You are on page 1of 2

EWE KIJANA! SHIRIKI KATIKA UJASIRIAMALI!

UNALIPA

KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI


• Katika Maendeleo yoyote Uchumi ni sehemu kubwa ya maisha
• Kujikwamua kiuchumi ni kufanya jitihada na michakato mbali mbali ya kuboresha kipato na kuinua
ufanisi wa matokeo yanayotazamiwa kutokana na uchumi
• Sehemu kubwa ya ufanisi katika mchakato wa kujikwamua kiuchumi unapatikana katika ujasiriamali
• Ujasiriamali husaidia kuinua kipato cha vijana na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo yao

UJASIRIAMALI NI NINI?
• Utekelezaji au utendaji ambao mtu anapanga ana simamia, kuendesha na kukisia mashaka au hatari
kwa kuthubutu kufanya jambo la kiuchumi au kijamii au biashara
• Ujasiri au mushawasha wa kupata mali
• Uwezo wa kuzitambua fursa za haraka na uthubutu za kuzitekeleza fursa pindi zinapojitokeza
• Uwezo wa kuthubutu kushinda vikwazo zinazoweza kuzuia utekelezaji wa fursa hizo
NINI SIFA ZA MJASIRIAMALI?
• Anatafuta fursa
• Ni mbunifu
• Anadiriki kutenda
• Anatafuta habari
• Anatimiza makubaliano katika kazi
• Hayumbi
• Ana utashi wa ubora na ufanisi
• Anaweka malengo
• Anapanga na kusimamia
• Anajali muda
• Anayajali matatizo ya wateja wake kama yake
• Anauamini uwezo wake

UJASIRIAMALI NA MITAJI
• Ujasiriamali huanzishwa kutokana na vyanzo mbali mbali
• Vijana wengi hutaka kuanzisha biashara kwa kutegemea mikopo au ruzuku kutoka kwa wafadhili
• Mikopo na ruzuku zinasaidia lakini mjasiriamali mzuri ni Yule anaetegemea alichonacho kuanzishia
biashara
• Mikopo hutumika kutanulia biashara lakini sio chanzo cha kuanzisha biashara

Ujasiriamali Huinua Kipato cha Vijana

‘Chakarika’
Ujumbe huu Umeletwa kwenu na

ZAIADA

kwa kushirikiana na

Foundation for Civil Society

Mawasiliano: zaiada@hotmail.com

You might also like