You are on page 1of 16

MAANA NA CHANZO

CHA USHIA

Kimeandikwa na:
Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

Kimetafsiriwa na:
Dr. Muhammad S. Kanju

Kimetolewa na Kuchapiswa na:


Bilal Muslim Mission of Tanzania
S.L.P. 20033
Dar es Salaam
Tanzania
Haki za kunakili imehifadhiwa na:
Bilal Muslim Mission of Tanzania

ISBN 9987 620 25 6

Toleo la Kwanza: 1998 Nakala 1000


Toleo la Pili: 1998 Nakala 1000
Toleo la Tatu: 1999 Nakala 2000
Toleo la Nne: 2000 Nakala 2000
Toleo la Tano: 2001 Nakala 2000
Toleo la Sita: 2002 Nakala 2000
Toleo la saba: 2003 Nakala 2000
Toleo la Nane: 2004 Nakala 2000

Kimetolewa na Kuchapishwa na:


BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
S.L.P 20033
DAR ES SALAAM - TANZANIA
4
Kwa Jina la Allah Mwenye Rehema
Mwenye kurehemu

MAANA YA SHIA

Neno Shia )‫ (شيعة‬limetokana na neno la Kiarabu


at-tashayyu )‫ (التشیع‬lenye maana ya kufuata. Kulingana
na al-Qamus na Lisanu ’l-‘Arab, marafiki na wafuasi wa
mtu wanaitwa Shia wake. Kulingana na Taju ’l-‘urus,
kikundi cha watu wanoafikiana juu ya jambo (lolote)
wanaweza kuitwa Shia. Neno hili hutumika sawa sawa
kwa umoja na wingi, vile vile hutumika sawa sawa kwa
wanaume na wanawake.

Katika Qur’ani imetumiwa kwa wafuasi wa Mitume wa


Allah (s.w.t.)

(a) Katika kisa cha Musa (a.s.) inasema hivi:-


َّ‫َ لَىَ ذ‬ َّ‫َ َ ْ َ ُ َ ْ َ َ َ ُ ذ‬ َ َ
‫الي ِم ْن َع ُد ِّو ِه‬ َ
ِ ‫ه ٰـذا ِمن ِشيع ِت ِه َوه ٰـذا ِمن عد ِّوهِ ۖ فاستغاثه‬
ِ ‫الي ِمن ِشيع ِت ِه ع‬

1
Huyu ni katika Shia wake na yule ni katika adui zake,
yule ambae alikuwa Shia wake alimuomba msaada juu
ya yule adui yake.1

(b) Katika kisa cha Nuh (a.s.) inasema hivi:-


َ ‫يعت ِه إَلب ْ َرا ِه‬
َ َّ َ
‫يم‬ ِ ِ ‫وإِن ِمن ِش‬
Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi (Shia) lake.2

Kamusi za Kiarabu baada ya kutoa maana ya kawaida


ya neno Shia, kwa kawaida huongeza: “Jina hili
kijumla hutumika kwa wale wenye mapenzi na
kumfuata Ali (a.s.) na watu wa nyumbani kwake, na
imekuwa ndio jina lao makhsusi”.3

Shaykh al-Mufid (aliyekufa 413 A.H. / 1022 M.)


ameeleza kwamba wakati neno Shia linapotumika na
Sarufi yenye kuainisha ‘al’ (al-Shia) basi ina maana
ya “kundi pekee lenye kumfuata Imam Ali (a.s.) kwa
mapenzi na imani (itikadi) na kwamba alikuwa ni Imamu
baada ya Mtume (s.a.w.w.) bila mwonya wowote.”4

Kwa ufupi, Shia wamepata jina hili kwa sababu


1 Qur’ani 28:15
2 Qur’ani 37:83
3 Al-Qamus, Juzuu ya 2; at-Turayhi, Majma‘ul ’l-Bahrayn, Juzuu
ya 2 uk. 539; Ibn al-Athir al-Jazari, an-Nihayah, toleo la Misri,
[1383/1963], Juzuu ya 2 uk. 519-520.
4 al-Mufid, Shaykh, Awa’ilu ’l-Maqalat (Qum: Toleo la 2, 1370
A.H.) uk. 2-3.

