You are on page 1of 66

MAOMBOLEZO YA

ASHURA
Toleo la Kwanza

Kimekusanywa na:
Musabah Shaban Mapinda

Kimetolewa na Kimechapishwa na
Bilal Muslim Mission of Tanzania
S.L.P. 20033
Dar es Salaam - Tanzania
Haki za kunakili imehifadhiwa na:
Bilal Muslim Mission of Tanzania

ISBN 9987 620 55 8

Toleo la kwanza 2008, Nakala 200


Toleo la Pili 2009, Nakala 500

Kimetolewa na Kuchapishwa na:


BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
S.L.P 20033
DAR ES SALAAM - TANZANIA
YALIYOMO

Majlis ya Kwanza
Hali ya Bara Arabu kabla ya Uislamu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 1

Majlis ya Pili
Makundi matatu: Muumini, Mwislamu na Mnafiki . . . . . . . . . . . . . 7

Majlis ya Tatu
Kosa kubwa limetendeka . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .13

Majlis ya Nne
Kizazi cha Hashim na Kizazi cha Umayyah . . . . . . . . . . . . . . . . . . .18

Majlis ya Tano
Kizazi cha Hashim na Kizazi cha Umayyah . . . . . . . . . . . . . . . . . . .23

Majlis ya Sita
Kizazi cha Hashim na Kizazi cha Umayyah:
Mtume Kuhamia Madina . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 29

Majlis ya Saba
Kisasi cha Banu Umayyah dhidi ya Mtume (s.a.w.w.) . . . . . . . . . . 34

Majlis ya Nane
Fathu Makka . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .38

Majlis ya Tisa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 44

Majlis ya Kumi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 48

Majlis ya Kumi na Moja . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 52

Majlis ya Kumi na Mbili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 57


Majlis ya Kwanza :
Hali ya Bara Arabu Kabla ya Uislamu

Ili tupate kufahamu ni zipi sababu zilizomfanya Sayyidina


Husein (a.s.) asimame kupinga utawala wa Yazid bin Muawiyah, ni
wajibu wetu kurejea nyuma hadi mwanzoni mwa kuja kwa dini ya
ki-Islamu.

Kukirejea kipindi hicho ni jambo litakalo saidia kuyabaini matukio


kadhaa yanayoonesha kuwepo kwa mapambano baina ya imani na
ushirikina, au tuseme baina ya haki na batili, na uadilifu na dhulma.

Kwa hiyo basi, kila unapoisoma tarekh, unakuta kuwa, katika nchi
ya Hijaz ambako ndiko uliko anzia Uislamu, kulikuwa na mvutano
au mapambano kati ya koo mbili za ki-Quraish; yaani ukoo wa Banu
Hashim na ukoo wa Banu Umayyah.

Msimamo wa kila mmoja kati ya koo hizi mbili, kuhusu Uislamu


pia ni jambo la dharura kuelezwa, kisha uongozi baada ya
kuondoka Mtume (s.a.w.w.) unahusika kubainisha uhakika wa
muhanga wa Sayyidina Husein (a.s.) huko Karbala.

Kwanza kabisa ni vema tukafahamu kuwa; waarabu kwa ujumla


walikuwa wamegawanyika katika makabila mengi ambayo kwa
bahati mbaya sana hayakuwa na umoja baina yao. Waarabu hao
walikuwa wakipigana wao kwa wao kwa muda mrefu. Hapakuwa na
aina ya utamaduni wa aina moja unaoweza kuwakusanya pamoja,
na wala hawakuwa na dini yoyote kati ya dini zilizoteremshwa na
Mwenyeezi Mungu.

Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa: “Watu hawa hawakuwa na


uongozi unaowajumuisha na kuwafanya wawe na umoja, na
mshikamano.”

1
Vita vya mara kwa mara baina yao, na mauwaji hasa ya watoto wa
kike, yalikuwa ni mambo yaliyoenea sana huko bara Arabu. Hayo
na mengine mengi yaliifanya hali ya eneo hili kuwa kama kituo cha
maovu.

Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) ameieleza hali ya waarabu hao
ilivyokuwa kabla ya kuja kwa Uislamu amesema: “Nanyi enyi
wa-Arabu mlikuwa na dini mbaya mno, na mlikuwa (mkiishi)
katika eneo baya mno.” (ufafanuzi wa hali ya waarabu, na dini zao
unahitajika). (Qur’an, 81:8) Na mtoto mwanamke aliyezikwa hai
atakapoulizwa.

Kuja kwa dini ya ki-Islamu ulikuwa ni ukombozi kwa watu wa


eneo hili, kwani kwa muda mfupi waliweza kubadilika na kuacha
mwenendo wao wa kijahiliyyah. Uislamu uliwabadili wakawa ni
watu wenye kuheshimika kwa utu na maendeleo. (Imam Ali (a.s.)
katika Nahjul-Balaghah juu ujio wa Mtume (s.a.w.w.))

Kuipigania dini hii lilikuwa ni jambo la mwanzo walilolithamini


kwa kuwa waliamini kabisa kwamba utu wao, heshima yao na
mustaqbali wao kwa ujumla umo ndani ya Uislamu.

Inasimuliwa kuwa: Sahaba Amri bin Jumuuh, alikataa kubakia


nyumbani katika vita ya Uhdi pamoja na kuwa sheria inamruhusu
asende vitani kutokana ulemavu aliokuwa nao.

Sahaba huyu alitoka na akapigana vita ile huku akisema: “Ewe


Mwenyeezi Mungu! Niruzuqu shahada, na wala usinirejeshe kwa
watu wangu hali ya kuwa sina kitu.”

Inafaa kusema kuwa: “Sababu ya mabadiliko ya haraka kiasi hiki


ndani ya jamii hii ya wa-Arabu, yalitokana na jinsi mafunzo ya
dini hii yalivyoshughulikia matatizo ya watu hao na kuyapatia
ufumbuzi.”

2
Kwa muda mrefu nafsi za watu zilikuwa zikisubiri kwa hamu
mkombozi dhidi ya madhila yaliyokuwa ndani ya jamii yao.
Dhulma, utumwa, mauwaji na maovu mengine mengi yalipata
ufumbuzi baada ya kuja Uislamu.

Kwa hiyo siri kubwa ya mafanikio ya Uislamu ilitokana na dini


hii kuwapatia watu kitu walichokuwa wakikihitajia kwa muda
mrefu. Uadilifu, haki na usawa ni mambo ambayo nafsi za watu
zinayahitajia wakati wote.

Pamoja na Uislamu kukubaliwa na kuenea kwa haraka ndani ya


jamii ya wa-Arabu, kuna baadhi ya watu hawakupendezwa na hali
ile, kwa kuwa iliwafanya wakose baadhi ya maslahi waliyokuwa
wakiyapata katika zama hizo kabla ya Uislamu.

Kwa hali hiyo, walilazimika kuingia katika dini si kwa sababu


wameamini, bali wazikinge nafsi zao kutokana na nguvu ya Uislamu
iliyokuja kutetea haki, uadilifu na usawa ndani ya jamii.

Mwenyeezi Mungu anasema: “Walisema (wa-Arabu wa jangwani):


Tumeamini. Waaambiye: Hamjaamini lakini semeni tuemesilimu,
maana imani haijaingiya katika nyoyo zenu .......... Kwa hakika
wenye kuamini ni wale waliyomwamini Mwenyeezi Mungu na
Mtume wake, kisha wakawa hawana shaka na wakapigania dini ya
Mwenyeezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao, hao ndiyo wakweli.”
(Qur’an, 49:14-15.)

Hadithi ya Karbala: Je! kuomboleza kifo cha Sayyidina Husein bin


Ali (a.s.) ni uzushi katika dini?

Kuomboleza kifo cha Sayyidina Husein bin Ali bin Abi Talib
(a.s.), kwa kuyakumbuka mateso yaliyompata, ni sunna ya Mtume
Muhammad (s.a.w.w.). Wanachuoni wa somo la historia ya

3
Ki-Islamu wamenukuu matukio kadhaa yanayo onesha kwamba
Mtume Muhammad (s.a.w.w.), aliomboleza kifo cha mjukuu wake
huyu muda mfupi tu baada ya kuzaliwa kwake.

Mtume (s.a.w.w.) aliendelea kuomboleza kifo hicho katika minasaba


mbali mbali, kuna baadhi ya nyakati maombolezo hayo aliyafanya
katika nyumba za wake zake, na wakati mwingine mbele ya
masahaba wake.

Kuna riwaya nyingi zilizo simuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.)


juu ya yeye kuomboleza kifo cha Sayyidina Husein (a.s.), siku ile
ile aliyozaliwa na kama tulivyotaja hapo kabla kwamba; ziko riwaya
nyingine zinazo sema kuwa: “Maombolezo hayo yalifanywa na
Mtume katika siku nyingine kadhaa mahali mbali mbali kwa
nyakati tofauti.” Tutaeleza baadhi ya riwaya hizo kama ushahidi wa
kuthibiti kitendo hicho cha Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kuhusu
kuomboleza kifo cha mjukuu wake huyu hata kabla ya mauti
kumfika.

Riwaya ya Kwanza: Al-Hafidh Al-Hakim An-Nishapuri ndani ya


kitabu chake kiitwacho Al-Mustadrak As-Sahihain1 ameandika
kama ifuatavyo: Imesimuliwa kutoka kwa Ummul-Fadhli binti
Al-Haarith2, kwamba yeye aliingia kwa Mtume (s.a.w.w.) akasema:
“Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu! Hakika usiku wa leo mimi
nimeona ndoto mbaya. Mtume (s.a.w.w.) akasema: Ni ndoto gani
hiyo? Ummul-Fadhli akasema: Ni mbaya mno! Mtume akasema:
Ni ndoto gani hiyo? (Ummul-Fadhli) akasema: Nimeona kipande
cha mwili wako kimekatwa na kikawekwa mapajani mwangu! Basi
Mtume (s.a.w.w.) akasema: Umeona jambo jema; kwa mapenzi ya
Mwenyeezi Mungu Fatimah atazaa mtoto wa kiume na utampakata
mapajani mwako. Hatimaye Fatimah (s.a.) alimzaa Husein (a.s.)
1 Juz 3 uk 176.
2 Ummul-Fadhli, jina lake ni Lubaah binti Al-Harith. Huyu ni dada wa Ummul-
Muuminina Maimunah (r.a.)

4
na nikampakata mapajani mwangu, kama alivyosema Mjumbe wa
Mwenyeezi Mungu (s.a.w.w.).”

Ummul-Fadhli anaendelea kusema: “Kuna siku nyingine tena


nilikwenda kwa Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu (s.a.w.w.), na
nikamuweka Husein (a.s.) mapajani mwa Mtume (s.a.w.w.). Kisha
kuna wakati nilishughulishwa na jambo fulani, basi mara ghafla
macho ya Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu yaliaanza kutiririka
machozi! Ummul-Fadhli anasema: Nikasema ewe Mtume wa
Mwenyeezi Mungu! Naapa kwa baba yangu na mama yangu,
umepatwa na jambo gani? Mtume (s.a.w.w.) akasema: Amenijia
Jibril (a.s.) akanieleza kwamba, umati wangu watamuuwa
mwanangu huyu. Mimi nikasema: Huyu? Akasema: Ndiyo, na
amenionesha sehemu ya udongo wake mwekundu (mahala atakapo
uliwa).”

Riwaya ya Pili: Imesimuliwa kutoka kwa Ummul-Muuminina


Ummu Salamah amesema: “Hasan na Husein (r.a.) walikuwa
wakicheza mbele ya Mtume (s.a.w.w.) nyumbani mwangu. Mara
Jibril (a.s.) alishuka akasema: Ewe Muhammad! Hakika umati wako
watamuuwa mwanao huyu baada yako - Akamuashiria Husein
kwa mkono wake - Basi Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu akalia
na akamkumbatia Husein kifuani kwake kisha Mtume (s.a.w.w.)
akasema (kuniambia mimi): Uhifadhi udongo huu ..... Kisha
akasema: Ewe Ummu Salamah udongo huu utakapogeuka na kuwa
damu mbichi, basi fahamu kwamba mwanangu Husein kisha uliwa.

Msimulizi wa hadithi hii anasema: Ummu Salamah akauweka


udongo ule ndani ya chupa, kisha akawa huutazama kila siku na
huku akisema: “Bila shaka siku utakapogeuka na kuwa damu,
wallahi siku hiyo ni siku inayotisha.”3

3 Al-Mu’jamul-Kabiir cha Al-Hafidh Abul-Qaasim At-Tabraani kwenye tarjama


ya Sayyidina Husein (a.s.)

5
Kuna riwaya nyingi mno zinazohusu kitendo hiki cha bwana Mtume
kuomboleza kifo hiki cha Sayyidina Husein (a.s.), kiasi kwamba si
rahisi kuzitaja zote. Lakini hazipungui riwaya kumi na tisa ambazo
baadhi yake bwana Mtume (s.a.w.w.) alilieleza jambo hili ndani
ya nyumba zake, na kuna wakati mwingine alilieleza mbele ya
Maswahaba wake. Na katika kila mara alipolieleza, hakuwacha kulia
kwa huzuni kutokana na kitendo kitakacho fanywa na umma wake
baada yake dhidi ya watu wa nyumbani mwake.

Kwa mukhtasari huu wa riwaya hizi, bila shaka kuomboleza kifo


hiki cha Sayyidina Husein (a.s.) si jambo la uzushi katika dini, kwa
sababu bwana Mtume (s.a.w.w.) ndiye mtu wa kwanza kuomboleza
kifo hiki kitakatifu cha mjukuu wake.

6
Majlis ya Pili :
Makundi Matatu: Muumini, Mwislamu na Mnafiki

Mwenyeezi Mungu anasema: “Walisema (wa-Arabu wa jangwani):


Tumeamini. Waaambiye: Hamjaamini lakini semeni tuemesilimu,
maana imani haijaingiya katika nyoyo zenu ..... Kwa hakika
wenye kuamini ni wale waliyomwamini Mwenyeezi Mungu na
Mtume wake, kisha wakawa hawana shaka na wakapigania dini ya
Mwenyeezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao, hao ndiyo wakweli.”
(Qur’an, 49:14-15.)

Jambo la kwanza linalo jitokeza wazi katika aya hizi ni kwamba;


japokuwa Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiwakubali watu kuingia
katika dini pindi wanapodhihirisha Uislamu, lakini hilo halikuwa
ndiyo lengo la msingi katika dini.

Na unapotafuta ni kwa nini Mtume alifanya hivyo, huwezi kupata


sababu nyingine zaidi ya kwamba kufanya kwake hivyo makusudio
yalikuwa ni kuandaa mazingira mazuri ya kufikisha ujumbe.

Mwenyeezi Mungu anasema: “Waite (watu) kwenye njia ya Mola


wako kwa hekima na mawaidha mazuri, na ujadiliane nao kwa
namna iliyokuwa bora. Kwa hakika Mola wako ndiye anayemjua
sana aliyepotea katika njia yake, naye ndiye anaye wajua sana waliyo
ongoka.” (Qur’an, 16:125.)

Kwa hiyo mwenendo wa Bwana Mtume (s.a.w.w.) kumkukubali


na kumkaribisha katika Uislamu kila aliyesilimu ni mbinu za
ufikishaji, lakini mwenendo huo haukuwa ndilo lengo la msingi,
bali kwa lugha ya leo tunaweza kusema: “Hicho kilikuwa ni
kipindi cha mpito, kuelekea kwenye lengo kamili la kumjenga na
kumpa mwanadamu misingi imara ya imani na kuwa na roho ya
ubinadamu ambao kwa muda mrefu ulikuwa umetoweka.”

