You are on page 1of 3

TOFAUTI KATI YA MKABALA SARUFI MAPOKEO NA SARUFI MIUNDO

Imeandaliwa na mwalimu AFRA PAUL MPABANYANKA

TAREHE4/4/2019

Sarufi ni taaluma ya lugha inayochunguza na kuchanganua vipashio na kanuni mbalimbali


zinazotawala muundo wa lugha, (Matinde, 2012. Sarufi ni utaratibu wa kanuni ambazo
humwezesha mtumiaji wa lugha kutunga tungo sahihi zinazoeleweka mara zinapotamkwa
(Kapinga, 1983). Hivyo basi, dhana ya sarufi inatafsiriwa katika mitazamo tofauti lakini yenye
kuhusiana. Mtazamo wa kwanza tunaweza kusema Sarufi ni taaluma ya uchambuzi wa lugha
inayojumuisha viwango vyote vya uchambnuzi yaani kiwango cha umbo sauti (fonolojia),
kiwango cha umbo neno (fonolojia), kiwango cha miundo maneno (sintaksia) na kiwango cha
umbo

Kwa mujibu wa Massamba (2004) Saruf mapokeo ni Jumla ya mikabala mbalimbali iliyokuwa
ikitumiwa zamani kuelezea miundo na mifumo ya lugha min!i ilikuwa imekitwa katika kiunzi
cha sarufza Kilatin na Kigiriki na Sarufi Mapokeo inanasibishwa na kipindi kabla ya karne ya
kumi na nane.

Sarufi muundo ni mkabala wa kimapokeo ambao haujihusishi na sarufi miundo katika marefu
na mapana yake, ambapo zilijihusisha sana na sentensi sahili, (Massamba 1999). Sarufi muundo
ni kitengo cha sarufi geuza maumbo zalishi, ambacho hujikita katika matumizi ya sheria chache
kuzalisha sentensi nyingi zisizo na kikomo, ambazo zina usarufi na hata zile ambazo hazijawahi
kutungwa, (Matinde, 2012). Sarufi muundo virai ni mpangilio wa vitu vidogo vilivyowekwa
pamoja na kujenga kitu kikubwa zaidi. Sarufi miundo virai ni mkabala wa kuchambua lugha kwa
kuigawa sentensi katika virai vinayoiunda na kisha kuvichanganua zaidi hadi kufikia neno
mojamoja lililokiunda kirai, (Massamba, 2001).

Zifuatazo ni tofauti kati ya sarufi miundo na sarufi mapokeo

Hutofautiana katika lengo. Lengo lao halifahamiki zaidi ya kutumia taratibu za kijarabati
zinazohusu ukusanyaji wa data na kuzichambua pamoja na kuunda kanuni kwa kutumia data
hizo. Lakini, Lengo la sarufi mapokeo
liko bayana, hujitokeza dhahiri. Lengo la sarufi hii ni kufafanua umilisi wa ujuzi lugha ambao
huwa mwanalugha anao. Umilisi huo humfanya mwanalugha kutambua viambajengo katika
tungo, katika mtazamo wa ndani yaani muundo wa ndani.

Hutofautiana katika miundo. Sarufi miundo hii huwa inajikita katika miundo ya nje, ambayo
huchunguza na kuchambua sentensi katika umbo la nje. Mfano; Mama anakula ugali

Hivyo huonyesha tu aina ya maneno husika katika sentensi au tungo kama vile: Mama- Nomino,
Anakula- Kitenzi, na Ugali- Nomino. Ilihali, Sarufi mapokeo hii huwa imejikita katika
kuchungaza sentensi kama umbo la ndani na umbo la nje. Muundo wa ndani ni uchopekwaji
katika miundo hiyo ambapo muundo wan nje lazima upitie katika muundo wa mofofonemiki na
kuweka katika kitengo cha fonolojia. Hutofautiana katika vitengo. Sarufi mapokeo ni sarufi
ambayo inafumbata vitengo vyote vya lugha ambavyo ni fonolojia, sintaksia, semantiki, na
mofofonemiki ambapo kitengo cha fonolojia hushughulikia sauti za lugha, kitengo cha
kisintaksia hushughulika na uundaji wa sentensi, kitengo cha semantiki hushughulika na ufasili
wa maana, na kitengo cha mofofonemiki huwa na kazi ya kuibadili njeo za wakati.

Ilihali Sarufi miundo hufumbata kitengo cha mofolojia ambapo sentensi iligawanywa katika
kiunzi cha aina za maneno kama Nomino, Kitenzi, Kivumishi, Kielezi na kihunzi hicho
kilijulikana kama utaratibu wa uchanganuzi wa viambajengo.

Hutofautiana katika uhusiano wa sentensi. Sarufi mapokeo ilipiga hatua kubwa, kwanza
huonyesha uhusiano uliopo kati ya maumbo mbalimbli ya sentensi au tungo. Na pia kuonyesha
uhusiano unaoweza kuwepo baina ya sentensi moja na sentensi nyingine.

Mfano: (1) Mtoto mrefu anacheza, na si kusema kuwa Mtoto anacheza mrefu Huu ni uhusianao
kati ya maumbo.

Mfano: (2) Juma alipiga mpira Mpira ulipigwa na Juma Huu ni uhusiano wa sentensi moja na
sentensi nyingine. Ilihali Sarufi miundo haionyeshi uhusiano kati ya sentensi moja na sentensi
nyingine. Hutofautiana katika uwazi. Sarufi mapokeo huonesha sentensi sahihi na ambazo sio
sahihi pia huonesha sentensi ambazo zinakubalika na sentensi zisizokubalika kwa msemaji
mzawa. Ilihali Sarufi miundo virai yenyewe haina uwazi huo.
Hitimisho ni kwamba, Sarufi mapokeo ilianzishwa kutokana na mapungufu katika sarufi
muundo virai. Sarufi iliyokuwepo, sarufi miundo virai, ilishindwa kuonyesha mahusiano
yaliyokuwepo baina ya sentinsi zinazo husiana kimaana. Hivyo kutokana na upungufu huo
kulikuwa na haja ya kuonyesha uhusiano huo

REJEA

Kapinga,M.C.(1983). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA). Dar-es-Salaam:


TUKI.

Massamba, D.T., Kihore,M.Y. & Hokororo.(1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu


(SAMIKISA). Dar-es-Salaam: TUKI.

Matinde,S.R.(2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia. Mwanza: Serengeti Educational


Publishers (T) LTD.

You might also like