2
wanamfuata Imam Ali (a.s.) na kizazi chake Maasumin,
na kupuuza madai ya watu wengine ya Uimamu. Kama
itakavyoelezwa baadae, ni Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe
aliyewapa jina hili wafuasi wa Ali (a.s.).

CHANZO CHA USHIA

Asili ya Ushia ni sawa sawa na ile ya Uislamu. (Kwa


maana Ushia ndio Uislamu na Uislamu ndio Ushia).

Tofauti kubwa iliyo baina ya Masunni na Mashia ni kuhusu


mshika makamu baada ya Mtume wa Uislamu. Masunni
huwamini kwamba Abu Bakar ndiye aliyekuwa mshika
makamu wa kwanza; Mashia huwamini kwamba Ali
ndiye mshika makamu wa haki wa kwanza. Kama
msomi asiye na chuki akichunguza matangazo ya
Mtume (s.a.w.w.) kama yalivyoandikwa na Wanachuoni
wa Kisunni katika tafsir zao za Qur’ani, hadithi za
Mtume (s.a.w.w.), wasifu na tarekh (historia), hana budi
kukubali kwamba alikuwa ni Mtume mwenyewe ndiye
muanzilishi wa Ushia.

Tangazo la kwanza la kubaathiwa (Utume wa


Muhammad (s.a.w.w.)) limeandamana wakati mmoja na
tangazo la ukhalifa la kwanza kutolewa kwa Ali (a.s.).
Tukio hilo linajulikana kama “karamu ya ndugu wa
karibu.” Vifungu vinavyohusu habari hii vimenukuliwa
hapa kutoka kitabu cha Tarikh cha at-Tabari:

3
Ali (a.s.) alisema “wakati Aya ‘na uwaonye jamaa zako
wa karibu’5 iliposhushwa kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w.)
aliniita mimi na akaniamrisha kutayarisha sa‘ moja (kiasi
cha kilo 3) cha chakula na niwakaribishe ukoo wa Abdu’l
Muttalib ili apate kuzungumza nao. Walikuwa karibu
watu arubaini, miongoni mwao walikuwepo ami zake
Abu Talib, Hamza, Abbas na Abu Lahab. Kisha Mtume
wa Allah (s.a.w.w.) akatoa khutba isemayo:-
‘Enyi watoto wa Abdu’l Muttalib! Simjui mtu yeyote
katika bara-Arabu yote ambaye amewaletea watu wake
kitu kilicho bora zaidi kuliko kile nilichokuleteeni mimi.
Nimekuleteeni mema ya hii Dunia na Akhera. Na Allah
(s.w.t.) ameniamrisha nikuiteni ninyi kwayo. Ni nani basi
miongoni mwenu atakayenisaidia katika jambo hili, kwa
masharti kwamba atakuwa ndugu yangu, wasii wangu na
Khalifa wangu miongoni mwenu?’”

Ali aliendelea kusema: “Hakuna hata mmoja aliyejibu;


hivyo nilisema (ingawa nilikuwa mdogo kuliko wote
katika umri):
‘Mimi, ewe Mtume wa Allah! nitakuwa msaidizi
wako katika kazi hii.’ Basi Mtume (s.a.w.w.) akaweka
mkono wake kwenye shingo yangu na kusema: ‘Hakika
huyu ni ndugu yangu, wasii wangu na Khalifa wangu
miongoni mwenu. Msikilizeni na mumtii.’ Waliokuwa
kwenye mkutano wote wakaamka, huku wakicheka
na kumuambia Abu Talib kwamba Muhammad