7
Ni jambo lililo wazi, ya kwamba: Mafunzo ya Mtume (s.a.w.w.)
yalilenga kuwapata watu watakao kuwa tayari kutoa kila kilicho
chao, kuanzia mali hadi nafsi zao kwa ajili ya kupambana na
udhalimu na uovu uliyokuwa ukitawala enzi hizo kabla ya kuja dini
ya ki-Islamu. (Mfano urejewe kwa sahaba Amri bin Jumuuh).

Tunapo zisoma tena aya hizi tunaona zinatuambia kuwa:


“Haifai kwetu sisi kumzingatia na kumkubali kwa dhati kila
anayetangaza kusilimu, kuwa ni muumini.”

Ushahidi wa hilo ni kauli ya Mwenyeezi Mungu aliposema:


“Walisema (wa-Arabu wa jangwani): Tumeamini. Waambiye:
Hamjaamini lakini semeni tumesilimu, maana imani haijaingiya
katika nyoyo zenu.....”

Kwa ujumla ujumbe wa aya hii unatufahamisha kuwa: Katika


Uislamu kuna kundi la watu waliyoingia katika dini kujisalimisha
na kupata amani ya Uislamu, lakini hawakuamini kwa imani ya
kweli. Ndiyo maana pakasemwa: “... Waaambiye: Hamjaamini lakini
semeni tumesilimu, maana imani haijaingiya katika nyoyo zenu...”
(Qur’an, 49:14.)

Aya inayofuatia hapo inasema: “... Kwa hakika wenye kuamini ni


wale waliyomwamini Mwenyeezi Mungu na Mtume wake, kisha
wakawa hawana shaka na wakapigania dini ya Mwenyeezi Mungu
kwa mali zao na nafsi zao, hao ndiyo wakweli.”

Aya hii kwa ujumla wake inakusudia kutonesha kundi la pili katika
Uislamu. Hili ni kundi la Waumini.

Mwili wa binadamu ni kielelezo rahisi katika kuelewa tofauti kati ya


mwislamu na muumini. Inatupasa kuutazama mwili wa binadamu
ambao una sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza ya mwili ni ile
iliyoko nje, na ya pili ni roho.

8
Uislamu kadhalika una sehemu kuu mbili ambazo moja ni ile ya
dhahiri, na nyingine ni ile ya ndani au tuseme kuwa ndiyo imani ya
kweli iliyoko moyoni.

Uislamu kwa nje ni kutekeleza hukmu za kisheria ambazo ni


mashuhuri; kama vile swala, hijja, zakka na nyinginezo. Na
Uislamu kwa ndani ni ile hali ya muumini, baada ya kuwa
anatekeleza hukmu za kisheria, yuko tayari kujitolea katika njia ya
kutetea haki na uadilifu na kupambana na madhalimu na waovu wa
aina nyingine.

Wanafiq:
Wanafiki ni wale watu ambao imani kamwe haikupta nafasi ya
kuingia katika roho zao. Ukweli wa mambo watu wa aina hii kamwe
hawakukubali Uislamu, bali wanautumia Uislamu kwa maslahi yao
na tamaa zao binafsi.

Kila inapotokezea kwamba Uislamu unapingana na kutokubaliana


na maslahi yao, basi wao husimama upande wa upinzani
lakini kwa kutumia mbinu zilizopangwa kitaalamu, kiasi kwamba
siyo rahisi kugundua. Kwa hakika watu hawa kwa mbinu na ufundi
wanaoutumia, kwa nje utawaona wanapigania au wanaitetea dini,
lakini kumbe kwa ndani ni waasi wakubwa.

Mwenyeezi Mungu anasema: “Basi ole wao wanao swali. Ambao


wanapuuza swala. Ambao wao hujionesha.” (Qur’an, 107:4-6.)
Qur’an inaiona ile swala wanayoswali kuwa ni ya kujionesha mbele
za watu kwamba wao ni watu watakatifu wasiyokuwa na madhambi
mazito. Lakini baada ya maonyo hayo dhidi ya wanafiki, Qur’an
inahimiza na kuwajibisha kuwapiga vita katika mizani moja na
makafiri.

Mwenyeezi Mungu anasema: “Ewe Nabii! Wapige makafiri na


wanafiki na uwe mgumu kwao.....” (Qur’an, 9:73.)

9
Kwa mukhtasari ni kwamba: Daraja ya muumini iko juu zaidi
kuliko daraja ya mwislamu. Na ama unafiki; wenyewe pia ni siyasa
ya shetani. Kumbuka vita ya Siffin, na kunyanyuwa mishafu.

Huenda tukajiuliza kwa mujibu wa aya ya sabini na tatu sura ya tisa


inayo wajibisha kuwapiga makafiri na wanafiki, kwamba ilikuwaje
kwa Imam Ali (a.s.) kunyamaza kwa muda wote wa watwala
waliyomtangulia asichukuwe hatua dhidi yao? Au Imam Hasan
(a.s.) kumwachia Muawiyah bin Abi Sufiyan awe Khalifa wakati
yeye ndiye aliyestahiki?

Hapana shaka kwamba kuna mazingira yanayo sababisha hali kama


hiyo, lakini kuna sharti zake na misingi yake ambayo kwa leo siyo
mahala pake kulieleza hilo.

Hadithi ya Karbala. Maombolezo gani yasiyo malizika?


Pamoja na kuwa tumeonesha kuwa Mjumbe wa Mwenyeezi ndiye
wa kwanza kuonesha huzuni na maombolezo ya kifo cha Sayyidina
Husein (a.s.) hata kabla ya kifo hicho kutokea, kuna swali ambalo
linaulizwa mara nyingi kuhusu kuendelea kwa majonzi ya msiba
huu, kuanzia zama hizo mpaka leo.

Watu wengi wanajiuliza wanasema: “Ni msiba gani huu usiyo


malizika? Kwani tangu kuuliwa Sayyidina Husein (a.s.) mnamo
mwaka wa sitini na moja hijiriyyah hadi sasa kuna miaka
isiyopungua elfu moja mia tatu na sitini na nane. Hivyo basi ni
machungu gani haya yasiyopowa?”

Mapokezi yanayohusu kuendelea kwa maombolezo ya msiba wa


Sayyidina Husein (a.s.) ni mengi sana, kiasi kwamba nafasi ya
kuyasimulia yote haitoshi, lakini nukuu tatu zifuatazo zitatosha
kubainisha ni kwa nini maombolezo haya hayamaliziki.

10
Nukuu ya kwanza: “Nabii Yaqub bin Is-Haqa bin Ibrahim (a.s.)
alimlilia mwanawe Yusuf (a.s.) kwa muda wa miaka mingi.

Kilio hiki cha Nabii Yaqub (a.s.) hakikuwa ni kwa sababu ya kuuliwa
kwa mwanawe, bali Nabii Yusuf bin Yaqub alitoweka tu machoni
mwa baba yake.

Qur’an inaeleza kuwa Nabii Yaqub alilia mpaka macho yake yakawa
meupe. “... Oooh! Majonzi yangu kwa Yusuf!!! Na macho yake
yakawa meupe kwa huzuni, naye alikuwa amejawa na huzuni.”
(Qur’an, 12:84)

Mwanachuoni wa tafsir ya Qur’an inayoitwa Tafsirul-Kashaaf


anasema kuwa: “Kutokana na kilio cha Yaqub (a.s.), imefikia hadi
kusemwa kwamba: Macho yake hayakukauka (machozi kwa kilio)
tangu alipotengana na Yusuf (a.s.) mpaka alipokuja kukutana naye
ukiwa umepita muda wa miaka themanini.”

Nukuu ya Pili: Riwaya nyingine ni ile aliyoiandika Al-Allaamah


Al-Majlisi ndani kitabu chake Bihaarul-Anwaar amesema:
“Imesimuliwa kwamba, wakati Mtume (s.a.w.w.) alipomjulisha
binti yake Fatimah (s.a.) kuwa mwanawe Husein atauliwa na pia
akumueleza juu ya mitihani itakayompata. Fatimah (s.a.) alilia
sana kisha akasema: Ewe Baba yangu! Basi ni nani atakaye mlilia?
Na ni nani atakayedumisha maombolezo yake? Mtume (s.a.w.w.)
akasema: Ewe Fatimah! Bila shaka wanawake wa umma wangu
watawalilia wanawake wa nyumba yangu, na wanaume wa umma
wangu watawalilia wanaume wa nyumba yangu. Na maombolezo
haya watayahuyisha (na kupokezana) kizazi baada ya kizazi kila
mwaka, mpaka itakapokuwa siku ya qiyama wewe utaomba shufaa
kwa ajili ya wanawake na mimi nitaomba kwa ajili ya wanaume.
Na kila mtu aliyelia kutokana na masaibu yaliyomfika Husein
tutamshika mkono wake na tutamuingiza peponi. Ewe Fatimah!

11
Siku ya qiyama kila jicho litalia isipokuwa lile jicho lililolia kutokana
na masaibu ya Husein, jicho hilo litakuwa lenye furaha kwa neema
ya peponi.”4

Nukuu ya Tatu: Katika riwaya iliyosimuliwa kutoka kwa Ja‘far


bin Muhammad (a.s.) amesema kwamba: “Mtume (s.a.w.w.)
alimtazama Husein bin Ali (a.s.) alipokuwa akimjia, na kisha
alimkalisha mapajani mwake halafu akasema: Bila shaka kuuliwa
kwa Husein (kutaleta) fukuto katika nyoyo za waumini ambalo
kamwe halitapoa.”

4 Bihaarul-Anwaar juz 44, Babu thawabil-bukai alaa musiibatih, hadithi ya 137.

12
Majlis ya Tatu :
Kosa Kubwa Limetendeka

Waandishi wa ki-Islamu na wale wa ki-Magharibi wamefanya


kosa kubwa waliposhindwa kuyatenganisha makundi haya matatu
yaliyomo ndani ya dini ya ki-Islamu.

Siyo hao tu waliyotenda kosa hilo, bali na watu wa kawaida nao


wamejumuika katika dhana ya kuwaona waislamu wa hapo mwanzo
wote walikuwa na imani moja katika dini na lengo moja.

Ni jambo la wajibu hasa kwa kila mwislamu kufahamu kuwa ndani


ya uislamu kuna mgawanyiko huu, yaani kuna muumini, mwislamu
na mnafiki. Kwa bahati nzuri Qur'an imefanunua hali hii.

Labda kisa cha Abu Sufiyan kinaweza kuwa mfano hai wa


kuitambua hali waislamu wa awali. Inasimuliwa kuwa:
“Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akiingia mjini Makka siku ile ya Fathi
Makka (ushindi wa Wa-Islamu dhidi ya makafiri na washirikina),
Abu Sufiyan alimwambia Abbas bin Abdil-Mut-Talib: Kwa hakika
ufalme wa mwana wa nduguyo umekuwa mkubwa!!!

Mtazamo huu wa Abu Sufiyan, na msimamo wa Banu Umayyah


na wapinzani wengine wa Mtume (s.a.w.w.), unaonesha wazi kuwa
kimsingi, ni mtazamo unaojali maslahi ya kilimwengu.

Kwa watu kama hawa; ujumbe wa dini ya ki-Islamu wanauona


kuwa ni njia moja wapo ya kujipatia utawala na mali. Kwa upande
mwingine waliupinga Uislamu na kwa sababu ulikuwa unataka
kuleta uwiyano baina ya watu katika nyanja za maisha ya kila siku.

Kwa hali hiyo kwao wao Uislamu ulikuwa ni kipingamizi cha


mambo yao mengi khususan tunapo isoma tarekh tunawakuta

13
Banu Umayyah tangu hapo zamani walisifika kwa maovu ndani ya
jamii ya wa-Arabu huko Hijaz.

Hadithi ya Karbala:
Mnamo mwezi wa Rajabu mwaka wa sitini hijiriya, khalifa wa Ki-
Banu Umayyah kwa jina Muawiyah bin Abi Sufiyan alifariki dunia.
Wakati Muawiyah anafariki dunia, mwanawe aliyekuwa akiitwa
Yazid, alikuwa huko Hauraan.

Shughuli ya kuongoza mazishi ya Muawiyah ilisimamiwa na


Dhahhaak bin Qais, ambaye alimsalia na akamzika kwenye
makaburi yaliyokuwa yakijulikana kwa jina la Babus-Saghir. Baada
ya maziko haya, Dhahhaak alifanya haraka kupeleka ujumbe
kumwita Yazid huko Hauraan ili aje kuchukua baia (kiapo cha utii)
kwa mara nyingine kutoka kwa watu.

Mwishoni kabisa mwa barua aliyoipeleka kwa Yazid, Dhahhaak


aliandika akasema: “Mwana wa Abu Sufiyan ameondoka (yeye)
na mambo yake peke yake, na wewe umerithishwa, basi tazama
utafanya nini baada yake....”

Yazid alipoipata barua hii, aliondoka kuelekea Dimishqi


(Damascus), na akawasili baada ya siku tatu tangu kuzikwa
kwa Muawiyah. Alipoingia mjini hapo, alilakiwa na Dhahhaak
mwenyewe pamoja na watu wengine kisha moja kwa moja akapelekwa
mahala lilipo kaburi la baba yake. Na hatimaye Yazid alipanda juu
ya mimbari na kuwahutubia watu, ambapo alieleza wasifu wa baba
yake na pia wa kwake mwenyewe.

Baada ya mazishi haya, Yazid hakupata mtu wa kumpa pole


kutokana na msiba ule mpaka alipokuja Abdallah bin Humaam
As-Saluuli akawa ndiye mtu wa kwanza kutoa pole kwa Yazid
kutokana na msiba wa kufiwa na baba yake.

14
Ili kukifahamu vyema kisa cha Sayyidina Husein bin Ali (a.s.) na
yaliyompata huko Karbala katika nchi ya Iraq, ni vizuri tukaeleza
maandalizi yaliyofanywa na Muawiyah bin Abi Sufian katika suala
la kumrithisha ukhalifa Yazid bin Muawiyah.

Hadithi ya Karbala:
Jinsi Yazid alivyourithi Ukhalifa kutoka kwa Muawiyah:
Mughira bin Shu’bah alikuwa gavana wa Basra katika zama za
ukhalifa wa Muawiyah bin Abi Sufiyan. Kuna wakati Muawiyah
alikusudia kumuondoa madarakani Mughira bin Shu’bah. Taarifa
za kuuzuliwa ugavana wa mji wa Basra zilipomfikia Mughira,
alifunga safari kwenda Shamu ili kuomuona Muawiyah bin Abi
Sufiyan. Alipofika huko alikaribishwa na kisha akatoa rai kwa
Muawiyah kwamba, hakuna mwenye kustahiki ukhalifa baada ya
yeye Muawiyah ila ni Yazid mwanawe.

Rai hii ilimpendeza sana Muawiyah, lakini alitaka kujua kutoka


kwa Mughira kwamba ni nani atakayeweza kufanikisha jambo
lile huko kwenye majimbo ya dola ile ya ki-Islamu. Mughira
alimwambia Muawiyah kwamba: “Katika mji wa Kufah, yuko Ziyad,
na kwa upande wa Basra atasimamia yeye kufanikisha jambo hilo.”
Bali alisema: “Baada ya wakaazi wa miji hii miwili (kukubali) basi
hakuna tena mtu mwingine atakaye pinga.”

