You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

TANZANIA EDUCATIONAL PERISCOPE


(TEP)

INTERKNOWLEDGE, QUALITY AND UNIQUE EXAMS


SECOND GRADE IV IQUE MOCK

KISWAHILI

MUDA: SAA 1:30 25/07/2019

JINA LA MWANAFUNZI : ___________________________________________________

JINA LA SHULE : ___________________________________________________

MKOA : ___________________________________________________

WILAYA : ___________________________________________________

MAELEKEZO

1. Jibu maswali yote katika kila sehemu.


2. Soma maelekezo yote vizuri katika karatasi ya kujibia.
3. Andika jina lako kwenye karatasi ya kujibia

1|Page
SEHEMU A: IMLA

1. Sikiliza kwa makini sentensi zinazosomwa kisha andika kwa usahihi katika kipengele
cha i hadi v

i) __________________________________________________________________________

ii) __________________________________________________________________________

iii) __________________________________________________________________________

iv)__________________________________________________________________________

v) ___________________________________________________________________________

SEHEMU B: SARUFI

2. Chagua jibu sahihi na uandike herufi yake kwenye nafasi iliyoachwa wazi.
i) Nilimweleza kama anahitaji kuwaona aende ________________ hatokosa kuwaona wachuuzi.
A. uwanjani B. sokoni C. mbugani D. mjini
ii) Selina ni mtoto wa mjukuu wangu, hivyo Selina ni_______________
A. mpwa B. mjukuu C. kitukuu D. babu
iii) _____________ mwalimu wetu wa Kiswahili alifundisha somo lake vizuri
A. kesho B. leo C. jana D. keshokutwa
iv) Neno linalosimama badala ya maneno kabati, meza, kiti na kitanda ni______________
A. samani B. thamani C. miti D. mbao
v) Kaka na dada waligombana jana usiku lakini mama aliwapatanisha. neno lilopigiwa mstari
linamaana sawa na ________________________
A. suluhisha B. suruhisha C. zuluhisho D. zuruhisho

SEHEMU C: LUGHA YA KIFASIHI

3. i) Nahau ipi inafaa katika maelezo yafuatayo, ‘matokeo ya mtihani wa darasa la nne katika
shule yetu yalikuwa mazuri sana, hivyo yalitufurahisha sote.’ __________________________
A. ona fahari B. Tia moyo C. vaa njuga D. kaa kitako
ii) Kamilisha kitendawili kisemacho Babu kavaa koti la chuma_________________
A. Pikipiki B. kobe C. Konokono D. Popo
iii) Mwenda pole_______________
A. hufika mbali B. hajikwai C. anajikwaa D. hana haraka
iv) Wanafunzi wote walikubaliana na mawazo yote yaliyotolewa na walimu katika baraza la
shule. Nahau ipi inafaa kutumika kuonesha maelezo haya. ____________________
A. kumpa heko B. unga kichwa C. unga mkono D. unga mawazo
v) Methali isemayo Kidole kimoja hakivuji chawa inatufundisha nini?____________________
A. umuhimu wa kugombana B. umuhimu wa kushirikiana C. umuhimu wa kutengana
D.vidole viwili vina nguvu kubwa

2|Page
SEHEMU D: UTUNGAJI
4. Zifuatazo ni sehemu tano muhimu za barua ya kirafiki. Zipange sehemu hizo zilete
mtiririko sahihi kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E.
i) tarehe 25/03/2019
ii) Mkuu wa shule, Shule ya msingi Majaliwa, S.L.P 30 Geita
iii) Kwa mama mpendwa
iv)Wako mwanao, Shida matatizo.
v) Matumaini yangu ni wazima wa afya

SEHEMU E: USHAIRI
5. Soma shairi lifuatalo kasha jibu maswali yanayofuata.
Uzembe barabarani, walemaza na kuua,
Madereva firauni, wakimbia kama hua,
Wanakimbilia nini, hilo wenyewe wajua,
Wallahi mwatumaliza, ninyi msio makini.

Visimu vya mkononi, wapiga wakiendesha,


Vipo juu sikioni, nayo sigara kuwasha,
Miwani nayo machoni, dereva madawa tosha,
Wallahi mwatumaliza, ninyi msio makini,

Magari ya chakarani, moshi mweusi tititi,


Yajaa barabarani, kelele kama baruti,
Atatuokoa nani, na kelele hizi ati?
Wallahi mwatumaliza, ninyi msio makini

MASWALI
I) kutokana na shairi, ajali nyingi husababisha? __________________
A. ulemavu B. uzembe C. simu D. uhai
ii) Kichwa cha shairi kinafaa kuwa______________
A. Matumizi ya barabara B. ajali nyumbani C. Uzembe barabarani D. Uzembe wa gari
iii) Shairi lina jumla ya beti ngapi?____________________
A. 3 B. 2 C. 4 D. 1
iv) Katika shairi hili, kuna jumla ya mistari mingapi? _________________
A. 4 B. 12 C. 3 D. 9
v) Shairi hili linatufundisha nini? ________________
A. umakini nyumbani B. Umakini shuleni C. Umakini barabarani D. umakini wa gari

3|Page

You might also like