5 Qur’ani 26:214

4
ameamrisha yeye kumsikiliza mtoto wake na kumtii.”6
6 At-Tabari, Muhammad bin Jarir, Tarikh, Juzuu 3 (Laden: E.J.Brill,
1882-1885) uk.1171-1173. Ni kitu cha kushangaza kwamba katika
Tarikh ya at-Tabari toleo la Misri (Kairo) 1939 (ambao inadaiwa kuwa
imechekiwa na kile cha toleo la Laden) yale maneno muhimu “wasiyyi
wa Khalifati” (Wasii na Khalifa wangu) yamebadilishwa kuwa “kadha
wa kadha.” Masikitiko yalioje kuona ulimwengu wa usomi kutoa
mhanga uaminifu wake kwa ajili ya siasa. Ni lazima itajwe hapa kwamba
hadithi hii pamoja na maneno yale imesimuliwa na wanachuoni wa
Kisunni thelathini, au zaidi, Wanahistoria, Muhaddithina na Mufassirina
wa Qur’ani. Imam Ahmad bin Hanbal ameisimulia hadithi hii
katika Musnad yake (Juzuu ya 1. uk.111) pamoja na sanad hii ifuatayo
(1) Aswad bin Amir kutoka kwa (2) Sharik, kutoka kwa (3) al-A‘mash
kutoka kwa (4) al-Minhal, kutoka kwa (5) Ibad bin Abdullah al-Asadi,
kutoka kwa (6) Ali. Sasa (1), (3) na (5) ni miongoni mwa wasimuliaji
wa hadithi wa al-Bukhari na Muslim, ambapo (2) ni miongoni mwa
wasimuliaji wa hadithi wa Muslim na (4) ni miongoni mwa wale wa
al-Bukhari.

Vile vile Ahmad bin Shu’ayb an-Nasa’i ambaye kitabu chake cha
Sunan ni kimoja miongoni mwa vitabu sita sahihi vya rejea vya hadithi
za Masunni, amesimulia hadithi hii kutoka kwa Ibn Abbas katika kitabu
chake al-Khasa’is uk. 6.

Kwa rejea zingine za hadithi hii, tazama al-Muraja’at cha Abdul


Husayn Sharafu d-‘Din (Barua ya 20-23). Hii ni kitabu muhimu sana
cha Ki-Shia cha wakati huu; kimechapishwa mara nyingi huko Iraq,
Iran, Lebanon na Kuwait. Tarjuma yake ya Kiurdu ‘Din-e-Haqq’
ilichapishwa Kujhwa (Saran) India; ambapo baadae ilitafsiriwa kwa
Kiingereza kwa jina la ‘The Right Path’ na Mohammad Amir Haider
Khan na hivi karibuni kimechapishwa na Peermohamed Ibrahim Trust,
Karachi. (Tafsiri ya Kiingereza tangu wakati huo kimechapishwa mara
nyingi huko Iran, Uingereza na Marekani)

5
Hii ilikuwa ni wakati wa mwanzo kabisa.

Katika siku za mwisho za uhai wake, Mtume (s.a.w.w.)


alitangaza katika sehemu inayoitwa Ghadir Khum, kati
ya Makka na Madina, kwamba Ali alikuwa ndiye Khalifa
wake na Kiongozi wa Waislamu. Tukio hili limeandikwa
na wanachuoni wengi wa Kisunni. Imam Ahmad bin
Shu‘ayb an-Nasai (amekufa 303 A.H./915-16 M)
amesimulia tukio hili kupitia Sanad (nyororo) mbali
mbali za wasimuliaji wa hadithi katika kitabu chake
al-Khasa’is, mojawapo ikiwa kama ifuatavyo:-