Huko Basra Mughira bin Shu’bah alifanikiwa kupata watu waliyo


unga mkono mapendekezo yake. Ama kwa upande wa mji wa
Kufah, Ziyad aliona ni mapema mno kuunga mkono rai hiyo,
na ndipo alipomtuma Ubaid bin Ka’b An-Numairi kwenda kwa
Muawiyah kumuomba aiakhirishe azma yake ya kumtawalisha
mwanawe. Muawiyah alikubali lakini Ziyad alipofariki Muawiyah
aliirejesha tena niya yake ya kumtawalisha Yazid.

Kwa mukhtasari Muawiyah alipoona kuwa siku zake za kuishi

15
zinaendea ukingoni, alimwita na kuwambia Yazid kwamba: “Ewe
mwanangu! Nimekuandalia mambo vizuri na maadui nimekwisha
kuwadhibiti kwa ajili yako. Na waarabu nimewafanya wawe watiifu
kwako na nimekukusanyia mambo ambayo hakuna mtu yeyote
aliyewahi kuyakusanya.”

Si hivyo tu, bali alimtaka mwanawe huyu awe mkarimu kwa watu
wa hijazi kwani huko ndiko kwenye asili yake. Kadhalika alimuasa
mno kutokana na watu wa Iraq akamwambia: “Endapo watu wa
Iraqi watakutaka kumuuzulu gavana (yeyote yule) kila siku basi
fanya hivyo, kwa sababu kumuuzulu gavana ni jambo jepesi mno
kuliko kukabiliwa na mapanga laki moja.”

Muawiyah hakuacha kumuusia Yazid kuwa mwema kwa watu wa


Shamu akamwambia: “Waangalie sana watu wa Shamu, kwa hakika
wao ndiyo wasiri wako na wandani wako. Iwapo utakuwa na
shaka na jambo lolote toka kwa adui yako, basi waombe msaada.
Na ukishapata ushindi mara moja warudishe watu hawa wa
Shamu mjini kwao, kwani kama watakaa katika mji usiyokuwa wa
kwao, mwenendo wao utabadilika.”

Zaidi ya hapo Muawiyah alimtahadharisha Yazid akamwambia:


“Kwa hakika mimi sikuhofii kuwa na mpinzani yeyote yule juu
ya jambo hili (la ukhalifa) isipokuwa watu wanne wa ki-Quraish.
Watu hao ni Husein bin Ali (a.s.), Abdallah bin Omar, Abdallah bin
Zubair na Abdur-Rahman bin Abu Bakr.” Kisha alimtaja kila mmoja
kati ya watu hawa wanne kwa wasifu wake.

Kuhusu wasifu wa Imamu Husein (a.s.) Muawiyah alimwambia


Yazid: “Ama Husein bin Ali (a.s.) yeye ni mtu mwepesi, na hapana
shaka kwamba watu wa Iraqi kamwe hawatamwacha mpaka
wamtowe. Iwapo atatoka dhidi yako basi ukimshinda msamehe
(umwache), kwani yeye anayo haki kubwa na ni katika jamaa wa
Muhammad (s.a.w.w.)”

16
Maelezo haya ni kwa ufupi sana kuhusu maandalizi yaliyofanywa
na Muawiyah bin Abi Sufiyan kumrithisha mwanawe Yazid
ukhalifa juu ya wa-Islamu. Insha Allah majlis ijayo tutaona ni
hatua gani alizochukua Yazid kujiimarisha mwanzoni tu mwa
utawala wake baada ya kifo cha baba yake.5

5 Tarikh Al-Kamil ya Ibn Athiri, matukio ya mwaka wa 59 hijiriyyah juz 3 uk 503-


506; chapa ya Darul-Fikri Beirut ya mwaka 1399 A.H sawa na 1979 A.D.
Pia Tarikh Tabari matukio ya mwaka wa 60 A.H juz 5 uk 322 chapa ya Darut-
turathi, Beirut.

17
Majlis ya Nne :
Kizazi cha Hashim na Kizazi cha Umayyah

Wanachuoni wa historia ya ki-Islamu wanaeleza kuwa: Banu Hashim


na Banu Umayyah ni koo mbili mashuhuri toka zama za jahiliyyah,
kwa maana kabla ya kudhihiri dini ya ki-Islamu.

Koo hizi mbili kila moja ilikuwa na wasifu tofauti na mwenzake


katika jamii ya wakati huo katika bara Arabu. Wakati Banu Hashim
walisifika kwa sifa njema, Banu Umayyah walisifika kwa sifa ya
maovu.

Kwa mfano Umayyah mwenyewe, katika maovu aliyoyatenda ni


pamoja na kumuozesha mkewe kwa mwanawe, na kwa ndoa hiyo
akazaliwa Abu Muait.

Kwa mujibu wa wanachuoni wa historia wanasema kuwa: “Kitendo


kama hiki katika zama hizo kilikuwa ni kitendo cha aibu kubwa, na
wala hakuwahi kukifanya yeyote ndani ya jamii ya waarabu wa zama
hizo.”6

Amma Harb bin Umayyah, naye ni kama baba yake kwa maovu.
Bwana huyu alipanga njama za mauaji dhidi ya myahudi mmoja
aliyekuwa jirani ya Abdul-Muttalib.

Ibn Athiir ndani ya kitabu chake cha tarekh anasema kuwa: “Abdul-
Muttalib alikuwa na jirani yake myahudi kwa jina akiitwa Udhyah.
Myahudi huyu alikuwa ni mfanya biashara na alikuwa na mali
nyingi. Kutokana na utajiri wa myahudi huyu Harb bin Umayyah
aliingiwa na chuki kubwa dhidi yake.”

6 As-Siraau bainal-Amawiyyiina wa Mabaadiul-Islaam uk 34; An-Nahdhatul-


Huseiniyyah cha Sayyid Ali Al-Huseini Al-Farhiyyi uk 23 ambaye amenukuu
toka An-Nizaau wa At-Takhaasumu cha Maqrizi uk 50.

18
Ibn Athiir anaendelea kueleza anasema: “Harb alikodi vijana wa
ki-Quraish ili kumuuwa yule myahudi na kuchukuwa mali zake.
Amir bin Abdi Manaaf bin Abdid-Daar na Sakhru bin Amri bin
Ka’bi At-Taimi (babu yake Abu Bakr) ndiyo waliyomuuwa yule
myahudi. Kwa bahati mbaya Abdul-Muttalib hakufahamu ni nani
aliyemuuwa jirani yake, lakini alifanya uchunguzi na hatimaye
alifahamu kuwa vijana wale ndiyo waliyo muuwa.

“Katika kuwafuatilia, akagundua kuwa wote wawili wamepewa


hifadhi kwa Harb bin Umayyah. Bwana Abdul-Muttalib alikwenda
kwa Harb akamlaumu na kumtaka awatowe wauwaji hao, lakini
Harb alikataa.....”7

Hadithi ya Karabala:
Majlis iliyopita, katika hadithi ya Karbala, tulieleza namna
Muawiyah alivyompa nasaha Yazid juu ya mambo kadhaa ikiwemo
jinsi yeye Muawiyah alivyofanikiwa kuwadhibiti maadui zake, na
kwamba hakuna kiongozi aliyefanikiwa kumuandalia mrithi wake
kama alivyofanya yeye kwa mwanawe huyu.

Pamoja na hayo Muawiyah alimtaka Yazid awe mkarimu kwa watu


wa Hijaz kwa kuwa asili yake inatoka huko na pia awe msikivu
mno kwa watu wa Iraq akamwambia: “Endapo watu wa Iraqi
watakutaka kumuuzulu gavana (yeyote yule) kila siku, basi fanya
hivyo kwa sababu kumuuzulu gavana ni jambo jepesi mno kuliko
kukabiliwa na mapanga laki moja.”

Tulisema pia kwamba: Muawiyah hakuacha kumuusia Yazid kuwa


mwema kwa watu wa Shamu akamwambia: “Waangalie sana watu
wa Shamu, kwa hakika wao ndiyo wasiri wako na wandani wako.”

Aliendelea kumwambia: “Iwapo utakuwa na shaka na jambo


7 Tarekh Ibn Athir juz uk. As-Siraau bainal-Amawiyyiina wa Mabaadiul-Islaam
uk 36.

19
lolote toka kwa adui yako, basi waombe msaada. Na ukishapata
ushindi mara moja warudishe watu hawa mjini kwao, kwani
endapo watakaa katika mji usiyokuwa wa kwao, mwenendo wao
utabadilika.”

Muawiyah hakuacha kumzindua Yazid kuhusu watu ambao yeye


Muawiyah aliwaona kuwa ni hatari inayoweza kumkabili mwanawe
huyu akamwambia: “Kwa hakika mimi sikuhofii kuwa na mpinzani
yeyote yule juu ya jambo hili (la ukhalifa) isipokuwa watu wanne wa
ki-Quraish. Watu hao ni Husein bin Ali (a.s.), Abdallah bin Omar,
Abdallah bin Zubair na Abdur-Rahman bin Abu Bakri.”

Kisha tulieleza jinsi Muawiyah alivyotoa wasifu maalum wa


Sayyidina Husein bin Ali bin Abi Talib akasema: “Ama Husein bin
Ali (a.s.) yeye ni mtu mwepesi, na hapana shaka kwamba watu wa
Iraqi kamwe hawatamwacha mpaka wamtose. Iwapo atatoka dhidi
yako, basi ukimshinda msamehe (umwache), kwani yeye anayo haki
kubwa na ni katika jamaa wa Muhammad (s.a.w.w.)”

Leo ndani ya hadithi yetu ya Karbala, tutaeleza hatua alizozichukua


Yazid kujiimarisha mwanzoni tu mwa utawala wake baada ya kifo
cha baba yake.

Ibn Athir ndani ya Tarikh Al-Kamil anasema kuwa: “Mwezi wa


Rajab mwaka wa sitini hijiriyya, Yazid alipewa baia ya ukhalifa
baada ya kifo cha baba yake. Wakati huo magavana wa majimbo
ya dola ya ki-Islamu walikuwa kama ifuatavyo: Gavana wa Madina
alikuwa Walid bin Utbah bin Abi Sufiyan, na Makka alikuwa Amri
bin Al-A’s. Ama kule Basra gavana wake alikuwa Ubaidullahi bin
Ziyaad, na kule Kufah, Nu’man bin Bashir alikuwa ndiye gavana.”

Jambo muhimu kuliko yote baada ya Yazid kuingia madarakani,


yeye alikusudia kupata baia (kiapo cha utii) kutoka kwa watu

20
ambao hapo kabla walikataa kumbai Muawiyah bin Abi Sufiyan.
Ndipo Yazid alipomwandikia barua Walid kumueleza habari ya kifo
cha Muawiyah.

Ndani ya barua hiyo aliambatanisha barua nyingine ndogo yenye


ujumbe usemao: “Ama Ba’d; Mlazimishe Husein na Abdallah bin
Umar na mwana wa Zubeir wale kiapo cha utii. Walazimishe na
usiwape nafasi hata kidogo mpaka wale kiapo. Was-Salaam.”

Baada ya kuisoma barua hii, Walid alimwitisha Marwan bin Al-


Hakam akamuomba ushauri afanye nini kuhusu yaliyomo ndani ya
barua ile.

Marwan alimwambia Walid kwamba: “Waite sasa hivi na


uwaamuru wale kiapo cha utii (kwa Yazid).” Aliendelea akasema:
“Ikiwa watakula kiapo cha utii basi wakubalie na wala usiwafanye
lolote, na kama watakataa basi wauwe kabla hata hawaja fahamu
kwamba Muawiyah amekwisha kufariki.”

Marwan aliendelea kumwambia Walid kwamba: “Hapana shaka


endapo watu hawa watafahamu kwamba Muawiyah amekwisha
kufa, basi kila mmoja ataelekea upande wake na kudhihirisha
upinzani na kisha atajitangazia ukhalifa kwa ajili ya nafsi yake.”

Kisha Marwan akasema: “Ama Ibn Umar hawezi kupigana na wala


hapendi kuwatawalia watu isipokuwa tu iwapo atapewa jambo hili
kwa bahati tu.”

Baada ya ushauri huu, Walid alimtuma kijana mdogo aliyekuwa


akiitwa Abdallah bin Amri bin Uthman aende kuwaita Husein bin
Ali (a.s.) na Abdallah bin Zubair. Kijana huyu aliwakuta wawili hawa
wakiwa msikitini na akawapa ujumbe kwamba Walid anawaita.
Walimjibu wakasema: “Wewe nenda nasi tutakuja hivi punde.”

21
Abdallah bin Zubair alimwambia Husein (a.s.) kwamba: “Kuna nini
kwa mtu huyu kutuletea ujumbe saa hizi, ambapo hana kawaida
ya kuwa na vikao katika nyakati kama hizi?” Imam Husein bin Ali
(a.s.) akamjibu Bin Zubair akasema: “Nadhani kwamba yule muovu
wao amekufa, na hapana shaka ametuita ili atulazimishe kula kiapo
cha utii kabla habari za kifo hiki hazijaenea miongoni mwa watu.”

Abdallah bin Zubair naye akasema: “Nami pia sidhani kama kuna
jambo jingine lisilokuwa hili, sasa je! Utafanya nini?” Imam Husein
(a.s.) akasema: “Sasa hivi mimi nitawakusanya vijana wangu kisha
nitakwenda kwake. Vijana wangu nitawakalisha mlangoni halafu
mimi nitaingia ndani.”

Pale pale Sayyidina Husein bin Ali (a.s.) alisimama akawakusanya


wafuasi wake na watu wa nyumbani mwake, kisha wakaelekea kwa
Walid aliyekuwa gavana wa Madina kwa wakati ule.

Walipofika mlangoni Sayyidina Husein (a.s.) akawaambia wafuasi


wake: “Mimi naingia ndani, basi nitakapokwiteni au mkisikia sauti
yangu imepaa juu ingieni nyote kwa pamoja, vinginevyo bakieni
hapa mpaka nitoke.” Kisha Sayyidina Husein (a.s.) aliingia ndani na
akatoa salamu. Miongoni mwa watu waliokuwa mbele ya Walid ni
Marwan bin Al-Hakam.

Insha Allah tukijaaliwa katika Majlis ijayo tutaona ni mambo gani


yaliyo tokea baada ya Sayyidina Husein (a.s.) kuingia katika kikao
kile. Je! Walid atafanya nini? Atafuata ushauri wa Marwan au
hapana? Ahsanteni.

22
Majlis ya Tano :
Kizazi cha Hashim na Kizazi cha Umayyah

Kuzungumzia ukoo wa Banu Umayyah na jinsi walivyo katika tarekh


ya ki-Islamu ni jambo muhimu sana, kuliko kueleza koo nyingine
ukitoa ukoo wa Banu Hashim, ambao nafasi yao ni ya kipekee.

Hata hivyo kwa kiwango ambacho si cha kutosha, Banu Hashim


wanafahamika, na mchango wao katika dini unatambulikana kiasi.

Miongoni mwa sababu zilizofanya Uislamu uwe hivi ulivyo leo hii,
Banu Umayyah wamechangia kwa asilimia kubwa mno.

Ndiyo maana bado tunaendelea kueleza kuhusu namna walivyo


Banu Umayyah, kabla ya zama za kuja Uislamu na baada ya kuja
Uislamu.

