZANGIRA to death by hanging.

Mahakama (Court):

L.M. Mlacha.

Judge
6/3/2019.

Haki ya kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa imefafanuliwa


(Right of Appeal to the Court of Appeal Explained).

L. M Mlacha
Judge
6/3/2019

MWISHO (WA KUTAFSRI).

Thanks for your time.


Imetafsiriwa na ZECHARIAH LEARNING ADVOCATE (Mwanafunzi wa sheria)
FROM: UDOM, CBSL.
zachariamaseke@gmail.com
Saidia kushare, Iwafikie walengwa (Waalimu wote na wazazi).

You might also like