Abu ’t-Tufayl alisema kwamba Zayd bin Arkam alisema,


“wakati Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anarudi toka Hijja
yake ya mwisho na akapumzika penye bwawa (Ghadir)
la Khum akasema: ‘Inaelekea kama vile nimeitwa
(kurejea kwa Mola) nami nimekubali wito huo. Na
nakuachieni miongoni mwenu vitu vizito viwili
vyenye thamani, kimoja ya hivyo ni kikubwa
kuliko kingine: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul
Bayt wangu (Kizazi changu). Hivyo angalieni jinsi
mtakavyojikhusisha navyo baada yangu kwa sababu
vitu hivyo havitatengana mpaka vitakapokuja kwangu
kwenye chemchem (ya ‘Kauthar’ siku ya hukumu).
Mimi ni mwenye kutawalia (walii) mambo ya kila
muumini.’ Wakati anasema hivyo aliunyoosha mkono
wa Ali (a.s.) na akasema, ‘Yeyote yule ambaye mimi
ni mwenye kumtawalia mambo yake, huyu (Ali) ni
mwenye kumtawalia mambo yake. Ee! Allah! Mpende
mwenye kumpenda Ali, na uwe adui kwa kila mwenye
6
kumfanyia uadui yeye.”

Abu ’t-Tufayl anasema: “Nilimuuliza Zayd, ‘maneno


haya uliyasikia kutoka kwa Mtume wa Allah (s.w.t.)?’
akasema: ‘Hakuna mtu aliyekuwa mahala pale ila
alimuona kwa macho yake na kumsikia kwa masikio
yake.’”7 Hadithi hii inajulikana kama hadithi ya vizito
viwili vyenye thamani.

Katika kitabu hicho hicho, Imam an-Nasa’i ananukuu


hadithi kutoka kwa Zayd bin Arkam ambayo ina maneno
haya ya Mtume (s.a.w.w): “Je! Mimi sina mamlaka
kwa Muumini kuliko alivyo kwa nafsi yake?” Wote
wakajibu: “Kwa hakika! Ewe Mtume wa Allah,
Tunashuhudia kwamba wewe unayo mamlaka juu ya kila
Muumin kuliko nafsi yake.” Mtume (s.a.w.w.) akasema:
“Basi hakika ambaye yeye namtawalia mambo yake
(Mawla), huyu vilevile ni mwenye kumtawalia mambo
yake.” Wakati anasema hivyo aliunyoosha mkono wa
Ali.8 Hadithi hii inajulikana kama, “Hadithi ya Wilayya.”
Hadithi za “Vizito Viwili vyenye thamani” na “Mawla”
ziko pamoja na zimesimuliwa mara nyingi sehemu
mbali mbali na mamia ya wahadithiaji (muhadithina).
Mwanachuoni mashuhuri wa Kiwahhabi, Nawwab
Siddik Hassan Khana wa Bhopal (India) anasema:
“Hakim Abu Sa‘id anasema kwamba hadithi za ‘Vizito

7 An-Nasa’i, al-Khasa’is uk. 15.


8 An-Nasa’i, al-Khasa’is uk. 16.

7
Viwili vyenye thamani’ na ‘Mawla’ ni hadithi mutawatir,9
kwa sababu idadi kubwa ya masahaba wa Mtume wamez-
isimulia kiasi kwamba Muhammad bin Jarir ameziandika
hadithi hizi mbili kwa nyororo (asnad) tofauti sabini na
tano za Wasimuliaji.”10

Abdu’l-Husayn Ahmad al-Amini ameainisha wapokezi


wa hadithi hii, na akakuta miongoni mwao wako sahaba
wa Mtume (s.a.w.w.) mia moja na ishirini, na themanini
na nne ni tabi‘in (wafuasi wa masahaba). Idadi ya
muhaddithiin wa Kisunni ambao wameisimulia inafikia
mia tatu na sitini. Vitabu maalumu mia mbili na sitini
(vingi vikiwa katika juzuu nyingi) vimeandikwa na
wanazuoni wa Kishia na Kisunni kwa ajili ya hadithi hii
tu.11