Majlis iliyopita tulimazia kueleza fitna iliyofanywa na Harb bin


Umayyah alipopanga njama za kumuuwa yule myahudi mwenye
mali kutokana chuki na husda zake. Leo tutamzungumzia Abu
Sufiyan na vitimbi vyake alivyo fanya dhidi ya Mtume na waislamu
kwa niya ya kuizima nuru ya Uislamu.

Banu Umayyah na washirika wao (wakiongozwa na Abu Sufiyan)


walitumia njia mbali mbali za pamoja au binafsi kumkera na
kumuudhi Mtume (s.a.w.w.).

Kuna wakati walimtuma Abdallah bin Abi Rabia‘ na Amr bin Al-
A’as waende kwa Najjaashi, yule mfalme wa Uhabeshi, ili kumtaka
awafukuze waislamu waliyohamia huko kukimbia mateso ya
Maquraish.

Banu Umayyah na washirika wao chini ya uongozi wa Abu Sufiyan,

23
ndiyo wale waliyofanya mateso makubwa dhidi ya waislamu
wanyonge kama vile; Bilal (mwadhini wa Mtume (s.a.w.w.)),
Ammaar bin Yaasir na baba yake na mama yake na wa-Islamu
wengine wengi.

Upinzani wa Banu Umayyah na washirika wao dhidi ya Mtume


(s.a.w.w.), kwa njia ya kuwaadhibu wa-Islamu ulishindwa, na badala
yake watu wengi walizidi kuingia katika dini. Kushindwa huku
kuliwafanya maquraishi na Banu Umayyah wabadili mbinu.

Banu Umayyah waliandaa ujumbe wa watu watatu kwenda kwa


Abu Talib wazungumze naye ili amkataze mwanawe kuwatia dosari
miungu yao.

Bwana Abu Talib aliyakataa maombi yao, na badala yake akazidi


kumtia nguvu bwana Mtume (s.a.w.w.) katika kazi ya kufikisha
ujumbe wa dini hii tukufu.

Njama hii iliposhindwa Banu Umayyah wakabuni njia nyingine


ambayo ni kumkera na kumuudhi Mtume (s.a.w.w.). Watu hawa
walianzisha mashambulizi ya kumwita mchawi, mwenda wazimu
na mengine katika mambo ya kumtia kombo.

Walengwa wa uzushi huu zaidi ni wale wageni kutoka nje ya mji


wa Makka, na madhumuni ni kuwafanya wasimwamini Mtume
(s.a.w.w.) wala kumfuata. Njama hizi nazo hazikufaulu kurudisha
nyuma kasi ya kulingania Uislamu.

Historia inasimulia kwamba: Baada ya hatua hii kushindwa na


kutokuwa na mafanikio, Banu Umayyah waliteuwa watu maalum
ambao kazi yao ni kufanya maudhi, kero na kejeli dhidi ya Mtume
(s.a.w.w.).

24
Watu hao walikuwa wengi, kama ifuatavyo: Utbah na Shaibah
ambao ni watoto wa Rabia‘, Uqbah bin Abi Muiit, Abu Sufiyan na
Al-Hakam bin Abil-A’s. Wengine ni Al-A’s bin Waail As-Sahmi
ambaye ni baba wa Amr, na watoto wa ami yake ambao ni Nabiih
na Manbah.

Al-Hakam, baba wa Marwan, alikuwa na kejeli nyingi mno na


maudhi makubwa dhidi ya Mtume (s.a.w.w.).

Maudhi, kero na kejeli za Banu Umayyah dhidi ya Mtume


hazikufanywa na wanaume tu, bali hata wanawake wa ki-Banu
Umayyah walishiriki. Ummu Jaamil, yule Hammaaltul-Hatabi
aliyetajwa ndani ya Qur’an, ni miongoni mwa wanawake hao.8

Yote haya yalifanywa na Banu Umayyah katika kipindi ambacho


Mtume (s.a.w.w.) alikuwa bado yuko Makka.

Hadithi ya Karbala:
Katika majlis iliyopita ndani ya hadithi ya Karbala, tuliona jinsi
Sayyidina Husein (a.s.) alivyokuwa na tahadhari kutokana na
madhara yanayo weza kutokea kwenye kikao baina yake na gavana
wa Madina, Walid.

Kwa hali hiyo basi, Sayyidina Husein (a.s.) alipofika mlangoni kwa
Walid aliwaambia wafuasi wake kuwa: “Mimi naingia ndani, basi
nitakapokwiteni au mkisikia sauti yangu imepaa juu ingieni nyote
kwa pamoja, vinginevyo bakiyeni hapa mpaka nitoke.”

Tulieleza pia kwamba: Sayyidina Husein alipoingia ndani, alimkuta


Walid na watu wengine akiwemo Marwan bin Al-Hakam. Sayyidina
Husein alitoa salamu kisha akaketi.
8 Huyu ndiye yule mwanamke ambaye Qur’an ilishuka kwa ajili yake kukemea
matendo yake dhidi ya Mtume (s.a.w.w.). Rejea sura ya 111, suratul-Masad aya
ya nne.

25
Walid bin Utbah aliitumia fursa hiyo kumsomea Sayyidina Husein
(a.s.) barua kutoka kwa Yazid inayoeleza habari za kifo cha
Muawiyah bin Abi Sufiyan, kisha akamtaka Sayyidina Husein (a.s.)
ale kiapo cha utii mbele yake kwa niyaba ya Yazid.

Sayyidina Husein (a.s.) alijibu akasema: “Innaa lillahi wa Innaa


Ilaihi rajiuun! (Sisi ni milki ya Mwenyezi Mungu na kwake
tutarejea). Mwenyezi Mungu amrehemu Muawiyah, nawe akulipe
ujira mwingi.”

Baada ya maneno hayo Sayyidina Husein bin Ali akasema: “Amma


kuhusu kula kiapo cha utii kwa Yazid, bila shaka mtu kama mimi
hawezi kula kiapo kwa siri, na wala wewe huwezi kunitosheleza kwa
kufanya siri kuhusu jambo hilo.”

Aliendelea kusema kuwa: “Pindi utakapo waita watu kwa ajili ya


kula kiapo hiki, basi nasi utatuita.”

Katika riwaya nyingine inasemekana kuwa; Sayyidina Husein


bin Ali (a.s.) aliposomewa barua inayoeleza habari za kifo cha
Muawiyah na kisha kutakiwa kula kiapo cha utii kwa Yazid alisema:
“Innaa lillahi wa Innaa Ilaihi rajiuun! Sasa Uislamu tuuage (kwa heri
ya kuonana), kwa hakika ummah umepata mtihani kwa kuwa na
kiongozi mfano wa Yazid.”

Baada ya majibu haya, Walid akamwambia Sayyidina Husein: “Basi


nenda kwa jina la Mwenyezi Mungu, na utakuja pindi tutakapo
waita watu.”

Majibu haya yanaonesha wazi kabisa kwamba, Walid hakuwa mtu


mwenye kupenda ufisadi. Lakini kabla ya Sayyidina Husein (a.s.)
kuondoka, Marwan bin Al-Hakam alimwambia Walid kwamba:
“Endapo Husein ataondoka hapa hivi sasa bila ya kula kiapo, basi

26
kamwe hutampata. Usimruhusu kutoka mpaka kwanza ale kiapo, na
akikubali hakuna neno, lakini akikataa mkate shingo yake.”

Sayyidina Husein (a.s.) alipoyasikia maneno ya Marwan,


alikasirika mno na akamwambia Marwan: “Ewe mwana wa Zarqaa,
hivi ni wewe unayeniuwa au yeye? Namuapa Mwenyezi Mungu!
Kwa hakika wewe ni muongo na umefanya kosa (kutoa ushauri
kama huo).” Kisha Sayyidina Husein bin Ali (a.s.) alitoka
akawachukua watu wake akarejea nyumbani kwake.

Baada ya Sayyidina Husein (a.s.) kuondoka kwenye kikao kile bila


ya kula kiapo cha utii, Marwan alimwambia Walid: “Umepinga
ushauri wangu, basi namuapa Mwenyezi Mungu kamwe hutampata
tena Husein.”

Walid alimjibu Marwan akamwambia: “Muonye mwingine ewe


Marwan! Bila shaka (kwa ushauri wako huo) wewe umenichagulia
jambo ambalo ndani yake nitaikosa dini yangu na dunia yangu.
Namuapa Mwenyezi Mungu, sipendi kuwa na milki ya mali ya
ulimwengu wote na ufalme wake hali kuwa mimi ndiye niliye
muuwa Husein (a.s.).”

Walid aliendelea kusema: “Umetakasika mno ewe Mwenyezi


Mungu! Miye nimuuwe Husein ati kwa sababu tu amesema kuwa
hataki kula kiapo cha utii? Namuapa Mwenyeezi Mungu, hakika
mimi naona kuwa mtu yeyote atakaye muuwa Husein, bila shaka
siku ya qiyama mbele ya Mwenyeezi Mungu mtu huyo mizani yake
itakuwa nyepesi. Si hivyo tu, bali Mwenyeezi Mungu hatomtazama
mtu huyo wala kumtakasa na atapata adhabu kali.”

Marwan alimjibu Walid akamwambia: “Ikiwa hayo ndiyo maoni


yako, basi maamuzi yako na ulivyo fanya ni sawa.” Wana historia
wanasema kuwa: Marwan aliyasema maneno hayo kumridhisha tu
Walid, lakini hakuwa na maana ya kuunga mkono rai yake.

27
Ndani ya kisa hiki cha Sayyidina Husein bin Ali (a.s.), kuna watu
wengi wanahusika kutajwa kwa namna hii au ile. Tuonavyo sisi si
muhimu sana kuendelea kuwataja watu hao kila hatua inayoendelea
katika kisa hiki, japokuwa hapo mwanzoni tuliwataja. Watu hawa
ni kama vile Abdallah bin Zubair na Abdallah bin Umar ambao pia
waliendelea kupelekewa wajumbe ili waonane na Walid kwa ajili ya
kula kiapo cha utii.

Sababu kubwa inayotufanya tusione umuhimu wa kuendelea


kuzitaja habari zao ndani ya hadithi hii ya Karbala, ni kwa kuwa kila
mmoja kati ya watu hao alikuwa na msimamo wake na umuhimu
wake kuhusu jambo hili la kiapo na mengineyo yanayoihusu dola ya
ki-Islamu ya kipindi hicho .

Msimamo wa Sayyidina Husein (a.s.) na umuhimu wake kwa Yazid


na utawala wa Banu Umayyah, ulikuwa na nafasi ya pekee tofauti na
msimamo na umuhimu wa watu wengine kwa Yazid mwenyewe na
hata kwa watawala wengine wa ki-Banu Umayyah.

Mwenyezi Mungu akitujaaliya tutaendelea na hadithi ya Karbala


katika majlis ijayo. ambapo tutaona jinsi Walid na Marwan
walivyojitahidi kumfanya Sayyidina Huseina (a.s.) akubali kula
kiapo kile.

28
Majlis ya Sita :
Kizazi cha Hashim na Kizazi cha Umayyah :
Mtume Kuhamia Madina

Banu Umayyah waliposhindwa kila mbinu waliyopanga dhidi ya


Mtume (s.a.w.w.), waliamua kupanga njama za kumuuwa Mtume
(s.a.w.w.) hapo Makka, na ndipo akalazimika kuhamia Madina.

Pamoja na yeye kuhamia Madina lakini watu hawa hawakumwacha


apumzike, bali walimfuata huko huko wakiongozwa na Utbah bin
Rabia’,9 Abu Sufiyan, Al-Hakam bin Al-A’s ambaye ni Ibn Ammi ya
Abu Sufiyan.

Matokeo ya wao kumfuata Mtume (s.a.w.w.) huko Madina ni ile vita


kuu ya Badri iliyopiganwa mnamo mwaka wa tatu wa hijra kati ya
wa-Islamu na washirikina wa Makka.

Miongoni mwa Banu Umayyah waliyo uliwa siku hiyo ni Utbah


bin Rabia’ na mwanawe pamoja na Uqbah bin Abi Muiit.
Waliochukuliwa mateka vitani kwa upande wa Banu Umayyah,
ni Abul-A’s bin Rabii na Amr bin Abi Sufiyan. Katika vita hii
Muawiyah alisalimika kuuliwa na pia hakuchukuliwa mateka
akakimbia.

Matokeo haya yalizidisha chuki na hasira za Abu Sufiyan na Banu


Umayyah kwa jumla dhidi ya Mtume (s.a.w.w.) na waislamu,
kutokana na kuvunjika kwa nguzo za washirikina na maegemeo yao.

Wana historia wanasema kuwa: “Abu Sufiyan aliporejea Makka


aliwazuwia watu kuomboleza vifo vya jamaa zao na wala washairi
hawakuruhusiwa kusoma mashairi ya maombolezo. Abu Sufiyan
amenukuliwa akisema: “Basi ikiwa ninyi mtaomboleza vifo vyao,
9 Utbah bin Rabia’: Ni baba yake Hind mke wa Abu Sufiyan, mama wa Muawiyah
na ndiye nyanya yake Yazid.

29
na mkawalilia kwa kusoma mashairi (ya maombolezo) mtaondosha
hasira zenu na chuki zenu, na kwa hali hiyo hamtakuwa tena na ua-
dui dhidi ya Muhammad na masahaba wake.”10

Baada ya vita kuu ya Badri, Abu Sufiyan akawa ndiye kiongozi wa


kundi la maadui wa Mtume (s.a.w.w.). Alitengeneza jeshi ambalo
lilitoka kwenda Madina kupigana na Mtume na wa-Islamu.

Ndani ya jeshi hilo alihamasisha wanawake wajitokeze kwa wingi.


Abu Sufiyan mwenyewe alitoka na mkewe Hind na mkewe
mwingine, kama ambavyo Sufiyan bin Umayyah alitoka na
wanawake wawili. Talha alitoka na mkewe, na Harith bin Hishaam
naye akatoka na mkewe, ambapo Khunas binti Maalik alitoka na
mwanawe.

Wengine waliotoka na wake zao walikuwa ni: Al-Harith bin Sufiyan


alitoka na mkewe, Kinanah akatoka na mkewe, na Sufiyan bin Auf
naye akatoka na mkewe. Ama Nuuman na Jabir ambao ni watoto wa
Mask, wao walitoka na mama yao.

Hadithi ya Karbala:
Tumeona ndani ya majlis yetu iliyopita kwamba Sayyidina Husein
(a.s.) aliondoka kwenye ile baraza ya Walid moja kwa moja
akaelekea nyumbani kwake. Alibakia hapo Madina usiku ule,
ambao ulikuwa ni usiku wa kuamkia siku ya Jumamosi mwezi
ishirini na saba Rajab, mwaka wa sitini hijiriyyah.

Kulipokucha Sayyidina Husein (a.s.) alitoka ili kufahamu nini


kinacho endelea kuhusu qadhiya hii ya yeye kutakiwa kula kiapo
cha kumkubali Yazid kuwa ndiye khalifa baada ya kifo cha
Muawiyah bin Abi Sufiyan. Mara alikutana na Marwan bin
Al-Hakam ambapo Marwan alimwambiya Sayyidina Husein (a.s.)
10 As-Siraau bainal-Amawiyyiina wa Mabaadiul-Islaam uk 40 akinukuu toka
Maghaazi Rasulillahi s.a.w.w. uk 90-93 cha Al-Waaqidi.

30
kwamba: “Ewe Baba Abdillah! Mimi ninayo nasaha kwa ajili yako,
nakuomba unitii (katika nasaha hiyo).” Sayyidina Husein (a.s.)
akasema: “Ni nasaha gani hiyo, hebu sema nisikilize?”

Marwan akamwambiya: “Kwa hakika mimi nakuamuru ule kiapo


cha utii kwa Yazid, kwani jambo hili ni lenye kheri kwako katika
dini yako na dunia yako.”

Basi pale pale Sayyidina Husein (a.s.) alijibu akasema: “Innaa lillahi
wa Innaa Ilaihi rajiuun! Sasa Uislamu tuuage (kwa heri ya kuonana),
kwa hakika ummah umepata mtihani kwa kuwa na kiongozi mfano
wa Yazid.” Mazungumzo kati ya wawili hawa yalikuwa marefu kiasi
kwamba Marwan aligeuka akaondoka hali ya kuwa amekasirika.

Ilipofika jioni ya Jumamosi ile, Walid aliwatuma tena watu wake


wamwite Sayyidina Husein (a.s.) aje kula kiapo cha utii. Sayyidina
Husein (a.s.) aliwajibu watu wale akawaambiya: “Nendeni hadi
kutakapo kucha asubuhi mtaona nini cha kufanya na sisi tutaona
nini cha kufanya.” Watu wale walimwacha Sayyidina Husein bin Ali
(a.s.) bila kumlazimisha kwenda kwa Walid.

Usiku wa Jumamosi ile Sayyidina Husein (a.s.) alikwenda kwenye


kaburi la Mtume (s.a.w.w.) kisha akasema: “Amani iwe juu yako ewe
Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Mimi ni Husein mtoto wa Fatimah.
Mimi ni mwanao, na ni mtoto wa binti yako nami ni mjukuu wako
ambaye umeniacha ndani ya umma wako. Shuhudia ewe Nabii wa
Mwenyeezi Mungu, kwamba watu hawa wamenidhalilisha na wala
hawakuniheshimu. Haya ndiyo malalamiko yangu kwako mpaka
siku nitakayo kutana nawe.” Sayyidina Husein (a.s.) alibakia pale
hali ya kuwa anasali na kuomba.

Katika riwaya nyingine inasemwa kuwa: Sayyidina Husein (a.s.)


kwenye kaburi la Mtume (s.a.w.w.) alisali rakaa nyingi sana, kisha

31
akaanza kuomba kwa kusema: “Ewe Mwenyeezi Mungu! Hili ni
kaburi la Mtume wako Muhammad (s.a.w.w.). Bila shaka Wewe
Unayafahamu mambo yote yaliyonifika. Ewe Mwenyeezi Mungu!
Mimi nayapenda mema na ninayachukia maovu. Ewe Mola
uliyetukuka! Nakuomba kwa utukufu wa kaburi hili na yule
aliyemo, Unichagulie maamuzi ambayo Wewe Mwenyewe na
Mjumbe wako Mtayaridhia.” Kisha baada ya maombi haya,
Sayyidina Husein (a.s.) akalia sana.

Usiku ule alikesha pale pale kwenye kaburi la Mtume (s.a.w.w.)


akifanya ibada mbali mbali mpaka asubuhi. Kulipokucha alikutana
na watu wa nyumba yake wakiwemo ndugu zake. Sayyidina Husein
(a.s.) aliwaeleza azma yake ya kuondoka mjini Madina. Baadhi
yao walimtaka akubali kula kiapo cha utii ili asalimike na kubakia
Madina, na wengine walimtaka aondoke Madina aende Makka na
awaambiye watu wa huko wampe baiya yeye.

Miongoni mwa nduguze aliozungumza nao kabla hajaondoka,


walikuwa ni Muhammad Al-Hanaffiyyah bin Ali bin Abi Talib
na Umar Al-Atraf bin Ali bin Abi Talib. Kadhalika Abdallah bin
Umar bin Khattaab naye alipata nafasi ya kumpa ushauri Sayyidina
Husein (a.s.).

Ummu Salamah ambaye ni mke wa Mtume (s.a.w.w.), yeye alimtaka


Sayyidina Husein (a.s.) asiondoke kwa kuwa anajuwa huko aendako
atauliwa kutokana na bishara aliyoisikia kutoka kwa Mtume
(s.a.w.w.). Majibu ya Sayyidina Husein kwa Mama Ummu Salamah
yalikuwa kama ifuatavyo. “Ewe Mama! Kama sintaondoka leo,
basi kesho nitaondoka, na kama si kesho basi baada ya kesho
nitaondoka, kwa hakika kwangu mimi mauti ni jambo la lazima.....”

Kwa mukhtasari ni kwamba Sayyidina Husein bin Ali (a.s.)


hakuafiki rai ya yeyote isipokuwa aliazimia kondoka Madina na
kuelekea Makka mji wa amani.

32
Alijiandaa na akatoka mjini Madina usiku wa kuamkia Jumapili
kuelekea Makka akiwa na wanawe na baadhi ya ndugu zake. Ndani
ya msafara huo watoto wa Sayyidina Hasan bin Ali bin Abi Talib
walikuwa miongoni mwa watu aliofuatana nao.

InshaAllah majlis ijayo tutaona jinsi Sayyidina Husein (a.s.)


alivyoondoka mjini Madina, na ni kwa nini aliendelea kushikilia
msimamo wa kukataa kula kiapo cha utii kwa Yazid bin Muawiyah.

33
Majlis ya Saba :
Kisasi cha Banu Umayyah dhidi ya Mtume (s.a.w.w.)

Banu Umayyah na washirikina wenzao waliondoka Makka


kuelekea Uhd kupitia Ab’waa. Walipofika hapo Abu Sufiyan alitoa
ushauri kwa wenzake kwamba walifukuwe kaburi la Bibi Aminah
binti Wahbi, mama yake Mtume (s.a.w.w.)11 akawaambiya: “Endapo
Muhammad atafanikiwa kumkamata mmoja katika wanawake
wenu, basi ninyi mtamwambia: mifupa ya mama yako hii hapa.”

Aliendelea kusema: “Na kama hatofanikiwa kumkamata mmoja kati


ya wanwake wenu, basi ataikomboa mifupa ya mama yake kwa mali
nyingi.”

Ushauri huu ulipingwa na wala haukupata mtu aliyeunga mkono


miongoni mwa maquraish.

Katika vita hii ya Uhud, Hind binti Utbah, mke wa Abu Sufiyan,
alikuwa mhamasishaji mkubwa wa chuki dhidi ya Mtume na
waislamu. Na ni mwana mke huyu ndiye aliyemkodi Wahshi kwa
ajili ya kumuuwa Sayyidina Hamza, ami yake Mtume (sa.w.w.).12
Hakutosheka na kumuuwa tu, bali alimpasua na kula ini lake.

Sababu ya kufanya kitendo hiki kiovu, ni kupoza hasira zake na


kulipa kisasi dhidi ya Mtume (s.a.w.w.) na waislamu, baada ya
kuuliwa kwa baba yake na ndugu zake wawili katika vita kuu ya
11 Bibi Aminah binti Wahbi alifishwa huko akiwa na Mtume (s.a.w.w.) wakirejea
Makka baada ya kuwatembelea ndugu zake katika Bani Adiyyi ibn Najjaar.
Wakati huo bwana Mtume alikuwa na umri wa miaka miwili.
12 Huyu Wahshi alikuwa mtumwa wa Binti Al-Haarith bin Aamir bin Naufal,
ambapo baba wa mama huyu aliuliwa siku ya Badri. Mwanamke huyu
alimwambia Wahshi kwamba ikiwa atamuuwa Muhammad au Hamza au
Ali, basi yeye atampa uhuru. Yaonesha wazi kwamba mama huyu hakuona
mwingine yeyote miongoni mwa waislamu ambaye atakuwa ni fidia ya baba
yake isipokuwa Mtume (s.a.w.w.), au Hamza na au Ali (a.s.).

34
Badri. Vita hii ilikuwa baina ya washirikina wa Makka na waislamu,
na ilipiganwa mnamo mwaka wa tatu wa hijra.

Hadithi ya Karbala:
Baada ya kueleza sababu zilizomfanya Sayyidina Husein bin Ali
(a.s.) akatae kula kiapo cha utii kwa Yazid, sasa turejee tena Ma-
dina na tuyaone mazingira ya safari yake kutoka Madina kuelekea
Makka. Vile vile tutaeleza hali ya mambo ilivyokuwa hapo Makka
baada ya kuwasili kwake.

Ndani ya majlis iliyopita tulisema kwamba: Sayyidina Husein bin


Ali (a.s.) hakuafiki rai ya yeyote isipokuwa aliazimia kuondoka
Madina na kuelekea Makka mji wa amani.

Alijiandaa na akatoka mjini Madina usiku wa kuamkia Jumapili


mwezi 28 Rajab akiwa na wanawe na baadhi ya ndugu zake, pamoja
na watoto wa Sayyidina Hasan bin Ali bin Abi Talib (a.s.).

Wakati Sayyidina Husein (a.s.) anaondoka mjini Madina alisoma


aya ya ishirini na moja iliyoko ndani ya sura Al-Qasas isemayo: “Basi
akatoka, hali ya kuwa ana khofu akiangalia huku na huku. Akasema:
Mola wangu Mlezi! Niokoe kutokana na watu madhaalimu.”

Sayyidina Husein (a.s.) na msafara wake walipita njia kuu


inayoelekea Makka. Kuna baadhi ya watu walimuomba abadili
njia (kama alivyofanya Abdallah bin Zubair) kuepuka kufuatwa
na watu wa yule liwali wa Madina. Sayyidina Husein (a.s.) alikataa
kubadili njia na akasema: “Kamwe siwezi kuiwacha njia hii mpaka
Mwenyeezi Mungu atakapo kuniamulia chochote kile.”

Mwezi tatu Sha’ban usiku wa kuamkia Ijumaa, Sayyidina Husein


(a.s.) na watu wake waliwasili mjini Makka. Wakati anaingia
Makka alikuwa akisoma aya ya 22 sura Al-Qasas isemayo: “Na

35
alipo elekea upande wa Madyan alisema: Huenda Mola wangu Mlezi
ataniongoza njia iliyo sawa.”

Watu wa mji mtukufu wa Makka walipofahamu kwamba mjukuu


wa Mtume (s.a.w.w.) yupo hapo, walianza kumtembelea kwa wingi.
Kadhalika kuna watu wengine waliofika Makka kutoka miji
mbali mbali kwa ajili ya kufanya ibada ya umra, nao waliungana
na watu wa Makka kumtembelea Sayyidina Husein (a.s.). Kwa
kifupi watu walikuwa wakipishana baina ya wenye kuingia na wenye
kutoka.

Miongoni mwa watu waliyofika kumuona Sayyidina Husein (a.s.)


ni Abdallah bin Abbas na Talha bin Zubair. Wawili hawa walimtaka
Sayyidina Husein abakie hapo Makka na anyamaze. Sayyidina
Husein (a.s.) aliwajibu akasema: “Hapana shaka kwamba Mjumbe wa
Mwenyezi Mungu aliniamuru jambo ambalo mimi nitalitekeleza.”

Abdallah bin Umar bin Khattaab naye ni miongoni mwa watu


waliokwenda kumtembelea Sayyidina Husein (a.s.), na kisha
kumtaka afanye mapatano na Yazid bin Muawiyah.

Sayyidina Husein (a.s.) alimjibu akamwambia: “Ewe baba Abdur-


Rahman! Unafahamu kuwa dunia hii kwa uovu uliyomo ni pamoja
na kuvinyanyasa viumbe vitakatifu vya Mwenyezi Mungu? Fahamu
kwamba kichwa cha Mtume Yahya bin Zakariya kilitolewa zawadi
kwa mtu muovu miongoni mwa watu waovu wa kibani-Israil?"

Sayyidina Husein (a.s.) aliendelea akasema: “Je! Unafahamu


kuwa wana wa Israil walikuwa wakiwauwa Manabii sabini katika
kipindi cha kuchomoza alfajiri na kutoka kwa jua, na baada ya
kufanya tendo hili huondoka na kwenda sokoni kufanya biashara
zao za kununua na kuuza kama kwamba hawakutenda chochote
cha uovu? Lakini pamoja na maovu yao hayo Mwenyeezi mungu

36
hakufanya haraka kuwaadhibu, bali baadaye aliwaadhibu kwa
adhabu kali. Basi muogope Mwenyeezi Mungu ewe baba Abdur-
Rahman na wala usiwache kunisaidia.”

Sayyidina Husein (a.s.) alibakia mjini Makka kuanzia mwezi huo wa


Sha’ban mpaka mfungo pili na siku nane za mwezi wa mfungo tatu.
Lakini hatimaye aliona usalama wake kuwa ni mdogo pale Makka,
na hapakuwa tena na utulivu wa kufanya ibada ya hija kutokana na
khofu ya kukamatwa na majasusi wa Yazid.

Majasusi hao tayari walikuwa wametumwa kumfuatilia na


kumkamata kisha wampeleke Sham kwa Yazid bin Muawiyah.
Hali hii ilimlazimu kufungua ihram yake na kuibadili ibada ya hija
akaifanya kuwa umra.

Kutokana na hali hii, ilimbidi Sayyidina Husein (a.s.) kuutoka


mji mtukufu wa Makka, mji wa Mwenyeezi Mungu ambao ndege
na wanyama wanapoingia hapo wanapewa amani. Ni jambo la
kuhuzunisha mno! Basi ni vipi mjukuu wa Mtume (s.a.w.w.) asipewe
amani katika mji huo?

Sayyidina Husein (a.s.) aliutoka mji wa Makka kama alivyoutoka


mji mtukufu wa Madina mji wa babu yake ambaye ndiye Mtume wa
umma huu. Sayyidina Husein alitoka hapo hali ya kuwa ni mwenye
khofu anangojea nini kitamtokea baada ya kuondoka mjini
Makka.

InshaAllah tukijaaliwa majlis ijayo tutaeleza mengi zaidi miongoni


mwa mambo yaliyojitokeza mjini Makka katika kipindi chote cha
Sayyidina Husein (a.s.) kuwepo pale.

37
Majlis ya Nane :
Fathu Makka

Maquraishi wakiongozwa na Banu Umayyah, walishindwa


kurudisha nyuma kasi ya kuenea kwa dini ya ki-Islamu, kama
ambavyo walishindwa kuwadhoofisha wa-Islamu.

Mwaka wa nane wa hijra ndani ya mwezi wa Ramadhan, Mtume


(s.a.w.w.) alitoka na jeshi kubwa kwa siri akaelekea Makka. Jeshi hili
lilifanikiwa kuuzingira mji wa Makka wakati maquraishi hawana
habari.

Baada ya waislamu kufanikiwa kuudhibiti mji wa Makka, maquraish


hawakuwa na njia ila kusalim amri. Abbas bin Abdul-Muttalib
alimfuata Abu Sufiyan aakmwambia: “Silimu utaslimika.” Abu
Sufiyan alijibu akasema: “Kwa hakika ufalme wa mwana wa nduguyo
umekuwa mkubwa.” Abbas akamwambia: “Huu siyo ufalme, bali ni
Uislamu.”

Zaidi ya hapo Abbas bin Abdul-Muttalib alikwenda kwa Mtume


(s.a.w.w.) kumuomba ampe amani Abu Sufiyan. Mtume (s.a.w.w.)
akasema: “Nenda kamwambiye, bila shaka sisi tumekwisha kumpa
amani na kesho umlete kwangu.”