9 Mutawatir ni Hadithi iliyosimuliwa na watu wengi katika kila


ngazi, kiasi ambacho mtu hawezi kuitilia shaka kuhusu usahihi
wake.
10 Siddik Hassan Khan Minhajul-Wusul uk. 13.
11 Tazama al-Amini, al-Ghadir J.1, ambacho kimeshughulikia suala
hili pekee. Hii ni ni kitabu kingine muhimu cha Ki-Shia cha
wakati huu. Juzuu kumi na moja zilichapishwa kabla ya al-Amini
kufariki mwaka 1969. Kimechapishwa mara nyingi huko Iraq,
Iran na Lebanon. Nimeona tafsiri yake ya Kiajemi. Marehemu
Sheikh Muhammad Mustafa Jawhar, wa Karachi, alitafsiri juzuu
ya kwanza katika Kiurdu lakini ikapotea wakati ikwa kwenye
mashine ya uchapishaji. Sasa tafsiri nyingine ya Kiurdu ya juzuu
ya kwanza imechapishwa huko India.

8
ASILI YA JINA

Tunapoona kwamba baina ya matukio haya mawili,


Mtume (s.a.w.w.) mara kwa mara alikuwa akiwaashiria
wafuasi wa Ali kama Mashia, tunalazimika kukubali
kwamba sio imani ya Kishia tu, bali hata jina (hilo)
limeanzishwa na Mtume mwenyewe. Hadithi zifuatazo
zinanukuliwa kutoka rejea za Kisunni:-

Ibn ‘Asakir anasimulia kutoka kwa Jabir bin Abdullah


kwamba alisema: “Tulikuwa pamoja na Mtume
(s.a.w.w.) wakati Ali alipokuja (hapo tulipokuwa).
Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Naapa kwa yule ambaye
nafsi yangu ipo mikononi mwake, hakika huyu (Ali) na
Shia wake ndio wenye kufuzu siku ya ufufuo.’ Kisha
Aya ifuatayo ikashushwa. “Hakika wale walioamini na
kutenda mema, basi hao ndio wema wa viumbe. (Qur’ani
98:7)”12

12 As-Suyuti, Jalalu’d-Din (amekufa 910/1504 – 05) katika Tafsiri


yake ad-Durrul-Manthur, J. 6 uk. 379. Anasimulia hadithi kama
hii kutoka kwa Ibn Abbas na Ali kadhalika katika sehemu hiyo
hiyo; Al-Khuwarizmi (amekufa 569/1173-4) katika al-Manakib.

Hadithi nyingine za Mtume (s.a.w.w.) zitamkazo kwamba Shia


wa Ali watafuzu siku ya kiyama zinasimuliwa na Wanachuoni
wa Kisunni kutoka kwa Abdullah, Abu Rafi, Jabir bin Abdullah,
Ibn Abbas na Ali; Mingoni mwa wanachuoni hawa ni at-Tabarani
katika kitabu chake al-Mu‘jam al-Kabir, Ahmad bin Hanbal katika
al-Manaqib yake, Ibn Mardawayh al-Kanji ash-Shafi’i katika kitabu
chake Kifayatu ’t-Talib na wengine wengi.

9
At-Tabarani anasema kwamba, Mtume (s.a.w.w.)
alimuambia Ali: “Ewe Ali! Hakika utakuja mbele ya
Allah, wewe na Shia wako hali ya kuwa mmeridhika
(na Allah) na hali ya kuwa mnaridhia kwa Allah.”13

Kuna hadithi nyingi kutoka kwa wasimuliaji wengi


ambazo wanachuoni wa Kisunni wasingeweza kuzipuuza.
Hivyo walijaribu kuzifanya hadithi hizi zioane na upande
wao. Kwa mfano baada ya kunukuu hadithi hizi, Ibn
Hajar al-Makki anaandika hivi: “Na Shia wa Ahlul Bayt
ni Ahlu’s-Sunnah wa’l-Jamaa (yaani Sunni) kwa sababu
ni wao waliowapenda Ahlul Baty kama ilivyoamrishwa
na Allah na Mtume wake. Ama wengine basi wao ni
maadui (wa Ahlul bayt).”14

Dai hili lilirudiwa tena na Shah Abdu ’l Aziz Dehlawi


ambaye anasema: “Ni lazima ieleweke kwamba Shia wa
kwanza (ambao ni Sunni na Tafadhiliyya) katika siku
za zamani walijulikana kama Mashia.Wakati Ghulat na
Rawafidh, Zaydiyyah na Ismailiyyah walipochukuwa jina
hili kuwa lao...... Sunni na Tafadhiliyyah hawa kulitaka
jina hili kwa upande wao, na kwa hivyo wakajichukulia
jina la Ahlu ’s-Sunnah wa’l-Jamaa.”15

13 Ibn Athir katika an-Nihayah; Ibn Hajar al-Makki katika as-


Sawa‘iqu ’l-Muhriqah (Misri, Hakuna tarehe) uk. 92. Anasimulia
hadithi nyingi kuhusu suala hili.
14 as-Sawa‘iqu ’l-Muhriqah.
15 Shah ‘Abdu ’l-Aziz Dehlawi, Tuhfah-e-Ithnâ-‘ashariyyah,
Nawalkishor Press, Lucknow, hakuna tarehe; uk. 4, 11, 59

10
Madai kama haya hayastahili kujibiwa. Lakini baada
ya kuona mukhtasari wa tafsiri ya Kiarabu ya Tuhfah
umechapishwa hivi karibuni huko Misri, na nukuu
hapa maoni ya mwanachuoni mwingine wa Kisunni,
Ubaydullah Amritsari, ambaye baada ya kunukuu madai
hayo hapo juu katika kitabu chake Arjahu’l-matalib,
Amristsari anasema: “Kusema kwamba hapo mwanzo
Sunni walikuwa wakijulikana kama Shia ni madai
yaliyotupu, kwa sababu hakuna uthibitisho unaoweza
kupatikana. Ingelikuwa masunni walikuwa wakiitwa
Shia, basi angalau baadhi ya viongozi wa Kisunni
wangelijulikana kwa jina hili kabla ya kuja
kwa Zaydiyyah (120 A.H.). Aidha, kama Sunni
wangelijulikana kwa jina hili, Zaidiyyah na Ismailiyyah,
wasingeweza kulivumilia jina hili kuwa lao (kwa sababu
ya uadui uliokuwepo) na wangejichagulia jina lingine.”16

MASHIA WA KWANZA

Wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.) neno Shia lilikuwa


linatumika kabla ya yote kwa Masahaba wanne
wakubwa walioheshimiwa: Salman al-Farsi, Abu Dharr
Jundab bin Junadah Al-Ghifari, Miqdad bin Aswad al-
Kindi na Ammar bin Yasir.

Kashfu ’z-Zunun (J.3), ananukuu kutoka Kitabu ’z-Zinah


cha Abu Hatim Sahal (kadhaa) bin Muhammad Sajastani

16 ‘Ubaydullah Amritsari, Arjahu ’l-Matalib, (Lahore: Toleo la 2)


uk. 608 (ambayo imechapishwa kimakosa kama 164).

11
(alikufa 205 A.H.): “Katika siku za uhai wa Mtume
(s.a.w.w.) neno Shia lilikuwa linatajwa kwa kuwaashiria
watu wanne: Salman al-Farsi, Abu Dharr Ghaffar
(Kadhaa), Miqdad bin Aswad al-Kindi, na Ammar bin
Yasir.”17

Hawa ndio waliokuwa Shia wa kwanza, na huo ndio


uliokuwa mwanzo wa Imani ya Shia chini ya uongozi
mpole na usimamizi wa Mtume wa Uislamu mwenyewe.

17 Kama ilivyonukuliwa na Hasan al-Amin katika Islamic Shi’ite


Encyclopaedia J.1 (Beirut 1968) uk. 12-13.

12
ISBN: 9987 620 25 6

Kimetolewa Kuchapishwa na:


Bilal Muslim Mission of Tanzania
S.L.P 20033
Dar es Salaam

You might also like