Siku ya pili Abu Sufiyan alikuja kwa Mtume (s.a.w.w.) akatamka


shahada mbili, kwa maana ya kusilimu.

Kuna riwaya nyingine inasema kuwa: Abu Sufiyan alipofikishwa


mbele ya Mtume (s.a.w.w.), Mtume alimwambiya: “Je! Hivi
wakati haujafika kwako wewe kutambua kwamba: hapana Mola
apaswaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyeezi Mungu?” Abu
Sufiyan alijibu akasema: “Naapa kwa baba yangu na mama yangu,
wewe ni mpole mno, na wewe ni mkarimu mno, na wewe

38
unathamini mno udugu! Namuapa Mwenyeezi Mungu, bila shaka
jambo hilo nimekwisha kulitambua, kwani lau angekuwepo Mungu
mwingine asiyekuwa yeye, basi angetusaidia.”

Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ole wako! Je! Hivi wakati haujafika


kwako wewe kutambua kwamba; mimi ni Mjumbe wa Mwenyeezi
Mungu?” Abu Sufiyan alijibu akasema: “Naapa kwa baba yangu na
mama yangu, wewe ni mpole mno, na wewe ni mkarimu mno, na
unathamini mno udugu! Ama juu ya hili ndani ya nafsi kuna kitu.”
Abbas bin Abdil-Muttalib akamwambiya Abu Sufiyan: “Wele wako!
Silimu kabla shingo yako haijakatwa.”

Nukta Muhimu:
Ibn Hisham ndani ya kitabu chake Siraatun-Nabiyyi ameandika
hivi: Al-Harth bin Hishaam na Abu Sufiyan walipomsikia
mwadhini anasoma adhana; Hisham alimwambiya Abu Sufiyan:
“Ama Wallahi kama mimi ningekuwa najua kuwa Muhammad ni
Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, basi bila shaka ningemfuata.” Abu
Sufiyan alijibu akasema: “Mimi sisemi kitu.....”

Kwa hakika kama Abu Sufiyan angekuwa amesilimu kwa imani,


basi asingeridhika na usemi wa Harth bin Hisham, kwa hiyo kukiri
kwake ndani kwa ndani ni dalili tosha kwamba yeye alikuwa bado
ni mshirikina.

Ama Hind, mke wa Abu Sufiyan, huyu naye alisilimu kwa kukosa
budi kama mumewe. Mama huyu alipofika mbele ya Mtume
(s.a.w.w.) ili asilimu, Mtume alimwambiya: “Nipe baia ya
kwamba hutawauwa watoto wako.” Hind alijibu akasema: “Ama siye
tuliwalea watoto wetu walipokuwa wadogo, walipokuwa wakubwa
wewe ukawauwa siku ile Badri.” Mtume akasema: “Na unipe baia
ya kwamba hutazini.” Hind alijibu akasema: “Hivi kweli mwanamke
aliye huru atazini?” Mtume (s.a.w.w.) alimgeukia Abbas bin Abdil-

39
Muttalib, akatabasamu. Kwa nini Mtume alimtazama Abbas bin
Abdil-Muttalib kisha akatabasamu?

Mazingatio:
Abu-Talib baba yake Imam Ali (a.s.), na Abu Sufiyan, nani
mwislamu?

Hadithi ya Karbala:
Bila shaka bado tunakumbuka jinsi Sayyidina Husein (a.s.)
alivyoshindwa kuendelea na ibada ya hijja pale Makka na
ikamlazimu kuutoka mji huo wa amani hali ya kuwa anangojea nini
kitamtokea.

Ahadi yetu ilikuwa ni kukufahamisheni mambo mengi zaidi


yaliyotokea Makka kabla ya Sayyidina Husein kuondoka mjini
humo.

Ni vizuri kwa sasa tuitazame hali ya mji wa Al-Kufah huko Iraqi


ilikuwaje baada ya kifo cha Muawiyah, na pia baada ya ukhalifa
kuingia mikononi mwa Yazid bin Muawiyah.

Wanahistoria wa ki-Islamu wanatwambia kwamba: habari za


kifo cha Muawiyah zilipofika katika mji wa Al-Kufah na kwamba
Yazid ametawazwa kuwa khalifa baada yake, waislamu wa mji huo
hawakupendezwa na jambo hilo.

Kadhalika walipopata habari kwamba Sayyidina Husein (a.s.)


amekataa kula kiapo cha utii kwa Yazid, watu hao walikusanyika
katika nyumba ya bwana Suleiman bin Surad Al-Khuzzai.

Miongoni mwa watu waliyohudhuria kikao hicho pamoja na


Suleiman bin Surad ni hawa wafuatao: Musayyab bin Najabah, Rifa’
bin Shaddaad, Habib bin Madhahir na wengineo.

40
Watu hawa walipokamilika, Suleiman bin Surad Al-Khuzzai
alisimama akawaambia: “Kwa hakika Muawiyah amekufa, na
Husein bin Ali amekataa kuwatii wale waliojitwalia mamlaka na
amekwisha kuondoka Madina na sasa hivi yuko Makka.”

Aliendelea akasema: “Ninyi ndiyo wafuasi wa baba yake, na kama


mnafahamu kuwa mnawajibika kumsaidia na kumpiga adui yake na
kuziangamiza nafsi zenu kwa ajili yake, basi mwandikieni barua aje,
na kama mnaogopa kushindwa basi msimwite mtu huyu.”

Wale watu walijibu wakasema: “Sisi tuko tayari kutoa nafsi zetu kwa
ajili yake na tutampiga adui yake.”

Baada ya ahadi hii kutoka kwa jamaa hawa, bwana Suleiman bin
Surad Al-Khuzzai aliwaambia: “Basi mwandikieni.”

Barua iliandikwa kama ifuatavyo: “Bismillahir-Rahmanir-Rahiim.


As-Salaamu alaikum. Kwa hakika sisi tunamhimidi Mwenyeezi
Mungu ambaye hapana mola mwingine ila Yeye. Amma baada ya
salamu na kumhimidi Mwenyeezi Mungu: Ametukuka Mwenyeezi
Mungu ambaye amemuangamiza adui yako aliyekuwa jeuri na
mpinzani wa haki hali ya kuwa anajua.

Adui yako aliukandamiza umma huu kwa nguvu, akapora mali za


umma na akautawala umma huu hali ya kuwa hautaki kutawaliwa
na yeye, na akawa anawauwa watu wema na kuwabakisha waovu.

Si hivyo tu, bali mali ya Mwenyeezi Mungu akaifanya ni ya


kutumiwa na matajiri na watu wakatili. Basi na alaaniwe kama
walivyolaaniwa watu wa Thamuud.

Kwa hakika sisi hatuna kiongozi wa kutuongoza, basi njoo ili


Mwenyeezi Mungu apate kutuunganisha katika haki kupitia kwako.

41
Hapana shaka kwamba, huyu Nu’maan (liwali wa hapo mjini Kufah)
hatushirikiani naye kwenye ibada ya Ijumaa wala hatutoki pamoja
naye kwenye swala ya Idi.

Iwapo tutafahamu tu kwamba umeshafika mjini hapa, basi tutamtoa


tumrudishe Shamu Insha Allah. Amani iwe juu yako ewe mwana wa
Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, na pia amani imshukie baba yako.
Hapana hila wala nguvu isipokuwa (vitoke) kwa Mwenyeezi Mungu
Mtukufu.”

Barua hiyo ilifungwa na wakapewa mabwana Abdallah bin Masma’a


Al-Hamadani na Abdallah bin Wail kuipeleka Makka kwa Sayyidina
Husein (a.s.). Watu hawa waliamuriwa kwenda mwendo wa haraka.

Kabla ya kuendelea, ni vizuri kwanza tuyafanyie mazingatio mambo


kadhaa ambayo kwa namna moja au nyingine yatakuwa ni dira yetu
katika kukisimulia na kukifahamu vizuri kisa hiki.

Jambo la kwanza ni maelezo ya watu wa mji wa Al-kufah ndani ya


barua yao waliyo mwandikia Sayyidina Husein (a.s.). Inaonesha
wazi kuwa utawala wa Muawiyah bin Abi Sufiyan haukuwa wa haki
na wala waislamu walikuwa hawaridhiki nao. Ndani ya barua yao
wameeleza mambo muhimu yafuatayo:
1. Muawiyah alikuwa jeuri na akipinga haki hali ya kuwa anajua.
2. Muawiyah alikuwa ni mtawala aliyeutawala umma kwa nguvu
na ukandamizaji.
3. Muawiyah alipora mali za umma, na kuhodhi mali ya
Mwenyeezi Mungu akawamilikisha matajiri na watu katili.

Kwa upande wa pili watu hawa hawakuwa tayari kuongozwa na


khalifa aliyekuja baada ya Muawiyah kutokana na sababu kubwa
mbili. Ya kwanza ni mwenendo na tabia ya khalifa huyu, kwani
hakuwa na mwenendo wala tabia ya ki-Islamu.

42
Sababu ya pili ni kwamba, waislamu walikuwa bado wanakumbuka
ule mkataba kati ya Muawiyah na Sayyidina Hasan (a.s.) kuhusu
ukhalifa. Mkataba huo ulikuwa unasema kuwa:
“Ikiwa Sayyidina Hasan (a.s.) atatangulia kufa basi Muawiyah
aurudishe ukhalifa ndani ya nyumba ya Mtume (s.a.w.w.).”

Muawiyah hakutekeleza makubaliano hayo na badala yake


akamrithisha Yazid mwanawe.

Ili kufahamu kwa njia nyepesi mazingira haya ya utawala wa


Muawiyah na mwanawe Yazid, tafadhali rejea vitabu vya maisha
ya Sayyidina Hasan na Sayyidina Husein (a.s.), vilivyo andikwa
na marhum Sheikh Abdallah Saleh Farsi aliyekuwa Kadhi Mkuu
wa Jamhuri ya Kenya. Vitabu hivi vinapatikana katika maduka ya
vitabu vya ki-Islamu.

Kwa mapenzi ya Mwenyeezi Mungu majlis ijayo tutayaona majibu


ya Sayyidina Husein (a.s.) kwa watu wa mji wa Al-Kufah na hatua
alizozichukuwa kufuatia wito huo.13

13 Marejeo: Tarikh Al-Kamil, matukio ya mwaka wa 60 a.h, j 4 uk 20; Tarikh


Tabari matukio ya mwaka wa 60 A.H j 5 uk 347. Murujud-Dhahabi cha Al-
Mas-oud juz 3 uk 64 chapa ya Daarul-Ma’rifa Beirut

43
Majlis ya Tisa

Mpaka kufikia mwaka wa sitini na moja hijiriyyah, Uislamu ulikuwa


umetimiza umri wa miaka sabini na nne tangu Mtume Muhammad
(s.a.w.w.) alipoanza kuitangaza dini hii, na ni kiasi cha miaka
hamsini tangu kufariki kwa Mtume (s.a.w.w.).

Kipindi hiki cha miaka sabini na nne tangu kuja kwa dini ya
ki-Islamu, kilikuwa ni kipindi cha misuko suko mingi ikiwemo
upinzani wa Maquraishi wakiongozwa na Banu Umayyah dhidi ya
Mtume na waislamu. Kadhalika Banu Umayyah walifanya mateso
mengi na mauwaji ya wafuasi wa dini hii tukufu.

Miongoni mwa matukio muhimu katika historia ya dini ya


ki-Islamu, ni lile la kuhama kwa Mtume (s.a.w.w.) kutoka Makka
kwenda Madina kuepuka bughdha ya maquraish, na tishio la
kuuliwa Mtume (s.a.w.w.).

Vita vya Badri, Uhudi, Khandaq, Hunein na vingine kadhaa


alivyopigana Mtume wetu dhidi ya maquraish na washirika wao,
ambavyo kwa asilimia kubwa vilicho chewa na Banu Umayyah kwa
lengo la kudhoofisha nguvu ya Uislamu.

Kwa hakika kupambana na maquraishi halikuwa jambo jepesi


kutokana na uwezo wao kivita na idadi ya watu. Hapana shaka
kwamba kukabiliana na watu wenye sifa hizi inahitaji kuwa na
imani thabiti, subira, uvumilivu na kujitoa muhanga kwa hali na
mali. Na hivyo ndivyo walivyokuwa masahaba wa Mtume (s.a.w.w.).

Chukua mfano wa vita ya Badri ambapo waislamu walikuwa


na idadi ya watu mia tatu kumi na tatu takriban, na waliweza
kupambana na washirikina wapatao elfu moja. Majeshi ya pande
hizi mbili yalipokutana katika uwanja wa vita, waislamu pamoja na

44
uchache wao kwa idadi, lakini walipata ushindi mkubwa dhidi ya
maquraish.

Kwa ujumla ushindi wa Mtume (s.a.w.w.) na wa-Islamu dhidi ya


maquraish, ulikamilika siku ile ya Fathi Makka, ambapo Banu
Umayyah na washirika wao walilazimika kusilimu, na baada ya
kusilimu kwao Mtume (s.a.w.w.) aliwaacha huru. Ndiyo maana
baada ya hapo Banu Umayyah walikuwa wakijulikana kama At-
Tulaqaa yaani waliyo achwa huru.

Watu hawa kama tulivyokwisha ona hapo kabla, ni wazi


hawakusilimu kwa imani, bali walijisalimisha tu ili kuhifadhi damu
yao.

Kuingia kwao katika dini kuliwapa nafasi ya kuanzisha vita mpya


ya ndani kwa ndani dhidi ya Mtume (s.a.w.w.) na waislamu. Vita hii
haikuwa na mafanikio wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.).

Hadithi ya Karbala:
Majlis iliyopita tulisoma barua ya watu wa mji wa Al-Kufah kwenda
kwa Sayyidina Husein bin Ali (a.s.), na tukaona ahadi yao ya kutaka
kushirikiana naye ili awaongoze, na kwamba wako tayari kujitolea
nafsi zao kwa ajili yake.

Kwa mujibu wa historia ya ki-Islamu ni kwamba, baada ya siku mbili


kupita tangu kutumwa kwa barua ile, watu wa mji wa Al-Kufah
walipeleka tena barua nyingi mno kwa Sayyidina Husein (a.s.).

Barua hizo walikabidhiwa mabwana Qais bin Mas-Har As-Saidaawi,


Abdallah na Abdur-Rahman watoto wa Shad-Daad Al-Ar-Habi.
Pamoja na hawa alikuwa ni bwana Ammaarah bin Abdallah As-
Saluuli, na kila mmoja alipewa barua mia tano.

Baada ya siku mbili tena, watu wa mji huu walimtuma Hani bin

45
Hani As-Subai na Said bin Abdallah Al-Hanafi waende Makka kwa
Sayyidina Huseina (a.s.), kumpelekea barua ambayo ilikuwa na
maneno yafuatayo:
Bismillahir-Rahamanir-Rahim.
Kwa Husein bin Ali (a.s.), barua kutoka kwa wafuasi wake miongoni
mwa waumini na waislamu. Amma baada ya salaam: “Njoo haraka;
kwa hakika watu wanakusubiri, hawana rai nyingine isipokuwa
wanakusubiri wewe. Basi fanya haraka tena haraka sana.”

Kwa mujibu wa Sayyid Sharafud-Din Al-Musawi ndani ya kitabu


chake Al-Majalisul-Faakhirah amesema kuwa: “Pamoja na wingi wa
barua na kuhimizwa alikokuwa akihimizwa Sayyidina Husein na
watu mji wa Al-Kufah ndani ya barua zao, yeye alikuwa mzito kutoa
majibu kwa watu hao.”

Sayyid Sharafud-Din anaendelea kusema kuwa: “Kuna siku moja


Sayyidina Husein (a.s.) aliletewa barua zipatazo mia sita, na
wajumbe waliyotumwa kuleta barua hizo wote walikutana mbele
yake kwa wakati mmoja.”

Baada ya watu hawa kumkabidhi Sayyidina Husein (a.s.) barua zile,


aliwataka wamueleze hali ya watu huko watokako kisha aliwauliza
mabwana Hani na Said bin Abdallah Al-Hanafi akasema: “Hebu
nambiyeni; ni kina nani hasa waliyo jumuika kuniandikia barua
hii?”

Mabwana hawa walimfahamisha Sayyidina Husein (a.s.) hali halisi


ya watu wa mji ule wa Al-Kufah ilivyo, na wakamtajia majina ya
watu wenye msimamo na rai ya kumwita. Baada ya kutoshelezwa na
na maelezo yao, Sayyidina Husein (a.s.) alisimama kisha akaswali
rakaa mbili halafu akaandika barua ifuatayo:
“Bismillahir-Rahmanir-Rahim.
Barua kutoka kwa Husein bin Ali kwenda kwa watukufu waumini na
waislamu. Amma baad, hakika Hani na Said wamenifikia wakiwa na

46
barua zenu. Wao wamefika mwisho miongoni mwa wajumbe wenu
mliowatuma.

Kwa hakika mimi nimeyafahamu yote mliyo yaeleza, na jambo


muhimu mlilozungumza ni kwamba: ‘Bila shka sisi hatuna kiongozi,
basi njoo huenda Mwenyeezi Mungu akatuimarisha kwenye haki na
uongofu kupitia kwako.’

Mimi namtuma ndugu yangu na mwana wa ami yangu naye ni


miongoni mwa watu wa nyumba yangu aje huko. Basi endapo
ataniandikia kuniarifu kuwa maoni ya viongozi wenu na watu bora
miongoni mwenu yameafikiana kama ambavyo wajumbe wenu
walivyonijulisha na nilivyosoma barua zenu, basi mimi nitakuja huko
haraka Mwenyeezi Mungu Mtukufu akipenda.

Kwa hakika naapa! Hawezi mtu kuwa kiongozi ila yule


anayehukumu kwa mujibu wa Qur’an, mwenye kusimamia haki na
anayeishi kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya haki na kuifunga
nafsi yake katika dhati ya Mwenyeezi Mungu. Was-Salaam.”

Baada ya kuandika barua hii Sayyidina Husein alimwita nduguye


bwana Muslim bin Aqil na akamtuma aende huko Al-Kufah.
Alimwagiza afuatane na mabwana Qais bin Mas-Har As-Saidaawi,
Ammaarah bin Abdallah, Abdur-Rahman na Abdallah, watoto wa
Shad-Daad Al-Ar-Habi.

Sayyidina Husein (a.s.) alimuusia Muslim bin Aqil kumcha


Mwenyeezi Mungu na pia awe mpole, kisha akifika asizungumzie
sababu iliyomfanya kwenda huko.

Mwisho alimtaka afanye haraka kwenda Al-Kufah, kwani yaone-


sha watu wameshikamana pamoja juu ya kumtaka yeye Sayyidina
Husein (a.s.) kwenda huko. Muslim bin Aqil aliondoka kuelekea
Al-Kufah kupitia Madina.

47
Majlis ya Kumi

Kufariki kwa Mtume (s.a.w.w.) mnamo mwaka wa kumi na moja


hijiriyyah, ni jambo ambalo halikuwa na budi kutokea. Tokeo hili
halikuwa la ghafla, kwa sababu kila nafsi itaonja kifo, na kwamba
Mwenyeezi Mungu alikwisha kuliweka bayana katika Qur’an
akasema: “Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume, wamepita kabla
yake Mitume (wengi). Basi je! Akifa au akiuliwa mtarudi nyuma kwa
visigino vyenu?.........” (Qur’an, 3:144)

Kwa kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa anafahamu


kuwa iko siku atakufa, basi aliandaa mrithi wa kazi hii mapema ili
kuepusha hitilafu na kutokuelewana baina ya waislamu baada yake.

Kwa mujibu wa vitabu vya tafsir ya Qur’an, tarekh na vingine


visivyokuwa hivyo, vinasema kuwa: “Sababu ya kushuka kwa aya ya
sitini na saba katika sura ya tano, ilikuwa ni kubainishwa uongozi
wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) juu ya umma wa ki-Islamu baada
ya Mtume (s.a.w.w.).”

Vitabu hivyo vinaeleza kuwa: “Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akirejea


Madina kutoka Makka baada ya ibada ya hijja, hali ya kuwa
amefuatana na waislamu wapatao laki moja, walipofika kwenye
bonde la Khum, ambapo kuna njia panda ya kuelekea Madina,
Misri na Iraq, Mwenyeezi Mungu aliiteremsha aya isemayo: “Ewe
Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako. Na kama
hukufanya, basi (utakuwa) hukufikisha ujumbe wake.....”

Haya yalitendeka mnamo mwezi kumi na nane mwaka wa kumi


hijiriyyah majira ya asubuhi hapo kwenye bonde la Khum njia
panda inayoelekea Madina, Misri na Iraq.

Lakini kwa huzuni kubwa baada ya Mtume (s.a.w.w.), waislamu

48
hawakujali wala kukumbuka tangazo la Ghadir. Waligombea
uongozi ule wakaacha nidhamu aliyoiweka Mtume (s.a.w.w.).
Walipitisha maamuzi yao na kumuweka Abu Bakri kuwa khalifa
baada ya Mtume (s.a.w.w.).

Twaweza kusema kitendo hicho kilikuwa ni msiba mkubwa wa


kwanza katika Uislamu uliyozaa misiba mingine mingi ikiwemo
kuuliwa kwa Sayyidina Husein (a.s.) huko Karbala.

Hadithi ya Karbala:
Tumekwisha kuona jinsi barua nyingi kutoka mji wa Al-Kufah
zilivyokuwa zikitumwa kwa Sayyidina Husein (a.s.) wakati akiwa
mjini Makka. Na barua zote zilikuwa zinamtaka aende huko ili
akawaongoze watu wa mji ule.

Tulieleza pia juu ya maamuzi ya Sayyidina Husein (a.s.) kukubaliana


na maombi ya watu hao, lakini kabla ya yeye kwenda huko aliona ni
vema kumtuma Muslim bin Aqil aende kuiangalia hali na mazingira
yaliyoko huko Al-Kufah. Bwana Muslim bin Aqil aliondoka
kuelekea Al-Kufah kupitia Madina.

Wanahistoria wa ki-Islamu wanaeleza kuwa: Muslim bin Aqil


alipofika mjini Madina, moja kwa moja aliingia ndani ya msikiti wa
Mtume (s.a.w.w.) akaswali kisha aliwaaga watu wa nyumbani mwake
na watu wengine ambao aliona ni vizuri kuwaaga kisha aliondoka
kuelekea mjini Al-Kufah nchini Iraq.

Bwana Muslim bin Aqil alipowasili mjini Al-Kufah, alipokelewa na


akafikia ndani ya nyumba ya bwana Mukhtar bin Ubaid At-Thaqafi.

Habari za kuwasili kwa Muslim bin Aqil ambaye ni mjumbe


wa Sayyidina Husein (a.s.) zilipoenea mjini hapo, watu wakawa
wanapishana nyumbani kwa bwana Mukhtar At-Thaqfi kwa lengo la
kuonana na Muslim bin Aqil.

49
Watu hawa kila wanapokusanyika ndani ya nyumba alimofikia
Muslim bin Aqil, yeye huwasomea barua ya Sayyidina Husein (a.s.),
jambo ambalo lilikuwa linawaliza. Bila shaka walikuwa wakilia
kutokana na shauku yao juu ya Sayyidina Husein (a.s.).

Haikuchukua muda mrefu ila watu wapatao elfu kumi na nane


walikula kiapo cha utii kwa Muslim bin Aqil, ambapo naye alikipokea
kiapo chao kwa niaba ya Sayyidina Husein (a.s.).

Mazingira haya ya watu wa Al-Kufah yalimfanya Muslim bin


Aqil amuandikie Sayyidina Husein (a.s.) kumjulisha hali ilivyo na
kumtaka aende huko.

Watu wa mji wa Al-Kufah waliendelea kumtembelea Muslim


bin Aqil kiasi kwamba Nuuman bin Bashir aliyekuwa liwali wa
mji huo tangu utawala wa Muawiyah na katika utawala wa Yazid,
akautambua mkusanyiko ule unaofanyika mahali alipofikia Muslim
bin Aqil.

Pamoja na liwali huyu kuutambua mkusanyiko ule, lakini


hakumfanyia lolote la ubaya Muslim bin Aqil.

Baada ya muda kupita na hali ya mji wa Al-Kufah ikiwa katika


mazingira hayo, Abdallah bin Muslim bin Rabia’ Al-Hadhrami
alimuendea Nuuman bin Bashir akamwamba:
“Bila shaka mambo yote unayo yaona yanatendeka hapa hayana
mafanikio kwako, ila utapoteza madaraka. Na huu msimamo unao
uonesha baina yako na adui yako ni msimamo wa watu wanyonge.”

Abdallah bin Muslim bin Rabia’ Al-Hadhrami hakuridhika kwa


kumpa onyo Nuuman bin Bashir, bali aliandika barua kwenda
kwa Yazid bin Muawiyah na akamwambia katika barua hiyo kama
ifuatavyo:

50
“Hakika Muslim bin Aqil amefika hapa Al-Kufah, na watu tayari
wamekula kiapo cha utii kwake kwa niyaba ya Husein bin Ali. Basi
iwapo wewe unaitaka nchi hii ibakie mikononi mwako, mlete mtu
imara atakayesimamia maslahi yako na atafanya vile ambavyo wewe
unamfanyia adui yako. Huyu Nuuman ni mtu dhaifu au pengine
anajifanya dhaifu.”

Abdallah bin Muslim bin Rabia’ ambaye ndiye mwandishi wa barua


hii alikuwa ni mfuasi mkubwa wa bani Umayyah.

Kwa hakika siyo yeye peke yake aliyemwandikia barua Yazid


kumjulisha kuwa Muslim bin Aqil yupo pale Al-Kufah, bali
Ammarah bin Uqbah na Omar bin Saad nao walimwandikia Yazid
barua mfano wa ile aliyoandika Abdallah bin Muslim bin Rabia’.

Insha Allah tukijaaliwa majlis ijayo tutaona ni hatua gani


alizochukua Yazid bin Muawiyah baada ya kupata barua
zinazoelezea hali ya mji wa Al-Kufah ilivyokuwa tangu Muslim bin
Aqil mjumbe wa Sayyidina Husein (a.s.) awasili mjini hapo.

51
Majlis ya Kumi na Moja

Baada ya Mtume (s.a.w.w.) kufariki, maquraishi walikutana


katika klabu ya Bani Saidah kumchagua mtu atakaye mrithi Mtume
(s.a.w.w.) katika uongozi wa umma.

Walisahau au walijisahaulisha maagizo ya Mtume aliyo yatoa pale


Ghadir Khum kuhusu nani atakaye mrithi.

Uchaguzi huo haukuwa mwepesi na rahisi kama ambavyo


waislamu wengi wanavyo dhani. Ilikuwa ni patashika yenye
mwelekeo wa kumwaga damu.

Umar bin Khatab alipoiona hali ile alifanya haraka kumpa mkono
wa baia Abu Bakr, na akawataka waliyo hudhuria kikao kile
wamuunge mkono.

Jambo hili lilitimia ingawaje baadhi ya watu walikataa kumpa baia


Abu Bakr.

Wakati yote haya yanatendeka, Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) na watu
wa nyumba ya Mtume walikuwa wameshughulika kuandaa mwili
wa Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili ya maziko.

Baada ya kumzika Mtume (s.a.w.w.), Imam Ali (a.s.) hakuwa na


nafasi yoyote katika uongozi ule, bali alitengwa yeye pamoja na watu
wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.).

Pamoja na hali hiyo, Sayyidina Ali (a.s.) hakuwacha kushiriki


katika qadhiya mbali mbali zinazo husu Uislamu. Alishiriki na kutoa
mchango wake kila alipohitajika.

Baada ya kifo cha khalifa wa tatu Uthman bin Affan, waislamu

52
walimtaka Imam Ali (a.s.) awe khalifa, lakini hakuwakubalia
akasema: “Niwacheni; tafuteni mwingine asiyekuwa mimi.”

Baada ya shinikizo dhidi yake, alikubaliana nao akawaambia:


“Fahamuni ya kwamba, ikiwa mimi nitakubaliana nanyi, basi
nitakuongozeni kwa mujibu wa vile nijuavyo mimi. Sintasikiliza
kauli ya yeyote yule, na wala lawama ya yeyote awaye.”

Baada ya Imam Ali (a.s.) kukubali uongozi, kwa bahati mbaya sana
alikabiliana na upinzani mkali uliyokuwa unaongozwa na Banu
Umayyah.

Vita nyingi alipigana dhidi ya wapinzani wake ikiwemo vita ya


Ngamia, Siffin na Nahrawaan. Vita ya Ngamia ilikuwa chini
ya uongozi wa mama Aisha, Siffin ilikuwa chini ya uongozi wa
Muawiyah, na ile ya Nahrawan ilitokana na watu walioasi kutoka
katika jeshi la Imam Ali (a.s.) baada ya vita ya Siffin.

Wote hawa kila mmoja kwa wakti wake alizusha vita dhidi ya
Sayyidina Ali (a.s.), kiasi kwamba kipindi cha miaka minne ya
uongozi wake kiliandamwa na vita na upinzani wa kila aina.

Mauwaji dhidi ya waislamu wasiyo na hatia:


Mnamo mwaka wa arobaini hijiriyyah baada ya vita ya Siffin,
Muawiyah akiwa liwali wa Shamu, alijitwalia mamlaka ya
kukusanya zakka na kodi. Akawa hupeleka majeshi katika miji ya
ki-Islamu chini ya makanda waovu.

Makamanda hawa walifanya mauwaji mengi dhidi ya wa-Islamu.


Wanahistoria wanatwambiya kuwa: “Mmoja wa makamanda hao ni
Busr, ambaye katika safari hiyo ya kwenda na kurudi jeshi lake peke
yake liliuwa watu elfu thelathini.”

53
Kama ilivyokuwa katika zama za Mtume (s.a.w.w.), Banu Umayyah
walijaribu kuuangamiza Uislamu wakiwa nje ya dini wakashindwa,
na walipojisalimisha pia wakashindwa. Katika kipindi hiki lilikuwa
ni jaribio jengine la kutaka kuungamiza Uislamu wakiwa ndani ya
dini.

Hatimaye mnamo mwaka wa arobaini hijiriyyah, Imam Ali (a.s.)


alipigwa dharuba ya upanga ndani ya msikiti wa Al-Kufa siku ya
mwezi kumi na tisa Ramadhan. Na ilipofika mwezi ishirini na moja
alifariki.

Hadithi ya Karbala:
Majlis iliyopita tumeeleza kuwasili kwa mjumbe wa Imam
Husein (a.s.) bwana Muslim bin Aqil mjini Al-Kufah na jinsi
alivyopokelewa na watu wa mji ule.

Kadhalika tumeeleza namna Nuuman bin Bashir liwali wa mji


wa Kufah alivyoonesha kutojali maslahi ya uliwali wake, ingawaje
alikwisha kuonywa na wafuasi wa utawala wa Banu Umayyah
waliyokuwa mjini hapo.

Pia tukaeleza kwamba watu hawa hawakutosheka tu kumuonya


Nuuman bin Bashir bali walimwandikia barua Yazid kumjulisha
hali ilivyo mjini hapo.

Kwa mujibu wa tarerkh Tabari imeelezwa kuwa: Barua zile


zilipomfikia Yazid huko Sham, yeye mara moja alimwita Sarjoun
ambaye alikuwa huru wa baba yake akamwambiya:
“Naomba maoni yako! Kwa hakika Husein yuko njiani anaelekea
Al-Kufah, na Muslim bin Aqil tayari yuko mjini Kufah na watu
wanakula kiapo cha utii kwake kwa niyaba ya Husein.”

Yazid aliendelea kumwambiya Sarjoun: “Bila shaka zimenifikia

54
habari kwamba Nuuman ni mtu dhaifu, na vile vile kauli yake
si nzuri.” Kisha alimsomea barua zile, halafu akamwambiya: “Je!
Unayo maoni gani, nani nimpe uliwali wa mji wa Al-Kufah?”

Sarjoun alimjibu Yazid akamwambiya: “Waonaje lau Muawiyah


angefufuliwa, je! Ungekubaliana na maoni yake juu ya jambo hili?”
Yazid akajibu: “Naam.”

Basi pale pale Sarjoun akatoa waraka unaohusu wasia wa Muawiyah


kwa Ubaidullahi bin Ziyad kupewa uliwali wa mji wa Al-Kufah.
Kisha Sarjoun akasema: “Haya ndiyo maoni ya Muawiyah na
amekufa hali ya kuwa aliamuru kutekelezwa kwa maandiko haya.”

Yazid hakuchelewa kufanya maamuzi, bali pale pale alikubaliana na


maoni hayo akamtawalisha Ubaidullah bin Ziyad uliwali wa miji
miwili, Basra na Al-Kufah.

Ikumbukwe kwamba, kabla ya hapo Yazid alikuwa hapendezwi na


Ubaidullah bin Ziyad na juu ya hivyo alikuwa akimlaumu.

Baada ya maafikiano haya, Yazid alimwandikia barua Ubaidullah


bin Ziyad ambaye alikuwa Basra akamwambiya katika barua hiyo
maneno yafuatayo: “Amma baada ya Salaam. Mashia wangu
waliyoko Al-Kufah wameniandikia barua wakinieleza kwamba:
mwana wa Aqil yuko hapo Al-Kufah na anakusanya watu kwa lengo
la kuvunja umoja wa waislamu. Basi ukisha soma barua yangu
hii nakuamuru uwende mpaka Al-Kufah na umtafute mwana wa
Aqil kama tundu ya sindano inavyotafutwa, mpaka umkamate au
umuuwe au umfukuze. Was-Salaam.”

Baada ya hapo Yazid akamwita Muslim bin Amri na kumkabidhi


barua ile aipeleke Basra kwa Ubaidullah bin Ziyad. Muslim bin
Amri alipoifikisha tu barua ile na ikasomwa, pale pale Ubaidullah
aliamuru iandaliwe safari kuelekea Al-Kufah kesho yake.

55
Tabari anaeleza kwamba: Kabla ya hapo, Sayyidina Husein (a.s.)
aliwaandikia barua watu kadhaa wa mji wa Basra, na akaeleza humo
haki aliyo nayo kuhusu uongozi wa dini ya Mwenyeezi Mungu.

Tabari anasema: “Kila mtu aliyeisoma barua ile alinyamaza asiseme


kitu isipokuwa Mundhir bin Al-Jaaruud. Yeye kwa mujibu wa
madai yake alichelea asije akaonekana kuwa anapanga njama dhidi
ya Ubaidullah. Kwa hiyo alimtuma mtu usiku ule wa kuamkia safari
ya Ubaidullah kwenda Al-Kufah. Yule mjumbe akamsomea barua
ile ya Sayyidina Husein (a.s.), lakini pale pale alimwita yule mjumbe
na kumkata shingo yake.”

Baada ya mauaji haya Tabari anasema: “Ubaidullah alipanda kwenye


mimbari ya mji wa Basra akamtukuza Mwenyeezi Mungu na
kumsifu kisha akasema: ‘..... Bila shaka mimi natoa onyo kwa
yeyote anaye nifanyia uadui. Mimi ni sumu kali kwa mwenye kutaka
kupambana na mimi... Enyi watu wa Basra! Kwa hakika Amirul-
Muuminina (Yazid), amenipa uliwali wa Al-Kufah, nami kesho
nitaondoka kuelekea huko. Hapana shaka kwamba nimemuweka
Uthman bin Ziyad bin Abi Sufiyan kuwa kiongozi wenu.
Tahadharini msilete upinzani wala kufanya maandalizi ya vita.
Namuapa Mwenyeezi Mungu ambaye hakuna mola ila Yeye, kama
zitanifikia habari kwamba kuna mtu miongoni mwenu analeta
upinzani, basi naapa kuwa mtu huyo nitamuuwa.....’”

Tabari anaendelea kusema: “Kisha Ubaidullah bin Ziyad


aliondoka Basra akamwachia uongozi wa mji huo nduguye
Uthman bin Ziyad. Katika safari hii alifuatana na Muslim bin
Amri Al-Baahili pamoja na wasaidizi wake na watu wa nyumbani
mwake.”14

14 Marejeo: Tarekh Tabari juz 5 uk 356; Tarekh Al-Kamil juz 4 uk 23.

56
Majlis ya Kumi na Mbili

Kutokana na kufariki kwa Sayyidina Ali (a.s.), Sayyidina Hasan bin


Ali (a.s.) alichukuwa nafasi ya ukhalifa baada ya baba yake.

Habari hizi zilipofika Shamu, Muawiyah bin Abi Sufiyan


hakupendezwa, na pale pale akawaita washauri wake ili kupanga
jinsi ya kukabiliana na Sayyidina Hasan (a.s.).

Kikao hicho kilimalizika kwa makubaliano ya kuingiza majasusi


ndani ya jamii ya ki-Islamu katika maeneo yaliyo kuwa yanamtii
Sayyidina Hasan (a.s.). Kazi ya majasusi hawa ilikuwa kueneza
vitisho na uzushi dhidi ya uongozi wa watu wa nyumba ya Mtume
(s.a.w.w.). Kadhalika rushwa na ahadi nzuri nzuri vilitumika
kuwahadaa watu.

Hali ilimuwiya ngumu Sayyidina Hasan (a.s.), katika kukabiliana na


njama hizi za Banu Umayyah mpaka akalazimika kufanya sulhu na
Muawiyah.

Masharti ya sulhu yalikuwa kwamba: Muawiyah awaongoze


waislamu kwa mujibu wa Qur’an na Sunna ya Mtume (s.a.w.w.),
na kwamba Muawiyah hana haki ya kumrithisha ukhalifa mtu
yeyote yule baada yake. Kadhalika sulhu hiyo ilihusisha sharti ya
kutokuwabughudhi wafuasi wa Sayyidina Ali bin Abi Talib.

Muawiyah hakutekeleza makubaliano hayo, na badala yake


hakutumia kitabu wala sunna ya Mtume (s.a.w.w.) katika
kuwaongoza waislamu, na wala hakuwacha kuwauwa watu wema.

Kwa hakika alifanya ufisadi mkubwa ikiwemo kupora mali za


waislamu na uchafu mwingine mwingi uliyo chafua historia ya dini
ya ki-Islamu.

57
Muawiyah alikamilisha ufisadi wake kwa kumtawalisha mwanawe
Yazid mlevi na muuwaji kama baba yake, na muovu wa wazi wazi.

Sayyidina Husein (a.s.) alipopewa habari za kifo cha Muawiyah na


kwamba anatakiwa kula kiapo cha utii kwa Yazid alisema: “Na huyu
Yazid ni mtu muovu, anakunywa ulevi, anafanya maovu wazi wazi,
muuwaji; Mtu kama mimi hawezi kula kiapo cha utii kwa Yazid.”

Na amesema tena: “Umma umepata mtihani kwa kuwa na kiongozi


mfano wa Yazid.”

Kwa mukhtasari huu kuhusu njama za Banu Umayyah dhidi ya


Uislamu, kilifika kipindi ambacho ilikuwa ni lazima kutokee tukio
litakalo amsha umma wa waislamu ili uyatambue maovu na njama
za wanafiki waliojipenyeza katika dini kwa niya ya kuvuruga
mafunzo ya dini.

Imam Husein (a.s.) alikubali kufa kuliko kumpa mkono wa baia


Yazid ambaye lengo lake ilikuwa ni kuendeleza maovu ya wazee
wake wa ki-Banu Umayyah dhidi ya Mtume (s.a.w.w.) na Uislamu.

Hadithi ya Karbala:
Yaliyo tokea Al-Kufah baada ya Ubaidullah bin Ziyad
kufika hapo:
Ubaidullah bin Ziyad aliingia mjini Al-Kufah usiku, na watu wa mji
ule walidhania kuwa ni Sayyidina Husein bin Ali (a.s.) amewasili
na kwa hali hiyo walifurahi na kumsogelea. Ama walipotambua
kwamba mtu huyo alikuwa ni Ubaidullah bin Ziyad, walitawanyika
wakamwacha wakaenda zao.

Baada ya watu hao kutawanyika, Ibn Ziyad alikwenda moja kwa


moja hadi kwenye jumba la utawala wa Bani Umayyah akalala hapo
usiku ule mpaka asubuhi.

58
Kulipokucha alitoka akaanza kuonya na kuwatishia kwa ukali watu
wote wanao muunga mkono Muslim bin Aqil. Habari za vitisho
vya Ubaidullah bin Ziyad zilipomfikia Muslim bin Aqil, alichelea
usalama wake na ikambidi aende nyumbani kwa Hani bin Ur-wah
ambapo alipewa hifadhi.

Baada ya vitisho na maonyo ya Ibn Ziyad, hali ya mji wa Al-Kufah


ilibadilika ikawa mbaya mno kiasi cha kuwafanya watu waliyokuwa
wamempa Baia Muslim bin Aqil wahitilafiane na kutenguwa kiapo
chao cha utii.

Watu hawa hawakuthubutu tena kujitokeza kumtetea Muslim bin


Aqil, kwa hiyo walishindwa kutimiza ahadi yao ya kumsaidia.

Kutokana na hali hii, Muslim bin Aqil bila matarajio aliingia ndani
ya kipindi kigumu, kwani kilikuwa ni kipindi cha mateso na tishio
la kuuwawa. Watu waliyo muahidi kumsaidia na kumhifadhi
walimtelekeza.

Kutelekezwa alikotelekezwa Muslim bin Aqil kulitoa mwanya kwa


adui yake kuzidisha uovu wake dhidi yake. Hali ilifikia Muslim
akaanza kusakwa kila mahali na kizingirwa bara bara kila upande
akiwa mpweke hana wa kumsaidia.

Bila shaka Muslim bin Aqil alifikwa na mtihani unao wafika watu
wema, ambapo naye alivumilia hali ya kuwa anangoja matokeo ya
vitisho vya panga za maadui zake.

Ubaidullah bin Ziyad alizidi kujiimarisha kwa kutawanya majasusi


kufuatilia nyendo za Muslim bin Aqil. Matokeo ya ujasusi huo
yalimfanya Ibn Ziyad agunduwe kuwa Muslim yumo nyumbani
kwa Hani bin Ur-wah.

59
Baada ya kugunduwa hivyo, Ibn Ziyad aliwaita mabwana Hani bin
Ash-A’th, Hasan bin Asma bin Khaarijah na A’mru bin Al-Hajjaaj
akawaambia: “Ni kitu gani kinachomzuwiya Hani asije kwetu?”

Wao walimjibu wakasema: “Hatujuwi, lakini inasemekana kuwa


ni mgonjwa.” Ibn Ziyad akasema: “Habari hizo nazifahamu, lakini
pia nafahamu kwamba yeye amekwisha pona, na kwamba mara
kwa mara anaonekana nyumbani kwake mlangoni amekaa. Na lau
ningefahamu kuwa bado anaumwa bila shaka ningemtembelea
kumjulia hali.”

Ibn Ziyaad aliendelea kusema: “Nendeni mkamwambie asiache


kufanya wajibu wake juu ya haki yetu; kwa hakika mimi sipendi
kuona ufisadi mbele yangu unaotokana na mtu mwenye heshima
miongoni mwa waarabu mfano wake yeye Hani.”

Jioni ya siku ile mabwana hawa walikwenda nyumbani kwa Hani


na wakasimama mlangoni kwake wakamwambia: “Ni jambo gani
linalo kuzuwia usikutane na amiri?” Mabwana hawa waliendelea
kumwambia Hani: “Yeye amekutaja na amesema: Laiti ningefahamu
kuwa Hani anaumwa ningemtembelea nikamjulia hali.” Hani
aliwajibu akasema: “Ni maradhi ndiyo yanayo nizuwia nisiende
kukutana naye.”

Wale mabwana walimjibu Hani wakamwambia: “Bila shaka


zimekwisha kumfikia habari kwamba kila siku jioni, wewe unakaa
mlangoni kwako, lakini anakuvumilia kutokana na jambo hilo.”

Waliendelea wakasema: “Fahamu ya kwamba, mtawala hawezi


kuendelea kuwavumilia watu mfano wako, kwani wewe ni kiongozi
wa watu wako. Sisi tunakwambiya kweli ni bora ukafuatana nasi
mpaka kwa Ibn Ziyad.”

60
Watu hawa waliendelea kujadiliana naye mpaka wakamshinda.
Hani bin Ur’wa aliagiza mavazi yake akavaa kisha akaomba aletewe
nyumbu wake, akapanda na wakaondoka.

Walipolisogelea jumba la Ibn Ziyad, Hani alihisi kuwa kutatokea


mambo ambayo si mazuri kwake, jambo ambalo tangu hapo
mwanzo alikuwa akilihisi. Basi pale pale alimwambiya Hasan bin
Asma bin Khaarijah: “Ewe mtoto wa ndugu yangu; kwa kweli mimi
ninahofu kubwa juu ya mtu huyu je! Wewe unaonaje?”

Ibn Khaarijah akasema: “Ewe ami yangu! Mimi sina hofu yoyote
ile juu yako, basi usianze kujitia mashaka mwenyewe.” Inasemekana
kuwa kwa bahati mbaya huyu Hasan alikuwa hafahamu dhamira na
malengo ya Ibn Ziyad dhidi ya Hani.

Hani bin Ur’wa alikwenda pamoja na jamaa hawa mpaka kwa


Ibn Ziyad na wakaingia wote pamoja hadi wakafika mbele ya Ibn
Ziyad. Insha Allah tukijaliwa toleo lijalo tutaona nini kilichotokea
baada ya Hani na jamaa hao kufika mbele ya Ibn Ziyad.15

15 Marejeo: Tarekh Tabari juz 5 uk 364; Tarekh Al-Kamil juz 4 uk 27.

61
ISBN: 9987 620 55 8

Kimetolewa na Kuchapishwa na:


Bilal Muslim Mission of Tanzania
S.L.P 20033
Dar es Salaam

You might also like